Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1070 | 1071 | (Page 1072) | 1073 | 1074 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Picha kwa hisani ya TFF

  0 0

  Telecom Company, Halotel has celebrated Christmas in style with its customers in the regions by organizing five epic concerts in five different regions, dubbed Hallo Xmas.

  The concerts, which have attracted thousands of fans that came to witness top artists preforming in their backyards aimed to entertain and connect with their customers, took place in Tukuyu, Ruangwa, Moshi Vijijini, Chato and Mpwapwa.


  In Tukuyu, the concert took place at Bulyaga grounds attracting huge crowds with Makomando and Tunda Man delivering sterling performances.


  With the energetic Makomando on stage, the fans cheered from the first song making the concert live and one that anyone would love to watch again.
  Chato residents also had the privilege to witness Shetta and Baraka Da Prince on stage, at the event that took place at Stand ya Zamani.


  In Ruangwa, the concert took place at Likangala Primary school grounds with Amin and Matonya dominating the stage with their hit songs, while in Mpwapwa the local residents had Madee and Malaika on stage.


  The talk of town on Friday and a place to be for any reveler in Kahe village in Moshi Rural was Kahe grounds to witness unmatched performances from Dancer turned Musician, Msami and Shilole.


  Ms Halima Sanare from Kahe village was full of praises for Halotel for bringing such a big concert to a remote village like Kahe.‘Most brands would prefer doing concerts like these in urban areas, but Halotel is different, and such uniqueness is even found in their services’ said Miss Halima.

  On his part, Halotel Managing Director, Nguyen Thanh Quang, they were pleased that the objective of ensuring every Tanzanian is connected to the widest 3G coverage of their network is being realized and as such they aimed to thank Tanzanians for welcoming their company in Tanzania.

    
  ‘We thank Tanzanians for their overwhelming response to the concerts and of course our customers for the great welcome they have given our network and the belief they have had in us’ said Quang, who also noted that concerts of these caliber will be a trademark of their brand.


  0 0

   Baadhi ya wazee wanaotunzwa katika kituo cha Elders, Kilichopo Bukumbi Mkoa wa Mwanza wakitafakari baada ya kukabidhiwa misaada ya magodoro na vyakula mbalimbali na Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa,Ikiwa ni utekelezaji wa kutoa misaada mbalimbali kwa wahitaji kupitia mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni hiyo”Vodacom Foundation” kwa ajili ya sikukuu za Chrismasi na Mwaka mpya,kupitia progamu yake ya Pamoja na Vodacom inayofanyika kila mwaka wakati wa msimu wa sikukuu. Msaada huo uligharimu jumla ya shilingi Milion 27/-
  Mkuu wa kanda ya ziwa wa Vodacom Tanzania, Dominician Mkama(kushoto)akimkabidhi moja ya zawadi ya godoro Mzee mtoto Rajabu Lugwisha anayeshi katika kituo cha wazee cha Elders kilichopo Bukumbi jijini  Mwanza, kwa ajili ya sikukuu za Chrismasi na Mwaka mpya,Msaada huo ulitolewa pamoja na vyakula mbalimbali na mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni hiyo”Vodacom Foundation”kupitia progamu yake ya Pamoja na Vodacom unaotoa misaada mbalimbali wakati wa msimu wa sikukuu. Msaada huo uligharimu jumla ya shilingi Milion 27/-

   Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Village of hope kilichopo Mkoa wa Mwanza,wakiwa na nyuso za furaha baada ya kukabidhiwa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali na Mkuu wa kanda hiyo wa Vodacom Tanzania,Dominician Mkama(hayupo pichani)kwa ajili ya sikukuu za Chrismasi na Mwaka mpya,Msaada huo ulitolewa na mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni hiyo”Vodacom Foundation”kupitia progamu yake ya Pamoja na Vodacom unaotoa misaada mbalimbali wakati wa msimu wa sikukuu. Msaada huo uligharimu jumla ya shilingi Milion 27/-
   Mkuu wa kanda ya ziwa wa Vodacom Tanzania, Dominician Mkama(kulia)akimkabidhi moja ya zawadi mtoto Rajabu Sanga(4)anayelelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Village of hope kilichopo Mkoa wa mwanza kwa ajili ya sikukuu za Chrismasi na Mwaka mpya,Msaada huo ulitolewa na mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni hiyo”Vodacom Foundation”kupitia progamu yake ya Pamoja na Vodacom unaotoa misaada mbalimbali wakati wa msimu wa sikukuu. Msaada huo uligharimu jumla ya shilingi Milion 27/-
  Afisa mfawidhi makao ya wazee wasiojiweza wa kituo cha wazee cha Elders kilichopo Bukumbi jijini  Mwanza,Michael Bundala(kulia)akipokea misaada ya vyakula,magodoro 111 pamoja na Neti za kuzuia Mbu kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa,Dominician Mkama ikiwa ni utekelezaji wa kutoa misaada mbalimbali kwa wahitaji kupitia mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni hiyo”Vodacom Foundation” kwa ajili ya sikukuu za Chrismasi na Mwaka mpya,kupitia progamu yake ya Pamoja na Vodacom inayofanyika kila mwaka wakati wa msimu wa sikukuu,Msaada huo uligharimu jumla ya shilingi Milion 27/-

  0 0


   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Chama wakati alipowasili Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja katika Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar leo
   Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa siku moja wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar wakiwa katika mkutano chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Sheinuliofanyika leo  katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiendesha Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar uliofanyika leo  Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja(kushoto)  Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai
   Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri  Kuu ya CCM Zanzibar (NEC) wakifuatilia kwa makini Mkutano wa siku moja uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein
  Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa siku moja wa  Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar wakiwa katika mkutano chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein uliofanyika leo  katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja. Picha na Ikulu

  0 0
 • 12/27/15--06:48: TANZIA

 • Ndugu Crammer Chiduo wa Tabata Dar es salam anasikitika kutangaza kifo cha kaka yake Dr Elizer Chiduo kilichotokea siku ya Jumamosi tarehe  27/12/15 katika Hospitali ya Taifa  ya Muhimbili jijini Dar es salaam. 

  Misa ya kumuombea marehemu pamoja na kutolewa kwa heshima za mwisho kwake itafanyika nyumbani kwake Chuo Kikuu cha Dar es salaam Jumatatu tarehe 28/12/15 kabla ya kuanza safari ya kuelekea Kilosa mkoani Morogoro  katika kijiji cha Magubike kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumanne tarehe 29/12/15. 

   Bwana alitoa na Bwana ametwaa
   jina lake na  Lihimidiwe.

   Amen

  0 0

   Wafanyakazi wa Kupatana.com na wateja wao walikula na kunywa. Kupatana.com ni website ya matangazo madogo madogo ya bidhaa mbalimbali kutoka kwa wauzaji hapa Tanzania. Website hii ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 2013 ambapo wakati wa kuanzishwa kwake ilikuwa ikitembelewa na watu takriban elfu tatu kila siku.
  Burudani ya mziki vilikuwepo vya kukata na shoka.

  0 0
  0 0

   Shaban Ibrahim akimshika bukta Didier Kavumbagu.
   Uniwezi.....
   Kavumbagu akimtoka Shaban Ibrahim.
  Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco (kulia) akichuana na beki wa Kagera Sugar, Shaban Ibrahim katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam. Azam ilishinda 2-0.
  Golikipa wa Kagera Sugar, Agathony Anthony akiokoa moja ya hatari langoni mwake. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  Mwandishi Wetu

  Baada ya kilio cha muda mrefu, hatimaye, wakulima wadogo 21,000 walio katika vikundi 89 vya ushirika katika Kata ya Igomaa, mkoani Iringa keshokutwa wanatarajiwa kupatiwa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shbilioni 1 kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) nchini kwa ajili ya maendeleo ya shghuli zao za kilimo.

  Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi wa Mikopo na Usimamizi wa Biashara wa benki hiyo, Robert Pascal alisema maandalizi kwa ajili ya utoaji wa mikopo hiyo yamekamilika.

  Wakulima hao wapatewa mikopo hiyo keshokutwa Jumatano (Desemba 30) mwaka huu kijijini kwao Igomaa, baada ya kukamilisha mafunzo na kuandika andiko la mradi na itatolewa kijijini kwa wakulima hao Igomaa lengo likiwa pia kuwachochea wengine kutumia huduma za benki hiyo.

  Pascal alisema, mikopo kwa wakulima hao ni mwanzo wa utekelezaji wa malengo ya benki hiyo ambayo si ya kibiashara ya kuwasaidia wakulima waingie katika mnyororo wa thamani wa mazao yao na kufuta dhana kuwa wakulima hawakopesheki.

  “Lengo ni kuwawezesha wakulima hao kutoka katika kilimo cha kujikimu hadi cha biashara” alisema na kuongeza kuwa mikopo hiyo kwa sasa imeanza kutolewa kwa wakulima na wengine watafuata katika mikoa mingine mitano.

  Aliitaja mikoa hiyo kuwa ukiacha Iringa ni pamoja na Njombe, Pwani, Tanga na Dar es Salaam na mkazo katika mikopo hiyo kwa sasa umewekwa kwa wakulima wa mpunga na mahindi pamoja na wadau wengine muhimu ikiwa ni pamoja na wakulima wa mashamba makubwa.

  “Wakulima wa mashamba makubwa pia ni walengwa wetu hususan wale ambao wamekuwa na msaada kwa wakuima wadogo wanaowazunguka” alisema na kuongeza kuwa mikopo hiyo ni ya kwanza toka kuanzishwa kwa benki hiyo ambayo ina mtaji wa zaidi ya sh60 bilioni.

  Alisema fedha hizo ni taslimu achilia mbali zaidi ya zingine sh35 bilioni ambazo zipo katika utaratibu mwingine na lengo ni kuhakikisha baada ya miaka itano inakuwa na mtaji wa zaidi ya sh800 bilioni baada na haipo katika kuhudumia wateja wa amana za kila siku kama ilivyo benki zingine.

  Alisema mikopo hiyo itatolewa na wakuima watafanya marejesho baada ya kuvuna na wale ambao iatokea bahati mbaya wakaumbwa na majanmga ya binadaamu kama ukame na majanga mengine kuna utaratibu ambao utafuatwa na wataendelea kukopeshwa ili kufidia pengo hilo.

  “Tunatoa mikopo ya aina tatu na yote riba yake ni nafuu sana wastani wa tarakimu moja na italipwa kwa awamu na sio wote kwa mkupuo na walengwa kwa sasa ni wakulima wadogo wadogo walio katka vikundi na wanaosaidiwa na wakulima wakubwa” alisema Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa benki hiyo, Francis Assenga.
  Mkurugenzi wa Mikopo na Usimamizi wa Biashara katika Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Robert Pascal akizungumza kuhusiana na mikopo kwa wakulima wa kijiji cha Igomaa ambayo itaanza kutolewa keshokutwa, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika, jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa benki hiyo, Francis Assenga.
  Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Francis Assenga akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, kuhusiana na mikopo kwa wakulima wa kijiji cha Igomaa ambayo itaanza kutolewa keshokutwa
  Ofisa Habari wa Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Saidi Mkabakuli akieleza mzunguko wa thamani kwa wakulima ambao wataanza kukopeshwa na benki hiyo kwa ajili ya kuboresha shughuli zao wakati wa mkutano na wanahabari, jijini Dar es Salam juzi

  0 0

  Serikali imesema ifikapo mwaka 2018 Mfumo wa umeme katika Mkoa wa Kagera utakua umeingizwa kwenye Gridi ya Taifa. Hayo yalisemwa jana tarehe 27 Desemba na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipofanya ziara mjini Bukoba, Mkoani Kagera ili kukagua miundombinu ya umeme. 
   Ilielezwa kwamba Mkoa huo kwa sasa unapata umeme kutoka nchini Uganda ambao umekuwa ukikatika mara kwa mara na hivyo kulilazimu Shirika la TANESCO kutumia mitambo yake inayotumia mafuta ambayo hata hivyo haikidhi mahitaji ya umeme ya Mkoa. 
   Profesa Muhongo aliliagiza shirika hilo kuhakikisha linaharakisha taratibu za kuunganisha mkoa wa Kagera kwenye umeme wa Gridi ya Taifa.
  "TANESCO ni lazima muharakishe mipango ya kuunganisha mkoa huu kwenye gridi ya taifa ili kuwapatia wananchi huduma ya umeme wa uhakika," aliagiza. 
  Aidha, Profesa Muhongo aliiagiza TANESCO kuhakikisha mafuta kwa ajili ya kuendeshea mitambo hiyo yanakuwepo yakutosha kwa muda wote. 
   Alisema ifikapo mwaka 2025, Tanzania itaingia kwenye uchumi wa kati ambao utatokana na uwekezaji mkubwa kwenye viwanda ambavyo vitahitaji umeme wa kutosha na uhakika. 
   Mbali na hilo, Profesa Muhongo aliliagiza Shirika la Tanesco mara baada ya mkataba uliopo wa kuuziana umeme kati ya Tanzania na Uganda kuisha, wahakikishe wanaingia mkataba wa muda mfupi mfupi lengo likiwa ni kuepusha kuwa ndani ya mkataba wakati tayari mkoa huo utakua kwenye gridi ya taifa. 
   Akielezea hali ya umeme mkoani humo, Meneja wa Tanesco Kanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga alisema kwa sasa Tanzania inanunua umeme kwa gharama ya senti za Marekani 8.4 kwa kila unit. Alisema Tanzania inao mkataba wa kununua umeme kutoka Uganda kiasi cha megawati 10 ambao unahudumia wilaya za Bukoba Mjini na Vijijini, Karagwe, Muleba na Misenyi.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto mbele) akimsikiliza  Mhandisi wa kituo cha kufua umeme wa dharura cha Kibeta- Bukoba mjini, Mhandisi Filbert Mlaki wakati wa ziara yake kituoni hapo leo (27 Desemba, 2015). Kituo hicho chenye mitambo minne kinao uwezo wa kuzalisha megawati 2.1 ambacho hutumiwa pale umeme wa kutoka Uganda unapokatika.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella kabla ya kuanza ziara ya kukagua miundombinu ya umeme mkoani humo.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kushoto) akimsikilizaMhandisi Filbert Mlaki.
  Waziri wa nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akikagua moja ya mtambo wa kuzalisha umeme wa Kituo cha Kibeta

  0 0  0 0


  0 0

  Na Magreth  Kinabo- MAELEZO

  Serikali imesema kwamba tamko lake lilitolewa hivi karibuni kuhusu matangazo ya Tiba Asili na Tiba Mbadala palepale kwa kuwa lengo lake ni kuboresha huduma hiyo. Hivyo kama  kuna mtoa huduma ambaye amekwazika na tangazo hilo ipo tayari kuzungumza naye.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamko hilo kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

  Tamko hilo ambalo lilitolewa Desemba 24, mwaka huu,ambapo limepiga marufuku  matangazo yote yanayohusu tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
   Ambapo kwa wale wenye vibali wanatakiwa kuviwasilisha vibali na matangazo yao kwenye Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ili vifanyiwe mapitio.

  Tamko hilo  liliendelea  kufafanua kwamba  utoaji wa elimu ya afya kwa umma unaofanywa na watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii umepigwa marufuku hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa.

  ‘Watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini kote wanaagizwa wawasilishe kwenye Baraza nyaraka zote muhimu ndani ya wiki mbili kuanzia leo Desemba 2015. Baadhi ya nyaraka hizo ni zile zinazohusu kuuza dawa za asili na tiba mbadala, nyaraka za kumiliki mashine zinazotumika katika kufanya uchunguzi katika tiba asili na tiba mbadala,’ lilieleza tamko hilo.

  Tamko hilo lilifafanua kwamba  Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala linaagizwa katika kipindi cha siku 14 kuanzia leo 24 Desemba 2015, lipitie nyaraka zote zikapowasilishwa zinazohusu usajili wa watoa huduma, usajili wa vituo vyao, ikiwa ni pamoja na maduka ya dawa za asili na dawa za tiba mbadala, usajili wa dawa zote zinazotumika katika huduma hizo na usajili wa mashine zote zinazotumika katika huduma za tiba asili na tiba mbadala.

  Aidha  akizungumzia kuhusu tangazo hilo, Waziri   Ummy alisema  ‘Mimi  niko tayari kuzungumza na mtoa huduma ambaye amikwazika na tangazo hili, ili aweze kueleza ni sababu zipi zinazomfanya asisajiliwe.  Tunafanya hivi kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu,’ alisisitiza.

  Aliongeza kwamba Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala  Namba 23 ya Mwaka 2002 inaeleza  wazi.

  Kwa mujibu wa Waziri huyo alitaja idadi ya watoa huduma hiyo kuwa ni  wako 75,000 kwa takwimu za nchi nzima.
  Naye Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili  na Tiba Mbadala, Dkt. Edmund Kayombo alisema hadi sasa hawajapokea mrejesho wa tamko la tamko  hilo la  Serikali.

  Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama  Vya Tiba Asili Tanzania(SHIVYATIATA), Abdulrahaman  Lutenga alisema  hakuna mganga yoyote aliyepinga tamko hilo na Serikali, hivyo tamko lililotolewa  hivi karibuni la kupinga agizo hilo si halali kwa kuwa halikupitia katika shirikisho hilo.
  ‘ Hatutambui kampuni hii iliyotoa tamko la kupinga tangazo la Serikali kwani ya mtu binafsi yenye wanahisa 11,’ alisema Lutenga.
  Akizungumzia kuhusu hatima ya tamko hilo, Dkt. Kayombo alisema baada ya siku walizotoa  kumalizika  watatangaza hatua zipi zitachukuliwa kama vile kuwaondoa wasiofuata sheria.

  0 0

  Leo tarehe 28 Desemba, Profesa Mark Mwandosya amesherehekea kufikisha miaka 66 tangu kuzaliwa. Amesherehekea sikukuu yake hiyo akiwa kijijini kwake Lufilyo, Busokelo Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya. Anamshukuru Mwenyezi Mungu na Watanzania wenzake kwa baraka anazoendelea kupata. 
  Profesa Mark Mwandosya  akiwa akijiandaa kukata keki ya asili pamoja na maandazi wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa leo tarehe 28 Desemba, akiwa pamoja na ndugu zake ambao walimtayarishia keki hiyo.
  Profesa Mark Mwandosya akilishwa kipande cha keki na Mkewe, Mama Lucy Mwandosya wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa leo tarehe 28 Desemba.

  0 0


  Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (mbele kulia) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Selestine Gesimba wakati wa mapokezi yake leo tarehe 28 Desemba 2015 katika ofisi yake mpya Mpingo House mara baada ya kuapishwa Ikulu mapema asubuhi ya leo. Nyuma yake kulia ni naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Ramo Makani na anaeongoza utambulisho katikati yao ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru.
   Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akisaini kitabu cha wageni mara tu baada ya kuingia katika ofisi yake mpya iliyopo Mpingo House mapema leo tarehe 28 Desemba 2015 baada ya kuapishwa Ikulu na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Wanaoshuhudia kulia ni Naibu Wazari wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Ramo Makani na Katibu Mkuu Dkt. Adelhelm Meru (kushoto).
  Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (kushoto) na Naibu Waziri Mhe. Eng. Ramo Makani (kulia) mara baada ya kusaini kitabu cha wageni ofisini kwake mapema leo tarehe 28 Desemba 2015.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0


  0 0


  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akipata ufafanuzi kuhusu namna ya kuhifadhi makontena kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Aloyce Matei (kushoto), mara baada ya kukagua Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Aloyce Matei (wa tatu kushoto), huku Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Eng. Edwin Ngonyani (wa pili kulia), akifatilia.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa na Naibu wake wakikagua mtambo wa kuchunguza makontena (scanner) katika eneo la TPA.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipiga makofi na kufurahia baada ya kuzindua rasmi soko la kisasa la samaki na dagaa katika mwalo wa Kibirizi, Mkoani Kigoma leo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua dagaa walioanikwa kisasa katika mwalo wa kibirizi baada ya kufungua rasmi soko la kimataifa la Samaki lililopo Kibirizi, Mkoani Kigoma leo.
  Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini Zitto kabwe akiongea na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya mwalo wa kibirizi.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na wananchi (hawapo pichani)kwenye viwanja vya mwalo wa kibirizi.

  Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Kigoma waliojitokeza kumsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika mwalo wa kibirizi.Picha na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma.

older | 1 | .... | 1070 | 1071 | (Page 1072) | 1073 | 1074 | .... | 3272 | newer