Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1107 | 1108 | (Page 1109) | 1110 | 1111 | .... | 3286 | newer

  0 0

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wawili wa mikoa ya Mwanza na Katavi ili kujaza nafasi za Makatibu Tawala wa mikoa hiyo.

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Rais amemteua Kamishna wa Polisi, Clodwing Mtweve (kulia) kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

  Kabla ya Uteuzi huo, Kamishna Mtweve alikuwa Kamishna wa fedha na Utawala wa Jeshi la Polisi Tanzania.

  Balozi Sefue amesema Rais Magufuli pia amemteua Kamishna wa polisi Paul Chagonja (kushoto) kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Madeni Kipande ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

  Kabla ya Uteuzi huo, Kamishna Chagonja alikuwa Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania.

  Aidha, Balozi Ombeni Sefue amesema Rais Magufuli ameamua kuwateua Makamishna hawa wa Polisi kama alivyowateua Majenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania kuwa Makatibu Wakuu wa Wizara, kwa lengo la kujenga nidhamu katika utumishi wa umma.

  Makamishna Clodwing Mtweve na Paul Chagonja pamoja na Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim ambaye ameteuliwa kuwa Balozi Mpya wa Kuwait, wataapishwa leo Jumamosi tarehe 30 Januari, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, saa nne asubuhi.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dar es salaam.


  29 Januari, 2016


  0 0
  0 0

  Na Mwandishi Maalum

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewaasa  vijana wa Kiislam nchini kuzingatia misingi waliyoipata ya elimu ya Kur-an na elimu ya dunia kupambana na matatizo mbalimbali yanayolikwaza Taifa yakiwemo ya rushwa, ufisadi, dawa za kulevya, ujambazi na mengineyo.

  Makamu wa Rais alitoa kauli hiyo jana katika hafla ya kuwapongeza vijana wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur’an Tanzania waliohitimu katika vyuo vikuu mbalimbali vya ndani na nje ya nchi iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam,

  Samia alisema anaamini kwamba misingi hiyo itawapa miongozo ya kupambana na matatizo hayo na hivyo kumwezesha kijana kuwa kioo cha jamii yeyote ile atakayoishi na kufanya nayo kazi.

  Makamu wa Rais aliwaasa pia vijana hao waliohifadhi Kur-an na wasomi kutenda matendo mema katika maisha yao kwa kuwa elimu waliyoipata ni daraja na heshima waliyonayo kwa Mungu na hapa Duniani.

  “Heshima mliyopata ya kuwa mabingwa wa elimu ya Kur-an na elimu ya sayansi ya dunia, iwape muongozo katika maisha yenu,” alisema Samia na kuongeza “Kile mlichobeba, ujumbe mzuri na mzito uliomo kwenye Kur-an mkioneshe kwa vitendo, na pia vitendo vyenu vitoe tafsiri/taswira ya kuonesha nyinyi ni nani.”

  Makamu wa Rais alitumia fursa hiyo kuipongeza Jumuiya hiyo chini ya uenyekiti wa Sheikh Othman Kaporo kwa kuanzisha mpango huo madhubuti zaidi ya miaka 30 iliyopita wa kuwalea vijana kiimani na kuwaendeleza kielimu, ili hatimaye walinufaishe Taifa lao.

  Mapema, akizungumza katika hafla hiyo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi aliwaomba Mabalozi wa nchi za Kiarabu nchini kuangalia uwezekano  wa kuanzisha shule itakayofundisha lugha ya kiarabu.

  Alisema Waislamu wengi wanasoma Kur-an lakini hawajui kile wanachosoma kwa sababu ya kutokujua lugha ya Kiarabu ambayo ndiyo lugha ya Kur-an.

  “Wengi tunasoma Kur-an, lakini hatujui kwa sababu hatujui Kiarabu ambayo ndiyo lugha ya Kur-an. Ni wajibu wa serikali kufundisha Kiarabu…. Lakini mjue nchi yetu haina dini, watu wake wana dini; sasa Mabalozi, nchi zenu za Kiislam zina wajibu wa kufundisha wenzenu Kiarabu,” alisema Alhaji Mwinyi na kuongeza

  “Ndugu zetu mtufunze Kiarabu, mtufungulie skuli ya kusomesha lugha ya Kiarabu. Waingereza wanayo inaitwa British Council, wanafundisha lugha ya Kiingereza; jambo hili mlifikirie, lugha ya Kiarabu ni lugha ya Kur-an.”

  Katika hafla hiyo, pamoja na kuonesha video ya safari ya Kur-an nchini Makamu wa Rais alitoa vyeti kwa vijana wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Kur-an Tanzania wapatao 20 waliohitimu katika vyuo vikuu mbalimbali vya ndani na nje ya nchi. 

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizung4umza na wanahabari ofisini kwake kuhusu ugeni wa Waziri mkuu ,Majaliwa Kassim Majaliwa mkoani Kilimanjaro.


  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  WAZIRI mkuu, Majaliwa Kassimu Majaliwa, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ibada maalum ya kumuingiza kazini askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kiluteri Tanzania(KKKT),Askofu Dk Frederick Shoo katika kanisa kuu la Moshi mjini.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla,amesema waziri mkuu anatarajiwa kuwasili mkoani Kilimanjaro kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) ambapo atapokea taarifa ya mkoa kabla ya kufanya shughuli za kanisa.

  Alisema waziri mkuu hataongozana na waziri yeyote wa serikali ya awamu ya tano bali wasaidizi wake na baada ya ziara hiyo maalum atarejea Dodoma kuendelea na shughuli za serikali.

  Ibada hiyo maalumu itajumuisha viongozi mbalimbali wa serikali ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro sanjari na viongozi wa madhehebu tofauti ya dini,wadau wa maendeleo,waumini na wananchi kwa ujumla.

  Kutokana na ujio huo wa waziri mkuu, mkuu wa mkoa,aliwataka wananchi hususani katika wilaya za Hai na Moshi kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo ambaye pia atapokea changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa

  Kadhalika waziri mkuu anatarajiwa kutoa maelekezo ya serikali kulingana na changamoto zitakazojitokeza wakati anapewa taarifa ya mkoa.

  Dk Shoo ambaye pia ni askofu wa dayosisi ya Kaskazini amechaguliwa kuongoza kanisa hilo kwa miaka minne na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na mtangulizi wake askofu Dk Alex Malasusa ambaye amemaliza muda wake wa uongozi.

  Askofu Dk Shoo alichaguliwa mapema mwezi Agosti mwaka jana katika mkutano mkuu wa 19 wa kanisa hilo uliofanyika chuo kikuu cha Tumaini jijini Arusha baada ya kuwashinda wenzake wawili.

  Uchaguzi wa nafasi hiyo uliwashindanisha askofu Dk Stephen Munga wa dayosisi Kaskazini Mashariki na Askofu Charles Mjema wa dayosisi ya Pare.

  0 0


  0 0
 • 01/30/16--19:00: NGOMA AZIPENDAZO ANKAL

 • 0 0   Vijimambo ilizaliwa Januari 31, 2010 na kuzinduliwa Oktoba 23, 2010 na aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Maajar. Picha ni siku ya uzinduzi ukumbi wa Mirage  uliopo Hyattsville, Maryalnd.
  Hapa Balozi Mwanaidi Maajar akiwa mgeni rasmi miaka 2 ya Vijimambo iliyofanyika Machi 31, 2012 ukumbi wa Mirage uliopo Hyattsville, Maryalnd.
   
  Rais mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo iliyofanyia Julai 6, 2013 katika ukumbi wa Hampton Inn uliopo Capitol Heights. Maryland.
  Mwenyekiti wa Vijimambo akiwapokea wasanii Shilole na Masanja waliokuja kunogesha sherehe ya miaka 3 ya vijimambo.
  Mhe. Nyarandu (kulia) akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo iliyofanyika Septemba 13, 2016 Hotel ya Growne Plaza iliyopo Rockville, Maryland.
  Wasanii Aunty Ezekiel na Cassim Mganga wakija kunogesha miaka 4 ya Vijimambo, kushoto ni NY Ebra akipata ukodak moment na wasanii hao walipotembelea New York City.
  Cassim Mganga na Aunty Ezekiel wakitia saini kitabu cha wageni Ubalozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York siku walipotembelea pande za New York City, kulia ni Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Tuvako Maniongi

  0 0

   The Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS)  Medical Center is the first building to be constructed as part of the Mloganzila New Campus of the premier national university in Tanzania. 

  It is the largest general hospital in East Africa, which provides an advanced medical system to fulfill public health and medical needs, nurture the training of medical specialists, and improve the level of medical services specific to the nature and environment of Africa. 
  The façade of the building, to which a passive system is applied, has distinct regional characteristics such as deep window sills and light shelfs.
  Overall the design is quietly associated with cultural characteristics of the region, and is inspired by the local baobab tree that is called the tree of cure and life. Entering the main entrance under the pergola that shields against the strong African sunlight, and passing by the landscape space that emphasizes the healing power of Nature, one experiences a clear and functional flow of building users at the lobby that attracts beautiful nature inside.
  Satellite image from Google Maps.

  0 0


  0 0
  0 0

  Mwigizaji bora wa kike wa Komedi Swahiliwood Salma Jabu ‘Nishabebee’ anawashukru wadau wote wa tasnia ya filamu kwa ujumla wake kutokana na mchango wao ambao wamempa kupitia kazi zake ambazo ameshiriki katika kuigiza na kutayarisha  filamu zaidi ya 8 chini ya kampuni yake ya Nisha’s Film Productions. 
  Akiongea na wanahabari msanii huyo ambaye ana sifa za kimataifa amesema kuwa baada ya filamu yake ya Kiboko Kabisa inamfungulia mwaka na kuwa kazi yake ya awali kuingia sokoni leo siku ya Ijuma,  anasema kuwa amejifunza mengi na anatoa shukrani kwa wadau wa filamu ambao wamekuwa bega kwa bega katika kuhakikisha anasonga mbele kisanaa. 
  “Nawashukru wote wanahabari jamaa zangu hata wale ambao wamekuwa wakinishauri kupitia njia mbalimbali, kila mtu kwangu ana mchango mkubwa sana naheshimu hilo kwa kila mtu kwa nafasi aliyo nayo na kuhakikisha wanafanya jambo kubwa kwa ajili yangu Asanteni sana na Mungu awabariki,”anasema Nisha. 
  Aidha msanii huyo ameamua kuanzisha utaratibu wa kutoa taarifa za maendeleo ya kazi yoyote ambayo atakuwa akiifanya na taarifa kuwafikia wapenzi wa filamu nchini nzima na kuwa ndio njia ya wasanii kujenga mahusiano mema na watazamaji wao ambao kuna wanataka kujua maisha ya wasanii ya kawaida nje ya uigizaji lakini si rahisi.
   Anawashukru sana wapenzi wa filamu Swahiliwood ambao siku zote wamekuwa wakimuunga mkono katika kazi zake ambazo zimepita kama vile Gumzo, Mtaa kwa Mtaa na leo hii anaingia na filamu ya Kiboko Kabisa sinema hiyo imewashirikisha wasanii wakali katika tasnia ya filamu King Majuto, Nishabebee, Ben Blanco, Mzee Jengua.
  Filamu ya Kiboko kabisa imeingia sokoni siku ya ijumaa ya tarehe 29.January . 2016 na inapatikana nje nzima anaomba kila mwananchi ajenge tabia ya kununua kazi ambazo ni halali na si kazi bandia ambazo zinashusha maisha ya wadau wa filamu.
   Nisha ambaye kwa sasa ni kipenzi cha watoto na wapenzi wa komedi anasema kuwa anatamani kumfikia kila mtu kwa kuongea naye ana kwa ana lakini si rahisi waamini kuwa anawajali ni rafiki wa kweli kwa kila raia wa Tanzania kwani anaamini wote ni ndugu zake.
  Nisha mwigizaji bora wa Kike kushinda tuzo za action & cut Views Choice Awards (ACVA 2013/2014) amekuwa ndio msanii pekee ambaye kila kazi yake anapoifanya na kuingia sokoni huwa gumzo kama jina la moja ya filamu ambayo aliwahi kutengeneza ya Gumzo. 
  Kwa mwaka huu Nisha amesema kuwa katika sherehe zake muhimu ambazo huzifanya atahakikisha anakula pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, akina mama wajane na watu walio katika shida kubwa kwenye maisha ya kawaida.
  Aidha msanii huyo anachukua muda kuwashukru wanahabari kwa kuwataarifu wapenzi wa kazi zake kwani anaamini bila wao wana mchango mkubwa sana hadi alipofika na anaendelea kuwaheshimu na kutoa ushikiano kwao katika kuhabarisha jamii.

  0 0
 • 01/30/16--22:30: Article 18


 • 0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza mbio za Wabunge za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon zilizoanzia Bungeni hadi uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Januari 30, 2016. Kushoyo kwake ni Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson. Mwansasu.
  Baadhi ya Washiriki wa mbio za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon wakishiriki mbio hizo mjini Dodoma Januari 30, 2016.
  Mmoja wa wapigapicha walioshiriki mbio za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon alilazimika kuomba msaada kwa askari wa usalama barabarani Mjini Dodoma Januari 30, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza wa mbio za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon upande wa wanaume, Emmanuel Giriki kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Januari 30, 2016. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


  MAJALIWA ATAKA WATANZANIA WAFUNGUE SPORTS ACADEMY

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wafungue shule za michezo yaaniSports Academy ambazo zitalenga kukusanya wahitimu wa shule za msingi na sekondari na kuwafundisha sayansi ya michezo.

  Ametoa wito huo jana mchana (Jumamosi, Januari 30, 2016) kwenye uwanja wa Jamhuri wakati akizungumza na mamia ya viongozi na wananchi mbalimbali walioshiriki mashindano ya mbio za nusu marathon (km. 21 na km. 5) zilizofanyika mjini Dodoma. Mashindano hayo yalijulikana kama “HAPA KAZI TU HALF MARATHON”.

  “Michezo ni sayansi kwa hiyo tunahitaji kuwafundisha vijana wetu sayansi ya michezo na kuwapa mbinu tofauti za kufaulu kwenye mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa,” alisema Waziri Mkuu.

  Alisema wapo Watanzania wachache ambao wamethubutu kufungua shule za michezo na kuwataja Filbert Bayi (shule ya Filbert bayi) na Kanali Mstaafu Iddi Kipingu (shule ya Lord Baden). “Tumeona matunda ya sports academy hizo kwani zimeibua vijana ambao tayari wameshiriki michuano ya kimataifa,” alisema.

  Alisema michezo ina nafasi kubwa ya kulitangaza Taifa la Tanzania na ndiyo maana Serikali imeamua kuimarisha sekta ya michezo, utamaduni, sanaa na habari. 
  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimpongeza kijana Joseph Stanford ambaye ameamua kutembea kwa miguu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kumuunga mkono Rais Dk. John Pombbe Magufuli kwa utendaji wake wa kazi. 
  Kijana Joseph (19) ambaye alikuwepo uwanja wa Jamhuri, alisema ametumia siku 13 tangu aanze safari hiyo ikiwa ni wastani wa km. 80 kwa siku. “Ninatembea kwa saa 12 kwa siku na ikifika jioni natafuta mahali penye mji na kupumzika,” alisema. 
  Joseph ambaye amehitimu kidato cha nne mwaka jana katika shule ya sekondari ya Mtoni iliyoko Mwanza-Mabatini, amesema hivi sasa anasubiri matokeo ya mitihani yake lakini ameguswa na utendaji kazi wa Rais Magufuli ndipo akaamua kuanzisha matembezi hayo ili kumuunga mkono.

  Alipoulizwa anafanyaje anapopita kwenye maeneo ya misitu mikubwa au mapori ya kutisha, Joseph alisema hajakutana na misitu mikubwa ya kutisha isipokuwa kwenye milima ya Sekenke na eneo moja kabla ya kuingia mkoa wa Dodoma.

  Joseph amesema anatarajia kuanza safari ya kuelekea Dar es Salaam kesho kutwa (Jumanne, Februari 2, 2016) kwani anasubiri kukutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Nape Nnauye hapo kesho.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,

  JUMAPILI, JANUARI 31, 2016.

  0 0

   Taswira mbalimbali za vijana kutoka vilabu mbalimbali vya jogging walipokusanyika kwa mazoezi ya pamoja katika kiota cha maraha cha Dar Live Mbagala jijini Dar es salaam leo asubuhi
   Mazoezi na nyimbo za hamasa
   Mchakamchaka
  Mazoezi kwa furaha na afya

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewaagiza Makandarasi wa ujenzi wa barabara kutoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi kwa kuzingatia haki, usawa na taaluma ya mtu kama ilivyoelekezwa kwenye sheria ya ajira hapa nchini ili kuwezesha kazi za ujenzi kukamilika kwa wakati.

  Amesema hayo wilayani Chemba Mkoani Dodoma wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Dodoma-Babati ambao ujenzi wake umegawanywa katika sehemu tatu ambazo Dodoma-Mayamaya Km. 43.65, Mayamaya-Mela Km. 99.35 na Mela-Bonga Km. 88.8 ili kuharakisha kasi ya kukamilika kwake.

  “Hakikisheni leo hii mnawapa mikataba halali kwa mujibu wa taaluma zao na inayozingatia sheria za Tanzania ili kujega uhusiano mwema wa kiutendaji na hivyo kazi zenu zitakuwa na tija na ubora unaokusudiwa”, amesema Prof. Mbarawa.

  Waziri Mbarawa amekagua madaraja makubwa manne katika barabara hiyo ambayo ni Daraja la Kelema lenye urefu wa mita 200, Msui lenye urefu wa mita 45, Kingali lenye urefu wa mita 30, na Mela lenye urefu wa mita 30 na kuhimiza kasi ya ujenzi wa madaraja hayo kabla ya mvua za masika.

  Barabara ya Dodoma-Babati ni sehemu ya Barabara Kuu ya Kaskazini (The Great North Road) inayoanzia Cairo nchini Misri hadi Cape town Afrika Kusini.

  “Barabara hii ni kiungo muhimu cha miundombinu ya barabara za Tanzania kwani inaunganisha mikoa maarufu ya kilimo ya nyanda za juu kusini, nyanda ya kati na nyanda ya kaskazini na pia ni kiungo kikuu cha kwenda nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

  Kwa upande wake Eng. Deusdedit Kakoko kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) makao makuu, amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa wamejipanga kuhakikisha barabara hiyo ujenzi wake unakamilika kwa wakati ili kufungua fursa za kiuchumi na kuunganisha kirahisi mkoa wa Dodoma, Manyara na Arusha.

  “Mheshimiwa Waziri tutaendelea kusimamia mradi huu umalizike kwa wakati na muda uliopangwa na hatutaendelea kuvumilia wale wote wasioweza kumaliza mradi huu kwa wakati”, amesisitiza Eng. Kakoko.

  Waziri Mbarawa amezungumzia umuhimu wa ubora wa barabara zinazojengwa na makandarasi wote nchini kudumu  kwa muda mrefu ili thamani ya fedha inayotumika kuwalipa iwiane na huduma inayotolewa.

  Hadi sasa sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya (Km. 43.65), ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 80 wakati barabara ya Mayamaya-Mela (Km. 99.35), ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 52.2  na ujenzi wa barabara Mela-Bonga (Km. 88.8), umekamilika kwa asilimia 45.17 ambapo ujenzi wa barabara yote Dodoma-Babati unatarajiwa kukamilika baadaye mwakani.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

   Kazi ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela yenye urefu wa Km. 99.35 ukiendelea.

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akimuagiza Mkandarasi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela kampuni ya China Henan International Corporation Group Ltd (hayupo pichani) kuwapa mikataba bora ya kazi wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo (wanaomsikiliza).

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) akiagiza kuwekwa lami juu ya Daraja la Kola Wilayani Kondoa mkoani Dodoma ili kuanza kupitika na kupunguza usumbufu wa magari wakati wa mvua. (kushoto) ni Meneja ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga (Km.88.8) Eng. Stone Cheng na (Kulia) ni Mhandisi Mshauri wa barabara hiyo.

   Mkandarasi wa SynoHydo Corporation Ltd akimkabidhi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa Km. 43.65 inaojengwa kwa kiwango cha lami

  Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) kuhusu hatua ya ujenzi iliyofikiwa katika barabara ya Mela-Bonga (Km. 88.8) inayojengwa kwa kiwango cha lami, (Wa pili kulia) ni Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Godfrey Kombe na (wa kwanza kushoto) ni Eng. Deusdedit Kakoko kutoka TANROADS makao makuu.


  0 0
 • 01/31/16--00:00: ZIFF's Call for artists
 • ZIFF is East Africa’s largest film, music and arts festival, bringing together talent from all over the world for a Zanzibar Tamasha!

  ZIFF puts together the island’s best parties. Bringing live music, dance, DJs and performances on a number of platforms. A carnival fever hits Zanzibar for 10days! We bring musicians together from all over Africa, and the world at large. 
  Zanzibar International Film Festival is currently calling for Musicians and Performing Artists to send their requests to be part of ZIFF 2016. Applying is free. Please submit you sample works by sending a YouTube link, Vimeo, Sound Cloud, pictures and Artist profile to mpa@ziff.or.tz.

  Deadline: 31st March, 2016 at 12Noon.

  0 0

  SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa auagiza uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha dawa zinapatikna katika hosptali ya mkoa ya Mawenzi;https://youtu.be/f2hoFZV9qxk
   SIMU.TV: Serikali yafanikiwa kukusanya kodi zaidi ya trioni moja kwa mwezi wa kwanza kiasi ambacho ni kikubwa kulinganisha na mwezi Disemba;https://youtu.be/Tx0b2Y7P_1M
   SIMU.TV: Inaelezwa kuwa mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro za sababisha zoezi la kuitoa ndani ya maji MV Kilombero kukwama;https://youtu.be/2LD3eHis4ow
   SIMU.TV: Serikali yaiagiza bohari ya dawa nchini MSD kuweka rangi maalum katika dawa zinazonunuliwa na serikali ili kuthibiti wizi; https://youtu.be/5wLCh_2k23w
    SIMU.TV: Rais John Magufuli aagiza kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi kwa tuhuma kutokana na utata wa ujenzi wa barabara wilayani humo; https://youtu.be/JinxH3O_Q_4
   SIMU.TV: Wakazi wa jijini Dar es Salaam washauriwa kuendelea kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kutaka kufanya usafi kila mwisho wa mwezi;https://youtu.be/0b-sNdaWXA8
   SIMU.TV: Timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam yaangukia pua baada ya kunyukwa goli 2-0 na timu ya Coastal Unioni ya jijini Tanga; https://youtu.be/AHSLnOLlgj8
   SIMU.TV: Serilkali visiwani Zanzibar yawataka wananchi kuacha kujenga karibu na vyanzo vya maji ili kuepuka maafa kama vile mafuriko; https://youtu.be/BZhpecxxUHA
   SIMU.TV: Serikali yaanza utekelezaji wa kuthibiti wizi wa dawa inazozinunua kwa kuweka nembo maalum; https://youtu.be/i4y78bjsotQ
   SIMU.TV: Uboreshaji hafifu wa mitaro ya maji na taka ngumu zachangia kuziba mitaro ya maji na kusababisha mafuriko jijini la Dar es Salaam; https://youtu.be/_xUEq2tElFQ
   SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Musoma mkoani Mara awaagiza watendaji kata kuwabaini wananchi wanaotumia vibaya fedha za TASAF ili wachukuliwe hatua kali;https://youtu.be/Auaq1HkiTQk
   SIMU.TV: Serikali ilitaka shirikisho la mchezo wa riadha nchini kuwa na mkakati sahihi katika kuinua mchezo huo hapa nchini; https://youtu.be/Tk0vcDNWtBg  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili mkoani Kilimanjaro na kufanya ziara kushtukiza kwenye hospitali ya rufaa ya Mawenzi ambayo ni hospitali ya mkoa huo. 
  Waziri Mkuu Majaliwa ambaye mara baada ya kuwasili Ikulu ndogo ya Moshi mjini jana jioni (Jumamosi, Januari 30, 2016) alipangiwa kupokea taarifa ya mkoa huo, alimweleza Mkuu wa mkoa huo kwamba anataka kufanya ziara katika hospitali hiyo na kuwaomba radhi watendaji waliokuwa wanasubiri taarifa ya mkoa iwasilishwe. 
  “Mheshimiwa Waziri Mkuu ameamua kufanya ziara katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi ambayo ni hospitali yetu ya mkoa na atakuja kupokea taarifa ya mkoa wetu tukishatoka huko,” alisema Mkuu wa mkoa huo, Bw. Amos Makalla. 
  Mara baada ya kuwasili hospitalini, Waziri Mkuu alielekeza apelekwe kwenye chumba cha upasuaji (theatre) huku akimuuliza maswali kadhaa Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Bingileki Lwezaula. 
  Katika chumba cha upasuaji ilibainika kuwa kuna vyumba vitatu  vya kufanyia upasuaji lakini kinachotumika ni kimoja tu kwa sababu vingine havina dawa za kulaza wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji (anesthesia) licha ya kuwa jengo la upasuaji lina mwaka sasa tangu lilipozinduliwa Februari, 2015 na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete. 
  Akiwa katika wodi ya utabibu ya wanawake, Waziri Mkuu alipokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa juu ya kukosekana kwa dawa hospitalini hapo. Afisa Muuguzi wa wodi hiyo, Bi. Anjela Mwakalile alisema wametuma maombi ya kupatiwa dawa kutoka MSD lakini bado hazijafika. 
  Hali hiyo ilijitokeza pia kwenye wodi ya watoto. Akizungumza na wazazi wa watoto aliowakuta wamelazwa, mama mmoja alimweleza Waziri Mkuu kwamba sera ya Taifa inasema watoto wachanga hadi walio na miaka mitano wanapaswa kupata matibabu bure, lakini wao hapo hospitalini wanalazimika kununua dawa. 
  Waziri Mkuu alimtaka Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Mtumwa Mwako kubadili haraka mfumo wa uagizaji wa dawa baada ya kupokea maelezo ya Dk. Lwezaula kwamba wametuma maombi MSD tangu miezi miwili iliyopita lakini hadi sasa hawajaletewa dawa walizoomba. 
  “RMO ni kwa nini hamuwezi kuagiza dawa nyingi (bulk) kwa magonjwa ambayo mnajua yanajirudia mara kwa mara ili wagonjwa weu wasipate usumbufu? Hii ni hospitali ya mkoa na mgao wa dawa unaopaswa kuja hapa ni wa level ya mkoa? Haiwezekani mnafanya hivyo ili wagonjwa wajinunulie dawa kutoka kwenye maduka yenu?,” alihoji Waziri Mkuu.

  “Hii hospitali ni kubwa kuliko idadi ya wagonjwa wanaofika kutibiwa hapa na hii ni kwa sababu wengi wao wanaishia kwenye hospitali za wilaya. Kwa hiyo mlipaswa kuwa na dawa za kutosha. Wodini nimekuta wagonjwa wachache katika wodi nilizopita, ina maana mna ahueni hapa… mnao madaktari wa kutosha, wataalamu 12, lakini ni kwa nini hakuna dawa za kutosha?” alihoji. 
  Wakati akitoka wodi ya watoto, kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Bakari Hussein ambaye anauguza mgonjwa wake hospitalini hapo alimweleza Waziri Mkuu kwamba dawa pekee wanayopatiwa kwenye hospitali hiyo ni paracetamol tu. 
  “Hapa dawa ya bure pekee unayopata ni paracetamol tu. Dawa nyingine zote unaandikiwa ukanunue maduka ya nje. Na ukizipata ni kati ya sh. 60,000/- hadi 70,000/- kwa mkupuo. 
  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Severine Kahitwa apeleke maombi ya kupatiwa mafundi wa mashine zaxray haraka iwezekanavyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

  Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo baada ya kukuta mashine kubwa kwenye chumba cha mionzi cha hospitali haifanyi kazi na inayofanya kazi ni ndogo haiwezi kufanya baadhi ya vipimo. 
  Akitoa maelezo mbele ya Waziri Mkuu, Mkuu wa kitengo cha Radiolojia, Dk. Ephraim Minja alisema: “Tuliambiwa spare parts zimekwama bandarini, na vifaa hivyo vikipatikana vitaweza kutatua tatizo lililopo.” 
  Alipoulizwa na Waziri Mkuu kabla ya mashine ya kuharibika alikuwa akihudumia wagonjwa wangapi, Dk. Minja alisema kwa wastani alikuwa akihudumia wagonjwa 60 hadi 70. “RAS fuatilia mafundi kwa Katibu Wizara ya Afya. Hii ni hospitali kubwa tena ya Serikali kwa hiyo haiwezekani wagonjwa waje hapa na kuambiwa waende kupata vipimo mtaani,” alisema.
    
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,

  JUMAPILI, JANUARI 31, 2016.
  Waziri mkuu akiwasili katika hosiptali  ya rufaa ya Mawenzi alipofanya ziara  ya  kushtukiza.
  Waziri mkuu akitizama chumba cha kupigia  pcha za mionzi (X Ray) katika hospitali  ya rufaa  ya Mawenzi.
  Waziri mkuu akiwa wodi ya watoto alipotembelea kujionea namna ambavyo  wagonjwa wanahudumiwa.
  Waziri mkuu Majaliwa akizungumza jambo na mganga  mkuu wa mkoa  wa Kilimanjaro, Dkt Mtumwa  Mwako.
  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akitoa taarifa ya mkoa kwa Waziri  Mkuu  Kassim Majaliwa. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Dkt. Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi  January 30, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Luteni Jenerali Venance Salvatory  Mabeyo  kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Ikulu jijini Dar es salaam January 30, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza  Ikulu jijini Dar es salaam January 30, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam  January 30, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  na viongozi wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi  katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya  Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam  January 30, 2016.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1107 | 1108 | (Page 1109) | 1110 | 1111 | .... | 3286 | newer