Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1075 | 1076 | (Page 1077) | 1078 | 1079 | .... | 3282 | newer

  0 0
 • 01/01/16--00:53: VIFAA HIVI VINAUZWA
 • Tyre Changer, Wheel Balancer na Compressor vinauzwa, ni used kutoka UK lakini vipo katika hali nzuri. Vyote vipo Dar es Salaam. 
  Mawasiliano: 
  0774 65 98 95 au +255 788 741 125  0 0
  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akizungumza na wananchi katika kijiji cha Chimwenga wilaya ya Mbeya vijijini ambapo Naibu Waziri aliwaeleza wananchi hao umuhimu wa kukaa mbali na vyanzo vya maji ili kutoviharibu na kusababisha upungufu wa maji unaopelekea bwawa la uzalishaji umeme la Mtera kukauka.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa wakiwa katika kijiji cha Makwenji wilaya ya Mbeya vijijini ambapo Naibu Waziri alikagua vyanzo vinavyotiririsha maji kwenye mito inayopeleka maji katika bwawa la uzalishaji umeme la Mtera.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (mwenye tai nyekundu) akikagua moja ya miradi mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji inayofanyika katika wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya ambayo hutumia maji kutoka katika mapitio yanayopeleka maji katika bwawa la uzalishaji umeme la Mtera.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza Matembezi ya wanamichezo katika Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo kwa kuwanzia Uwanja wa Tumbaku Mjini Unguja na kumalizia Uwanja wa Amaan Studium.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanamichezo wa Vikundi mbali mbali kama ishara ya kuyapokea maandamano ya vikundi hivyo katika kilele cha Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
  Wamamichezo wa Vikundi vya mazoezi wakipita mbele ya jukwaa kubwa Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika kilele cha Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
  Wamamichezo wa Vikundi vya mazoezi wakipita mbele ya jukwaa kubwa Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika kilele cha matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.


  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo alielazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo January 1, 2016. Kardinali Pengo alilazwa hospitalini hapo jana jioni kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake. PICHA NA IKULU

  0 0

   Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Tano Dr. Salmin Amour kati kati akibadilishana mawazo na Makamu wa Rais Mstaafu wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal (kushoto)  na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi nyumbani kwake Kidombo mara baaya ya chakula cha mchana.
  Hafla hiyo inayojumuisha mamia ya waumini wa Dini ya Kiislamu kutoka pembe zote za Unguja huambatana pia na Maulidi ya Kuzaliwa kwa Kiongozi wa Dini ya Kiislamu Duniani Mtume Muhammad { SAW  } wakati wa usiku ukiwa ni utaratibu wa  Dr. Salmin kuandaa ifikapo Mfunguo Sita wa kila mwaka.
   Rais Mstaafu wa Tanzania Alhaj Ali Haasn Mwinyi (wa pili kutoka Kushoto)  akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (wa kwanza kutoka kushoto) na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt Mohamed Gharib Bilal (wa pili kulia)  wakijumuika na waislamu katika Hitma ya kuwaombea dua Waumini waliotangulia mbele ya haki hapo Msikiti wa Ijumaa Kidombo Kijijini kwa Rais Mstahafu wa Zanzibar Awamu ya Tano Dr. Samlin Amour.
  Waumini wa Dini ya Kiislamu kutoka sehemu mbali mbali Nchini wakihitimisha Hitma ya kuwaombea waislamu walitangulia mbele ya haki hapo kwenye Msiki wa Ijumaa Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja Kijiji alipozaliwa Rais Mstahafu wa Zanzibar Dr. Salmin Amour.
  Picha na OMPR, ZNZ.


  0 0

  bella (69)Bella akicheza na mashabiki wakebella (71)bella (73)Shoo ikinogabella (74)Bella na mashabiki jukwaanibella (75)Mashabiki wakizidi kupagwa.
  PICHA NA MUSA MATEJA/GPL
  Kwa picha zaidi


  0 0

  Ligi Daraja la Daraja la Kwanza (StarTimes League) inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo kumi na mbili kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, huku kituo cha StarTv kikitarajiwa kuonyesha moja kwa moja michezo miwili ya ligi hiyo.
  Kundi A Ijumaa, Januari Mosi 2016 Polisi Dar watawakaribisha Mji Mkuu katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, huku kesho Jumamosi michezo tisa ikichezwa katika viwanja mbalimbali nchini.
  Jumamosi StarTv watakua uwanja wa Karume jijini Dar es salaam kurusha moja kwa moja mchezo kati ya Ashanti United dhidi ya Polisi Dodoma, Polisi Morogoro watawakaribisha Kurugenzi FC ya Mafinga katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, huku Kimondo FC wakicheza dhidi ya Burkinafaso kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
  Maafande wa Ruvu Shooting watacheza dhidi ya Mji Njombe katika uwanja wa Mabatini Mlandizi, Lipuli dhidi ya JKT Mlale katika uwanja wa Wambie mkoani Iringa, maafande wa JKT Kanembwa wakiwakaribisha Mbao FC katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
  Geita Gold watawakaribisha Polisi Mara kwenye uwanja wa shule ya Nyankumbu mjini Geita, JKT Oljoro watacheza dhidi ya Rhino Rangers uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, huku maafande wa Polisi Tabora wakiwakaribisha Panone FC katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  StarTv Jumapili wataonyesha moja kwa moja mchezo kati ya Africa Lyon dhidi ya Kiluvya United uwanja wa Karume, huku timu ya Kinondoni Municipal Council (KMC) wakicheza dhidi ya Friends Rangers katika uwanja wa Mlandizi Mabatini.

  0 0

  WAZIRI MKUU  Mhe. Kassim Majaliwa amewapongeza Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu, mara baada ya kuapishwa Ikulu  jijini Dar es Salaam leo. 
  Ametoa pongezi hizo wakati Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu wakiwa wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya waandishi wa habari.
  Mhe. Majaliwa pia amewataka viongozi hao, kuwa waaminifu, kuwajibika na  kutoa taarifa ya utendaji kwa wananchi. Aidha, alisema kuwa, viongozi wengine watakao apa mbele ya Kamishna wa Tume ya Maadili ni pamoja na  Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri, ikiwa ni hatua ya Serikali kudhibiti na kufuatilia matumizi ya rasilimali fedha.
  “Wakuu wa Wilaya watahakikisha fedha zilizoenda katika Halmashauri zao lazima zitumike katika shughuli zilizokusudiwa” alisema Waziri Mkuu.
  Waziri Mkuu alitoa wito kwa watanzania kuendelea kuwa na imani na Serikali ya Awamu ya Tano, kwakuwa itatimiza ahadi zote ambazo Mheshimiwa Rais na Makamu wa Rais walizitoa wakati wa Kampeni.
  Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu hao, wameapishwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli, ambapo shughuli hiyo ilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mke wa Mheshimiwa Rais mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali.
   Mhe. Kassim Majaliwa akiwapongeza Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu, baada ya  viongozi hao kutia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa Ikulu  jijini Dar es Salaam leo January 1, 2016

    Mhe. Kassim Majaliwa akiwapongeza Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu, baada ya  viongozi hao kutia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa Ikulu  jijini Dar es Salaam leo January 1, 2016
  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Masaju wakishuhudia Makatibu wakuu na Naibu Katibu wakiapa kabla ya kusaini Hati ya Maadili ya Umma mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016
   Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Masaju wakishuhudia Makatibu wakuu na Naibu Katibu wakiapa kabla ya kusaini Hati ya Maadili ya Umma mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016
  Makatibu wakuu na Naibu Katibu wakiapa kabla ya kusaini Hati ya Maadili ya Umma mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016. PICHA NA IKULU

  0 0

  Wakisubiri zamu zao za kula kiapo mbele ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ni Meja Jenerali Gaudence Salim Milanzi (kushoto) na Jaji, Wakili Mkuu Meja Jenerali Projest Anatory Rwegasira Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016. Picha na IKULU

  0 0  0 0

   Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyakea wakiwa katika mkesha wa mwaka mpya.
    Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na mkewe wakicheza kwa furaha wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akiwa na furaha wakati wa mkesha wa mwaka 2016 kwenye Uwanja wa Uhuru.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye(katikati) akicheza nyimbo za injili wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkesha wa Kuliombea Taifa (Dua maalum), Mchungaji Godfrey Mallassu akizungumza katika mkesha huo.

  0 0

    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
   Waziri akiwa katika picha ya pamoja.
    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
  Waziri waWizara ya Ujenzi,. Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prtof Makame Mbarawa akisaini kitabu cha wageni katika jingo la kikosi cha zimamoto cha kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

  0 0
  0 0

  Baada ya kufanikisha kwa Tamasha la siku ya Kandanda hapo Oktoba 17 mwaka jana, Tamasha lililobeba Ujumbe wa "#OneBallOnTxt Book" ikiwa ni Dhima kamili ya kunyanyua Mchezo wa mpira wa miguu kuanzia ngazi ya shule ya msingi na kuwasisitizia watoto wetu umuhimu wa kusoma pia, Timu nzima ya Wanakandanda imeonelea Kuufungua Mwaka 2016 kwa kwenda kutembelea Kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kukabidhi Mchango wao ambao ulitokana na mauzo ya fulana za Tamasha la Siku ya Kandanda mwaka jana.

  Ikumbukwe tulieleza kwamba kwa kila Fulana moja itakayonunuliwa, asilimia kumi itaenda katika kampeni ya #MpiraMmojaKitabuKimoja (#OneBallOneTxtBook). Kamati ilifanikiwa kuuza Fulana 100 ambazo tumefanikiwa kutumia asilimia iliyotakiwa katika kununulia vifaa ambavyo tunakabidhi  katika kituo cha House of Blue Hope Leo hii.

  Vitabu vilivyonunuliwa ni vya Hisabati, Kiingereza, Kiswahili, Sayansi, Jiografia na Teknohama. Mipira imekabidhiwa miwili, ambayo tulipewa na mdhamini, hivyo pesa iliyotakiwa kununulia mipira tuliongezea katika vitabu.

  “Tunashukuru Kandanda Day kwa mchango huu katika kituo chetu, utasaidia kuwajenga watoto kimasomo na kimichezo” Amesema Msimamizi wa kituo hicho, Daudi Mboma.

  Pia Tunachukua nafasi hii kutoa shukrani zetu za dhati kwa wadhamini wetu wote( BinSlum , BayPort TZ, SDS, Michuzi Media Group, MacAuto Accessories, SalehJembe Blog, Pepsi, GALACHA na Kandanda.co.tz) tuliokuwa nao toka Tunaanza Tamasha hili la Siku ya Kandanda kwa Mwaka wa Tatu mfululizo kwa kujitolea kwao kwetu katika kufanikisha Siku yetu pia kuwapa Mrejesho wa kile ambacho tumekifikia kwa Mwaka wa Tatu!. Pia bila kuwasahau Chama cha Madaktari, TASMA, kwa kushiriki nasi katika Tamasha la mwaka jana.

  Hakika mafanikio ni mengi sana si rahisi ya kuyaorodhesha yote lakini kwa Uchache ni kukua kwa Muamko kwa Familia ya watu wa Kandanda katika ushiriki wa Siku hii, pia Kujua umuhimu wa kushiriki katika michezo kwa Jamii katika kudumisha Afya za miili yetu pamoja na kushiriki katika upimaji wa Afya zetu siku ya Tamasha.

  Malengo ya Siku hii ya Kandanda ni kuinua Ari na Muamko kwa wananchi wote katika kushiriki katika matamasha na kurudisha kile ambacho jamii ya wasionacho wangekihitaji kukipata kupitia matamasha haya.

  Kama Taifa mchezo upendwao zaidi ni Kandanda lakini bila Maarifa na Vifaa hatuwezi kuja kuwa na Kina Mbwana Samatta ama Thomas Ulimwengu wengi zaidi hivyo basi tunapenda tutoe Rai kwa Watanzania wote waliopo ndani na nje ya Nchi kushirikiana nasi katika kufikia malengo yetu makuu ya kupeleka Kitabu Kimoja na Mpira Mmoja katika kila Kaya ya Mtanzania mmoja ili kuinua Elimu, Michezo pamoja na kujenga  Afya ya miili yetu.

  Tungependa watu wengi zaidi, kutoka katika jamii tofauti, mashirika tofauti na hata makampuni tofauti tukaungana kwa pamoja Mwaka huu 2016 na kuifanya siku hii iwe kubwa zaidi na Tupeleke na kuwafikia watoto wengi Zaidi. Tunatarajia kuwa na siku ya kandanda mwaka huu Katika siku ya Jumamosi ya Tatu ya Oktoba (#Oktoba15), ikitanguliwa na matamasha madogo madogo ambayo tutatoa utaratibu hapo baadae ili kuwapa wadau wa kandanda kote kushiriki. Lengo letu ni kuhusisha Tamasha hili kufanyika siku moja katika sehemu mbalimbali Tanzania, tukiwa na lengo moja.

  Kwa kuwapelekea Kitabu Kimoja na Mpira Mmoja

  Pamoja Tutaweza


  Kamati ya Maandalizi Kandanda Day 2015

  Mwenyekiti wa Kamati, Patrick 'Patoo' Dumulinyi, akimkabidhi vitabu na mpira Mlezi wa kituo cha House of Blue Hope, Daudi Mboma. Kulia kwa Patoo ni Bi Fatma Hassan mwakilishi wa TeamDizoMoja na Kushoto kwa Mboma ni Meneja wa TeamIsmail (Mabingwa 2015/16), Ismail Mohammed.
   Picha ya Pamoja na baadhi ya watoto wa Kituo cha House of Blue Hope wakiwa na vitabu na mpira.

   Bi Fatma (Team DizoMoja) akiwa na Msimamizi wa Kituo, Daudi Mbnoma.
   Mwenyekiti wa Kamati, Patrick 'Patoo' Dumulinyi, akimkabidhi vitabu na mpira Mlezi wa kituo cha House of Blue Hope, Daudi Mboma. Kulia kwa Patoo ni Bi Fatma Hassan mwakilishi wa TeamDizoMoja na Kushoto kwa Mboma ni Meneja wa TeamIsmail (Mabingwa 2015/16), Ismail Mohammed.
    Watoto wa kituo cha House of Blue Hope wakifurahia mpira

  0 0


  0 0

  Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,Mh.Mwigulu Lameck Nchemba akisikiliza kero za wadau wa machinjio ya Vingunguti usiku  wa January 01/01/2016.Mwigulu Nchemba akishuhudia Ng'ombe aliyetayari kwa taratibu za kuchinjwa kwa ajili ya kitoweo.
  Mbuzi wakiwa tayari kwa ajili ya kuchinjwa kwenye machinjio hayo ya Vingunguti.Mbuzi hawa asilimia kubwa wanatoka mnada wa Pugu ambao Ushuru wake unakusanywa na serikali kuu.Waziri Mwigulu Nchemba akikagua maeneo ya machinjio hayo usiku huu.
  Mwigulu Nchemba akitoa maagizo kwa uongozi wa Machinjio ya Vingunguti kukutana kesho saa 2:00 asubuhi kwa wahusika wote wenye dhamana na Machinjio hayo,Mkutano utafanyika eneo la Machinjio hayo.
  ----------------------------------

  Katika hatua ya kushitukiza,Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba amefanya ukaguzi wa Machinjio ya Vingunguti usiku wa Ijumaa Januari 1, 2016.
  Mh.Mwigulu Nchemba amefika kwenye Machinjio hayo usiku huo ilikushuhudia Mifugo ikiandaliwa kwa ajili ya kitoweo cha wananchi.Uchinjaji wa Ng'ombe na Mbuzi katika machinjio haya hufanyika nyakati za Usiku kuanzia saa 4 hadi 10 alfajiri.
  Mbali na kusikiliza kero na maoni ya wananchi kuhusu uendeshwaji wa Machinjio hayo,Mwigulu Nchemba ameshuhudia utafunwaji wa kodi ya serikali inayokusanywa kwenye mnada wa Pugu.
  Utafunwaji huo unatokana na uandikaji wa kibali cha mifugo michache kuja Machinjioni ili hali mifugo zaidi huingizwa machinjioni bila kibali.
  Mathalani  Mh.Waziri ameshuhudia Ng'ombe waliotoka mnada wa Pugu ambao wameshalipiwa kodi wakiwa 1450 lakini kibali chake kimeandikwa Ng'ombe 300 tu.Ikimaanisha kuna ng'ombe 1150 wamelipiwa ushuru lakini machinjioni kimeletwa kibali cha ng'ombe 300 wakati kwa hesabu ng'ombe hao wanazidi 1000.
  Kutokana na hali hiyo,Mh.Waziri ameagiza wahusika wote kufika kesho kwenye mkutano wa asubuhi kwa ajili ya hatua stahiki kuchukuliwa.
  Mhe Mwigulu amesisitiza kuwa kwa mtu yeyote mwenye dhamana na kusimamia sekta ya kilimo,Mifugo na Uvuvi afanye kazi  kwa mujibu wa sharia,vinginevyo hakutakuwa na huruma kwa wanaohujumu.

  0 0


  0 0  Wachezaji wa klabu ya Simba jana wamelionja joto la jiwe baada ya mashabiki wa Ndanda FC kuwavamia wachezaji wakati wa mazoezi.  https://youtu.be/6kqjr9XjQ00

  Timu ya CDA imetupwa nje katika mashindano ya kombe la shirikisho baada ya kupokea kichapo cha bao 1 toka kwa Singida United.  https://youtu.be/KmxQHdfWOqU
  Serikali imetoa tamko kuwa itaendelea kuwalipa mishahara makocha wote  wa timu za taifa   https://youtu.be/Ochi73k6Q64
  Fahamu mengi kutoka kwa Mch. Samwel Maela akikufundisha mengi kuhusu mpango wa Mungu na taifa la Tanzania mwaka 2016: https://youtu.be/rO96gpssLDs

  Jionee mengi jinsi watanzania wanavyosherekea kwa furaha mwaka mpya na wakizungumza  matarajio yao kwa mwaka mpya mwaka 2016:https://youtu.be/A7jcptFyuAw

  Kutana na wachambuzi wa masuala ya maendeleo kutoka visiwani Zanzibar wakikuelimisha mambo kadha wa kadha kuhusu ujenzi wa taifa:https://youtu.be/1SVUJ6ElmDA

  Msikilize Mkurugenzi wa gesi kwa matumizi ya nyumbani akikuhabarisha kuhusu usambazaji na matumizi ya gesi majumbani:  https://youtu.be/MtYkLmdwXW8

  Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi mhe. Lukuvi awaongoza wakazi wa jiji la Dar katika mkesha wa mwaka mpya.   https://youtu.be/HIk94oLcmNc

  Serikali yaahidi kuwawekea walemavu mpango maalumu ili kuwatengezea mazingira bora ya ajira.   https://youtu.be/GH9uvGzSIAk

  Jeshi la polisi mkoani Simiyu limekamata gari aina ya Toyota Harrier lililoibiwa December 7 jijini Dar   https://youtu.be/Z17Ly6KRuBY

  Kamishna Suleiman Kova aliyekuwa mkuu wa kanda maalumu ya Dar es Salaam amestaafu kulitumikia jeshi la polisi.   https://youtu.be/u5xOJa44sRQ
older | 1 | .... | 1075 | 1076 | (Page 1077) | 1078 | 1079 | .... | 3282 | newer