Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110132 articles
Browse latest View live

JAJI MKUU WA ZANZIBAR ATANGAZA MAADHIMISHO YA JUMA LA SHERIA ZANZIBAR

$
0
0
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Vuga, Mjini Zanzibar, kuhusiana na maadhimisho ya wiki ya Sheria Zanzibar iliyoanza tarehe 5 mwezi huu.
Baadhi ya Waandishi wa Habari walioshiriki mazungumzo ya Jaji Mkuu wa Zanzibar kuhusu wiki ya Sheria Zanzibar inayoanza tarehe 5 mwezi huu wakisikiliza kwa makini mazungumzo hayo.
Rais wa Wanasheria Zanzibar Omar Saidi akitoa ufafanuzi kuhusu jumuiya hiyo inavyotoa huduma za kisheria kwa wananchi kwenye mkutano ulioitishwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar uliozungumzia wiki ya sheria Zanzibar.
Hakimu anaeshughulikia kesi za watoto katika Mahakama ya Vuga Mjini Zanzibar Sabra Ali Mohd akielezea changamoto zinazoikabili kesi za watoto kwenye mkutano huo. PICHA NA ABDALLA OMAR-HABARI MAELEZO ZANZIBAR

HALMASHAURI JIJI KUJA NA MRADI WA UBORESHAJI MJI (SMART AREA)

$
0
0
 Mkuu wa Itifaki na Mawasiliano wa Jiji la Dar es Salaam Gaston Makwembe, akizungumza na wandishi wa habari (hawapo picha)  leo jijini Dar es Salaam, juu ya mradi wa kuboresha jiji unagharimu sh.milioni 500 ambao unatarajia kuanza Julai Mwaka huu,kulia ni Mkuu wa Idara ya Udhibiti Taka Protus Membe. 
Wandishi wahaba habari wakimsikiriza Mkuu wa Itifaki na Mawasiliano wa Jiji la Dar es Salaam Gaston Makwembe.
(Picha na Emmanue Massaka wa Globul ya Jamii)


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
HALMASHAURI ya Jijin la Dar es Salaam kutengeneza jiji katika ubora (Smart Area) ikiwamo kuondoa biashara zisizo rasmi katikati ya jiji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo,Mkuu wa Itifaki na Mawasiliano wa Jiji, Gaston Makwembe amesema kuwa mradi huo wa kuboresha jiji unagharimu sh.milioni 500 ambao unatarajia kuanza Julai Mwaka huu.

Makwembe amesema katika uboreshaji huo utakwenda sambasamba na uondoaji wa ombaomba katika ya jiji la Dar es Salaam.

Maeneo yatakayoguswa ni barabara ya Kawawa kutoka makutano ya Kawawa na Karume hadi makutano ya Kawawa na Ali Hassan Mwinyi ,Makutano ya Mandela na Pungu pamoja maeneo ya mjini na Uwanja wa Ndege.

Makwembe amesema katika uboreshaji huo ni pamoja na uzuiaji wa Pikipiki,bajaji,Maguta pamoja na gari zinazozidi tani 10 kuingia katikati ya jiji.


ASSEMBLY MUST SAFEGUARD ITS INDEPENDENCE & IMMUNITIES

$
0
0
The East African Legislative Assembly has urged Partner States, Organs and Institutions of the Community to uphold and apply the principles and provisions as enshrined in the Treaty in respect to privileges of Members of EALA.   In this regard, it is now official the tenure of the four Members of EALA from Burundi whom the Burundi National Assembly had wanted recalled from the Assembly, will be upheld.

Late yesterday, the Assembly has passed a Report of the Committee on Legal Rules and Privileges on the consideration of a Resolution moved under Rule 30 (J) of the Assembly Rules and Procedures on a matter of Privileges arising from a threat of tenure of office of Office of four Members of EALA.  The Report was presented by Hon Peter Mathuki, Chairperson of the Committee. 
                                                                                                                                           
The Assembly also passed the Resolution on the same – which was the main subject matter but with amendments contained in the Report of the Committee on Legal Rules and Privileges.
Hon Peter Mathuki reads the Report of the Committee on Legal Rules and Privileges on the Resolution moved under Rule 30 (J) on a matter of privileges arising from a threat of tenure of office. 

The Resolution moved in November 2015 by Hon AbuBakr Ogle, had advised the Assembly to urge Partner States not to introduce attempts to manipulate institutions, threaten Members or undermine their status, terming such a move unlawful and an affront to the principles under the EAC Treaty.

The Resolution (then had) condemned in the strongest term possible all attempts to undermine the authority of the Assembly and claims to the privileges and status of its Members.  However, the Committee in its Report yesterday suggested and made changes to the Resolution reaffirming to the position taken by the Speaker of EALA as communicated to the Speaker of Burundi National Assembly on the matter.
Hon Martin Ngoga contributes to the House.

In November 2015, the Speaker of the Burundi National Assembly, Rt. Hon Pascal Nyabenda wrote to the EALA Speaker, ceasing membership of four Members from Burundi to EALA. The four are Hon Jeremie Ngendakumana, Hon Frederic Ngenzebuhoro, Hon Yves Nsabimana and Hon Dr. Martin Nduwimana.

STATEMENT BY UNFPA EXECUTIVE DIRECTOR, DR. BABATUNDE OSOTIMEHIN, ON THE ZIKA VIRUS

$
0
0
Press Conference by Dr. Babatunde Osotomehin, Executive Director, United Nations Population Fund (UNFPA), to brief on the General Assembly High-level event on the Demographic Dividend and Youth Employment.
UNFPA, the United Nations Population Fund, is closely monitoring the outbreak of the Zika virus and warning about its potentially adverse effects on the health of women and babies, particularly in Latin America. We are also closely monitoring its possible spread to other regions.

UNFPA will continue to lead efforts to promote widespread information about the virus and about voluntary family planning. Given reported cases of Zika virus transmission through sexual contact, the role of UNFPA as the world’s leading agency on reproductive and maternal health, and the biggest public sector supplier of family planning commodities, including condoms, is ever more pertinent.

Women and girls should be able to make informed decisions about their reproductive health and family planning methods, and to protect themselves and their babies if they decide to be pregnant. UNFPA will continue to work with countries around the world to scale up access to information and to a wide range of voluntary family planning commodities so that women can make informed decisions and protect themselves.

JOB OPPORTUNITIES WITHIN THE INTERNATIONAL TELECOMMUNICATION UNION (ITU)

$
0
0

JOB OPPORTUNITIES WITHIN THE INTERNATIONAL TELECOMMUNICATION UNION (ITU)
The Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation has received an advert on various job opportunities from the International Telecommunication Union (ITU) for qualified individuals, particularly women to apply. 
The vacancies and application deadline are as follows:-
    i.        1. Information Systems Engineer-Deadline: 18 March 2016;
  ii.        2. Technical Support Officer-Deadline: 15 March 2016;
iii.     3. Head, Least Developed Countries Division-Deadline: 14 March 2016; and
iv.        4. Head, Area Office, Moscow-Deadline: 14 March 2016
For further details on the above mentioned vacancies including application procedures can be accessed at http://www.itu.int/employment/Recruitment/index.html.
“The Ministry encourages qualified Tanzanians to apply”.
Issued by: The Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Dar es Salaam.
05th February, 2015

TFF YAONYA UPANGAJI WA MATOKEO

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limewaonya viongozi wa vilabu, wachezaji, waamuzi na wasimamizi wa mchezo kutojihusisha na upangaji wa matokeo (Match fixing) katika michezo inayoendelea sasa katika ligi za ngazi mbalimbali za nchini.

TFF imejipanga na inasimamia vizuri michezo ya Ligi Kuu (VPL), Daraja la Kwanza (FDL), Daraja la Pili (SDL) na Azam Sports Federation Cup (ASFC) inayoendelea na yoyote atakayebainika kujihusisha na mchezo huo wa upangaji matokeo, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa.

Katika michezo yote inayoendelea TFF ina maofisa wake wanaofuatilia kwa ukaribu michezo hiyo, hivyo endapo kiongozi, mchezaji, msimamizi au mwamuzi atabainika kujihusisha na upangaji wa matokeo hatua kali zitachukuliwa .

TFF inawaomba viongozi, wachezaji, wasimamizi wa michezo na waamuzi kutojihusisha na mchezo huo wa upangaji wa matokeo kwani kufanya hivyo ni kukiuka katiba, sheria na kanuni zinaongoza mpira wa miguu nchini.

Benki ya Exim yazindua mpango wa kuwajengea uwezo wafanyakazi wake

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa Benki ya Exim hiyo, Bw Frederick Kanga, akizungumza wakati wa semina maalumu ya kuzindua mpango maalum wa kutambua, kusimamia na kuwajengea uwezo wa kiutendaji wafanyakazi wake, iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.


BENKI ya Exim Tanzania imezindua mpango maalum wa kutambua, kusimamia na kuwajengea uwezo wa kiutendaji wafanyakazi wake hasa wale wanaonyesha uwezo mkubwa katika kutimiza majukumu yao ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.
Mpango huo unaofahamika kama ‘Talent Management Program’ umetajwa kuwekeza zaidi katika kuwajenga kiutendaji wafanyakazi hao ikiwa ni jitihada za benki hiyo kuandaa watendaji waandamizi wa benki hiyo kutoka ndani ya benki.
Akizungumza kwenye semina maalumu ya kuzindua mpango huu iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu wa benki hiyo Bw Frederick Kanga alisema mpango huo unaoendeshwa kwa uwazi ulianzishwa mahususi  kubaini manufaa ambayo benki hiyo inayapata kutoka kwa wafanyakazi na zaidi kuyatumia manufaa hayo kujiendeleza na kuboresha huduma zake.
“Kama benki tumebaini uwepo wa nguzo tatu muhimu katika ukuaji wetu ambazo ni pamoja na rasilimali watu ambayo ndio nguzo kuu, ikifuatiwa na teknolojia  na kisha michakato (processes).Ni kutokana na filosofia hiyo Exim tunaamini katika uwepo wa msingi imara unaojengwa na wafanyakazi wetu kuwa ndio chachu ya ukuaji na uendelezaji wa biashara yetu,’’ alisema.
Alisema ili kufanikisha mpango huo, uongozi wa benki hiyo umebuni mchakato wa wazi katika utambuzi wa wafanyakazi watakaonufaika na mpango huo huku akibainisha kwamba tayari kamati maalumu imeundwa kusimamia zoezi hilo na hatimaye kuwapata walengwa.

“Kwa kuanzia uongozi tayari umefanikiwa kupata orodha ya wafanyakazi 16 wenye sifa kunufaika na mpango huu kutoka matawi yote na tayari wamepewa wataalamu wa kuwasaidia kujijengea uwezo zaidi kwa usimamizi wa benki ikiwasimamia,’’ alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi walioteliwa kunufaika na mpango huo, Meneja Msaidizi wa Mipango, Maendeleo na Uendeshaji wa benki hiyo Bw Liberat Mtui alisema;“Ujio wa mpango huu kwa upande wetu wafanyakazi ni kama ngazi ya kutusaidia kufika kule tunapotaka kwa kuwa utatuwezesha kujijengea uwezo zaidi katika masuala ya kibenki,’’

TUNDAMAN APATA UBALOZI WA KUHAMASISHA WANAWAKE WA AFRICA

$
0
0
MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake mpya wa Mama Kijacho Khalid Ramadhani ‘Tundaman’’ hatimaye amepata dili la ubalozi wa kampeni ya kuhamasisha wanawake wa Africa kuhusiana na tamasha la wanawake liitwalo (AFWAB AMSHA MAMA2016)

Tamasha hilo ambalo lilianza tangu mwishoni mwa Desemba mwaka jana, kunako Hoteli ya nyota tano ya The Tribe na vitongoji vya Nairobi, Kenya, mfanyabiashara mashuhuri na mwenye jina kubwa music , alifanya bonge la tamasha liliacha gumzo kwa kuvuta maelfu wa watu kutoka kila kona ya dunia. 

 Mkurugenzi Mtendaji wa ‘lebal’ ya Candy na Candy Records, Joe Kariuki, aliratibu tamasha maridadi lililojulikana kama Amsha Mama, maalum kwa Wanawake wa Kiafrika, tamasha lililofanyika katika Hoteli ya kifahari ya Tribe, sehemu ambayo ni maarufu sana pia kwa wasanii kutoka Marekani, akiwemo Akon. 
tunda-man
Msanii wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake mpya wa Mama Kijacho Khalid Ramadhani ‘Tundaman’.

 Tamasha hilo ambalo lengo kubwa lililenga kuzungumzia bayana hali halisi ya maisha ya mwanamke wa Afrika kuhusu safari yake, mapigano yake kimaisha, mafanikio, biashara, ubunifu na ushindi wake katika maisha.   Kama mwanaume ambaye siku zote aliye karibu na moyo wa mwanamke ambaye alitaka kumtuza ama kumzawadia kwa hatua aliyofikia, kumtia moyo, kumhamasisha katika safari yake ya mafaniko katika jamii hii yenye mfumo dume barani Afrika. 

  Akizungumza katika event hiyo, Joe alisema:"Kuwawezesha wanawake ni muongozo katika jamii, nami nataka kutumia ujuzi wangu na uzoefu nilionao kujenga jukwaa kwa ajili ya wanawake kukua biashara zao."  Washiriki wengi ambao ambao wengi wao walisafirishwa kutoka nchi za mbali kwa ajili ya kuhudhuria ‘event’ hiyo, waliunga mkono mawazo ya Joe, mfano Uganda na Italia. Lisa raia wa Italia alisema: "Dhana ya Amsha Mama ni ya kipekee. Naangalia wanawake wenye uwezo wa kuzalisha hila zitakazotumika huko Milan. 
Joe Kariuki Blog pic
Mkurugenzi Mtendaji wa ‘lebal’ ya Candy na Candy Records,Joe Kariuki.

"  Sophie kutoka Uganda, alisema: "Ninawezaje ku-miss hii! Kama mwenyekiti wa chama chetu cha wanawake 600 nataka kuhakikisha wanapata aina hii ya fursa kwa ajili ya kuonyesha bidhaa zao na kwa ajili ya kupata mtandao na wanawake wengine." Rundo la wanawake waliokuwa na hisia kama hizo, akiwemo mwingine kutoka Copenhagen, Denmark: "Tamasha haya ndiyo tunahitaji kwa ajili ya kukuza wanawake. Inaonyesha nguvu za wanawake na mipango yao."

   Na katika hilo, Joe anaendeleza jitihada zake za si tu kumwezesha Mwanamke wa Afrika, bali pia kumuinua, kumtia moyo wake, kumpa mwangaza na kujihusisha kwake.   Hivyokwa sasa na ndiyo maana ameandaa maonyeshwa makubwa ya wanawake (AFWAB AMSHA MAMA 2016), yatakayofanyikia katika Uwanja wa Kedong ranch uliopo katika jiji la Naivasha nchini Kenya Machi 25-27 2016.

HOTUBA YA MHE. WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA YA KUAHIRISHA MKUTANO WA PILI WA BUNGE

$
0
0
HOTUBA YA MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA MKUTANO WA PILI WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAREHE 5 FEBRUARI, 2016

I:       UTANGULIZI
(a)                Masuala ya Jumla

Mheshimiwa Naibu Spika,
1.            Kwanza nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kutujalia afya njema na uwezo katika kutenda yote yaliyo mema. Tumekuwepo hapa kwa takriban siku 11 katika shughuli za Mkutano wa Pili wa Bunge lako Tukufu. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo.

2.            Tumekutana hapa tukiwa tumeshuhudia uundwaji wa Serikali unaoendelea ambapo Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya uteuzi wa Baraza jipya la Mawaziri ambao ni Waheshimiwa Wabunge wenzetu. Niruhusu nitumie nafasi hii ya awali kuwapongeza Mawaziri na Naibu Mawaziri wote ambao wameteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali ya Awamu ya Tano.

(b)        Chaguzi Mbalimbali  

Mheshimiwa Naibu Spika,
3.            Katika Mkutano huu, tumeweza kufanya Chaguzi za Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge. Vilevile, tumefanya chaguzi za Wenyeviti wa Bunge letu na Wajumbe wa kutuwakilisha katika Taasisi mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa. Kwa vile orodha ni ndefu, napenda nitumie nafasi hii kuwapongeza kwa dhati kabisa na kwa ujumla wao wote waliogombea nafasi hizo na kushinda. Ni matarajio yangu kwamba tutatumia nafasi hizo vizuri katika kuleta ushirikiano, mshikamano na kufanya kazi pamoja kama Wawakilishi wa Wananchi na kutekeleza majukumu yetu kama Wabunge ndani ya Bunge hili.

BREAKING NYUZZZZZ......: MRAMBA NA YONA SASA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA NJE

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia waliokuwa Mawaziri wastaafu Basil Mramba na Daniel Yona kutumikia adhabu ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali ya Sinza Palestina.

Hatua hiyo inatokana na Mramba ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, kupitia Mawakili wao kuwasilisha barua mahakamani hapo kutoka Magereza kuhusu kutumikia kifungo cha nje.

Mawaziri hao wa zamani waliwasilisha barua hiyo ya kuitaarifu mahakama yenye kumbukumbu namba 151/DA/3/11/223 ya Desemba 5, mwaka jana, wakiongozwa na jopo la mawakili wao watatu Peter Swai, Cuthbert Nyange na Elisa Msuya.

Katika barua hiyo waliyoiwasilisha kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho ‘Wafungwa wenye sifa ya kutumikia vifungo vyao chini ya Mpango wa Huduma kwa Jamii”.

Hakimu Mkeha alisema mchakato huo ulianza baada ya Magereza kuwasilisha barua hiyo mahakamani hapo kwa kupeleka majina ya watu wanaotumikia kifungo cha nje ikiwemo mawaziri hao.

Alisema mahakama haihusiani na mchakato huo, kwani ilishamaliza kazi yake ya kuhumu, hivyo jukumu la kutumikia kifungo cha nje ni kazi ya Magereza.

“Baada ya kuleta barua hiyo kisheria mahakama inaishinikiza Ustawi wa Jamii ili ifanye uchunguzi kutokana na majina yaliyowasilishwa mahakamani,”alisema.

Hakimu Mkeha alisema kupitia barua hiyo, Mawaziri hao wa zamani wamepangiwa kutumikia adhabu ya kufanya usafi kwenye Hospitali ya Sinza Palestina kwa saa nne za kila siku.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

RAIS DKT. MAGUFULI AWASALIMIA WAKAZI WA MOROGORO PAMOJA NA KUKAGUA BARABARA YA MOROGORO- DODOMA ENEO LA KIBAIGWA

$
0
0
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ukipita katika eneo la Msamvu mjini Morogoro kuelekea Dodoma.Kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Sherehe za Miaka 39 ya Chama cha Mapinduzi (CCM) zitakazoadhimishwa Kitaifa mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Msamvu mjini Morogoro wakati akiwa njiani kuelekea Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ukarabati unaondelea katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la Kibaigwa . sehemu ya barabara hiyo inakarabatiwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

MTEMVU AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO OFISI YA CCM TEMEKE

$
0
0
 Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akimkabidhi  vifaa vya michezo Katibu Kata ya Mtoni kwa Azizi Ally vyenye thamani ya sh.800,000 kwa wenyeviti wa CCM wa Kata mbalimbali wilayani Temeke katika Hafla fupi ya kusheherekea miaka 39 ya  kuzaliwa kwa chama hicho ambapo kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika kesho Mkoani Singida  ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  Rais Mstaafu Dtk  Jakaya Kikwete
Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akisaini katika kitabu cha wageni katika ofisi za (CCM) Mtoni

Na Khamisi Mussa

Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ametoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh.800,000 kwa wenyeviti wa CCM wa Kata mbalimbali wilayani Temeke.

 Mtemvu alitoa vifaa hivyo ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo kilele chake kitaifa kinafanyika leo mkoani Singida na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mtemvu alisema lengo lake ni kuimarisha michezo kwenye kata hizo na kuwaepusha vijana kujiingiza katika vitendo vya kiovu na kujenga afya zao.

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWATEMBELEA WAHADZABE NA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA JAMII HIYO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakishiriki kupanda mihogo kwenye shamba ya la Wahadzabe kwenye kijiji cha Kibampa wilaya ya Mkalama.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Ndugu Christopher Ngubiagai akimuelekeza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana namna Wahadzabe wanavyosaga mtama kwa kutumia jiwe. 

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo ameweka historia ya kuwa kiongozi wa nne mkubwa wa Kitaifa kufika kwenye kijiji cha Munguli na Kibampa ambavyo wanaishi jamii ya Wahadzabe .Kijiji cha Munguli kilitembelewa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere, akifuatiwa na aliyekuwa Makamu wake Abdu Jumbe na Mama Sofia Kawawa.

Jamii ya Wahadzabe inaishi kwa kutegemea uwindaji,kula matunda ya porini,mizizi ,wadudu na miti hata hivyo juhudi kubwa zimefanyika kuanza kuwafundisha kilimo, kuwapeleka watoto shule ,zaidi ya Wahadzabe  305 wanasoma kwenye shule ya msingi Munguli, pamoja na vijana zaidi ya 50 kupelekwa kujiunga na JKT.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone kwa jitihada zake za kuwasaidia jamii ya Wahadzabe ikiwa pamoja na kuhakikisha wanapata elimu, wanajifunza kilimo lakini pia uamuzi wa kupima maeneo ya Wahadzabe ili wamiliki ardhi yao wenyewe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akiwa kwenye nyumba maalum ya chifu wa wahadzabe pamoja na Mwenyekiti wa Wahadzabe Edward Mashimba na Mama Sarah Philipo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kwenye nyumba ya Chifu wa Wahadzabe iliyopo kijiji cha Kibampa kata ya Mwangeza wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kibampa ambako wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya Wahadzabe,kushoto ni Mwenyekiti wa Wahadzabe Ndugu Edward Mashimba (kushoto) ambaye alikuwa akitafsiri kwa lugha ya Kihadzabe.

 wakazi wa kijiji cha Kibampa ambako wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya Wahadzabe wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kibampa ambako wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya Wahadzabe,kushoto ni Mwenyekiti wa Wahadzabe Ndugu Edward Mashimba (kushoto) ambaye alikuwa akitafsiri kwa lugha ya Kihadzabe



SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

Imeelezwa kwamba licha ya serikali kuendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya elimu bado sekta hiyo imeendelea kukumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa miundombinu. https://youtu.be/nYm0I2QUYNs  

Wakati manispaa ya Kinondoni ikifanya jitihada za ujenzi wa shule za sekondari ili kuwanusuru wanafunzi waliofaulu na kukosa shule wilayani humo, changamoto ya walimu wa hisabati na sayansi yaendelea kujitokeza.https://youtu.be/A6ZFwZQwaCE   

Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma latengua uamuzi wake wa kulifukuza shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya uboreshaji wa sekta ya afya la SIKIKA.https://youtu.be/pXyKSCJIR78  

Wachimbaji wadogo mkoani Geita wailalamikia ofisi ya madini ya mkoa huo kwa madai ya kuwatimua kwenye eneo la madini waliloligundua siku kadhaa zilizopita huku wakiwasilisha kilio chao kwa waziri mwenye dhamana.https://youtu.be/3L5G_GI4WHY  

Imeelezwa kwamba mikakati ya kukabiliana na matatizo ya macho haitafanikiwa endapo wananchi wenyewe hawatawahi kupata matibabu mapema ili kuzuia upofu utotoni hadi uzeeni. https://youtu.be/7GTQ33OHYHQ 

Rais John Magufuli awataka wamiliki wa mashamba na viwanda vilivyotelekezwa kuviendeleza kabla ya hatua kali kuchukuliwa dhidi yao;https://youtu.be/gRoVPtGQYu0  

Serikali yasema itadhibiti matumizi yasiyo ya lazima ili kusimamia vilivyo fedha za umma katika matumizi yaliyokusudiwa; https://youtu.be/z1vfSCMiM-M  

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata magari mawili yalihusika na wizi katika ofisi ya kamishina wa TRA;https://youtu.be/DW9Vanzv6qY  

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt Jakaya Kikwete awataka wazee mkoani Singida kuunga juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano;https://youtu.be/XQ6MgRBjVRE  

Wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiliano yataja gharama zilizotumika katika ununuzi wa mabehewa 274  ya mamlaka ya reli nchini TRL;https://youtu.be/jvbjeliDXig  

Mkuu wa wilaya ya Monduli, Mhe. Francis Miti  aamuru kuwekwa ndani kwa maafisa wanne wa idara ya ardhi kwa tuhuma ya ubadhlifu wa fedha za umma;https://youtu.be/5Q2fNVhqzJY  

Wakulima wilayani Makete waiomba serikali kutazama upya  bei ya zao  la  Pareto ili mkulima aweze kunufaika na zao hilo; https://youtu.be/DmNtToiwvjI 

Serikali yashauriwa kuzingatiwa suala la mabadiliko ya tabia nchi katika ujenzi wa miundombinu ikiwemo  ya barabara na kilimo; https://youtu.be/lb95LitE0Fk 

Jeshi la polisi kanda ya maalum ya Dar es Salaam yapiga marufuku kwa madereva wa bodaboda kufanya biashara hiyo bila ya kuwa na leseni;https://youtu.be/wI0Yi3Y3i1Q   

Timu ya Azam yajitapa kufanya vizuri katika michezo ya ligi kuu soka Tanzania Bara; https://youtu.be/JiDQDNV6l4A

TFF YAONYA UPANGAJI WA MATOKEO KATIKA LIGI MBALIMBALI NCHINI

$
0
0
"Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limewaonya viongozi wa vilabu, wachezaji, waamuzi na wasimamizi wa mchezo kutojihusisha na upangaji wa matokeo (Match fixing) katika michezo inayoendelea sasa katika ligi za ngazi mbalimbali za nchini" amesema Baraka Kizuguto msemaji wa TFF (Pichani). 

 Kizuguto amesema TFF imejipanga na inasimamia vizuri michezo ya Ligi Kuu (VPL), Daraja la Kwanza (FDL), Daraja la Pili (SDL) na Azam Sports Federation Cup (ASFC) inayoendelea na yoyote atakayebainika kujihusisha na mchezo huo wa upangaji matokeo, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa. 

"Katika michezo yote inayoendelea TFF ina maofisa wake wanaofuatilia kwa ukaribu michezo hiyo, hivyo endapo kiongozi, mchezaji, msimamizi au mwamuzi atabainika kujihusisha na upangaji wa matokeo hatua kali zitachukuliwa", amesema Kizuguto, akiongezea kuwa  TFF inawaomba viongozi, wachezaji, wasimamizi wa michezo na waamuzi kutojihusisha na mchezo huo wa upangaji wa matokeo kwani kufanya hivyo ni kukiuka katiba, sheria na kanuni zinaongoza mpira wa miguu nchini.

Earth Wind & Fire " September " After The Love Has Gone "

JOB OPPORTUNITIES WITHIN THE INTERNATIONAL TELECOMMUNICATION UNION (ITU)

$
0
0


The Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation has received an advert on various job opportunities from the International Telecommunication Union (ITU) for qualified individuals, particularly women to apply. 
The vacancies and application deadline are as follows:-
    i.        1. Information Systems Engineer-Deadline: 18 March 2016;
  ii.        2. Technical Support Officer-Deadline: 15 March 2016;
iii.     3. Head, Least Developed Countries Division-Deadline: 14 March 2016; and
iv.        4. Head, Area Office, Moscow-Deadline: 14 March 2016
For further details on the above mentioned vacancies including application procedures can be accessed at http://www.itu.int/employment/Recruitment/index.html.
“The Ministry encourages qualified Tanzanians to apply”.
Issued by: The Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Dar es Salaam.
05th February, 2015

BAJETI YA MANISPAA YA ILALA YA 2015/2016 NI SH.BIL 55

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
BAJETI ya Manispaa ya Ilala kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ni sh.bilioni 55 kutoka sh.bilioni 30 ya mwaka wa fedha 2014/2016. 

 Akizungumza katika baraza la madiwani katibu wa baraza hilo na Mkurgenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi (Pichani)  amesema kuwa kutokana na bajeti hiyo kuwa juu madiwani wanatakiwa kufanya kazi katika kubuni vyanzo vya mapato. 
 Amesema kuwa baraza ndilo linaweza kufanya bajeti hiyo ikatimia katika makusanyo kutokana na vyanzo vya mapato vilivyopo au kuongeza vyanzo vingine. Mngurumi amesema katika kuanza kufanya kazi kwa baraza la madiwani lazima kamati zipatikane ambapo hilo limefanyika kwa kufanya uchaguzi. 
 Aidha amesema kuendana na bajeti hizo kamati ziweze kujadili bajeti jinsi ya kuweza kupata bajeti itakayosaidia kuendesha na kutoa huduma kwa wananchi wa manispaa ya Ilala. Meya wa Manispa kwa ya Ilala, Charles Kuyeko amewataka madiwani kujadili kwa kina bajeti hiyo katika kamati.

Vodacom yazindua ofa mpya Sasa watanzania kuzungumza kwa saa moja bure kila siku

$
0
0
Sasa ni wakati wa watanzania kuongea, ambapo  kuanzia leo wateja wa Vodacom, mtandao unaongoza nchini wataweza kuongea bure kwa saa nzima kila siku! 
Kupitia ofa yake maalum kwa wateja ya Ongea Bure Deilee, wateja wa Vodacom wataweza kuongea kwa muda wa saa moja bure kila siku. 
Ili kujiunga na ofa hii ambayo haijawahi kutokea nchini, mteja anachotakiwa kufanya ni kuongea kwa dakika 10 kila siku kwa viwango ya malipo vya kawaida na hapo hapo atapata ofa ya kuongea kwa muda wa saa  moja bure ndani ya kipindi chote cha ofa hii kabambe. 
Ofa hii ya Ongea Bure Deilee pia imemuhusisha mwanamuziki nguli wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Diamond Platnumz, ambaye moja ya kibao chake kinachotamba ni  ‘Number One’, ambao pia ni mwito wa simu maarufu kwa watumiaji wa mtandao wa Vodacom. 
Akiongea wakati wa uzinduzi wa ofa hii, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Bw. Ian Ferrao amesema “Ongea Bure Deilee ni ofa ya aina yake kutolewa kwa wateja wa Vodacom popote walipo nchini. Ofa hii imebuniwa kubadilisha maisha ya wateja wetu walio wengi na kuendelea kuyafanya kuwa murua!” 
Aliendelea kusema kuwa Vodacom Tanzania imedhamiria kuendelea kuvuka kile ambacho wateja wake wanakitarajia, kwa  kuwaunganisha kwa viwango nafuu ambavyo wanazoweza kuvimudu, lengo kubwa likiwa ni kuweza kuwainua 
Ofa hii itatolewa kwa wateja milioni moja wa kwanza watakaojiunga kila siku kwa kupiga *149*01# ambapo watakuwa huru kuongea wakati wowote watakao, iwe usiku au mchana, ili mradi watakaowasiliana nao ni watumiaji wa  mtandao wa Vodacom.  
“Huu ni mwendelezo wa kampeni yetu ya Maisha ni Murua  ambayo jitihada zetu katika kuwaletea wateja ofa za kipekee na ambapo kupitia ubunifu wa kutumia mtandao, tunawezesha maisha ya wateja wetu wote nchini kuwa murua. Kama ambavyo tunasema siku zote, tutaendelea toa huduma zinazowawezesha wateja wetu kuwasiliana kwa urahisi na wapendwa wao na hata katika shughuli zao za uzalishaji mfululizo,” aliongeza Ferrao.


Kwa upande wake, Diamond Platinumz, ambaye sasa ni balozi wa Vodacom alisema “Ninayo furaha kuwa sehemu ya kampeni hii kabambe kutoka Vodacom. Nilipopata taarifa kwa mara ya kwanza kuhusu ofa hii nilipata mshtuko na kusema dah, Vodacom imeleta tena bonge la ofa, kwa hakika ofa hii  itaniunganisha na washabiki wangu, marafiki, familia na wafanyabiashara wengine”. 
Aliongeza “Nitawaelezea washabiki wangu, familia na marafiki jinsi wanavyoweza kufanya maisha yao kuwa murua kupitia kampeni hii mpya kutoka Vodacom. Wanachotakiwa kufanya ili kujiunga na kufurahia ofa  ya Ongea Bure Deilee ni rahisi tu, yaani ni kupiga simu *149*01#.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kushoto) akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa promosheni ya”Ongea Deilee” Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea  jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom leo jijini Dar es Salaam,anayeshuhudia kulia ni Balozi wa Vodacom  Tanzania,Nasibu  Abdul (Diamond Platinum)

 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(wapili kushoto) Balozi wa Vodacom  Tanzania,Nasibu  Abdul (Diamond Platinum) Kaimu Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Rosalynn Mworia(kulia) na Zarina Hassan(kushoto)wakionesha mabango  yenye ujumbe wa jinsi  ya kujiunga na Promosheni ya “Ongea Deilee”,wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo  leo jijini Dar es Salaam, Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea  jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao( kushoto)   na Zarina Hassan(Kulia) wakionyeshwa tangazo la promosheni ya”Ongea Deilee” kwenye simu lililofanywa na msaanii wa muziki wakizazi kipya Abdul Nasibu”Diamond Platinum”( katikati) wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo  leo jijini Dar es Salaam, Promosheni hiyo itawawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea  jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(wapili kushoto) akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa promosheni ya”Ongea Deilee” Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi waongeapo jumla ya dakika 10 Vodaocom kwenda Vodacom, leo jijini Dar es Salaam,wengine katika picha kutoka kushoto,Zarina Hassan, Balozi wa Vodacom,Nasibu  Abdul (Diamond Platinum) Kaimu Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Rosalynn Mworia.

DIRA YA DUNIA IJUMAA 05.02.2016

Viewing all 110132 articles
Browse latest View live




Latest Images