Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli atuma salamu za Rambirambi kufuatia kifo cha Askofu Nkalanga

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa kufuatia kifo cha Askofu Mstaafu Plasdus Gervas Nkalanga (OSB) kilichotokea Ijumaa tarehe 18 Desemba, 2015 katika hospitali ya Mtakatifu Joseph Peramiho, Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.

Mhashamu Askofu Nkalanga aliyekua Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba alistaafu uaskofu mwaka 1974 na kujiunga na watawa wabenediktini wamonaki ambapo aliamua kwenda kuishi katika Abasia ya Hanga iliyopo katika Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.  

Katika salamu zake Rais Magufuli amesema  Askofu Nkalanga aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96 atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa kuhimiza imani na uchapakazi kazi katika kipindi chote cha miaka 54 ya uaskofu wake na utawa wake akiwa katika Abasia ya Hanga.

Amesema Marehemu Askofu Nkalanga ambaye baada ya kustaafu aliamua kuingia katika utawa akianzia katika ngazi ya chini kabisa ya Unovisi hadi alipofunga nadhili za milele za utawa mwaka 2009, ameacha mfano mzuri unaohimiza jamii kuishi kwa upendo, unyenyekevu na kutokata tamaa. 

"Kupitia kwako Baba Askofu Ngalalekumtwa napenda kuwapa pole nyingi Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Abate wa Abasia ya Hanga, watawa na waumini wote wa kanisa Katoliki kwa kupoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kanisa na jamii kwa ujumla" amesema Rais Magufuli.

Rais John Pombe Magufuli amemuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu Mhashamu Askofu Mstaafu Plasdus Gervas Nkalanga mahali pema peponi, Amina.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU



20 Desemba, 2015

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAKAGUA MIRADI YA VITUO VYA KUZALISHA UMEME VYA KIDATU NA KIHANSI

$
0
0
Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Florence Mwanri (aliyevaa nguo nyeusi) akiangalia na kupata maelezo kutoka kwa Injinia wa kituo Bw. Rajabu Kindunda (wa tatu kulia) kuhusu Bwawa la Kidatu ambalo maji hukusanywa kutoka mto Rufiji kabla ya kutumika kwa ajili ya kuzalisha umeme. Wengine pamoja nae ni wataalamu kutoka Tume ya Mipango na TANESCO.
Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Florence Mwanri (aliyevaa nguo nyeusi) akiangalia eneo la mradi wa kuzalisha umeme Kidatu na kupata maelezo kuhusu faida na changamoto za mradi kutoka kwa Injinia wa TANESCO kituo cha Kidatu Bw. Rajabu Kindunda (wa tatu kulia). Wengine ni wataalamu kutoka Tume ya Mipango na TANESCO.
Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Florence Mwanri (aliyevaa nguo nyeusi) pamoja na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa Injinia kituo cha Kidatu Bw. Yonah Mwasajone (wa kwanza kushoto) kuhusu Sub Station ambayo baada ya umeme kuzalishwa katika mitambo ya kufua umeme Kidatu hutumika kuuingiza katika Grid ya Taifa.
Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Florence Mwanri (aliyekaa) akipata maelezo kuhusu namna Kituo cha Kihansi kinavyofanyakazi kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambayo imeboresha utendaji kazi kwa wafanyakazi na mitambo ambayo inatumika kuzalisha nishati ya umeme.

MAGUFULI NAMPENDA AMERUDISHA ENZI ZA KARUME NA NYERERE HUYU - MZEE KUNDIHERI, ZANZIBAR

BALOZI WA TANZANIA NCHINI OMAN MAALIM DR ALI AHMED SALEH ALAMBA NONDOZ YA SHAHADA YA UZAMIFU YA FALSAFA YA UDAKTARI (Phd) YA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA(OUT)KATIKA MAHAFALI YA 29 HAPO TAREHE 16/12/15

$
0
0
BALOZI, MAALIM DR. ALI AHMED SALEH AKISIDINDIKIZWA NA MSIMAMIZI WAKE WA MASOMO(SUPERVISOR) PROF. HOSSEA RWEGOSHORA KUPOKEA SHAHADA YAKE YA PhD.

Tanzanite iliyokamatwa KIA yafikia Dola za Marekani milioni 1,207,990

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Omar Chambo (wa pili kulia) akitembelea baadhi ya vitalu vya uchimbaji madini ya Tanzanite katika eneo la Mirelani mkoani Manyara mara baada ya kumaliza kikao kikao chake na Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara ambazo zimeamua kufanya kazi kwa pamoja ili kudhibiti utoroshaji wa madini ya Tanzanite.Kulia kwake ni Afisa Madini Mkazi katika Ofisi ya Madini Mirelani, Mhandisi Henry Mditi.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Omar Chambo (wa kwanza kulia) akiangalia moja ya mashine zinazotumika katika shughuli za uchimbaji madini katika eneo la Mirelani mkoani Manyara wakati alipotembelea eneo hilo mara baada ya kumaliza kikao kikao chake na Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara ambazo zimeamua kufanya kazi kwa pamoja ili kudhibiti utoroshaji wa madini ya Tanzanite.
Mwenyekiti wa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara (hawapo pichani) ambazo zimeamua kufanya kazi kwa pamoja ili kudhibiti utoroshaji wa madini ya Tanzanite nje ya nchi. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo, wa kwanza kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi na wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Omar Chambo (wa kwanza kulia) akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara ambazo zimeamua kufanya kazi kwa pamoja ili kudhibiti utoroshaji wa madini ya Tanzanite nje ya nchi.

Airtel yashinda tuzo mbili kwa kutoa huduma bora kwa wateja

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma za kibunifu imetunikiwa tuzo mbili za ubora za Tanzania Leadership Awards 2015 katika halfa iliyofanyika katika hotel ya Hyatt jijini Dar es salaam.

Airtel imejishindia tuzo hizo katika kipengele cha matumizi bora ya huduma za kimtandao kufikia wateja wake (best use of social Media in marketing) pamoja na kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wateja (brand excellence) katika sekta ya mawasiliano na kuwashinda makapuni mengine yaliyokuwa wakichauana nayo katika kinyanganyiro cha tuzo hizo Wakionge wakati wa kukabidhi tuzo hizo , waandaaji wa tuzo hizo za Tanzania Leadership Awards, Kishore Bollakpalli alisema " Airtel imepata tuzo hizi kutokana na kufanya vizuri zaidi katika kuwasiliana na wateja wake kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii na hivyo kuwafikia wateja wake nchini nzima kwa urahisi zaidi.

Lakini kwa upande wa tuzo ya Brand excellence, Airtel imeonyesha kwa vitendo dhamira yao ya kutoa huduma bora kwa wateja wake huku ikitoa bidhaa na huduma za kibunifu ili kukidhi mahitaji ya wateja wake na kuboresha maisha yao.

Akipokea tuzo hizo Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso alisema" Tunayofuraha kupokea tuzo hizi za Tanzania Leadership award na tunaamini huu ni ushuhuda kamili unaoonyesha kwa vitendo dhamira yetu ya kutoa huduma zenye zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu zikiwemo huduma za intaneti, huduma za kifedha kupitia simu za mkononi na kuchochea kukua na upatikanaji wa huduma za kifedha nchini".

Colaso aliongeza kwa kusema Airtel itaendelea na dhamira yake yakutoa huduma zinazogusa mahitaji ya wateja wake u na kuwaweka karibu ili kuendelea kutoa huduma bora zaidi katika miaka ijayo.

Tuzo za Tanzania Leadership Awards zinalenga kutambua na kupongeza jitihada zinazofanya na watu binafsi na makapuni katika kuboresha uchumi wa Tanzania na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso akipokea tuzo ya ubora katika kipengele cha kutoa huduma za kimtandao kutoka kwa waandaaji wa tuzo za Tanzania Leadership Award, Kishore Bollakpalli (kushoto). Airtel Tanzania imejishindia tuzo mbili za ubora katika kipengele cha kutoa huuduma za kimtandao pamoja na huduma zinazokidhi mahitaji ya wateja.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso akionyesha tuzo mbili za ubora mara baada ya kukabidhiwa na waandaji wa Tanzania Leadership Award 2015. Airtel ilijishindia tuzo hizo katika kipengele cha kutoa huuduma za kimtandao pamoja na huduma zinazokidhi mahitaji ya wateja katika sekta ya mawasiliano.

Prof. Mbalawa atoa miezi mine kuhakikisha mradi wa maji mjini Geita unawafikia watu waliokusudiwa

BILIONI 137 ZIMETENGWA KWA AJILI YA ELIMU YA BURE - WAZIRI MKUU

$
0
0
SERIKALI imekwishatenga kiasi cha sh. bilioni 137 kwa ajili ya kugharamia utoaji wa elimu ya bure kuanzia Januari hadi Juni, mwakani.

Kauli hiyo imetolewa jana jioni (Jumapili, Desemba 20, 2015) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliofika kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa uwanja wa mikutano wa Likangala wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.

“Kazi ya utumbuaji majipu imezaa matunda kwani tumeweza kupata fedha za kugahrimia elimu ya bure ambayo iliahidiwa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli wakati wa kampeni. Fedha hiyo tunayo, na tumeshaanza kuisambaza kwa sababu tunataka shule zikifunguliwa Januari, 2016 watoto waanze kufaidika,” alisema huku akishangiliwa.

“Atakayezigusa fedha hizi na kuzitumia vibaya ni lazima tutamtumbua tu! Tumeshawapa maelekezo Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Elimu wao na kuwaonya kuhusu matumizi ya fedha hizo,” alisema.

“Hatuhitaji mwanafunzi achangishwe hela ya mitihani, na zile shilingi 10,000/- kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma Sekondari nazo pia tutazipeleka. Na huu ni mpango wa dharura ambao haukuwemo katika bajeti ya mwaka 2015/2016, kwa hiyo tutalazimika kuziombea kibali,” alisema.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema Serikali imekwishafanya hesabu za kubaini kiasi kinachohitajika kwa ajili ya milo ya watoto shuleni kwa wale walioko bweni na wale wa kutwa. Hesabu tunazo na tumebaini kuwa tutazimudu,” alisema huku akishangiliwa.

“Serikali ilitoa ahadi kwa wananchi na sisi tumedhamiria kuzitekeleza. Tuliahidi elimu bure nasi tutaitekeleza,” alisema.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Bw. Nape Nnauye amewataka madiwani wa jimbo la Ruangwa kuhakikisha wanamsaidia Waziri Mkuu Majaliwa kusimamia kazi za jimboni ili aweze kuwa huru kutekeleza majukumu ya kitaifa.

“Madiwani wa jimbo hili msaidieni Waziri Mkuu kusimamia shughuli za maendeleo ili wakati yeye anaendelea kutekeleza majukumu ya kitaifa, ya jimbo naye yawe shwari. Msaidieni kusimamia fedha za umma ziende kwenye miradi iliyokusudiwa ili wakati akitumbua majipu huko kwingine na huku pia yasiote,” aliongeza.

WAZIRI MKUU MAJALIWA, KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA RUANGWA

$
0
0
rua1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa zawadi ya shati la asili la  Wamwera  na Mzee Saidi Issa Hanga katika mkutano wa hadhara aliouhutubia  mjini Ruangwa Desemba 20, 2015.
rua2
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na Mkewe Mary wakisalimiana na wazee wa Ruangwa kabla ya mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu mjini Ruangwa Desemba 20, 2015.
rua3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha na kufurahia  silaha  za asili alizokabidhiwa na wazee wa Ruangwa kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini hapo Desemba  20, 2015.
rua4
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa alipokea zawadi ya rungu kutoka kwa Mzee  Issa Juma Nangalapa ikiwa ni ishashara ya kumtaka awaadhibu wotw wanaokiuka sheria. Alikuwa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia mjini Ruangwa Desemba 20, 2015.
rua5

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia moja kati ya zana na silaha  za asili alizokabidhiwa na wazee wa Ruangwa kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini hapo Desemba  20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

‘BILIONI 137 ZIMETENGWA 
KWA AJILI YA ELIMU YA BURE’

* Awaonya Wakurugenzi, Maafisa elimu.

SERIKALI imekwishatenga kiasi cha sh. bilioni 137 kwa ajili ya kugharamia utoaji wa elimu ya bure kuanzia Januari hadi Juni, mwakani.

Kauli hiyo imetolewa jana jioni (Jumapili, Desemba 20, 2015) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliofika kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa uwanja wa mikutano wa Likangala wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.

“Kazi ya utumbuaji majipu imezaa matunda kwani tumeweza kupata fedha za kugahrimia elimu ya bure ambayo iliahidiwa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli wakati wa kampeni. Fedha hiyo tunayo, na tumeshaanza kuisambaza kwa sababu tunataka shule zikifunguliwa Januari, 2016 watoto waanze kufaidika,” alisema huku akishangiliwa.

“Atakayezigusa fedha hizi na kuzitumia vibaya ni lazima tutamtumbua tu! Tumeshawapa maelekezo Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Elimu wao na kuwaonya kuhusu matumizi ya fedha hizo,” alisema.

“Hatuhitaji mwanafunzi achangishwe hela ya mitihani, na zile shilingi 10,000/- kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma Sekondari nazo pia tutazipeleka. Na huu ni mpango wa dharura ambao haukuwemo katika bajeti ya mwaka 2015/2016, kwa hiyo tutalazimika kuziombea kibali,” alisema.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema Serikali imekwishafanya hesabu za kubaini kiasi kinachohitajika kwa ajili ya milo ya watoto shuleni kwa wale walioko bweni na wale wa kutwa. Hesabu tunazo na tumebaini kuwa tutazimudu,” alisema huku akishangiliwa.“Serikali ilitoa ahadi kwa wananchi na sisi tumedhamiria kuzitekeleza. Tuliahidi elimu bure nasi tutaitekeleza,” alisema.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Bw. Nape Nnauye amewataka madiwani wa jimbo la Ruangwa kuhakikisha wanamsaidia Waziri Mkuu Majaliwa kusimamia kazi za jimboni ili aweze kuwa huru kutekeleza majukumu ya kitaifa.

“Madiwani wa jimbo hili msaidieni Waziri Mkuu kusimamia shughuli za maendeleo ili wakati yeye anaendelea kutekeleza majukumu ya kitaifa, ya jimbo naye yawe shwari. Msaidieni kusimamia fedha za umma ziende kwenye miradi iliyokusudiwa ili wakati akitumbua majipu huko kwingine na huku pia yasiote,” aliongeza.


GEPF WATOA MSAADA KWA TAASISI YA ALLIANCE FOR SOCIAL ALLEVATION (ASE)

$
0
0
Meneja wa GEPF mkoa wa Kinondoni, Mohammed Nyallo akikabidhi vifaa (computers, printers na camera) kwa Bi Tipwa Mapunda kiongozi mwandamizi wa ASE taasisi ya vicoba ambayo ina wanachama katika Mfuko wa GEPF, ikiwa ni sehemu ya msaada wenye lengo la kuwasaidia ASE katika kufanikisha shughuli zao kwa ufanisi zaidi.

Asilimia 49 kati ya asilimia 100 ya uchunguzi wa DNA yaonyesha baba si mzazi halali wa mtoto

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-Maelezo

Asilimia 49 kati ya asilimia 100 ya matokeo ya uchunguzi wa makosa ya vinasaba (DNA)  yanayowasilishwa katika ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa mwaka yanaonyesha kuwa baba si mzazi halali wa mtoto katika kesi hizo.

Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa wadau wa wakala wa afya ya mazingira leo jijini Dar es Salaam.

“Kesi zinazopokelewa katika maabara yetu zinazohusu sampuli ya Vinasaba kwa mwaka zinaonyesha kuwa asilimia 49% kati ya asilimia 100% ya matokeo hayo huonyesha mzazi mmoja ambaye ni baba kuwa si mzazi halali wa mtoto huyo”.

“Vinasaba ni utambulisho wa kipekee wa kila kiumbe ambao unabeba taarifa muhimu na inayorithisha tabia au umbile fulani la mhusika. Vinasaba ni kama vile kitabu cha kumbukumbu kinachohusu maisha binafsi”, aliongeza Prof. Manyele.

Profesa Manyele aliongeza kuwa mikoa ya kanda ya Ziwa, Arusha, Dar es Salaam na Mbeya ndio inayoongoza kwa matokeo ya uchanguzi huo wa makosa ya Vinasaba nchini.

Akizungumza kuhusu lengo la mkutano huo, Profesa Manyele amesema kuwa ni kuimarisha uhusiano uliopo kati ya wadau wa kemikali na wadau wa afya ya mazingira kutoka katika halmashauri tofauti nchini pamoja na ofisi ya Mazingira.

Aidha Profesa alibainisha baadhi ya majukumu yanayofanywa na wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa ni kufanya uchunguzi ili kuhakiki ubora na usalama wa vyakula, dawa, maji, maji machafu, bidhaa za viwanda na mashambani, sampuli za mazingira na sampuli zinazohusiana na makosa ya jinai.

“Matokeo ya uchunguzi wa makosa ya jinai na vinasaba (DNA) huviwezesha vyombo husika kufikia maamuzi stahili na kusaidia kutendeka kwa haki katika tuhuma za kesi za jinai ikiwemo ulevi, mauaji, ubakaji, wizi wa watoto, uhalali wa mtoto kwa mzazi, kwa kupitia vyombo husika” alifafanua Profesa.

Mbali na hayo, alisema  wakala  kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatarajia kuwasilisha mapendekezo ya kutunga sheria ya kuunda maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Sheria ya kusimamia taaluma ya Wakemia, kuimarisha upatikanaji wa mitambo na vifaa vya maabara kila teknologia inapobadilika pamoja na kuimarisha zaidi taratibu za uchunguzi ziwe za kisasa ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknologia.

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LATANGAZA KUSAMBAZWA KWA BOEING 787S KWA SAFARI ZAKE MWAKA 2016

$
0
0
SHIRIKA la ndege la Etihad, ndege rasmi ya taifa kwa Falme za kiarabu limetangza kuanzisha mipango ya kurusha ndege aina ya boeing 787s kwa safari za kwenda Dusseldorf, Perth, Shanghai, Istanbul na Johannesburg kwa mwa mwaka 2016.

Matarajio ya kuwasili kwa ndege hizo mpya aina ya Boeing 787s ni ndani ya miezi saba ijayo, kuanzia Mei 2016, ndege hizo “Dreamliners” zenye uwezo wa kubeba abiria 299 zitaanza kutoa huduma kwenda Dusseldorf, Perth, Shanghai, Istanbul na Johannesburg kutoka Abu Dhabi zikichukua nafasi ya ndege zinazotumika sasa.

Kwa sasa Shirika la ndege la Etihad lina ndege tano tu aina ya 787s ambazo zinafanya safari zake kati ya Brisbane, Washington, Singapore na Zurich moja kwa moja kutoka Abu Dhabi. 

Matarajio ya Shirika hilo ni kuongeza zaidi ya Boeing 66 ndani ya miaka kadhaa ijayo ambapo ndege hizo aina ya “Dreamliners”zitakuwa ndege rasmi za shirika hilo kwa masafa marefu.

James Hogan, ambaye ni Rais na afisa mkuu wa shirika la ndege la Etihad alisema: “Tangu kuanzishwa kwa ndege aina ya 787 ya kwanza katika huduma za kibishara mnamo februari mwaka huu, tumekuwa tukipata maoni mazuri kutoka kwa abiria wetu  ambayo yamekuwa kama alama ya ubora wa hali ya juu katika kanda na dunia nzima.

“Kuanzia mwezi Mei mwakani, shirika la ndege la Etihad litazindua ndege mpya Boeing 787 aina ya dreamliners zitakazotumika rasmi badala ya hizi zilizopo kwa safari za masafa marefu ambapo zitatoa fursa kwa abiria wetu kupanda ndege za teknolojia mpya.

“Abiria na wateja wetu wa siku hizi wanapenda kusafiri bila kero wala pirika pirika kwenye usafiri wa viwango vya juu, wanataka chaguo zuri zaidi na bei nafuu. Hivi ndivyo vigezo vyao vikuu katika kuchagua na sisi hapa Etihad tunajitahidi kufikia matarajio hayo kwa tafiti na uvumbuzi wa aina mbalimbali kama vile kuleta ndege mpya na kuendelea kuboresha njia zetu za usafiri.

KUTOKA MAKTABA YA GLOBU YA JAMII

$
0
0
 Abiria wa Treni ya Reli ya kati inayofanya safari zake kati ya Dar es salaam kwenda Kigoma, wakimuangalia mmoja wa abiria mwenzao akiwa nje ya Treni hiyo wakati ikiendelea na safari, kwa madai ya kumkwepa mkaguzi wa tiketi (TT) wa Treni hiyo.Hii ilikuwa ni mwanzoni mwa mwaka 2013.

MAITI ZALAZWA SAKAKFUNI HOSPITALI YA MAFINGA

$
0
0
Udogo wa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mafinga yalazimu wahudumu wa hospitali hiyo kulaza maiti sakafuni.

WASHINDI 16 WAPATIKANA KATIKA DROO YA AIRTEL MKWANJIKA

$
0
0

 Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando (katikati) akiongea na

moja ya  washindi kupitia simu ya mkononi wakati wa kuendesha droo ya
kwanza ya promosheni ya Airtel Mkawnjika ambapo washindi 16 kutoka
katika mikoa mbalimbali walipatikana.  Akishuhudia  Msimamizi wa bodi
ya michezo ya kubahatisha nchini , Bwana Abdallah Hemed  na Afisa
Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma (kulia)

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati) akiongea na
waandishi wa habari wakati wa kuendesha droo ya kwanza ya promosheni
ya Airtel Mkawnjika ambapo washindi 16 kutoka katika mikoa mbalimbali
walipatikana.  Akishuhudia  Msimamizi wa bodi
ya michezo ya kubahatisha nchini , Bwana Abdallah Hemed  na Meneja
masoko wa Airtel bi Anethy Muga (kulia)


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel leo imechezesha droo ya kwanza ya
promosheni ya Airtel Mkwanjika  na kuwapata washindi 16 wa  siku nne
za mwanzo
Promosheni ya Airtel Mkwanjika imezinduliwa na Airtel wiki iliyopita
ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja wake katika msimu huu wa siku kuu
za mwisho wa mwaka na X-mass  ambapo jumla ya shilingi milioni 300
zimetengwa na kampuni hiyo kushindaniwa na wateja wake kama  zawadi.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa droo hiyo Meneja Uhusiano
wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Airtel Mkwanjika leo tumewanyakuwa
washindi 16 wa siku nne za mwanzo ambapo kila siku ni washindi wanne
na kila mmoja ataweza kujizolea hadi shilingi milioni moja katika
boksi letu la Airtel Mkwanjika.

Mmbando aliwataja walioibuka washindi wa kuingia katika boksi la
Airtel Mkwanjika kuwa Mama Masisimba ,  Abdallah S Rashid, Amani
Maruma, Msafiri Saidi Ruwia , Hassani Hamis Suleyman na  Aida Asabwile
Mwafi wakazi wa mkoa wa Dar, es  salaam. 

Carston Magoah na Godfrey
Frank Kamota wakazi wa Morogoro, Hassan Ngakoma mkazi wa Manyara ,
Safari Aidaru mkazi wa Mbulu, Lupembe Massanja  kutoka Rufiji , Rachel
Obedi Muhumu mkazi wa Moshi na Rodrique kimei  mkazi wa Msumbiji.
Washindi hawa  watapigiwa simu na kupatiwa maelekezo zaidi jinsi ya
kupata na kupoke zawadi zao.

Nae Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga alisema “Promosheni yetu
imeanza kufanikiwa kwa kuwa tayari tumewapata wateja wetu 16 na
tumeshaandaa jumla ya milioni 16 ilikila mmoja akishajizolea pesa
kwenye sanduku la pesa papo hapo tutampatia pesa yake aliyokusanya
kupitia Airtel Money ili akasherehekee sikukuu kwa furaha zaidi”
Promosheni ya “Airtel MKWANJIKA” itawawezesha wateja wote wanaojinga
na kifurushi chochote cha yatosha au kuongeza muda wa maongezi wa
kiwango chochote kwenye simu zao kuingia moja kwa moja kwenye droo ya
siku na kupata nafasi ya kujishindia pesa taslimu.

Hakuna gharama ya ziada wala  malipo yeyote unaongeza salio kwa
kutumia vocha, huduma ya Airtel money au kununua vifurushi vya yatosha
na kujishindia pesa kila siku” alisisitiza Muga.

ORODHA YA WAUZA DAWA ZA KULEVYA HAINISADII-KITWANGA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu wakati alipokuwa anawasili Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi. Waziri Kitwanga alifanya mazungumzo na Viongozi Wakuu wa jeshi hilo na kukubaliana kuweka mikakati zaidi ya kukabiliana na uhalifu nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mazungumzo na Viongozi Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini. Waziri Kitwanga aliwaambia waandishi wa habari kuwa, wamekubaliana na Viongozi Wakuu wa jeshi hilo kuweka mikakati zaidi ya kukabiliana na uhalifu nchini. Wapili kushoto meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Wapili kulia meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki. Kulia ni Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo, Paul Chagonja. Kushoto meza kuu ni Kamishna wa Polisi Jamii nchini, Mussa Ali Mussa. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati aliyekaa), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (watatu kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini mara baada ya kikao chao kilichofanya katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi hilo kumalizika. Waziri Kitwanga alifanya mazungumzo na Viongozi hao na kukubaliana kuweka mikakati ya kupambana na uhalifu.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAZIRI wa Mambo Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema njia ya kudhibiti dawa za kulevya kuingia nchini ni kuweka mfumo wa kisasa wa kudhibiti uingiaji dawa hizo, kuwa na orodha ya waingizaji wa dawa ni kazi bure kutokana na kukosa mamlaka ya kisheria.

Kitwanga ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Maafisa Wakuu wa Jeshi la Polisi, amesema katika kukabiliana na uingizaji wa dawa za kulevya ni kuweka mfumo imara na jeshi la polisi lazima lijipange katika udhibiti huo.

Kitwanga amesema kuwa mfumo wa kiteknolijia ukiwekwa hautabagua mtu yeyote au mkubwa katika madaraka awe mdogo wakishajulikana watachukuliwa hatua za kisheria bila kuangaliwa nafasi walizo nazo.

“Orodha ya wauza unga ukiwanayo haitasaidia na kufanya hivyo ni kuhisi, lakini huna sheria ya kuweza kuwabana katika orodha hiyo” amesema Kitwanga.

Kitwanga amesema kuwa katika mambo waliyojpanga nayo na jeshi la polis ni kuhakikisha wanaimarisha ulinzi katika bandari ili kuweza kudhibiti utoroshaji wa vitu mbalimbali ambavyo vinatoka bila utaratibu.

Hata hivyo amewataka polisi watu washitakiwe kwa kesi walizo nazo na sio kuwabambikia watu wasio na hatia kusababisha kufungwa kwa kesi zisizowahusu.

Kitwanga amesema utoroshaji wa madini,jeshi la polisi haliwahusu wakihitajika na Wizara ya Nishati na Madini watafanya hivyo katika kukabiliana na utoshaji huo.

Aidha amesema kati ya askari 45,000 ni askari 10,000 ndio wenye makazi hivyo wanatarajia kujenga nyumba 5000 ikiwa nia nia askari wote kukaa katika makambi ni rahisi kuweza kuhitajika kwa muda wowote.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKAGUA UJENZI WA MAHAKAMA YA UMOJA WA MATAIFA JIJINI ARUSHA

$
0
0

Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa akipata maelekezo ya ziada kuhusu ujenzi wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Lakilaki Jijini Arusha. Aneyetoa maelezo ni Afisa Mambo ya Nje na Mwansheria Bw. Elisha Suku. Kushoto kwa Waziri Mahiga ni Nd. Hamdouny Mansour, Katibu Tawala Msaidizi upande wa miundombinu. 
 Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa na ujumbe wake wakiangalia eneo la eka 16 ambapo majengo manne ya Mahakama ya Umoja wa Mataifa yanajengwa. Ujenzi huo unatarajiwa kukamilika Mwezi Aprili mwaka 2016. 
Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Mhe. Wilson Nkhambaku baada ya kukagua eneo hilo na kuridhika na kasi ya ujenzi uliozingatia viwango vya kimataifa na vile vya Umoja we Mataifa. 

MBUNGE WA MLALO ATIMIZA AHADI YAKE KWA WANAMLALO

$
0
0
 Katika utekelezaji wa ahadi zake Mbunge wa jimbo la Mlalo Rashid Shangazi amekabidhi mabati 40 ya geji 28 kwa wanajimbo la Mlalo  kwaajili ya  kwa ajili ya jengo la Maabara shule ya Sekondari Mtae pamoja na Mifuko 10 ya sementi kwaajili ya kwa ajili ya ukarabati msikiti mkuu wa makose. Alikabidhi vitu hivyo mwishoni mwa wiki mkoani Tanga.
Wana Mlalo wakishusha Mifuko ya Sementi 10  kwa ajili ya ukarabati msikiti mkuu wa makose, kutoka kwenye gari pamoja na Mabati 40 kwa shule ya Mtae wishoni mwa wiki katika jimbo la Mlalo mkoani Tanga.
sambamba na hilo alikabidhi mifuko ya Sementi 30 kwa ajili ya kukarabati  jengo la maabara shule ya sekondari kalmere na mifuko ya  sementi 10 kwa ajili ya ukarabati msikiti mkuu wa makose,hii ni kupelekea kuhakikisha mlalo inasonga mbele katika maendeleo ya jamii.

WANAOTAKIWA KUSTAAFU WASIPEWE MIKATABA YA KUENDELEA NA KAZI SERIKALINI - MH. KAIRUKI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akitoa maelekezo kwa watumishi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu-Utumishi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu-Utumishi.


TSHABALALA AKABIDHIWA TUNZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI

$
0
0
Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015.

MSHINDI wa mwezi wa Oktoba, 2015 ni Mohamed Hussein Tshabalala ambapo amepata kura nyingi zaidi zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News.

Akikabidhiwa tunzo pamoja na pesa taslim Tsh 500,000/= na Mwanachama na Shabiki wa Simba Mbunge wa Busega Simiyu Mh. Raphael Chegeni, beki wa kushoto Mohamed Tshabalala alisema “tangu nilipotata taarifa za kushinda tunzo ya mchezaji bora kwa mwezi wa 10 nilifurahi sana na leo furaha yangu inazidi zaidi, kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuwa mchezaji na kuweza kushinda tunzo hii, pili kuushukuru Uongozi na wapenzi wa Simba walioona mchango wangu kwenye kikosi cha Simba na kunipigia kura kwa wingi na mwisho napenda kushukuru familia yangu pamoja na watu wangu wote wa karibu ambao wamekuwa mchango mkubwa kwenye mafanikio yangu ya soka”. 

Ninachoweza kuwaahidi ni kuwa kamwe sitowaangusha kwani tunzo hii itakuwa chahu katika mafanikio yangu aliongeza Tshabalala.

Mwanachama na Shabiki wa Simba Mh. Chegeni alisema “kwanza kabisa nashukuru kwa Simba kunipa heshima ya kuweza kuwa mgeni rasmi katika kutoa tunzo hii kwa Tshabalala, napenda kumshauri Tshabalala na wachezaji wetu wengine kuendelea kujituma kwa bidii kwa ukiweka nidhamu, kujituma na kufanya kazi kwa bidii ni lazima mafanikio utayapata”.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Rais wa Simba Evans Aveva alisema “Uongozi, wanachama na wapenzi wa Simba wanathamini mno mchango wa wachezaji katika kuifanya timu yetu ifanye vizuri, hivyo tumeona ni jambo la busara kuwa klabu ya kwanza Nchini Tanzania kuwa na tunzo za mchezaji wake bora. Tunaamini kuwa Tunzo ya Mchezaji bora wa mwezi wa Simba itaongeza ari na kujituma kwa wachezaji wetu. Sisi tukiwa kama viongozi ni kazi yetu ya msingi kuhakikisha kuwa wachezaji wetu hasa wale wanaojituma zaidi wanatambuliwa na kuenziwa’’.

Akizungumza jinsi tunzo ya mchezaji bora itakavyoendeshwa, Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Imani Kajula alisema “Wanachama na wapenzi wa Simba na wapenda michezo ndio watakao kuwa wanachagua mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma jina la mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460, Ni wale tu ambao wamejiunga na Simba News kupitia mtandao wa Voda na Tigo wataweza kupiga kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi wa Simba’’

Tukumbuke kuwa unaweza kumchagua mchezaji bora wa mwezi ukiwa umejiunganisha na huduma ya Simba News kwa kutuma jina la mchezaji kwenda namba 15460. 

Zoezi la kumchagua mchezaji bora wa mwezi wa October, 2015 linaanza tarehe October 10, 2015. Piga kura mara nyingi zaidi kuweza kumpata mchezaji wako bora wa Mwezi October, 2015.

Simba News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya Simba. Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 ni maalum kwa Tigo na Vodacom.
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images