Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1108 | 1109 | (Page 1110) | 1111 | 1112 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Watu wanaodaiwa kuwa ni majangili na wawindaji haramu wameitungua kwa risasi helkopta hiyo ya doria na kumuua rubani wake raia wa Uingereza katika pori la akiba la Maswa mkoani Simiyu.

  Katika tukio hilo ambalo pia lilimjeruhi askari wa wanyamapori, helkopta hiyo mali ya kampuni ya uhifadhi iitwayo Friedkin Conservation Fund ilikuwa katika doria kwenye pori la uwindaji wa kitalii la Mwiba.

  Tukio hili la majangili kutungua helkopta kwa risasi ni la kwanza kutokea katika historia ya uhifadhi nchini Tanzania na imeelezwa kuwa doria hiyo ilikuwa inafanyika kufuatia milio ya risasi iliyotokea katika eneo hilo la pori la akiba la Maswa ambapo majangili hao walikuwa wameuwa tembo watatu na kuchukua meno yao.

  Waziri wa Maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe amefika katika eneo la tukio na amesema Serikali inaanzisha mkakati mpya wa kupambana na ujangili na maharamia hao waliotungua helkopta hiyo na kusababisha kifo cha rubani lazima wakamatwe- picha na Vedasto Msungu Technologies.


   Waziri wa Maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe akifafanua jambo kwenye tukio hilo

  0 0


  Watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wadau mbalimbali wa wakiingia katika viwanja vya Mnazi mmoja kwa maandamano leo jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.


  Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Askari wa Jeshi la Magereza na Watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakiwa wamebeba mabango ya Ofisi zao wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini leo jijini Dar es salaam.


  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (Mwenye T-shirt nyeupe kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki (wa Pili kulia) na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania wakishiriki mazoezi ya viungo ya pamoja na wadau mbalimbali wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini.


  Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (katikati) akiongoza mazoezi ya pamoja ya Wadau wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria nchini.


  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  akizungumza na wadau mbalimbali wa Mahakama waliohudhuria Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria mwaka 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini Dar es salaam.


  Baadhi ya Wanachi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Katika mwendelezo wake wa kufanya maisha ya watanzania kuwa murua na kuwapeleka katika karne ya sayansi na teknolojia, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imezindua simu ya mkononi ya gharama nafuu kabisa ambayo haijawahi kutokea nchini.
  Simu hiyo  aina ya Alcatel ambayo bei yake ni nafuu ya shilingi 20,000/- imeanza kusambazwa sehemu mbalimbali nchini na itapatikana katika maduka ya Vodacom na mawakala wake wote nchini kote hususani maeneo ya vijijini.
  Akiongea kuhusu uzinduzi wa simu hii mpya,Mkurugenzi Mtendaji wa  Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema “Vodacom imeingiza simu hii ya gharama nafuu ambayo imetengenezwa kumuwezesha mtumiaji kupata huduma mbalimbali na dhamira yetu kubwa ni kuendelea kufanya ubunifu wa kiteknolojia wa kurahisisha maisha ya watumiaji wa simu pia kuwapeleka katika ulimwengu wa teknolojia”.Alisema.
  Alisema kwa mwaka huu kampuni itaendelea kubuni huduma mbalimbali  za kurahisisha mawasiliano dhamira yake kubwa ikiwa ni kuhakikisha kila mtanzania ameunganishwa kwenye mtandao na anafurahia maisha kupitia teknolojia ya simu.
  Nae Meneja wa huduma na bidhaa wa kampuni hiyo,Edwin Byampanju aliielezea simu hiyo kuwa ina uimara mkubwa, ina kioo chenye ukubwa wa inchi 2 na mwonekano wa mbele wenye rangi maridhawa,ina kamera yenye ukubwa wa MP 1.3, betri inayotunza chaji  kwa muda mrefu zaidi ya siku tano,ina redio pia inao uwezo wa kutumia kadi ya kumbukumbu hadi GB 16”.
  Aliwataka wateja wote wanaotumia mtandao wa Vodacom kuchangamkia fursa ya kumiliki simu imara na yenye ubora wa kisasa kwa gharama nafuu na kuendelea kupata huduma bora zinazorahisisha maisha.
   Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(kushoto) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa  uzinduzi wa simu mpya aina ya Alcatel mwishoni mwa wiki yenye vioo 2, kamera ,radio, MP 1.3, kadi yenye GB 16 na betri  yake inayotunza chaji  kwa muda mrefu.Simu hiyo inapatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini  kwa   Tsh.20,000 tu ,Kulia ni Meneja wa huduma na bidhaa wa kampuni hiyo,Edwin Byampanju.

  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)na Meneja wa huduma na bidhaa wa kampuni hiyo,Edwin Byampanju wakionesha simu mpya aina ya Alcatel kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa simu hiyo mwishoni mwa wiki inayopatikana kwenye maduka yote ya kampuni hiyo nchini kwa Tsh.20,000 tu.Simu hiyo ina vioo 2,kamera,radio,MP 1.3, na kadi yenye GB 16 na betri inayotunza chaji  kwa muda mrefu zaidi.

  0 0

  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Manyara, umekabidhi mashuka 170 kwenye zahanati ya Kijiji cha Engusero na hospitali ya wilaya ya Kiteto kwa ajili ya kutumiwa kujifunika na wagonjwa wanaofika kulazwa.
  Mashuka hayo yalikabidhiwa kwa mkuu wa wilaya hiyo Kanali Samuel Nzoka na meneja wa NHIF wa mkoa huo Isaya Shekifu, kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wa kujiunga mfuko wa afya ya jamii (CHF) uliofanyika juzi kijiji cha Engusero.
  Akizungumza wakati akipokea mashuka hayo Kanali Nzoka aliushukuru mfuko huo na kuzitaka kaya za eneo hilo kujiunga na CHF ili wajipatie matibabu kwa mwaka mzima kwani kaya moja yenye watu sita italipia sh10,000. 
  Alisema tatizo la ukosefu wa dawa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitalini litamalizika, endapo kaya nyingi zikijiunga na CHF kwani serikali nayo itaweka mkono wake ili kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa. 
  Wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo Kanali Nzoka alijitolea sh20,000 kwa ajili ya kuzilipia kaya mbili za watu 12 wa kijiji cha Engusero na Dosidosi na kuungwa mkono na viongozi wanne wa wilaya hiyo waliojitolea sh10,000 kwa kila mmoja.
  Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Kanali Samuel Nzoka (kulia) akipokea moja kati ya mashuka 170 yaliyotolewa juzi na Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) wa mkoa wa Manyara, Isaya Shekifu (kushoto) kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF.

  0 0

  Na Raymond Mushumbusi Maelezo
  Wananchi wa Tanzania watahadharishwa juu ya ugojwa wa  homa ya Zika uliripotiwa kutokea katika nchi za Amerika ya kusini hivi karibuni.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo  Mijini Dodoma na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa akitoa tamko juu ya uvumi ulioenea kuhusu homa ya Zika iliyoenea katika nchi za Amerika ya kusini.
  Mhe.Ummy Mwalimu amewaasa watanzania kuwa na tabia ya kwenda hospitali kila wanapojisikia dalili za homa na kupima kwani sio kila homa ni malaria kwani dalili za homa ya malaria zinafanana kabisa na dalili za ugonjwa wa homa ya Zika.
  “ Nawaomba ndugu zangu watanzania tuzingatie usafi ili kuzuia mazalia ya mbu kwani ugonjwa huu unatokana na virusi vinavyoenezwa na mbu na hao mbu wanapatikana sana nyakati za asubuhi mchana na jioni hivyo nawasihi kutumia dawa za kuua mbua na vyandarua wakati wa kulala.”
  “Napenda kutoa tamko kuwa ugonjwa huu wa homa ya Zika haujaingia Tanzania na tunawaomba watanzania kuwa makini sana na waripoti dalili zozote ambazo sio za kawaida zitakazojitokeza na mpaka jana kwa taarifa tulizonazo hakuna mgonjwa aliyegundulika kuwa na homa ya Zika”  Alisema Mhe.Mwalimu.
  Aidha naye Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Dodoma Dkt Zainabu Chaula amesema wamejiandaa kukabiliana na kesi zozote zinatazojitokeza za homa ya Zika na wana mfumo mzuri wa kubaini magonjwa ya mlipuko  na pia kuna maabara ya NIMR ambayo inafanya uchunguzi juu ya magonjwa mbalimbali.
  “ Nawaomba watanzania kutopuuzia dalili zozote za homa na kuamua kujitibia manyumbani au kunywa dawa bila kupima na kujua hiyo homa ni ugonjwa gani kwani yaweza kuwa homa ya Zika” Alisema Dkt Chaula.
  Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee wa kushirikiana na Shirika la Afya Dunianoi (WHO) wanafatilia kuhusu ugonjwa huu na watatoa maelekezo ya kuzingatia ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu ila mpaka sasa ugomjwa huu haujaingia Tanzania.
  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa Habari Mijini Dodoma (Hawapo Pichani)  akitoa tamko la Wizara juu ya ugonjwa wa homa ya Zika kushoto ni Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Dodoma Dkt Zainabu Chaula. Picha Na Raymond Mushumbusi Maelezo

  0 0

  Msimamizi wa Duka la MSD Arusha Twaha Kabandika akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Kigwangalla wa namna mfumo unaotumika kwa mauzo unavyofanya kazi.Kulia ni M/Kiti wa Bodi MSD, Prof Idris Mtulia, Mkurugenzi wa MSD Laurean Bwanakunu (Kushoto)  na Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Fadhili Nkurlu.
  Naibu Waziri wa Afya akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Prof. Idris Mtulia alipowasili duka la MSD Mount Meru, Arusha kwa ajili ya kulizindua rasmi jana. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bw. Cosmas Mwaifwani.
  NaibuWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Hamis Kigwangalla (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka la Dawa la MSD jijini Arusha.


  0 0
  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa UNIDO lenye makamo makuu yake Nchini Vienna Ausria Bw. Li Yong  walipokuta katika  Ofisi za Umoja wa Afrika  (AU) Addis Ababa leo Januari 31,2016, Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Ujumbe wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa lenye Makao Makuu yake Nchini Vienna Austria uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bw. Li Yong, leo Januari 31,2016 kwenye Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa, katika mazungumzo yao Viongozi hao walizungumzia juu ya kuendeleza ushirikiano kwenye maendeleo ya Viwanda utakaotolewa na UNIDO kwa Serikali ya Tanzania ili kuifanya Tanzania iwe Nchi ya Viwanda kuanzia mwaka 2015/2020, ambapo Mkurugenzi huyo ameahidi kuitembelea Tanzania wakati wowote kuanzia sasa. Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa UNIDO lenye makamo makuu yake Nchini Vienna Ausria Bw. Li Yong  akisisitiza jampo kwa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan walipokuta katika  Ofisi za Umoja wa Afrika  (AU) Addis Ababa leo Januari 31,2016.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea taarifa yenye mipango ya Maendeleo ya Viwanda kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa Bw. Li Yong baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika leo Januari 31,2016 katika Ofisi za Umoja wa Afrika  (AU) Addis Ababa, Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika. (Picha na OMR)

  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametoa dola za Marekani milioni 100 (US$ 100m, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 220) kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) kwa shughuli za misaada katika maeneo tisa yenye dharura duniani na yasiyo na fedha za kutosha. 

  Tanzania—ambayo kihistoria imepokea mamilioni ya wakimbizi kutoka nchi jirani kwa miaka mingi—imetengewa dola za Marekani milioni 11 (Sawa na shilingi za Tanzania bilioni 24) kutoka katika kiasi hicho kwa lengo la kushughulikia mahitaji ya wakimbizi kutoka Burundi.
  Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa msaada katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo mkoani Kigoma wakati alipofanya ziara mkoani humo


  Zaidi ya raia 126,000 wa Burundi wamekimbilia nchini Tanzania tangu mwezi Aprili, 2015, kufuatia machafuko ya kisiasa nchini humo. Huku tayari wakimbizi 64,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) wakiwa tayari nchini. Tanzania hivi sasa ina zaidi ya wakimbizi 193,000. Kutokana na ukweli kwamba takribani wakimbizi 1,500 wanawasili nchini kila wiki, inabashiriwa kwamba huenda idadi jumla ya wakimbizi ikafikia 230,000 hadi mwisho wa mwaka 2016. Hali hii inasababisha changamoto nyingi hasa katika kutoa msaada na kinga ya kutosha kwa wakimbizi.

  Mchango huu mkubwa kutoka CERF utakuwa muhimu sana katika kutoa misaada ya kiutu kwa wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nyarugusu, Nduta na Mtendeli katika mkoa wa Kigoma, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, na vilevile kwa jamii za wenyeji ambazo zinahitaji kwa haraka huduma bora za maji safi, usafi wa kutosha, matunzo ya afya, chakula na makazi. 

  Sehemu ya fedha hizo pia itatumika kushughulikia mlipuko uliopo wa ugonjwa wa kipindupindu ambao umeathiri mikoa 19 nchini. Fedha za CERF kwa hiyo zitasaidia kuhakikisha kwamba maeneo muhimu zaidi katika dharura yanafanyiwa kazi na kwamba wakimbizi wanapewa kinga na huduma za msingi.

  Baadhi ya wakimbizi waliopo katika kambi ya Nyarugusu iliyopo mkoani Kigoma

  “Shirika la Kushughulikia Wakimbizi (UNHCR) linakaribisha mchango huu wenye ukarimu mkubwa kutoka CERF ambao unakuja katika kipindi mwafaka kabisa. Utoaji msaada kwa wakimbizi ulikuwa ukikabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha katika mwaka 2015, hali iliyoathiri sana uwezo wetu wa juhudi za pamoja katika mwaka 2015. 

  Tuna imani kwamba hii ni ishara ya kwanza kwa upatikanaji wa fedha nyingi zaidi kwa utoaji msaada katika mwaka 2016. Kwa hakika, mchango huu utasaidia kuziba upungufu mkubwa uliojitokeza katika wito wetu wa sasa na hivyo kushughulikia mahitaji makubwa zaidi ya wakimbizi na jamii za wenyeji,” alisema Mwakilishi wa UNHCR nchini Tanzania, Bi. Joyce Mends-Cole.


  Kadiri mahitaji ya kiutu yanavyoongezeka, mchango kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) umetoa matumaini ya kuendelea kushughulikia dharura ya wakimbizi kutoka Burundi. Tangu mwaka 2006, Nchi 125 Wanachama wa Umoja wa Mataifa na waangalizi, wahisani kutoka sekta binafsi na serikali katika kanda zinazohusika wameendelea kuusaidia Mfuko huo hadi sasa. 

  CERF hadi sasa imetoa jumla ya dola za Marekani bilioni 4.2 (US$ 4.2bn, sawa na shilingi za Tanzania trilioni 9) kwa miradi ya kiutu katika nchi 94. CERF hupokea michango ya hiyari katika mzunguko wa mwaka ili kutoa msaada wa kifedha kwa hatua za kiutu za kuokoa uhai. CERF inapata fedha zake kutoka kwa washirika wengi huku michango mingi zaidi ikitoka: Uingereza, Swideni, Norwei, Uholanzi na Kanada.

  0 0


  0 0
 • 01/31/16--23:44: Article 22
 • Enjoy VIP treatment, Sip champagne and revel in the romantic seaview served a sumptuous 5 star buffet feast.. show your class and amplify your soul with the sound of timeless live music..Share an unforgettable with luxurious Valentine experience with your loved ones at Ramada Resort-Dar

  0 0


  0 0

  Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki akimuongoza Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya kukagua athari za upepo kwa mashamba ya migomba kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.
  Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki akionesha sehemu ya mgomba iliyoanguka baada ya upepo mkali kuathiri shamba lake la ekari 3, wakati Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, ilipokuwa ikikagua athari za maafa hayo katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.
  akimueleza jambo Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki mara baada ya kukagua athari za upepo kwa mashamba ya migomba katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.


  0 0

  Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma mara tu baada ya kuteuliwa kuwa mwakilishi wa Afrika katika mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya.
  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa na Mheshimiwa  Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (kulia) kuwa Mwakilishi wa Umoja wa Afrika  katika mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya.
  Kufuatia uteuzi huo uliotangazwa rasmi na AU jana katika Kikao cha Wakuu wa Nchi za Afrika, Rais Mstaafu Kikwete leo asubuhi amekutana na Dkt. Zuma makao makuu ya AU leo na kufanya nae mazungumzo kuhusu jukumu alilokabidhiwa.
  Mheshimiwa Dkt. Kikwete amemshukuru Dkt. Zuma na Wakuu wa Nchi za AU kwa imani kubwa waliyoonyesha kwake kwa kukabidhiwa jukumu hilo zito.  Amewashukuru pia wadau wa siasa nchini Libya kwa kuridhia uteuzi wake.
  Naye Dkt. Zuma amemshukuru Dkt. Kikwete kwa kukubali uteuzi huo na  kuwa tayari kubeba jukumu hilo. Amemueleza kuwa Umoja wa Afrika na Afrika nzima inayo matarajio makubwa juu yake na iko nyuma yake. Amemuhakikishia kumpa kila aina ya ushirikiano atakaouhitaji kukamilisha katika kutekeleza majukumu yake.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya walipokutana kwenye ukumbi wa mikutano katika Ofisi ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa Ethiopia, Viongozi hao wanahudhuria mkutano wa 26 wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili masuala ya Usalama Barani Afrika ambapo Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.  (Picha na OMR)

  0 0

  Mkurugenzi  wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu  muendelezo na msimamo wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa 2 katika ofisi za Airtel makao makuu Jijini Dar es saalam ili kuendelea kuwezesha  vijana wengi nchini.
  Airtel Fursa yachanja mbuga
  ·         Airtel FURSA kutumia Simu kuwafikia vijana nchi nzima
  AWAMU ya pili ya mpango wa Airtel FURSA imezidi kujimarisha nchini baada ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kujipanga kutoa mafunzo ya ujasiriamali na kutumia mtandao wa Airtel kuwafikia vijana nchi nzima kwa njia ya simu.
  Akizungumza jijini hapa mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano, alisema mafunzo yajayo ya semina zinazoendelea kwa vijana wajasiriamali yatafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Lindi.
  “Pia wakati wowote kuanzia sasa Airtel FURSA tutaweka wazi mfumo wa mafunzo kwa njia mpya ya kiubunifu zaidi  kwa njia ya simu za mkononi ili kuwafikia vijana wengi zaidi wanaokabiliwa na changamoto za ajira,” alisema Bi, Singano.
  Alisema walengwa wa mpango huo ni vijana wenye kati ya umri wa miaka 18 na 24 na kwamba tangu mradi huo uanze mwaka jana na kudumu kwa miezi sita, takribani vijana 2,500 nchini wamekwishafaidika na sasa wanamiliki biashara na miradi mbalimbali.
  Mkurugenzi huyo wa Airte Bi, Beatrice Singano  aliwaomba wadau na serikali kujitokeza na kushirikiana na Airtel kuwawezesha vijana ili nao waweze kuleta mabadiliko katika jamii inayowazunguka.
  “Katika msimu huu wa pili wa Airtel FURSA, tutawafikia vijana wengi zaidi na kuwapa mafunzo na semina, ushawishi na kuwainua kwa misaada ya vitendea kazi. “Tayari tumefika na kutoa mafunzo katika mikoa ya Manyara na Morogoro, sasa  tunaingia Dodoma, kisha vijana wa Lindi na Dar es Saalam wajiandae,” alisema.
  Alisema uzinduzi wa mpango wa mafunzo kwa njia ya simu utawezesha hata wale wasio na nafasi ya kuhudhuria mafunzo na semina, wataweza kufanya hivyo popote walipo. “Tunaamini kuwa msimu huu utakuwa na mafanikio zaidi kwani wengi watawezeshwa kupitia programu hii,” alisema
  Mpango wa Airtel FURSA ni mradi endelevu unaowalenga vijana nchi nzima kwa kuwapatia vifaa, mafunzo ya biashara na mafunzo mbalimbali kwa njia tofauti waweze kufikia malengo yao. Pia mpango huu unawawezesha vijana kuongeza mitaji au kupanua biashara zao za ujasiriamali kwa kuwapa msaada wenye thamani ya hadi Sh. milioni 10 kwa kila mmoja.
  Ili kijana kufaidika na msaada huo, anatakiwa kutuma maombi kwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenda namba 15626 akiwa jina kamili, umri wake, aina ya biashara anayoifanya, mahali alipo na namba za simu, au kupitiaairtelfursa@tz.airtel.com au kujaza fomukutoka kwenye tovuti www.airtel.com.

  0 0

  KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetuma salamu za pongezi kwa viongozi wapya wa Chama cha Wahariri Tanzania waliochaguliwa katika mkutano wao uliomalizika mwishoni mwa wiki.

  Katika salama zake za pongezi Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema “Kwa niaba ya Vodacom nawapongeza viongozi wa Chama Cha Wahariri waliochaguliwa kuongoza Jukwaa la Wahariri nchini.

  Aliongeza kuwa Vodacom itaendelea kufanya kazi kwa karibu na viongozi hao kwa kuwa inaamini kuwa vyombo vya habari ni njia kubwa inayotumika kwa mawasiliano kama zilivyo simu za mkononi na mawasiliano yakiwa mazuri katika jamii yoyote ile ni lazima ipate maendeleo kwa haraka.

  Ferrao alitoa shukrani kwa uongozi uliomaliza muda wake kwa jinsi ulivyofanya kazi nzuri ya kukuza taaluma ya habari na kufanya kazi kwa ushirikiano na makampuni na taasisi mbalimbali.

  Katika uchaguzi Bw.Theophil Makunga, ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited (JCTL) alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Mhariri Mtendaji wa Jamhuri, Deodatus Balile, amechaguliwa kuwa Makamu wake na Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Neville Meena, ameendelea kuwa Katibu Mkuu wa jukwaa hilo.

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati) pamoja na ujumbe wake, wakiingia katika lango kuu la kuingilia abiria wakati alipotembelea eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero II na kushuhudia shughuli za uokoaji wa magari, utafutaji miili ya watu na uokoaji wa kivuko hicho ukiendelea. Balozi Simba alifanya ziara ya kikazi mkoani Morogoro kwa kutembelea miradi ya maendeleo ya Jeshi la Magereza mkoani humo.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia), akisalimiana na Askari wa Kikosi cha Wanamaji wa Uokoaji wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao wanashiriki katika shughuli za uokoaji miili ya watu waliozama baada ya kivuko cha MV Kilombero II kuzama Januari 27.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akiondoka eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero mara baada ya kushuhudia shughuli za uokoaji zikiendelea vizuri.

  0 0
 • 02/01/16--03:46: BEI YA MADAFU HII LEO.


older | 1 | .... | 1108 | 1109 | (Page 1110) | 1111 | 1112 | .... | 3286 | newer