Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1074 | 1075 | (Page 1076) | 1077 | 1078 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Mheshimiwa January Makamba (mbele), akitafakari jambo wakati wa kikao cha kujadili changamoto na utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC) jijini Dar es Salaam leo, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Abdulrahaman Jumbe. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Mheshimiwa January Makamba (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC) katika Mkutano wa kujadili changamoto na utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo. (Picha na OMR)

  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitangaza Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu Ikulu jijini Dar es Salaam jioni ya leo December 30, 2015. Kushoto ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakisikiliza kwa makini.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kumkabidhi  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue orodha ya Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu aliowateua huku Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akishuhudia.
  PICHA NA IKULU


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu katika Wizara mbalimbali.

  Walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

  1. Katibu Mkuu Kiongozi

  Balozi - Ombeni Sefue

  1. Katibu Mkuu Ikulu

  Peter Ilomo

  1. Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

  Dkt. Laurian Ndumbaro  1. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

  Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu)

  Dkt. Deo  Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu - Afya)

  Bernard Makali (Naibu Katibu Mkuu - Elimu)  1. Ofisi ya Makamu wa Rais

              Mbaraka A. Wakili ( Katibu Mkuu)

              Mhandisi Ngosi Mwihava (Naibu Katibu Mkuu)


  1. Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu)

  Erick Shitindi (Katibu Mkuu Kazi na Ajira)

  Mussa Uledi (Katibu Mkuu Bunge)

  Dkt. Hamis Mwinyimvua (Katibu Mkuu - Sera)  1. Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi

  Dkt. Frolence Turuka (Katibu Mkuu - Kilimo)

  Dkt. Mashingo (Katibu Mkuu Mifugo)

  Dkt. Budeba (Katibu Mkuu - Uvuvi)


  1. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  Mhandisi Joseph. Nyamuhanga (Katibu Mkuu - Ujenzi)

  Dkt. Leonard M. Chamuliho (Katibu Mkuu - Uchukuzi)

  Profesa Faustine R. Kamuzora (Katibu Mkuu - Mawasiliano)

  Mary Sassabo (Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano)  1. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

  Dkt. Yamungu Kayandabira (Katibu Mkuu)

  Dkt. Moses Kusiluka (Naibu Katibu Mkuu)  1. Wizara ya Maliasili na Utalii

  Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi (Katibu Mkuu)

  Anjelina Madete (Naibu Katibu Mkuu)  1. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji

  Dkt. Adelhem James Meru (Katibu Mkuu - Viwanda)

  Profesa Adolf F. Mkenda (Katibu Mkuu - Biashara na Uwekezaji)

  Mhandisi Joel Malongo (Naibu Katibu Mkuu)


  1. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

  Maimuna Tarishi (Katibu Mkuu)

  Profesa Simon S. Msanjila (Naibu Katibu Mkuu)

  Dkt. Leonard Akwilapo (Naibu Katibu Mkuu)  1. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

  Dkt. Mpoki Ulisubisya (Katibu Mkuu - Afya)

  Sihaba Nkinga (Katibu Mkuu - Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto)  1.  Wizara ya Habari, Utamaduni,  Sanaa na Michezo

  Profesa Elisante Ole Gabriel Mollel (Katibu Mkuu)

  Nuru Halfan Mrisho (Naibu Katibu Mkuu)  1. Wizara ya Maji na Umwagiliaji

  Mhandisi Mbogo Futakamba (Katibu Mkuu)

  Mhandisi Kalobero Emmanuel (Naibu Katibu Mkuu)  1.  Wizara ya Nishati na Madini

  Profesa Justus W. Ntalikwa (Katibu Mkuu)

  Profesa James Epifani Mdoe (Naibu Katibu Mkuu)

  Dkt. Paulina Pallangyo (Naibu Katibu Mkuu)  1.  Wizara ya Katiba na Sheria

  Profesa Sifuni Mchome (Katibu Mkuu)

  Suzan Paul Mlawi (Naibu Katibu Mkuu)

  Amon Mpanju (Naibu Katibu Mkuu)  1.  Wizara ya Mambo ya Ndani

  Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira (Katibu Mkuu)

  Balozi Hassan Simba Yahaya (Naibu Katibu Mkuu)


  1.  Wizara ya Fedha na Mipango

  Dkt. Silvacius Likwelile (Katibu Mkuu)

  Dorothy Mwanyika (Naibu Katibu Mkuu)

  James Dotto (Naibu Katibu Mkuu)

  Amina Hamis Shaban (Naibu Katibu Mkuu)  1. Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa

  Dkt. Aziz Mlima (Katibu Mkuu)

  Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi ( Naibu Katibu Mkuu)  1. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
  2. Job D. Masima (Katibu Mkuu 
  3. Immaculate Peter Ngwale (Naibu Katibu Mkuu
  Makatibu wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wote ambao hawajatajwa katika orodha hii watapangiwa kazi nyingine.
  Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Eliakimu Maswi kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na ametengua uteuzi wa Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Lusekelo Mwaseba, ambaye atapangiwa kazi nyingine


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  30 Desemba, 2015

  0 0

   Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa. Joyce Ndalichako, akitembezwa katika maeneo ya ofisi za Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) jijini Dar es salaam jana na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk.Primus Nkwera. Waziri huyo alikuwa katika ziara ya kutembelea taasisi za elimu zilizochini ya wizara yake.
   Na Mpigapicha wetu.
   Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako (kushoto), akisisitiza jambo, alipokuwa akizungumza na wafanykazi wa Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi (NACTE) jana alipotembelea makao makuu ya baraza hilo lililopo jijini Dar es Salaam jana,wapili toka kushoto ni na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk.Primus Nkwera.
   Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako,akimsikiliza kwa makini Vincent Jacob, mtalamu wa mtandao wa udhibiti wa utoajia wa vyeti vya satifiketi na Diploma wa Baraza la Taifa la Elimu na ufundi (NACTE). Waziri alifanya ziara ya kutembelea makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam jana,Watatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk.Primus Nkwera.
  Waziri wa Elimu Sayansi,Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kuzungumza na wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Elimu na ufundi (NACTE) jijini Dar es salaam jana.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.


  Kesho Ijumaa 01 Januari, 2016 Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wataapishwa rasmi katika Ukumbi wa Ikulu, uliopo lango kuu litazamalo baharini kuanzia saa nne asubuhi.


  Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wote ambao wataapishwa na wale ambao walishaapishwa wanapaswa kuhudhuria katika tukio hili, ili mara baada ya kiapo kukamilika washiriki zoezi la kutia saini Hati ya Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma (Integrity Pledge).  


  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema zoezi la kutia saini hizo, litafanyika kwa uwazi mbele ya vyombo vya habari.

  Aidha, Balozi Sefue amefafanua kuwa hata kama wapo baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu ambao walishasaini Hati hizo, watapaswa kusaini upya mbele ya vyombo vya habari.

  Tukio hili pia litarushwa ‘live’ kupitia luninga.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi Mawasiliano, IKULU


  31 Desemba, 2015.

  0 0

  MERY MICHAEL LASWAI anatangaza kuibiwa kwa Wallet ikiwa na  Nyaraka (Document) nyingi pamoja na Vitambulisho, Leseni ya Uderava, Kadi za Benki na Kadi ya Mpiga kura vyote vikiwa na jina la  MERY MICHAEL LASWAI.

  Vitu hivyo aliibiwa akiwa maeneo ya Boko jijini Dar es Salaam
   atakayeviona mahari popote pale tunaomba apige simu namba 0754441165 na 0688045999.
   SHUKRANI.

  0 0

  Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto) akipokelewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam. 
  Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) akitembelea maeneo mbalimbali ya Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao leo. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam. 

  Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akizungumza na Watendaji na baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam. 

  Na. Aron Msigwa –MAELEZO. 
  Serikali imepiga marufuku matumizi ya Barua pepe za kawaida kwa watumishi wa umma wanaotuma au kupokea taarifa za Serikali na kuwataka watumishi hao kuhakikisha kuwa wanatumia mfumo rasmi wa Mawasiliano ya Barua Pepe Serikalini (GMS) ulioanzishwa na Serikali kwa lengo la kuimarisha mawasiliano kwa njia ya Mtandao. 

  Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angella Kairuki alipokuwa akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao ( e Government Agency) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji na ufanisi wa matumizi ya TEHAMA Serikalini. 

  “Sasa kuna watumishi 7000 wanaotumia anwani za Barua pepe za Serikali ,idadi hii ni ndogo lazima iongezeke, hatuwezi kuendelea kuruhusu utumaji wa taarifa za Serikali kwa kutumia Barua Pepe nje ya mfumo huu” Amesisitiza na kuongeza kuwa Serikali haijakataza matumizi ya barua pepe za kawaida kwenye mawasiliano binafsi. 

  Amesema kwa kutambua umuhimu wa uimarishaji wa mawasiliano ya TEHAMA Serikalini na kuongezeka kwa matumizi ya TEHAMA katika utumaji wa taarifa kupitia mitandao mbalimbali ipo haja ya kuweka msisitizo kwa watumishi wa umma kutumia Barua Pepe za Serikali. 

  Mhe. Kairuki amewataka watendaji wa Wakala hiyo kuhakikisha kuwa wanasimamia uratibu wa zoezi hilo ili kuhakikisha kuwa Wizara, Idara na Taasisi zote za umma zinaunganishwa na mfumo rasmi wa Serikali ili kuwa na mfumo mmoja wa Mawasiliano. 

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akikabidhi sehemu ya msaada kwa baadhi ya watoto kutoka Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni Malapa cha jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa leo na Kampuni ya TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akimkabidhi Mlezi wa Watoto na Vijana, Stella Mwambenja wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni Malapa cha jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya watoto wa kituo hicho.
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada wa chakula kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016 kwa vituo vitatu vya watoto yatima Dar es Salaam. Kulia ni Mlezi wa Watoto na Vijana wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede, Stella Mwambenja. 
  Mmoja wa watoto kutoka Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede cha Buguruni Malapa Dar es Salaam akitoa shukrani kwa kampuni ya TTCL baada ya kukabidhiwa msaada huo na Kampuni ya TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Amanda Luhanga (kulia) wakipewa historia fupi ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge kwa Ofisa Mfawidhi, Ojuku Mgezi (katikati) kabla ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya. 
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Ofisa Mfawidhi wa Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge, Ojuku Mgezi (wa pili kushoto) msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. Wengine ni viongozi na wawakilishi wa jumuiya ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge. 
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Ofisa Mfawidhi wa Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge, Ojuku Mgezi (wa pili kushoto) msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. Wengine ni viongozi na wawakilishi wa jumuiya ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge. 

  0 0


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na  Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Palestina hapa nchini, Mhe. Hazem Shabat. Tukio hilo lilifanyika Wizarani tarehe 30 Desemba, 2015.
  Waziri Mahiga akizungumza na Mhe. Balozi Mteule wa Palestina nchini, Mhe. Shabat mara baada ya kupokea nakala za hati  za utambulisho wake. Katika mazungumzo yao Balozi Shabat alimpongeza Waziri Mahiga kwa kuteuliwa kwenye wadhifa huo na kumuahidi ushirikiano. Pia Waziri Mahiga alimkaribisha nchini Balozi Shabat na kumuomba aendeleze mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Palestina.
  Balozi Mteule wa Palestina nchini, Mhe. Shabat naye akizungumza huku Mhe. Dkt. Mahiga akimsikiliza.
  Balozi Mteule Mhe. Shabat akimkabidhi Mhe. Mahiga zawadi ya picha inayoonesha Kanisa  lililopo katika mji wa  Jerusalem
  Picha ya pamoja


  0 0
 • 12/31/15--12:30: HAPPY NEW YEAR TO YOU ALL


 • 0 0

  Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mohamed Utaly akimkabidhi mkazi wa kijiji cha Kiegea, Bibi Sarah Matereka mbegu za mtama kwa ajili ya shamba lake kama mpango wa wilaya hiyo kuhamasisha wananchi wilayani humo kulima mazao yanayohimili ukame ili kukabili maafa ya njaa , wanaoshuhudia kushoto ni Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofsi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya na katikati ni mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Mhe. George Lubeleje tarehe 31 Desemba, 2015.
  Mmiliki wa shamba la Uzalishaji Mbegu bora za Muhogo aina ya Mumba katika Kijiji cha Choka wilayani Mpwapwa, Edward Kusenha akieleza ubora wa mbegu ya muhogo huo kuwa tangu apande mbegu hiyo mwaka 2014 anaouhakika wa chakula kwa kipindi chote cha hali ya ukame kijijin hapo anayemsikiliza ni Dereva Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Uratibu maafa, Nuru Gagu wakati ofisi hiyo ilipokuwa ikifuatilia hali ya upungufu wa chakula kijijini hapo tarehe 31 Desemba, 2015.
  Kufuatia ziara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa maafa katika Wilaya za Mpwapwa na Kondoa mkoani Dodoma tarehe 30 Desemba, 2015, iliyolenga kufuatilia hali ya upungufu wa chakula katika wilaya hizo hususan katika maeneo yote yaliyoathirika na ukame. Ofisi ya waziri mkuu, Idara ya Uratibu wa maafa imetembelea wananchi wa Wilaya hizo na kufanikiwa kuona baadhi yao wanayo mashamba ya mbegu na mazao yanayohimili ukame suala linalowezesha familia zao kuwa na uhakika wa chakula kwa  kutohitaji chakula cha msaada kutoka Ofisi ya waziri mkuu. 

  Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa inazishauri Kamati za Maafa za Mikoa, Wilaya, Kata na Vijiji ambazo ndizo zenye jukumu kubwa la kusimamia masuala ya maafa katika ngazi hizo ziombe mbegu za mazao yenye kuhimili ukame katika Halmashauri zao na kuzigawa bure kwa wananchi badala ya kuwa wanawaombea chakula cha msaada kila mwaka.


  0 0

  Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki Jumuiya ya Ulaya. Mabalozi hao wamemshukuru Balozi Kamala kwa kazi aliyofanya ya kuongoza Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki. Balozi Kamala amemaliza kipindi chake cha kuwa Balozi wa Tanzania Ubeligiji, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge.

  0 0

  Na Lucas Mboje, Dar es Salaam

  WATUMISHI wa Jeshi la Magereza wametakiwa kuzingatia utendaji kazi wenye tija mahala pa kazi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea(Business as usual).

  Rai hiyo imetolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja wakati akizungumza kwenye Baraza la kufunga Mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka mpya 2016 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini, Dar es Salaam.

  Jenerali Minja amewaagiza Watumishi wote wa Jeshi hilo kuhakikisha kuwa wanawajibika kwenye maeneo yao ya kazi ili kufikia ufanisi uliotarajiwa pamoja na kutumia vizuri rasilimali za Ofisi kwa manufaa yaliyokusudiwa.

  "Utekelezaji wenu wa kazi za kila siku lazima uwe na tija na uendane sambamba na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano ili kufikia ufanisi unaotarajiwa". Alisema Jenerali Minja.

  Aidha Jenerali Minja amezungumzia baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kwa Mwaka 2015 ambayo ni pamoja na kukamilika kwa Sera ya Taifa ya Magereza ambayo italiwezesha Jeshi hilo kutekeleza mpango wake wa Maboresho ya maeneo mbalimbali, kusainiwa kwa Mkataba na Kampuni ya Poly Teknology ya China itakayojenga nyumba 9,500 za Makazi ya Maafisa na Askari, kusainiwa kwa Mkataba wa Magari 9,05 na Kampuni ya Ashok Leyland ambapo magari hayo yanatarajiwa kupokelea mapema mwakani.

  Mafanikio mengine ni pamoja na Usajili wa kudumu wa Chuo cha Urekebishaji ambapo Chuo hicho kitatoa elimu stahiki ya Urekebishaji itakayotambulika ndani na nje ya Nchi, Jeshi la Magereza limepeleka Maafisa wake kwenye shughuli za Ulinzi wa Amani kwenye nchi mbalimbali zenye migogoro, Jeshi limeingia ubia na Wawekezaji mbalimbali katika miradi ya Kilimo, uchimbaji madini ya chokaa, ujenzi wa maduka makubwa(shopping Malls) katika Mikoa ya Morogoro na Kilimanjaro ambapo miradi hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa Jeshi.

  Vilevile Jeshi limefanikiwa kuandaa Maandiko mbalimbali ikiwemo andiko la kujitosheleza kwa chakula na miradi minane ambayo miradi hiyo ikiwezeshwa inaweza kuongeza thamani za mali zinazozalishwa na Jeshi hilo.

  Aidha Jenerali Minja alieleza changamoto mbalimbali ambazo Jeshi hilo linakabilianazo ambazo ni ufinyu wa bajeti, uhaba na uchakavu wa vyombo vya usafiri, ukosefu wa zana za kilimo, mabadiliko ya hali ya hewa hivyo kuathiri Uzalishaji, tatizo la miundombinu ya magereza na msongamano magerezani hali inayopelekea kwa kiasi fulani kuathiri utekelezaji wa majukumu ya Jeshi hilo.

  Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja ametoa Salaam za kheri ya Mwaka mpya 2016 kwa Watumishi wote wa Jeshi hilo na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotawala uendeshaji wa Jeshi la Magereza.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba kwa Watumishi wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) kwenye Baraza la kufunga Mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka mpya 2016. Baraza hilo limefanyika Desemba 31, 2015 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
  Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa timamu kumpokea Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati akiwasili tayari kwa kulihutubia Baraza la kufunga Mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka mpya wa 2016.
  Maafisa ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba fupi aliyoitoa Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo ya uboreshaji unaoendelea kufanyika wa kiwanja cha Ndege Terminal Two kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Eng. Suleiman Suleiman jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa TAA Eng. Suleiman Suleiman akimwonyesha Waziri Prof. Mbarawa ujenzi unaoendelea wa jengo la tatu la abiria (Terminal three), ambapo jengo hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 6 kwa mwaka.
  Mkurugenzi wa TAA Eng. Suleiman Suleiman akimwonyesha Prof. Makame Mbarawa eneo ambalo limefanyiwa ukarabati kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere International Airport (JNIA), wakati alipotembelea eneo hilo, jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0


  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.) akisalimiana na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Nassem Ibrahim Al Najib alipofika Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha salamu za pongezi kwa Mhe. Dkt. Kolimba kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait. 
  Mhe. Balozi Al Najib akimkabidhi Mhe. Dkt. Kolimba salamu za pongezi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait.
  Mhe. Dkt. Kolimba nae akimshukuru Balozi Al Najib kwa kuwasilisha salamu hizo za pongezi na kwamba amezipokea na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Kuwait katika masuala mbalimbali ya maendeleo. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Ndugu zangu,

  Imekuwa ni utamaduni wangu kutuma salamu za Mwaka Mpya kwa wajumbe wangu wa Mjengwablog, marafiki zangu kwenye FB na wengine walio ndani na nje ya mitandao ya kijamii.
  Nimefanya hivyo tangu mwaka 2006 ilipoanzishwa Mjengwablog. Na mwaka huu naendeleza utamaduni huo.
  Ndugu zangu,

  Naandika salamu hizi nikiwa hapa Iringa, na nikiwa na mambo mawili ya kuwaeleza; 
  Mosi, napenda kuwahakikishia kuwa Mjengwablog/KwanzaJamii itaingia mwaka mpya wa 2016 na kasi zaidi ya mwaka jana. Tutazidisha ubunifu katika kuwaletea huduma mpya na bora zaidi.
  Ikumbukwe, Mjengwablog ilikuwa blogu ya kwanza hapa Tanzania kuja na ubunifu wa kuweka kurasa za mbele za magazeti mwaka 2007. Mwaka huu tumekuwa blogu ya kwanza Tanzania kwa kuwa wa kwanza kila alfajiri kuwaletea habari za magazetini zikiwa na uchambuzi wa habari ku 3 ikiwamo uchambuzi wa katuni bora ya siku.

  Mwakani tumedhamiria kuunganisha huduma hizo na radio blogging ikiwa na maana ya kufanya chambuzi kwa njia ya radio ya mtandaoni na kuposti ( KwanzaJamii Radio). Mengine mapya ya kiubunifu yako jikoni, yatakuja kwa mwaka ujao, 2016.

  Jambo la pili nililotaka kulisema linahusu hali ya mtanziko wa kisiasa Zanzibar. Ni majuzi tu nilikuwa Zanzibar kwa takribani juma moja. Nilitembea Zanzibar mjini na vijijini.

  Hakika, sijawahi kupanda boti na kuviacha visiwa vya Zanzibar nikiwa na shaka ya kitakachotokea nyuma baadae. Safari hii niliondoka Zanzibar nikijisikia hivyo. Zanzibar sikuikuta hali njema ya upepo wa kisiasa. Nakumbuka nikiwa kitongoji kimoja pale Jambiani nilioongea na wenyeji walioonyesha shaka kwenye mazungumzo. yao wakati wakiongea nami.

  Pale Jambiani niliiona chuki baina ya wenyeji iliyotokana na tofauti za kiitikadi. Chuki iliyoonyeshwa hata kwenye maandishi ya kutani na kwenye milango ya nyumba. Ni chuki iliyoonyeshwa hata kwenye mijadala ya mitandaoni ambayo binafsi niliianzisha kwa madhumuni ya kuamsha fikra na kubadilishana maarifa na uzoefu.
  Niliyoiona si Zanzibar niliyoifahamu. Bado naamini, Zanzibar imejaa watu wakarimu na wenye upendo. Suluhu ya Zanzibar itapatikana na Wazanzibar wenyewe na kwa njia ya mazungumzo hadi kufikia muafaka.

  Na walio kwenye meza ya mazungumzo wasitangulize maslahi binafsi. Kwenye kujadiliana ili kutatua mgogoro pande husika ziwe tayari kupata na kupoteza. Si vema pia kwenda kwenye meza ya mazungumzo ukihitaji jambo moja tu, kwamba kama ukilikosa ndio mwisho wa dunia.

  Na duniani hapa mengine yaliyofutwa, na kama ni kisheria na yakachapwa hata kwenye gazeti la serikali, basi, si rahisi yakarejeshwa kwa wino ule ule. Ni vema ikatangulizwa hekima na busara. Ni vema na ni busara yakawekwa mazingira ya, hatma ya yote, kuwa pande zinazokinzana zote zikaibuka washindi.

  Na hakuna namna yeyote ile ya kuvifanya visiwa vikawa tulivu bila ya uwepo wa makubaliano ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambapo viongozi wakuu wa pande zote mbili wafanye kazi ya ziada ya kuwahimiza wananchi wao kuchimba makuburi marefu ya kuzizika chuki zao baina ya wao kwa wao. Chuki zilizojengeka kwenye misingi ya ubaguzi. Na sote tunajua dhambi ya ubaguzi, ni kama dhambi ya mwanadamu kuonja nyama ya mwanadamu mwenzake, hawezi kuacha.

  Ni iwekwe wazi, kuwa suala la Muungano wetu halipaswi kuwa mjadala tena kama uwepo au usiwepo, bali ni kwa namna gani tutauimarisha.

  Maana, daima utabaki kuwa ukweli, kuwa jambo la Zanzibar ni letu Bara, na kinyume chake.
  Na tuwe tayari kupambana hadi risasi ya mwisho, na nguvu zote hasi, za ndani na nje ya mipaka yetu, zinazotaka kututenganisha kwa misingi ya Uzanzibar, Upemba, Ubara na hata udini.

  Ni imani yangu, kama ilivyotokea huko nyuma, kuwa Zanzibar imeweza kuvuka mitihani migumu na ikasimama tena.

  Naziona ishara za tumaini jipya la Zanzibar linalokuja. Kwamba viongozi wakuu wa CCM na CUF Zanzibar watazishinda nguvu hasi na zinazochagizwa na wahafidhina wa pande zote mbili, hivyo, kupata formula mpya ya kuvivusha visiwa vya Zanzibar na Pemba kutoka kwenye mtanzuko wa kisiasa uliopo sasa.
  Mungu Ibariki Tanzania na Heri Ya Mwaka Mpya.

  Maggid Mjengwa,
  Iringa.

  0 0


  0 0

  BENDI MPYA
  •Tarehe 31-Jan-2015, BMM Classic Band, ilizinduliwa katika ukumbi wa BMM Mwenge, opposite TRA.
  •Tarehe 21-Feb-2015,  JJ Band yazinduliwa katika ukumbi wa. JJ Band ni bendi dada ya Skylight Band itakayokuwa inatumbuiza mjini Mwanza katika hotel ya Jembe ni Jembe Resort.
   •Tarehe 06-Mar-2015 (Ijumaa), Ruby Band ilitambulishwa rasmi katika ukumbi wa Coco Beach Pub ambapo pia ilizindua video ya wimbo mpya wa “Noma”.
  •Tarehe 18-Jul-2015 (Jumamosi), Stars Band yazinduliwa katika ukumbi wa Mzalendo Pub. Bendi hiyo inaongozwa na mwanamuziki Aneth Kushaba aka “AK47” aliyekuwa Skylight Band. Meneja wa bendi ni mpiga drums James Kibosho. Bendi hii inaundwa pia na mpiga solo Alain Kisomundele na Mao Santiago aliyekuwa Machozi Band.
  •Dec-2015, bendi mpya itakayojumuisha Mule Mule FBI, Totoo Ze Bingwa, Alain Mulumba Kashama, Montana Amarula na Didi “Number” Kayembe (Numero) aka “Dume la Mende” ipo katika maandalizi ya kuundwa na kuzinduliwa huku Mule Mule FBI akiwa rais (prezidaa) wa bendi hiyo huku Losso Mukenga, mpiga solo wa Ally Kiba, akiipigia pia bendi hiyo.


  0 0

  Wananchi wa Jiji la Mbeya washerehekea kwa kupiga Videbe Mkesha wa Mwaka Mpya ikiwa ni kuonyesha Furaha za kuuona Mwaka Mpya na kuamua kukatiza Mitaa Mbalimbali huku wakiimba Nyimbo za Kuukaribisha Mwaka Mpya kama waonekanavyo hapo Juu katika Taswira....
  Furaha ikiwa imetawala kwa baadhi ya Wakazi wa Jiji la Mbeya.
  Mwaka waanza vibaya pia kwa mwenye Gari hilo Pichani lenye Nambari za Usajli (T 240 BCB) kwa kuparamia Ukuta Eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya,
  PICHA NA MR.PENGO MBEYA.

older | 1 | .... | 1074 | 1075 | (Page 1076) | 1077 | 1078 | .... | 3284 | newer