Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1080 | 1081 | (Page 1082) | 1083 | 1084 | .... | 3282 | newer

  0 0


  Shirika la ndege la bei nafuu lapanua wigo wa safari zake barani Afrika na kufungua safari ya kimataifa ya moja kwa moja kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam na Kilimanjaro.

   Kampuni ya Fastjet imetangaza safari yake mpya ya kimataifa ya kutoka Dar es Salaam kwenda Nairobi, Kenya kuwa itaanza rasmi mnamo tarehe 11 Januari 2016.
  Fastjet imepewa ruhusa na serikali ya Kenya kufanya safari zake nchini humo kufuatia makubaliano ya pamoja na mashirika yanayotoa huduma za usafiri wa anga kati ya nchi hizi mbili za Tanzania na Kenya, kama ilivyopitishwa na serikali ya Tanzania.
  Vilevile Fastjet imetangaza kuwa inatarajia kuzindua safari zake za anga kati ya Zanzibar na Nairobi na pia kati ya Dar es Salaam na Mombasa ambapo uzinduzi huo utafanyika mapema mwaka huu 2016.
  Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

  TAARIFA KWA UMMA


  Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali anakusudia kuyachukulia hatua Mashirika yanayoendesha shughuli zao kinyume cha Sheria ya NGOs Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005. 

  Mashirika hayo ni yale ambayo hayajawasilisha taarifa za mwaka kwa kipindi cha miaka miwili pasipo kutoa sababu za msingi, kulipa ada ya mwaka au kuendesha shughuli za NGOs bila kusajiliwa chini ya Sheria ya NGOs.
  Kwa taarifa hii, Mashirika husika yanatakiwa yawe yamerekebisha dosari tajwa ndani ya siku thelathini (30) kuanzia tarehe ya tangazo hili. Baada ya kipindi hicho, Msajili wa NGOs atayafutia usajili Mashirika ambayo yatakuwa hayajawasilisha taarifa na kuyachukulia hatua stahiki Mashirika yanayoendesha shughuli za NGOs bila ya usajili chini ya Sheria husika.

  Malipo yote ya ada yafanyike kupitia Benki ya NMB, NGO Account Na. 20110014074 na stakabadhi halali ya malipo itumwe kwa Msajili wa NGOs.


                                                        Imetolewa na:


  M.S. Katemba

  MSAJILI WA NGOs

  WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, 
  JINSIA, WAZEE NA WATOTO

   06 Januari, 2015

  0 0


  0 0

   Washiriki wa Mafunzo hayo wakisikiliza kwa Makini Mafunzo hayo..

  Awamu ya Tatu ya Mafunzo ya Ujarisiamali kwa Mkoa wa Dar es salaam yameanza leo. Wanawake 35 wa jiji la Dar es salaam Watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanayoendeshwa na mtaalamu wa mambo ya Biashara Bw Felix Maganjila na Shekha Nasser. Mafunzo haya yenye lengo la kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukossefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo
   Mafunzo haya yamegawanywa katika awamu mbili ili kumsaidia mjasiriamali wa kike kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya Biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika Mpangilio wa Biashara ikiwemo Matumizi sahihi ya Rasilimali Muda, Fedha, Muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na Biashara yake.
   Awamu ya Pili mshiriki anafundishwa Matumizi sahihi ya Vipodozi kuendana na wakati, mfano office makeup, day, evening na namna ya kumpamba bi Harusi. Pia wanafundishwa namna bora ya kutumia Vipodozi vya LuvTouch Manjano kwa lengo ya kuwa kila mshiriki atakayehitimu mafunzo haya aweze kujiajiri na kujitegemea kwa kuendesha maisha yake ya kila siku kwa kuwapambamba watu wenye Shuguli Mbalimbali
   Pamoja na mafunzo, kila mshiriki anaunganishwana Mwanamke mmoja mwenye mafanikio katika biashara au uongozi katika jamii kwa Lengo la kumuongoza katika safari yake ya biashara kwa muda wa mwaka mzima. Baada ya Wanawake hawa kuhitimu Mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa Mikopo kwajili ya kuwawezesha Kuanzisha Biashara wakiwa chini ya Uangalizi Maalum wa taasisi hiyo kwa Lengo la Kuhakikisha kila Mhitimu wa Mafunzo haya anapiga hatua na kuweza Kujitegemea.

  0 0

  Na Teresia Mhagama, Geita

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani ametoa siku 14 kwa mgodi wa dhahabu wa Buckreef kuanza uzalishaji ama sivyo wataandikiwa hati ya makosa na Afisa Madini Mkazi katika mkoa wa Geita. Naibu Waziri alitoa agizo hilo baada ya kufika katika mgodi huo uliopo katika kata ya Lwamgasa mkoani Geita na kuona hakuna shughuli zozote za uzalishaji zinazoendelea.

  “Najua kuwa hamjazalisha dhahabu mpaka sasa, lakini lazima mzalishe ili kulipa kodi na mrabaha, bila kufanya hivyo ndani ya siku 14 zijazo mtaandikiwa hati ya makosa kama sheria ya madini ya mwaka 2010 inavyoelekeza, mgodi huu mnaumiliki toka mwaka 2011, lazima muanze uzalishaji,” alisema Kalemani.

  Aidha Naibu Waziri alisema kuwa mgodi huo umechukua maeneo makubwa ya uchimbaji madini lakini hawayatumii, hivyo wayaainishe maeneo wanayohitaji kutumia na mengine wapewe wachimbaji wadogo.

  Akijibu suala la ugawaji wa maeneo kwa wachimbaji wadogo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzam2000 inayomiliki mgodi huo kwa ubia na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Joseph Kahama alisema kuwa wako tayari kukaa na Ofisi ya Madini mkoani Geita na STAMICO ili kuainisha maeneo watakayowaachia wachimbaji wadogo.

  Kutokana na hilo Naibu Waziri alimwagiza Afisa Madini Mkazi mkoa wa Geita, Mhandisi Laurian Rwebembera kukaa na watendaji wa mgodi huo tarehe 10 mwezi huu ili kuainisha maeneo hayo na kisha wayagawe kwa wachimbaji wadogo.

  Awali akizungumza na wachimbaji wadogo katika kijiji cha Lwamgasa, Dkt. Kalemani aliwaeleza kuwa serikali imeongeza kiwago cha utoaji wa ruzuku kutoka Dola za Marekani 50,000 hadi Dola Laki Moja kwa kikundi na kuwaasa wachimbaji hao kujiunga katika vikundi ili kuweza kuwa na sifa ya kupata ruzuku hizo.

  “Tunataka ruzuku hizi ziwafaidishe wananchi wengi lakini si mtu mmoja mmoja, ruzuku iwasaidie katika shughuli za uchimbaji madini ikiwemo kununua vifaa vya uchimbaji lakini na ninyi lazima mlipe kodi,” alisema Naibu Waziri.

  Awali Mkuu wa mkoa wa Geita, Fatma Mwasa alimweleza Naibu Waziri kuwa maeneo yanayotengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo ni vyema yakawa yanafanyiwa utafiti ili kuhakikisha kama yana madini na hivyo kuepusha wachimbaji hao kuwekeza katika maeneo yasiyo na madini.

  Vilevile alisema kuwa maeneo yanayotengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo yagawiwe kwanza kwa wachimbaji wasio na vitalu ili ili kuepusha suala la mtu mmoja kumilikishwa vitalu vingi wakati wengine hawana.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kalemani (mwenye suti) akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini katika kijiji cha Lwamgasa mkoani Geita wakati alipowatembelea wachimbaji hao ili kutatua changamoto wanazokabiliana nazo katika shughuli za uchimbaji madini.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (mwenye suti) akiwa katika eneo la mgodi wa dhahabu wa Buckreef mkoani Geita wakati alipotembelea mgodi huo na kukuta shughuli za uzalishaji madini zimesimama.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kalemani (wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya wananchi katika kijiji cha Lwamgasa mkoani Geita wakati alipofika kijijini hapo ili kutatua changamoto wanazokabiliana nazo katika sekta za Nishati na Madini.Wa kwanza kushoto ni Afisa Madini Mkazi mkoa wa Geita, Mhandisi Laurian Rwebembera.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kalemani (wa tatu kulia) akiwa na watendaji mbalimbali wa kijiji cha Lwamgasa mkoani Geita wakati alipofika kijijini hapo ili kutatua changamoto wanazokabiliana nazo katika sekta za Nishati na Madini.Wa kwanza kulia ni Afisa Madini Mkazi mkoa wa Geita, Mhandisi Laurian Rwebembera.

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kusindika  tumbaku  cha mkoani Ruvuma na kuwasimamisha kazi viongozi wa Chama Cha Kikuu Cha Ushirika cha SONAMCU.

  Akizungumza  jana jioni(Jumanne, Januari 5, 2016), katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Ndogo ya Songea, wakati alipokutana na wakulima wa zao la tumbaku wa Wilaya ya Namtumbo, Wananchama wa Vyama Vya Ushirika vya Mkoa wa Ruvuma, viongozi wa Mkoa pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini.

  Waziri Mkuu amesema, Serikali ina dhamira ya kufufua kiwanda cha kusindika tumbaku cha SONAMCU, na lengo la kutembelea kiwanda hicho ni katika utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufufua viwanda nchini.

  Waziri Mkuu Majaliwa, ametembelea maeneno mbalimbali ya kiwanda hicho na kukagua mitambo iliyokua ikitumika kusindika tumbaku, kabla kiwanda hicho kuzimwa miaka kadhaa iliyopita  baada ya kukosa malighafi za kuendelea na uzalishaji.

  Pia, amemtaka Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bibi. Stela Lugongo kuandaa na kuwasilisha kwake mkakati wa kufufua kiwanda hicho cha kusindika tumbaku, na baadae kuwasimamisha kazi viongozi wote wa Chama Kikuu cha Ushirika cha SONAMCU waliohusika na tuhuma hizo na kutaka wafikishwe Mahakamani.

  “Serikali imeazimia kufufua viwanda, hasa vile ambavyo havina wawekezaji vimebaki vyenyewe, Tunahitaji kujua namna ya kuvifufua”. Alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.

  Waziri Mkuu Majaliwa pia, amesikiliza  na kujibu kero mbalimbali za wakulima wa tumbaku wa Mkoa huo, ambao walilalamikia  mfumo wa Vyama vya Ushirika na namna ambavyo vyama hivi vimekua vikiwaibia fedha zao  hadi kushindwa kuendelea kulima zao la tumbaku na kukosa masoko ya mazao yao.

  Aidha, Waziri Mkuu amewasihi wakulima kuwa watulivu na kusubiri maamuzi ya Mahakama baada ya kuwa viongozi wa Chama cha Ushirika SONAMCU ambao wamehusika na wizi wa fedha za wakulima kiashi cha Shilingi milioni 800 kwa kipindi cha mwaka 2011 hadi 2014 tayari wamefikishwa Mahakamani na uchunguzi unaendelea. Pia, amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu kukutana na wakulima hao ili kupatia ufumbuzi matatizo yao.

  Aidha, ametoa wito kwa wakulima kuendelea kulima zao la tumbaku kwa kuwa linaongeza pato la mtu mmoja mmoja, linasaidia kuchangia pato la Mkoa na kukua kwa uchumi wa nchi. Amewashauri wakulima kuunda  na kuviendesha Vyama Vya Ushirika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

  Waziri Mkuu amemaliza ziara yake mkoani Ruvuma, atafanya majumuisho ya ziara hiyo leo, kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kurejea jijini Dar es Salaam.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P 3021,
  11410 DAR ES SALAAM

  JUMMATANO, JANUARI 6, 2016.

  0 0

    mwi5
  Waziri wa Kilimo Mifugo na Ushirika Mh. Mwigulu Nchemba  akipokelewa katika  ofisi ya Mkuu wa Iringa na kupokelewa na  Mkuu wa Mkoa Mh. Amina Masenza na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela.
  mwi3
  Waziri wa kilimo Mh Mwigulu Nchemba leo amesikiliza malalamiko ya wakulima wa Tumbaku na kuwahakikishia zao la tumbaku halitakufa kwani linaleta pato kwa taifa. Waziri wa kilimo Mh Mwigulu Nchemba leo amesikiliza malalamiko ya wakulima wa Tumbaku na kuwahakikishia zao la tumbaku halitakufa kwani linaleta pato kwa taifa. 

  wakulima wamelalamika sana uchelewashwaji wa pembejeo, bei duni ikiwemo madaraja mengi ya mfano kuna madaraja zaidi 72 ya grade za tumbaku kitu ambacho wakulima wamesema inawaumiza sana kwenye bei. 
   
  Pia wakulima wamelalamika ubadhirifu wa chama cha mtandao (Union) kiitwacho ITCOJE. Katika ziara hiyo Mh waziri aliambatana na Mrajisi wa vyama vya ushirika Dr. Rutabanzibwa na Mkurugenzi wa bodi ya Tumbaku Bwana Mushi. Mh. waziri ameagiza matatizo mengi yawe yametattuliwa kabla kikao cha bunge hakijaanza.
   
  Mh. Mwigulu aliwasili kwanza ofisi ya Mkuu wa mkoa na kupokewa na Mkuu wa Mkoa Mh Amina Masenza na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela. Mh Masenza alimpa taarrifa fupi ya hali ya Kilimo katika mkoa wa IRINGA.
  mwi4
  Wajumbe mbalimbali wa mkutano huo wakiwa katika mkutano
  mwi2

  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Ushirika akisalimiana na wajumbe mbalimbali wa mkutano huo.

  0 0

   Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Eng Stella Manyanya akizungumza na washiriki wa mafunzo ya Walimu Wawezeshaji wa masomo ya Hisabati, Kiingereza na Kiswahili kutoka shule za msingi katika Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma  na Halmashauri ya Ludewa Mkoa Njombe.
   Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Eng Stella Manyanya akishiriki katika darasa mojawapo la mafunzo ya Walimu Wawezeshaji wa masomo ya Hisabati, Kiingereza na Kiswahili kutoka shule za msingi katika Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma  na Halmashauri ya Ludewa Mkoani Njombe.


  Afisa wa Kitengo cha Ufatiliaji cha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Lawrence Sanga akitoa taarifa fupi juu ya mafunzo ya walimu wawezeshaji yanayoendelea kufanyika katika vituo Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea, Shule Sekondari Mwangaza - Katavi na Shule ya Sekondari Mwenge - Singida

   Baadhi ya Washiriki wa mafunzo  ya Walimu Wawezeshaji wa Masomo ya Hisabati, Kiingereza na Kiswahili wakimsikiliza mgeni rasmi Mhe. Stella Manyanya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya  hayo mkoani Ruvuma

  0 0
 • 01/06/16--01:06: DONDOO ZA MAGAZETI

 • SIMU.TV:  Mbunge UKAWA azuia bomoa bomoa Dar, Basi laua 4 na kujeruhi 33. Pata dondoo za magazeti ya leo hapa.  https://youtu.be/d8XiGPe8RQ8 
  SIMU.TV:  Siku 60 tofauti ya Ikulu ya Kikwete na Magufuli, Dodoma wamuaga polisi aliyekufa maji na familia yake. Pata dondoo hizi hapa.   https://youtu.be/oh9E7-Vtk2M
   SIMU.TV:  Mawaziri wa JPM Watumbua majipu, Dkt. Mwakyembe ajilipua atoboa madhambi ya mahakimu, makarani, polisi na magereza.   https://youtu.be/-Xai70SMThE
  SIMU.TV:  TFF Yampeleka Samatta Nigeria, Chupu chupu Yanga na Azam ngoma droo, Pata dondoo za magazeti ya michezo hapa.https://youtu.be/rTT_jXBEQmM   
   SIMU.TV:  Pata habari za kina zilizopewa uzito na wahariri katika magazeti ya leo Januari 6.2015; https://youtu.be/-S0u9gjreLA

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDA-RT), Bw. David Mgwassa akifafanua jambo wakati wa majadiliano ya wadau juu mapendekezo ya nauli zitakazotumika na mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) jijini Dar es Salaam jana.  Majadiliano hayo yanaendelea.
  Wadau wa sekta ya usafiri wakiwa katika majadiliano ya mapendekezo ya nauli zitakazotumika baada ya kuanza kwa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) jana jijini Dar es Salaam.  Majadiliano ya mapendekezo hayo yaliyotolewa na kampuni ya UDA-RT bado yanaendelea. 


  Mamlaka ya Udhibi wa Usafiri wa Majini na Nchi kavu (SUMATRA) jana imewaomba  wakazi wa Jiji la Dar es Salaam  kupendekeza kwa maandishi ya nauli zitakazotumika katika Mradi wa Mabasi ya Yaendayo Haraka (BRT) wa jijini Dar es Salaam.Huduma  katika kipindi cha mpito zimepangwa kuanza Januari 10, mwaka huu.

  Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA,Bw. Gillird Ngewe, ametoa ombi hilo baada ya nauli zilizopendekezwa naKampuni ya UDA Rapid Transit (UDA-RT) kukataliwa na mkutano wa wadau wa usafiri uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini jana. UDA-RT itatoa huduma za kipindi cha mpito.

  “Tumeletewa mapendekezo haya ya nauli na UDA-RT na wote tumeyajadili na wengi wetu tunahitaji yafanyiwe kazi zaidi.  Tuleteeni mapendekezo yenu. Na sisi tunawaondoa wasiwasi kuwa mapendekezo ya nauli na maoni yenu tutavifanyia kazi,” aliahidi Bw Ngewe.

  Ameeleza kuwa  katika  kuamua suala la nauli SUMATRA haiwezi kuangalia tu mapendekezo ya waendeshaji wa mradi mabasi hayo, bali inazingatia pia maoni ya wadau, wananchi na hali halisi ya nchi, na kuahidi kwamba maoni na mapendekezo yote yatapewa uzito wakati wa kuamua nauli za kutumika.

  “Sisi ni wadhibiti  maoni yenu yatafanyiwa kazi na endeleni kujenga utamaduni wa kushiriki majadiliano kama ilivyo hivi leo;   hii itasaidia mamlaka kufanya kazi zake kwa urahisi na kwa maslahi ya nchi”, amesisitiza Bw.Ngewe.

  Amewahakikishia wananchi kuwa nauli zitakazopangwa ndizo tu zitakazotozwa na wenye mabasi na si vinginevyo.Bw Ngewe ametumia nafasi hiyo kuwataka wenye mabasi ya abiria kufuata sheria kwa kutoza nuali elekezi nchi nzima ili kujenga utamaduni wa kufanya biashara yenye maslahi kwa pande zote mbili.

  Mkurugenzi Mkuu wa UDA-RT,Bw. David Mgwassa, amesifu mchango wa wadau na kuahidi kuutumia katika kupendekeza nauli zenye maslahi kwa pande zote mbili.

  “Tunathamini maoni ya wadau na tunaomba pia mamlaka izingatie hali ya uendeshaji wa mabasi ili watumiaji na kampuni tuweze kufaidika na mradi mzima”, alisema,Bw. Mgwassa.

  Awali kampuni yake ilipendekeza nauli ya 1,200/- kutoka Kimara hadi Kivukoni na 700/- kutoka Mbezi hadi Kimara Tsh. 700 na 1,400/- kwa njia za mrisho  wa nji kuu.  Mapendekezo yote yalikataliwa na wadau katika mkutano wa jana.

  Katibu Mtendaji wa Baraza la Wakaji la SUMATURA (SUMMATRA Consumers’ Council),Dkt. Oscar Kikoyo, ameitaka mamlaka hiyo kuzingatia maoni ya wadau na nauli zinazotumika sasa ndizo zitumiwe na mradi wa BRT  ili kuwapunguzia wananchi mzigo.Amesema nauli zitozwe kwa kilometa au ukanda na amepinga wazo la nauli ya aina moja kwa barabara nzima.

  “Tunatambua kuwa huu ni uwekezaji mkubwa na kwa maoni umekuja kuboresha maisha ya wananchi. Kwa hiyo  nauli za mabasi hay zibaki ni hizi zilizopo”, amesema Dkt. Kikoyo.Wachangia wengine waliona nauli zilizopendekezwa na Kampuni ya UDA-RT ni kubwa mno.

  0 0  Vitambaa vya Kanga vilivyopendekezwa kwa ajili ya kutumika kama Vazi la Taifa.

  Vitambaa aina ya Vitenge vilivyopendekezwa kwa ajili yaVazi la Taifa


  Imetolewa na
  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

  0 0

   Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo kuhusuiana na mtandao huo kutanua huduama zake hadi kufikia asimimia 95 ya watazanzania. Wanaoshuhudia ni Naibu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Emanuel Malyeta (kushoto), na kulia kwake ni  mwanasheria wa kampuni hiyo,Christopher Masai.
  Naibu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Halotel, Emanuel Malyeta akifafanunua jambo kwa waandishi wa habari. Katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai kulia kwake ni  mwanasheria wa kampuni hiyo,Christopher Masai.
  Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai akimkabidhi zawadi mwandishi wa gazeti la the Guardian, Sylivester Domaso.

  Dar es Salaam, 5/1/2016: Kampuni mpya ya simu za mikononi, Halotel, leo imetangaza mpango wake wa kufikisha mtandao wa simu kwa asilimia 95 ya watanzania hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Wakiongozwa na kauli mbiu yao ya Pamoja katika Ubora, wanalenga kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na simu ya mkononi pamoja na kupata huduma ya mtandao kwa kila sehemu ya Tanzania, ambapo mpaka sasa imeshaunganisha mtandao wa simu kwa zaidi ya vijiji 1500 ambavyo havikuwa vimeunganishwa na huduma ya mtandao awali.

  Hadi sasa Halotel imeshawekeza zaidi ya dola bilioni 1 za kimarekani mpaka sasa kwa kutengeneza miundombinu na kuboresha mtandao wa mawasiliano, kampuni ya Halotel imefanikiwa kufikisha huduma za mtandao katika mikoa yote 26 nchini, pamoja na miji na vijiji, ikiwa ni zaidi ya asilimia 95% ya watanzania wote hivyo kuifanya kuwa kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini.

  Akizungumzia mipango ya kampuni yake kwa mwaka 2016, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Halotel, bwana Le Van Dai amesema kampuni yake itaendelea kupeleka mtandao katika vijiji vingine 1500 katika mwaka 2016 na kuweka mkazo wa hali ya juu katika mrejesho kwa wateja pamoja na kuboresha mtandao, huduma kwa wateja, huduma kwa jamii hali itakayopelekea mapinduzi katika sekta ya mawasiliano nchini.
  ‘Kampuni yetu itashirikiana na watanzania katika kuhakikisha inaleta maendeleo kwa watanzania, kama ambavyo kauli mbiu yetu ilivyo, Pamoja katika Ubora, ndivyo ambavyo tutaendelea kuwekeza hapa nchini hali itakayopelekea kukua haraka kwa kampuni yetu’ alisema Bwana Dai.
  Katika hatua nyingine Dai amewashukuru watanzania na serikali yao kwa mapokezi waliyoipa kampuni yao, na pia amewahakikishia kuwa Halotel itaendelea kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za nchi na wataendelea kushirikiana nao katika kusukuma maendeleo ya nchi.
  ‘Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa waliotupa, na kuelekea mwaka 2016, kampuni yetu itaendelea kukuza ubunifu, zawadi pamoja na huduma nyingine kwa wateja wetu’ alisema Dai.
  Kwa mwaka 2015 pekee, kampuni ya Halotel imelipa kodi ya zaidi ya dola milioni 27 za kimarekani, ambayo kati ya hiyo dola milioni 24 imetumika kulipa kodi uingizaji bidhaa na dola laki saba ni kodi inayohusuiana na rasrimali watu.
  Dai amesema pia kampuni yake imetengeneza zaidi ya ajira 1,500 za moja kwa moja na zaidi ya 20,000 za ajira zisizo za moja kwa moja, akisisitiza kuwa kampuni yake itahakikisha inafata sheria za ajira za Tanzania.
  Katika hatua nyingine, Dai alielezea masikitiko yake kwa matukio ya wizi na uporaji wa mitambo ya Halotel, akielezea kuwa zaidi ya matukio 52 yameripotiwa kuanzia mwezi wa kwanza hadi Disemba mwaka huu, ambapo imewasababishia hasara ya jumla ya shilingi milioni 393.Lengo la Halotel ni kuhakikisha kila mtanzania ana simu ya mkononi ili kubadilisha namna watanzania wanaishi na namna wanavyokuza na kujenga uchumi wao.
  ‘Kampuni yetu ina zaidi ya kilomita 18,000 za fibre optic, pamoja na zaidi ya minara 2500, hivyo kuifanya Halotel kuwa kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini, ambayo pia itatumika kuunganisha serikali za mitaa 150, hospitali 150, vituo vya polisi 150, ofisi za posta 65 na intaneti ya bure kwa shule zaidi ya 450’ alimaliza Dai. 

  0 0

   Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira,Mhe Anthony Mavunde (watatu toka kushoto) akikagua vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini vya mfanyakazi wa kigeni wa Vodacom Tanzania , Valentino Giron (kushoto),wakati alipofanya ziara ya kikazi Makoa makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni,Anayeshuhudia kulia ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu. 
   Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira,Mhe Anthony Mavunde(Kulia) akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakati alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni kwa ajili ya kujua kero na maendeleo mbalimbali ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
  Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira,Mhe Anthony Mavunde(Mwenye suti katikati)akimsikiliza  Mkuu wa kitengo cha rasilimali watu wa Vodacom Tanzania, Conrad  Msoma (kushoto) wakati alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni kwa ajili ya kujua kero na maendeleo mbalimbali ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

  0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kushoto akiongea na Balozi wa Norway nchini Tanzania Hanne-Marie Kaarstad wakati wa Kikao kilichofanyika Ofisini kwa Waziri,katika kikao hicho Norway iliahidi kuendelea kudumisha ushirikiano na Tanzania katika sekta ya utamaduni, Sanaa na Michezo. 

  Balozi wa Norway nchini Tanzania Hanne-Marie Kaarstad kulia akiongea na  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kushoto wakati wa Kikao kilichofanyika Ofisini kwa Waziri,katika kikao hicho Norway iliahidi kuendelea kudumisha ushirikiano na Tanzania katika sekta ya utamaduni, Sanaa na Michezo. (Picha na Benjamin Sawe-WHUSM).


  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


  Simu: 255-22-2114512, 2116898

  E-mail: press@ikulu.go.tz

  Tovuti : www.ikulu.go.tz              

  Faksi: 255-22-2113425


  OFISI YA RAIS,

        IKULU,

   1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  

  11400 DAR ES SALAAM.

  Tanzania.

   

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa Nchini IGP Ernest Mangu kufuatia kifo cha msaidizi wake Inspekta - Gerald Ryoba aliyepoteza maisha katika ajali ya kusombwa na mafuriko ya maji wakati akikatiza katika eneo la Kibaigwa, Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.


  Katika ajali hiyo iliyotokea 03 Januari, 2016 Inspekta Ryoba akiwa na Mkewe na watoto wake wawili, pamoja na watu wengine wawili walikua wakisafiri kutoka Geita kuja Jijini Dar es salaam na walipofika katika eneo la Bwawani gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji na wote sita kupoteza maisha.


  Rais Magufuli amempa pole nyingi Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa msiba huo mkubwa, na amemuomba amfikishie salamu za pole kwa familia ya Marehemu Ryoba na kueleza kwamba anaungana nayo katika kipindi hiki kigumu.


  "Nimesikitishwa sana na tukio hili la kuondokewa na msadizi wako pamoja na familia yake, ni tukio linalotia uchungu mkubwa" amesema Mheshimiwa Rais.Aidha, Rais Magufuli amemuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu na uvumilivu wafiwa wote, na aziweke roho za marehemu mahali pema peponi Amina.

  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dar es salaam


  06 Januari, 2016


  0 0

  Jumla ya shilingi trilioni 1.4 imekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015.

  Kiasi hicho ni sawa na ongezeko la wastani wa shilingi  bilioni 490 kwa mwezi ukulinganisha na wastani wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba ambapo ,TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa mwezi.

  Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA) Alphayo Kidata wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi nchini.

  Ameongeza kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi kufikia Desemba mwaka huo TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi trilioni 6.4 ambayo ilikuwa ni sawa na asilimia 95.5 ya lengo la kukusanya trilioni 6.5 katika kipindi hicho.

  Kaimu Kamishna huyo ametaja sababu za kuongeza kwa makusanyo ya kodi kuwa ni pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuweka mifumo mizuri ya ufuatiliaji ili kumrahisishia mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu.

  Kidata amesema kuwa katika kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano ya kuongeza mapato Mamlaka hiyo itasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato na kuwabana wote wenye nia ya kukwepa na hatimaye kuwafikisha katika vyombo vya sheria watakaobainika wamekwepa kodi.
   
  Katika hatua nyingine Kaimu Kamishina Mkuu wa TRA huyo amesema jumla ya shillingi billioni 11.8zimekusanywa kutoka kwa wafanyabiashara walioondosha makasha katika Bandari Kavu kinyume na taratibu za forodha.

  Amesema kuwa makusanyo hayo yanajumuisha shilingi bilioni 5.3 kuoka kwa Kampuni na wafanyabiashara 19 ambao wamemaliza kulipa kodi za makasha yao na wengine 19 ambao wamelipa sehemu ya kodi ya makasha yao

  Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO
  Dar es Salaam
  6.1.2016. 

  0 0

  MWANDISHI wa habari wa magazetila Uhuru,Mzalendo na Burudani mkoani Arusha Shaaban Mdoe amejitokeza kuwania nafasi ya ukatibu wenezi wa CCMmkoa wa Arusha katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mnamo Januari 28mwaka huu ili kuziba nafasi zilizo wazi kutokana na sababu mbalimbali.

  Mdoe ambaye amewahi kuwamjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Arusha na mjumbe wa kamati mbalimbali zamaadhimisho ya sherehe mbalimbali za chama amesema amejitokeza kuwania nafasihiyo kutokana na msukumo wa fani yake,uzoefu katika chama na kazi mbalimbali zachama kupitia taaluma yake ya habari.

  Akizungumza na gazeti hilialisema kutokana na nia yake hiyo
  kesho(leo)atachukua fomu ya kuwania nafasihiyo katika ofisi kuu ya CCM
  mkoa wa Arusha ambapo pia atapata nafasi ya kuelezamikakati yake pindi
  jina lake litakaporejeshwa na vikao mbalimbali vya chama.

  Alisema sasa wakati umefikawa chama kupata viongozi wake katika baadhi
  ya nafasi kulingana na taalumakwakua ni jambo la muhimu taalumu
  kuzingatiwa katika kushika nyadhfa hizokwakua itasaidia katika
  utendaji kazi wake na kuleta mafanikio.

  Alisema kupitia taalumayake ya habari ameweza kufanya mambo mengi
  ikiwemo kuwaunganisha waandishi wahabari na vyombo mbalimbali wa mkoa
  wa Arusha katika kukitangaza chama jamboambalo anaamini pindi
  atakapopewa ridhaa hiyo ataifanya kazi hiyo zaidi ya palealipofikia.
  Mdoe anaeongozwa na kaulimbiu yake kuwa “Mshale unarudi porini”
  akimaanisha nafasi ya uenezi inahitajitaaluma ya habari,mahusiano na
  utendaji kazi wa kazi hiyo wakati wote na sikuwa na taaluma pekee bila
  kuifanyia kazi.

  “unajua ile dhana ya zamaniya uenezi kuwa ni ya kupanda jukwaani na
  kutambulisha wageni imepitwa na wakatikinachohitajika kwasasa ni
  kupata kiongozi wa nafasi hii mwenye kutenda kazihiyo kila wakati
  kwani mimi ni mwandishi sizuiwi na kazi nyingine hivyo nikiwa
  katikaziara za kujenga chama pia niko katika ajira yangu”alisema
  Mdoe.

  Mbali na mdoe wenginewaliotajwa kuwania nafasi hiyo ni pamoja na
  aliyewahi kuwa mwenyekiti waChadema Monduli Amani Silanga,aliyekuwa
  katibu wa siasa na uenezi wilaya yaArusha Semi Kiondo na Ally Rajabu.
  Nafasi hiyo ya ueneziiliachwa wazi na Isack Joseph aliyejiunga Chadema
  ambapo chaguzi huo mdogo pia piaunajumuisha nafasi ya mwenyekiti wa
  CCM mkoa kufuatia aliyekuwa mwenyekitiOnesmo Nangole kukihama chama.

  Pia uchaguzi huo utafanyikakatika kiti cha uenyekiti wilaya ya Monduli
  kufuatia aliyekuwa mwenyekitikujiunga Chadema,mchumi na mjumbe wa
  halmashauri kuu ya taifa(NEC) wa wilaya hiyo kufuatia aliyekuwa Mnec
  Edward Lowasa kuhamia Chadema.

  NA WOINDE SHIZZA-ARUSHA.

  0 0

  Ubunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari akimsalimia moja wa watoto
  wanaouguzwa katika Hospitali ya Tengeru ,katika ziara yake alipofika
  kusikiliza matatizo yanawakumba wagonjwa haswa wakina mama waliolazwa katika hospitali ya tengeru alipofanya ziara ya ghafla hospitalin
  Ubunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari akimsalimia moja wa watoto
  wanaouguzwa katika Hospitali ya Tengeru ,katika ziara yake alipofika
  kusikiliza matatizo yanawakumba wagonjwa haswa wakina mama waliolazwa katika hospitali ya tengeru alipofanya ziara ya ghafla hospitalin
  Ubunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari Akisikiliza kero za wagonjwa
  wanaoitibiwa katika Hospitali ya Tengeru ,katika ziara yake alipofika
  kusikiliza matatizo yanawakumba wagonjwa haswa wakina mama waliolazwa katika hospitali ya tengeru alipofanya ziara ya ghafla hospitalin hapo

  0 0

   kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata akisisitiza jambo wakati alipofanya mazungumzo na waandishi wa habari kuhusu taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi Kushoto ni Kaimu Kamishna wa Forodha Jocktan Kyamuhanga na kulia  ni Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani Yusufu Salum .
   Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi.Picha Na raymond Mushumbusi MAELEZO

   Jumla ya shilingi trilioni 1.4 imekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015.

  Kiasi hicho ni sawa na ongezeko la wastani wa shilingi  bilioni 490 kwa mwezi ukulinganisha na wastani wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba ambapo ,TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa mwezi.

  Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA) Alphayo Kidata wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi nchini.

  Ameongeza kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi kufikia Desemba mwaka huo TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi trilioni 6.4 ambayo ilikuwa ni sawa na asilimia 95.5 ya lengo la kukusanya trilioni 6.5 katika kipindi hicho.

  Kaimu Kamishna huyo ametaja sababu za kuongeza kwa makusanyo ya kodi kuwa ni pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuweka mifumo mizuri ya ufuatiliaji ili kumrahisishia mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu.

  Kidata amesema kuwa katika kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano ya kuongeza mapato Mamlaka hiyo itasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato na kuwabana wote wenye nia ya kukwepa na hatimaye kuwafikisha katika vyombo vya sheria watakaobainika wamekwepa kodi.
  Katika hatua nyingine Kaimu Kamishina Mkuu wa TRA huyo amesema jumla ya shillingi billioni 11.8zimekusanywa kutoka kwa wafanyabiashara walioondosha makasha katika Bandari Kavu kinyume na taratibu za forodha.

  Amesema kuwa makusanyo hayo yanajumuisha shilingi bilioni 5.3 kuoka kwa Kampuni na wafanyabiashara 19 ambao wamemaliza kulipa kodi za makasha yao na wengine 19 ambao wamelipa sehemu ya kodi ya makasha yao

  Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO
  Dar es Salaam
  6.1.2016


  0 0

  MICHUANO ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa tatu inatarajiwa kuendelea Januari 12 na wikiendi ya Januari 23-27 kwa timu 32 kuchuana kuwania kufuzu kwa hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

  Timu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom zimeingia moja kwa moja mzunguko wa tatu ambapo sasa zinajumuika na timu 16 zilizofuzu kutoka raundi ya pili yenye timu kutoka ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili.

  Jumamosi, Januari 12, Majimaji itacheza dhidi ya JKT Mlale uwanja wa Majimaji mjini Songea, Januari 23 Pamba v Toto Africans uwanja wa CCM Kirumba, Ndanda FC v Mshikamano Nagwanda Sijaona Mtara, huku Burkinafaso wakiwakaribisha Simba SC katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

  Januari 24, Young Africans watacheza dhidi ya Friends Rangers uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Njombe Mji v Tanzania Prisons uwanja wa Amani Makambako, mjini Shinyanga Stand United watachuana dhidi ya Mwadui FC.

  Mechi zingine ni Kagera Sugar v Rhino Rangers, Panone v Madini, Mtibwa Sugar v Abajalo, Lipuli/Kurugenzi v JKT Ruvu, Ashanti United v Azam FC, Africa Sports v Coastal Union, Geita Gold v Mgambo Shooting, Singida United v Mvuvuma na Wenda v Mbeya City.

  Timu 15 zilizofuzu hatua ya tatu kutoka raundi ya pili ni Ashanti United, Friends Rangers, Panone, Geita Gold, Pamba, Mvuvuma, Burkinafaso, Rhino Rangers, Madini FC, JKT Mlale, Mshikamano FC, Njombe Mji, Wenda FC, Singida United, Abajalo huku mchezo mmoja kati ya Lipuli dhidi ya Kurugenzi ukichezwa leo hii kusaka timu ya kufuzu raundi ya tatu.

  Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.

older | 1 | .... | 1080 | 1081 | (Page 1082) | 1083 | 1084 | .... | 3282 | newer