Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1064 | 1065 | (Page 1066) | 1067 | 1068 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Chunya Elias John Tarimo akizindua Mradi wa Kisima cha Maji Kijiji cha Ngwala Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya kilicho jengwa na Kampuni ya utafiti wa madini yaPeak Resources Katika kata ya Ngwala Wilayani humo.
  Baadhi ya Wananchi wakishuhudia uzinduzi wa Mradi wa Maji Kijiji cha Ngwala Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.

  Na Ezekiel Kamanga ,Mbeya,Jamiimojablog 
  SERIKALI wilayani Chunya Mkoani Mbeya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wameendelea na jitihada mbalimbali katika kuhakikisha wanatatua changamoto ya ukosefu wa maji wilayani humo.

  Hatua hiyo inakuja kufuataia kampuni ya Peak Resource limited ambayo hujihusisha na utafiti wa madini adimu chini ya ardhi yanayopatikana katika kata ya ngwala wilayanii chunya mkoani mbeya kuchimba visima viwili vya maji vyenye thamani ya shilingi milioni 16.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano ya visima hivyo Mkuu wa Wilaya ya Chunya Ndugu Elias Tarimo amesema hatua ya kampuni huyo inayojihusisha na utafiti wa madini kuamua kuchimba visima hivyo kwa lengo la kuwasaidia wananchi ni jambo jema nalinalotakiwa kuungwa mkono na wananchi hao.

  Amesema katika kuunga mkono jitihada hizo wananchi hao hawana budi kutunza miundo mbinu hiyo waliojengewa kwani wakiiharibu watarudi katika adha ya shida ya maji walikuwanayo hapo awali na kwamba waendeleze ushirikiano bora na kampuni hiyo.

  Akisoma tarifa fupi ya ujenzi wa miradi mbalimbali waliojenga katika kata hiyo meneja mradi wa Peak Resource limited Patrick Ochieng amesema miradi waliojenga ni visima viwili vilivyogharimu milioni 16kila kimoja unjezi wa nyumba ya mwalimu iliyogharimu shilingi milioni 55 na ujenzi wa eneo la kupumzikia wagonjwa katika kituo cha Afya cha Ngwala iliyogharimu shilingi milioni 7 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 94.

  Ochieng alindelea kueleza kuwa kwa sasa Kampuni yao ipo katika hatua za mwisho za utafiti na kwamba wanafwatilia leseni ya uchimbaji madini na kibali kutoka nemki ili kuanza uzalishaji na kwamba mgodi huo unauwezo wa kudumu kuchimbwa kwa miaka 40.

  Aidha baadhi ya waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa miradi ni pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha Neston Simoni na Diwani wa Kata ya Ngwala Donard Maganga ambao walisema wamefurahishwa na kile kinachofanywa na kampuni hiyo kwani wanajenga miradi bora kwa kutumia gharama nafuu.

  Maganga aliwataka wakazi wa Ngwala kuiga mfano wa kampuni hiyo kwani nalisema nyumba waliojenga ya shilingi milioni 55 ukiweka Mkandarasi wangeweza kujenga kwa shilingi milioni 100 hivyo alisema mfano wa kampuni hiyo unapaswa kuigwa ili kuondoa ufisadi katika jamii yetu.

  Kwaupande wa wananchi waliokuwepo hapo walishukuru kampuni hiyo kwa kupunguza adha walizokuwa nazo katika Kata yao kwani kwasasa wamekuwa na matumaini wa kupata walimu ambao watafundisha watoto wao katika mazingira yalio bora kutokana na uwepo wa nyumba bora ya Mwalimu ukilinganisha na hapo awali walikuwa wanakosa eneo la kujihifadhi, alisema Raisoni George.

  Vile vile Elizabeti Yusuph mkazi wa ngwala alisema wao kama wakinamama walikuwa wachelewa kufanya shughuli za shambani kutokana na kufwata maji umbali mrefu kwani kutokana na uwepo wa mrado huo wa maji utarahisisha shughuli nyingine.

  0 0

  maa5

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Tonia Kandiero Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  maa6

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuelekeza jambo Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Tonia Kandiero Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  maa8

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Tonia Kandiero Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  maa9

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Rwanda hapa nchini Eugene Kayihura aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.

  maa10

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Rwanda hapa nchini Eugene Kayihura aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Picha zote na IKULU


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. amemuhakikishia Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt.Tonia Kandiero kuwa Serikali yake ya Awamu ya Tano itaendelea kushirikiana na benki hiyo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.


  Dkt. Magufuli amesema hayo leo Tarehe 21 Desemba, 2015 Ikulu Jijini Dar es Salaam, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi huyo.

  Pamoja na kumhakikishia ushirikiano Rais Magufuli ametoa wito kwa benki hiyo kupunguza michakato ya kuelekea katika utekelezaji wa miradi na badala yake ameshauri uwepo utaratibu wa haraka unaowezesha kuanza kwa miradi katika kipindi kifupi baada ya fedha kutolewa.

  Kwa upande wake Dkt. Tonia Kandiero pamoja na kumpongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano, amemhakikishia kuwa benki iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maendeleo kama ambavyo imekuwa ikifanya na kwamba kwa sasa imetenga dola Bilioni mbili nukta tatu kwa ajili ya kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo.

  Ameongeza kuwa katika mipango yake ADB imelenga kujielekeza katika utoaji wa mikopo katika sekta ya nishati na usafiri.

  Naye Rais Magufuli ameipongeza ADB kwa kuamua kujielekeza katika sekta hizo za nishati na usafiri na pia ameisisitiza kuangalia namna itakavyounga mkono mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani standrd gauge.

  Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Rwanda hapa nchini Mh Uegene Sagore Kayihura Ikulu Jijini Dar es salaam.

  Kwa upande wake Rais Magufuli amemuhakikishia Balozi Kayihura kuwa serikali yake ya awamu ya tano itaendelea kushirikiana na Rwanda ili wananchi wa nchi zote mbili waweze kunufaika kimaendeleo.

  Katika mazungumzo hayo Balozi Kayihura amewasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania.

  Balozi Kayihura amesema Rais Kagame amefurahishwa na hatua ambazo Rais Magufuli anazichukua hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa bandari na kumhakikishia kuwa Rwanda iko tayari kushirikiana na Tanzania hasa kuitumia bandari ya Dar es salaam ambayo hupitisha asilimia zaidi ya 70 ya mizigo ya Rwanda.

  Ameongeza kuwa Rwanda na Tanzania ni nchi marafiki na majirani hivyo kuna kila sababu ya kujenga ushirikiano madhubuti katika sekta ya uchumi.

  Rais Magufuli amemuomba Balozi Kayihura kumfikishia Rais Kagame salamu za shukrani kwa kumpongeza kuchaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba amedhamiria kuimarisha zaidi ushirikiano na Rwanda.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  21 Desemba, 2015


  0 0


                                                      
                                                 DOWNLOAD HAPA

  0 0

  Nabaki Afrika Ltd would like to thank you for a wonderful year. We wish you a Merry Christmas and a Happy 2016.
  Our head office and branches will be closed for:
  Christmas - 24th, 25th, and 26th December
  New Year - 1st and 2nd January
  Visit our showroom this holiday season for a small gift from Nabaki Afrika to you.
  Once again, thank you for an amazing year!

  Team Nabaki Afrika

  0 0


  0 0


  0 0

  Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya dada yake, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015.
  Rais John Pombe Joseph Magufuli akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya dada yake Rais Mstaafu Dkt JAkaya Kkikwete, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015.
  Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya dada yake Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kkikwete, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015
  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Marais Wastaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakishiriki katika dua wakati wa wa mazishi ya dada yake Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015.
  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Rais Mstaafu kt Jakaya Mrisho Kikwete wakiondoka makaburini baada ya mazishi ya dada yake Rais Mstaafu Dkt JAkaya Kikwete, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015. 
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  maa1
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha  Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ikulu jijini Dar es Salaam na kufanya  Mazungumzo kuhusu hali ya kisiasa ya  Zanzibar. Katika Mazungumzo hayo viongozi wote wamefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea.
  maa2
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ikulu jijini Dar es Salaam.Rais amemshukuru  Maalim Seif  na amemsihi waendelee na mazungumzo hadi suluhisho la muufaka lipatikane.
  maa3
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ikulu jijini Dar es Salaam, wakwanza kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.
  maa4
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha  na Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana naMakamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharrif Hamad, leo tarehe 21 Desemba, 2015 Ikulu Jijini Dar es Salaam  kufuatia maombi yake ya siku nyingi.

  Mazungumzo ya Viongozi hao pia yamehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

  Viongozi hawa kwa pamoja wamejadili hali ya kisiasa Zanzibar na wamefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea. Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais  wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, na viongozi wote wanaoshiriki katika mazungumzo ya kuleta hali ya uelewano Zanzibar. 

  Rais Magufuli pia  amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kudumisha amani na utulivu wakati wa mazungumzo baina ya viongozi wa CUF na CCM yakiendelea huko Zanzibar. 

  Katika Mazungumzo hayo Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharrif  Hamad amemueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya hali ya siasa Zanzibar kadiri anavyoielewa yeye na Rais Magufuli amemshukuru Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa taarifa yake nzuri huku akimsihi waendelee na mazungumzo hadi suluhisho muafaka lipatikane. 

  Majadiliano yanayoendelea yanatoa fursa ya kudumishwa kwa utulivu na sifa njema ya nchi yetu. Wote kwa pamoja wamewaomba wananchi waendelee kuwa watulivu ili kutoa nafasi ya majadiliano yanayoendelea kufikia hatma njema. Wameelezea matumaini yao kuwa vyama vya CCM na CUF haviwezi kushindwa kupata suluhu ya mgogoro huo. 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemuhakikishia kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano itahakikisha kuwa amani na utulivu unaendelea kudumishwa Zanzibar. 

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU. 

  21Desemba, 2015

  0 0

  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP Nuru Selemani akiwakiwaelimisha abiria ndani ya basi lilofanya safari zake mikoani ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inadhaminiwa na Vodacom Tanzania.
  Askari wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma SGT. Tunu Kuta(kulia) akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Masoud Seleman ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kitengo hicho katikati Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa huo SSP Nuru Selemani na wapili kulia ni Kaimu mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania,Heladius Kisiwani.
  Kaimu mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania,Heladius Kisiwani(kulia)akimpa maelezo dereva wa basi liendalo mikoani,Masoud Selemani kuhusiana na pete ya kidoleni inayotolewa na Kampuni hiyo kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani yenye ujumbe“Wait To Send” unaohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Zoezi hili lilifanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mkoani cha Dodoma.Katikati Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP Nuru Selemani.


  0 0

  ‪#‎AfyaYako‬ Vyakula Vinavyoongoza kuongeza AKILI kwenye ubongo
  Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo:

  1.MAFUTA YA SAMAKI

  Samaki na Mafuta ya samaki ambayo ni muhimu katika mwili

  Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa ufahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.
  2.PILIPILI KALI
  Pilipili kali 

  Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa.
  3.MBEGU ZA MABOGA
  Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, inakuwa poa.
  4.NYANYA
  Nyanya 
  Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.
  5. BROKOLI
  Brokali

  Brokoli ni mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo inafaida sana kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamin K inahusika moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na uzee.
  6.KARANGA
  Aina zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.
  7.MAYAI
  Mwisho ni mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.CHANZO CRI SWAHILI.

  0 0

   Naibu waziri ofisi ya raisi tamisemi utumishi na utawala bora Mh Selemani  Jafo akipata maelezo kutoka kwa kaimu meneja mafao wa LAPF Bw. Amani Sindato akionyeshwa mafaili ya wanachama wanaostaafu mwezi januari 2016 lakini wameshaandaliwa mafao yao.
  Naibu waziri ofisi ya raisi tamisemi utumishi na utawala bora Mh Selemani  Jafo  akionyeshwa orodha ya wanachama wanaotarajia kustaafu miezi sita ijayo na Afisa mafao mwandamizi Bw. Franklin Boga. LAPF huwatambua wanachama hao mapema ili kuwaandalia mafao yao na kutimiza azma ya LAPF kulipa jana wastaafu wa kesho.
     Naibu waziri ofisi ya raisi tamisemi utumishi na utawala bora Mh Selemani  Jafo katika picha ya pamoja na menejimenti ya LAPF. 
   Naibu waziri ofisi ya raisi Tamisemi utumishi na utawala bora Mh Selemani  Jafo akisaini kitabu cha wageni, pembeni ni Kaimu Mkurugenzi mkuu wa LAPF Bw. John kida
   

  0 0

  Dar es Salaam Tourism is getting a boost following another luxury cruise ship which docked in Dar es Salaam Port on Monday December 21, 2015 with more than 450 tourists and crew. MS Nautica, which is operated by Oceania Cruises, docked at Dar es Salaam Port at 09h30. The vacationers were from different countries including South Africa, the United States, Germany, Australia, and the United Kingdom.

  At the Port, the tourists were welcomed by the energetic traditional snake dance, which was really exiting. While some tourists travelled to Bagamoyo to visit historical sites, others enjoyed a tour of Dar es salaam City including the National Museum, Tinga Tinga Arts, The Slip Way Craft Market and Mwenge Craft Market.

  The cruise Ship will also dock in Zanzibar on Tuesday December 22, 2015 and provide opportunity for tourists to visit various attractions including the beautifully preserved old Stone Town which is a UNESCO World Heritage Site, historical monuments such as the Arab Fort and the House of Wonders.

  Tourists will also be having opportunity to hang around the markets in the Stone Town, shop for the exquisite handicraft items and artifacts made by the local people, as well as taking time for spice tour.

  Tanzania is expected to receive another cruise Ship on December 31, 2015 and January 1, 2016 respectively with approximately 1000 tourists.
  The Oceania Cruises arriving in Dar es salaam Port.
  The tourists entertained by a snake traditional dance while disembarking from the Cruise ship.
  Tourists are having information from TTB'S Tourist Information Officer Maria Lazaro before starting a City tour.


  0 0

  Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akitoa maagizo ya utekelezaji kwa Kamati za maafa katika ngazi zote nchini kuhusu tahadhari ya uwezekano wa kuwepo kwa mvua za El- Nino tarehe 22 Desemba,2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.)

  0 0

   Mkurugenzi wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga (picha zifuatazo)akiwatunuku vyeti wafanyakazi bora wa idara mbalimbali za taasisi hiyo kwa mwaka 2015.
   Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mamanga akihutubia wafanyakazi wa TASAF (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo jijini DSM.
  Wataalamu waelekezi wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya TASAF.


  0 0

  Meneja Uendelezaji wa Biashara wa Benki ya NBC, Eddie Mhina (kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo kuhusu huduma za kibenki zinazofuata kanuni na misingi ya kiislamu (Islamic Banking) katika warsha ya siku moja waliyowaandalia wateja wa NBC mkoani Mtwara hivi karibuni.
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu (Islamic Banking), cha Benki ya NBC, Yassir Masoud (kulia), akielezea kuhusu huduma hizo wakati wa warsha ya siku moja waliyowaandalia wateja wa NBC mkoani Mtwara hivi karibuni.
  Meneja Uendelezaji wa Biashara wa Benki ya NBC, Eddie Mhina (kulia), akiagana na mmoja wa wateja wao Mohamed Kioze mara baada ya kuisha warsha ya siku moja waliyowaandalia wateja wa NBC kwa ajili ya kuwaelezea kuhusu bidhaa mbalimbali zinazopatikana kupitia kitengo cha Islamic Banking cha NBC, mjini Mtwara hivi karibuni.

  0 0


  Katibu mkuu wa chama cha ADA-TADEA, John Shibuda akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na viongozi wa mashirkiano ya umoja wa vyama vya UDA, TADEA,UDP,UPDP,na SAU kwa kuwaomba viongozi wa ZEC,CUF,CCM na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili waweze kukutana na kuzungumza pamoja kuhusiana na migoro wa kisiasa nchini humo, ameyasema leo jijini Dar es Salaam.

  Katibu mkuu wa chama cha ADA-TADEA, John Shibuda katikati akizungumza na waandishi a habari jijini Dar es Salaam leo, kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti SAU na mjumbe wa URAWU, Yusuf Manyanga, na Mwenyekiti wa Taifa UPDP, Katibu mkuu wa URUWA, Comrade Fahami Dovutwa na kulia ni Naibu Katibu mkuu wa UDP na mjumbe wa URAWU, Izaak Cheyo.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimksikiliza Katibu mkuu wa chama cha ADA-TADEA, John Shibuda wakati akizungumza leo katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Legho jijini Dar es Salaam.

  Na Avila Kakingo Globu ya Jamii.
  UMOJA wa Rufaa ya Wananchi (URUWA)
  unaoundwa na viongozi wa Mashirikiano ya umoja wa vyama vya UDA,TADEA,UDP,UPDP na SAU (URUWA) wameomba kukutana na viongozi wa ZAC, CUF,CCM na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa chama cha ADA-TADEA, John Shibuda wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Legho jijini Dar es Salaam leo.

  Ombi hilo limekuja baada ya viongozi hao kutaka kuelimishwa kuhusu sintofahamu ya uchaguzi wa Zanzibar na kuwataka viongozi wa zanzibar waache kutoa kauli na matamko ya mivuno iliyo na tija kwa wanchini humo.


  Pia Shibuda amesema kuwa wanataka ifahamike kwamba ugomvi wa Akili makini na giza totoro ni mwanga nao wameamua kuwa mwanga na kubaini kilichomo katika hili giza la mabishano kati ya ZAC, CUF,CCM na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Wakati huhohuo Shibuda amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Joseph Magufuri pamoja na wasaidizi wake wakuu Makamu wa Rais, Samia Suluhu pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kuwaunga mkono kwa juhudi zao za utumishi, uaminifu na utiifu kwa ustawi wa maendeleo ya jamii na Taifa.

  0 0

  03
  MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili Afrika, Rebecca Malope anatarajia kuwasili nchini kesho saa tisa alasiri kwenye uwanja wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika keshokutwa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama kabla ya kuwasili kwa Malope leo watawasili watangulizi wake ambao watafika kwa ajili ya kufanya maandalizi ya tamasha hilo.

  Msama alisema mwimbaji Faustine Munishi aliwasili jana usiku akitokea Kenya, ambako Sarah K anatarajia kuwasili kesho saa 10 jioni.
  Aidha Msama alisema Solomon Mukubwa anatarajia kufika Ijumaa asubuhi ambaye ataelekea moja kwa moja ukumbini kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa Watanzania.

  Msama alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ili kurudisha shukrani kwa Mungu baada uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani.“Nawaomba Watanzania tujitokeze kwa wingi kwenye Tamasha la Krismasi ili tumrudishie Mungu shukrani baada ya kupita kwenye uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani na utulivu,” alisema Msama.

  Viingilio katika tamasha hilo ni shilingi 50,000 kwa Viti maalum, VIP shilingi 10,000, shilingi 5000 viti vya kawaida na shilingi 2000 kwa watoto.
  “Viingilio tulivyopanga vitasaidia wenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu, wajane na wengineo ambao wanahitaji msaada,” alisema Msama.

   Aliwataja waimbaji watakaopanda jukwaa la Tamasha la Krismasi ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Jesca Honore, Christopher Mwahangila, Joshua Mlelwa, Martha Mwaipaja, Christina Shusho, Sifael Mwabuka, Kwaya ya KKKT  Yombo na Kwaya ya Wakorintho wapili ambayo itazindua albamu yake ya Mchepuko sio dili.Waimbaji wa nje ni pamoja na Rebecca Malope (Afrika Kusini), Sarah K, Solomon Mukubwa na Faustin Munishi ‘Malebo’  (Wote kutoka Kenya).


  Msama alisema mgeni rasmi katika tamasha hilo ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye.

  0 0
 • 12/22/15--04:34: KOMBE LA FA KUENDELEA LEO
 • Michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa pili unaendelea leo kwa mchezo mmoja kuchezwa mmoja katika uwanja wa Majimaji mjini Songea kati ya JKT Mlale dhidi ya Mighty Elephant.

  Kesho Jumatano kutakua na michezo miwili, Kariakoo ya Lindi watawakaribisha Mshikamano FC katika uwanja wa Ilulu – Lindi, Disemba 24 Njombe Mji watakua wenyeji wa Green Warriors katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, na Pamba FC watacheza dhidi ya Alliance uwanja wa CCM Kirumba.

  Ijumaa siku ya sikukuu ya Krisamsi Lipuli FC watawakaribisha Kurugenzi katika uwanja wa Wambi Mafinga.

  Mzunguko huo wa pili unatarajiwa kumalizika Disemba 29 mwaka huu kwa michezo minne, Wenda FC v Kimondo (Sokoine), Mji Mkuu (CDA) v Singida United (Jamhuri), Mvuvuma v JKT Kanembwa (Tanganyika), Abajalo FC v Villa Squad (Karume)

  Timu saba za Ashanti United, Burkinafaso, Geita Gold, Friends Rangers, Madini FCM, Panone na Rhino Rangers zimeshakata tiketi ya kucheza mzunguko wa tatu wa Kombe la FA mwezi Januari 2016, pamoja na timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.

  Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.

  0 0

  Na Zainabu Hamis wa Globu ya Jami.
  CHAMA cha wafanyakazi wa viwanda na sekta mbalimbali(IGWUTA) champongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Joseph Magufuli (Pichani)kwa namna na jinsi anavyofanya kazi yake hasa ile ya kupambana na mafisadi na wanafiki.

  Akizungumza na Waandishi wa habari leo Katibu Mkuu wa chama chama cha IGWUTA, Michael Kashamba amesema kuwa,Wamefurahishwa kwa  kumpata Rais Magufuli na wanatoa wito kwa Wafanyakazi wote hapa nchini kujitokeza na kumuunga mkono Rais wetu katika mapambano dhidi ya ufisadi.

  Aidha Kashamba ametoa tamko la kumpongeza Magufuli kuwa ni kiongozi asiyekuwa wa kawaida, Hana ubinafsi na anaweka maslahi ya nchi mbele huku akimfananisha kwa utendaji wa kazi zake ni kama Rais wa awamu ya kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Pia Kashamba amesema kuwa, Chama chao kinatoa huduma ya kuelimisha na kuhamasisha wanachama kutimiza wajibu wao wa kufanya kazi kwa bidii, nidhamu na uaminifu mkubwa.

  Pia IGWUTA inatoa Huduma za utetezi kwa Wanachama dhidi ya uonevu wowote uliofanywa na baadhi ya waajiri hapa nchini.

  0 0


  Mwanamuziki wa Dansi Patcho Mwamba Akiwa anaimba mbele ya washabiki wake waliouthuria onyesho la bendi hiyo lililofanyika ndani ya ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha
  Wanenguaji wa bendi ya Fm Academia wakifanya mambo ndani ya ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha.
  Washabiki wa fm wakiwa waangalia show ya nguvu iliyokuwa inadondoshwa na bendi hiyo.
  Picha zote na Woinde shizza wa libeneke la kaskazini blog.

older | 1 | .... | 1064 | 1065 | (Page 1066) | 1067 | 1068 | .... | 3283 | newer