Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1106 | 1107 | (Page 1108) | 1109 | 1110 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wanne kutoka kushoto), akimkabidhi kijana Diana Mosha, msaada wa vifaa mbali mbali vya kutengenezea keki kupitia mpango wa Airtel ‘FURSA Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao Ilala jijini Dar Es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa Airtel waliohudhuria hafla hiyo.
   Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (pili kushoto), akimkabidhi kijana Diana Mosha, msaada wa vifaa mbali mbali vya kutengenezea keki kupitia mpango wa Airtel ‘FURSA Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao Ilala jijini Dar Es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni (kulia) ni Meneja mauzo wa Airtel Dar Es Salaam ,James Moillo na wafanyakazi wengine wa Airtel.
   Kijana Diana Mosha (kushoto), akifafanua jambo baada ya kukabidhiwa msaada wa vifaa mbali mbali vya kutengenezea keki kupitia mpango wa Airtel ‘FURSA Tunakuwezesha’, kwa meneja masoko kanda ya Dar Es Salaam James Moillo (pili kushoto) katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao Ilala, Dar Es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni meneja masoko wa Airtel kanda ya Mbagala, Saleh Safi akifuatiwa na meneja wa huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.


  KUFUATIA uzinduzi wa hivi karibuni wa Airtel FURSA msimu wa mbili, Airtel inaendelea kugusa maisha ya vijana nchini Tanzania na kuwawezesha kufikia matarajio yao ya ujasiriamali. Leo Airtel FURSA imemfikia kijana Diana Moshi, mwenye umri wa miaka 22 anayejihusisha na upikaji wa keki jijini Dar Es Salaam. 

  Diana amepokea ruzuku katika mfumo wa vifaa vya kufanyia kazi vikiwemo trei za keki, mashine za kuchanganyia unga wa keki, mashine za kupambia keki, jokofu na jiko la gesi .Mbali na vifaa hivyo Diana atapokea mafunzo maalum ya ujasiriamali na ushauri wa biashara ya keki kutoka kwa mtaalam maalum na maarufu wa biashara ya keki hapa jijini.

  Kutoka alipoanzia akiwa na mtaji mdogo sana wa kuanzia biashara, Diana aliendelea kuwa makini na kutilia mkazo wa ndoto yake. Pamoja na ukosefu wa vifaa Diana hakukata tamaa bali alijifunza kupitia kwa jirani na kukodisha vifaa vya kufanyia kazi kutoka kwa wafanyabiashara wengine. Akiwa na furaha kubwa alisema; "Niliona Airtel FURSA kama fursa ambayo inaweza kusaidia kupunguza mapambano na kuongeza matumaini yainua biashara yangu, ninashukuru kwamba leo Airtel FURSA imenifikia na kuweza kubadilisha maisha yangu. Nimeanza nikiwa na mtaji mdogo sana lakini leo Airtel imenidhihirishia kwamba kufanya kazi kwa bidii na uvumilivu inaweza kutimiza ndoto yako ".

  Diana aliahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa vile yeye sasa anauwezo kwa kuwa na zana madhubuti za kuzalisha zaidi. "Ninaamini katika kipindi cha muda mfupi nitaweza kuzalisha zaidi na kuajiri wengine ili kusaidia biashara yangu. Mimi ni shuhuda wa kweli kabisa wa walengwa wa Airtel FURSA walioomba na kupata msaada . Ninaahadi kusaidia jamii yangu inayonizunguka kwa sababu ninaelewa fika ni jinsi gani vijana wenzangu wanavyopata tabu huko mtaani na sitaacha kuendelea kuwahamasisha. "

  Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa
  Bayumi alimpongeza Diana kwa kufwata ndoto zake na kuhimiza vijana wengine kuiga mfano wa Diana. Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano Bi Bayumi alisema "Diana ametutia nguvu na kuweza kushiriki sehemu ya safari ya ndoto zake kwani ameanza akiwa hana kitu , si kwa mtaji tu lakini hata uzoefu wa kufanya biashara hii. Lakini leo hii ameweza kuuza keki kupitia mitandao na kujipatia hela. Tunaamini vifaa tunavyompatia Diana leo vitabadilisha maisha yake na kuinua biashara yake na kuongeza wateja wengi zaidi.

  Tunawahimiza vijana wengi hapa nchini kuchangamkia Airtel FURSA si tu inayotolewa kwa vitendea kazi bali na elimu ya biashara ambayo imekuwa ikitolewa nchi nzima hapa Tanzania, pia kwa kupata maelekezo ya biashara kupitia mitandao yetu ya kijamii inayosadia kuelekeza vijana jinsi ya kukuza biashara zao, kujenga fursa kwa ajili ya wengine na kuwa na huduma na jami zao zinazowazunguka.

  Airtel, kwa mara nyingine tena katika mpango wake wa Airtel FURSA umeahidi kuendelea kugusa maisha ya wa Tanzania kwa kuwawezesha vijana kupitia Airtel FURSA. Hadi sasa Airtel imeweza kufikia vijana zaidi ya 2,500 nchini Tanzania na na imeahidi kufikia vijana zaidi ya 1500 katika kipindi cha miezi sita ijayo.

  0 0

  NA VICTOR MASANGU, PWANI
  SHULE ya msingi ya mkoani iliyopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani kwa sasa inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa madawati, madarasa pamoja na miundombinu ya madarasa kuwa mibovu na vyoo kuwa na nyufa hali ambayo inatishia usalama wa maisha yao kutokana na mazingira wanayosomea ni hatarishi na sio rafika kwao. 

  Hali hiyo imebainika baada ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikio kufanya ziara ya kushitukiza katika shule hiyo na kuweza kujionea ubovu wa majengo hayo wanayoyatumia katika shule hiyo kuwa ni chakavu kutokana na kutofanyiwa ukarabati kwa kipindi kirefu.

  Mkuu wa shule hiyo Pregua Mseja amekiri kuwepo kwa hali hiyo ambapo alisema kwamba licha ya shule hiyo kukabiliwa na changamoto ya ubovu wa miundombini lakini bado inakabiliwa na uhaba wa madawati pamoja na nyumba sita vya madarasa vina vuja maji kutokana na mapaa yake kutoboka hivyo wanafunzi wananyeshewa na mvua.

  “Kwa sasa Mkuu wa Mkoa shule hii ina changamoto nyingi sana kwani licha ya ubovy wa majengo pamoja na vyoo bado mambo ya msingi yanahitajika kwa shule hii ili wanafunzi waweze kujisomea katika mazingira mazuri kwa mfano sasa kuna madasara sita ambayo yanavuja kweli wanafunzi wananyeshewa na mvua,” alisema Mseja.

  Akizungumzia kuhusiana na fedha ambazo tayari wameshakwisha zipokea katika shule hiyo kutoka serikalini kwa ajili ya uendeshaji wa elimu bure alisema kwamba wameshapokea kiasi cha shilingi laki 437 ambazo zitatumika katika mahitaji mbali mbali ikiwemo suala la utawala michezo pamoja na mahitaji mengine ya msingi.

  Baada ya Mkuu wa Mkoa kumaliza kufanya ukaguzi katika maejengo ya utawala, madarasa ya wanafunzi pamoja na kutembelea vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi hao alitoa agizo kwa halmashauri ya mji wa Kibaha kuhakikisha wanatafuta fedha haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kukarabati miundombinu hiyo ili kuwatendea haki ya msingi watoto hao.

  Ndikiro alisema kuwa majengo hayo yanatakiwa kufanyiwa ukarabati wa haraka na kwamba halmashauri ya mji wa Kibaha ihakikishe inatafuta fedha ambazo zitaweza kusaidia katika kukarabati miundombinu hiyo ya majengo ili watoto waweze kujisomea katika mazingira mazuri.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kibaha Mauld Bundala aliunga mkono kauli ya Mkuu wa Mkoa ambapo alisema anaskitishwa sana na kuona wanafunzi wnasoma katika majengo amabyo yana nyufa kwani kunaweza kupelekea watoto hao kuangukiwa na majengo.

  Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kibaha Grory Diamunye ambao nao walikuwepo katika ziara hiyo alisema atalivalia njuga suala hilo na kuahidi kulishughulikia haraka sana ili wanafunzi hao waweze kusoma katika mazingira ambayo ni rafiki kwao kwani kufanya hivyo kutaweza kuwafanya waongeze hata kiwango cha ufaulu.

  Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 764 kwa sasa bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madawati, madarasa, matundu ya vyoo, uchakavu wa miundombinu ya majengo ahali mbayo inwapa wakati mgumu wanafunzi hao kusoma katika mazingira ambayo ni hatari kwa masiha yao.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wawili wa mikoa ya Mwanza na Katavi ili kujaza nafasi za Makatibu Tawala wa mikoa hiyo.

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Rais amemteua Kamishna wa Polisi, Clodwing Mtweve kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

  Kabla ya Uteuzi huo, Kamishna Mtweve alikuwa Kamishna wa fedha na Utawala wa Jeshi la Polisi Tanzania.

  Balozi Sefue amesema Rais Magufuli pia amemteua Kamishna wa polisi Paul Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Madeni Kipande ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

  Kabla ya Uteuzi huo, Kamishna Chagonja alikuwa Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania.

  Aidha, Balozi Ombeni Sefue amesema Rais Magufuli ameamua kuwateua Makamishna hawa wa Polisi kama alivyowateua Majenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania kuwa Makatibu Wakuu wa Wizara, kwa lengo la kujenga nidhamu katika utumishi wa umma.

  Makamishna Clodwing Mtweve na Paul Chagonja pamoja na Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim ambaye ameteuliwa kuwa Balozi Mpya wa Kuwait, wataapishwa kesho Jumamosi tarehe 30 Januari, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, saa nne asubuhi.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam.
  29 Januari, 2016


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha J. Mshomba akitoa mada kwa Wahariri wa vyombo vya habari Tanzania chini ya Jukwaa la Wahariri, (TEF) wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa TEF mjini Morogoro leo Januari 29.01.2016. Mshomba aliwaeleza Wahariri hao WCF  inakusudia kuanza kulipa mafao kuanzia julai mosi mwaka huu wa 2016. Kati ya mambo yaliyojumuisha mada hiyo ni pamoja na uchangiaji katika Mfuko, adhabu kwa mujibu wa sheria namba 20/2008. (Picha na Imma Matukio)
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw. Absalom Kibanda akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha J. Mshomba kutoa mada katika ukumbi wa Nashera Morogoro. WCF inakusudia kuanza kulipa mafao kuanzia julai mosi mwaka 2016. Kati ya mambo yaliyojumuisha mada hiyo ni pamoja na uchangiaji katika Mfuko, adhabu kwa mujibu wa sheria namba 20/2008
   Mhariri Haura Shamte akizungumza
   Picha ya pamoja

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na Kaimu Mkuu wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana .
  Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, DIGP Abdulrahman Kaniki akimkabidhi zawadi Kaimu Mkuu wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana.DIGP ni mmoja wa Viongozi waliopitia katika chuo hicho.
  Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, DIGP Abdulrahman Kaniki akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa NDC (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba na Brigedia Jenerali Minja.
  Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, DIGP Abdulrahman Kaniki akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho katika makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Mikataba na Ununuzi wa BG East Africa David Johnson akijibu swali la mmoja wa wageni waliohudhuria hafla hiyo jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Pietro Firentini, Abdul;samad Abdulrahim akiuliza swali katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi wa Programmu wa Kampuni ya Achilles, Christopher House akijibu maswali ya baadhi ya washiriki wa hafla hiyo. 

  Wakati fursa za biashara za mabilioni ya shilingi zikiendelea kuibuka katika sekta ya mafuta na gesi hapa nchini, Wafanyabiashara na makampuni yenye dhamira ya kutoa huduma za mafuta na gesi nchini wamepatiwa fursa mpya kujitangaza duniani kote hususan kwa makampuni makubwa ya mafuta ambayo yanahitaji wadau wa kushirikiana nao katika biashara hiyo hapa nchini. 

  Huku ikikadiriwa kuwa na takriban futi za ujazo Trilioni 55 za gesi asilia, Tanzania inaonekana kwenye jicho la biashara hiyo kimataifa kama mdau muhimu anayechipukia na eneo lenye fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi. 

  Katika hatua ya aina yake, ambayo ni sehemu ya mpango mkakati wa muda mreffu, makampuni maakubwa ya mafuta BG Tanzania, Statoil Tanzania AS kwa kushirikiana na lile la mtandao la Achilles wamezindua mfumo mpya wa kimtandao kuhusu Tanzania utakaotumika kama njia rahisi ya kutambua na kuchagua makampuni ya ndani yanayofanya biashara ya mafuta na gesi kwa ajili ya kupata fursa mbalimbali za kibiashara kote ulimwenguni. 

  Makampuni hayo yamekubaliana kuwa na utaratibu mmoja kwenye utambuzi wa wa makampuni yanayofanya biashara hiyo hapa nchini. Utaratibu huo unazingatia viwango vinavyokubalika ambavyo watoa huduma wote wanapaswa kuwa navyo ili waweze kuwepo kwenye mfumo huo wa utambuzi na kunufaika na fursa zinazopatikana. Katika hatua ya awali, makampuni ya mafuta na gesi yatapaswa kuwasilisha taarifa muhimu zinazohitajika kuhusu hali yao ya kibiashara na mambo ya kimsingi kama afya, usalama, mazingira na huduma za jamii. Taarifa hizi zitaingizwa moja kwa moja kwenye mtandao. 

  Kwa taarifa hizo, washirika wataweza kutambua wabia muafaka na kuweza kushirikiana katika kujenga uwezo hususan katika kuala la viwango na kushughulikia suala la mahitaji na taratibu kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo. Pia kwa kuwa na usajili huu na mfumo wa pamoja watoa wasambazaji wanaweza kuwasiliana na kufanya kazi na wanunuzi waliopo kwenye.

  Gareth Palmer, Mkurugenzi wa Achilles Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika, ambao wanafanya kazi kwa niaba ya takriban mashirika 200 ya ununuzi wa mafuta na gesi kote duniani amesema “kwa kuweka na kutumia utaratibu huu wa kimtandao, BG na Statoil wanarahisisha sana uwezo wa makampuni ya hapa nchini kujitangaza na kuweza kupata wabia mbalimbali na kupanua wigo wa fursa za kibiashara”

  Naye John Ulanga, Afisa muandamizi wa BG Tanzania amesema “Kuwasaidia na kuwaunga mkono wafanyabiashara katika sekta hii hapa nchini in maana kubwa sana kibiashara. Kwa msingi huu tunafurahi kuwekeza katika mfumo huu muhimu hapa nchini na nje pia. Kwa kutumia mfumo huu tunatumaini kuwa tutaweza kuzitambua, kuzisaidia na kuzitangaza fursa zilizopo Tanzania kwa wadau wa kote duniani” 

  Kwa upande wake Mkuu wa Mawasiliano wa Statoil Tanzania AS Genevieve Kassanga amesema kwa wamefurahishwa sana na kukamilika kwa mfumo huu muhimu ambao utawawezesha wauzaji na wanunuzi kote Tanzania kuweza kutambulika na kufunguliwa kwa fursa za kufanya biashara kwa ufanisi zaidi. “Tunaamini kuwa ushirikiano huu utachochea ukuaji wa makampuni ya ndani na kuchangia kwa kasi zaidi katika ukuaji wa uchumi wa nchi. 

  Godfrey Simbeye Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF amesema mtandao huo ni suluhisho kubwa kwa wawekezaji wazawa katika sekta ya mafuta na gesi kwani utawawezesha kufahamika na kueleweka kote duniani. Ametoa rai kwa wadau kuhakikisha kuwa gharama za kujiunga na mtandao huo ni ndogo ili kuyawezesha makampuni ya kizalendo kumunu kuwepo kwenye mtandao huo.

  0 0


   WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe. Fredrick Sumaye (wa pili kulia), na mke wake mama Esther Sumaye wakimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda (kulia) eneo la shamba lake la ekari 33 lililopo Mabwepande Manispaa ya Kinondoni lililovamiwa na wananchi walipotembea eneo hilo Dar es Salaam leo asubuhi.
   Hapa Sumaye na viongozi wengine wakitafakari jambo.
   DC Makonda akihutubia katika mkutano huo. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mabwepande, Suzan Masawe.
   Mheshimiwa Sumaye (kushoto), akiongoza kuonesha mpaka wa shamba lake.
   Mhe. Sumaye akielezea uhalali wake wa kumiliki eneo hilo.
  Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Head of Cooperation for European Union, Eric Beaume gives his  remarks during the event. Looking from (right) is; Tanesco Managing Director, Eng Felchesmi Mramba, Embassy of Federation Republic of Germany, Counselor Claudia Imwolde-Kraemer and KFW Director, Dr Helmut Schon
  Agence Francaise Development (afd) Country Representative, Emmanuel Baudran shares views with Charg'e de Mission-Multi-sectoeurs Dennis Munuve. Right is Embassy of Federation Republic of Germany, Counselor Claudia Imwolde-Kraemer and KFW Director Dr Helmut Schon.
  Some delegates follow the proceeding of the event.
  The Acting Commissioner for Energy in the Ministry of Energy and Minerals Norbert Kahyoza gives his welcoming remarks to the delegates.
  TANESCO Public Relation Officer Leila Muhaji welcomes the delegates to the function.

  Tanesco Managing Director, Eng Felchesmi Mramba speaks to reporters during the function. Looking on is the Acting Commissioner for Energy in the Ministry of Energy and Minerals, Norbert Kahyoza.
  For more Click HERE

  0 0
 • 01/29/16--19:00: NGOMA AZIPENDAZO ANKAL

 • 0 0


  0 0

  Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza, Morogoro
  NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya "Tanzania Building Works ya Jijini, Dar es Salaam" inayojenga mradi wa umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete kuukamilisha mradi huo katika muda walioongezewa ili kuwezesha kuanza kwa shughuli za uzalishaji gerezani hapo.
  Akizungumza na Wakandarasi wa Kampuni hiyo alipofanya ziara ya kikazi Gereza Idete, Balozi Yahya amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo ni mkombozi kwa Jeshi la Magereza kwani utawezesha uzalijashi wa chakula cha kutosha cha wafungwa waliopo magerezani pamoja na kuzalisha ziada itakayouzwa kwa Wananchi ili kuongeza Mapato Serikalini.
  "Ni matarajio yangu kuwa Mkandarasi wa Mradi huu kwa kushirikiana na Mshauri Mwelekezi na Wadau wa Jeshi la Magereza atakamilisha mradi huu kwa wakati kama alivyotuahidi hivyo kuanza mara moja shughuli za uzalishaji". Alisisitiza Balozi Yahya.
  Naye Msimamizi wa mradi huo Mhandisi Lodia Mallion alisema kuwa mradi huo umekamilika kwa asilimia 60 ambapo tayari uchimbaji na ujenzi wa mifereji itakayokuwa ikipitisha maji kwenda mashambani imekwisha kukamilika.
  "Mito inayotumika kama vyanzo vya maji ni mto Kilombero pamoja na mto Kiwiliwili ambapo banio linalotunza maji kwa shughuli za umwagiliaji tayari limekamilika". Alisikika Mhandisi Mallion.
  Awali Mkuu wa Gereza Idete, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja akiwasilisha taarifa kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Yahya amesema kuwa kazi ya kuandaa mradi huu ilianza rasmi mwaka 2013 ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika Mwaka huu 2016 ambapo gharama za mradi huo zinakadiriwa kufikia kiasi cha Tsh. 2.5 Bilioni.
  Aidha amesema kuwa chakula kitakachopatikana katika mradi huo wa Gereza Idete kitatumika kulisha wafungwa waliopo magerezani na ziada itakayopatikana itauzwa kwa Wananchi hivyo kuongeza pato la Taifa.
  Gereza la Kilimo Idete lipo Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro linajishughulisha na Kilimo cha mpunga wa chakula na pia mpunga kwa ajili ya mbegu bora za Kilimo hapa nchimi. Gereza hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1983 kwa ajili ya Kilimo cha mazao mbalimbali hususani Kilimo cha mpunga.

   Mshauri wa Mradi, Mhandisi Nzobonaliba Imani akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya(katikati) alipotembelea mradi wa umwagiliaji wa Gereza la Kilimo Idete lililopo Mkoani Morogoro(kulia) ni Mkuu wa Gereza hilo, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja wakiaangalia ujenzi wa mradi wa umwagiliaji wa Gereza hilo.
   Wakandarasi wa Kampuni ya ujenzi wa mradi wa umwagiliaji wa Gereza Kilimo Idete, lililopo Mkoani Morogoro wakiendelea na ujenzi wa mifereji ya maji kama inavyoonekana katika picha.
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya akiangalia sehemu ya banio la kutunzia maji ya mradi wa Gereza la Kilimo Idete akiwa pamoja na msafara wa Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi(wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Manyama Mapesi(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya(wa pili kulia) akiwa ameongozana na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kushoto) kuelekea katika Ukumbi wa Gereza hilo kwa ajili ya kupata taarifa kamili ya utekelezaji wa mradi wa umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete kutoka kwa Wakandarasi wa mradi na Mshauri Mwelekezi mradi(kulia) ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero, Bw. Yahya Sinaniya.
  Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakipata maelezo ya Kitaalam kutoka kwa Mshauri Mwelekezi walipotembelea mradi huo kujionea hatua mbalimbali za ujenzi. Wengine ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kilombero.

  0 0

  Mwonekano katika lango Kuu la Kuingilia katika Uwanja wa mpira wa CCM Kirumba Jijini Mwanza pindi mvua inaponyesha. Ni zaidi ya Usumbufu, kero na adha kwa wanaoingia na kutoka Uwanjani hapo pindi mvua inaponyesha.
  Ni zaidi ya Usumbufumbu kwa mashabiki wa mpira pindi mvua inaponyesha wanapokuwa wakiingia amba kutoka Uwanjani, katika Uwanja wa CM Kirumba Jijini Mwanza kutokana na maji kutuama katika barabara inayoingia na kutoka katika lango Kuu la kuingilia Uwanjani hapo.
  Wahusika mlione hili kama changamoto inayopaswa kutafutiwa utatuzi.
  Picha na George Binagi-GB Pazzo Wa BMG.

  0 0


  MWILI WA SWAI KUSAFIRISHWA LEO KWENDA KILIMANJARO
  Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) linapenda kuwajulisha wapenzi, wadau, wa mpira wa miguu nchini kuwa, mwili wa aliyekua Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Simiyu, Epaphra Swai utaangwa leo saa 9 alasiri katika hosiptali ya Muhimbili, na baadae saa 11 jioni itaanza safari ya kuelekea mkoani Kilimanjaro. Fuata link chini kwa taarifa zaidi

  LIGI KUU KUENDELEA JUMAMOSI
  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja tofauti, ikiwa katika mzunguko wa 16 kwa kila timu kusaka pointi 3 muhimu katika raundi hiyo ya lala salama. Fuata link chini kwa taarifa zaidi

  STARTIMES RAUNDI YA 12 WIKIENDI HII
  Vita ya kuwania kupanda daraja msimu ujao itaendelea wikiendi hii kwa michezo 12 ya Ligi daraja la kwanza nchini (Startimes League) kuchezwa katika viwanja mbalimbali kwa makundi A, B, C, kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu. Fuata link chini kwa taarifa zaidi

  SDL KUENDELEA WIKIENDI
  Ligi Daraja la Pili nchini (SDL) mzunguko wa pili unatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, kwa timu nne za juu kutoka makundi A, B, C na D kusaka kupanda daraja msimu ujao. Fuata link chini kwa taarifa zaidi

  0 0


  006Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Flaviana Matata Foundation, Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi wakiwa pamoja na baadhi ya watu walioongozana nao wakielekea kwenye eneo la tukio.
  008
  Muonekano wa jengo la choo ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Mo Dewji Foundation.
  012
  Muonekano wa choo ambacho kilikuwa kikitumika awali kabla ya ujenzi wa choo kipya ambacho kimejengwa kwa ufadhili wa Mo Dewji Foundation.
  010
  Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Flaviana Matata Foundation, Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi wakitoka kukagua vyoo hivyo kabla ya uzinduzi rasmi.
  014
  Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Flaviana Matata Foundation (kushoto) na Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi kwa pamoja wakifunua kitamba kuzindua jiwe la msingi wakati wa hafla ya uzinduzi wa vyoo vya kisasa katika Shule ya Msingi Msinune iliyopo Bagamoyo, Pwani. Kwa picha na habari zaidi BOFYA HAPA


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Vifaa vya Michezo Nahodha wa Timu ya Mafunzo Mpira wa Miguu (Football) Haji Ramadhan Mwambe katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Unguja leo,timu hiyo itashiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika kwa kupambana na Timu ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) kwenye Uwanja wa Amaan tarehe 13 Februari, 2016 (katikati) Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi.Sharifa Kahamis
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Vifaa vya Michezo Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu JKU Ponsiana Malik Joseph katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Unguja leo,timu ya JKU ambayo inashiriki Kombe la Shirikisho itapambana na timu ya Gaborone United ya Botswana katika uwanja huo huo  wa Amaan Studium tarehe 14 Februari,2016. Picha na Ikulu.

  0 0

  ISO 9001:2008 CERTIFIED


  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitoa tangazo la nafasi za kazi katika magazeti mbalimbali ambapo waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi kupitia tovuti ya TRA.

  Kutokana na maombi ya nafasi za kazi kuingiliana na shughuli za kulipa kodi mwisho wa mwezi kupitia tovuti, TRA inasitisha kwa muda upokeaji wa maombi ya kazi kupitia tovuti hadi Jumanne Februari 2, 2016 ili kuruhusu ulipaji wa kodi uendelee bila usumbufu.

  Pia TRA imeongeza muda wa kupokea maombi hadi tarehe 17 Februari 2016.

  Waombaji wote wa nafasi za kazi zilizotangazwa wanaombwa kutuma maombi yao kuanzia Jumanne tarehe mbili Februari 2016.

  Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya. 

  Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:

  kituo cha huduma kwa wateja

  08000780078, 0800750075, 0713800333


  Limetolewa na:

  Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi


  TRA-Makao Makuu


  0 0


  Meneja Matekelezo wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw.Francis Mselem, (kulia), akipena mikono na Mkuu wa Kituo cha Walimu, Mbagala, Bi.Fausta B.Luoga, wakati akimkabidhi msaada wa viti kwenye kituo hicho jijini Dar es Salaam leo Januari 29, 2016. Kituo hicho kinatumiwa na Walimu zaidi ya 1500, na wanafunzi 55. Wanaoshuhudia ni Afisa Masoko na Uhusiano wa PSPF, Bi. Coleta Mnyamani (wapili kushoto) na Balozi wa Mfuko huo, Bw. Mrisho Mpoto.

   Balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto, a.k.a Mjomba, (kushoto), na Afisa Masoko na Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Scola Mnyamani, wakiwasili kwenye kituo cha Walimu Mbagala jijini Dar es Salaam, Januari 29, 2016
   Balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto, na Afisa Masoko na Mahusiano wa Mfuko huo, wakiwasalimia wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbagala.

  0 0

   Mwenyekiti wa Mfuko wa Kusaidiana wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jackline Semu (kulia meza kuu) akizungumza na wajumbe wa Umoja huo walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano uliopo ndani ya umoja wao. Katikati meza kuu ni Katibu wa Mfuko huo, Joyce Ngonyani na kushoto meza kuu ni Mweka Hazina wa mfuko huo, Christina Kaale. 
  Mwenyekiti wa Mfuko wa Kusaidiana wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jackline Semu (kulia meza kuu) akizungumza na wajumbe wa Umoja huo walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano uliopo ndani ya umoja wao. Katikati meza kuu ni Katibu wa Mfuko huo, Joyce Ngonyani na kushoto meza kuu ni Mweka Hazina wa mfuko huo, Christina Kaale. 
  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  0 0

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amemteua Ndugu Julian Banzi  RAPHAEL (pichani) kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

  Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imeeleza kuwa uteuzi huo umeanzia tarehe 26 Januari, 2016.

  Kabla ya uteuzi huu Ndugu Julian Banzi RAPHAELalikuwa Katibu mkuu, Wizara ya Biashara na Viwanda, Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar. 

  Ndugu Julian Banzi RAPHAEL anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Juma RELI ambaye muda wake umemalizika tarehe 12 Julai, 2015.


  Gerson P. Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU,

  DAR ES SALAAM.


  28/01/2016


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha J. Mshomba akitoa mada kwa Wahariri wa vyombo vya habari Tanzania chini ya Jukwaa la Wahariri, (TEF) wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa TEF mjini Morogoro leo Januari 29.01.2016. Mshomba aliwaeleza Wahariri hao WCF  inakusudia kuanza kulipa mafao kuanzia julai mosi mwaka huu wa 2016. Kati ya mambo yaliyojumuisha mada hiyo ni pamoja na uchangiaji katika Mfuko, adhabu kwa mujibu wa sheria namba 20/2008. (Picha na Imma Matukio)

  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw. Absalom Kibanda akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha J. Mshomba kutoa mada katika ukumbi wa Nashera Morogoro. WCF inakusudia kuanza kulipa mafao kuanzia julai mosi mwaka 2016. Kati ya mambo yaliyojumuisha mada hiyo ni pamoja na uchangiaji katika Mfuko, adhabu kwa mujibu wa sheria namba 20/2008
   Mhariri Haura Shamte akizungumza
   Mhariri Balinagwe Mwambugu, akizungumza
   Mhariri Paul Maregesi, akizungumza
   Picha ya pamoja

older | 1 | .... | 1106 | 1107 | (Page 1108) | 1109 | 1110 | .... | 3272 | newer