Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1078 | 1079 | (Page 1080) | 1081 | 1082 | .... | 3282 | newer

  0 0


  Maafisa wa kitengo cha Mahusiano ya Jamii katikamgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, William Chungu (kulia) na Zuwena Senkondo (kushoto) wakikabidhi vifaa vinavyotumika wakati wakujifungulia kwa zahanati ya Mwingiro Wilayani Nyang’wale Mkoani Geita .

  Zuwena Senkondo wkikabidhi vifaa vya kujifungulia kwa mmoja wa wauguzi katika zahanati ya Mwingiro Wilayani Nyang’wale Mkoani Geita

  Kiongozi wa kitengo cha Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Sara Ezra Teri akikabidhi Video Camera ya kisas kwa Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana Thoams Mshilu kwa ajili ya kurekodia tamthiliya zao. 


  0 0

  Picha za mitambo ya kuzalisha umeme na  wadau wa maji waliotembelea maeneo ya mito na kugundua baadhi ya njia za asili za  mito inayomwaga maji yake kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme imezibwa.  kitendo hicho kinadaiwa kuathiri utiririshaji wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme.

   pia wadau hao wameshauri taasisi zote ikiwemo wizara ya nishati na madini,wizara ya kilimo , mifugo na uvuvi, wizara ya maji na umwagiliaji pamoja na bonde la mto Rufiji  zinazotumia rasilimali maji katika shughuli zake kushirikiana ili kumaliza tatizo la kukauka na kupungua kwa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme.
   Cable wire za Umeme zikipitishwa katika moja ya njia zililizopo chini ya  mwamba wa mlima( tannel) ambapo ndipo zilizopo mashine za kuzalisha umeme wa maji na shughuli zote za uzalishaji.

   Mashine  za kuzalisha umeme wa maji katika vituo vya Kihansi, kidato na Mtera  vinanyonekana ambapo shughuli zote za uzalisha wa umeme wa maji na mashine hizo ziko chini ya mwamba wa mlima uliotombelea . 
   Sehemu iliyochepushwa maji kitaalamu kutoka katika moja ya mito inayomwaga maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ili maji hayo  yatumike kwa kilimo cha umwagiliaji.

   Sehemu iliyochepushwa maji kitaalamu kutoka katika moja ya mito inayomwaga maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ili maji hayo  yatumike kwa kilimo cha umwagiliaji.

  Wataalam kutoka Wizara ya Nishati  na Madini , Wizara ya kilimo ,uvuvi na mifugo, Wizara ya maji na umwagiliaji pamoja na watalaam kutoka bonde la mto Rufiji wakipita eneo ambalo kumejengwa tuta ili kuzua njia ya asili ya moja ya mito inayomwaga maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji kwa nia ya kupisha ujenzi wa mfereji wa maji yatakayotumika katika kilimo cha umwagiliaji, jambo ambalo  limedaiwa kuwa huathiri mazingira na utiririshaji wa maji katika mabwawa.

  0 0  MAKATABA wenya thamani ya dola za kimarekani milioni $700m uliosainiwa na washirika wa ndege ya Etihad kwa ajili ya upanuzi wa shirika hilo umetambuliwa na shirika lenye sifa duniani katika nyanja ya masuala ya kifedha na uchumi la “International Financing Review (IFR)” na hivyo kuitunuku shirika la ndege la Etihad na tuzo maalum. 

  Mkataba huo wa miaka mitano ulitambulika kama dhamana kubwa kabisa ya mwaka iliyosainiwa kutoka barana ulaya, mashariki ya kati na Afrika, katika hafla iliyofanyika jijini London Januari 27

  Mwezi Septemba , shirika la ndege la ndege la Etihad lilianza safari ya maonyesho, likiongozwa na mshauri mkuu, Goldman Sachs, katika bidi za kuongeza thamani ya hisa za Shirika hilo, kampuni yake tanzu ya huduma za viwanja vya ndege ya Etihad na washirika wengina wake watano wa huduma za angani – airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia na Jet Airways – wote wakiwa ndani ya shirika la ndege la Etihad.

  Kupitia michango ya washirika wa ndege ya Etihad BV, kikundi kilifanikiwa kupata dola za kimarekani milioni 500, kiasi hicho kiliongezeka kwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 200 ndani ya siku chache tu kufuatia kuongezeka kwa shauku kutoka jamii ya fedha ya kimataifa.

  Ikiwa kama mkataba wakifedha wa kipekee katika sekta ya masuala ya anga, hii ni mara ya pili ndani ya wiki chache kwa shirika hili la ndege kutambulika na kupata tuzo kupitia mkataba wake huo. Washirika wa ndege la Etihad walipokea tuzo ya mkataba wa kifedha wa mwaka kutoka mashariki ya kati, katika hafla iliyofanyoka jijini London kupitia Makala ya Global Transport Finance ya nchini UK.

  James Hogan, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la Ndege la Etihad, alisema: “Uvumbuzi ndio msingi wa uendeshaji wa biashara zetu katika shirika hili. Tuzo hii kutoka “International Financing Review” inaonyesha dhahiri ni jinsi gani taasisi za kifedha zina uamini juu ya mafanikio yetu pamoja na mifumo yetu ya kibiashara katika kuunganisha biashara zetu zite tulizo wekeza” 

  Akiongezea Bw Hogan, alisema: “Katika sekta ya biashara yenye ushindani mkubwa, siri ni kukuza uzalishaji pamoja na kuongeza ufanisi ili kukuza biashara. Kwa upande wa wahirika, kila mmoja wao ni kujikuza kibiashara. Ila kwa pamoja, nguvu inajumuishwa kwa pamoja. Mfumo huu wa uelewano ndio unatambua na kuidhinisha nguvu ya shirika zima. 

  “Ningependa kumshukuru na kumpongeza afisa wetu mkuu wa masuala ya kifedha, Bw James Rigney, na timu yake nzima kwa juhudi zao za hali ya juu katika kuunda mfumo thabiti uliokuwa kivuto katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Walifanya kazi kwa bidii sana kuleta shauku kubwa juu ya mifumo yetu ya kibiashara na tunayo furaha kuona bidi zao zikizaa matunda na kupata tuzo hizi, hasahasa wakati huu ambapo masoko mengi duniani yamejaa mashaka na wasiswasi juu ya kuwekeza fedha kutokana na changamoto za kiuchumi duniani”. 

  Mkurugenzi mtendaji wa Goldman Sachs, Bw. Martin Weber, alisema: “ Tunafuraha kubwa kufanya kazi pamoja na washirika wa ndege ya Etihad katika kuwapatia dhamana hii kubwa na tunapongeza timu iliyohusika katika ushindi wa tuzo ya IFR. Mafanikio haya yanatokana na uongozi wa shirika la ndege la Etihad kukutana na wawekezaji mbalimbali dunia nzima, na hivyo kufanikisha kukamilisha mkataba huu. Hii pia ni ishara ya jinsi gani mfumo wao wa kibiashara ua nguvu ya kufurahisha masoko hata katika kipindi hichi kigumu cha masoko ya dunia” 

  Safari za kuchangia fedha zilifanyyika Abu Dhabi, Dubai na London zikiwa zinasimamiwa na washauri wakuu Goldman Sachs, kampuni kutoka Abu Dhabi ya ADS Securities na Anoa Capital. Fedha zilizopatikana ziligawanywa katika Nyanja saba tofauti, ikiwa mchanganyiko wa matumizi ya mtaji na uwekezaji katika ndege, pamoja na kujazia fedha kulingana na mahitaji ya vitengo mbalimbali vya shirika hili la ndege ya Etihad. 

  International Financing Review ndio chombo kinachoongoza duniani katika kutoa uchambuzi wa kina juu ya masoko, ikitoa ushauri na uchambuzi wa kina juu ya uwekezaji wa masuala ya kibenki kwa kauu wa benki duniani, pia hutoa habari juu ya masoko ya kibiashara kupitia Makala zake za kila wiki ma ripoti zao za kila siku mtandaoni

  Uongozi wa shirika la ndege la Etihad ulisifiwa na IFR kwa kukamilisha na kufanikisha uchangishaji fedha, huku wakijenga uaminifu na kuungwa mkono na wawekezaji. 

  Tukio hilo kubwa kabisa katika kalenda ya wawekezaji masoko wa dunia kila mwaka, litavutia wawekezaji wakubwa na wenye mafanikio zaidi ya 1,000 mwezi ujao jijini London ili kusherekea tuzo za IFA za kila mwaka.

  0 0

  Chumba cha habari cha GLOBU ya Jamii kimepata taarifa kuwa Basi la abiria  la kampuni ya Luwinzo (ambalo namba zake za usajili hazijafahimika mapema),lifanyalo safari zake Dar-Njombe inaelezwa kuwa limepata ajali asubuhi hii likitokea Njombe kuelekea Dar kwa kuligonga Lori (ambalo nalo namba zake za usajili hazikufahamika mapema), kwa taarifa za awali ambazo bado hazithibitishwa na jeshi la Polisi zinaeleza kuwa kuna vifo vya watu kadhaa,ambayo idadi yake haijajulikana mpaka sasa sambamba na majeruhi.

  TUTAZIDI KUPEANA TAARIFA ZAIDI KADIRI YA ZITAKAVYOKUWA ZIKIPATIKANA.
   Baadhi ya Abiri na Wasamalia wema wakisaidia kuwaokoa baadhi ya abria waliokuwa wamenasa ndani ya basi hilo.
   Baadhi ya abiria wakiwa kwenye masikitiko makubwa.
   Kazi ya kuokoa baadhi ya abiria ikiendelea  
  Namna basi hilo lilivyogonga Lori kwa nyuma.

  0 0  Challenges for the East African Community”.

  The 1stEast Africa Congress of Accountants (EACOA) will be held at  AICC Arusha – Tanzania from 2th to 4thMarch 2016.


  The objective of the conference is to create a forum for professional accountants in the region to interact, seek opportunities and to discuss issues impacting the accounting profession in the region.

  The conference is jointly organised by the Accounting Bodies in the Region: OPC Burundi; Institute of Certified Accountants Kenya (ICPAK); Institute of Certified Accountants of Rwanda (ICPAR); National Board of Accountants and Auditors –Tanzania (NBAA); Institute of Certified Accountants of Uganda (ICPAU).NBAA is the host of the conference.Members of the accountancy profession, academicians and all interested persons are invited to attend this important professional conference.

  Registration and Conference Fee
  Early registration start on 7th December,  2015 to 29th January 2016 conference fee is Tsh. 800,000 or USD 400.  Late registration is from 1st– 29th February 2016 conference fee  Tsh. 950,000 or USD 450.  The fee include 1 day trip to Ngoro Ngoro Crater.

  Register online through eacoa.nbaa-tz.org or download the form through www.nbaa-tz.org scan and send toeacoaregistration@nbaa-tz.org

   FOR MORE INFORMATION CLICK HERE www.nbaa-tz.org

  0 0  SIMU.TV:  ZECO kufunga LUKU taasisi zote za serikali. Jambazi hatari lanaswa Arusha.  Hukumu ya mahekalu Dar  Kesho; https://youtu.be/N8i_HdmIiSY
   SIMU.TV:  CHADEMA yavurugwa, Bulembo amshukia Lowassa. 15 kushitakiwa kwa ubadhilifu.  Zitto ampa jipu rais Magufuli;https://youtu.be/t-a9Dnf2b2k
   SIMU.TV:  TFF yambeba Niyonzima. Cheka kuzichapa na bingwa wa Ulaya.  Ajib kuziba pengo la Samatta TP Mazembe; https://youtu.be/exXCg2p0KaA
   SIMU.TV:  Afungwa miaka 60 kwa kuiba laki 3. Bomoabomoa yatumika kumhujumu rais Magufuli. Mwalimu arejesha fedha za wanafunzi; https://youtu.be/Yt0DzgdHeTU


  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefurahishwa na hali ya chakula mkoani Ruvuma, ikiwa kati ya mikoa inayotegemewa kwa uzalishaji wa chakula kwa wingi nchini.

  Akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali jana jioni (Jumapili, Januari 3, 2016) katika ukumbi uliopo Ikulu ndogo Songea, Waziri Mkuu  ameutaka  uongozi wa mkoa kuhakikisha kuna  upatikanaji wa masoko kwa mazao mbalimbali pamoja na kuendelea kutoa msukumo kwa wananchi.

  Pia, ameupongeza uongozi  wa mkoa huo kwa kutoa msukumo kwa wananchi na kufanyakazi, na kusema ni jambo linalosaidia kupanda kwa pato la mtu mmoja  mmoja, hata hivyo hakusita kuwashukuru kwa mapokezi makubwa aliyopata.

  “Nawapongeza sana wana Ruvuma kwa kuongeza pato la ndani kutoka kutoka shilingi 654,227, hadi kufikia shilingi 1,800,000 kwa kipindi cha mika 4 tuendelee kujiweka vizuri kwa kuongeza pato la mtu mmoja mmoja” alisema Waziri Mkuu.

  Waziri Mkuu Majaliwa pia amesisitiza  kilimo cha umwagiliaji katika maeneo yote yenye mabonde ili wakulima waweze kuvuna bila kutegemea sana kipindi cha masika. Amesema ni lazima kuimarisha huduma muhimu na kusisitiza matumizi mazuri ya fedha zinazopatikana katika mazao hayo.

  Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu amesema  zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wa Ruvuma hutegemea kilimo cha mazao  mbalimbali ya chakula na biashara  yakiwemo mahindi, mpunga ambao unalimwa sehemu za Tunduru na Songea vijijini, korosho  ambazo zinalimwa sehemu za Tunduru, Namtumbo, Nyasa, Mbinga na Songea vijijinina tumbaku  maeneo ya Namtumbo,Mbinga na Songea vijijini.

  Alisema, Ruvuma imekua ikizalisha chakula kwa kiwango cha utoshelezi na ziada kwa kipindi cha mwaka 2012 - 2013, 2013 - 2014 hali hiyo imeendelea kuwa nzuri hadi kipindi cha mwaka 2015 - 2016. Mahitaji yakiwa ni tani 469,172 na ziada ikiwa tani 1,950,111, ametaja baadhi ya sababu za ongezeko hilo la tani  ni pamoja na matumizi ya dhana  bora za kilimo, matumizi ya pembejeo za kisasa na urahisi wa upatikanaji wa pembejeo, aliongeza Mkuu wa Mkoa.

  Waziri Mkuu Majaliwa ambaye jana (Jumapili, Januari 3, 2016) ameanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma, kesho  siku ya jumatatu  atakuwa na shughuli za kufungua  tawi la Benki ya Posta mjini Songea, kukagua  maghala ya Wakala wa Taifa wa  Hifadhi ya chakula  (NFRA) kanda ya Songea na kukagua  Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

   Kupitia ziara hii Serikali ina lengo la kuona hali halisi ya utendaji wa shughuli za maendeleo kutoka kwa watendaji mbalimbali, kuwatia moyo na kuweka msisitizo  katika maeneo yaliyopewa kipaumbele hasa katika sekta ya Afya.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  JUMATATU, JANUARI 4, 2016.


  0 0

  Mtu mmoja Jijini Mbeya (PICHANI JUU) ambaye hakuweza kutambulika kwa Majina,inadaiwa amekutwa amefariki  leo asubuhi kwenye moja ya uchochoro  wa nyumba zilizopo katika mtaa wa Mwamfupe.

  Kifo cha Mtu huyo ambaye inaelezwa ni kijana wa makamo alikutwa amefariki kwenye uchochoro wa nymba hiyo mara baada ya kubainika na baadhi ya Wananchi,waliokuwa wakikatiza mtaa huo kuelekea mtaa mwingine,Baadhi ya Mashudhua wa eneo hilo wameeleza kuwa mtu huyo si mkazi wa mtaa huo,

   "Mtu huyo si Mkazi wa Eneo hili, bali Jioni ya jana waliomuona maeneno hayo akiwa katika hali ya kupepesuka Pepesuka kotokana na kunywa Pombe, na huenda hicho ndicho kilicho pelekea Kifo chake kwani hakuwa mwenye afya njema." Alibainisha mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo wakati akihojiwa na Mwandishi wa Globu ya Jamii iliofika eneo la tukio
  Baadhi ya Wanachi wa Mtaa wa Mwamfupe wakijadiliana jambo katika eneo la  tukio.
  Huzuni  ikatawa Eneo hilo.
  Baadhi ya Wanachi sambamba na Wenyenyumba zilizo zunguka Eneo hilo la Tukio wakisubiri msaada kutoka Jeshi la Polisi.Globu ya Jamii inafuatilia taarifa kamili kutoka kwa jeshi la Polisi mkoani Mbeya.

  \Picha na Fadhiri Atick - Mr.Pengo wa Globu ya Jamii-Mbeya.

  0 0

  PUBLIC NOTICE

  (NBAA)
  THE NATIONAL BOARD OF ACCOUNTANTS AND AUDITORS
  TANZANIA
  INTRODUCTION OF DIPLOMA IN INTERNATIONAL PUBLIC SESCTOR ACCOUNTING STANDARDS FROM 1ST FEBRUARY 2016.

  Introduction 

  Due to growing demand in public sector entities to prepare and present high quality transparent financial statements, the National Board of Accountants and Auditors has introduced Diploma in International Public Sector Accounting Standards to be known as “Diploma in IPSAs” which will start on 1st of February, 2016

  The introduction of Diploma in IPSAS is in accordance with the mandate granted to the Board under Section 4 of the Accountants and Auditors (Registration) Act [Cap. 286 Revised in 2002], where the Board has been mandated to conduct examinations and grant diplomas, certificates and other awards in accountancy, auditing and allied subjects.

  Course Objective
  The Course principal objective is to provide an in-depth understanding of the practical application of the International Public Sector Accounting Standards. At the end of the course, the Board shall award Diploma in IPSAS for those who will be successful.

  Targeted learners
  Diploma in IPSAS will benefit anyone who requires an understanding and application of international accounting standards in the public sector. In particular, it is suitable for: 

  · Accountants and finance staff at all levels who are involved in the preparation of financial statements 
  · Trainers wishing to acquire advanced knowledge of the standards 
  · IPSAS’s implementation and sustainability teams 
  · Both internal and external auditors and consultants dealing with financial reporting 
  · Officers responsible for public sector financial reporting and auditing
  Entry Qualifications: Holders of Certified Public Accountant (CPA) Certificate or its equivalent or Holders of Postgraduate Studies in Accounting, Finance, Tax or related subject.

  Venue: will be at NBAA Campus

  Training hours per week: The time for classes will be from 5.00 PM to 7.00 PM
  Duration of the Course: Duration of the course will be six months and examinations will be held in two sessions in a year that is February and August. Two hour classes will be held for three days per week on Monday, Wednesday and Friday. To begin with, classes and examinations centre will be in Dar Es Salaam only.

  Fees and Registration: Application for admission in the February 2016 intake has commenced since 16th November, 2015 and deadline will be on 15th January, 2016.

  Registration form can be downloaded from NBAA website (www.nbaa-tz.org) or collected at Mhasibu House Room No. 208. 

  Total cost for the programme is Tshs.1,500,000/- which includes registration, tuition and examination fees.


  For more Information contact:

  EXECUTIVE DIRECTOR
  NBAA MHASIBU HOUSE
  BIBI TITI MOHAMED STREET
  P.O. BOX 5128,
  DAR ES SALAAM
  TEL: 255 22 2211890 -9
  FAX: 2151746 E-mail: info@nbaa-tz.org

  0 0

  NA VICTOR MASANGU.
  KIVUMBI cha ligi daraja la kwanza (FDL) kwa msimu wa mwaka 2015-2016 kinazidi kushika kasi ambapo timu ya Kiluvya United (Wabishi wa Pwani) jana iliweza kuifunga timu ya African Lyon kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopingwa katika uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam.

  Katika mchezo huo wa Kundi 'A' ulikuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na kila timu kucheza kufa na kupona kwa lengo la kuweza kuibuka na ushindi na kujinyakulia pointi tatau muhimu ili iweze kujiwekea mazingira mazuri ya katika msimamo wa ligi hiyo ya daraja la kwanza ambayo imeonekana kuwa upinzani wa hali ya juu kwa timu zote hususan katika kundi '
  A'
  .

  Kipindi cha kwanza katika dakika za mwanzoni wachezaji wa pande zote mbili walionekana kuanza mchezo huo kwa kasi kwa kuanza kushambuliana kwa zamu ambapo timu ya Kiluvya united iliweza kuandika bao la kwanza kunako katika dakika ya 23 lililowekwa kimiani na mshambuliaji Kassim Kilungo.

  Kuingia kwa bao hilo kulionekana kuwachanganya wachezaji wa Africa Lyon na kuonekana wamebaki wameduwaha huku mashabiki wa kiluvya united waliokwenda uwanjani hapo wakiendelea kushangilia kwa staili ya aina yake ambayo iliweza kuwafurahisha wadau na wapenzi wa soka waliofika kushuudia mpambano huo.

  Dakika ya 32 ya kipindi cha kwanza timu ya African Lyon nayo iliweza kufanya shambulizi la kushitukiza ambalo liliweza kuzaa matunda kwa kuandika bao la kusawazisha lililofungwa na mchezaji Kasakala Ndela baada ya safu ya ulinzi ya Kiluvya united kujichanganya katika eneo la hatari.

  Kikosi cha wachezaji wa kiluvya kiliweza kujipanga upya na kuyarekebisha madhambi yaliyotendeka na kuanza kuliskama lango la wapinzani wao na kufanikiwa kuandika bao la pili katika dakika ya 44 lililofungwa na mchezaji Ayoub Lipat baada ya kuunganisha mpira safi kwa njia ya kichwa.

  Hadi kipinga cha kipindi cha kwanza kinapulizwa timu ya Kiluvya United ilikwenda mapumziko ikiwa iko mbele ya mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao timu ya African Lyon ya Jijini Dar es Salaam, ambapo kipindi milango ya timu zote mbili ilikuwa migumu na kufanya hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika Kiluvya kutoka kifua mbele kwa ushidi huo.

  Kwa matokeo hayo Kiuvya United Wabishi wa Pwani kwa sasa wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 16 huku nafasi ya kwanza ikikamatwa na timu ya Ashanti United ya Jijini Dar es Salaam yenyewe ikiwa na pointi 18.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Profesa Mussa Juma Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Profesa Mussa Juma Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuber Ally, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Picha zote na IKULU.


  0 0

  Wakati Taifa na Mataifa yakiendelea kutoa pongezi zao kwa serikali ya Rais.J.P.Magufuli kwa speed yake ya kuchapa kazi,Mawaziri wake pia wameendelea kuonesha namna walivyodhamiria kusimamia shughuli za maendeleo ya Nchi yetu.

  Hii leo,Mh:Mwigulu Nchemba mwenye dhamana ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi amefanya ziara ya siku moja kwenye ranchi ya Taifa ya Ruvu kukagua ujenzi wa majengo ya machinjio ya kisasa ulioanza mwaka 2010.

  Katika hali ya kusikitisha na kulazimu kuchukua hatua za kinidhamu,Mwigulu Nchemba amekutana na ubadhilifu wa Bilioni 5.7 ambazo zilitolewa kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo,Fedha hizo zilizokuwa zimelengwa kuwezesha ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa hazijafanya kazi kama ilivyokusidiwa.

  Waziri huyo wa kilimo amekuta mradi huo umetelekezwa tangu mwaka 2010 bila kuendelezwa,Sababu za kutelekezwa kwa mradi huo zikidaiwa kuwa ni kutofautiana kwa mkandarasi na bodi ya NARCO(kampuni ya usimamizi wa ranchi za Taifa) hazikukubalika na Mh:Mwigulu Nchemba ambaye baada ya kusikiliza kwa makini ufafanuzi wa kutoka kwa viongozi wa ranchi hiyo aliamua ifuatavyo.

  Kwanza,Mwigulu Nchemba amewatimua wakurugenzi wote wa bodi ya NARCO yenye dhamana ya kusimamia ranchi za Taifa kwa kushinda kukamilisha ujenzi wa mradi huo.Mbali na kushindwa,bodi hiyo imeutelekeza mradi huo na hivi sasa inapendekeza kujengwa kwa mradi mwingine kama huo ndani ya eneo hilohilo la ranchi ya ruvu.

  Pili,Mwigulu Nchemba amesitisha utumishi wa Mkurugenzi mkuu wa ranchi za Tiafa kwa kushindwa kuchukua hatua za kusimamia ujenzi wa mradi huo hadi kukamilika kwake.

  Pia,waziri huyo wa kilimo ameagiza kupitia vyombo vya sheria,wahusika wote walioshiriki ama kwa makusudi au kwa njia yoyote kuhujumu mradi huo usifanikiwe wanachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.

  Mwisho,Nchemba amewaagiza wataalam wa wizara yake kuhakikisha ndani ya siku 7 wanampelekea ripoti ya thamani ya jengo lililokwisha kujengwa na fedha zinazotakiwa kumalizia ujenzi wa jengo hilo.

  Sambamba na hatua hizo,Mwigulu ametoa rai kwa watumishi wote wa umma kuwa mstari wa mbele kusimamia kwa ufanisi na uzalendo miradi yote ya maendeleo ya nchi yetu,Mbali na hapo,serikali ya Magufuli haitakuwa tayari kuona mali ya umma inachezewa na kuibiwa wakati kuna watanzania wanaweza kusimamia mali hizo na kuziendeleza.
  Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi akiwasili kwenye mradi uliodumaa wa Ujenzi wa machinjio ya kisasa wa ranchi ya Ruvu mapema hii leo.Sehemu ya jingo lililobaki kama Gofu mara baada ya kutelekezwa na Uongozi wa Bodi ya ranchi za Taifa(NARCO)Mwigulu Nchemba akishangaa namna mali hii ya Umma ilivyotekelezwa.Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Chalinze Mh.Ridhiwani wakisikiliza kwa makini sababu zilizopekea jingo hilo kutelekezwa.Anayetoa maelezo wa mwisho kushoto ni msimamizi wa ranchi hiyo Ngd.Bwire.Mwigulu Nchemba akiendelea kupewa maelezo ya kina kuhusu ubadhilifu uliojitokeza kwenye ujenzi huu.Picha/maelezo na Festo Sanga Jr.


  0 0  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akisalimiana na watumishi wa TAKUKURU alipotembelea ofisi hiyo  Jumatatu. 
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Valentino Mlowola alipotembelea ofisi za TAKUKURU Jumatatu.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa TAKUKURU alipotembelea ofisi hiyo Jumatatu.
   Mtumishi wa TAKUKURU akiuliza swali kwa Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati Waziri alipokuwa akizungumza na watumishi wa TAKUKURU Jumatatu.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto) akipokea Nyaraka kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Valentino Mlowola alipotembelea ofisi za TAKUKURU.

  0 0

   FAMILIA YA BWANA NA  BIBI MOSES MWANGENDE WA KIMARA B, WANAPENDA KUMPONGEZA  NA KUMTAKIA MTOTO WAO MPENDWA  BRAYDEN MOSES MWANGENDE  SIKU YA LEO TAREHE 05.01.2016 KWA  KUTIMIZA MIAKA  NNE(4),WAZAZI WAKE  WANAMTAKIA AFYA NJEMA NA MWENYEZI  MUNGU AMLINDE.


  0 0

  Wakati  mwingine  kujilinda  waweza  kukuita  kujitetea,kujiokoa au kujikinga.  Ni  hali  ambapo  mtu  hufanya  jitihada  za  kujinasua  katika  tendo  ovu  ambalo  linatekekezwa na  mtu  mwingine  dhidi  yake.  
  Mfano  wake  ni  kama  kuvamiwa  na  majambazi, kutekwa, kufanyiwa  fujo  ya  aina  yoyote, kupigwa au  kujaribu  kupigwa n.k. Matukio ya  namna  hii  au  yanayofanana  na  haya ni  sehemu  yetu  ya  maisha.  Yumkini  yanapotutokea  huw  tunachukua  hatua.  Na moja  ya  hatua    ya  awali  kabisa  tunayochukua  huwa  ni  kujaribu  kujitetea   au  kujikinga  nayo.
  Umevamiwa  nyumbani   na  majambazi,  umefanyiwa  fujo  njiani  kwasabasbu  yoyote  ile  na  wewe  unaamua  kujitetea  ili  usidhurike,  na  katika  kujitetea  huko   unasababisha  kifo  cha  mtu, awe  yule aliyetaka  kufanya  fujo au mwingine  mpita  njia.  Sheria  inasemaje  kuhusu  mkasa  wa  aina  hii.  Makala  yataeleza  japo  mambo  ya  msingi  kuhusu  hali hii.

  0 0

  Aliyekuwa Katibu mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Alphayo Kidata kwa sasa ni Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akikabidhi baadhi ya nyaraka kwa Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Dkt. Yamungu Kayandabila wakati wa makabidhiano ya ofisi makao makuu ya wizara hiyo jijini Dar es salaam Jumatatu.

   Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Alphayo Kidata (wa pili kutoka kulia) ambaye kwa sasa ni Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) akimtambulisha Katibu Mkuu Mpya Dkt. Yamungu Kayandabila (wa pili kutoka kushoto) kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo mara baada ya kuwasili na kukabidhiwa rasmi ofisi.  Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Dkt. Moses Kusiluka na wa kwanza Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Rasilimaliwatu Bi. Teddy Njau.

  Katibu Mkuu mpya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akizungumza na Management Team mara baada ya mapokezi na kukabidhiwa ofisi


  0 0

  Maafisa wa kitengo cha  Mahusiano ya Jamii katikamgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, William Chungu (kulia) na Zuwena Senkondo (kushoto) wakikabidhi vifaa vinavyotumika wakati wakujifungulia kwa zahanati ya Mwingiro Wilayani Nyang’wale Mkoani Geita

  Zuwena Senkondo wkikabidhi vifaa vya kujifungulia kwa mmoja wa wauguzi katika zahanati ya Mwingiro Wilayani Nyang’wale Mkoani Geita

  Kiongozi wa kitengo cha Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Sara Ezra Teri akikabidhi Video Camera ya kisas kwa Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana Thoams Mshilu kwa ajili ya kurekodia tamthiliya zao.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii 
  Kanda ya Kaskazini,aliyekuwa mkoani Geita.

  Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu umekabidhi seti nane za vifaa vya kutolea huduma kwa akina mama wajawazito wanapojifungua, katika halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita vyenye thamani ya shilingi Milioni Tatu.
  Akipokea vifaa hivyo Mratibu wa Huduma ya Baba, Mama na Mtoto wa Halmashauri ya Nyang’wale Mkoani Geita Bi Neema Mhoja amesema, “Tunaushukuru Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu kwa kutupatia vifaa hivi muhimu kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama na mtoto kwani awali upungufu wa vifaa hivyo umesababisha Wauguzi Wakunga katika zahanati wilayani humo kutoa huduma katika mazingira magumu.”


  Naye Meneja wa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Bulyanhulu Bwana Elias Kasitila amesema, afya za akina mama ni nguzo ya msingi wa maendeleo katika jamii hivyo Mgodi kwa kutumia utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi mwaka huu ulipata maombi ya vifaa hivyo kutoka kwa wananchi wa vijiji vya Iyenze na Mwasabuka katika kata ya Mwingiro wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita na umeitikia ombi kwa kukabidhi vifaa hivyo kwa mratibu wa huduma za akina mama na watoto wa wilaya ya Nyang’wale.


  Wauguzi katika zahanati ya kata Mwingiro wamekabidhiwa vifaa hivyo ili waweze kuvitumia na kuvitunza kwa ajili ya matumizi kwenye zahanati hiyo inayohudumia wakazi wapatao 12,000 wa kata ya Mwingiro.
  Muuguzi  Mkunga wa zahanati ya Mwingiro bwa Costantine Matata Bahebe, na Pendo Ntabudyo, na Elizabeth Lameck amesema, “ Sasa itakuwa rah asana ukipata mzazi maana vifaa vinatosha kwani kwa mwezi tunazalisha akina mama kati ya 20 na 25 hivyo kwa vifaa hivi tufanya kazi katika mazingira ya usafi, usalama na utulivu hata pale tutakapopata wazazi nane kwani kila mmoja atakuwa na kifaa chake kuliko kumsubirisha mzazi wakati unapochemsha vifaa baada ya kuvitumia.
  Naye Afisa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo amewaasa wakunga katika zahanati ya Mwingiro kutumia na kuvitunza vifaa hiyo vyenye thamani ya shilingi Milioni Tatu.  0 0  0 0

  IMG_0681

  Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akitoa maelezo ya namna wanavyoendesha shughuli zao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
  IMG_0770
  Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akimwonyesha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla moja ya damu ambayo ni maalum kwa wamama wajawazito wakati wa kujifungua zilizohifadhiwa kwenye jokofu katika mabara hiyo.
  IMG_0760
  Mmoja wa watumishi katika maabara ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama (ambaye jina lake halipatikana) akiendelea kutekeleza majukumu yake kama alivyokutwa na mpiga picha wetu.

  Na Modewjiblog, Team.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza watanzania wote wasikubali kutozwa rushwa kwa ajili ya damu salama na baadala yake kwa mtu atakayefanya hivyo watamchukulia hatua kali.

  Kauli hiyo imetolewa mapema Januari 4 (jana) na Naibu huyo wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Kingwangalla alipofanya ziara katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dares Salaam.

  Dk. Kigwangalla amefafanua kuwa, kwa watu wote ikiwemo Nesi, Daktari ama mtaalamu wa afya, atakayemtoza mtu damu, atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi.“Kwa watanzania wote, msikubali kutoa rushwa kwa ajili ya damu. Na kama itatokea Nesi ama Daktari ama nani, anakuambia ulipie ili upate damu!. Kwa sababu kuna uhaba wa damu kwa sasa.. Ripoti kwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa ama Daktari Mkuu husika ama fika Wizara ya afya moja kwa moja na kuna namba tutaitoa kwa watanzania wote mtupatie ripoti.


older | 1 | .... | 1078 | 1079 | (Page 1080) | 1081 | 1082 | .... | 3282 | newer