Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1088 | 1089 | (Page 1090) | 1091 | 1092 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Meno ya Tembo vipande 8 vyenye uzito wa kilo 50 ya thamani ya milioni 120 ambayo ni sawa na Tembo hai wane aliyokamatwa nayo hivi karibuni mtuhumiwa Nzuri Ndizu Mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
  Mtuhumiwa Nzuri Ndizu Mkazi wa Kijiji cha Mbende Wilaya ya Mlele akiwa katika ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi baada ya kukamatwa na meno ya Tembo vipande nane yenye thamani ya shilingi milioni 120 hapo juzi .
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa Katavi Dhahiri Kidavashari akiwa ameshika meno ya Tembo aliyokamatwa nayo mtuhumiwa Nzuri Ndizu mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ambae alikamatwa juzi akiwa na vipande 8 yenye thamani ya milioni 120 .

  Picha na Walter Mguluchuma Katavi yetu blog

  Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Nzuri Ndizu (44) Mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi amekamatwa akiwa na meno ya Tembo nane yenye uzito wa kilogramu 50 yakiwa na thamani ya shilingi milioni 120 ambapo ni sawa na Tembo wanne waliuwawa.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa mida ya saa tatu na nusu .

  Kidavashari alisema mtuhumiwa Ndizu alikamatwa kufuatia misako na uparesheni mbalimbali zinazoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi ikiwa ni kuhakikisha wahalifu wa makosa mbalimbali wakimemo wawindaji haramu wa wanyama pori wanakamatwa.Siku hiyo ya tukio jeshi la polisi lilipata taarifa toka kwa Raia wema kuwa katika pori la akiba la Lwafe kuna watu wanajihusisha na biashara haramu ya meno ya Tembo .

  Kidavashari aliendelea kuwaambia waandishi wa Habari baada ya taarifa hizo kupokelewa ufuatiliaji ulifanyika kwa polisi kufika kwenye eneo hilo na kuweka mtego .Na walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Nzuri Ndizu akiwa na meno ya Tembo vipande nane akiwa ameyaficha kwenye pori kwa ajiri ya kusubilia wateja .

  Kamanda Kidavashari alisema mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi kwa hatua za upelelezi zaidi ilikuendelea kubaini mitandao yote inayojihusisha na biashara hiyo haramu ya meno ya Tembo na kufikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika .

  Hivi karibuni watu watatu walikamatwa katika mtaa wa Aiter Mjini hapa wakiwa na vipande kumi na mbili vya meno ya Tembo yenye thamani ya shilingi milioni 120 hari hiyo inaonyesha kuwa kuna kasi kubwa ya biashara haramu ya meno ya Tembo Mkoani Katavi .Na Katavi yetu blog/Blogs za Mikoa 

  0 0
 • 01/13/16--06:39: Pato la Taifa lazidi kukua
 • Na. Frank Shija

  Pato la Taifa katika kipindi cha Robo tatu ya mwaka 2015 limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 6.3 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.4 katika kipindi cha mwaka 2014.

  Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.

  Dkt. Albina amesema kuwa kutokana na ongezeko hilo Serikali imeendelea kutoa huduma za kijamii zikiwemo umeme, afya na maji “ Pato la Taifa kwa robo tatu ya mwaka 2015 limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 6.3 ukilinganisha na asilimia 5.4 katika robo tatu ya mwaka 2014” Alisema Dkt. Albina.

  Dkt. Albina ameongeza kuwa kuongezeka kwa Pato la Taifa kumeenda sanjari na kuongezeka kwa thamani ya bidhaa na huduma nje ya nchi kwa takribani asilimia 3.3 ambapo bidhaa na huduma zilizochangia ongezeko hilo ni pamoja na dhahabu, Almasi, madini mengine na Utalii.

  Aliongeza kuwa utangazwaji wa Takwimu za Pato la Taifa unazingatia matakwa ya Sheria ya Takwimu na 9 ya mwaka 2015 inayotoa mamlaka kwa Tume ya Taifa ya Takwimu kukusanya, kuchambua na kutangaza takwimu za Pato la Taifa.

  Aidha alitaja baadhi ya shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi kubwa katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2015 kuwa ni pamoja na Ujenzi (17.6%), Uchukuzi na Uhifadhi (10.6%), Uendeshaji Serikali na Ulinzi (10.6%) na Uchimbaji Madini na Kokoto (8.0%) Dkt. Albina amesema kuwa jumla ya thamani ya Pato la Taifa kwa bei za miaka husika katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba 2015 ni takribani shilingi tilioni 71.7 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 6.9.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi za Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa takwimu za pato la Taifa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2015 (Julai – Septemba), kulia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Haji Semboja na kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Utafiti toka Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) Bw. Hussein Kamote.
  Mhadhiri mwandamizi wa uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Haji Semboja (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wakitoa takwimu za pato la Taifa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2015 (Julai – Septemba), kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi za Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
  Mkurugenzi wa Sera na Utafiti toka Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania Bw. Hussein Kamote akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya mchango wa viwanda katika kuongeza pato la taifa wakati wakitoa takwimu za pato la Taifa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2015 (Julai – Septemba), kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi za Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
  Baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati akitoa takwimu za pato la Taifa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2015 (Julai – Septemba).Picha zote na Eliphace Marwa - MAELEZO

  0 0


  Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akiwa katika moja ya karakana ya kutengeneza vifaa tiba katika mji wa Guangzhou nchini China. 
   Mheshimiwa Nassari akifanya mazungumzo na wahusika wa karakana hiyo kuona namna ya kuapata vifaa hivyo kwa ajili ya kusidia katika Hosptali ya wilaya ya Arumeru na vituo vya afya. 
  Mh Nassari akifanya mazungumzo na wahusika wa karakana hiyo ambako anatarajia kutumia fedha za mkopo wa gari la Ubunge kwa ajili ya kununua vitanda 200 ,viti vya magaurudumu pamoja na kabati ndogo za kuhifadhia dawa pamoja na vifaa vidogo vya matibabu.


  0 0

  Januari 13,2016 Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza unawakutanisha Watanzania katika Uwanja wa Furahisha uliopo katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza kwa ajili ya Maombi ya rasmi ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Wasaidizi wake ili kuliongoza Taifa vema.

  Pia maombi hayo ni mahususi kwa ajili ya kuliombea Taifa kwa ajili ya kupata baraka mbalimbali. Kuanzia majira ya saa saba Wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wameanza kujongea kwa ajili ya kujumuika pamoja katika maombi hayo ambayo yatafikia tamati jioni.

  Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo huku wageni mbalimbali wakiwemo Viongozi wa dini pamoja na waimbaji nyimbo za injili wakihudhuria katika maombi hayo.
  Picha na George Binagi.

  0 0

  BAADA ya wasomaji kadhaa nchini kujinyakulia zawadi kwenye droo ya kwanza ya Shindano la Shinda Nyumba linaloendeshwa na Kampuni ya Global Publishers iliyofanyika Januari 7, mwaka huu katika Viwanja vya Mbagala Zakhem leo wamekabidhiwa zawadi zao katika Ofisi za Global Publishers, Bamaga Mwenge jijini Dar.
  HAPPYNESS HAULE (2)Mwakilishi kutoka Kampuni inayosambaza ving’amuzi vya TING, Anitha Chawe (kushoto), akimkabidhi zawadi mshindi wa kig'amuzi, Happyness Haule (katikati) na Ofisa Usambazaji wa Global Publishers, Yohana Mkanda (kulia) akimkabidhi TV leo katika ofisi za Global Publishers, Bamaga Mwenge jijini Dar.
  DONASIAN MSAKI AKIONESHA BEDSHEET ALIYOSHINDA (3)
  Donasian Msaki akiwa na bedsheet aliyoshinda
  DOREEN SAMUEL AKIONESHA ZAWADI YAKE (4)
  Doreen Samuel akionesha zawadi aliyoshinda.


  0 0

  WAZIRI wa Maji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge leo amekutana na mabalozi wa Misri na Denmark kwa nyakati tofauti ofisini kwake, Makao Makuu ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Ubungo Maji.


  Huu ni mwendelezo wa mazungumzo ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Lwenge na washirika wa maendeleo na wadau wa Sekta ya Maji ya kuweka mikakati ya kuinua na kuendeleza Sekta ya Maji nchini, mara baada ya juzi pia kukutana na Balozi wa Ubelgiji, Mhe, Paul Cartier.

   Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Misri, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf na Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Hamza Sadiki.
    Balozi wa Denmark, Mhe. Einar H. Jensen akisaini Kitabu cha Wageni, kwenye ofisi ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji, akiwa na msaidizi wake, Kansela wa Uchumi na Usimamizi wa Fedha za Umma , Mette Melson.
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge, Balozi wa Denmark, Mhe. Einar H. Jensen na Mkurugenzi wa Maji Mijini, Inj. Dkt. Justus Rwetabula.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,kabla ya uteuzi huo Mkuu huyo  alikuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba

   Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Bw. Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo kabla ya uteuzi huo Mkuu huyo  alikuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba
  Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Bw. Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo kabla ya uteuzi huo Mkuu huyo  alikuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba
   Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokuwa akisalimiana na kumpongeza Bw. Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo baada ua kuapushwa katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo kabla ya uteuzi huo Mkuu huyo  alikuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Picha na Ikulu, ZnZ


  0 0


   Mdau Lukindo Choholo ambaye ni Msaidizi wa Spika wa Bunge leo amelamba nondozzz ya  Stashahada ya Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia katika chuo cha Diplomasia kurasini jijini Dar es salaam

  Mdau Lukindo akiwa na mdau Lulu Mengele wa PPF ambaye naye kalamba nondozzzz chuoni hapo.

  0 0

  Meno ya Tembo vipande 8 vyenye uzito wa kilo 50 ya thamani  ya milioni  120  ambayo ni sawa na Tembo hai wanne aliyokamatwa nayo hivi karibuni mtuhumiwa  Nzuri Ndizu Mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
   
   Mtuhumiwa  Nzuri  Ndizu  Mkazi wa Kijiji  cha Mbende Wilaya ya Mlele akiwa katika  ofisi ya Kamanda  wa Polisi wa Mkoa wa Katavi  baada ya kukamatwa na meno ya Tembo  vipande  nane   yenye thamani ya shilingi  milioni  120  hapo juzi
  Kamanda wa  Polisi  wa Mkoa Katavi  Dhahiri Kidavashari akiwa ameshika meno ya Tembo  aliyokamatwa nayo mtuhumiwa  Nzuri Ndizu  mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele   Mkoa wa Katavi ambae alikamatwa juzi akiwa na vipande 8 yenye thamani  ya milioni 120. 
  Picha  na  Walter Mguluchuma Katavi yetu blog
  ---------------------------------------------
  Mtu mmoja aliyefahamika  kwa jina la  Nzuri  Ndizu (44) Mkazi wa Kijiji cha Mbede  Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi  amekamatwa akiwa  na meno  ya Tembo  nane  yenye uzito wa kilogramu 50 yakiwa na thamani ya shilingi milioni 120 ambapo ni sawa na Tembo wanne waliuwawa.
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari   kuwa  mtuhumiwa huyo alikamatwa   mida ya saa tatu  na nusu.
  Kidavashari alisema mtuhumiwa  Ndizu  alikamatwa  kufuatia   misako  na  uparesheni mbalimbali zinazoendelea kufanywa  na Jeshi la Polisi  ikiwa ni kuhakikisha  wahalifu  wa makosa mbalimbali wakimemo  wawindaji  haramu  wa wanyama pori  wanakamatwa.
  Siku hiyo ya tukio  jeshi la polisi  lilipata taarifa  toka kwa Raia  wema  kuwa katika  pori  la akiba  la Lwafe  kuna watu  wanajihusisha na biashara haramu ya meno ya Tembo.
  Kidavashari aliendelea kuwaambia waandishi wa Habari  baada ya taarifa hizo kupokelewa  ufuatiliaji  ulifanyika  kwa polisi kufika  kwenye eneo hilo  na kuweka  mtego.
  Na walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo  Nzuri Ndizu  akiwa  na meno ya Tembo  vipande nane  akiwa ameyaficha kwenye  pori kwa ajiri ya kusubilia wateja.
  Kamanda Kidavashari alisema mtuhumiwa   anaendelea  kushikiliwa  na  jeshi la Polisi  kwa hatua za  upelelezi  zaidi  ilikuendelea  kubaini  mitandao  yote inayojihusisha  na biashara  hiyo haramu  ya meno ya Tembo na kufikishwa Mahakamani  baada ya upelelezi  kukamilika.

  Hivi karibuni watu watatu walikamatwa katika mtaa wa Aiter Mjini hapa  wakiwa na vipande  kumi na mbili vya meno ya Tembo yenye thamani ya shilingi milioni 120 hari hiyo inaonyesha kuwa kuna kasi kubwa ya biashara haramu ya meno ya Tembo Mkoani Katavi 
  Na Katavi yetu blog/Blogs za Mikoa

  0 0

  Kampuni ya safari za ndege za bei nafuu iliyosajiliwa Tanzania, Fastjet,  imezindua safari zake za Dar es Salaam-Nairobi. 
  Ndege ya Fastjet kutoka Dar es Salaam ilitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi na kulakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule. 
  Wakurugenzi wawili wa kampuni hiyo, Balozi Ami Mpungwe na Bw. Lawrence Masha, pamoja na Meneja Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Jimmy Kibati, walijumuika kwenye safari hiyo. 
  Kwa kuanzia, Fastjet itafanya safari za Dar es Salaam-Nairobi-Kilimanjaro na baadae itaanzisha safari za Dar es Salaam-Mombasa-Zanzibar. 
  Mhe. Haule alipongeza uanzishwaji wa safari hizo, akisema zitaimarisha ushirikiano kati ya Kenya na Tanzania na kukuza utalii na biashara.
  Balozi Haule akiogoza kukata keki ya kusherehekea uzinduzi huo
   Picha ya pamoja ya Balozi Haule na Maofisa wa Fastjet.
  Abiria wakiwasili uwanja wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo
  Picha ya kumbukumbu ya uzinduzi huo
  Balozi Haule, Balozi Mpungwe, Bw. Masha na Bw. Kibati wakishangilia baada ya uzinduzi rasmi.akishangiliwa baada ya kukata utepe kuzindua safari za Fastje kati ya Dar es Salaam na Nairobi. Wanaoshuhudia ni Balozi Mpungwe (Kushoto) na Bw. Kibati (Kulia)


  0 0


  0 0  0 0
  0 0

  Kampuni ya BrighterMonday ambayo ni tovuti namba moja ya ajira nchini Tanzania. Leo hii imezindua kituo kipya ambacho kitatumika kwa ajili ya huduma ya mawasiliano na wateja ambao ama ni watafuta ajira wapya au wanataka kubadili ajira. 
  Akizungumza wakati wa hafla ya kifungua kinywa Bwana Lugendo Khalfan, Meneja Masoko wa Kampuni ya BrighterMonday Tanzania alisema kwamba changamoto kubwa nchini Tanzania ni kuwa kuna watafuta ajira wengi sana kuliko nafasi za ajira zilizopo sokoni, hivyo kwa kupitia kituo hiki itawarahisishia watafuta ajira kuongeza nafasi ya kupata ajira kiurahisi na huduma zote ni bure. 
  Naye Bi. Eva Slootweg, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BrighterMonday amekielezea kituo hicho cha ajira ambacho kipo katika tovuti ya kampuni hiyo ambayo ni www.brightermonday.co.tz kuwa kina mfumo wa kuchambua maombi ya kazi mpaka kupata wachache wenye kukidhi viwango. 
  Kwenye suala la upatikanaji wa watu wenye vigezo, utendaji mzuri, mahusiano kazini na ujuzi katika uongozi pamoja, kampuni ya Brighter Monday ina uwanja mpana ambao unakwenda sambamba na mabadiliko yaliyoko katika sekta ya ajira ambayo si tu inatilia mkazo uwezo wa utendaji kazi na ufanisi wa mwombaji ajira bali ni kwa namna gani mwomba ajira anaendana na utamaduni wa taasisi husika. 
  Bi Sabiha Monji, Mkurugenzi Mtendaji wa Shugulika Recruitment, alisema mojawapo ya changamoto wanayokutana nayo hapa Tanzania ni kukosa umakini kwa baadhi ya watafutaji ajira, “wengine wanashindwa kufika katika usaili bila hata kutoa taarifa”. Katika utafutaji kazi katika mtandao, Bi Sabiha alidokeza kwamba Tanzania kwa sasa ina watafuta ajira zaidi na zaidi wanaotafuta kupitia mtandao, hivyo kuna kuna ongezeko la watumiaji mtandao katika kutafuta ajira. 
  Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya waajiri 3000 kutoka sekta mbalimbali huajiri kupitia BrighterMonday.

  Kampuni ya BrighterMonday inafahamu changamoto zinazowakabili wadau wake hivyo hutoa ufumbuzi unaokidhi matakwa ya mwajiri kwa kumpatia mwajiriwa anayewafaa. Kutokana na uzoefu wa muda mrefu na kutokana na maoni kutoka kwa wateja, na kwa ubunifu wameweza kuongoza soko la ajira nchini. 
  Kampuni ya BrighterMonday inadhamiria kuendelea kuwashirikisha wadau wake kwa njia ya mijadala ya kiuongozi ili waelewe changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya ajira Tanzania na kutoa suluhisho kwa ubunifu na mikakati iliyo bora kama  mshirika na kampuni namba moja ya ajira nchini.

   Brighter Monday ni nini?
   BrighterMonday Tanzania ni kampuni kubwa ya ajira mtandaoni, yenye watafuta ajira bora kuliko kampuni yoyote. Kwa nia ya kuwarahisishia watafuta ajira, tumeshirikiana na waajiri mbalimbali kuhakikisha kuwa katika upatikanaji wa ajira kirahisi Zaidi, na ni daraja kati ya soko la ajira na waajiri. BrighterMonday iko chini ya mwamvuli wa makampuni ya One Africa Media (OAM), kampuni kubwa ya biashara za mtandaoni barani Africa. OAM inashughulika na safari za kiutalii mtandaoni, magari na ajira katika maeneo mbali mbali Afrika.
    
  Imetolewa na;

  Kitengo cha Masoko:

  BrighterMonday Tanzania Limited,

   Lugendo Khalfan,

  Meneja Masoko.


  0 0

  Image result for ARDHI YA KIJIJI
  Na Bashir Yakub
  Suala  la  kudai  fidia  pindi  ardhi  ya kijiji  inapotwaliwa  linaongozwa  na sheria  ya  ardhi  ya  vijiji  ya  1999. Fidia  ni  haki  pale  ardhi  ya  kijiji  inapotwaliwa. Ziko  sababu  zinazoweza  kuifanya  serikali  kutwaa  ardhi  ya  kijiji  kwa  mfano   kupisha  miradi  ya  maendeleo,  kupisha  uwekezaji  kwa  manufaa  ya  kijiji  husika  na  taifa  zima,  halikadhalika   kuondoka  katika  eneo  ambalo  limetangazwa  kuwa  hatarishi  kwasababu  za  kijiografia  au  nyinginezo.  
  Yumkini  kwasababu yoyote  katika    hizi  fidia  hubaki  haki  ya  msingi  kwa  mwananchi. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mbunge wa Chalinze, mkoani Pwani, Ridhwan Kikwete, akimuelezea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (kushoto), migogoro ya ardhi iliyopo kwenye jimbo lake hilo, wakati waziri Lukuvi alipofika Wilaya ya Bagamoyo, kusikiliza migogoro na matatizo ya ardhi inayoikabiri wilayani humo.

  0 0
 • 01/13/16--19:00: NGOMA AZIPENDAZO ANKAL

 • OFFSIDE TRICK - Kidudu mtu

  0 0  0 0

  SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS), LINAPENDA KUWAKUMBUSHA WAUZAJI WOTE WA BIDHAA ZA MATAIRI YALIYOTUMIKA, NGUO ZA NDANI ZA MITUMBA, VILAINISHI VYA MAGARI NA MITAMBO

  (OIL LUBRICANTS) NA BIDHAA ZOTE  AMBAZO HAZIJATHIBITISHWA UBORA WAKE NA TBS, KUZIONDOA SOKONI BIDHAA HIZO MARA MOJA. 

  HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA KWA YEYOTE ATAKAYEKAIDI AGIZO HILI.  TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MKURUGENZI MKUU WA   SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA.


older | 1 | .... | 1088 | 1089 | (Page 1090) | 1091 | 1092 | .... | 3286 | newer