Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

MFUMO WA KUDHIBITI MAFURIKO TANZANIA


TOYOTA AVENSIS FOR SALE

$
0
0
TOYOTA AVENSIS 1.9 cc DEISEL ENGINE MODEL 2005 MANUAL THE CAR IS IN DAR ES SALAAM JUST IMPORT FROM U.K LONDON 
PRICE T.SH. 7.5 MILION

CONTACT.
+255 718 030 320
+255774 659 895 

Asha Salum ‘Kidoa’ ashinda Shindano la Ijumaa Sexiest Girl 2015

$
0
0
IMG_1255 
Video Queen anayefanya pia filamu, Asha Salum ‘Kidoa’ akiwa na tuzo yake ya Ijumaa Sexiest Girl 2015 baada ya kuwafunika Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Vanessa Mdee ‘Vee ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar.

Fainali ya lile Shindano la Ijumaa Sexiest Girl 2015 ilifanyika jana ambapo Video Queen anayefanya pia filamu, Asha Salum ‘Kidoa’ aliibuka kidedea. Kidoa alitangazwa mshindi kufuatia kupigiwa kura nyingi na wasomaji wa Gazeti la Ijumaa hivyo kuwafunika wenzake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Vanessa Mdee ‘Vee Money’. 
 Akizungumza na Risasi, mratibu wa shindano hilo lililodhaminiwa na kampuni ya uandaaji na usambazaji wa filamu ya Hamadombe Distributor, Amran Kaima alisema kuwa, ushindani ulikuwa mkubwa kwani wasanii wote walioshiriki walikuwa wakali ile mbaya. 
 “Kidoa amefanikiwa kuibuka mshindi baada ya kupigiwa kura nyingi. Atapokea tuzo, cheti pia atapewa ofa ya kutengeneza nywele kwenye saluni ya Bulldozer iliyopo Kigamboni jijini Dar kwa miezi sita pamoja na kufanyiwa shopping ya nguvu,” alisema Amran.
IMG_1250 Kidoa (katikati) akiwasalimia mashabiki baada ya kutangazwa mshindi wa Ijumaa Sexiest Girl 2015.IMG_7945Kidoa akikabidhiwa tuzo na Mkurugenzi wa Hamadombe Distributor, Fatuma Makame.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

THOMAS MASHALI AMSHINDA FRANCIS CHEKA KWA POINTI KWENYE MPAMBANO WAO MJINI MOROGORO

$
0
0
 Bondia Thomas Mashali (kushoto)  akioneshana umwamba na Francis  Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika Katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana siku ya Krismasi. Mashali alishinda kwa point mpambambano huo usiokuwa wa ubingwa wa raundi kumi 
Bondia Thomas Mashali akikwepa konde la  Francis  Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika Katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana siku ya Krismasi. Mashali alishinda kwa point mpambambano huo usiokuwa wa ubingwa wa raundi kumi. Picha na Super D  Boxing coach

Waraghabishi wakoleza kasi ya mabadiliko wilayani Kishapu

$
0
0
 Watendaji wa Kituo cha Maendeleo cha Jamii ya Uchunga wilayani Kishapu wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi mbele ya jengo la kituo hicho likiwa limekamilika kutokana na michango yao ya fedha na nguvu kazi. 

Na Krantz Mwantepele ,Kishapu 

Mabadiliko katika jamii yoyote kwa kiasi kikubwa huchangiwa na ongezeo la mahitaji ya binadamu katika mambo mbalimbali. Kwamba, kadri dunia inavyopitia mabadiliko, kadiri ile ile changamoto, mahitaji na huduma katika jamii husika huongezeka.

Ili kufikia malengo yanayotokana na misukumo na mageuzi yasiyokwepeka, binadamu amelazimika kubuni mikakati mbalimbali ya maendeleo. Si hivyo tu, mabadiliko haya yamemfungulia binadamu fursa ya uthubutu wa kujaribu mambo mbalimbali, siyo tu kwa faida yake, bali jamii nzima inayomzunguka.

"Sikutegemea kama siku moja katika maisha yangu nitapata wazo ambalo lingebadili na kushawishi watu kuchukua hatua kwa mustakabali wa jamii.” 

Hiyo ni kauli ya mraghbishi Revocatus Richard ambaye pia, kitaaluma ni mwalimu katika shule ya msingi Uchunga. Richard alitoa kauli hiyo baada ya kupitia mafunzo ya uraghbishi na mwalimu mwenzake, Restusta Katobesi, ambao baadaye kwa pamoja, walianzisha Kituo cha KIMAJU (Kituo cha Maendeleo cha Jamii ya Uchunga) kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji na wananchi. Na hilo ndiyo lilifanya achaguliwe kuwa Mkurugenzi wa kituo hicho. 

KIPANYA LEO

Kampuni ya Ageco Energy & Construction Ltd yafunga mwaka kwa Kufunga Mtambo Mkubwa wa Sola Hospitali ya Mkoa Singida.

$
0
0


 Kampuni Ageco Energy & Construction Ltd ni kampuni ya kitanzania inayotoa huduma mbali mbali za ukandarasi ikiwemo ufungaji wa mitambo ya umeme wa jua (solar power) kwa watu binasfi, taasisi za umma, mashirika ya nje, na wateja wengine toka sekta binasfi.  Hivi majuzi Ageco ilikamilisha mradi wake wa mwisho wa mwaka kwa kufunga mtambo wa umeme wa sola ujulikanao kitaalamu kama solar hybrid backup system katika hospitali ya Mkoa wa Singida. 

 Mtambo huu wenye uwezo wa kuendesha vifaa vyenye jumla ya Kilowatt 15.7 utasaidia kutoa umeme kwa muda wa masaa 24 katika jingo la maabara la hospitali ya mkoa wa Singida hata kama umeme wa gridi ya taifa ukikatika. Mwezi wa Juni 2015, Ageco pia walifunga mtambo mwingine kama huu katika hospitali kuu ya mkoa wa Rukwa iliyoko Sumbawanga. Miradi hii imepewa ufadhili na Shirika la Misaada toka nchini Marekani linaloitwa Abbott Fund ambalo tayari limetoa misaada mingi katika kuimarisha sekta ya afya nchini Tanzania.

Ageco ni kampuni ya kitanzania inayotoa huduma za ufungaji wa mitambo ya umeme wa kawaida, umeme wa jua, umeme unaotokana na mabaki ya takataka (biomass) pamoja na huduma za ukandarasi wa majengo/nyumba na barabara.  Bei zao ni nafuu na wanatoa huduma kwa ustadi na weledi mkubwa. Wanapatikana kwa njia ya simu kupitia namba 0758 733 333 au 062 222 064. Vile vile wanapatikana kwa email kupitia info@agecoenergy.com. Ofisi zao ziko barabara ya Bima, Mikocheni B, jijini Dar es Salaam. Unaweza pia kutembelea tovuti yao www.agecoenergy.com kwa maelezo zaidi kuhusiana na huduma zao.

PROFESA MUHONGO AWATOA HOFU WACHIMBAJI WADOGO

$
0
0
Serikali imedhamiria kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa madini nchini ili kukuza uchumi wa Taifa, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kwenye kikao chake na wachimbaji wadogo wa madini kutoka mikoa ya Simiyu na Mara. 
Profesa Muhongo alisema sekta ndogo ya madini nchini inao mchango mkubwa kwenye pato la Taifa wa kuondoa umasikini nchini na hivyo Serikali kwa jitihada mbalimbali itahakikisha wachimbaji wadogo wananufaika ipasavyo pamoja na kuchangia ukuaji wa uchumi. 
“Tutawakaribisha wachimbaji wakubwa lakini tunataka na nyie wachimbaji wadogo mchangie ukuaji wa uchumi; mchangie upatikanaji wa ajira kwa vijana wetu,” alisema. 
Aliongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa uchimbaji mdogo wa madini, Serikali imeamua na imedhamiria kuwaheshimu na kuwatambua wachimbaji wadogo.
 Waziri Muhongo aliwataka wachimbaji hao kubadilika na sio kuendelea kulalamika badala yake wajitume na kufanya kazi kwa uadilifu huku wakitanguliza suala la uzalendo na pia kuamini kwamba Serikali inayo nia thabiti ya kuwasaidia. 
Aliwatoa hofu na kuwahakikishia kuwa Serikali inaendelea na juhudi za kuwatafutia maeneo zaidi ya uchimbaji madini na vilevile soko la uhakika ili kuongeza kipato chao na wakati huo huo kuliingizia taifa mapato zaidi. 
"Msiwe na wasiwasi, fanyeni uchimbaji wa uhakika; Serikali hii ni yenu; itawasaidia masuala mbalimbali pamoja na kuwatafutia ruzuku, masoko, mafunzo na pia kuwatafutia maeneo zaidi kwa ajili ya shughuli zenu," alisema. 
Aliwataka kuachana na fikra potofu kuwa Serikali haiwajali badala yake waiamini Serikali yao kwamba ipo kwa ajili ya kuwasaidia na huku wakijituma kwa kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uaminifu. 
“Matatizo ya zamani ya uchimbaji mdogo tuachane nayo, lazima ulipende taifa lako; huwezi ukawa mchimbaji wa dhahabu ya Tanzania unaipeleka Kenya; halafu inauzwa kama imetoka humo hili ni kosa kubwa,” alisema. 
Aliwaasa kuepuka kutorosha madini nje ya nchi; aliongeza kuwa Shirika la Madini la Taifa (Stamico) limepewa jukumu la kuwatafutia bei ya madini kusudi madini yanayopatikana nchini yauzwe nchini na yanunuliwe hapa hapa; iwe ni malighafi ya Tanzania. 
Aidha, Profesa Muhongo alimuagiza Meneja wa Tanesco Kanda ya Ziwa Mhandisi Amos Maganga kutembelea maeneo yote ya wachimbaji wadogo ili kujua mahitaji yao ya umeme pamoja na kutathmini namna ya kuwaunganisha na huduma ya umeme. 
 Rais wa Wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania, John Bina akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wanne kutoka kushoto).
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza wakati wa kikao chake na wachimbaji wadogo wa madini, Mkoani Mara.

KIOTA CHA MARAHA CHA CITY SPORTS LOUNGE CHAZINDULIWA UPYA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
jo1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concept na Gazeti la Jambo leo Bw. Juma Pinto akiwa katika picha ya pamoja na DJ John Peter Pantalakis kushoto na DJ Masoud Masoud kwenye uzinduzi wa kiwanja cha City Sports Lounge Posta jirani na Askari Monument jijini Dar es salaam maarufu kwa kuonyesha mipira ya ligi mbalimabli za Duniani kote. Uuzinduzi huo umefanyika alhamis wiki hii na kuhudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali. uzinduzi huo umefanyika kufuatia ukarabati na uboreshaji wa mambo mbalimbali katika klabu hiyo yaliyofanyika kwa muda wa mwezi mmoja.
jo2
Kutoka kulia ni Mwesa, Ally na Helman wakibadilishana mawazo huku wakishuhudia zunduzi huo.
jo3
Chacha Maginga na wadau wenzake wakipozi kwa picha.
jo4
Wahudumu waliovalia sare nzuri wakwasikiliza wageni waalikwa katika uzinduzi huo.

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

$
0
0

Watu wawili wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Nzega,huku sababu kuu ikielezwa kuwa ni wivu wa mapenzi:https://youtu.be/SjQN8nQ-GSQ

Wakati watu wengine wakifungua zawadi za siku kuu wengine wapigana na kupelekwa hospitali hii leo : https://youtu.be/CNiEYQDX9NI

Askofu mkuu wa kanisa la KKKT mkoa wa Ruvuma amewataka wakristo kuchunga midomo yao ili kuepuka mifarakano:https://youtu.be/EZhmGAqYE2M

Vijana nchini Tanzania wahimizwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kuacha kuagiza bidhaa kutoka nchi za nje: https://youtu.be/PNsBQT224uo

Bondia maarufu Thomas Mashali amefanikiwa kulipiza kisasi na kuibuka mshindi baada ya kumtwanga mangumi Francis Cheka:https://youtu.be/kdQGmITQ_qc

Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya lori mkoani Tanga, yaongezeka na kufikia 5 baada ya majeruhi mwingine kufariki hii leo.https://youtu.be/iA6uhiGFGCE

Wajawazito na watoto katika hospitali ya wilaya ya Maswa waelezwa kulazimika kulala wawili wawili katika kitanda kimoja kutokana na ufinyu wa wodi huku wakitoa rai kwa serikali Kufungua majengo ya wodi mpya zilizokamilika. https://youtu.be/4UGrJ-XO5ns

Serikali ya watu wa China yafadhili mradi wa maji safi katika wilaya ya Lindi na kuondoa kero kubwa iliyokuwa ikiwakabili wananchi kwa muda mrefu.https://youtu.be/F-ihrtUSTWg

Afya za wakazi wa Tabora zaelezwa kuwa hatarini kufuatia hali ya uchafu uliokithiri katika soko kuu la manispaa hiyo. https://youtu.be/JRtSDMDmJQM

Wakazi wa kata ya Mwandege wilayani Mkuranga mkoani Pwani watakiwa kuwa subira ili sheria ifuate mkondo wake baada ya mwekezaji mwenye asili ya Asia kuchukua kimabavu maeneno yao na kuharibu mazao yao.https://youtu.be/kRp5DMTSkvU

Wananchi wa manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wafanya usafi katika maeneneo mbalimbali wakishirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama.https://youtu.be/V079o04KIEg

Waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo awataka wananchi wa jimbo lake kuanzisha mfuko maalum wa kushughulikia maendeleo ya elimu badala ya kuitegemea serikali katika kila jambo. https://youtu.be/VinS-UwKh_Y

Maafisa maliasili wilaya ya Bukombe mkoani Geita walalamikiwa kukamata ng’ombe wa wafugaji zaidi ya 1000 na kuwafungia zizini kwa muda wa siku 5 bila malisho. https://youtu.be/ripm4lZ_qqU

Mwanadiplosia wa muda mrefu na katibu mkuu mstaafu wa umoja wa nchi huru za Afrika OAU asema mgogoro wa Burundi umelitia doa bara la Afrika.https://youtu.be/T-1yySKbwsA

Wafanyabiashara wa matunda ya jumla katika soko kuu la matunda mkoani Kigoma waiomba serikali kupitia SIDO kujenga viwanda vya usindikaji matunda ili kuepusha hasara wanayoipata kwa matunda kuoza.https://youtu.be/QKwcO_bGuUo

Wakulima wa zao la maharage machanga mkoani Arusha waiomba serikali kuwasidia kupata soko la uhakika wa zao hilo kwa kuwaandalia mfumo rasmi wa kukutan na wateja moja kwa moja. https://youtu.be/XI2cOiVEdFE

VIMBWANGA VYA MISS UNIVERSE 2015 - MC STEVE HARVEY ALIPOCHEMSHA KUTANGAZA MSHINDI...

WANANCHI MBEYA WAFAIDI BAADA YA GARI LA SODA KUPIGA MWELEKA......

YANGA YAIBONYEZA MBEYA CITY BAO 3-0 BONYEEEEE...

$
0
0
Mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke akichuana na beki wa Mbeya City, John Kabanda  katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 3-0. (Picha na Francis Dande).
 Mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke akiwatoka mabeki wa Mbeya City.
 Wachezaji wa Mbeya City wakimzonga mwamuzi Jeonesia Rukyaa kutoka Kagera baada ya Yanga kupata bao la kwanza.
 Donald Ngoma wa Yanga akichuana na Haruna Shamte.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA ZANZIBAR DKT ALI MOHAMED SHEIN IKULU DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimlaki Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein  Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 26, 2015
  Rais Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein  Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 26, 2015
RaisRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein  baada ya mazungumzo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 26, 2015. PICHA NA IKULU

NEEC yawadhamini wajasiriamali 185 milioni 244.5 Benki ya posta

$
0
0
Benki ya Posta Tanzania imetoa mikopo ya jumla ya million 244,500,000.00 kwa wajasiriamali 185 kwa ajili ya kukuza shughuli zao na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa. Mikopo hii imedhaminiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) 
 Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Anna Dominick, amewambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa wajasiriamali hao 185 ni wanachama wa vicoba vinane. 
 “Kati yao wanawake 137 sawa na asilimia 74 na wanaume 48 sawa na asilimia 26,” na mkopo huu ni matokeo ya makubaliano kati baraza na benki yaliyofikiwa julai 14, 2015,alisema Bi. Dominick. Amesema utoaji wa mikopo hii ni utekelezaji wa makubaliano ya Julai mwaka jana umeanza kwa kunufaisha baadhi ya vicoba katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, na kuongeza “huu ni mwanzo tu. Tutahudumia wajasiriamali wanaokidhi vigezo nchi nzima.
” Vikundi vya vicoba vivilivyopata mikopo hiyo alivitaja kuwa ni Juhudi, Tayeeo Vicoba, Mwanga, Maendeleo, Mzingira, Umoja ni Nguvu, Gosofu na Nyota Njema. 
 Bi Dominick ameeleza kuwa makubaliano kati ya baraza na benki yanalenga kwenye kuwawezesha wananchi ili kukabiliana na tatizo la ajira nchini na kuongeza kwamba vicoba ni taasisi ndogo za kifedha zinazofanya kazi nzuri katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana.
  Kwa mujibu wa takwimu za Ofisi Kuu ya Takwimu ya Taifa ya mwaka 2011 inakadiriwa vijana 800,000 hadi milioni moja wanapigania nafasi za ajira 60,000 katika sekta ya umma na 300,000 katika sekta binafsi 
 Bi. Dominick amesema kwa takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kwamba kiasi cha vijana kati ya 400,000 hadi 600,000 wanakuwa hawana ajira katika soko la ajira kila mwaka. 
“Hii ndiyo sababu tunayapa uzito mkubwa makubaliano haya kati ya baraza na benki.” Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba Moshingi, amevisifu vikundi vya kijasiriamali vya vicoba na kueleza kwamba mikopo kwa vikundi hivi jambo la msingi katika vita dhidi ya hali duni ya maisha katika jamii. 
 “Benki hii imeweka kipaumbele katika kuwawezesha wananchi kiuchumi na mikopo inayotolewa ni ya riba nafuu ya asilimia 11. Tunaamini mikopo hii itazifanya shughuli za kijasiriamali kuendelea zaidi,alieleza Bw. Moshingi. 
 Bw. Moshingi amesema vicoba na vikundi vingine vijenge utamaduni kuweka akiba na kuanzisha shughuli za kijasiriamali na kurejesha mikopo kwa wakati ili vikope tena na kutoa nafasi ya wateja wengine kukopa. Alisema baraza na benki ni vyombo vya serikali na kwamba mikopo inalenga kukinua wananchi na ili waweze kuinuka kiuchumi na kuchangia uchumi. 
 Mwenyekiti wa Nyota Njema,Bi. Pili Yomba, ambaye kikundi chao kiko Tandika Temeke alisema watatumia mkopo waliopata kukuza mtaji na kulipa marejesho kwa wakati.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba Moshingi (kulia), anafafanua jambo wakati hafla ya kuwakabidhi mikopo wananchama wa vikundi vinanne vya vicoba ambavyo wananchama wake wametimiza sifa za kupata mikopo. Mikopo hiyo imedhaminiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), (Kushoto) ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Anna Dominick.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba Moshingi (kushoto) akimkabidhi hundi Mkurugenzi wa TYEEO, Bw. Ayubu Luhunga (kulia). TYEEO ni kati ya vikundi  vinnane vilivyofuzu kupata mikopo ambayo imedhaminiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC.  (Katikati) ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Anna Dominick.

Mashine ya kuvunia nafaka tofauti (COMBINE HARVESTER) inauzwa

$
0
0
Mashine hiinIpo imara sana na inafaa sana kwa mazingira ya hapa kwetu Tanzania na inaweza kuishi muda mrefu na ni rahisi  sana kuifanyia matengenezo pindi inapo haribika... Tumeileta kutoka Denmark na haijatumika hapa Tanzania bei ni rahisi  na ya faida kwani ukivuna msimu moja tu kwa kiasi cha ekari 350 utakua umerejesha hiyo hela,,. Kama ni mkulima ikikupita hii utakuja kuikumbuka kwani ni moja ya zana chache hapa nyumbani.. Mashine hii  ipo MBWENI Daresalaam
BEI NI MIL..34 TSH  

wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani kupinga kufungiwa migodi yao

$
0
0
Wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wanatarajia kuandamana kwa amani ili kupinga migodi yao 19 inayopakana na kampuni ya TanzaniteOne kufungiwa.
 Mwanachama wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite (Marema) Tawi la Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Omary Mandari akizungumza kwenye mkutano wao ambapo waliazimia kuandamana kwa amani kupinga migodi yao 19 kusimamishwa kufanya kazi.
 Mwanachama wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite (Marema) Tawi la Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Zephania Joseph akizungumza kwenye mkutano wao ambapo waliazimia kuandamana kwa amani kupinga migodi yao 19 kusimamishwa kufanya kazi.
Wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye mkutano wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini (Marema) Tawi la Mirerani, ambapo waliazimia kuandamana kwa amani kupinga migodi yao 19 kusimamishwa.

SIMU TV: UCHAMBUZI WA MAGAZETI LEO JUMAPILI

$
0
0


STAR TV: Gwajima aibuka amkana Lowassa, JK akataa nyumba, Magufuli apokea ripoti ya Zanzibar, Magufuli aibua hofu serikalini. Tazama uchambuzi wa kina wa magazeti.https://youtu.be/ISjhdGiq2Fk   

CH10: Waziri mkuu kufanya ziara Kigoma, Prof. Lipumba awa gumzo London, Magufuli azua hofu serikalini, Gwajima amkana Lowassa. https://youtu.be/Nuj5jY8k27Y  

AZAM TV: Yanga ya paa, Manchester united yazama, Simba yabanwa, Mashali afuta ufalme wa Cheka moro, Chelsea yashikwa, Leicester City yazimwa, Samatta kimeeleweka ulaya. Fuatilia habari za magazeti ya michezo.https://youtu.be/8eVa2A6ry3s

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

SIMUTV: Baadhi ya familia wilayani  Mpwapwa mkoani Dodoma zinahangaika kutafuta pesa kwa ajili ya kununulia vyakula kufuatia kupanda kwa gharama za maisha; https://youtu.be/PFFhDlgHT1g

SIMUTV: Chama cha ushirika cha wakulima wa korosho mkoani Lindi kimesema mfumo wa stakabazi umewawezesha kunufaika na zao hilo:https://youtu.be/8pEeK_f2S7g

SIMUTV: Baadhi ya madereva pikipiki waiomba TRA kuwapatia elimu juu ya kubadilishwa kwa namba mpya za pikipiki: https://youtu.be/QJzL6mviErI

SIMUTV: Benki ya wanawake Tanzania kwakushirikiana na mipango miji wamewakwamua wanawake kwa kuwapatia mikopo ya viwanja:https://youtu.be/WQR4YZi_g0A
  
SIMUTV: Wakazi wa mkoa wa Njombe wailalamikia serikali kutokana na mkandarasi kusababisha uharibifu wa mazingira katika maeneo yao:https://youtu.be/Mq6cynfpt_8

SIMUTV: Baadhi ya vijiji vilivyo karibu na ziwa Tanganyika vyakabiliwa na tatizo la maji na kupelekea kutafuta maji kutoka umbali mrefu:https://youtu.be/sdwovGOD-Ls

SIMUTV: Watoto wasio na wazazi na wanaozaliwa na virusi vya ukimwi  waelezwa kukumbwa na matatizo kufuatia jamii inayowazunguka kuwatenga:https://youtu.be/KAnfcct5zVA

Mpiganaji Edwini Mjwahuzi aukacha rasmi ukapera

$
0
0
 Mdau Edwini Mjwahuzi ambaye ni Mpiga picha wa Magazeti ya Kampuni ya Mwananchi, jioni ya leo ameamua kuvunja kibanda cha Makapera na kukimbilia kwenye Mjengo wa wanandoa, kwa kufunga pingu za maisha na Bi. Hildegarda Mashauri kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam.
  Mdau Edwini Mjwahuzi na Mkewe Bi. Hildegarda Mashauri pamoja na Wasimamizi wao wakiwa kwenye ibada ya ndoa, iliyofanyika jioni ya leo kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam.
Mdau Edwini Mjwahuzi akimvisha pete Mkewe Bi. Hildegarda Mashauri, wakati wa Ibada ya Ndoa yao iliyofanyika kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam leo.
 Mdau Edwini Mjwahuzi na Mkewe Bi. Hildegarda Mashauri wakiwa ni wenye furaha tele mara baada ya kufunga pingu za maisha na kuwa mwili mmoja, kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam leo.

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images