Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1090 | 1091 | (Page 1092) | 1093 | 1094 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa umeme wa Kinyerezi Awamu ya Pili, akielezea kuhusu habari zilizoandikwa kimakosa katika moja ya magazeti ya kila siku nchini jijini leo. Kulia ni Ofisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari-Maelezo, Magreth Kinabo. (Picha na Kassim Mbarouk 

  Na Nyakongo Manyama- MAELEZO
  WIZARA ya Nishati na Madini  imekanusha habari iliyopotosha umma kuhusu   mradi wa umeme wa Kinyerezi II kuwa bado haujaanza na gharama zilizoandikwa si za kweli.
  Wizara hiyo imekanusha habari hiyo, iliyoandikwa katika gazeti la Mtanzania la leo Januari 14, mwaka huu toleo namba8063,  lenye kichwa cha habari “ Harufu ya Jibu Mradi wa Umeme.”
  Habari hiyo  ambayo ilieleza kwamba mradi huo ulizinduliwa na Rais Mstaafu wa  Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Dkt.Jakaya Kikwete uligharimu Sh. trilioni 1.6 na kwamba fedha za ujenzi wa mradi huo zimetokana ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Japan,ambapo Serikali ya Tanzania itakuwa na hisa ya asilimia 40 na kampuni ya SUMITOMO ya Japan asilimia 60. 
   Aidha habari hiyo ilidai kuwa Serikali inachangia fedha za ndani kwa asilimia 12 na zilizobaki zikiwa na mkopo kutoka benki ya Japan na kwamba gharama za mradi huo ziko juu ikilinganishwa miradi mingine akitolea mfano Kampuni ya TALLAWARA Power Station ya nchini Australia anayodai ilitaka kujenga mradi huo kwa dola za Marekani milioni 350.

  Hayo yamesemwa leo na  Mkuu wa Mawasiliano Serikali  wa wizara hiyo,  Badra  Masoud alipokuwa akizungumza  na waandishi wa habari kuhusu habari hiyo katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam. 
  “Serikali  ya Tanzania  iliingia makubaliano na Serikali ya Japan  ya mkopo wa masharti nafuu  wa dola za Marekani  milioni 292  kwa ajili ya kutekeleza mradi wa  kuzalisha umeme wa Megawati 240 utakaojengwa na kampuni ya SUMITOMO kama mkandarasi wa “EPC contractor” na sio kama mbia wa Serikali yaTanzania kama ilivyodaiwa.
  “Mradi huo unamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 kupitia TANESCO  na hakuna mwekezaji mwingine katika mradi huo.Hivyo si kweli kwamba Serikali ya Tanzania na kampuni ya SUMITOMO zinawekeza kwa ubia wa asilimia 40 (kwa Serikali ya Tanzania) na asilimia 60 kwa SUMITOMO. Kwa maana hiyo, hatutauziwa umeme utakaozalishwa na mradi huu kwani ni mali yetu na hakuna gharama yoyote ya ziada kama alivyodai mwandishi wa habari hiyo,” alisema Badra.
  Aidha Badra alisema mwandishi huyo alidai kwamba mradi huo ulizinduliwa na Rais wa  Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, wakati ni  kwamba mradi huo haujazinduliwa bado na sasa upo katika maandalizi ya kuwekwa katika jiwe la  msingi.
   Akizungumzia kuhusu gharama za mradi huo, alieleza kuwa unatekelezwa kwa dola za Marekani milioni 344 sawa na Sh. bilioni 740 zikiwa ni mkopo wa masharti nafuu wa asilimia 85 sawa  na dola za Marekani 292 na mchango wa Serikali ya Tanzania kwa asilimia 15 sawa na dola za Marekani milioni 52 na sio asilimia 12 kama ilivyodaiwa na mwandishi huyo. 
   
  “Mwandishi wa habari hii amejaribu kufananisha uwekezaji huu na uwekezaji wa TALLAWARA Power Station ya Australia na kudai kwamba gharama yake ingekuwa ndogo kuliko gharama ya mradi huu. 

  Taarifa hii haina ukweli wowote kwa sababu gharama ya dola milioni 344 zinazotarajiwa kutumika mkatika mradi huu iko chini kuliko dola milioni 350anazodai mwandishi kwamba zingetumiwa na kampuni TALLAWARA.

  “Aidha, kampuni ya TALLAWARA haijawahi kuomba au kuonesha nia ya kuwekeza katika mradi wowote wa kufua mradi wa umeme nchini. Pia ni muhimu ifahamike kwamba makubaliano ya mkopo huu yalikuwa yanakwenda sambasamba na utekelezaji wa mradi wenyewe (EPC with Financing).     
  Badra aliongeza kwamba pamoja na kwamba gharama za uwekezaji wa mradi huo wa kwanza wa aina ya “Combined Cycle” nchini zinawiana na gharama za miradi mingine ya aina hiyo duniani, gharama za uwekezaji zinaweza kutofautiana kutegemeana na mazingira ya nchi na nchi, teknolojia iliyotumika na aina ya mitambo.
  Hivyo sio suala la kulinganisha gharama ya mradi mmoja na mwingine.
  Wizara hiyo imeshauri waandishi wa habari kufuata miiko na maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari  zenye ukweli na sahihi na zilizozingatia pande zote mbili kwa kuwa ipo na tayari kujibu maswali ya waandishi wakati wowote.

  0 0

  Na:George Binagi.
  Jamii nchini imetakiwa kutowanyanyapaa waathirika wa dawa kulevya badala yake wawasaidie kuondokana na matumizi ya dawa hizo ikiwemo kuwafikisha katika vituo vya utimamu wa akili (Sobar House).

  Rai hiyo ilitolewa wiki hii na Eddy Darkis ambae ni Meneja wa Kituo cha Utimamu wa akili cha Back To Life Sobar House kilichopo Pasiansi Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, ambacho kinawasaidia wahanga wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo.

  Darkis alibainisha kuwa badhi ya wanajamii wamekuwa wakiwanyanyapaa waathirika wa dawa za kulevya, jambo ambalo linakwamisha mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya nchini.

  Kwa mwaka 2015, zaidi wahanga 50 wa dawa za kulevya waliokuwa katika Kituo hicho kutoka Mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mkoani Mwanza, wamerejea katika hali zao za kawaida baada ya kupatiwa tiba ya kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya huku wengine zaidi ya 25 wakiendelea kupatiwa tiba katika kituo hicho.

  Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wanaopiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu nchini (OJADACT) Edwin Soko, Idadi ya Watumiaji wa dawa za Kulevya Jijini Mwanza imefikia zaidi ya Watumiaji Elfu Kumi katika kipindi cha miezi sita iliyopita huku sababu za ongezeko hilo zikiwa ni kutokana na kukosekana kwa njia mathubuti za kupambana na uingizaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya kutokana na wanaojihusisha na biashara ya dawa hizo mara kwa mara kubuni mbinu mpya za usafirishaji jambo linalosababisha ugumu katika kupambana na biashara hiyo.

  0 0
 • 01/14/16--19:00: NGOMA AZIPENDAZO ANKAL
 • Vifuu Tundu - AT feat. mwa4

  0 0

  Na Woinde Shizza 
  Mkuu wa Wilaya ya SimanjiroMkoani Manyara, Mahmoud Kambona ameagizawanafunzi wote waliofaulu kujiunga nashule za sekondari wilayani  humo wawe wamewasili kwenye shule zao na kuanzamasomo baada ya wiki mbili.

  Kambona alitoa agizo hilo juzialipokuwa anakagua shule ya Sekondari Msitu wa Tembo na kuzungumza na watendajiwa vijiji, kata, madiwani na maofisa Tarafa, kuhusiana na wanafunzi waliofaulukujiunga na masomo ya sekondari. Alisema wanafunzi wote waliofaulukujiunga na Sekondari wanatakiwa wafike kwenye shule zao baada ya muda wa wikimbili kwa ajili ya masomo na endapo wasipotekeleza hilo atawachukulia hatuakali viongozi wa eneo husika.

   “Nitawachukulia hatua
  kali viongoziwote wakiwemo madiwani, maofisa tarafa, watendaji wa
  kata, vijiji na wenyevitiwa vijiji wa sehemu husika ambao wanafunzi wote waliofaulu watakuwa hawajafikashuleni,” alisema Kambona.

  Pia,
  aliwaagiza wakuu wa shule zasekondari za wilaya hiyo kuwaelekeza
  wazazi na walezi wa watoto ambao wamefaulukujiunga na shule zao, juu ya majukumu yao na majukumu ya serikali kuhusiana naelimu bure.Baadhi
  ya wazazi wa wanafunziwaliofaulu Joseph Odoyo na Mustafa Seif walisema
  dhana ya elimu bure ya RaisJohn Magufuli bado hawajaielewa kwani iliondolewa ni ada pekee ila chakula na mahitajimengine
  wanachangia.

  “Ada ya sh20,000 ndiyo pekee iliyofutwaila tunachangia huduma nyingine za mpishi sh.15,000 kuni sh15,000 kusaga na
  kukoboash15,000 kulima shamba la shule sh.15,000 na viungo sh10,000 kwa muhula mmoja,”alisema Odoyo. Alisema pia wazazi wanatakiwa
  kuchangiakilo 80 za mahindi, kilo 35 za maharage, kilo tano za sukari,
  kilo 12 za mchelena lita tano za mafuta ya kula kwa muhula mmoja ila sh5,000 ya muhuri wa nemboya shule imetolewa.

  0 0

  Mwenyekiti wa kikundi cha wajasiriamali wa kazi za Sanaa Bw.Henry Clemens akiishukuru serikali kwa kuonyesha nia ya kuwasaidia kwa kuanzisha Idara ya Sanaa na ivyo wataitumia kuimarisha kazi zao ili ziwanufaishe.Pembeni yake ni makamu mwenyekiti wa Kikundi icho Bw.Chief Eliewaha Shogholo Challi.
  Mwenyekiti wa kikundi cha wajasiriamali wa kazi za Sanaa Bw.Henry Clemens (kushoto) akimweleza jambo Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Leah Kihimbi (kulia).Bw.Clemens aliomba serikali kuwawezesha kupata wawekezaji, na pia shughuli za za Sanaa ziwe rasmi ili wajipate kipato na kutengeneza ajira kwani wazalishaji wa Sanaa wanafiki milioni 3 kwa sasa.
  Kaimu Mkurugenzi Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi akiongea na wajasiriamali wa kazi za Sanaa wa Mikono Cultural Heritage Ltd walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Bi leah aliwahaidi wasanii hao kufanya nao kazi kwa karibu na kuwapa ushirikiano mkubwa katika kazi zao.
  Picha ya pamoja. Picha zote na Daudi Manongi-WHUSM

  0 0

  Na Asteria Muhozya
  WAZIRI wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ameiaigiza  Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi  Tanzania (TGDC Ltd) kuwa ifikapo June 2016, iwe imeanza kuchoronga mashimo 3 katika eneo la Ziwa Ngozi ikiwa ni hatua ya mwisho inayohitajika kabla ya kuanza kujenga mitambo ya kuzalisha jotoardhi.

  "Utafiti muhimu umekamilika. Joto la maji ni kubwa, 230-250C linalokidhi uzalishaji wa umeme. Hiki kitakuwa ni chanzo kipya muhimu cha umeme jadidifu" ,alisema Prof. Muhongo.

  Ameongeza kuwa, jambo hilo haliwezi kuendelea kusubiri kutokana na mahitaji ya nishati hiyo nchini ikizingatiwa kuwa, Tanzania inapitiwa na  Bonde la Ufa kwa kiasi kikubwa.

  "Tayari wenzetu Kenya na Ethiopia wamepiga hatua kubwa katika nishati hii lakni kwa upande wetu hatuna megawati hata moja kwa hili lazima tuchukue hatua tutoke hapa tulipo. Hakuna kusubiri anzeni na Ziwa Ngozi" amesema Muhongo.

  Prof. Muhongo aliitaka Kampuni hiyo kuongeza nguvu katika eneo lenye viashiria vya jotoardhi la  Ziwa Ngozi kutokana na kuwepo maendeleo makubwa ya kitafiti ikilinganishwa na maeneo mengine yenye viashiria kama hivyo ikiwemo eneo la Mbaka lililopo Wilaya ya Rungwe.

  "TGDC tunataka umeme wa jotoardhi, wananchi wanataka umeme, hawatakuwa kusikia maneno, ifikapo Mwezi juni na  mimi nitakwenda Ngozi kuangalia mmefikia wapi na kama hakuna maendeleo tutabadilisha timu ya wataalamu", alisisitiza Prof. Muhongo.

  Akizungumzia kuhusu fedha za miradi, Prof. Muhongo alieleza kuwa, nchi nyingi duniani hazitegemei fedha za Serikali kutekeleza  miradi mikubwa ya nishati na ndiyo sababu hata Tanzania inatafuta fedha katika taasisi mbalimbali ikiwemo kukaribisha wawekezaji  ili kutekeleza miradi hiyo.

  "Serikali kwa upande wake itasaidia kuwezesha upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi na ninyi kazi yenu ni kuhakikisha umeme wa jotoardhi unaanza kutumika Tanzania kwa kuanza na Ziwa Ngozi".

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alisema kuwa amefarijika na maelekezo aliyoyatoa Prof. Muhongo na kuahidi kuweka nguvu kubwa katika kufuatilia suala hilo. " Ujio wako umetupa ari mpya katika kusimamia miradi hii kwa sababu rasilimali zipo lakini zimekaa tu nakuahidi kasi ya ufuatiliaji itaongezwa",alisema Kandoro

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rugwe ,Mwalimu Zainabu Mbusi alieleza kuwa maagizo ya Prof. Muhongo yamekuwa faraja na kuongeza kuwa, kukamilika kwa mradi huo itaongeza kasi ya ukuaji uchumi na kuifanya Tanzania kufikia lengo lake la kuwa miongoni mwa nchi za uchumi wa Kati ifikapo 2025.

  Kwa pande wake  Mbunge wa Jimbo la Busokelo, Fred Atupele alieleza kuwa, kukamilika kwa mradi huo kutachochea kasi ya uendelezaji wa viwanda vikubwa na vidogo na kueleza kuwa, kwa nafasi yake  watachukua jukumu la kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa vyanzo hivyo.

  Awali akieleza akieleza Mikakati ya Taasisi hiyo, Mkurugenzi wa TGDC , Mhandisi Boniface Njombe alisema eneo la Mbaka ni miongoni mwa maeneo ya maji moto yenye viashiria vya nishati ya jotoardhi.

  Vilevile, alieleza hivi sasa wataalam kadhaa wamesambaa wakifanya tafiti za mwisho katika  eneo la Mbaka ili kuanisha mipasuko na maeneo ya kuchimba nishati hiyo na kuongeza kuwa, TGDC imelenga kwa  kuanza kuzalisha umeme wa jotoradhi  wa kiasi cha  megawati 200 huku lengo ikiwa ni kufikia megawati 5000.

  Aidha, alieleza kuwa, mbali na kuzalisha umeme , maji moto yanaweza kutumika viwandani na majumbani katika kukausha mazao ikiwemo kuwa kivutio cha utalii kuoga kwa kuwa inaelezwa kuwa maji hayo yanatajwa kuwa tiba ya magonjwa ya ngozi.

  Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazopitiwa na Bonde la Ufa eneo ambalo linatajwa kuwa na viashiria vya nishati ya jotoardhi.

  0 0

  Na Woinde Shizza

  WACHUUZI wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wameiomba Serikali kutowabana walipe leseni ya ununuzi, kwani uwezo wao ni mdogo na wao ni madalali siyo wanunuzi wa madini hayo.

  Wakizungumza juzi wachuuzi hao walidai kuwa hawapingi kulipa mapato ya serikali ila zoezi la ulipaji wa leseni ya kununulia madini ya Tanzanite ingetakiwa kutekelezwa kwa wafanyabiashara peke yao na siyo kwa wachuuzi wadogo.

  Mmoja kati ya wachuuzi hao Anturusia Chande alisema wengi wao wanapewa madini hayo na kuzunguka kwenye masoko ya Mirerani kwa lengo la kujikimu maisha yao ikiwemo kusomesha watoto, mavazi, chakula na matibabu.

  “Sisi hatuvuki na madini nje ya eneo la Mirerani na tunategemea kuendesha maisha yetu kupitia uchuuzi huu mdogo mdogo na pia hatuna mtaji kwani tumejiajiri wenyewe serikali ituangalie kwa kupitia hili,” alisema Chande.

  Alisema wao wanachangia pato la Taifa kupitia sekta hiyo kwa kulipa kodi pindi wanaponunua bidhaa mbalimbali madukani ikiwemo sukari, mchele, mafuta ya kula, ya taa, sigara na nyinginezo ila bado wanasumbuliwa na serikali.

  Kaanael Minja alisema zoezi la kuwakamata wachuuzi ambao hawakulipa leseni lililoendeshwa wiki iliyopita, halikufanyika kwa haki kwani kuna baadhi yao waliporwa madini ambayo siyo yao na hawakurudishiwa hadi hivi sasa.

  “Kabla ya kuendesha kamata kamata hiyo wangetoa elimu kwanza kwa wachuuzi hao lakini kitendo cha kufika kijiweni na kuanza kuwakamata watu wasio na leseni siyo kizuri, wangepaswa kuwaelimisha kwanza,” alisema Minja.

  Hata hivyo, mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mahmoud Kambona aliwataka wachuuzi hao kujipanga na kulipia leseni ya ununuzi wa madini hayo ili waongeze mapato kwa serikali ambayo inawaletea wananchi maendeleo.

  “Wanatakiwa kutambua kuwa hiyo ni sheria ambayo imepitishwa na sasa kinachotakiwa ni utekelezaji kwani serikali zote hujiendesha kutokana na kodi ambazo zinalipwa na wananchi wake na siyo vinginevyo,” alisema Kambona.

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, (wanne kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Susan Kolimba, (watatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, EALA, kutoka Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji, 9wakwanza kushoto), Mh. Makongoro Nyerere (wapili kushoto), Mh. Angella Kizigha, (Wasita kutoka kushoto), naMh. Bernard Murunya). Wabunge hao walikwenda kumsalimia waziri Mahiga na kujitambuslisha ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza vikao vya bunge hilo jijini Arusha Januari 24, 2016. (K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

  NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, mapema leo Ijumaa Januari 15, 2016 amekutana na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania waliokwenda kujitambulisha na kubadilishana mawazo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  Wabunge hao waliongozwa na mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, Mh. Shy-Rose Bhanji, Mh. Angella Kizigha, na Mh.Bernard Murunya.

  Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Susan Kolimbanaye alikuwepo wakatiwa kikao hicho kifupi cha kutambuana.

  Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa wabunge wa EALA kutoka Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, alisema, “Tumefika kujitambulisha kwa Mh. Waziri kama ujuavyo yeye ni mgeni kwenye wizara hiyo, tulikuwana Dkt. Mwakyembe na sasa tunaye Dk. Augustine Mhiga, kwa hivyo tuliona ni vyematukafika kujitambulisha na kutambuana.” Alisema Mh. Makongoro na kuongeza, “Lakini pia lazima utambue kuwa vikao vya EALA, vinaanza Januari 24 pale Arusha na Mh. Mahiga ndiye mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, kwa hivyo sio busara tukakutanie kule ndio maana tumeona ni vema tukaja kumsalimia hapa atutambue na kubadilishana mawazo hapa na pale.” Alimaliza Mh. Makongoro.

  Bunge la Afrika Mashariki, EALA, ni chombo cha kutunga sheria cha Juamuiya ya Afrika Mashariki na linaundwa na nchiwanachama wa Jumuiya hiyo ambaonipamoja na Tanzania, inayoshikilia uenyekiti kwa sasa, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.
   Dkt. Mahiga, akisaliamiana na mmoja wa wabunge hao, Mh. Shy-Rose Bhanji.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  SAM_7218
  Kada maarufu wa chama cha mapinduzi ccm na mfanyabiashara wa madini mkoani Aarusha Thomas Munis akichukua fomu ya kuwania nafasi ya uwenyekiti wa mkoa ndani ya chama hicho hivikaribuni,  huku akiahidi mabadiliko makubwa ikiwemo kurudisha uhai wa chama katika jimbo la Arusha,kulia ni katibu msaidizi mkuu Omary Billaly
  SAM_7221
  Mgombea wa nafasi ya uwenyekiti wa mkoa ndani ya chama cha mapinduzi Mkoani Arusha Thomas Munis akionyesha fomu alizochukua kwa waandishi wa habari katika ofisi hizo jijini Arusha
  SAM_7250
  Thomas Munis akiongea na vyombo vya habari kuhusu nia yake ya kuchukua fomu hiyo ya kuwania nafasi ya uwenyekiti mkoa wa Arusha ambapo amehaidi ushirikiano mkubwa kwa wananchama pamoja na viongozi walipo katika kuleta mabadiliko ndani ya chama.
  ……………………
  (Habari picha na Pamela wa jamiiblog)
  OFISI ya chama cha mapinduzi, ccm, mkoa wa Arusha imetoa orodha ya wanachama 25,waliochukua fomu za kugombea uongozi ngazi ya mkoa kuziba nafasi ambazo ziko wazi ili kukamilisha safu ya uongozi ya Chama mkoa.
   
  Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibuni katibu msaidizi mkuu, Omary Billaly aliwataja waliochukua fomu na kurejesha nafasi ya mwenyekiti wa mkoa ndani ya ccm kuwa niJacob Meja Mollel, Juma Saidi Lossin,Victor Nicodemas Mollel, John Danielson Palangyo, Rabiel Fanuel Mbise,Hamis Saidi,Mussa Hamis Mkanga.Wengine ni Ally Jumbe, Metui Ailo ole Shaudo,MustafaPanju, Michael Lekule Laizer,Kenedy Danford Mpumilwa ,Raphael Long’idu Mollel, Karim Ephraim MushiGodson Loning’o,Thomas Munis,Emanuel Makongoro Lusenga.
   Wengine ni Henry Obed Mejooli,Veraikunda Zablon Urio,Babu Mohamed Kitume, Kisali Eliah, Bernadeth Silas Changulu,,Hafidhi Mwango Bakary,Agnes Gidion Mollel, na Ndewirwa Soori Mbise.Billaly aliongeza kuwa wanachama wawili ambao ni Shaaban Masawe na Rajab Mshana hawakurudisha fomu hizo.
   Walichukua fomu za kugombea ukatibu wa siasa na uenezi mkoa wa Arusha ni Peter Mathew Kasella, Veraikunda Zablon Urio,Gerald Eliaika Munisi, Lightness Ahadiel Mweteni,Japhet Zakaria Moirani, Anna Agatha Musuya,Jasper Augustino Kisumbua,Zam zam Ramadhan Abdalah, Emanuel Makongoro Lusenga,Amani Silanga Mollel, Victor Nicodemas Mollel, Ally Juma Mwinyimvua.
   Wengine ni Hamis Said Migire,Julius Laanyun Mollel,Cylius Daniel Mlekwa,Ahmed Mwita Chacha,Semmy Robson Kiondo,Revocutus Wiliam,Palapala ,Emanuel Abel Sirikwa,Loata Erasto Sanare,Joshua Hungura Mbwana,Njechele Eliakim Laizer.Godson Solomon Mollel, (Mzunguu).
   Wengine Shaaban Omar Mdoe, Wahabu Hemed MbagaaZIZI Abdalah Mfundo,Abel Smwel Kalama,Justus Enock Rwandezi,Sylevesta Kornen Meda, Lobora Petro Ndarapoi, na Victor Livingston Njau.

  0 0

  Miongoni mwa burudani maarufu duniani ni pamoja na "Fashion Industry' yaani mitupio inayowafanya watu kuwa katika good appearance Wanawake kwa Wanaume kuanzia miguuni mpaka kichwani. Wanamitindo kutoka hapa nchini Tanzania wamekuwa na utaratibu wa kuandaa Fashion Show ambazo zinatoa opportunity kwa Designers na Models.
  Hivyo basi new update kutoka Mama wa mitindo maarufu kama Asya Idarous ambaye kila mwaka huandaa Fashion Show inayo wakutanisha Designers "Lady in Red" amesema kuwa "Mwezi huu nitahakikisha "Lady in Red" inafanyika Tanzania coz tarehe 17 January, 2016, nategemea kukutana na designers pale Regency Hotel Mikocheni saa 10:00 jioni kwa ajili ya maandalizi ya "Lady in Red" inayotegemea kufanyika 31/1/2016 katika ukumbi wa "Danken House'.
  Pia Asya  Idorous aliongeza kuwa "2016  "Lady in Red" itaifanyika Tanzania na United_Kingdom (UK) Uingereza . So kwa wale wapenzi wa mitindo hapa ndio pake staytuned yaani kitu ni "Lady in Red" Cheers 2016.

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti wa Shughuli za Maendeleo ya Jamii Tanzania (RCSDS),Abraham Shempemba (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo , kuhusu mafanikio ya tafiti zao walizozifanya zinazoonesha takwimu za misaada iliyotolewa kisekta, gharama zilizotumika, uwajibikaji wa jamii na jinsi ilivyonufaika. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kituo hicho, Chrizostom Thadeo. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA).


  Na Celina Mathew

  KITUO cha Utafiti wa shughuli za maendeleo ya jamii Tanzania(RCSDS), kinatarajia kuzindua mfumo wa kielektroniki wa kukusanya, kuhifadhi na kuweka angani taarifa za kitafiti za uwajibikaji wa taasisi za binafsi, za umma na watu binafsi serikali kuu na za mitaa na hata mtu mmoja mmoja.

  Mfumo huo unatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi huu ambapo utapelekwa katika mikoa 30 Tanzania Bara pamoja na maeneo 100 yenye wananchi wenye uhitaji mkubwa.

  Akizungunza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa kituo hicho, Abraham Shempemba alisema lengo la mwendelezo huo ni kutoa nafasi kwa walengwa kutambua mchango unaotolewa kwao na wadau mbalimbali pamoja na misaada kwa jamii zenye uhitaji mkubwa.

  "Sisi kama RCSDS tunatambua uwepo wa makampuni, mashirika na taasisi mbalimbali za umma na binafsi zinazochangia kwa kiasi kikubwa mahitaji na hata majanga yanapotokea ili kunusuru na kuboresha maisha ya watanzania wenzetu na kuthamini michango na misaada yao,"alisema.

  Alisema mfumo huo unaoaznishwa una lengo la kutambua michango na misaada mbalimbali inayotolewa na wadau kwa jamii pia wadau nao wapate fursa ya kuweka malengo yao ya uwajibikaji kwa jamii kwa kuona ni wapi wanaweza kuwekeza zaidi kiuwajibikaji na eneo lipo nani amewekeza.

  Shempemba alisema utafiti walioufanya na kuutolea taarifa msimu ulipita kwa kushitikiana na taasisi ya ukaguzi ya Konsalt inayofanyika kila mwaka wapo waliosaidia jamii kwa sekta mbalimbali kama huduma za afya, maji, miundombinu, elimu, michezo, maafa na mambo mengine kwa asilimia tofauti.

  Aliongeza kuwa tafiti hizo pia zimesaidia takwimu za misaada iliyotolewa kisekta, gharama zilizotumika, uwajibikaji jamii ulivyowekezwa, jamii ilivyonufaika na misaada hiyo na wadau walivyonufaika na uwekezaji wao kwa jamii hizo.

  0 0

  Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro(kushoto)akiweka saini makubaliano kati ya Jiji la Arusha na kampuni ya Bondeni Seeds Limited yatakayowezesha eneo la Heka 750 kupimwa na kuwa kwenye mpango unaoendana mpango Mji wa Jiji katika eneo la Murieti wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Ngarenaro,Isaya Doita,Mbunge wa Arusha Mjini,Goodbless Lema,Mwanasheria wa Jiji,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji,Juma Idd na Mwanasheria wa Bondeni Seeds Limited leo.

  Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro(kushoto)akibadilishana hati za makubaliano  na Mkurugenzi wa kampuni ya Bondeni Seeds Limited ,Rakesh Vohora  ya kuendeleza eneo la Heka 750 eneo la Muriet linalomilikiwa na kampuni hiyo .

  Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro akizungumza  baada ya hafla kuweka saini makubaliano kati ya pande mbili.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,Juma Idd akifafanua umuhimu wa ushirikiano kati ya Jiji na kampuni hiyo.

  Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Goodbless Lema akizungumza katika hafla hiyo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
  Halmashauri ya Jiji la Arusha imesaini makubaliano na kampuni ya Bondeni Seeds Limited kupima eneo linalomilikiwa na kampuni hiyo lenye ukubwa wa Hekari 750 ili liwe sehemu ya Master Plan ya  Jiji .
  Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro amesema wameshawishika kuingia makubaliano hayo na mwekezaji huyo ili kuwezesha wananchi kuishi kwenye maeneo yaliyopimwa yanayoendana na hadhi ya Jiji na kulipatia mapato yanayotokana naupimaji huo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji,Juma Idd amesema wamekubaliana na mwenye eneo hilo kulipanga na kuliendeleza kama sheria ya makazi inavyotaka.
  "Hatutaweza kuendelea na makazi ambayo hayajapimwa kama Unga Limited ,Ngarenaro na mengine ,Arusha ni eneo lenye umuhimu wake katika sekta ya utalii,madini na ukizingatia hapa ndio Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na taasisi za kimataifa.
  Amesema baada ya kusaini makubaliano utekelezaji unaanza mara moja ili kufikia malengo ya kuweka mji uliopangika.
  Mbunge wa Arusha Mjini,Goodbless Lema amewataka wananchi wenye maeneo makubwa kushirikiana na uongozi wa Jiji ili maeneo yao yapimwe kuepusha makazi holela na kuwataka waliojenga maeneo ya mabondeni na kwenye vyanzo vya maji kubomoa nyumba zao.

  0 0


  0 0

   Taswira ya daraja la kisasa linalojengwa eneo la Kurasini jijini Dar es Salaam, ambalo litakatisha bahari ya hindi hadi eneo la Kurasini huko Kigamboni. 
  Daraja hilo linalojengwa kwa ubia kati ya serikali na mfuko wa hifadhi ya jamii wa NSSF litakuwa na urefu wa kwenda juu (Vertical) mita zaidi ya 680 wakati urefu mlazo (Horizontal) utakuwa zaidi ya kilomita 2. 
  Daraja hilo la kuning'inia (Cable-stayed bridge) linajengwa na kampuni ya China Railway Jiangchang Engineering (T) Ltd na China Major Bridge Engineering Company kwa gharama ya dola za Kimarekani  136 milioni. Lilianza kujengwa Februari 2012 na linatarajiwa kumalizika mwaka huu.


  0 0

   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni (kushoto), akiongozana  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),Dickson Maimu (kulia), wakati wa ziara ya kutembelea moja ya ofisi za mamlaka hiyo,iliyopo barabara ya Ali Hassani Mwinyi,jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri aliweza kupata fursa ya kuangalia jinsi utengenezaji wa kitambulisho cha Utaifa unavyofanyika.

   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni, akiwa katika kikao na viongozi mbalimbali wa Vitengo vya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),wakati wa ziara iliyoanzia Makao Makuu ya Mamlaka hiyo,jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Dickson Maimu.

  Afisa Msajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), Emmanuel Joshua(kushoto), akitoa maelezo jinsi taarifa za muombaji wa kitambulisho cha Taifa zinavyohakikiwa kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni(katikati),wakati wa ziara ya Naibu Waziri kwenye mamlaka hiyo,jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0
 • 01/15/16--09:09: INTRODUCING VIWANGO WEBSITE
 • Viwango is a Tanzania-based website containing crowd-sourced reviews and ratings of local service providers. Viwango was created to help people find the best local service providers like electricians, plumbers, mechanics, handymen, hotels, restaurants, bars, coffee shops, and more. 

  We collect reviews and ratings from consumers who have received different services from different service providers. All of our members are just like you looking for honest companies and individuals who provide high quality services. Our members provide highly detailed information regarding their experience from service providers. 

  FASTEST WAY TO FIND THE SERVICES YOU NEED!

   JOIN US  WWW.VIWANGOTZ.COM
  FOLLOW US ON SOCIAL MEDIA:
                                      INSTAGRAM: @VIWANGO
                                         FACEBOOK: @VIWANGO TANZANIA
                                             TWITTER: @VIWANGOTZ

  CONTACT US:
  PHONE: +255678223329
  SKYPE: VIWANGO.TANZANIA

  0 0

  Minister of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Hon. Dr. Augustine Mahiga (R) is in the conversation with the Namibian Ambassador to Tanzania, H.E Japhet Isaack whose tour of duty in the country is over. In their meeting, the two insisited the importance of enhancing bilateral cooperation between Tanzania and Namibia especially economic cooperation in order to increase the volume of trade.
  Dr. Mahiga presents a farewell gift to the Namibian Ambassador to Tanzania who finished the tour of duty.
  Minister of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Hon. Dr. Augustine Mahiga (R) is in the conversation with the Sudanese Ambassador to Tanzania, H.E Yassir Mohammed Ali whose tour of duty in the country is over. In their meeting, the two insisited the importance of enhancing bilateral cooperation between Sudan and Tanzania especially economic cooperation in the areas of irrigation, oil and gas and technology.
  Sudanese Ambassador to Tanzania presents gift of various publications to Dr. Mahiga.
  Dr. Mahiga presents a farewell gift to the Sudanese Ambassador to Tanzania who finished the tour of duty.

  0 0


   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Chimbeni  Kheir Chimbeni  kuwa Mshauri wa  Rais Masuala ya  Utamaduni hafla iliyofanyika  katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Juma Hassan Reli  kuwa  Katibu  Mtendaji wa Tume ya Mipango, katika hafla iliyofanyika  katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,kabla alikuwa Naibu Gavana wa Benki ya Tanzania
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Mdungi Makame Madungi kuwa  Katibu Kamisheni ya Utumishi wa Umma katika hafya  iliyofanyika  leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Kai Bashir Mbarouk  kuwa Naibu  Katibu Wizara ya Katiba na Sheiria katika  hafla iliyofanyika  katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo. Picha na Ikulu, Zanzibar.

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro (CHADEMA) Mh. Freeman Mbowe akimueleza jambo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson kabla ya kuanza kwa kikao cha wajumbe wa kamati ya kanuni na Spika, Katika Ofisi za Bunge leo Jijini Dar es Salaam
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai (Katikati) akiwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson (kushoto) na  Mbunge wa Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro (CHADEMA) Mh. Freeman Mbowe kabla ya kuanza kwa kikao kilichowakutanisha wajumbe wa kamati ya kanuni na Spika, Katika Ofisi za Bunge leo Jijini Dar es Salaam leo tarehe 15/01/2015.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akiongoza kikao cha wajumbe wa  kamati ya kanuni Katika Ofisi za Bunge leo Jijini Dar es Salaam.

   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akiongoza kikao cha wajumbe wa  kamati ya kanuni Katika Ofisi za Bunge leo Jijini Dar es Salaam.

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akiongoza kikao cha wajumbe wa  kamati ya kanuni Katika Ofisi za Bunge leo Jijini Dar es Salaam.  0 0


older | 1 | .... | 1090 | 1091 | (Page 1092) | 1093 | 1094 | .... | 3272 | newer