Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

WANANCHI WA KIJIJI CHA SHENDA WILAYANI GEITA WALALAMIKIA UCHAFU ULIOTUPWA TAREHE 9 DISEMBA

$
0
0
Krantz Mwantepele,Geita

Wananchi wa kijiji cha Shenda katika kata ya Masumbwe wilayani Mbogwe mkoani Geita Wameitaka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya Mbogwe kuziondoa takataka zilizowekwa kijijini kwao kufuatia zoezi la usafi la December 9 Lililofanyika nchi nzima.

Wakiongea na waandishi wa habari za mtandaoni wananchi hao wanakijiji hao wamesema kuwa wanashangazwa na kitendo cha halmashauri ya wilaya kutupa takataka katika kijiji chao licha ya kwamba hakuna dampo la uchafu eneo hilo.

Wameongeza kuwa taka hizo ni hatari kwa afya zao kwani zimetupwa karibu na eneo la shule ya msingi,Makazi ya watu na vibanda vya mama ntilie hali inayozua hofu ya kuzuka kwa magonjwa ya mripuko kwani taka hizo zimeanza kuoza na kusambaa katika makazi ya watu kipindi hiki cha masika.

Sambamba na hayo wameshangazwa na maamuzi ya ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri kutupa taka hizo katika kijiji chao licha ya kuwa yapo maeneo mengi ya wazi ambayo yangeweza kutumika kutupa taka hizo ambazo kwa sasa zimekuwa kero katika kijiji chao hasa kutoa harufu mbaya na funza.

Kwa mujibu wa kaimu mtendaji wa kijiji cha Shenda Joseph Jaseda amesema sehemu zilizotupwa taka hizo ni makazi ya watu na kwamba walipouliza kuhusu hatua hiyo waliambiwa kuwa gari la kuzoa taka liliharibika sehemu hiyo na ndipo walipoamua kutupa taka hizo.

Kwa upande wake afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe amesema kuwa baada ya wananchi kulalamika walienda kuweka dawa ya kuwa wadudu katika taka hizo na kwamba hawajaziamisha kutokana na taka hizo kutokuwa na madhara kwa wananchi.
Huo ndio uchafu uliotupwa katika kijiji cha shenda siku ya tarehe 9 Disemba ambapo ilikuwa siku ya usafi kwa nchi nzima.
 
Wanakijiji wa kijiji cha Shenda wilayani Geita wakiongea na waandishi wa habari waliotembelea kijiji hicho ambapo walilalamikia kutupwa kwa takataka katika kijiji hicho siku ya tarehe 9 ambapo ilikuwa siku ya usafi kwa nchi nzima.

SERIKALI KUPITIA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, TAMISEMI NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRA NA MUUNGANO KUANZISHA PROGRAMU YA PAMOJA WA UPANDAJI MITI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akizungumza kwenye kikao cha pamoja kati yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Januari Makamba (kulia) leo tarehe 29 Desemba 2015 katika ukumbi wa Selous Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii  Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuipa majukumu Kamati Maalum ya Wataalam ya kutengeneza andiko maalum litakalotumika kuandaa Programu ya pamoja ya kitaifa ya upandaji miti nchi nzima kuanzia mijini hadi vijijini kwa lengo la kuhifadhi na kuendeleza mazingira ikiwemo misitu. Kwa mujibu wa Prof. Maghembe Kamati hiyo imepewa wiki mbili kukamilisha kazi. Mpango huo utashirikisha pia Wizara ya TAMISEMI.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Januari Makamba (kulia) akizungumza katika kikao hicho. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akifafanua jambo katika kikao hicho.

SIMU TV: UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI December 29, 2015.

$
0
0
   
Serikali imetoa agizo kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanafikisha taarifa za ugonjwa wa kipindupindu wizarani kwa wakati.  https://youtu.be/wxauztmL6Rk

Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wameunga mkono jitihada za rais Dkt Magufuli kwa hatua anazochukua kupambana na vitendo vya ubadhirifu.   https://youtu.be/bYqUW5DXtao

wakazi wa eneo la Kinondoni Jijini Dar wameanza kujenga upya mabanda ili kujihifadhi baada ya nyumba zao kubomolewa.  https://youtu.be/BasLD6w7-xw
  
Watanzania washauriwa kupima afya zao kila baada ya miezi sita na kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa: https://youtu.be/VhTGpWvwizw

Wahitimu wa mafunzo ya awali JKT Dodoma wahimizwa kuwa wazalendo na kushirikiana vema kulinda taifa la Tanzania: https://youtu.be/3sbrd0q0XVc

Watuhumiwa nane washikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kumiliki silaha kinyume na sheria: https://youtu.be/IBx0BE0nwOo

Je, Kuna Tatizo Gani Kula Nyama?

$
0
0
 Je! Ni kawaida asili ya mwanaadam kuwa nakula nyama? Kufuatana na mafunzo ya sanaa ya Yoga, inashauri sana kuepuka madhara yanayosababishwa na athari ya kula nyama ambayo ni mjadala mrefu na uanaleta hoja nyingi katika maisha ya mfumo mzima wa sanaa hiyo.
Leo, kama tunajiandaa kuelekea mwaka mpya 2016 na malengo mapya, basi moja ya ushauri na mazungumzo ni kufahamishana na kuhusu mambo kazaa ya sanaa ya Yoga na uhusiano wake wa kutokula nyama kiafya.

Mfumo wa kuchanganya na kuyeyusha chakula wa binaadam “ Digestive system” pamoja na jinsi meno na maumbo yaliyo kunatofauti sana kulinganisha na wale walao nyama kiasilia “Carnivorous”, wanatofauti kubwa kama vile maumbile ya mfumo wao wa chakula tumboni. Tumbo lao“Bowel” ni  fupi mara tatu tu ya urefu wa mwili wao.  
Hii inawaruhusa kuweza kutoa  mabaki ya chakula chao cha nyama mwilini haraka sana kwa ufupi huo wa utumbo. Hivyo wadudu wa “Bacteria” hawakai muda mrefu tumboni na kutoka kupitia mfumo wa haja kubwa. Utumbo wa “Carnivorous”  unauwezo mara 10  zaidi ya kemikali ijulikanayo kama “Hydrochloric Acid” kulinganisha na wale wasiao kula nyama kisilia kama vile wanyama wanao kula majani tu, na huwawezesha wala nyama kuchanganya na kuyeyusha nyama  mbichi na hata mifupa bila taabu yeyote. Meno yao pia ni ushahidi dhahiri, “ Canines” meno yalioyochongoka na marefu kuwawezesha kumudu hali ya ulajiwao wa nyama.

Binaadam, ni wazi kabisa sio mlaji nyama asilia “ Natural”. Maumbile ya mfumo wao wa kuchanganya na kuyeyusha chakula “Digestive system”, unadhihirisha hivyo. Ni aina zote za mazao ( Maharage, kunde, mbaazi, soya) ya aina mbali mbali, matunda karanga aina zote ni vyakula ambavyo asili ya mwanaadam tokea enzi na enzi. 
Kimaumbile, utumbo wa binaadam una urefu mara 12 ya urefu wa mwili wake,  endapo kama utumbo utanyooshwa ndivyo jinsi utadhihiri urefu wake. Hii inaonyesha jinsi gani kwamba chakula cha binaadam huchukua muda mrefu kuchanganywa na kuyeyushwa tumboni kulinganisha na mfumo wa “Carnivorous” ulio mara tatu tu ya urefu wao. 
Nyama, huanza kuoza mara tu iingiapo tumboni, na kuchukua muda mrefu sana kutoka mwilini  kulinganisha na wa nyama wenye kula nyama.

Vilevile, nyama ina aina ya kemikali yenye sumu ijulikanayo kwa jina la “Toxic” na “Adrenalin” ambazo hubaki mwilini mwa mwanyama anapochinjwa au kuuwawa. Hii pia husababisha, aina nyingine ya kemikali ijulikanayo kama“ Uric Acid” ni sumu inayobaki katika viungo na damu ya nyama ambayo watu wanakula.

Kufuatana na “Encyclopidia Brittanica” protini “Protein” inayopatikana katika mazao kama vile karanga, maharage, kunde, mbaazi, maziwa  na soya, ambayo ni safi kabisa, kulinganisha na ile inayopatikana kutoka katika nyama, siyo safi kwa asili mia 56%.

Mafuta ya nyama “Meat Fat” au “Cholesterol” hujijenga katika mishipa au milija ya damu “ Arteries”, na jinsi mwili unavyo zeeka, ndivyo jinsi mishipa na milija hiyo uzeeka na kupoteza nguvu zake wakati ikikupungua ukubwa wa upana wake kwa sababu za mafuta kujaa ndani ya mishipa hiyo.  Hii husababisha njia ya damu kuwa nyembamba na kusababisha shinikizo katika kwenye moyo.

Hapo ndipo sasa, moyo haunabudi bali kufanya kazi mara dufu ya kawaida yake kusambaza damu mwili mzima. Matokeo, ni kuleta madhara ya kupasuka mishipa ya damu ( Stroke ), ni matatizo ya kiharusi, shinikizo la moyo ( Blood Pressure ) ni mingoni mwa matatizo makubwa sasa  katika  jamii yetu na ulimwengu mzima. 
Moja ya kazi kubwa na majukumu anayobeba mla nyama ni kemikali ya aina ya “Urea na Uric Acid” “(Nitrogen Compound)”, kutoka katika nyama. Moja ya mifano,  “Beefsteak” kwa mfano huu  ina gram 14  za “Uric Acid, kwa kila pound moja ya nyama. Hii ni kweli hasa kupitia vipimo vya mkojo wa mtu wanao  kula nyama na asiye kula, kuna tofauti kubwa ya ushahidi huo.

Matokeo yake, figo za mtu anaekula nyama hazina budi kufanya kazi mara tatu ya kawaida yake kutoa sumu au kemikali hiyo ya aina ya “Nitrogen Compound” iliyopo katika nyama na hubaki mwilini, na figo ndio yenye jukumu la kuhakikisha mwili upo katika mazingira ya usafi au ndio husafisha  kemikali zote zilizopo mwilini. Nahatimaye  kutoka kwa njia ya  mkojo mwilini.
 Mtu akiwa kijana na nguvu zake kikawaida, hilo huwa sio tatizo kabisa kwa figo kufanya kazi ya ziada.  
Hivyo basi, mwili unapo anza zeeka na kupoteza uwezo wake wa kawaida jinsi  maisha yalivyo, hivyo ndio jinsi figo nayo hupungua nguvu zake za kuwajibika kwa ziada kusafisha hizo kemikali mwilini. 
Figo zinapokuwa zimeelemewa kupita kiasi kiwango Fulani,  sababu ya kula nyama nyingi, kemikali ya “Uric Acid” inaanza sambaa mwilini mzima kutokana na kile kijulikana cho kama figo kushindwa ( Kidney failure) hazikufanya wajibu wake kama inavyo stahili.  Hiyo kemikali “ Uric Acid” husambaa katika viungo vya mwili, inavutwa kama jinsi sponji inavyo fyonza maji, na kuganda kama jiwe katika viungo au (Joints) na misuli ya mwili.

Hii matokeo yake husababisha maumivu makubwa ya viungo yaani (Joints pain) na misuli katika mwili. Kwa namna moja au nyingine, inaaminika pia huu ni chanzo cha matatizo ya magonjwa kama vile : Gout, Arthrititis na Rheumatism.

Hatua hiyo ndio yupasa madaktari kushauri wagonjwa kupunguza kula nyama au kuacha kabisa kula nyama, ambapo kwa kweli tayari madhara yameshafanyika mwilini. Na kupitia mazoezi ya sanaa ya Yoga, husaidia kuimarisha viungo na misuli kupitia mafunzo yake ya umakini na utaratibu kuambatana na pumzi kuwezesha mwili kupata nguvu zaidi kulinganisha na mazoezi ya aina nyingine yenye kutumia nguvu za misuli tu, na hatimae kuchoka haraka.


                        Imetolewa na Sensei Rumadha Fundi; mkufunzi wa Yoga;

                        Eastern Metropolitan Bypass, Tiljala, Culcutta, India.

                        College of Neo-Humanist    Studies; Gullringen, Vimmerby, Sweden.

JOTO LA ASUBUHI LA 93.7 EFM DISEMBA 30, 2015 KUANZIA SAA 12 ASUBUHI

bomoabomoa ya hiyari yaendelea bonde la msimbazi jijini Dar es salaam

$
0
0
 Baadhi ya wananchi wakiwa wamesha bomoa nyumba zao zilizo katika Bonde la mto Msimbazi, mtaa wa Magomeni Sunna jijini Dar es salaam, kabla ya serikali kuanza kuzibomoa nyumba hizo ifikapo tarehe 5 januari 2016

Twanga kupepeta shangwe za mwaka mpya ndani ya Dar live

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura atembelea Idara ya habari

$
0
0

 Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura katikati akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Assah Mwambene wa kwanza kulia ya jinsi ya kutunza picha za matukio mbalimbali wakati alipofanya ziara Idarani hapo leo.
 Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura kulia akimkabidhiwa moja ya vipeperushi vinavyotolewa na Bodi ya Filamu Tanzania ambavyo vina lengo vya kuwaelimisha wasanii, anayemkabidhi ni Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fissoo.

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura katikati akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Assah Mwambene wa kwanza kulia ya jinsi ya kutunza picha za matukio mbalimbali wakati alipofanya ziara Idarani hapo leo, kushoto ni Afisa Habari Mkuu Anna Itenda.  Picha na Benjamini Sawe-WHSUM.

wakongwe wa habari na sheria wanapokutana...

$
0
0
 Wakongwe wa habari na sheria wakijitahidi kuingia mwakani kwa sera za Hapa ni Kazi Tu! jijini Arusha ni Jenerali Ulimwengu na Danford Mpumilwa 
Wakongwe wa habari na sheria wakijitahidi kuingia mwakani kwa sera za Hapa ni Kazi Tu! jijini Arusha ni Jenerali Ulimwengu na Danford Mpumilwa wakiwa na mwanasheria mkongwe Chief Mirambo

INTRODUCING SIKILIZA MOYO WAKO (LISTEN TO YOUR HEART) KUTOKA KWA RAPA MACHACHARI KAPUKU DIGITAL

BALOZI KAMALA AAGANA VIONGOZI WA TAASISI YA WAFANYABIASHARA YA UBELIGIJI

$
0
0
Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa taasisi ya Wafanyabiara Ubeligiji baada ya kumaliza kikao cha kuagana nao  Brussels. Balozi Kamala anarejea Tanzania baada ya kumaliza kipindi chake cha Kuwa Balozi wa Tanzania Ubeligi, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya.

Ibada maalum ya kumuombea Dkt. Rais John Pombe Joseph Magufuli yafanyika jijini London

$
0
0
 Askofu Mkuu wa kanisa la CCBC Dr Sarpong (kushoto) kutoka Ghana na Pastor Bob kutoka Kenya wakiongoza Ibada maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli jijini London usiku wa kuamkia leo.
 Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Msafiri Marwa akitoa neno la Shukurani wakati wa ibada hiyo jijini London.
Wanakwaya wa kanisa la CCBC wakiimba kwenye Ibada hiyo jijini London
 Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Msafiri Marwa akipata picha ya pamoja na wanakwaya na viongozi wa kanisa la CCBC baada ya kumalizika kwa Ibada hiyo jijini London.

Hauli (Kumbukumbu) ya Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian kufanyika kesho mtaa wa Simba na Amani, Kariakoo, Dar es salaam

$
0
0
Hauli (Kumbukumbu) ya Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian (pichani) aliyefariki dunia mwaka mmoja uliopita itafanyika Mtaa wa Amani na Simba, Kariakoo,  jijini Dar es salaam mara baada ya Swalatul Ishai Zawiyan. 
Familia ya marehemu inawaalika ndugu, jamaa, marafiki na majirani popote pale walipo kuhudhuria shughuli hii,  kumkumbuka na kumuenzi Sheikh Comorian, aliyekuwa mwanazuoni nguli na mwalimu wa wengi.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA KAMBI YA WAKIMBIZI YA NYARUGUSU, MKOANI KIGOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa zawadi ya khanga,blanket na ndoo kwenye wodi ya wazazi katika zahanati iliyopo kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kwa Mama mkimbizi kutoka nchi ya Burundi aliyejifungua.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwajulia hali akina mama waliolazwa katika zahanati iliyopo ndani ya kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Mkoani Kigoma wanaotoka nchi ya Kidemokrasia ya Congo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na wakimbizi wa Congo na Burundi katika kambi ua Nyarugusu.
Baadhi wa wakimbizi kutoka nchi ya Congo na Burundi waishio katika Kambi ya wakimbizi Nyalugusu Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani) akiwahutubia.Picha na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma.


MSIJE MAKAMBINI NA SILAHA – WAZIRI MKUU
* Ataka walionazo wazisalimishe, asema watakaokiuka kukamatwa
* Awaonya wakimbizi kuhusu ngono zembe, asema siyo jambo la dharura

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaasa raia wanaokimbia nchi zao na kupata hifadhi Tanzania kutobeba silaha wanapoingia nchini kuja kuishi kwenye kambi za wakimbizi.

Ametoa onyo hilo leo mchana (Jumanne, Desemba 29, 2015) na wakati akizungumza na mamia ya wakimbizi wanaoishi kwenye kambi za Nyarugusu na Nduta zilizoko wilayani Kasulu na Kibondo, mkoani Kigoma waliofika kumsikiliza kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika kwenye kambi hizo.

“Ninawasihi mjitambue kuwa mmehama kutoka DRC na Burundi, na mnapoingia hapa inabidi mbadilike muwe na tabia za hapa. Hatuhitaji mje na silaha au vifaa hatarishi kwa sababu tunataka mkae kwa usalama,” alisema.

Alisema suala la usalama ni muhimu miongoni mwao, ni muhimu zaidi kwa majirani zao lakini pia ni muhimu sana kwa watoa huduma wanaowahangaikia. “Tunataka kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake ili siku mkiondoka mrudi nyumbani mkiwa salama,” alisema.

“Ninyi mko hapa mnatunzwa kwa hiyo hamruhusiwi kutoka kambini na kutembea hovyo huko nje. Hii ni kwa usalama wenu. Hatumruhusu kuingia na bunduki au mabomu na yeyote atakayemuona mwenzie ana silaha au ameificha mahali aje atuambie ili tumchukulie hatua na ninyi wengine mbakie salama,” alisisitiza.

Kuhusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU), Waziri Mkuu aliwataka wakimbizi hao wajiepushe na ngono zembe kwa sababu kiwango cha maambukizi kimeongezeka kwa asilimia moja ikilinganishwa na mwaka jana. 
“Nimetembelea hospitali yenu hapa kambini na kuelezwa kuwa maambukizi ya VVU hapa yapo na mwaka huu yamefikia asilimia mbili ya watu waliopimwa ikilinganishwa na mwaka ambapo ilikuwa ni asilimia moja tu,”

“Kutokana na uwingi wenu, naomba niwasihi sana mjizuie kufanya ngono zembe na kama mtu atashindwa kabisa kujizuia ni vema atumie kinga. La sivyo mtaleta maambukizi ya juu sana na wote mtakwisha,” alisema.

“Suala lenyewe siyo jambo la dharura, kawaida huwa kuna maandalizi baina ya wahusika, watu wanakubaliana juu ya muda na mahali pa kukutanandiyo maana nasema siyo jambo la dharura. Ndugu zangu tujihadhari sana kwa sababu kasi ya maambukizi mahali hapa iko juu sana,” alisisitiza. 
Mapema, Mkuu wa kambi ya Nyarugusu, Bw. Sospeter Boyo alimweleza Waziri Mkuu kwamba kambi hiyo ilifunguliwa Novemba 1996 kwa lengo la kuwahifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo waliokuwa wakikimbia vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Alisema kambi hiyo yenye ukubwa wa kilometa za mraba 28, ina uwezo wa kuhifadhi wakimbizi 50,000 lakini kwa sasa inao wakimbizi 151,032 ambao ni mara tatu zaidi ya uwezo halisi wa kambi hiyo.

“Tangu Aprili mwaka huu, idadi ya wakimbizi imeongezeka hadi kufikia 151,032 miongoni mwao ni wakongo 61,313, warundi 89,619, Wanyarwanda 75, Waganda 12, Wasudan kusini wane,Wakenya wane, Msomali mmoja, Mzimbabwe mmoja na raia wa Ivory Coast mmoja,” alisema Bw. Boyo.

Alisema wanakabiliwa na changamoto za uhaba wa maji safi, ufinyu wa huduma za afya na elimu na uharibifu wa mazingira.

Waziri Mkuu bado anatembelea pia kambi ya JKT ya Mtabila wilayani Kasulu na kesho asubuhi anatarajiwa kufanya majumuisho ya ziara yake.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, DESEMBA 29, 2015.


WAZIRI NAPE AZINDUA FILAMU YA HOME COMING DAR

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihojiwa na mtangazaji mashuhuri wa Azam TV Taji Liundi muda mfupi kabla ya kuzindua filamu mpya ya Home Coming kwenye ukumbi wa Century Cinema ,Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Wadau wa Sanaa na Utamaduni wakisubiri kushuhudia uzinduzi wa filamu mpya ya Home Coming.
 Mmoja wa washiriki wa Filamu hiyo ya Home Coming ,Susan Lewis maarufu kama Natasha
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye na Ayo TV muda mfupi kabla ya kuzindua Cinema ya Home Coming.
Muigizaji mkuu wa filamu ya Home Coming Daniel Kijo (kushoto) akisalimana na mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu hiyo Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye mara baada ya uzinduzi wa filamu hiyo kufanyika kwenye ukumbi wa Century Cinema, Mlimani City jijini Dar es Salaam.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.


MABALOZI WA AFRIKA, KARIBIANI NA PACIFIKI WAMUAGA BALOZI DR. KAMALA

$
0
0
Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki Jumuiya ya Ulaya. Mabalozi hao wamemshukuru Balozi Kamala kwa kazi  aliyofanya ya kuongoza Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki. Balozi Kamala amemaliza kipindi chake cha kuwa Balozi wa Tanzania Ubeligiji, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge.

DIRA YA DUNIA

VIONGOZI WAPYA WA TAHLISO WAAPISHWA RASMI,WAUNGANA NA KASI YA MAGUFULI

$
0
0
Mwenyikiti mpya wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania TAHLISO Ndugu STANSLAUS PETER akila kiapo kulitumikia shirikisho hilo mbele ya mwanasheria HAMZA JABIRI leo Jijini Dar es salaam kuanza kazi rasmi ya kuwatumikia wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania 

Na Exaud Mtei (msaka habari) wa Habari24 blog

Uongozi mpya wa shirikisho la elimu ya vyuo vikuu nchini Tanzania TAHLISO umesema kuwa upo tayari kumuunga mkono Rais wa Tanzania Dr John pombe magufuli kwa kasi aliyoanza nayo na kuhakikisha kuwa elimu ya Tanzania hasa elimu ya vyuo vikuu inakuwa ya ubora unaofaa na inaheshimika nchini Tanzania.
Makamu Mwenyekiti mpya wa TAHLISO Ndugu JUMA ALLY OMARI akila kiapo leo jijini Dar es salaam 

Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya kuwasimika viongozi wa shirikisho hilo wapya mwenyekiti mpya wa TAHLISO Tanzania Bw STANSLAUS PETER amesema kuwa kwa miaka mingi elimu ya juu nchini Tanzania imekuwa haina ubora unaotakiwa ikiwa ni pamoja na mitaala mibovu,ukosefu wa mokopo kwa wanafunzi wengi jambo linalowakatisha tamaa wengi kusoma,ambapo amesema uongozi wake umeona kasi nzuri ya serikali ya awamu ya tano na wapo tayari kushirikiana na serikali kutatua changamoto za wanafunzi nchini.
Naibu katibu mkuu wa TAHLISO KHAMIS ELLY akiapa leo Jijini Dar es salaam 

Mwenyekiti huyo amesema kuwa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka huu umeonyesha kuwa serikali ya Magufuli inawajali wanafunzi kwani asilimia kubwa ya wanafunzi walipata mikopo na wengine wanaendelea kupata mikopo huku akiwataka wanafunzi kutulia kwani neema kwao inakuja kutokana na kasi ya uongozi huo mpya pamoja na ule wa serikali ya awamu ya tano.

Uchambuzi wa habari za magazetini leo Jumatatu 30 December 2015.

SPIKA WA BUNGE, JOB NDUGAI AMEREJEA LEO KUTOKA INDIA

$
0
0
SPIKA WA BUNGE, JOB NDUGAI AMEREJEA LEO KUTOKA INDIA ALIKOKUWA KWA AJILI YA MATIBABU. AWASHUKURU WATANZANIA KWA MAOMBI YAO. AELEZEA HALI YAKE KUWA NI IMARA KABISA.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilakiwa na Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson mara baada ya kuwasili katika uwanja Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nchini India alikokuwa kwa ajili ya matibabu.
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Naibu Waziri wa Nishai na Madini Mhe. Medard Kalemani mara baada ya kuwasili katika uwanja Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nchini India alikokuwa kwa ajili ya matibabu. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambula na aliyeko kulia ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah 
 Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akifafanua jambo kwa Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya kumpokea katika uwanja Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nchini India alikokuwa kwa ajili ya matibabu. Katikati ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images