Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1089 | 1090 | (Page 1091) | 1092 | 1093 | .... | 3278 | newer

  0 0

    Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (katikati) akiwa na wahitimu wenzake walipokuwa wakitunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa wakati wa Mahafali yao yaliyofanyika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana Januari 13, 2016.
   Picha na Mafoto Media/Muhidin Sufiani
   Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (katikati) akiwa na wahitimu wenzake Janeth Nyoni (kushoto) na Hadija Hashim, baada ya kutunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa wakati wa Mahafali yao yaliyofanyika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana.
   Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (kushoto) akiwa na Meneja Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, baada ya kutunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa wakati wa Mahafali yao yaliyofanyika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana Januari 13, 2016. Kulia ni mke wa Balozi wa Tanzania nchini Geneva, Rose Mero.
  Picha na Mafoto Media/Muhidin Sufiani

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia), akimsikiliza Rais wa Mahakama ya Afrika Jaji Mstaafu, Mhe. Augustino Ramadhani alipofika kumtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Waziri. Pia kuzungumzia masuala mbalimbali yanayoihusu Mahakama hiyo likiwemo suala la ujenzi wa Mahakama hiyo katika Jiji la Arusha. 
  Afisa Mambo ya Nje, Bw. Elisha Suku naye akielezea jambo katika mazungumzo kati ya Waziri Dkt. Mahiga na Mhe. Ramadhani (hawapo pichani), wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Baraka Luvanda, na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizarani, Bi. Mindi Kasiga. 
  Mazungumzo yakiendelea.
  Picha na Reginald Philip.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Susan Kolimba akizungumza na Balozi wa Syria hapa nchini Mhe.Abdulmonem Annan, baada ya Balozi huyo kumtembelea Naibu Waziri kwa ajili ya kumpongeza na kuzungumzia namna ya kuimarisha mahusiano ya nchi hizi mbili.
  Balozi wa Syria hapa nchini Mhe.Abdulmonem Annan, akizungumza jambo na Mhe. Naibu Waziri wakati wa mazungumzo hayo.
  Msaidizi wa Naibu Waziri, Bw. Adam Isara (kulia), akifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.
  Picha na Reuben Mchome.

  0 0

  Na Nyakongo Manyama- MAELEZO.
  Wizara ya Nishati na Madini imekanusha habari iliyopotosha umma kuhusu mradi wa umeme wa Kinyerezi II kuwa bado haujaanza na gharama zilizoandikwa si za kweli.

  Wizara hiyo imekanusha habari hiyo, iliyoandikwa katika gazeti la Mtanzania la leo Januari 14, mwaka huu toleo namba 8063, lenye kichwa cha habari “ Harufu ya Jibu Mradi wa Umeme.”

  Habari hiyo ambayo ilieleza kwamba mradi huo ulizinduliwa na Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Dkt.Jakaya Kikwete uligharimu Sh. trilioni 1.6 na kwamba fedha za ujenzi wa mradi huo zimetokana ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Japan,ambapo Serikali ya Tanzania itakuwa na hisa ya asilimia 40 na kampuni ya SUMITOMO ya Japan asilimia 60. 

  Aidha habari hiyo ilidai kuwa Serikali inachangia fedha za ndani kwa asilimia 12 na zilizobaki zikiwa na mkopo kutoka benki ya Japan na kwamba gharama za mradi huo ziko juu ikilinganishwa miradi mingine akitolea mfano Kampuni ya TALLAWARA Power Station ya nchini Australia anayodai ilitaka kujenga mradi huo kwa dola za Marekani milioni 350.
  Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mawasiliano Serikali wa wizara hiyo, Badra Masoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu habari hiyo katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam. 

  “Serikali ya Tanzania iliingia makubaliano na Serikali ya Japan ya mkopo wa masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 292 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kuzalisha umeme wa Megawati 240 utakaojengwa na kampuni ya SUMITOMO kama mkandarasi wa “EPC contractor” na sio kama mbia wa Serikali yaTanzania kama ilivyodaiwa.

  “Mradi huo unamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 kupitia TANESCO na hakuna mwekezaji mwingine katika mradi huo.

  Hivyo si kweli kwamba Serikali ya Tanzania na kampuni ya SUMITOMO zinawekeza kwa ubia wa asilimia 40 (kwa Serikali ya Tanzania) na asilimia 60 kwa SUMITOMO. Kwa maana hiyo hatutauziwa umeme utakaozalishwa na mradi huu kwani ni mali yetu na hakuna gharama yoyote ya ziada kama alivyodai mwandishi wa habari hiyo,” alisema Badra.

  Aidha Badra alisema mwandishi huyo alidai kwamba mradi huo ulizinduliwa na Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, wakati ni kwamba mradi huo haujazinduliwa bado na sasa upo katika maandalizi ya kuwekwa katika jiwe la msingi.

  Akizungumzia kuhusu gharama za mradi huo, alieleza kuwa unatekelezwa kwa dola za Marekani milioni 344 sawa na Sh. bilioni 740 zikiwa ni mkopo wa masharti nafuu wa asilimia 85 sawa na dola za Marekani 292 na mchango wa Serikali ya Tanzania kwa asilimia 15 sawa na dola za Marekani milioni 52.( na sio asilimia 12 kama ilivyodaiwa na mwandishi huyo). 

  “Mwandishi wa habari hii amejaribu kufananisha uwekezaji huu na uwekezaji wa TALLAWARA Power Station ya Australia na kudai kwamba gharama yake ingekuwa ndogo kuliko gharama ya mradi huu. Taarifa hii haina ukweli wowote kwa sababu gharama ya dola milioni 344 zinazotarajiwa kutumika mkatika mradi huu iko chini kuliko dola milioni 350anazodai mwandishi kwamba zingetumiwa na kampuni TALLAWARA.

  “Aidha, kampuni ya TALLAWARA haijawahi kuomba au kuonesha nia ya kuwekeza katika mradi wowote wa kufua mradi wa umeme nchini. Pia ni muhimu ifahamike kwamba makubaliano ya mkopo huu yalikuwa yanakwenda sambasamba na utekelezaji wa mradi wenyewe (EPC with Financing). 

  Badra aliongeza kwamba pamoja na kwamba gharama za uwekezaji wa mradi huo wa kwanza wa aina ya “Combined Cycle” nchini zinawiana na gharama za miradi mingine ya aina hiyo duniani, gharama za uwekezaji zinaweza kutofautiana kutegemeana na mazingira ya nchi na nchi, teknolojia iliyotumika na aina ya mitambo.

  Hivyo sio suala la kulinganisha gharama ya mradi mmoja na mwingine .
  Wizara hiyo imeshauri waandishi wa habari kufuata miiko na maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari zenye ukweli na sahihi na zilizozingatia pande zote mbili kwa kuwa ipo na tayari kujibu maswali ya waandishi wakati wowote.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (hawapo pichani), katika ukumbi wa Chuo cha Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
   Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Rogatius Kipali, akitoa shukrani kwa mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (hayupo pichani), baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi hilo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa tatu kutoka kulia), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na washiriki wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ulifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Wa tatu kutoka kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Injinia Pius Nyambacha na wa poli kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utalawa na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Lilian Mapfa. 
  (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

  0 0

  1
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga akihutubia jana wakati wa mahafali ya Chuo cha Diplomasia yaliyofanyika jana chuoni hapo Kurasini jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wahitimu wa shahada mbalimbali, Wahadhiri na wageni waalikwa ambapo mmoja wa Mwanahabari kutoka kituo cha Televisheni cha ITV Bw. Spensor Lameck alikuwa ni mmoja wa wahitimu.
  2
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga akiwa katika jukwaa kuu na viongozi mbalimbaliwa chuo hicho pamoja na wahadhiri wakati wa mahafali hayo.
  6
  Mwanahabari kutoka kituo cha Televisheni cha ITV Bw. Spensor Lameck akipata picha ya pamoja na wahitimu wenzake wakati wa mahafali hayo.
  8
  Mwigizaji wa filamu Christina Manongi maarufu kama Sinta kulia akiwa na mhitimu mwenzake wakati wa mahafali hayo.
  10
  Mwanahabari kutoka kituo cha Televisheni cha ITV Bw. Spensor Lameck akipata picha ya pamoja na Christina Manongi maarufu kama Sinta kulia na mhitimu mwenzao.

  0 0

  Mugishagwe Zablon.

  Wafanyabiashara zaidi ya 300 wa jijini Dar es Salaam, wanakutana kesho Ijumaa jijini Dar es Salam, kujadili hotuba ya Rais John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati alipozungumza nao 3 Desemba mwaka huu kuona kama inajibu changamoto zinazowakabli.

  Akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari kuhusiana na mkutano wa wafanyabiashara wanachama wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa TCCIA, Francis Lukwaro alisema kuna hoja ambazo wameona wazijadili.

  Alisema mkutano huo umelenga kutazama mwelekeo wa sekta binafsi katika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha mazingira ya biashara na ukuzaji uchumi ili sekta hiyo iweze kutoa mchango wa maana tofauti na ilivyo sasa.

  Lukwaro alisema wanachama wa TCCIA wana mapendekezo ambayo watayawasilisha kwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage ambaye atakuwepo katika majadiliano hayo katika maeneo ya sheria na taratibu jinsi zitakavyoongeza faida na kukuza biashara na shghuli za kiuchumi.

  Mchango wa sekta binafsi katika kuongeza mapato ya serikali na fursa za uwekezaji ambazo zilidokezwa na Rais Magufuli wakati wa mkutano wake na wafanyabiashara ambao pamoja na mambo mengine aliwasisitizia kufuata sheria ikiwa ni pamoja na kulipa kodi stahiki serikalini.

  Awali Katibu Mtendaji wa TCCIA, Daniel Machemba alisema kuwa mkutano huo ni muhimu katika uboreshaji wa sekta hiyo na majadiliano kama hayo yatafanyika nchi nzima kupitia matawi ya taasisi hiyo yaliyopo takribani nchi nzima.

  “Lengo ni kuona tunafika sehemu nzuri na kuondoa vikwazo vya biashara vinavyowakabili wanachama wetu” alisema na kuongeza kuwa nchini kuna fursa nyingi za biashara lakini hazijatengenezewa mazingira mazuri ili ziweze kuwanufaisha wafanyabiashara, wananchi na serikali kwa ujumla.

  Katika hatua nyingine, Katibu Mtendaji wa TCCIA, Daniel Machemba alisema taassi yao haitakuwa na msaada wowote kwa wafanyabiashara wakwepa kodi kwani bila makusanyo hayo ya serikai hakuna maendeleo ambayo yanaweza kupatikana.

  Alisema wanapongeza atua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya nne katika kusimamia ukwepa wa kodi unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara na watendaji wasio waadilifu na wanaungana nae katka ilo na watahakikisha vita hiyo inafanikiwa ili kuwaletea wananchi maendeleo.

  “Kipindi kirefu tunashirikiana vizuri na serikali hivyo hata kwa ili tupo pamoja na tutatoa ushirikiano unaotakiwa ili kuhakikisha mianya yote ya ukwepaji odi inadhibitiwa na serikai inapata kodi na tzo zake zingine” alisema Machemba na kuongeza kuwa ndani ya taassis hiyi ‘ni kazi tu’.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara, Wenyeviwanda na Kilimo (TCCIA), Francis Lukwaro (kushoto), akizungumza jana kuhusiana na mkutano wa kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya biashara nchini, unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kesho Ijumaa. Kulia ni Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo, Daniel Machemba.
  Katibu Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara, Wenyeviwanda na Kilimo (TCCIA), Daniel Machemba akizungumza jana kuhusiana na mkutano wa kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya biashara nchini, unaotarajiwa kufanyika jijiji Dar es Salaam kesho Ijumaa. Kushoto ni Mwenyekiti wa BNN Group Ltd, Paul Koyi na mwenyekiti wa TCCIA, Francis Lukwaro. Picha na Mugishagwe Zablon.

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akizungumza na wandishi wa habari juu ya kuhairishwa kwa kesi dhidi ya bomoabomoa ambayo itasomwa tena Januari 25 mwaka huu.
   Kesi hiyoilifumguliwa ili kupinga agizo la wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ambapo walikuwa wanabomoa maeneo hatarishi na maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi. 
  Kesi hiyo ya zuio la bomoabomoa imesomwa leo na Jaji Panterine Kente leo katika mahakama kuu kitengo cha ardhi jijini Dar es Salaam.
   Wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia leo katika Mahakama kuu kitengo cha ardhi jijini Dar es Salaam leo.
  Wananchi wakiwa nje ya Mahakama kitengo cha Ardhi leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii.

  0 0

  Michezo ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa tatu imeendelea kwa mchezo mmoja kuchezwa mjini Songea, ambapo timu ya JKT Mlale imeiondosha Majimaji kwa mabao 2-1.

  Michuano hiyo ambayo Bingwa wake ataiwakilisha Tanzania kwenye kombe la Shirikisho Afrika 2017 (CC), imekua ya kuvutia na hasa kwa timu za madaraja ya chini kuziondosha timu za mdaraja ya juu.

  JKT Mlale imekua timu ya kwanza kutoka daraja la kwanza kufuzu kwa hatua ya 16 bora, ambapo sasa inasubiria washindi wengine 15 kutoka katika michezo itakayochezwa wikiendi ya Januari 23-17, 2015.

  Mpaka sasa kuna timu za saba za daraja la Pili zinawania kufuzu kwa hatua ya nne, timu hizo ni Abajalo  (Dasm), Madini (Arusha), Mvunvuma (Kigoma),

  Pamba (Mwanza), Wenda (Mbeya), Mshikamano (Dsm), na Singida United (Singida), huku za daraja la kwanza timu 8 zikisaka nafasi ya kuingia hatua ya 16.

  Timu za daraja la kwanza ni Ashanti United (Dsm), Burkinafaso (Morogoro), Friends Rangers (Dsm), Geita Gold (Geita), Lipuli (Iringa), Njombe (Njombe), Panone (Kilimanjaro) na Rhino Rangers (Tabora).

  0 0

  SHIRIKA la ndege la taifa la umoja wa falme za nchi za kiarabu la Etihad limefurahishwa na ufanisi na utendaji wa operesheni zake kwa mwaka wa 2015 zilizowafanikisha kufikia malengo yao ya ukuaji ambapo sasa wanabeba abiria wengi na mizigo mingi zaidi ya awali.
  Mwaka jana Shirika lilibeba abiria milioni 17.4, sawa na asilimia 17 zaidi ya mwaka 2014, wakiendesha safari 97,400 za ndege zilizofikisha jumla ya kilomita milioni 467. 

   Hii ni dhahiri kwamba abiria walifurahia huduma hizi na hivyo uhitaji uliongezeka, jambo ambalo lilisisitiza nguvu ya mikakati ya ukuaji iliyowekwa na shirika la ndege la Etihad.

  Kwa ujumla, ndege za Etihad pekee zimebeba zaidi ya asilimia 75 ya abiria waliosafiri kwenda na kuondokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi katika mwaka wa 2015. Etihad pamoja na washirika wake walio na ndege zinazofika mji huo mkuu wa UAE wamefikisha jumla ya asilimia 84 ya abiria waliotua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi.

  James Hogan, Rais na Afisa Mkuu Mtendaji wa Etihad, alisema: “Katika mwaka 2015, tumeweza kuwapa mamilioni ya wasafiri chaguo lenye thamani ya fedha katika usafiri wa anga na tumeleta nguvu mpya ya ushindani katika sekta hii. Yote haya yametokana na huduma zetu zinazokidhi viwango vya kimataifa ambazo pia zimejizolea tuzo mbalimbali. Pamoja na hayo, mashirika mengi yanavutiwa kujiunga nasi na tunazidi kuongeza idadi ya washirika wetu, kukuza ukubwa wa mitandao yetu ili kufika sehemu nyingi zaidi duniani. 

  Hamna shirika lingine lenye kuleta tija na ushindani wa viwango hivi katika sekta hii”. Katika mwaka 2015, Shirika la Etihad limezindua njia mpya kwenda Kolkata, Madrid, Edinburgh, Entebbe, Hong Kong na Dar es Salaam, pamoja na huduma ya moja kwa moja kwenda Brisbane.

  Mwaka jana pia Etihad walianza kutumia ndege aina ya Boeing 787-9 Dreamliner, ambayo ilianza kutoa huduma za ndege za biashara kwenda Washington DC, Zurich, Singapore na Brisbane. Mtandao wa ndege aina ya Airbus A380 umeongeza huduma zake za kuelekea London Heathrow na kuanza safari mpya za kuelekea Sydney na New York.

  Mwaka huu, Shirika litaongeza  safari zake za kwenda London Heathrow hadi kufikia safari tatu kwa siku hii ni pamoja na mwanzo wa safari mpya za ndege aina ya A380 kufika Mumbai na Melbourne, wakati Boeing 787 itaanza kupaa kwenda vituo vipya vya Düsseldorf, Perth, Shanghai, Istanbul na Johannesburg.

  Etihad pia iliongeza mizunguko katika njia za kusafiria 16 zinazotumika hivi sasa ambazo hufika Bangkok, Chennai, Dammam, Delhi, Hong Kong, Hyderabad, Istanbul, Jeddah, Kochi, Kozhikode, Melbourne, Mumbai, Muscat, Seychelles, Tehran na Trivandrum.

  Ili kukabiliana na kasi ya ukuaji wake, Shirika la ndege la Etihad liliongeza idadi ya washirika wake mwaka jana. Mkakati huu uliwapa fursa abiria zaidi ya milioni tano kutumia ndege za Etihad, iliyosababisha ongezeko la asilimia 43 ambayo ni abiria milioni 3.5 zaidi kuliko 2014.

  Mkakati mwingine ni makubaliano waliyozindua na Shirika la kimataifa la ndege la Pakistan (PIA), wakati Etihad inaendelea kukuza na kuendeleza ushirika wake na mashirika ya  Air Serbia, American Airlines, flynas, Jet Airways, Korean Air, NIKI and S7.

  Kutokana na hayo, Etihad sasa inawapa fursa abiria wake kuwa katika mtandao utakaowawezesha kusafiri na kusafirisha mizigo kwenda sehemu 600 kwa kuunganisha ndege na moja kati ya washirika wake 197 ama kusafiri na washirika wake wa “codeshare” 49.   
  Mnamo mwezi wa nne wa mwaka 2015, Shirika la ndege la Etihad lilipata kibali kutoka kwa Ofisi ya Shirikisho la Usafiri wa Anga ya Uswisi (FOCA) kukamilisha asilimia 33.3 ya uwekezaji katika shirika la ndege la Darwin, ambazo ni ndege zinazoruka kanda za Uswisi.

  Ndege za shirika la Etihad ziliripoti kubeba tani 592,090 sawa na ongezeko la asilimia 4 mwaka hadi mwaka. Mwaka jana, ndege hizi zimebeba asilimia 88 ya mizigo ya bidhaa kuingia na kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege wa Abu Dhabi.

  Katika mwaka 2015, Etihad imefikisha mizigo vituo vipya sita duniani na sasa huduma hii ya kusafirisha mizigo inapatikana katika jumla ya vituo 96 ambavyo hutumika na abiria wakati wa kusafiri. Shirika limepanua uwezo wake wa kusafirisha mizigo kufika masoko mapya yakiwemo Dakar, Nouakchott na Douala, ambapo imefanya jumla ya vituo vinavyosafirisha mizigo tu kuwa 20.

  Kufikia mwisho wa mwaka 2015, Etihad ilifikisha jumla ya ndege 121 (ogezeko la asilimia 9 mwaka hadi mwaka) yenye wastani ya umri wa miaka 5.8- kulifanya kuwa shirika lenye ndege changa na zisizoharibu mazingira kati ya wapinzani katika sekta nzima. Mwaka 2015 Shirika lilipokea Airbus 11 (A380 nne, A321 sita na A320 moja) na Boeing 787-9 Dreamliner nne huku wakiongeza nafasi za kukodi pia.

  Ili kuunga mkono mikakati iliyojiwekea ya kukuza mtandao wao duniani, shirika la Etihad litapokea ndege nyingine mwaka huu, zikiwemo Boeing 787-9 tano, A380 tatu na Boeing 777-200 Freighters mbili.

  Bwana Hogan alisema: “Tumeingia mwaka 2016 kwa kujiamini kwamba nguvu tulizoonesha awali zitaendelea na zitatumika kuitambulisha Abu Dhabi kama kitovu cha usafiri wa anga duniani.

  “Tunaendelea kukabiliana na changamoto, ikiwemo suala la ulinzi wa urithi wa wasafirishaji wakubwa Marekani na Ulaya. Tunaendelea kuboresha huduma zetu ili kuwahakikishia wasafiri wetu kwamba wanachagua kilicho bora kati ya sisi na washindani wetu”.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2016. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na kushoto kwake ni Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa. Picha na IKULU.

  0 0

  Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akizungumza na Ujumbe wa Wafanyabiashara wa Team Mabadiriko kutoka soko kuu la Kariakoo, Jijini Dar es salaam waliomtembelea Ofisini kwake leo Januari 14, 2016.
  Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Team Mabadiriko kutoka soko kuu la Kariakoo, Severin Mushi, akizungumza wakati akiutambulisha ujumbe wake kwa Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, walipokwenye kumuona leo Januari 14, 2016.
  Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyabiashara wa Team Mabadiriko kutoka soko kuu la Kariakoo, mara baada ya kuzungumza nao leo, Jijini Dar es salaam.

  0 0


  0 0

  Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald,(wakwanza kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani jinsi ya kupata taarifa kuhusu huduma mbalimbali za Airtel kupitia komputa zilizoweka katika duka jipya la Airtel Expo wakati wa uzinduzi rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso (nyuma katikati) na Meneja huduma kwa wateja bi, Zakia Omary
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani akiongea wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kisasa la Airtel Expo lililopo katika makao makuu ya Airtel Morocco, jijini Dar es Saalam. Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasilino wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya.
  Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald (kulia) akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani juu ya huduma zinazopatikana katika duka jipya wakati wa uzinduzi wa duka hilo. wakishuhudia (kutoka kushoto)katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano prof faustine Kamuzora, Naibu katibu mkuu Dr Mary Sasabo na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani pamoja na mkurugenzi mkuu wa Airtel kwa pamoja wakibonyesha kitufe kuashiria uzinduzi wa duka la Airtel Expo lililopo makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam.
  Shamrashamra za uzinduzi wa duka la Airtel Expo Morocco, jijini Dar es Saalam.
  Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald,(kwanza kushoto) akimuonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani vifaa na simu mbalimbali vinavyopatikana katika duka jipya la Airtel Expo wakati wa uzinduzi rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel Morocco, jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso (wa kwanza kulia) akifatiwa na Meneja huduma kwa wateja bi, Zakia Omary.

  0 0

  Na Veronica Simba – Dodoma.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa amefanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Chuo cha Madini Dodoma (MRI).

  Ziara hiyo iliyofanyika jana Januari 13, 2016 mjini Dodoma, ziliko Taasisi hizo, ililenga kujitambulisha kwa viongozi na watumishi pamoja na kujionea kazi na huduma mbalimbali wanazotoa kwa wananchi.

  Katibu Mkuu alikutana na viongozi wa GST na wa Chuo cha Madini ambapo alipokea taarifa ya utendaji, kisha akakutana na wafanyakazi wote wa Taasisi hizo na kuzungumza nao kuhusu majukumu yao na changamoto walizonazo kiutendaji.

  Baada ya kukutana na Wafanyakazi, Katibu Mkuu Ntalikwa alitembelea majengo mbalimbali ya Wakala kujionea kazi zinazofanyika ambapo ni pamoja na Maabara mpya ya kisasa ya Uhandisi wa Kijiolojia, Chumba chenye mitambo na mashine za kisasa zinazohifadhi data mbalimbali, chumba maalum kinachohifadhi nyaraka na machapisho mbalimbali pamoja na Maabara ya kuchenjua Madini (Mineral processing Laboratory).

  Ziara ya Katibu Mkuu Ntalikwa katika Ofisi za GST na MRI ni mwanzo wa ziara anayofanya kutembelea Mashirika na Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ili kujitambulisha na kujionea kazi na huduma wanazotoa. Profesa Ntalikwa ataendelea na ziara mjini Dodoma kwa kutembelea Ofisi za Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Ofisi za Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco).
  Mtumishi katika Maabara ya Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Kamana Camilius (mwenye Koti la Bluu) akimweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini (wa pili kutoka Kulia) namna Maabara hiyo inavyofanya kazi. Wengine pichani ni Viongozi wa GST.
  Mtumishi katika Maabara mpya ya kisasa ya Uhandisi wa Kijiolojia inayomilikiwa na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Godson Kamihanda (wa pili kutoka Kushoto) akimweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini (katikati) namna Maabara hiyo inavyofanya kazi. Wengine pichani ni Viongozi wa GST.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (mbele) akikagua Jengo jipya la Ofisi ya Madini – Dodoma. Pamoja naye pichani ni Viongozi wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST). Jengo hilo lipo jirani na Ofisi za GST.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Leticia Nyerere enzi ya uhai wake

  Familia ya Nyerere inependa kuwataarifu, kuwakaribisha na hatimae kujumuika nao katika misa ya kumbukumbu ya mpendwa mama yao Leticia Nyerere itakayofanyika siku ya Jumamosi Januari 16, 2016 saa 6 kamili mchana (12 pm sharp) katika kanisa la Mtakatifu Edward lililopo Baltimore, Maryland kwenye anuani ifuatayo hapo chini.
   901 Poplar Grove Street,
  Baltimore, MD 21216
  Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzio.
   Kwa maelezo na maelekezo zaidi tafadhali wasiliana na 
  Margareth Mageni 240 462 9138
  Emmanuel Muganda 240 447 2801
  Ramadhani Kamguna 202 459 3839

  Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe.

  0 0


  0 0
  0 0

  Pongezi nyingi kwa Basilla Mwanukuzi (Miss Tanzania 1998) kwa kulamba nondozzz ya  stashahada ya uzamili  (PGD)  katika menejimenti ya uhusiano wa kimataifa leo 13th January 2016 katika chuo cha Diplomasia jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kikanda, Afrika na Kimataifa Balozi Andrew Mahiga

   Basilla Mwanukuzi (Miss Tanzania 1998) akiwa na wanafunzi wenzie baada ya kutunukiwa stashahada ya uzamili  (PGD)  katika menejimenti ya uhusiano wa kimataifa

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  MFANYABIASHARA Morris John au Maliyanga (46) na wenzake watatu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu shitaka la unyang’anyi wa kutumia silaha wa vitu mbalimbali zikiwemo Dola za Marekani zenye thamani ya sh. milioni 18.5.

  Maliyanga, mkazi wa Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam, dereva pikipiki Frano Msaru au Singu (23) na wafanyabiashara Jeremiah Flavian (26) wakazi wa Sinza na Sandru Kamugisha (39), mkazi wa Kijitonyama, walifikishwa mahakamani hapo jana.

  Washitakiwa walipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Riwa, ambapo Wakili wa Serikali, Honolina Mushi, aliwasomea shitaka hilo.

  Akiwasomea shitaka hilo, Honolina alidai washitakiwa walitenda kosa hilo, Desemba 22, mwaka jana, maeneo ya Mabibo Ruhanga, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.

  Alidai kuwa siku hiyo washitakiwa hao waliiba Dola za Marekani 8,600 sawa na sh. milioni 18.5 fedha taslim sh. milioni 2.5, kompyuta mpakato, simu nne za mkononi mali ya Anderson Aloyce.

  Inadaiwa kabla na baada ya kutenda kosa hilo, washitakiwa hao waliwatishia Zeno Genes, Aneth Paulo na John Renatus kwa bastola ili waweze kufanikisha kupata vitu hivyo.

  Washitakiwa hao walikana shitaka hilo, ambapo Wakili Honolina alidai upelelezi haujakamilika na kuomba shauri hilo kuahirishwa hadi tarehe nyingine kwa kutajwa.

  Kwa upandewa mshitakiwa wa Msaru aliomba apewe kibali cha kwenda kutibiwa mguu kutokana na majeraha aliyodai kuyapata baada ya kupigwa akiwa polisi.

  Aidha Hakimu alimtaarifu mshitakiwa huyo kwamba atapata matibabu na Jeshi la Magereza kwa kuwa wanatoa huduma hiyo.

  Hakimu Hellen aliahirisha shauri hilo hadi Januari 27, mwaka huu kwa kutajwa na washitakiwa walirudishwa rumande kutokana na shitaka linalowakabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

older | 1 | .... | 1089 | 1090 | (Page 1091) | 1092 | 1093 | .... | 3278 | newer