Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1079 | 1080 | (Page 1081) | 1082 | 1083 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kanda ya Songea, wakati akiendelea na ziara yake mkoani Ruvuma. 
   Akizungumza na wafanyakazi wa Wakala hiyo, wadau wa kilimo pamoja na wananchi jana, (Jumatatu, Januari 4, 2016) nje ya majengo ya Wakala mara baada ya kukagua mahindi yaliyohifadhiwa katika maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kanda ya Songea , mkoani Ruvuma amesema kufuatia taarifa ya kuwepo na baadhi ya maeneo yenye njaa nchini, Serikali imetoa tamko kuwa hakuna mtanzania atayakekufa kwa njaa. 
  Ambapo, Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa imeweka mikakati ya kukabiliana na tatizo la njaa kwa kutoa msaada wa chakula katika maeneo yanayokabiliwa na njaa. 
   “Ni wajibu wangu kuhakikisha nasimamia vizuri hili, nimeona hali ya uhifadhi wa chakula, tunayo mahindi ya kutosha lakini hakuna sehemu ya kuhifadhi chakula” amesema Waziri Mkuu. 
   Waziri Mkuu Majaliwa ameendelea kwa kusema uwezo wa maghala hayo yaliyopo chini ya Wakala Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kanda ya Songea yana uwezo wa kuhifadhi tani 29 pekee na Songea inauwezo wa kuzalisha zaidi tani 70 hadi 80. 
   Pia , ameagiza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kanda ya Songea , kuanzia mwaka huu kwa kushirikiana na Wakuu wa Mikoa pamoja Wakuu wa Wilaya kuanzisha vituo vya kununulia mahindi na kuhakikisha magunia yanawafikia wakulima katika vituo hivyo ambapo wataweza kuhifadhi mahindi na kuuza kwa bei ya kwenye soko. 
   Waziri Mkuu pia, ameitaka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kanda ya Songea ,kutumia teknolojia ya kisasa ya uhifadhi wa chakula, kuandaa utaratibu maalum utakaozuia msongamano wa malori yanayosubiri kupata huduma ya kununua mahindi nje ya majengo ya Wakala na kukamilisha miradi itakayosaidia Wakala kuwa na fedha za kutekeleza majukumu yake. 
   Kwa upande wake, Meneja Hifadhi wa Chakula kanda ya Songea, Bwana. Morgan Mwaipaya amesema kati ya maghala 33 ya kuhifadhi mahindi nchi nzima, Songea ina maghala 6 kati ya hayo. Hivyo, Wakala imeweka vipaumbele vyake ambavyo ni pamoja na kutoa chakula cha msaada kwa maeneo yenye matatizo ya njaa, kuongeza upatikanaji wa mahindi ili kuzuia kupanda kwa bei ya chakula mwaka 2015 – 2016, Wakala kununua na kuhifadhi mahindi katika maeneo yaliyozalisha zaidi na kuzingatia sehemu ya sehemu ya akiba ya chakula na kuuza kwa wakulima, mawakala pamoja na Wakala wa Chakula duniani (World food program). Amesema Wakala imeandaa mikakati ya mbalimbali ikiwemo kuongeza uwezo wa tani 24600 hadi tani 45000 kwa mwaka 2014- 2017, kuboresha mfumo wa utendaji kazi kwa kutumia mifumo ya stahili ya TEHAMA na kutumia fursa za mikopo kutoka Taasisi mbalimbali za kifedha ili kuendesha shughuli za uwezeshaji I kiwemo kuelimisha taratibu za ununuzi kwa mawakala. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa nje ya majengo ya maghala ya  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA mjini Songea  akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Januari 4, 2016. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa nje ya majengo ya maghala ya  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA mjini Songea  akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Januari 4, 2016. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa nje ya majengo ya maghala ya  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA mjini Songea  akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Januari 4, 2016.  
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Jego la Halmashauri ya Wilaya ya Peramiho akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Januari 4, 2015.  
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Maposele wilayani  Peramiho baada ya kukagua ujenzi wa  jingo la Ofisi ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma  Januari 4, 2016. PIcha na Ofisi a Waziri Mkuu


  0 0
  0 0


  Mkurugenzi wa Mambo ya nje wa Chama cha NCCR-Mageuzi na Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki,Ndelakindo Kessy akizungumzia utaratibu ambao chama hicho umeuanzisha wa kusaidia watoto waishio katika mazingira magumu katika jimbo la Vunjo.
  Baadhi ya watoto kutoka kata 16 za jimboo la Vunjo walioandaliwa sherehe ya kuukarbisha mwaka mpya wa 2016 na Chama cha NCCR-Mageuzi katika jimbo la Vunjo.
  Mbunge wa Viti Maalum kupitia chama cha NCR-Mageuzi,Corona Kundi akizungumza na watoto.


  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Emmanuel Kalobelo akipokea nyaraka  kama ishara ya kukabidhiwa rasmi ofisi kutoka kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Inj. Ngossy Mwihava, wakishuhudiwa na Katibu Mkuu, Inj. Mbogo Futakamba.


  Wizara ya Maji imemuaga rasmi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Inj. Ngossy Mwihava na kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu mpya, Inj. Emmanuel Kalobelo katika Makao Makuu ya Wizara hiyo Ubungo Maji jana.   “Naomba ushirikiano wenu ili tuweze kufanikisha azma ya kuleta maendeleo kwenye Sekta ya Maji, na nasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kujituma kwetu sote ili tulete faraja kwa wananchi”, alisema Naibu Katibu Mkuu, Inj. Emmanuel Kalobelo katika hafla fupi ya kutambulishwa na makabidhiano ya ofisi.

   Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Ngossy Mwihava akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Emmanuel Kalobelo ofisini kwake, kabla ya kumkabidhi ofisi.

   Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba (katikati), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Emmanuel Kalobelo (kushoto), aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Inj. Ngossy Mwihava (kulia) na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Gideon Manambo.

   Naibu Katibu Mkuu, Inj. Emmanuel Kalobelo akizungumza na Menejimenti ya Wizara ya Maji mara baada ya kutambulishwa.

   Menejimenti ya Wizara ya Maji ikimsikiliza Katibu Mkuu, Inj.  Mbogo Futakamba alipokuwa akizungumza.

  0 0

  Mchungaji wa kanisa la Umoja wa Makanisa ya Ubatizo Lucas Machibya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu baadhi ya shughuli za uraghabishi katika kijiji cha Pandagichiza. 
  Baadhi ya waraghabishi wa kijiji cha Pandagichiza wakiwa na waandishi wa habari za mtandaoni katika moja ya jengo la jiko la shule ya msingi Pandagichiza ambalo limetoakana na juhudi zao za uraghabishi 

  Na Krantz Mwantepele ,Shinyanga 

  Si mara nyingi viongozi wa kidini hujihusisha moja kwa moja na harakati za kisiasa ila wamekuwa mstari wa mbele kukemea matendo yanayofanywa na wanasiasa. Hawafanyi hivyo kwa bahati mbaya ila kutokana na nafasi yao katika jamii, hususani kuwaongoza waumini wao kwenda mbinguni. 

  Hata hivyo, hii haimaanishi hakuna kabisa viongozi wa dini waioamua kujiingiza katika harakati za siasa ili kuleta maendeleo ya watu kwa haraka na ufanisi. Mchungaji Lucas Machibya ni mmoja kati ya viongozi wachache wa dini wanaoingia katika siasa. 

  Huyu ni mchungaji wa kanisa la Umoja wa Makanisa ya Ubatizo lililopo katika kijiji cha Pandagichiza chenye wakazi wanaokadiriwa 2,481, idadi kubwa ikiwa ni ya wanawake wanaokadiriwa kufikia 1,476. Hiki ni moja ya vijiji vilivyopo wilaya ya Shinyanga Vijijini, jimbo la Solwa.

  Machibya ni mmoja wa wachungaji waraghbishi toka mkoa wa Shinyanga ambao uraghbishi wao umepelekea wananchi kumchagua kuwa mwenyekiti wa kijiji. Kujibainisha kwake kama mtu mwenye uwezo wa kusimamia anachokiamini na kushawishi wananchi kutambua majukumu na haki zao na jinsi ya kuzidai vimekuwa nguzo yake kubwa ya kukubalika.


  0 0
 • 01/05/16--01:25: DONDOO ZA MAGAZETI

 • 0 0  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  OFISI YA RAIS
  TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA - TAMISEMI

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb) kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 2(2) cha Amri ya kuanzisha Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), (The Executive Agencies) (The Dar Rapid Transit Agency) (Establishment) Order ) Tangazo la Serikali  namba 120 la 2007, amemteuaMhandisi Ronald Lwakatare kuwa Kaimu Mtendaji Mkuuwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es salaam (DART) kuanzia tarehe 04/01/2016.

  Uteuzi huo unafuatia kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu Bibi Asteria L. Mlambo tarehe 23/12/2015. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Ronald Lwakatare alikuwa Naibu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) akishughulikia Ufuatiliaji na Tathmini. Mhandisi Lwakatare anatakiwa kuripoti na kuanza kazi mara moja.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Januari 05, 2016

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa kikao chake na watumishi hao kilichofanyika jana alasiri..
  Katibu Mkuu mteule Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurian Ndumbaro (kushoto) akipokea Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma (Standing Order) kutoka kwa aliyekuwa akishika nafasi hiyo Katibu Mkuu, Bw. HAB Mkwizu (kulia). Anayeshuhudia ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Tixon Nzunda. 
   Watumishi wa Ofisi ya Rais – Utumishi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Mhe. Waziri na watumishi wa ofisi hiyo kilichofanyika jana alasiri.


  0 0

  IMG-20160105-WA0026

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mama aliyejifungua kwenye wodi ya wazazi hospitali teule ya rufaa ya mkoa wa Geita.(Picha Zote na Catherine Sungura WAMJW-GEITA).
  IMG-20160105-WA0030
  Wauguzi wa wodi ya akinamama katika hospitali teule ya mkoa wa Geita.
  IMG-20160105-WA0029
  Tabibu wa kituo cha afya Nyankumbu, Abdallah Kiroboto akimsikiliza Waziri Ummy mara alipoingia kwenye chumba cha kutolea huduma, pembeni ni mama aliyefika kituoni hapo na watoto wake kupata matibabu.
  IMG-20160105-WA0031
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwlimu akisalimiana na wagonjwa kwenye kituo cha afya Nyankumbu mkoani Geita alipotembelea kituo hicho.
  IMG-20160105-WA0028
  Wagonjwa waliofika hospitalini hapo wakisubiri huduma kwenye hospitali hiyo.
  IMG-20160105-WA0027
  Mganga mfawidhi wa hospitali teule ya mkoa wa Geita, Dkt. Adam Sijaona (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu mara baada ya kutembelea hospitali hiyo.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Prof Faustine Kamuzora wa pili kulia akipokea nyaraka wakati wa makabidhiano ya ofisi kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Dkt Yamungu Kayandabila wa kwanza kutoka kulia.

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya Mawasiliano Mary Sassabo kulia wakati akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Faustine Kamuzora ( hayupo pichani) na kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na rasilimali watu Bi Selina Lyimo.

   Baadhi ya Watumishi  wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika Sekta ya Mawasiliano wakimsikiliza Katibu Mkuu wao  mpya Prof. Faustine Kamuzora hayupo pichani. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya Mawasiliano Prof. Faustine Kamuzora akizungumza na manajimenti ya sekta ya Mawasiliano (hawapo pichani).


  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na kampuni ya Mtibwa Sugar Estates Ltd.   Profesa Muhongo aliitaka kampuni hiyo  kuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme ili kukidhi mahitaji yake zaidi.

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini -  Madini,  Prof. James Mdoe (kushoto) na Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini – Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Palangyo (kulia) wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtibwa Sugar Estates Ltd, Nassor Seif (hayupo pichani)

   Mkurugenzi Mtendaji wa Mtibwa Sugar Estates Ltd, Nassor Seif akielezea shughuli zinazofanywa na kampuni ya Mtibwa Sugar Estate Ltd.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba akisisitiza jambo katika kikao hicho.
  0 0  Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt, Harrison Mwakyembe (kulia) akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Sheria ikiwemo majumuisho ya ziara yake aliyoifanya hivi karibuni. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome pamoja na Naibu Katibu Mkuu wake Bwana Amon Mpanju, leo 5 Januari, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi wa mashtaka Biswalo Mganga akieleza mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) moja ya kazi walizozifanya ikiwemo kuwashataki waliopatikana na hatia ya madawa ya kulevya pamoja na uchomaji wa moto madawa hayo yaliyokamatwa kwa mwaka uliopita wa 2015 wakati walipokutana na Waandishi wa Habari leo 5 Januari, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa toka Waziri wa Katiba na Sheria pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka (hawapo pichani) leo 5 Januari, 2016 Jijini Dar es Salaam.   0 0

  MAKAMU wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu, leo Januari 5, 2016 amezindua miradi ya maendeleo katika mkoa wa Geita iliyofadhiliwa na mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania.

  Mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya Tshs 12Billion uliojengwa kwa ushirikiano kati ya Mgodi na serikali ambao utapunguza tatizo la maji safi na salama kwa mkoa wa Geita kwa zaidi ya asilimia 35% umezinduliwa, ambapo kwa mara ya kwanza, wananchi wa Geita wataweza kunywa maji safi na salama kutoka Ziwa Zictoria.

  Tatizo la maji lilikuwa ni kero kubwa kwa wakazi wa Geita kwa miaka mingi ambapo kina mama na watoto wa kike wamekuwa ndio wakiathirika wakubwa kwa kutembea umbali mrefu ili kupata maji safi kwa matumizi ya nyumbani.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Makamu wa Rais alisema “Serikali ya awamu ya tano imekusudia kuleta maendeleo ya kasi kwa Wananchi kwa kushirikiana na wadau mablimbali wa maendeleo kama inavyodhihirika katika mradi huu”

  Makamu wa Rais aliweza pia kutembelea na kuzindua muendelezo wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita ambayo ilijengwa mwaka 1957. GGM imeweza kutoa ufadhili wa ukarabati wa majengo hayo kwa thamani ya zaidi ya shilingi 800 Milioni ambapo ukarabati umekwenda sambamba na utoaji wa vifaa adimu kwa ajili ya vipimo na matibabu ya moyo, meno nk. Hospitali hii teule inahudumia zaidi ya wagonjwa milioni 1.7 kwa mwezi.

  “Ni kusudio la GGM kuona kuwa jamii inayotuzunguka inakuwa katika hali nzuri na bora kuliko hapo mwanzo kwa kuwepo kwetu hapa Tanzania. Hii ni sehemu ya kutimiza dhamira yetu hii na tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wake thabiti na kwa kuweka mazingira mazuri ya utendaji” alisema Mkurugenzi Mkuu wa GGM, Terry Mulpeter.

  Miradi mingine aliyoweza kutembelea na kuzindua ni mradi wa ushonaji na kutarizi ulio chini ya mradi mkubwa wa kuendeleza uchumi kwa Wananchi wa Geita uitwao Geita Economic Development Program (GEDP) ambao unahusisha miradi ya kilimo cha Mpunga na Alizeti, Kufyatua Matofali ya Interlocking blocks na Uchomeleaji utakaoweza kuleta ajira zaidi ya 300 kwa vijana wa mkoa wa Geita.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea moja vifaa tiba vilivyokabidhiwa hospitalini hapo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM), Terry Mulpeter, ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwa jamii ya watu wa Geita, leo Januari 5, 2016. wengine pichani toka kulia ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mh. Suleiman Jaffo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mh. Fatma Mwassa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita, Dkt. Joseph Kisala, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na Mganga Mfawidhi wa Hospitali teule ya Mkoa wa Geita, Dkt. Adam Sijaona.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, GEITA.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM), Terry Mulpeter, tuzo ya maalum ya kutambua Mchango wa Kampuni hiyo, kwa kujitoa kwake kuisaidia jamii ya watu wa Geita.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimtishwa ndoo ya maji, Bi. Tatu Salum, Mkazi wa kijiji cha Nyankubi Mkoani Geita, mara baada ya kuuzindua mradi mkubwa wa Maji Mkoani humo leo. Nyuma yake ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mh. Gerson Lwenge.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  IMG_0903
  Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto) akitoa maelezo ya uwezo mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibuni ambayo hadi kufikia Januari 4, 2016 ikiwa na muda wa siku tatu tangu kuanza kutumika hospitalini hapo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla.
  IMG_0910
  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru baada ya kuona mabadiliko makubwa katika hospitali hiyo tangu alipokaimu kiti hicho wakati wa zaiara ya kushtukiza katika chumba kilichofungwa mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibu na inauwezo mkubwa wa kufanya kipimo kwa sekunde 6 na kutoa majibu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare.

  IMG_0873
  Baadhi ya watumishi katika kitengo cha vipimo cha MRI wakiandaa kitanda kwa ajili ya kumpokea mgonjwa wa kipimo cha MRI (hayupo pichani) kama walivyokutwa na mpiga picha wa wetu.
  IMG_0924
  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwa kwenye dirisha la malipo ya matibabu hospitalini hapo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya, Januari 4, 2016.
  IMG_0930
  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla aliyetembelea kitengo chake, Januari 4, 2016. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru.


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea Hati za Utambulisho za Mhe. Song Geum-young, Balozi wa Jamhuri ya Korea Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 5, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Mhe. Song Geum-young, Balozi wa Jamhuri ya Korea Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 5, 2016 baada ya kupokea hati zake za utambulisho
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini Mhe. Roeland Van de Greer  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 5, 2016
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini Mhe. Roeland Van de Greer  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 5, 2016 baada ya kupokea hati zake za utambulisho
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Palestina hapa nchini Mhe. Hazem M. Shabat Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 5, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli baada ya kupokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Palestina hapa nchini Mhe. Hazem M. Shabat alifanya naye mazungumzo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 5, 2016.PICHA NA IKULU.


  0 0


  0 0

  Usimshauri  mtu  kuhusika  katika  kitendo chochote  ambacho  kinakatazwa  na  sheria. Kufanya  hivyo  kutakufanya  nawe  kuhesabika  umehusika katika  kosa  hilo. Hii  ni  hata  katika  mambo  ya  kawaida  tuliyozea.  
  Ukimsikia  mtu  anapanga  kwenda  kumkomesha  fulani kwa  kumpa  kipigo  usitie  neno  lako labda  kama  unamzuia. Usijaribu  hata  kusema  nenda  kamfanyie  amezidi.  Maneno  hayo  ni  machache  lakini  kisheria  yatachukuliwa  kama  ushauri  kwa mtenda  kosa.
  Au  mtu  anakwambia  nakwenda  kumpa  vidonge  vyake  kwa  maana  ya  kumtukana na  kumdhalilisha  na  wewe  unasisitiza kwa  kumwambia  ndio kampe  maana  amezidi, utakuwa  nawe  umeingia  kwenye  kosa  bila  kujali  ulienda  huko  lilikotokea  tukio au  haukwenda . Hizi  ni  jinai  za  kila  siku  ambazo  watu  hujikuta  wameingia  bila  kujua  na  wakifikishwa  vituo vya polisi  huanza  kulaumu kuwa  wameonewa kwa kuamini hawakutenda. Jihadhari. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Shamba la kapunga lililokuwa na Mgogoro wa zaidi ya Miaka kumi ambalo kwa sasa limerudishwa kwa wananchi kutoka kwa Muwekezaji.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwarudishia wananchi shamba la Hekta 1,870 kutoka kwa Muwekezaji wa kampuni ya Export Trading Company kijiji cha Kapunga Wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro na Katikati ni Muwekezaji Mahesh Patel.
  Wananchi wa Kapunga wakiwa katika mkutano ulioitishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa kuwatangazia urejeshwaji wa Hekta 1,870 kutoka kwa Muwekezaji.
  Picha na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ardhi.

  0 0

  ​Multiple award-winning group Sauti Sol release the music video of RELAX, the seventh single off their new album: Live and Die in Afrika (released Nov 21st 2015). RELAX is a bona fide feel-good track and a dedication to all Sauti Sol fans, and music fans worldwide. 

  The video of RELAX features behind the scenes video clips of the group's 2015 shows, tours and events, summing up what was a successful year for Sauti Sol. From Rwanda to USA, they include Sauti Sol’s debut at Kigali Up Festival, Global Citizen Festival, Sauti SaSol Road to BET American Tour that also saw them attend BET Awards as nominees Best International Act - Africa, among others.
  RELAX has been written and produced by Sauti Sol. Executive Production: Sauti Sol Entertainment. Video produced and directed by Michael Rainin (RAINPIX)Edited by Joseph Remerowski (Pictures in a Row). Executive Production: Sauti Sol Entertainment
   

  Sauti Sol’s third album: Live and Die in Afrika was added in BBC Africa’s Top 10 tracks of 2015 and Okayafrica’s Top 15 Albums of 2015. They were also listed as Billboard Africa’s Most Promising Music Group, The Standard Newspaper’s 2016 Agenda Setters and DRUM Magazine East Africa's 2015 Movers and Shakers. 
  In 2015, Sauti Sol dance with Presidents Barack Obama and Uhuru Kenyatta at a State House dinner went viral. They are now the only African music group whose picture with Obama has been placed in White House Oval Office.

  The 2014 MTV Europe Awards (EMA) Winners also won several awards in 2015 including Best Song “Sura Yako” in East Africa at Kilimanjaro Awards (Tanzania), Most Downloaded Group at Mdundo Awards and Best Video in Kenya “Sura Yako” at 2015 Bingwa Music Awards (Kenya) and Best Group in Africa at AFRIMMA Awards (America) and AFRIMA Awards (Nigeria).

  The physical copies Sauti Sol third album Live and Die in Afrika is available for sale at Nakumatt Store and the below online platforms:

  iTunes: Smarturl.it/LiveAndDieInAfrika 


  For more: #SautiSolRelaxVideo #LiveandDieinAfrika #SolGeneration

  0 0

  IMG_0900
  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akipata maelezo ya mashine mpya ya CT Scan iliyonunuliwa hivi karibu na Serikali kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru.
  IMG_0903
  Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto) akitoa maelezo ya uwezo mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibuni ambayo hadi kufikia Januari 4, 2016 ikiwa na muda wa siku tatu tangu kuanza kutumika hospitalini hapo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla.
  IMG_0910
  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru baada ya kuona mabadiliko makubwa katika hospitali hiyo tangu alipokaimu kiti hicho wakati wa zaiara ya kushtukiza katika chumba kilichofungwa mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibu na inauwezo mkubwa wa kufanya kipimo kwa sekunde 6 na kutoa majibu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare.

older | 1 | .... | 1079 | 1080 | (Page 1081) | 1082 | 1083 | .... | 3272 | newer