Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

WATU 493 WAMEFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIPINDUPINDU HAPA NCHINI

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na ugonjwa wa Kipindupindu ulivyoweza kupungua ikiwa kukiwa na vifo vya watu 493 kwa Tanzania Bara.


Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Na Zainabu Hamis wa Globu ya Jamii.
JUMLA ya watu 493 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu Tanzania bara tokea ulipoibuka jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake leo, amesema kuwa jumla ya watu 12,222 wameugua ugonjwa huo tangu ugonjwa huo wa mlipuko kuaza hapa nchini.


“Ugonjwa wa Kipindupindu umeanza tokea tarehe Desemba 15, 2015 katika mkoa wa Dar es salaam na kusambaa katika mikoa 21 ya Tanzania” Mhe. Mwalimu amesema.



Hata hivyo,Waziri huyo,amesema waathirika wa kipindupindu wameanza kupungua katika mikoa ya 
Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es salaam.

Pia ameitaja Iringa na Kilimanjaro kuwa ni mikoa ambayo imeweza kuthibiti ugonjwa huo hatari.

Mwalimu akitoa takwimu za ugonjwa huo, amesema hivi sasa kuna wagonjwa wapya 76, hivyo idadi ya wagonjwa wapya imefikia 493 na kifo kimoja.

“Hadi sasa mkoa wa Morogoro vijijini unaongoza kwa wagonjwa 56, ukifuatiwa na Arusha (28), Rorya (22), Bunda (21) na Kigoma vijijini 17.” Mhe. Mwalimu amesema”

Aidha Mhe.Mwalimu ametoa agizo kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuwa ni marufuku kuuza matunda yaliyokatwa barabarani,kuuza vyakula katika mazingira yasiyo safi na salama,huku akitaka kuandaliwa kwa taarifa za kila wiki kuhusu ugonjwa huo.

Akitoa rai kwa wakuu wa wilaya na mikoa, kuwa walete taarifa sahihi za mlipuko wa ugonjwa huo kwa ajili ya kuudhibiti. Na kwa kuwasisitiza watanzania kunywa maji safi na salama na kunawa mikono kwa maji safi na salama.

VIJANA WAOMBA KUUNGWA MKONO KATIKA VIKUNDI WANAVYOUNDA HAPA NCHINI

$
0
0
Mwanzilishi wa kikundi cha Tanzania Talents Organisation, Isaya  Msabila akizungumza na mwandishi wetu leo jijini Dar es Salaam katika eneo wanalofanyia mazoezi kata ya Kwembe jimbo la Kibamba. Kikundi hicho cha sanaa za maigizo na ngoma asilia hapa nchini ambapo wameungana vijana 26 ili kupunguza idadi ya vijana wasio na ajira wameona kujikusanya na kufanya maigizo na ngoma asilia ili kujikwamua kiuchumi.
Vijana wa kikundi cha maigizo na ngoma asilia cha Tanzania Talents Organisation wakiwa katika picha ya moja leo jijini Dar es Salaam.

VIJANA 26 wameunda kikundi cha maigizo na mgoma za asili kijulikanacho kama Tanzania Talents Organisation(T.T.O). ili kupunguza ongezeko la vija wasio na ajira hapa chini.

Kikundi hiki cha maigizo na ngoma asilia kilichojichimbia katika kata ya Kwembe  jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam kikiwa na leongo la kutunza asili na tamaduni ya watanzania ili iweze kuigwa na mataifa mengine ulimwenguni kote.

Hayo yamesemwa na Mwanzilishi wa kikundi cha Tanzania Talents Organisation, Isaya  Msabila wakati akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam leo.

 Pia Msabila amesema katika kikundi hicho wanachangamoto kadhaa baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi pamoja na huduma ya kwanza kwa vijana hao endapo kama kukitokea majeruhi katika harakati za kuigiza au kufanya mazoezi.

Msabila aliwaomba wadau mbalimbali wanaoweza kusaidia kikundi hicho cha sanaa za uigizaji na ngoma asilia awasiliane na mwanzilishi wa T.T.O
Isaya Msabila kwa namba 071449415 ili kuweza kukisaidia kikundi hicho kwa namna mbalimbali ili vijana waweze kujikwamua kiuchumi.

RIDHIWANI KIKWETE ATETA NA KATIBU MKUU KIONGOZI,OMBENI SEFUE IKULU

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya Rais Dk John Magufuli kuwaapisha Mawaziri waliokuwa wamesalia Ikulu, Dar es Salaam leo.
Ridhiwani pia alipata wasaa wa kujadiliana mambo mbalimbali na kiongozi huyo wa watumishi wa Serikali. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.

UTT AMIS YAHAMASISHA WANAVIKOBA ARUSHA KUWEKEZA

$
0
0
Mratibu wa Alliance For Social Education (ASE), Sunayritha Tawata akimkaribisha Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga (kushoto) katika semina ya Uwekezaji wa Pamoja iliyofanyika jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga akizungumza katika semina ya uwekezaji wa Pamoja uliofanyika jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wa semina ya Uwekezaji wa Pamoja wakisikiliza mada.
Ofisa Masoko Mkufunzi wa UTT AMIS, Waziri Ramadhan akitoa mada katika semina ya Uwekezaji wa Pamoja iliyofanyika jijini Arusha.

RAIS JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kulia) kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Dkt. Joyce Ndalichako (kulia) kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge), leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia) kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge), leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge (kulia) kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Profesa Makame Mbarawa (kulia) (amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji) na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

DIRA YA DUNIA JUMATATU 28.12.2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU December 28, 2015 (FULL)

$
0
0
Photo Credits: govtech.com

Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu Tanzania ya sasa na ile tuitakayo. Wiki hii ni ya mwisho kwa mwaka 2015, hivyo kipindi hiki kimeangaza baadhi ya yaliyotokea katika siasa za Tanzania. Studioni alikuwepo Dj Luke Joe, Said Mwamende na Mama Jessica Mushala. Na kama kawaida, kwa njia ya simu tukaungana na wasikilizaji wengi ndani na nje ya Marekani 
KARIBU

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI


Childbirth Survival International wraps up 2015 on a high note.

$
0
0
 Stella Mpanda a veteran nurse midwife and CSI Tanzania Country Director highlights on the importance of skilled birth attendants to have necessary medical supplies to ensure safe childbirths in health facilities.


On November 30th, December 2nd, and December 3rd, pregnant women in three hospitals in Tanzania were fortunate to receive some well-needed gifts. CSI donated 100 sterile childbirth kits to Amana Hospital, 50 kits to Mwananyamala Hospital, and 50 kits to Temeke Hospital, respectively. 
Each kit contains all necessary supplies such as gloves, umbilical clamps, placenta bag, & more and costs $7 equivalent to 15,000 Tanzania shillings. Through generous donations from individuals and Rotary International, to date, CSI has distributed more than 250 sterile childbirth kits.

While CSI Team recognizes the need is greater and more kits are needed; midwives, nurses, physicians, and most importantly the pregnant women appreciate very much and remain with the hope that CSI shall return soon with additional kits and life-saving medicines.


 CSI donated 100 sterile childbirth kits to Amana Hospital, 50 kits to Mwananyamala Hospital, and 50 kits to Temeke Hospital, respectively. 
 Helping mothers and newborns survive preventable causes of death & disability in Tanzania and Uganda. For more CLICK HERE


NesiWangu Show hosts ChildBirth Survival International

$
0
0
Harriet Shangarai, Stella Mpanda and Tausi Suedi
"Pregnancy is not an illness or disease" say Childbirth Survival International (CSI) Co-founders - Stella Mpanda, CNM and Tausi Suedi, MPH.
It is estimated at least 800 women die every day due to pregnancy, childbirth, and post-childbirth complications, most of which are preventable.
Mama Mpanda and Tausi Suedi have an informative discussion with Harriet Shangarai of Nesiwangu show (click here) and leave no stone unturned as they passionately talked about the challenges, gaps, achievements, opportunities, and shared personal stories.
This video will give you an in-depth picture of Childbirth Survival International, the amazing work the team is doing, and how you can partner to make a difference.
 For more information, visit www.childbirthsurvivalinternational.com

Dkt. Mpango awaasa Watumishi Wizara ya Fedha na Mipango kufanya kazi kwa bidii ili kukuza uchumi wa nchi.

$
0
0
Watumishi Wizara ya Fedha na Mipango wameaswa kufanya kazi kwa weledi na kuwekeza nguvu zaidi katika ukusanyaji mapato ili kukuza uchumi wa nchi na kuifanya nchi iwe kitovu cha uchumi Barani Afrika. 
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiongea na watendaji wa Wizara hiyo alipowasili Wizarani hapo mara baada ya kuapishwa jana Ikulu jijini Dar es salaam. 
 Katika mazungumzo yake na watendaji hao, Mhe. Dkt. Mpango, aliuagiza uongozi wa Wizara yake kuunda na kisimamia sera za mfumo wa ukusanyaji kodi ambao utabaki kuwa rafiki kwa wafanyabiashara ili kukuza biashara na uwekezaji nchini.
 “Ili kutekeleza kutekeleza ukusanyaji wa kodi kwa kutumia mfumo rafiki kwa wafanyabiashara na Serikali, Wizara inawajibu wa kusimamia na kukuza uchumi ambao utawanufaisha wananchi walio wengi, kwa kuhakikisha kodi zote ndogondogo ambazo ziko chini na nje ya Wizara, ambazo ni kero kwa wanachi wa hali ya chini zinapatiwa ufumbuzi kwani wananchi hao nao wanastahili maisha mazuri” Alisema Mhe. Dkt. Mpango. 
 Waziri Dkt. Mpango aliwasisitiza watendaji kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi ili nchi iweze kupiga hatua kwa kuzingatia nidhamu katika kufanya kazi ambayo ni dhamana walizokabidhiwa. 
 Naye Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji aliwahimiza watendaji wa wizara hiyo kufanyakazi kwa umoja na mshikamano waliokuwa nao katika utendaji kazi ili kuleta maendeleo yenye tija huku akisisitiza kuwa wizara hiyo ndiyo msingi katika kukuza uchumi wa nchi. 
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile aliwapongeza Viongozi hao wapya wa Wizara kwa kuteuliwa kwao kuiongoza Wizara ambayo ndiyo muhimili wa Serikali. 
Aidha, Dkt. Likwelile alitoa wito kwa watendaji wa wizara hiyo kuzingatia maagizo ya Mhe. Waziri kwa maendeleo ya nchi ili kulinda hadhi na heshima ya wizara.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akisoma  kadi ya pongezi aliyoipokea kutoka kwa viongozi kwa niaba ya watumishi wa Wizara hiyo yenye lengo la kumpongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Bi. Deodatha Makani (katikati).

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kulia) ikiwa ni sehemu ya ukaribisho kwa Waziri huyo Wizarani hapo.

 Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sera Prof. Adolph Mkenda akifafanua jambo ofisini kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango mara baada ya kuwasili Wizarani hapo jana  jijini Dar es salaam.
 Watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango wakielezea majukumu ya Idara na Vitengo katika mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip mara baada ya kuwasili Wizarani hapo jana jijini Dar es salaam.
Habari na picha na Kitengo cha Mawasiliano 
Wizara ya Fedha na Mipango


OPERESHANI MAALUMU YA POLISI MORO KUEKELEA SIKUKUU YA X-MAS YABAMBA 23 MIONGONI MWAO RAIA WAKIGENI.

$
0
0
Na John Nditi, Morogoro 
POLISI mkoani Morogoro imewatia mbaroni watu 23 kati ya hao wawili wakiwa ni wahamiaji haramu raia wa kutoka nchini Ethiopia walioingia nchini bila kuwa na kibari wala pasi za kusafiria wakiwa njiani kuekelea Afrika Kusini. Raia hao walikamatwa wakiwa Mikumi, wilayani Kilosa. 
 Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, alisema hayo Desemba 28, mwaka huu (2015) wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu matukio mbalimbali yaliyotokea kuanzia Desemba 20 hadi 27, mwaka huu. 
 Hivyo alisema , miongoni mwa watanzania waliokamatwa wa nane wanatuhumiwa na kufanya vitendo vya ujambazi na unyang'anyi wa kutumia silaha katika tukio lililofanyika saa 2: 30 usiku wa Novemba 29, mwaka huu eneo la Lukobe, Manispaa ya Morogoro baaada ya kuvamia Kituo cha wamisionari wanaomiliki shule ya msingi wa hirika la Kidini liitwalo Youth With A Mission. Kamanda wa Polisi wa mkoa alisema, katika watu hao nane, sita wanadaiwa ndiyo walivamia kituo hicho na kuwapora vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh 3,250,000 pamoja na Bunduki moja aina ya shotgun Pump Action na risasi moja na kutokomea bila kuwajeruhi wamishionari hao. 
Kundi hilo la uporaji na ujambazi , 13 kati yao wanatuhimiwa kusafirisha na kuuza dawa za kulevya aina ya bhangi viroba vitatu na maboksi mawili pamoja na misikoto 109 sambamba na dawa inayodhaniwa ni aina ya cocain kete 113.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo akionesha sehemu ya madawa ya kulevya yaliyokamatwa
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo akiongea na wanahabari
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo akionesha pikipiki inayosadikiwa kutumiwa na majambazi
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo akionesha gari lililokamatwa na watuhumiwa
Sehemu ya dawa za kulevya aina ya bhangi viroba vitatu na maboksi mawili pamoja na misikoto 109 sambamba na dawa inayodhaniwa ni aina ya cocain kete 113.

MAPITIO YA MAGAZETI KUTOKA VITUO VYA TELEVISENI LEO

$
0
0
TBC

Ndalichako kuanza na shule za sekondari za serikali, Askari waliofanya mauji ya kinyama kizimbani. Pata dondoo za magazeti ya leo.   https://youtu.be/_72hzpy1xt8

Star TV

Mawaziri wapya watangaza kiama, IGP Mangu alifumua jeshi la polisi, serikali yastukia vifaa vya tiba asili na mbadala.  https://youtu.be/5N3StIbFYsY

Ch 10

Bosi Zantel auawa kinyama kwa risasi, Waziri Maghembe amshukia Kinana, Magufuli na Lowassa wamtesa Gwajima. Pata dondoo hizi hapa.   https://youtu.be/4rDMqlAJx8A

Azam TV

Ngoma atimkia Afrika kusini, Nimuboma na Majabvi sasa ki roho safi Msimbazi, Niyonzima Kitanzini. Pata dondoo za michezo hapa.  https://youtu.be/B7VEULSR87A

Mlimani TV

Taarifa ya kipindupindu sasa kutolewa kila wiki, mtuhumiwa wa dawa za kulevya aanguka kortini, Pata dondoo za magazeti ya leo hapa. https://youtu.be/xWi9yl1-jvM

Shukrani na Taarifa ya Arobaini

$
0
0
Familia ya marehemu Mwalimu Ngore N. Kondo wa Chang’ombe, Dar es salaam tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshirikiana nasi kwa kutufariji kwa hali na mali katika kumuuguza mpaka kumzika baba yetu mpendwa aliyefariki tarehe Novemba 28, 2015 katika hospitali ya Regency na kuzikwa tarehe Novemba 29, huko  Chamazi.

  Shukrani za pekee ziwafikie Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wa hospitali za Hindu Mandal na Regency za hapa DSM. Pia shukrani ziwafikie Uongozi na wafanyakazi wa Chuo cha Watumishi wa Umma (Magogoni) ambapo marehemu alifanya nao kazi kwa zaidi ya miaka thelathini (30). Na pia shukrani ziwafikie Uongozi na wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania, Hospitali ya Aga Khan pamoja na Kinondoni 'B' Dispensany & Medical consultant na Benki ya NMB ambako watoto wa marehemu Hadija, Nasra na Abdul ni watumishi wa taasisi hizo.
  Ni vigumu kuwashukuru wote kwa majina.  Tunawashukuru wote, ndugu, jamaa, marafiki na majirani wa Chang’ombe na Chamazi kwa ushirikiano wenu mkubwa.
  Tunapenda pia kutumia nafasi hii kuwataarifu na kuwakaribisha katika shughuli ya arobaini na hitma ya marehemu baba yetu mpendwa itakayofanyika Jumapili ya tarehe 3 Januari, 2016 saa sita mchana nyumbani Chang’ombe.

  Inna Lillahi wa inna ilayhi Rajiun 
“Hakika, sisi ni wa mwenyezi mungu 
na hakika kwake tutarejea” – Quran 2:156

NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU (WATU WENYE ULEMAVU) ATEMBELEA KITUO CHA NUNGE, KIGAMBONI

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ualemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi ametembelea Kituo cha Watu wenye Ulemavu na wasiojiweza cha Nunge Kigamboni Dar es Salaam Desemba 28, 2015 ili kuangalia mazingira na changamoto wanazokumbana nazo wakazi hao.
Afisa Mfawidhi Makazi ya Wazee wa kituo cha kulea watu wenye ulemavu cha Nunge Kigamboni, Bw. Ojuku Mgesi akimuonesha Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ualemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa kwanza kushoto) banda linalotumiwa kufuga kuku ikiwa ni sehemu ya mradi wa wazee wa kituo hicho.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ualemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (mwenye miwani) akimsikiliza Bw. Salum Omari mwenye ugojwa wa ukoma alipokuwa akielezea changamoto za uvamizi wa ardhi katika Kituo cha Kulea watu wenye ulemavu na wasiojiweza cha Nunge Kigamboni. Tarehe 28, Desemba, 2015.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ualemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akieleza jambo kwa mmoja wa wakazi wa Kituo cha Watu wenye ulemavu na wasiojiweza cha Nunge juu ya umuhimu wa kuhama na kuwapisha watu wenye matatizo wenye ulemavu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ualemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akimsikiliza Bi. Consolata Edward alipokuwa akieleza changamoto anazokumbana nazo juu ya tatizo la Kifafa kinachomfanya wakati mwingi kupoteza fahamu na kushindwa kufanya mambo yake kwa ufasaha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII PFOF. JUMANNE MAGHEMBE AKABIDHIWA RASMI OFISI LEO NA ALIYEKUWA WAZIRI WA WIZARA HIYO LAZARO NYALANDU

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) akikabidhiwa taarifa ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Lazaro Nyalandu (wa pili kulia) leo tarehe 29 Desemba 2015 ofisini kwake Mpingo House. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Selestine Gesimba (kulia).
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mhe. Lazaro Nyalandu (kushoto) akizungumza na Waziri wa sasa wa Wizara hiyo Mhe. Prof. Jumanne Maghembe na Katibu Mkuu Dkt. Adelhelm Meru (kulia) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika leo tarehe 29 Desemba 2015 katika ofisi za Wizara hiyo Mpingo House. Katika salamu zake Mhe. Nyalandu amepongeza uteuzi wa Prof. Maghembe ambapo amesema Mhe. Rais amefanya chaguo sahihi kwani Prof. Maghembe anao uwezo wa kufanya kazi nzuri katika Wizara hiyo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akizingumza na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) muda mfupi baada ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika ofisini kwake leo. Mhe. Prof. Maghembe amempongeza Mhe. Nyalandu kwa kazi nzrui aliyoifanya akiwa Waziri wa Wizara ya Malisili na kuahidi kuanzia alipoishia katika kuhakikisha Maliasili za nchi zinatunzwa ipasavyo ikiwemo kupambana na changamoto zilizopo za ujangili na uharibifu wa misitu na maliasili kwa ujumla.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri kabla yake Mhe. Lazaro Nyalandu, Makabidhiano hayo yamefanyika leo Makao Mkuu ya Wizara hiyo, Mpingo House jijini Dar es Salaam.

Katika makabidhiano hayo Mhe. Nyalandu amekabidhi taarifa rasmi ya makabidhiano kwa Mhe. Waziri Prof. Jumanne Maghembe kama ishara ya kukabidhi rasmi Ofisi ya Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Makabidhiano hayo ambayo ni utaratibu wa kiserikali wa kukabidhi ofisi umeshuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru, Naibu Katibu Mkuu, Bw. Selestine Gesimba, baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo na waandishi wa habari.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo Mhe. Nyalandu amempongeza Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua Prof. Maghembe kuwa Waziri wa Wizara ya Maliasili kwa kuwa ana sifa stahiki za kuongoza Wizara hiyo nyeti.

Aliongeza kwa kusema kuwa Prof. Maghembe ana sifa ya kuwa mhifadhi kwa kusomea na pia ni mhifadhi kwa asili yake hivyo Wizara imepata mtu makini kwenye masuala ya Uhifadhi.

“Natambua umahiri wako katika masuala ya uhifadhi nina imani utapambana na ujangili pamoja na usafirishaji haramu wa magogo kwa kasi inayotarajiwa na wananchi”. Alisema Mhe. Nyalandu.

Kwa upande wake, Waziri aliyechukua nafasi yake Prof. Jumanne Maghembe amempongeza Mhe. Nyalandu kwa kazi nzuri na juhudi aliozoonesha wakati akiwa Waziri wa Wizara hiyo katika kuhakikisha Maliasili zilizopo zinaendelea kuwepo kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho. 

Prof. Maghembe ameongeza kuwa kwa sasa vita kubwa iliyoko mbele yake ni vita dhidi ya ujangili na uharibifu wa misitu ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa rasilimali za misitu kinyume cha sheria. Ameomba ushirikiano kwa wadau wote wa Maliasili nchini kumpa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha anafanikiwa katika vita hiyo.

Pamoja na mambo mengine taarifa hiyo ya makabidhiano inaelezea kazi zilizokwisha kufanyika katika kipindi cha utawala uliopita, kazi zinazoendelea na zilizopo kwenye mpango wa utekelezaji pamoja na changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya Maliasili na Utalii ikiwemo Ujangili na uvunaji pamoja na usafirishaji wa magogo. 
(Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii)

WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAMPOKEA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MH. HAMAD MASAUNI

$
0
0
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni wa pili kushoto akipokelewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mbarak Abdulwakil wa watatu kulia mara baada ya Naibu waziri huyo kupokea Ua alilokabidhiwa na watumishi wa wizara hiyo ikiwa ni ishara ya kukaribishwa wizarani hapo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kumuapisha kushika wadhifa huo Ikulu jana jijini Dar es Salaam.
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni wa kwanza kushoto akisalimiana na Kamisha wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja wa pili kulia muda mfupi baada ya Naibu waziri huyo kukaribishwa wizarani hapo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kumuapisha kushika wadhifa huo Ikulu jana jijini Dar es Salaam wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni wa pili kushoto akisalimiana na Kamisha wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga wa pili kulia muda mfupi baada ya Naibu waziri huyo kukaribishwa wizarani hapo mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jana jijini Dar es Salaam.

Afya ya Uti wa Mgongo ni Afya ya Mgongo - Dk. Yash Gulati, Apollo Hospital

$
0
0
Dr Yash Gulati, 
Senior Spine and Joint Replacement Surgeon 
at Apollo Hospitals; Delhi
Na Mwandishi Wetu,

Maendeleo katika njia za ufanyaji kazi pamoja na matumizi ya teknolojia yanavyokuwa kwa kasi yanaweza kutufanya tuamini tumepunguza maumivu katika viungo vyetu vya mwili ila si hivyo. Tunatumia magari, mitandao mbalimbali ambayo vizazi vilivyopita havijawahi kuota kutumia. Mabadiliko haya mapya katika maisha yetu yenye msisitizo mdogo katika uimarishaji wa viungo umechukua hatamu na kuathiri maisha yetu kwa maana mwili wa binadamu ni ule ule toka miaka milioni iliyopita. Na hiyo inasababisha kuongeza matukio mengi ya maumivu ya mgongo kwa sababu uti wa mgongo umekwisha athirika.

Watu wengi lazima wakutwe na maumivu ya uti wa mgongo walau mara moja katika vipindi vya maisha yao. Sehemu kubwa inayoathirika katika uti wa mgongo ni sehemu ya chini kabisa na sehemu ya shingoni kwa sababu sehemu hizo ndizo zina beba uzito mkubwa wa mwili kila siku. Sababu nyingine zinazosababisha maumivu ya mgongo ni kuharibika kwa diski, mgandamizo katika vertebra na kudhoofika kwa mifupa kutokana na upungufu wa tishu (osteoporosis) kutokana na umri inaweza kusababisha mgandamizo wa vertebra na kusababisha ufa.

Zipo zaidi ya sababu 100 zinazoweza kusababisha maumivu ya mgongo upande wa chini; matukio ambayo yanaweza kusababisha maumivu mgongoni na yasitambulike. Sababu maalumu ya kuleta maumivu ya mgongo inabaki kuwa ni kuharibika au kuvunjika kwa sehemu zinazounga uti wa mgongo kutokana na pozi baya la ukaaji.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Ligi Kuu ya Zanzibar: Mafunzo na KMKM zatoka Sare ya Bao 1--1

$
0
0
Mchezaji wa Timu ya Mafunzo na Kmkm wakishindana nguvu wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Beki wa timu ya KMKM akimkata mtama mshambuliaji wa timu ya Mafunzo wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1
Kocha Mkuu wa Timu ya KMKM Ali Bushiri (Bush) akiwakaripia wachezaji wake wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Angelline Mabula astukizia baraza la ardhi kinondoni

$
0
0
 Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Angelline Mabula (Mb), akiangalia mafaili ya kesi mbalimbali katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Kinondoni, jijini Dar es salaam, alipofanya ziara ya kushtukiza katika Baraza hilo, kulia kwake ni karani wa baraza hilo, Bahati Rashidi.

 Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Angelline Mabula (Mb), akitazama utunzwaji wa mafaili katika masijala alipofanya ziara ya kushtukiza katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Kinondoni, pembeni yake ni karani wa baraza hilo; Bahati Rashidi
Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Angelline Mabula (Mb), akiongea na Wananchi wa King’azi Juu A, alipofika katika eneo hilo ambalo limekuwa na mgogoro wa ardhi kati ya wilaya ya Kinondoni, Kisarawe na Ilala.



Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images