Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1091 | 1092 | (Page 1093) | 1094 | 1095 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tija la Taifa (NIP) Novatus S. Massao (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya NIP Prof. Samwel Wangwe walipokuwa wakiangalia mazingira ya nje ya jengo la Shirika la Tija la Taifa.Januari 15, 2016.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tija la Taifa (NIP) Novatus S. Massao wakati akimonesha chumba cha ofisi ya fedha cha shirika hilo, Januari 15, 2016. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
  Na Mwandishi Maalum
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) ameuagiza uongozi wa Shirika la Tija la Taifa kuwa wabunifu katika utoaji wa elimu kwa umma ili jamii iweze kujua kazi na huduma zinazotolewa na shirika hilo.
  Mhe. Mhagama ametoa agizo hilo alipotembelea Shirika la Tija la Taifa (NIP) Januari 15,2016 kwa lengo la kujionea  kazi zinazotekelezwa pamoja na changamoto zinazolikabili shirika hilo.
  “Uongozi lazima uangalie changamoto zinazolikabili shirika hili na kuangalia namna ya kugeuza changamoto hizo kuwa fursa muhimu na kutoa elimu kwa umma wa Watanzania ili wajue umuhimu wa kutumia huduma yenu kwa lengo la kujiletea maendeleo,”alisema Mhagama

  Waziri alielekeza kuwa lazima viongozi wa NIP wawe wabunifu katika kutumia vyombo mbalimbali vya habari vinavyoweza kuwafikia wananchi wa aina zote huku akisisitiza kuangalia vipindi ambavyo havihitaji kulipiwa.

  "Nendeni mkaongee na wadau wa vyombo vya habari maana utakuta kuna fursa nyingi mngeweza kuzitumia bila gharama yoyote. kuna vipindi kama vile Kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC 1, kipindi cha Kumekucha cha ITV, kipindi cha 360 Clouds Tv na Tuongee asubuhi cha Star Tv na vingine vingi amabavyo mnaweza kuvitumia kuwafikia wananchi wengi," alisisitiza Mhe. Mhagama.
  Waziri alisema kuwa kwa kutumia ubunifu na  fursa zilizoko kwenye vyombo vya habari shirika litapata kujitangaza bila kutumia gharama na kuweza kuyafikia malengo kama kuboresha ujuzi na uelewa wa usimamizi wa  rasilimaliwatu, kuchapisha na kusambaza fasihi na kuboresha utendaji wa Taasisi za umma na zisizokuwa za umma.
  Wakati akimkaribisha waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa NIP  Bw.Novatus Massao alieleza kuwa miongoni mwa changamoto zinazokabili shirika hilo  ni suala la taswira hasi kwa jamii na uelewa mdogo wa jamii kuhusu faida  na umuhimu wa Shirika hilo.
  Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya NIP, Prof.Samwel Wangwe aliahidi kuwa shirika hilo litahakikisha linatekeleza maagizo yote ya Mhe. Mhagama ili kuwezesha watanzania kuelewa na kutumia huduma za shirika hilo.
  Aidha, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Bw.Raphael Loishiye alimshukuru Mhe. Waziri kwa kufanya ziara katika Shirika hilo na kujionea mazingira na changamoto wanazokabiliana katika utekelezaji wa majukumu yao.

  0 0

  Katibu Mkuu Msaidizi  Mwandamizi anayehusika na  Misaada ya  Kibinadamu na   Mratibu wa Misaada ya  dharua ambaye  hivi karibuni amehadharisha kwamba Tanzania ni kati ya nchi ambazo  zinauwezekano mkubwa kwa  kukumbwa na  mafuriko yatakayotokana na El-Nino
  Na Mwandishi Maalum, New   York

   Umoja wa Mataifa umetahadharisha kwamba Tanzania  ni kati ya nchi kadhaa ambazo zinauwezekano mkubwa wa kukumbwa na mafuriko  yatakayosababishwa na  El- Nino.
  Kwa mujibu wa  Taarifa ya  Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi  anayehusika na  Misaada ya  Ki-binadamu na  Uratibu wa Misaada ya Dharura, Bw Stephen O’Brien,  kipindi  ambacho  Tanzania inaweza kukabiliwa na mafuriko ya  El-Nino ni kati ya  mwezi Januari na Machi mwaka huu wa 2016.

  Nchi nyingine ambazo zinauwezekano wa kukumbwa na mafuriko makubwa pamoja na  Tanzania ni  Madagascar,   Malawi na  Msumbiji.

  Taarifa ya  Bw. O’Brien   kuhusu  madhara ya  El-Nino na namna  gani Jumuiya ya Kimataifa  inatakiwa kujiandaa au inajiandaa na kadhia  hiyo    iliyowasilishwa   mbele ya  wajumbe wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na  nakala yake kutumwa  kwa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  pamoja na  kutoa tahadhri hiyo, amewasihi nchi  ambazo  zinatarajiwa kukubwa na maafa ya  El -Nino kujiandaa   ipasavyo.

  Maandalizi hayo ni pamoja    utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa  wananchi watarajiwa wa    athari za El- Nino .

  Kwa mujibu  wa  Katibu Mkuu  Msaidizi Mwandamizi, kwa   upande wa  Afrika ya Mashariki,   nchi  kadhaa  hususan ukanda kwa magharibi zimekubwa na uhaba mkubwa wa mvua na hivyo  kuathiri kiwango cha upatikanaji wa  chakula.  
  Nchi hizo ni  Ethiopia  Sudan, Djibouti na  Eritrea, ili hali baadhi ya nchi zikipata kiwango cha mvua kilichovuka  mipaka.

  “  Kuanzia mwezi Januari hadi Machi, nchi za Tanzania,  Msumbiji, Madagascar na  Malawi  zinauwezekano mkubwa kwa kukubwa na  mafuriko  ya El- Nino” . anatahadharisha O’Brien

  Kwa mujibu wa  Bw. Stephen O’Brien hichi hizo zitahitaji  pamoja na mambo mengine misaada  ya  kujiandaa na kushughulikia ya kile kinachotabiliwa  kwamba kinauwezekano mkubwa wa  kutokea.

  Ukiacha nchi za Afrika ya Mashariki, nchi nyingine kwa upande wa Afrika ambazo zinakumbwa na hali tete ya uhaba wa mvua na hivyo kutishia usalama na  upatikanaji wa chakula ni  Angola,   Botswana, Malawi, Namibia, Afrika ya Kusini, Swaziland, Zambia na   Zimbabwe.

  Nchi hizi zimekubwa na uhaba mkubwa wa mvua kiasi kwamba na kwa mujibu mwa  Bw. Stephen O’Brien zitakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula ambapo  watu zaidi ya milioni 28 katika mataifa hivyo watakabiliwa na  uhaba wa chakula

  Akizungumzia kuhusu misaada ambayo imekwisha kutolewa na   nchi wahisani katika kukabiliana na  ukame na madhara yatokanayo na El-Nino  ,  Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi anasema kuwa hadi  wakati anatoa taarifa yake  kiasi  cha dola 360 milioni kilikuwa kimetolewa na wafadhili kwa lengo la kukabiliana na  madhara yatakayotokana na El-Nino ukiwamo usalama wa chakula.

  Pamoja na  michango hiyo,   Bw. O’Brien anasema   haitoshi kutokana na  ukweli kwamba  maafa yatakayotokana na   madhira ya El-Nino yanahitaji misaada zaidi

  Mbali ya   nchi za  kanda ya  Afrika  baadhi ya  nchi ulimwenguni ambazo  zinatakumbwa na ama zimeshakubwa na  balaa la El-Nino ni pamoja na  Nchi ambao  zimo katika  Bara la Latini ya  Amerika,  na nchi  za      eneo la Pacific ambazo  nyingi ni visiwa.


   Shirika  la  Kimataifa la  Hali ya    Hewa ( World Meteorogical Organization) litanatarajiwa katika  mwezi    February kutoa taarifa zaidi kuhusu mwelekeo wa El-Nino


  0 0

   JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,

  JINSIA, WAZEE NA WATOTO


  Ndugu Wananchi,

  Katika nchi yoyote ile uhuru usio na mipaka ni jambo la hatari; lakini pia hakuna haki isiyo na wajibu. Vivyo hivyo, katika huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala hapa nchini kuna Sheria, Kanuni na Taratibu za Maadili zinazoweka masharti, uhuru na mipaka; pia haki na wajibu wa kila mdau. 
  Huduma za tiba asili na tiba mbadala ni huduma zinazotambulika na Jamhuri yetu, watu wake na ina thamani kubwa. Aidha, ni huduma inayotambuliwa na sayansi ya tiba ya kisasa. 
  Hata hivyo huduma hizo zimekumbwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa watoa huduma wasiozingatia Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali. 
  Kutokana na hali hiyo na kutokana na ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (Mb) kwa Tabibu Juma Mwaka Juma tarehe 14/12/2015 na kufuatia uchambuzi uliofanywa na Wizara baada ya ziara hii, Wizara imebaini changamoto zifuatazo:-

  0 0

  Mwanamuziki Mahiri wa Nyimbo za Injili Nchini Ndugu Bahati Bukuku katika  akiwa mwenye Uso wa Simanzi na Majonzi katika Msiba wa Mama yake Marehemu, Enea Bukuku aliefariki Tar:12,01,2016 na Mazishi kufanyika Leo Tar:15,01,2016 katika Makaburi ya Mlima James huko Jijini Mbeya.


   Mwili wa Marehemu Enea Bukuku ukiingizwa ndani ya Kaburi   Baadhi ya Ndugu, Jamaa, marafiki n majirani waliohudhuria mazishi ya Marehemu Enea Bukuku Mama Mzazi wa Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Ndugu, Bahati Bukuku.

   Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili maarufu kwa Jina la Bonny Mwaitege akizungumza jambo kwa niaba ya Wanamuziki wote wa Nyimbo za Injili katika kumfariji mwanamuziki mwenzao Bahati Bukuku katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mama yake  Mzazi.      PICHA ZOTE NA MR.PENGO - MBEYA.


  0 0


  0 0

  Leticia Nyerere enzi ya uhai wake

  Familia ya Nyerere inependa kuwataarifu, kuwakaribisha na hatimae kujumuika nao katika misa ya kumbukumbu ya mpendwa mama yao Leticia Nyerere itakayofanyika leo Jumamosi Januari 16, 2016 saa 6 kamili mchana (12 pm sharp) katika kanisa la Mtakatifu Edward lililopo Baltimore, Maryland kwenye anuani ifuatayo hapo chini.
   901 Poplar Grove Street,
  Baltimore, MD 21216

  Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzio.

   Kwa maelezo na maelekezo zaidi tafadhali wasiliana na 
  Margareth Mageni 240 462 9138
  Emmanuel Muganda 240 447 2801
  Ramadhani Kamguna 202 459 3839

  Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe.

  Mheshimiwa Wilson Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani akiweka sign kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Laticia Nyerere Lanham. MD. U.S.A


  Kada wa CCM Washington, DC Salma akiweka sign kwenye kitabu cha maombolezo.


  Kushoto ni mume wa Marehemu Laticia Nyerere Bwana Madaraka Nyerere akiwa nyumbani hapo.
  Mtoto wa Marehemu Laticia Nyerere anaitwa,  Julia Nyerere.


  Na huyu ni Helena Nyerere mtoto wa marehemu pia.


  Colonel Adolph Mutta Defense Attaché, alikuwepo pia nyumbani kwa marehemu kutoa pole.

  Mr Suleiman Saleh Minister Plenipotentiary, Political Affairs alikuwepo pia.   Marafiki wa familia ya marehemu wakiwa nyumbani kutoa pole.
  Dr Temba, Temba Engineering Services kutoka Brooklyn New York katikati akiwa nyumbani kwa wafiwa.

  0 0
 • 01/15/16--19:00: NGOMA AZIPENDAZO ANKAL

 • Mr. Nice Kikulacho

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa ziara maalumu ya kutembelea Kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete Sports Park na kushiriki siku ya Albino Tanzania iliyoratibiwa na Kituo hicho kwa ushirikiana na Chama cha Albino Tanzania.Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Power Bw. Paul Hinks, Mkufunzi wa Michezo katika Kituo hicho Bw. Ray Power na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Alibino Tanzania Bw. Josephat Tomer.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa tatu kutoka kushoto) akimsikiliza kwa makini Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Alibino Tanzania Bw. Josephat Tomer wakati wa ziara maalumu ya kutembelea Kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete Sports Park na kushiriki siku ya Albino Tanzania iliyoratibiwa na Kituo hicho kwa ushirikiana na Chama cha Albino Tanzania.Kutoka kushoto ni Mkuu wa Utawala na Uendeshaji wa Kituo hicho Bw. Richard Mtui, Afisa Mtendaji Mkuu wa Syjmbion Power Bw. Paul Hinks na Mkufunzi wa Michezo katika Kituo hicho Bw. Ray Power.


  0 0


  0 0
  0 0


  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Babati Crispine Meela

  Na Woinde Shizza,Babati

  Maofisa ugani na makampuni ya usambazaji wa pembejeo Wilayani Babati mkoani Manyara, wametakiwa kuwaelimisha wakulima aina ya mbegu na mbolea bora zinazofaa kulingana na udongo wa eneo husika na kuachana na kilimo cha mazoea.

  Mkuu wa wilaya ya Babati Crispine Meela aliyasema hayo katika kikao cha kamati ya pembejeo kilichokuwa kikijadili utekelezaji wa mpango wa usambazaji wa pembejeo kwa mwaka 2015/2016 na changamoto za utekelezaji huo.

  Alisema kumekuwepo na dhana potofu kwa baadhi ya wakulima ya matumizi ya mbolea katika ardhi kuwa yanaharibu udongo na mbegu mpya zisizozoeleka kwa wakulima hazifai kutumika hivyo wataalamu wakitoa shamba darasa watawaelimisha wakulima ipasavyo.

  “Suala la pembejeo ni suala nyeti kwani ni mpango wa serikali wa usambazaji wa ruzuku za vocha za pembejeo kwa wakulima na pia kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa letu hivyo tunapaswa kuwa makini katika hilo,” alisema Meela.

  Alisema wilaya hiyo imepokea vocha za sh1 milioni 1 ambapo makampuni ya usambazaji wa pembejeo hizo kwa kupitia mawakala wao watawasambazia wakulima wa maeneo husika na kuwawezesha kupata aina zote tatu za mbegu, mbolea ya kupandia na kukuzia kwa wakati mmoja.

  Alikemea baadhi ya makampuni kupitia mawakala wa usambazaji wasio waaaminifu wanaoendelea kutoa aina moja ya mbegu na makampuni hayo yazingatie sheria na kanuni za mkataba waliowekeana na halmashauri, kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

  Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati Hassan Lugendo alitaka zoezi la usambazaji wa pembejeo kuharakishwa kuwafikia wakulima kwa wakati ili kuepuka malalamiko ya ucheleweshaji wa ruzuku za vocha hizo.

  Ofisa kilimo, umwagiliaji na ushirika wa mji wa Babati, Daniel Luther alisema kati ya aina ya vocha 3,000 zilizotolewa ni vocha 821 pekee zimekwishapatiwa wakulima kutokana na changamoto za wakulima kupendelea kuchukua mbegu bila mbolea.

  Luther alitaja sababu nyingine zilizosababisha kutochukuliwa vocha nyingi ni kuchelewa kuanza kwa msimu wa kilimo katika maeneo mengi na uelewa mdogo wa wakulima katika kutumia aina mpya ya mbegu na mbolea.

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangalla (kulia)akitembelea jana Makazi ya Wazee walioathirika na ugonjwa wa ukoma yaliyopo kijiji cha Nunge eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.mwenye shati la batiki Mkuu wa Makazi hayo Moses Gunza.
  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangalla akimsikiliza mmoja wa wazee aliyejulikana kwa jina la Salum Ubwabwa wakati alipotembelea jana Makazi ya Wazee walioathirika na ugonjwa wa ukoma yaliyopo kijiji cha Nunge eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.Mzee huyo ambaye alimpatia historia ya eneo hilo, ambalo sasa limevamiwa na baadhi ya watu.
  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangalla akiangalia mazingira ya makazi hayo.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  MWENYEKITI wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akiwa na Mjumbe Maalum wa Marekani katika Ukanda wa Maziwa Makuu, Thomas Perriello, baada ya mazungumzo yao kuhusu hali ya Burundi, yaliyofanyika jana, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0

  Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga akitazama migomba iliyoharibiwa na upepo mkali uliotokea jana jioni katika kata ya mto wa mbu.habari picha na Woinde Shizza, Monduli.

  Wananchi wa Kata ya Mto wa Mbu iliyoko wilaya ya Monduli wako hatarini kukumbwa na baa la njaa kutokana na upepo mkali uliotokea jana majira ya saa kumi na moja jioni na kuangusha migomba ya ndizi ambayo hutegemewa kama chakula kikuu na zao la biashara. 

   Wakulima hao walisema kuwa upepo huo mkali umeathiri mashamba makubwa ya migomba hivyo wameiomba serikali ichukue hatua za haraka kunusuru hali ngumu ya upatikanaji wa chakula itakayojitokeza siku zijazo. 

   Leyan Ngaboli na Moses Lengine ni wakulima wa ndizi wamesema kuwa upepo huo utasababisha kusimama kwa biashara ya ndizi kwa kiasi kikubwa kwani tayari wakulima wameanza kupata hasara kwa kulazimika kuuza ndizi kwa bei ya chini ili zisiharibikie mashambani. 

   Afisa Mtendaji wa Kata ya Mto wa Mbu Kusumu Hassan alisema kuwa karibu kaya na hekari zimeathiriwa na upepo huo hivyo ameiomba serikali isaidie wakulima hao waweze kurejea katika kilimo hicho ambacho huzalisha ajira nyingi. 

   Kwa upande wake Mbunge wa Monduli Julius Kalanga aliyefanya ziara ya kuwatembelea waathirika wa upepo huo amewataka wananchi kuchukua tahadhari huku akiahidi kushirikiana na serikali kutafuta chakula cha msaada kutoka serikalini ili kuwasaidia wakulima hao kwa kipindi ambacho wanaanza upya kulima mashamba yao kwani zao hilo huchukua muda mrefu. 

   "Nitazungumza na Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa mkoa tuangalie uwezekano wa kupata chakula cha msaada ili kunusuru kaya zilizoathirika" Alisema Kalanga 

   Kata ya Mto wa Mbu hutegemea kilimo cha matunda matunda kama zao la biashara na chakula ambapo matunda mengi kutoka kata hiyo hupelekwa katika masoko ya ndani nan je ya mkoa wa Arusha.

  0 0

  Na Lydia Churi-NEC

  Tume ya Taifa ya uchaguzi imeamua kuwa  viti vitatu(3) vya wabunge wanawake wa Viti Maalum vilivyobaki uteuzi wake utafanyika mara baada ya kukamilika kwa uchaguzi katika jimbo la Kijitoupele Zanzibar.

  Kikao cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kilichokutana Januari 14 na 15, 2016 kimefikia uamuzi huo kwa sababu ya kuahirishwa uchaguzi katika jimbo hilo. 

  Kwa mujibu wa mgawanyo wa viti Maalum uliofanywa na Tume, kuna jumla ya viti maalum 113 ambavyo ni asilimia 40 ya wabunge wote 281 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo CCM ilipata viti 64, Chadema viti 36 na CUF viti 10.

  Katika Mgawanyo huo, vimebaki viti vitatu kukamilisha idadi ya viti 113 ambavyo havikugawanywa kutokana na kutokukamilika kwa Uchaguzi katika majimbo nane ya Ulanga Mashariki, Arusha Mjini, Handeni Mjini, Ludewa, masasi Mjini, Lushoto,  Lulindi na Kijitoupele.

  Tayari chaguzi zimeshafanyika katika majimbo hayo saba na jimbo la Kijitoupele kubaki hali iliyosababisha kikao cha Tume kuamua kuwa uteuzi wa viti hivyo vitatu ufanyike mara baada ya kukamilika kwa uchaguzi katika jimbo la Kijitoupele.

  Kwa mujibu wa Ibara ya 78 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ili chama cha siasa kilichoshiriki katika Uchaguzi Mkuu kiweze kupata Viti Maalum ni lazima kiwe kimepata angalau asilimia tano (5) ya kura zote halali za Wabunge.

  Aidha, ili kuweza kukamilisha zoezi hili ni wazi kuwa, Uchaguzi ni lazima ukamilike katika majimbo yote. Kwa kuwa uchaguzi haujafanyika katika jimbo la Kijitoupele, Tume haitoweza kugawa viti vilivyobaki. Hii ni kutokana na ukweli kwamba endapo uteuzi utafanyika, kura za Kijitoupele hazitatumikja katika kupata viti Maalum vilivyobaki jambo ambalo litakuwa ni kinyume na matakwa ya Katiba.

  Kwa mantiki hiyo viti hivyo vitatu (3) vitagawanywa mara baada ya uchaguzi kufanyika katika jimbo la Kijitoupele.
       
  Wakati huo huo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inakusudia kutoa mashine za kuandikishia wapiga kura (BVR) 5000 kwa  Taasisi ya NIDA na 1000 kwa Taasisi ya RITA ili ziweze kufanya kazi za uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa na usajili wa vizazi na vifo.

  Katika kipindi cha uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mfumo wa ‘Biometric Voters Registration’ (BVR) Tume ilitumia mashine 8000 kukamilisha zoezi hilo kwa kipindi cha miezi miwili.

  0 0

  Ikiwa siku chache tu zimepita baada ya shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco) kubaini wizi mkubwa wa Maji kutumika katika shamba la mboga mboga na matunda katika chuo cha Islamic kilichopo Boko ununio jijini Dar es salaam. Dawasco imebaini wizi mwingine wa Maji katika kiwanda cha kutengeneza Maji ya betri cha Bahari Chemicals Ltd kilichopo kurasini wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam.

  Akizungumzia tukio hilo meneja wa Dawasco Temeke, Bw. Deogratius Rwegasira, amethibitisha kutokea kwa wizi huo ambapo kiwanda hicho kilikuwa kimejiunganishia Maji bila kibali cha Dawasco na kwamba hawakuwa na mita wala akaunti namba inayoonyesha kiasi cha Maji kinachopita katika system ya Maji iliyopo, na baada ya kufanya mawasiliano na Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw.Devendra Singh Parmar amekiri kutumia Maji hayo kinyume na taratibu .
  “Baada ya kufanya uchunguzi tumebaini kuwa kiwanda hiki kimekuwa kikituibia Maji yetu kwa muda mrefu, mmiliki wa kiwanda amekubali kosa,lakini akisema kwamba wenyewe ni wageni hapa hawana zaidi ya mwaka mmoja tangu waanze kazi.hivyo hawakujua taratibu za kufuata”. Alisema Bw. Rwegasira.

  Aidha meneja wa kiwanda hicho, Bw. Abdul Gulam, amekiri kuihujumu Dawasco kwa kuiibia Maji, lakini amesema kuwa wao ni wapangaji tu wamepanga katika eneo hilo na wana muda wa miezi saba tangu wahamie kiwandani hapo, walikuta wizi huo wa Maji ukifanyika katika kiwanda hicho   na hawakujua taratibu husika za kufuata ili wapate huduma ya Maji kihalali.
  “Sisi tumekubali kuwa tulikuwa tunatumia Maji ya DAWASCO bila kuyalipia, lakini sio sisi ambao tuliounganisha bomba hili, wapangaji waliopita walijiunganishia Maji haya hivyo tunaomba tulimalize hili, ili tuanze kuwa wateja wenu rasmi” alisema Bw.Gulam.

  Aidha bwn Gulam ameainisha kuwa wao kama wamiliki wa kiwanda wamekubali kulipa faini iliyotolewa na DAWASCO ya Shiling million 3.5 ili warudishiwe huduma kama wateja wengine na waweze kuendelea na biashara.
   Vitendo vya uhujumu wa Miundombinu ya Maji hususani wizi wa Maji unaendelea kuwa changamoto kwa DAWASCO licha ya kampeni na elimu inayotolewa kila siku juu ya uhalali na utaratibu wa kuungiwa huduma ya Maji inayotolewa na DAWASCO.

  0 0
 • 01/16/16--04:50: DIWANI AFARIKI DUNIA MUFINDI
 • Diwani wa kata ya Igombavanu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa Mh. HABIBU KILONGE amefariki Dunia katika hospitali ya wilaya ya Mufindi usiku wa kuamkia leo ilikokuwa amelazwa kwa matibabu.

  Taarifa ya mwenyekiti wa Halmsahauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. FESTO MGINA kupitia kitengo cha habari na mawasiliano cha Halmashauri ya Wilaya, ameeleza kuwa, marehemu amefarikia baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa takribani mwezi mmoja na mara kadhaa alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Wilaya na kurejea nyumbani.

  Aidha, amebainisha ratiba ya shughuli za maziko kuwa marehemu atazikwa Jumapili ya Tarehe 17 ambapo mapema asubuhi ya saa mbili mwili wa marehemu utaondolewa katika Hospitali ya Wilaya Mafinga na kupekwa katika kata ya Igombavanu ambakoa utaagwa na wapiga kura wake na itakapofika saa tano asubuhi mwili huo utasafirishwa kwenda Kijiji cha kichiwa Mtwango Mkoani Njombe ambako ndiko mwili huo utazikwa.


  Marehemu Diwani HABIBU KILONGE alichaguliwa kwa mara ya kwanza na wananchi wa Kata ya Igombavanu kupiti atiketi ya chama cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi Mkuu uliyofanyika mapema mwezi wa 10 mwaka jana kwa jumla ya kura Elfu 2 na 34 ikiwa ni ushindi mkubwa dhidi ya mpinzani wake wa karibu kutoka chama cha Chadema aliyepata kura 361 na mpaka mauti inakuta diwani huyo alikuwa amehudhuria kikao kimoja pekee, ambacho kilikuwa maalu kwa kuapishwa.

  0 0

  Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko akizungumza na madiwa wa Manispaa ya Ilala leo mara bada ya kushinda  kwa Kura 31 katika uchaguzi wa meya wa manispaa hiyo katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Salum Kumbilamoto  akiwashukuru madiwani waliompigia kura leo mara ya kuibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.

  Matokeo ya Meya na Naibu Meya yakujumlishwa na baadhi ya wajumbe wa Meya,naibu Maya  wakiwa na Mwanasheria wao leo mara baada ya kumaliza kugika kura katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
  Wananchi wakishangilia ushindi wa Maya na Naibu Meya mara baada ya kutangazwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

  ____________________

  Kamati ya Kanuni ya Bunge iliyoundwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai hivi karibuni, leo imekutana Jijini Dar es Salaam na Kuridhia mapendekezo ya mabadiliko katika muundo wa kamati za Bunge yaliyowasilishwa na Mhe. Spika ili kuendana na mabadiliko ya Muundo wa Wizara katika Serikali ya awamu ya Tano.


  Mabadiliko hayo ambayo yamefanywa chini ya kanuni ya 155 (3) ya kanuni za Kudumu za Bunge yamezingatia madaraka aliyonayo Spika kufanya marekebisho kwenye nyongeza za kanuni kwa kushauriana na kamati hiyo.

  Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo Mh. Ndugai ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo amesema amelazimika kufanya mabadiliko katika muundo wa kamati ili kuendana na mabadiliko ya Wizara na kwa kuzingatia kuwa muundo wa kamati umetajwa kwenye nyongeza ya nane.

  Katika muundo huo Kamati mbili mpya zimeundwa ambazo ni kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo na kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.

  Akifafanua kuhusu maamuzi ya Kikao hicho, katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah amesema kikao hicho kimekuwa na mafanikio makubwa na kuridhia mapendekezo ya Mhe. Spika kama yalivyowasilishwa.

  Aidha Dkt. Kashililah aliongeza na kusema kuwa Kamati nyingine zimefanyiwa mabadiliko kwenye majina na nyingine mbili kuunganishwa na kufanya kamati mpya za Bunge kuwa kama ifuatavyo: 

older | 1 | .... | 1091 | 1092 | (Page 1093) | 1094 | 1095 | .... | 3285 | newer