Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live

ZIARA YA MKURUGENZI WA MAUZO NA MASOKO WA NHC LINDI, MTWARA NA RUVUMA

$
0
0
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Lindi Patrick Mussa Kamendu akimpa taarifa ya hali ya mauzo na masoko na utekelezaji wa miradi ya shirika la nyumba la taifa katika mkoa wake kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa katika ziara ya NHC mkoa wa Lindi kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo mikoani.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Lindi Patrick Mussa Kamendu akiongozana na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Mtanda Lindi, katika ziara ya NHC mkoa wa Lindi kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo mikoani.
Nyumba za gharama nafuu za NHC Mtanda, Lindi linavyoonekana katika picha.

Mbwana Samatta akutana na Mufti Mkuu Sheikh Zuberi

$
0
0
 Mwanasoka Bora Afrika Ndg. Mbwana Samatta akikabidhiwa baadhi ya zawadi mbalimbali na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir katika ofisi kuu za Bakwata zilizopo Kinondoni Jijini Dar Es Salaam. 
Leo tarehe 11 January 2016, Mwanasoka Bora Afrika Ndg. Mbwana Samatta alimtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir katika ofisi kuu za Bakwata zilizopo Kinondoni Jijini Dar Es Salaam.

Mufti Mkuu mbali na kumpatia zawadi mbalimbali kwa ajili ya kumsaidia katika imani yake pia alipata nafasi ya kumuombea dua ya mafanikio zaidi huko aendako Ulaya na kumpa nasaha asisahau kumuomba Mwenyezi Mungu kila wakati na kufanya ibada muda wote atakaokuwa nje ya mazoezi. 

Mwisho Mufti alimtakia mafanikio mema na kumuambia dua za watanzania wote zipo naye. 

Airtel Fursa Msimu wa 2 wazinduliwa, kuendelea kuinua maisha ya watanzania wengi zaidi

$
0
0
 Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde ( wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil Colaso,akifatiwa na Mshauri wa Airtel Fursa, Eng George Mulamula kwa pamoja wakionyesha bango kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Airtel Fursa msimu wa pili. Akishuhudia (kushoto) ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya.
 Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil Colaso akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa 2. mradi unaowawezesha vijana kati ya miaka 18 hadi 24
kupata fursa za kuinua biashara zao, uliyozinduliwa Naibu waziri Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde  katika ofisi ya Airtel makao makuu Jijini Dar es saalam
 Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa 2 mradi unaowawezesha vijana kati ya miaka 18 hadi 24  kupata fursa za kuinua
biashara zao. Uzinduzi huo ulifanyika katika ofisi ya Airtel makao makuu Jijini Dar es saalam
 Kijana aliyewezesha kupitia mradi wa Airtel FURSA msimu wa 1, Mohamed Kigumi akipongezwa na  Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil Colaso kwa kufanya vizuri katika biashara yake wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa mradi wa Airtel FURSA , mradi wenye lengo la kuwawezesha vijana kufikia malengo yao na kukuza biashara zao. Wakishuhudia (kushoto) ni Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde  akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya. (kulia) ni Mshauri wa Airtel Fursa, Eng George Mulamula
 Mshauri wa Airtel Fursa, Eng George Mulamula akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa pili
 Wageni waalikwa na waandishi wa habari wakifatilia uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa pili uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel Morocco jijini Dar es Saalam
Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde  akiteta jambo na  Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa pili.
 

  *   zaidi ya shilingi billion 1 kusaidia  miradi ya kuwawezehsha vijana llings
 Kampuni ya simu ya mkononi
ya Airtel leo imezindua msimu wa pili wa mradi wake wa kuwawezesha
vijana ujulikanao kama "Airtel FURSA" kwa lengo kuendelea kudhihirisha
kutimiza dhamira yake kuendeleza huduma za kijamii nchini
Mradi wa "Airtel FURSA" ulizinduliwa Mei 2015, ukiwa na lengo la
kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mbinu mbalimbali za biashara na vifaa
vitakavyowawezesha kukuza biashara zao

Msimu wa kwanza wa "Airtel FURSA"  umewawezesha vijana zaidi ya 2500
wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 kupata mafunzo ya biashara na
wengine 13 wafanyabiashara chipukizi wanaofanya vizuri zaidi kupokea
vifaa vilikvyowasaidi kuboresha biashara zao na kutengeneza fursa
zaidi kwa jamii inayowazunguka.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil
Colaso, alisisistiza dhamira ya kampuni yake  kuwawezesha vijana na
kutambua mchango walio nao katika kuendesha uchumi wa Tanzania
" Mradi huu wa "Airtel FURSA"   unadhihirisha dhamira yetu ya
kuwawezesha vijana wa kitanzania wenye malengo ya kuinua maisha yao na
kutimiza ndoto zao. Msimu wa kwanza wa "Airtel FURSA" umetoa matokeo
mazuri sana na  tumefanikiwa  kugusa maisha ya  maelfu ya vijana wengi
kutoka katika mikoa mbalimbali nchini,"

"Katika msimu huu wa pili tunawekeza takribani  shilingi  billion moja
ili  kuweza kufikia vijana wengi zaidi ambao wako tayari kutumia fursa
na vipaji vyao. Tutaendelea kuwapatia mafunzo ya kibiashara, misaada
ya vifaa na kuanzisha mfumo wakisasa wa mafunzo kupitia simu zao za
mkononi" alisema Colaso.

Akizindua rasmi mradi wa "Airtel FURSA" Naibu waziri  Wizara ya Kazi
Vijana na Ajira Anthony Mavunde aliwapongeza Airtel kwa kuanzisha  na
kuwekeza kwenye mradi huu mkubwa na kutoa wito kwa vijana kutumia
fursa hii ili kuboresha maisha yao. alisema Mh Mavunde
"Nchi yetu ya Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na rasilimali,
zikiunganishwa pamoja na fulsa zinazoletwa na miradi kama hii ya
"Airtel FURSA" ni wazi vijana wenye malengo Dhahiri ya kujiendeleza
wataweza kuboresha maisha yao. Napenda kuwahasa vijana wetu kutumia
fursa hii na kufanya kazi kwa bidii:"

"Serikali chini ya Wizara yetu na itaendelea kushirikia Airtel na
kufanya kazi kwa pamoja huku ikiweka mazingira bora yatakayochochea
vijeza ana kupata fursa ili waweze kuchangia katika kuendeleza  uchumi
wa nchi" aliongeza Mavunde

"Airtel FURSA"  ni mradi endelevu unaowalenga vijana nchi nzima kwa
kuwapatia vifaa  ,mafunzo ya biashara na mafunzo mbalimbali kupitia
mtandao ili kufikia malengo yao. Kutuma maombi tuma ujumbe mfupi
kwenda namba 15626 ikiwa na taarifa zifatazo Jina, umri, aina ya
biashara unayoifanya, mahali na namba za simu. Unaweza pia kutuma
maombi yako kwa kupitia barua pepe ya
airtelfursa@tz.airtel.com<
mailto:airtelfursa@tz.airtel.com>. Or
tembelea tovuti yetu ya  www.airtel.com<http://www.airtel.com>  na
ujaze fomu yako ya maombi
 

PRESS CONFERENCE YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD JIJINI DAR ES SA SALAAM

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) na aliyekuwa Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa tiketi ya Chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamadi amesema kuwa hana taarifa zozote juu ya swala la  kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar na badala yake ametaka kura zilizobaki zihesabiwe na mshindi aweze kutangazwa.

Maalim Seif ameyasema hayo leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji Mstaafu Jecha Salum Jecha alikuwa hana mamlaka ya kufuta uchaguzi kutokana na hatua zote za uchaguzi.

Amesema kuwa Mwenyekiti wa ZEC hana mamlaka ya kufuta uchaguzi bila kuwa na wajumbe walio wengi wanaounga mkono kile wanachotaka kuamua, hali ambayo haikufanyika wakati wa kufuta uchaguzi huo.

Maalim amesema Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha alikwenda kufuta uchaguzi bila kuwataarifu makamishna wa tume hiyo wakati siku mbili hakuweza kufika katika kutangaza matokeo ya urais, hivyo alichokifanya ni ukiukwaji wa maadili na Sheria na wanashangaa kwa Rais kushindwa kumchukulia hatua.

Maalim amesenukuu kifungu kinachomuongoza Mwenyekiti wa ZEC kinachoeleza kuwa “Kiwango cha mikutano ya ZEC ni Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanne na kila uamuzi wa tume ni lazima uungwe mkono na wajumbe walio wengi”

Aidha Maalim Seifu amesema katika mazungumzo wanayoyafanya huko Zanzibar chini ya Mwenyekiti, Dk. Ali Mohamed Shein hana imani nayo kutokana na kile kinachojadiliwa kuwa wanakitoa wakati sio makubaliano katika kamati hiyo.

Maalim Seif amemtaka Rais Dk. John Pombe Magufuli kuingilia kati suala hili katika kuweza kupata suluhu ya mwafaka kwa amani kutokana na Dk. Ali Mohamed Shein kushindwa kuhimili mazungumzo hayo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Aliekuwa Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari juu ya mustakabali wa hali ya kisisa Visiwani Zanzibar, uliofanyika leo Januari 11, 2016 kwenye Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam. Katika Mkutano huo, Maalim Seif amesema kuwa hana taarifa yeyote juu ya swala linalosikika kutoka kwa baadhi ya viongozi kuhusiana na kurudiwa kwa Uchaguzi wa Zanzibar. PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG
Sehemu ya wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini wakiendelea kumsikiliza kwa makini, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Aliekuwa Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, alipokuwa akiongea nao leo leo Januari 11, 2016 kwenye Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
 Waandishi wa habari wakifatilia kwa makini Mkutano huo.


NGOMA AFRICA BAND AKA FFU INAWATAKIENI HERI YA MIAKA 52 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

$
0
0
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni inawatakieni heri ya kuazimisha miaka 52 ya  mapinduzi ya Zanzibar,Mapinduzi yaliyofanyika 12 January 1964 ambayo yaliwakomboa wananchi wanyonge wazanzibar walikuwa chini ya utawala wa Kisultan,Mapinduzi hayo ya tarehe 12 January 1964 yaliyomfanya Sultan kuikimbia Zanzibar na kusahau kiremba kitandani.
Mungu yabariki Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Mungu wabariki Wanzibari na kudumisha amani na upendo daima, Mungu ibariki Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tusherehekee Mapinduzi day kwa burudani ya www.ngoma-africa.com

JK AMPONGEZA SAMATTA LEO

$
0
0

Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Kikwete akizungumza na kumpongeza Nyota wa Soka Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta (kushoto), alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kutana na mchezaji huyo leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili ya kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo.Kulia ni Waziri Nape.
Nyota wa Soka wa Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta, akimkabidhi Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Kikwete, aliyokuwa akiitumia katika timu ya TP Mazeembe ya Congo DRC, katika hafla ya Kikwete iliyofanyika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili yaRais huyo mstaafu kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo.
JK na Samatta wakitoka ukumbini.

PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

MATEMBEZI YA UMOJA VIJANA CCM KUADHIMISHA MIAKA 52 YA MAPINDUZI

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Matembezi ya Umoja wa Vijana wa CCM katika kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo katika viwanja vya maisara Suleiman Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa Vijana wa Umoja wa Vijana UVCCM walioshiriki matembezi ya kuadhimisha Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyomalizia leo katika Viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja(kulia) Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan,na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM TaifaSadifa Juma Khamis(kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi PPandu Ameir Kificho na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Picha ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume kutoka kwa Kiongozi wa Matembezita Umoja wa Vijana wa CCM Daudi Ismail katika kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo katika viwanja vya maisara Suleiman Mjini Unguja (kushoto) Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma khamis.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikimkabidhi  Picha ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma khamis baada ya  kupokea picha hiyo kutoka kwa Kiongozi wa Matembezita Umoja wa Vijana wa CCM Daudi Ismail katika kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo katika viwanja vya maisara Suleiman Mjini Unguja. 


MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA KITUO CHA KUKUZA WAJASIRALI ZANZIBAR LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua kituo cha kukuza na kulea wajasiriamali (ZANZIBAR TECHNOLOGY AND BUSSNESS INCBATTION CENTER-ZTIBI) kiliopo Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar leo Januari 11, 2016, ikiwa ni moja ya miongoni mwa shamra shamra ya kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi Zanzibar inayofikia kilele chake kesho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Time Mohammed juu ya utenganishaji wa maji na maziwa katika kituo cha kukuza na kulea wajasiriamali (ZANZIBAR TECHNOLOGY AND BUSSNESS INCBATTION CENTER-ZTIBI) kiliopo Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar leo Januari 11, 2016, ikiwa ni moja ya miongoni mwa shamra shamra ya kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi Zanzibar inayofikia kilele chake kesho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya mitambo inayotumia nguvu ya umeme wa jua ya kutengenezea nafaka za aina mbalimbali katika kituo cha kukuza na kulea wajasiriamali (ZANZIBAR TECHNOLOGY AND BUSSNESS INCBATTION CENTER-ZTIBI) kiliopo Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar leo Januari 11, 2016, baada ya kukifungua rasmi ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra ya kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi Zanzibar inayofikia kilele chake kesho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na mama Mwanamwema Shein katikati na Mama Asha Ali Iddi baada ya kutembelea maonesho ya kazi mbalimbali zinazofanywa na kituo cha kukuza na kulea wajasiriamali (ZANZIBAR TECHNOLOGY AND BUSSNESS INCBATTION CENTER-ZTIBI) kiliopo Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar leo Januari 11, 2016, ikiwa ni moja ya miongoni mwa shamra shamra ya kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi Zanzibar inayofikia kilele chake kesho. (Picha na OMR)

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI WAZIRI MKUU MSTAAFU SUMAYE ALIYELAZWA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI LEO

$
0
0
  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye na Mama Esther Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Jumatatu Januari 11, 2016
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Jumatatu Januari 11, 2016
PICHA NA IKULU.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAFARIJI FAMILIA YA NYERERE.

$
0
0
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na wanafamilia  alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani. 
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimfariji  na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,na wanafamilia  alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani. 
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na wanafamilia alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani.

JESHI LA POLISI KITENGO CHA USALAMA BARABARANI PAMOJA NA VODACOM TANZANIA WAENDESHA ZOEZI LA KUTOA ELIMU KWA MADEVA KUTOKUTUMIA SIMU WAKATI WAKITUMIA VYOMBO VYA MOTO

$
0
0
Msaidizi Mkaguzi Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Wilaya ya Mtwara(DTO) Ahmed Mutabuzi(wapili toka kushoto) akiwakiwaelimisha madereva wa mabasi yanayofanya safari za mikoani kuhusiana na mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto,Zoezi hilo lilifanyika stendi kuu ya mabasi ya Mtwara mjini,Katikati pichani ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambao ni wadhamini wakuu wa kampeni hiyo.
Madereva wa mabasi ya Mkoani Mtwara yanayofanya safari za mikoa mbalimbali wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(wapili toka kushoto)akiwasomea ujumbe maalum ambao ni kauli mbiu ya kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto,Zoezi hilo lilifanyika stendi kuu ya mabasi ya Mtwara mjini,Kushoto ni Msaidizi Mkaguzi Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Wilaya ya Mtwara(DTO) Ahmed Mutabuzi.
Msaidizi Mkaguzi Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Wilaya ya Mtwara(DTO) Ahmed Mutabuzi pamoja na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambao ni wadhamini wakuu wa kampeni ya”Wait to Send” inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto wakipandika stika yenye ujumbe maalum wa kampeni hiyo kwenye basi linalofanya safari za mikoani wakati wa zoezi hilo lililofanyika stendi kuu ya mabasi ya Mtwara mjini.
Askari wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mtwara SGT. Martin Muyomba(kushoto) akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Masoud Ramadhani ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send” inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto,Zoezi hilo lilifanyika stendi kuu ya mabasi ya Mtwara mjini,Katikati pichani ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambao ni wadhamini wakuu wa kampeni hiyo.
Askari wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mtwara SGT. Martin Muyomba(kushoto)akiandika maelezo ya Mohamed Rashid(kulia)ambaye ni dereva wa basi linalofanya safari za mikoani ili ampime kiwango cha pombe mwilini wakati wa zoezi la mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send” inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto,Zoezi hilo lilifanyika stendi kuu ya mabasi ya Mtwara mjini,Katikati pichani ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambao ni wadhamini wakuu wa kampeni hiyo.

EALA TO HOLD PUBLIC HEARING WORKSHOP ON REPUBLIC OF BURUNDI JANUARY 13-16 IN ARUSHA

$
0
0
East African Legislative Assembly, Arusha, Tanzania: January 12, 2016: EALA will from Wednesday (January 13, 2016) hold a four-day public hearing workshop on the humanitarian crisis in Burundi.

The EALA Regional Affairs and Conflict Resolution Committee (RACR) has called for the public hearing workshop that is intended to review the petition by the Pan African Lawyers Union (PALU) submitted to EALA in November 2015 on the subject matter.

The Committee on Regional Affairs and Conflict Resolution is set to establish the facts of humanitarian atrocities as reported in the petition and to make recommendations to the House during the next Sitting scheduled to commence on January 24th, 2016 in Arusha.

Participants are expected from the Committee Membership, government officials from the Republic of Burundi, Civil Society Organisation representatives from Burundi, representatives from the country’s Political Parties and the petitioners.

On November 16th, 2015, four Civil Society Organisations led by PALU petitioned EALA to urgently undertake specified number of actions within its mandate to contain the situation in the Republic of Burundi.The petition was presented to the Speaker of EALA, Rt. Hon Daniel F. Kidega, in Arusha by PALU and the East African Civil Society Organisations’ Forum (EACSOF).

In addition to PALU (Principal Petitioner) and EACSOF, Atrocities Watch Africa, Centre for Citizens’ Participation on the African Union, East Africa Law Society (EALS) and the Kituo Cha Katiba (KcK) also appended their signatures to the petition.

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi yaipa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu timu ya Polisi Dodoma

$
0
0
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi umeipa Polisi Dodoma ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Mji Mkuu FC kumchezesha mchezaji Peter Ngowi aliyekuwa na kadi tatu za njano kwenye mechi yao ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes iliyochezwa Desemba 26, 2015 mjini Dodoma.

Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 37(4) na 14(37) ya Ligi Daraja la Kwanza. Mji Mkuu FC ilikuwa imeshinda mabao 2-1 katika mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Mgambo mjini Mpwapwa.

Kamishna wa mechi ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Polisi Tabora na Panone FC ya Moshi, Shabani Funyenge amesimamishwa kutokana na ripoti yake ya mechi hiyo iliyochezwa Januari 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kuwa na upungufu.

Klabu ya Friends Rangers ya Dar es Salaam imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kutokana na washabiki wa timu yake kutoa kashfa na lugha za matusi wakati wa mechi ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes dhidi ya Kiluvya United iliyofanyika Novemba 8, 2015 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Kaume jijini Dar es Salaam.

Pia imetakiwa kulipa kibendera cha kona (corner flag) pamoja ubao wa matangazo wa geti la kuingilia ndani kwenye Uwanja wa Karume ambavyo vilivunjwa na washabiki wa timu hiyo mara baada ya mechi hiyo.

Mtunza vifaa wa timu ya Kimondo, Emily Nehemia, Meneja wa timu ya Polisi Tabora, Idd Kibwana, Kiongozi wa Panone FC, Said watafikishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu kwenye mechi za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes.

Mji Mkuu FC imepigwa faini ya sh. 100,000 (laki moja) kwa kutohudhuria kikao cha awali cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) katika mchezo kati yao na Polisi Dar es Salaam uliochezwa Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Klabu za Polisi Tabora na Panone FC kila moja imepigwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(48) kugombania kuingia uwanjani kupitia mlango wa VIP badala ya ule wa kawaida kwenye mechi yao ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes iliyochezwa Januari 2, 2016 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Wachezaji Ally Mwanyiro wa Rhino Rangers na Hamisi Shaban wa Lipuli wamepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kila mmoja na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kupiga wachezaji wa timu pinzani wakati wa mechi zao za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes kinyume na Kanuni ya 37(3) ya Ligi hiyo.

Pia Polisi Mara imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya mshabiki wao kuingia uwanjani na kumvamia mwamuzi kwa madai maamuzi yake hayakuwa sahihi wakati wa mechi yao ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes dhidi ya Mbao FC iliyofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

WAZIRI KITWANGA AKUTANA NA VIONGOZI WA WILAYA YA MISUNGWI, ACHANGIA MIRADI YA MAENDELEO.

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza mara baada ya kupokelewa wilayani hapo. Waziri Kitwanga aliwataka viongozi hao kuongeza nguvu kubwa ya kukusanya kodi kwa wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa na si kuwasumbua wafanyabiashara wadogowadogo. Pia aliwataka viongozi hao wahakikishe hakuna mwanafunzi atakayekaa chini darasani ifikapo mwakani.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akiwauliza maswali viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wakati alipokuwa anakagua ujenzi wa Maabara katika Shule ya Sekondari Aimee Milembe wilayani humo.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kushoto) akiangalia ufa katika moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Lubuga iliyopo Kata ya Mabuki wilayani Misungwi. Waziri Kitwanga aliagiza darasa hilo livunjwe na ameahidi kuchangia matofali pamoja na mifuko ya saruji.
Picha zote na Felix Mwagara.

UTT AMIS YATOA SEMINA KWA WAFANYAKAZI WA MAZNAT JUU YA UWEKEZAJI WA PAMOJA

$
0
0
Mkurugenzi wa Maznat Bridal akifungua semina kwa wafanyakazi wake juu ya huduma bora kwa wateja, ujasiriamali na Uwekezaji wa Pamoja iliyofanyika katika hoteli ya Kebbs jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa masoko na uhusioano UTT AMIS akihamasisha Uwekezaji wa Pamoja katika semina ya wafanyakazi wa Maznat Bridal and Beauty Services katika hoteli ya Kebbs jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusioano UTT AMIS akihamasisha Uwekezaji wa Pamoja katika semina ya wafanyakazi wa Maznat Bridal and Beauty Services katika hoteli ya Kebbs jijini Dar es Salaam.

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA ALIYEKUWA MBUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA MHESHIMIWA LETICIA NYERERE

$
0
0

Napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Viongozi, wanachama na wapenzi wa CHADEMA wa Tawi la Washington DC, Marekani,  kutuma salamu za pole kwa familia ya aliyekuwa Mbunge wa viti maalum Chadema Kupitia Jimbo la Kwimba Mheshimiwa Leticia Nyerere (pichani) kilichotokea baada ya kuugua kwa muda mfupi hapa Maryland, Marekani, siku ya Jumapili Tarehe 10 Januari 2016. 

Kwa hakika tumepokea taarifa ya msiba wa mheshimiwa Leticia Nyerere kwa mshtuko mkubwa kutokana na kumbukumbu ya mchango mkubwa aliyotoa kwenye kufungua Tawi letu la Chadema hapa Washington DC, Marekani. Pia kwa mchango wake aliyotoa akiwa kama mbunge wa Viti Maalum kupitia Chadema. Kwa kweli bado tulikuwa tunahitaji sana mchango wake lakini mpango wa mungu hauna makosa.


Mungu ailaze roho ya Marehemu Leticia Nyerere 
mahali pema peponi, Amin.

Mwenyekiti wa CHADEMA Washington DC, Marekani


Kalley Pandukizi

WAZIRI LUKUVI AWAONYA MADALALI WA ARDHI, AFANYA ZIARA KIBAHA ADHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi akikagua mafaili ya hati za ardhi za wananchi yanayodaiwa kukaa kwenye shelvu kwa zaidi ya miaka mitatu pasipo kufikishwa kwa wahusika. Anayempa maelezo ni Afisa Ardhi Mteule, Majaliwa Jaffari. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi akikagua mafaili ya hati za ardhi za wananchi yanayodaiwa kukaa kwenye shelvu kwa zaidi ya miaka mitatu pasipo kufikishwa kwa wahusika. Anayempa maelezo ni Afisa Ardhi Mteule, Majaliwa Jaffari. 
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Bi. Halima Kiemba akimsomea muhtasari Waziri wakati wa kikao na viongozi pamoja na watendaji wa wilaya hiyo Mkoa wa Pwani jana. Kutoka (kulia) ni Mkubge wa Kibaha, Mhe. Koka Foka na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mgeni Bauani. 


Samatta kupongezwa Dar Live leo

$
0
0
Mchezaji Bora wa Mwaka 2015 kwa Wachezaji wa Ndani, mchezaji wa Taifa Stars na Klabu ya TP Mazembe ya DRC Congo, Mbwana Samatta.

BAADA ya kushinda Tuzo ya Afrika kama Mchezaji Bora wa Mwaka 2015 kwa Wachezaji wa Ndani, mchezaji wa Taifa Stars na Klabu ya TP Mazembe ya DRC Congo, Mbwana Samatta anatarajiwa kupongezwa na kuagwa rasmi na mashabiki wake leo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.  Akizungumza na Uwazi, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa mapema kabla ya saa kumi na mbili jioni kutakuwa na matembezi sambamba na Samatta maeneo ya Temeke na baada ya hapo, saa kumi na mbili atatinga ndani ya Dar Live kuwaaga mashabiki wake. 

“Kutakuwa na red carpet ambapo mashabiki wote watapata fursa ya kupiga picha na Samatta sambamba na kuzungumza naye mawili matatu kisha burudani kabambe itafuatiwa kutoka kwa Khalid Chokoraa ambaye tayari amemtungia wimbo, Twanga Pepeta chini ya Ali Chocky pamoja na Msagasumu,” alisema Mbizo na kumalizia kuwa kiingilio kitakuwa ni 5,000 kwa wote.

BALOZI MASILINGI AHANI MSIBA WA LETICIA NYERERE LANHAM, MARYLAND

$
0
0

 Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi (Wapili kushoto) akitoa pole kwa Madaraka Nyerere ( wakwanza kushoto) mume wa marehemu Leticia Nyerere nyumbani Lanham, Maryland nchini Marekani siku ya Jumatatu January 11, 2016. Wengine kwenye picha ni Emmanuel Muganda na Mwenyekiti wa CHADEMA DMV Kalley Pandukizi (kulia). PICHA NA VIJIMAMBO/KWANZA PRODUCTION
 Kutoka kushoto ni Zuberi, Afisa Ubalozi Swele na Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Colonel Adolph Mutta.
Wanne toka kushoto ni Mke wa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Marystella Masilingi akiongea jambo na Swahiba Mdeme Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani (wapili toka kulia). Kulia ni Mrs Muganda wakijumuika na wafiwa katika kuwafariji katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
Afisa Ubalozi Suleiman Saleh akiwa na Katibu Muenezi na Itikadi CCM DMV Bi. Salma Moshi  wakihani msiba wa marehemu Leticia Nyerere aliyeaga Dunia siku ya Jumapili January 10, 2016 katika hospitali ya Jumuiya ya Madakatari iliyopo Lanham, Maryland nchini Marekani.

Viewing all 110031 articles
Browse latest View live




Latest Images