Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

SERIKALI yakusudia kuanza kuzalisha drip za maji za IV katika hospitali zake zote kubwa nchini

$
0
0
SERIKALI inakusudia kuanza kuzalisha drip za maji za IV (Intravenous Fluids) katika hospitali zake zote kubwa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipotembelea mtambo wa kutengenezea drip hizo za majimaji katika hospitali ya Mtakatifu Joseph ya Peramiho, Mkoani Ruvuma.

Amesema haoni kwa nini hospitali hizo ziendelee kuagiza wakati uwezo na watalamu wa kufanya hivyo upo hapa hapa nchini.

Drip hizo zina manufaa makubwa kwa wagonjwa ikiwemo kuongeza maji kwa wagonjwa waliopungukiwa na maji mwilini na vilevile inatumika kwa ajili ya kutolea baadhi ya dawa ambapo huchanganywa.

Vilevile hutumika wakati wa huduma za upasuaji.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiongea na Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Peramiho, Dr. Venance Mushi alipotembelea hospitali hiyo leo asubuhi
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisalimiana na Padre Lucius wa Hospitali ya Peramiho, mkoani Ruvuma.
Baadhi ya wanachama wa NHIF wakiwa sehemu ya mapokezi tayari kupata huduma.

SERIKALI KUKAMILISHA UKARABATI WA KITUO CHA AFYA CHIPOLE.

$
0
0
 Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya akisisitiza umuhimu wa kuwa na Kituo cha Afya chenye vifaa tiba, tarehe 12 Januari 2016, wakati alipokuwa akikagua ukarabati wa kituo cha Afya cha Chipole wilayani songea vijijini, baada ya kituo hicho kuungua mwaka 2013 na Ofisi hiyo kukikarabati. (wa kwanza kulia) ni Makamu wa Mama Mkubwa Chipole, Sista. Sairis Mkinga.
 Daktari wa Kituo cha Afya cha Chipole, Ismail Mzimya akieleza umuhimu wa kituo hicho kwa wananchi wa Kata ya Magagura wilayani Songea vijijini wakati Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya tarehe 12 Januari 2016, alipokuwa akikagua ukarabati wa kituo hicho baada ya kituo hicho kuungua mwaka 2013 na Ofisi hiyo kukikarabati. (wa kwanza kulia) ni Makamu wa Mama Mkubwa Chipole, Sista. Sairis Mkinga.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya akiwa katika picha aya pamoja na Viongozi , watumishi na wananchi wanao hudumiwa na Kituo cha Afya Chipole wilayani songea vijijini tarehe, 12 Januari, 2016, baada ya kukagua ukarabati wa kituo hicho , kilichoungua mwaka 2013 na Ofisi hiyo kukikarabati.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na. Mwandishi Maalum. 
SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa imeahidi kukamilisha ukarabati wa Kituo cha Afya cha Chipole Songea Vijijini kilichopata majanga ya moto baada ya kituo hicho kuungua mwaka 2013 na Ofisi hiyo kutoa fedha za kukikarabati. 

Akiongea wakati wa ziara ya kukagua ukarabati wa kituo hicho, tarehe 12 Januari, 2016, Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amebainisha kuwa kufuatia kuungua kwa hospitali hiyo Ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa kiasi cha shilingi milioni 35 kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho. 

“Tumekagua ukarabati wa kituo hiki cha afya na tumeona pamoja na kuambiwa na uongozi wa hospitali hii kuwa pamoja na fedha tulizozitoa lakini bado kuna mahitaji ya msingi yanahitajika ili hospitali hii iweze kuwahudumia wanakijiji wanao izungunka hospitali hii. Tunaahidi kukamilisha ujenzi wa chumba cha kuhifadhi maiti pamoja na maabara” alisema Msuya. 

Awali akitoa maelezo ya maendeleo ya ukarabati wa kituo hicho cha afya , Makamu wa Mama Mkubwa wa Chipole, Sairis Mkinga, alifafanua kuwa pamoja na mapungufu ya chumba cha maabara lakini bado kituo hicho cha afya kinao upungufu wa vyumba vya kuhudumia wagonjwa. 

“Tunayo changamoto bado ya kuwa na sehemu maalum ya Mapokezi ya wagonjwa na wagonjwa kupokea dawa. Pia panahitajika mahali kwa akina mama wajawazito kujifungulia kwani kwa sasa vyumba hivi viko karibu sana na vyumba vya wanaume lakini tunahitaji chumba maalum kwa aijili ya kliniki ya watoto” alisisitiza Sista Mkinga. 

Kituo cha Afya cha Chipole kilichopo Kata ya Magagura wilayani Songea vijijini kinamilikiwa na Shirika la watawa wa Mtakatifu Agnesi Chipole na inahudumia takribani wakazi 7,434 wa kata hiyo, hivyo kukamilika kwa Hospitali hiyo kutawezesha kupunguza vifo vya mama na motto pamoja na uboresha hali za afya za wakazi hao.

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAPINDUZI ZANZIBAR.

KILELE CHA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Vikosi vya Ulinzi liliandaliwa rasmi katika kilele cha sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa kilele cha sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika kilele cha sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteta na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa kilele cha sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWAJULIA HALI MHE. SUMAYE NA BALOZI KIBELLOH

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Waziri Mkuu, Mstaafu Frederick Sumaye  ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu leo Januari 12, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kushoto) wakizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amnaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu  leo Januari 12, 2016. Kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Esther Sumaye na Mama Majaliwa. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Balozi Hassan Kibelloh ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika  hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa Matibabu Januari 12, 2016.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI UMMY MWALIMU AFANYA ZIARA KATIKA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO LA MKOA WA RUVUMA

$
0
0
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu (Mb.)akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Mtoto, mbele ya Ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto la Mkoa wa Ruvuma.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu (Mb.) leo ametembelea Dawati la Polisi la Jinsia na Watoto la  Mkoa wa Ruvuma, kwa lengo la kufuatilia hali ya Ulinzi na Ustawi wa Mtoto Mkoani humo.

Wakati wa ziara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu aliwapongeza Wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Mtoto Mkoani Ruvuma kwa Ushirikiano waliouonyesha hadi kufanikisha Ujenzi wa Kituo hicho. 

Alieleza kuwa kwa Mkoa wa Ruvuma Wizara yake kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo ya Mtoto, itahakikisha inashughulikia kwa haraka tatizo la Usafirishwaji wa watoto kwenda nchi za jirani kutumikishwa katika kazi mbalimbali.

Pia aliagiza Uongozi wa Mkoa kuongeza jitihada zaidi katika kukabilina na Vitendo vya Ukatili wanavyofanyiwa Wanawake, kwakuwa Mkoa huo ni miongoni mwa mikoa mitatu yenye wastani mkubwa wa vitendo vya vipigo kwa wanawake.

JK na mama Salma Kikwete wampa pole Mama Maria Nyerere kwa msiba wa marehemu Leticia Nyerere

$
0
0
 Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiongea na Mama Maria Nyerere, mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, walipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam kumpa pole kwa kufiwa na mkwewe Marehemu Leticia Nyerere leo Jumanne Januari 12, 2016

Mama Salma Kikwete akimfariji  Mama Maria Nyerere, mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, walipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam kumpa pole kwa kufiwa na mkwewe Marehemu Leticia Nyerere leo Jumanne Januari 12, 2016
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akifariji familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, walipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam kumpa pole Mama Maria Nyerere kwa kufiwa na mkwewe Marehemu Leticia Nyerere leo Jumanne Januari 12, 2016

news alert: SIMBA YAMTIMUA KOCHA WAKE DYLAN KERR

$
0
0


Kwa masikitiko makubwa klabu ya Simba inawaarifu umma kupitia vyombo vya habari.uamuzi wake wa kuvunja mikataba yake na makocha wake  - kocha mkuu Dylan Kerr kutoka uingereza na kocha wake wa makipa Iddi Salim.
Katika uamuzi wake uliofanywa mchana huu na kikao cha kamati ya utendaji, ambapo makocha hao waliitwa, klabu ya Simba na walimu hao kwa pamoja wamekubaliana kuvunja mikataba ya ajira zao kwa faida ya pande zote mbili.
Kwa sasa kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja atakuwa na timu.huku mchakato wa kumpata kocha mkuu ukiendelea.
Mwisho uongozi unawashukuru walimu hao kwa huduma waliyoitoa katika kipindi chote cha uwepo wao klabuni.

Imetolewa na Haji S.Manara
Mkuu wa mawasiliano wa klabu ya Simba.
Simba nguvu moja

Aliyekuwa msajili mkuu wa mahakama wa Kenya Gladys Shollei apandishwa kizimbani kujibu mashataka

MABASI YA DALADALA MAWILI AINA YA ISUZU JOURNEY YANAUZWA

$
0
0
MABASI HAYA YAKO KATIKA HALI NZURI SANA NA YANA FANYA KAZI. YAPO ILALA DAR-ES-SALAAM. BEI YAKE NI SHILINGI MILIONI 60 KWA YOTE MAWILI. WASILIANA NA HENRY KILAMBA 0755 723897.
Kwa ubavu
Kwa mbele
Kwa mbele 
Kwa ubavu

DIRA YA DUNIA JUMANNE 12.01.2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

CLUB YA MAZOEZI YA MANGO GARDEN YAFANIKISHA BONZANA LA MIAKA 15 TANGU KUANZISHWA

$
0
0
Wanachama wa club ya Mango Garden ya Kinondoni jijini Dar es salaam wakijumuika na wenzao wa Club ya Mazoezi ya Kisutu jijini  katika mazezi ya pamoja katika kuadhmisha miaka 15 tangu club hiyo ilipoanzishwa.Picha kwa hisani ya Mango Club
Tizi la nguvu
Hapa si Twanga Pepeta tu, uani kuna tizi la nguvu
Mambo ya Mango Garden
Kazi moja tu
Tizi na tabasamu
Mango Garden oye!

MAKALA YA SHERIA: JE UNAHITAJI “NGO”, UJUE UTARATIBU MZIMA WA KUSAJILI

$
0
0
Na  Bashir  Yakub

NGO  ni  kifupi  cha  neno  Non  Government  Organisation.  Kwa  Kiswahili  neno  hili  humaanisha  shirika  lisilo  la  kiserikali. Kawaida  serikali  huwa  ina  mashirika  yake, kwa  mfano  shirika  la  bima, shirika  la  nyumba,shirika  la umeme,mashrika ya vyakula n.k.  

Tunapozungumzia  NGO  maana  yake ni  kuwa  ni mashirika  ambayo  kwa  namna  yoyote  ile  serikali haihusiki  na  umiliki  wake. Ni  mashirika ambayo  humilikiwa  na   watu  binafsi.  Serikali huweza kushirikiana  nayo  tu lakini  si  kuyamiliki. 

Taratibu  za  uanzishaji,  usajili  na uendeshaji  huratibiwa bayana  na  Sheria  ya  mashirika  yasiyo  ya  kiserikali Na 24, 2002.

1.YAPI  YAWE  MALENGO  YA  KUANZISHA  NGO.
Malengo  makuu  ya  kuanzisha  NGO  yawe  ni  kusaidia  makundi  au  kundi  maalum  katika  jamii.  NGO  sio  shirika  la  biashara.  Sio  kampuni  ambayo  muanzishaji  wake hutaraji  kutengeneza  faida. NGO  ni  shirika  la  hisani.  Ni  shirika  la  kujitolea  kusaidia  makundi  jamii.  Usitegemee  kuanzisha  NGO  kwa  ajili  ya  kutengeneza  faida  ya  fedha. 

2.   MGAWANYO  WA  USAJILI  WA  NGO.
Usajili  wa  NGO  umegawanyika  katika  makundi  makuu  manne. Kwa  mujibu  wa  sheria  mgawanyo  huu  umelenga  maeneo  ya  kijiografia. Hata  hivyo  ada  za  usajili  na  mambo  mengine  muhimu  katika  usajili   hutegemea  mgawanyo  huu.  

Kwanza  kuna  mgawanyo  wa usajili  wa  ngazi  ya  wilaya. Usajili  wa  aina  hii  huiwezesha  NGO  kufanya  shughuli  zake  ndani  ya  mipaka  ya  wilaya.  Husajiliwa  hapohapo  wilayani  na  hufanya  kazi  zake  ndani  ya  mipaka  hiyo. 

Pili usajili  ngazi  ya  mkoa. Huu huhusisha  usajili ngazi  ya   mkoa na  mipaka ya  kazi  itakuwa  ni  ndani  ya  mkoa  husika. 

Tatu  usajili  ngazi ya  taifa  ambao  hufanyika  makao makuu  na  mipaka  ya  kazi  ni  taifa  zima. Nne ni   usajili  ngazi  ya  kimataifa  ambao  huiwezesha  NGO kufanya  kazi  zake katika  taifa  zaidi  ya  moja.

3.  WAPI  UKASAJILI  NGO.
Kwa  ngazi  ya  wilaya  nenda  makao  makuu  ya  wilaya  yako,  na  ulizia  afisa  maendeleo  ya  jamii.  Hawa  ndio  huhusika  na  usajili. Halikadhalika  ngazi  ya  mkoa utaenda  makao  makuu  ya  mkoa  wako   ndipo  usajili  utakapofanyika. 

Aidha  kwa  ngazi  ya  taifa  usajili  hufanyika  makao  makuu  ya  wizara  kwa  msajili  wa  NGO. Kwa  sasa  wizara  husika  ni  Wizara  ya  Maendeleo  ya  Jamii,Jinsia  na  Watoto. Wasajili  wa  ngazi  zote  hupata  mamlaka  ya  kusajili kutoka  kifungu  cha  22(1) cha  sheria  ya  mashirika  yasiyo  ya  kiserikali.

4.  VITU  GANI  VINATAKIWA  KATIKA  USAJILI.
( a ) Katiba  ya NGO.  Hizi  hutakiwa  nakala  tatu  zilizojaladiwa( binding).
( b ) Maelezo  binafsi  ya  viongozi  watatu wa  NGO. Mwenyekiti, Katibu, na  mhazini.  Maelezo  binafsi  ni  wasifu( CV) pamoja  na  picha  mbili  za  kila  mmoja.
( c ) Mukhtasari  wa  kikao  cha  kuanzishwa  kwa  NGO  ukienda  sambamba  na  majina na  sahihi  za  waanzilishi.

( d )Fomu  ya  maombi  ya  usajili  iliyojazwa ( NGO FORM NO 1). Hii  hupatikana  kwa  msajili. Itatakiwa  kubandikwa  ushuru  wa  stempu wa  Tshs 1500/=.
( e ) Barua  ya  utambulisho  kutoka kwa  afisa  maendeleo  ya  jamii  wa wilaya, mkoa  husika.
( f  )  Taarifa  nyingine  yoyote  ambayo  msajili  anaweza  kuomba kutoka  kwako.

5.  ADA  ZA  USAJILI  NI  KIASI  GANI.
Ngazi  ya  wilaya 80,000/=,  ngazi  ya  mkoa 100,00/=, ngazi  ya  taifa 115,000/=  na  kimataifa  dola  za  kimarekani 350.

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL


Diamond Platnumz - Utanipenda Behind The Scenes Episode 1&2

RADIO AFM YA MKOANI DODOMA SASA KUSIKIKA MTANDAONI

WAMILIKI WA TAASISI ZA FEDHA WATAHADHARISHWA.

$
0
0
Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
WAMILIKI wa Taasisi za Kifedha wanatakiwa kujiridhisha kama waajiliwa katika taasisi hizo kama wanahusika kwa njia moja ama nyingine katika uharifu unaohatarisha maisha ya wakazi wa jijini la Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na  Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam leo.

Kamanda Sirro amesema kuwa hatua za makusudi zimechukuliwa katika maeneo mbalimbali hasa ya eneo la Kibiashara la Mlimani City kutokana na matukio mengi ya uporaji  wa fedha kwa kutumia pikipiki.

Pia amesema kuwa pamoja na sheria hizo kuchukuliwa watafanya operasheni maalumu katika eneo hilo na kutafuta namna nzuri ya kuondoa pikipiki katika maeneo hayo.

Katika Operasheni zilizofanywa na Jeshi hilo wamefanikiwa kuwakamata majambazi nane pamoja na kumamata Bunduki mbili aina ya Pump Action ambazo namba zake zilifutwa na kukatwa Mtutu.

Aidha Kamanda Sirro amesema kuwa katika Operasheni hiyo wamemkamata jambazi aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu anayejulikana kama Mkama Hassan mkazi wa Gomgolamboto jijini Dar es Salaam na alipopekuliwa alikutwa na Bastola aina ya Chinese iliyofutwa namba ikiwa na magazine yenye risasi saba. 

Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Operasheni kali inayoendelea jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionyesha Siraha zilizokamatwa katika Oparasheni ya kutokomeza uharifu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro leo wakati akizungumuza nao
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

TTCL YAKOPA DOLA MILIONI 22 KUSAMBAZA MTANDAO 3G NA 4G LTE.

$
0
0
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Uwekezaji (TIB), Jaffer Machano mara baada ya kutiliana saini. TTCL na TIB zimesaini mkataba wa makubaliano ya dhamana ya Benki na Mkopo wa Dola za Marekani milioni 22 ikiwa ni awamu ya kwanza ya mkopo wa Dola za Marekani milioni 329 zitakazotolewa kwa kampuni ya TTCL. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Uwekezaji (TIB), Jaffer Machano mara baada ya kutiliana saini. TTCL na TIB zimesaini mkataba wa makubaliano ya dhamana ya Benki na Mkopo wa Dola za Marekani milioni 22 ikiwa ni awamu ya kwanza ya mkopo wa Dola za Marekani milioni 329 zitakazotolewa kwa kampuni ya TTCL. Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

KAMPUNI ya Simu Tanzania TTCL na Benki ya TIB leo zimetiliana saini Mkataba wa makubaliano ya dhamana ya Benki na Mkopo wa Dola za Marekani Milioni 22 ikiwa ni awamu ya kwanza ya mkopo wa Dola za Marekani milioni 329 itakazopewa TTCL. 

Akizungumza katika hafla ya kusaini hati ya makubaliano ya mkopo huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura alisema mkopo huo ni mahususi kwa ajili ya kuiwezesha TTCL kusimika mitambo mipya na ya kisasa kuboresha huduma zake kwa kujenga na kusambaza huduma za Mitandao ya 3G na 4G LTE nchini kote.

Dk. Kazaura alisema hatua hiyo ni habari njema kwa Watanzania, hasa wateja na wadau wa huduma za kampuni ya TTCL. “…TTCL inaishukuru sana Benki ya TIB kwa kutuamini na kukubali kushirikiana nasi baada ya kujiridhisha kuwa tunao uwezo na nia thabiti ya kufanya mageuzi makubwa ya kibiashara ili kuboresha huduma zetu,” alisema Dk. Kazaura akizungumza.

“Kupatikana kwa mkopo na dhamana hizi kutapunguza tatizo la ukosefu wa fedha lililokuwa linatukabili na sasa tutaweza kutekeleza kwa kasi mpango wetu wa mageuzi ya Ki biashara ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu, kuleta mitambo na vifaa vya kisasa vitakavyoongeza ufanisi katika huduma zinazotolewa na TTCL kwa Wateja wa ndani na nje ya nchi. Natoa wito kwa Watanzania na Wateja wetu wote kwa ujumla waendelee kutegemea huduma na bidhaa zenye viwango vya juu kabisa vya ubora, uhakika na gharama nafuu kutoka TTCL.” Amesema Dk. Kazaura. 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Jaffer Machano amesema katika kutimiza wajibu wa TIB kama benki ya maendeleo, ujenzi wa miundombinu umepewa kipaumbele na hii ni pamoja na miundombinu ya sekta ya Mawasiliano.

“Kama alivyosema Dk. Kazaura, lengo la mpango mzima ni kuwapatia Dola milioni 329 na TIB ipo tayari kuhakikisha mradi huu unafanikiwa kwa kushirikisha kampuni zote za TIB group. Mfano mzuri ni mradi huu wa kwanza ambao umefanywa na kampuni tanzu ya TIB group- TIB Corporate Bank, amesema Jaffer Machano.”

Baadhi ya huduma za TTCL zitakazoimarika baada ya uwezeshaji huu ni pamoja huduma za simu na intaneti yenye kasi kubwa inayowezesha huduma za kijamii kufanyika kwa urahisi kwa njia ya mtandao. Huduma kama vile za Elimu kwa njia ya mtandao (E education), Afya kwa njia ya mtandao (E health) na huduma katika Sekta nyingine za kiuchumi kama vile Biashara, Viwanda na Kilimo nazo zitanufaika sana ambapo wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali watapata Mawasiliano ya uhakika katika kufanikisha shughuli zao.

Kampuni ya Simu Tanzania TTCL ipo mbioni kuanzisha huduma ya kusafirisha fedha kwa njia ya Mtandao ifikapo robo ya pili ya mwaka huu ili kutekeleza ombi la muda mrefu la Wateja wake wanaohitaji sana kuanzishwa kwa huduma hii kutokana na Mtandao mpana wa Kampuni uliosambaa ndani na nje ya nchi na unafuu wa gharama.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA DKT. KIJAJI AIAGIZA TRA MBEYA KUKUSANYA MAPATO KWA WABADILISHAJI WA FEDHA TUNDUMA

$
0
0
Naibu Waziri Fedha na Mipango Dkt, Ashatu Kijaji akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Mbeya (hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara katika Mpaka wa Tunduma na Zambia. 
Baadhi ya waandishi wa Habari Mkoani Mbeya wakiwa makini kumsikiliza Naibu waziri wa Fedha na Mipango Dkt Kishatu Kijaji katika ofisi za Mamlaka ya Mapato TRA Mkoani humo kwa lengo la kutoa tathimini yake ya ziara aliyoifanya katika Mpaka wa Tunduma na Zambia . 

Na Jamiimojablogu,Mbeya

Naibu waziri wa fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji ameitaka Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Mbeya kuhakikisha inaanda mpango maalumu kwa ajili kudhibiti mapato yanayopotea kutokana na kushamili kwa biashara ya ubadilishaji wa fedha kiholela katika mpaka wa Tunduma na Zambia.

Naibu waziri huyo ametoa kauli hiyo Mkoani Mbeya mara baada ya kutembelea Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani humo na kutoa tathimini ya ziara yake aliyoifanya katika Mpaka wa Tunduma na Zambia.

Amesema serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi hasa kutokana na kuwepo kwa biashara hiyo kiholela pasipo serikali kupata mapato yake hivyo ameitaka mamlaka hiyo kuhakikisha inaweka mpango kabambe utakao iwezesha serikali kupata mapato yake kutokana na biashara hiyo.

Amesema serikali lazima ijiendeshe yenyewe kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato sanjali na kuzuia mianya yote ya ukwepaji wa kodi pamoja na watu wote kuhakikisha wanalipa kodi.

Amebainisha kuwa nchi inategemea mapato kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kwa wananchi na hivyo kuwaongezea wananchi matumaini kwa kuwafikishia huduma muhimu.

Sehemu nyingine ambayo ameiagiza mamlaka hiyo kuishughulikia mara moja ili serikali iweze kupata mapato yake ni pamoja kuibuka kwa Saccos pamoja vikundi mbalimbali ambavyo vimekuwa vikijihusisha na ukopeshaji wa fedha kwa liba kubwa hali ambayo pia imekuwa ikiwapa mzigo mkubwa wananchi.

Katika hatua nyingine Naibu waziri huyo ameuagiza uongozi wa mamlaka ya mapato (TRA) Katika mpaka wa Tunduma na Zambia kuhakikisha kuwa mizigo yote inayosafilishwa kupitia mpaka huo inafanyiwa tathimini na kulipiwa kwa muda wa usio zidi siku moja tayari kuendelea na safari kwa inayoingia na kutoka nje ya Tanzania.

Ziara ya Naibu Waziri Dr. Kijaji ni ya kwanza Mkoani Mbeya tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 11 Desemba 2015 kushika wadhifa huo.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images