Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1062 | 1063 | (Page 1064) | 1065 | 1066 | .... | 3348 | newer

  0 0


  0 0


  0 0


  0 0


  0 0


  Moja ya barabara zitakazotumiwa na mabasi yaendayo kwa haraka (BRT).
  Moja ya vituo vitakavyotumiwa na mabasi yaendayo kwa haraka pindi mradi utakapo kamilika kwa ajili ya kubeba abiria.
  Kituo cha mabasi yaendayokasi cha Kangwani jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya vituo vitakavyotumika na mabasi hayo tarehe 10 Januari, 2016.

  Mabasi yaendayo kasi yakiwa tayari kwa kuanza safari za kubeba abiria ifikapo tarehe 10 Januari, 2016. 
  Picha zote na Abraham Nyantori - MAELEZO
  0 0

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akipungia mkono wakazi wa mkoa wa Lindi mara baada ya kuwasili mkoani humo ikiwa ndio ziara yake ya kwanza tangia kuteuliwa kwake.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama  Mhe.Nape Nnauye mara baada ya kuwasili mkoani Lindi.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Zamani wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, anayewaangalia katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa mkoa wa Lindi.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa jeshi mkoani Lindi waliojitokeza kumpokea kwenye viwanja vya ndege mkoani Lindi.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri wilaya ya Lindi Vijijini Ndugu Matei B. Makwinya.BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  The Prime Minister of the Republic of Uganda, Rt. Hon. Dr. Ruhakana Rugunda has hailed the EAC Secretariat and various partners for creating a platform for young people to discuss their role in the future of their respective countries and most importantly the East African region.

  Dr. Ruhakana Rugunda, who was today officially opening the 4th EAC University Students’ Debate on Regional Integration at the International University of East Africa campus in Kasanga, Kampala, said as young people, the youth should continue to explore the opportunities being availed by the East African Community and to use such platforms to hasten their knowledge and network among themselves 
  The Prime Minister, who was represented by Prof. Dr. Sandy Stevens Tickodri Tagaboa, the State Minister in charge of Higher Education, Science and Technology, said there was need to encourage dialogues among the youths to promote the ethos of ethical and accountable leadership aimed at developing positive attitudes among the young people in the region.

  He said since the 4th EAC University Students’ Debate was focussing on values, ethics and leadership, the three form the moral fibre of society and were critical to moulding the choices that youth make by imparting in them the desired principles such as integrity and accountability which are key in advancing the broad aims of the EAC integration, with youth as key stakeholders. 
  The Prime Minister disclosed that a National Youth Policy in Uganda was formulated in 2002 with the aim of enhancing youth participation in overall development processes and improving their quality of life. 
  Dr. Rugunda noted that corruption remains a key challenge in the region and it was worrying that only about 53% of East Africans think they can make a difference in the fight against the vice. “This is an alarming statistic and as young people, you should ensure that you fight this trend”

  The Prime Minister noted that young people today had embraced the power of the internet and social media to interact, express themselves and to make their voice heard in a way that was not possible before. He therefore called upon the youth in the region to make linkages between democratic processes and these new ways of expression and communication and to use them to reinforce rather than threaten democracy. 
  While welcoming the students and invited guests to the event, the EAC Deputy Secretary General in charge of Political Federation, Mr. Charles Njoroge said the Debate was one among other initiatives aimed at bringing young people on board to dialogue on core issues pertinent to the EAC integration agenda.

  The Deputy Secretary General reaffirmed that the theme for the debate; the importance of upholding democratic principles, ethics and accountability among youth in advancing EAC integration, was very timely as ethics, integrity and upholding principles of democratic governance were among the fundamental principles and core values of the EAC.

  “Other values that we hold dear, include celebrating unity in diversity, being accountable to the people, upholding the rule of law and ensuring transparency.  The current dialogue on this theme is promising … it is in sync with the on-going debate in most of the EAC Partner States”, noted the EAC official. 
  Prof. Olubayi Olubayi, Vice Chancellor, International University of East Africa urged the students in the region to nurture the culture of innovativeness, while Prof. Pontien Ndabandeza, the Deputy Executive Secretary, Inter-University Council of East Africa, hailed the EAC Secretariat for introducing the spirit and culture of competitiveness within and among the students and University communities in East Africa.

  Director Dr. Alex Awiti, who was also the Moderator for the 4th EAC University Students Debate, represented Aga Khan University. 
  Over 200 young men and women from different Universities in Republics of Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania and Uganda are participating in the 2-day event.
   State Minister in charge of Higher Education, Science and Technology, Prof. Dr. Sandy Stevens Tickodri Tagaboa make his remarks during the officially opening the 4th EAC University Students’ Debate

  EAC Deputy Secretary General in charge of Political Federation, Mr. Charles Njoroge addressing  the  participants


  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa kigoma akiwaeleza wafanyabiashara(ambai hawapo pichani) wa Kigoma umuhimu wa kujiunga na mfuko wa bima ya afya(NHIF)
   Ofisa matekelezo kutoka mfuko wa bima ya afya Kigoma Evance Ndyamkama akiongea na wafanyabiashara wa Kigoma jinsi ya kujiunga na mfuko huo
   Makamu mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara Mkoa wa Kigima(TCCIA) Sethi Naftari akisona hotuba ya wafanyabiashara kwa Mgeni rasmi Issa Machibya na maofisa mfuko wa bima ya afya
   Baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Kigima wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano huo

  =====  ====   ====    =======

  Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii,Kigoma

  WAFANYABIASHARA Mkoani hapa wametakiwa kujiunga na mfuko wa bima ya afya(NHIF) ili waweze kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali mstaafu Issa Machibya wakati akifungua mkutano wa wafanyabiashara na maofisa wa NHIF wa Mkoa wa Kigoma.

  Machibya alisema kuwa suala la kuugua ni la kila mtu na ugonjwa huwa unakuja bila ua taarifa,na magonjwa menfine gharama za matibabu zipo juu lakini kama mtu ana kadi ya bima atakuwa na uhakika wa matibabu.

  "Nina waomba wafanyabiashara mjiunge na mfuko huu wa bima ya afya kwani mtakuwa na uhakika wa matibabu kipindi cha mwaka mzima"alisema Machibya

  Aliwautaka mfuko huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na bima ya afya ili kuongeza wigo mpana wa wananchi wanaonufaika na huduma zao.

  Naye ofisa matekelezo wa mfuko wa bima ya afya Mkoani Kigoma Evance Ndyamukama alisema kuwa kila mfanyabiashara anatakiwa kulipia shilingili elf 76000 itakayomwezesha kupata matibabu kwa kipindi cha mwaka mzima.

  Naye Makamu mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara mkoa wa Kigoma(TCCIA)Sethi Naftari aliuomba mfuko huo uwape kipaumbe cha kuweka na wategemezi wao wanne katika hiyo shilingi elf 76000 kama wafanyavyo watumishi na watu wa makundi mbali mbali.

  "Kama kweli NHIF mmelenga kutusaidia sisi wananchi wa kawaida tunaomba tuwaingize na sisi wategemezi wetu kwenye hayo malipo na yasiwe malipo ya mtu mmoja kwani sisi tumejiajiri"alisema Naftari

  0 0  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatama na Viongozi wakuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar katika maandamano wakati wa mahfali ya kumi na moja ya mwaka 2014/2015 yaliyofanyika leo chuoni hapo Tunguu wilaya ya kati Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake katika sherehe ya mahfali ya kumi na moja ya mwaka 2014/2015 yaliyofanyika leo katika kampasi ya Chuo Tunguu wilaya ya kati Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dk.Ali Mohamed Shein akimtunuku Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika kemia "Master of Science in Chemistry" ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar mhitimu Aflah Abeid Khamis wakati wa mahfali ya kumi na moja ya mwaka 2014/2015 Tunguu wilaya ya kati Unguja.


  0 0

  SONY DSC
  Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (aliyekaa) akipata maelezo kuhusu namna Kituo cha Kihansi kinavyofanyakazi kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambayo imeboresha utendaji kazi kwa wafanyakazi na mitambo ambayo inatumika kuzalisha nishati ya umeme. 

  SONY DSC
  Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (aliyevaa nguo nyeusi) pamoja na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa Injinia kituo cha Kidatu Bw. Yonah Mwasajone (wa kwanza kushoto) kuhusu Sub Station  ambayo baada ya umeme kuzalishwa katika mitambo ya kufua umeme Kidatu hutumika kuuingiza katika Grid ya Taifa.
  SONY DSCBibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (aliyevaa nguo nyeusi) akiangalia na kupata maelezo kutoka kwa Injinia wa kituo Bw. Rajabu Kindunda (wa tatu kulia) kuhusu Bwawa la Kidatu ambalo maji hukusanywa kutoka mto Rufiji kabla ya kutumika kwa ajili ya kuzalisha umeme. Wengine pamoja nae ni wataalamu kutoka Tume ya Mipango na TANESCO.
  SONY DSCBibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (aliyevaa nguo nyeusi) akiangalia eneo la mradi wa kuzalisha umeme Kidatu na kupata maelezo kuhusu faida na changamoto za mradi kutoka kwa Injinia wa TANESCO kituo cha Kidatu Bw. Rajabu Kindunda (wa tatu kulia). Wengine ni wataalamu kutoka Tume ya Mipango na TANESCO.


  0 0


  f3940726-a5ba-43fe-8d8a-66bdb6a1cb19
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na wapigakura wke baada ya kuwasili kijijini kwake Nndagala wilayni Luangwa kwa mapumziko mafupi Desemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  ……………………………………………………………………..
  *Asema wabadhirifu watang’olewa mara moja
  *Asema wako wasomi wengi wanaotafuta ajira
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaonya watendaji wa halmashauri nchini kwamba atakayebainika ametumia vibaya fedha za Serikali atang’olewa kazini kwa sababu Serikali ya Awamu ya Tano haina mchezo na mtu.
   Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Desemba 20, 2015)  wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliofika kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu uliopo Lindi mjini.
   “Natoa onyo kwa watendaji wote wa halmashauri. Fedha ya Serikali itakayotumwa kwenu halafu mtu aifanyie ubadhirifu,  ole wake. Yeyote atakayebainika kuzitumia kwa ubadhirifu fedha hizi tutamng’oa. Wako wasomi wengi huko nje tena wazuri tu, wanasubiri kupata ajira.”
   “Nataka watumishi wa umma watambue kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inajielekeza kujali wananchi.  Wao wana dhamana ya kuwasilikiliza na kuwahudumia wananchi ili kuhakikisha wanatatua kero zinazowakabili, ” alisema huku akishangiliwa na wengine wakisema huyu sasa ni Sokoine wa pili. (Edward Moringe Sokoine alikuwa ni Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Kwanza).
   Waziri Mkuu ambaye amewasili Lindi leo, aliwaeleza wakazi hao kwamba amekuja kuwashukuru wazee na wana Lindi kwa dua zao na kuwaahidi kwamba hatawaangusha Rais John Pombe Magufuli na Makamu wake Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumpa dhamana ya kuwatumikia Watanzania katika ngazi ya Uwaziri Mkuu.
   Waziri Mkuu pia alimpa kazi Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Jordan Rugimbana ya kuhakikisha anaufufua uwanja huo na kuurudisha kwenye enzi yake ulivyokuwa maarufu katika mikoa yote ya Kusini. “Uwanja huu lazima uboreshwe kwa sababu unanikumbusha mwaka 1984 wakati nachezea timu ya Amri Rangers.  Kulikuwa na ukoka wa nguvu hapa uwanjani. Kwa hiyo timu aliyoiunda Mkuu wa Mkoa itafanya kazi lakini pia iwajumuishe Meya na mbunge wa Lindi Mjini kwa sababu huu uwanja ni mali ya Halmashauri ya Lindi, ” alisema.

  Akielezea kuhusu mipango ya Serikali kuendeleza sekta ya viwanda, Waziri Mkuu alisema hivi karibuni mkoa huo utapata wawekezaji kwenye sekta ya gesi baada ya kampuni ya BG kutoka Uingereza kupata umiliki wa eneo la Kikwetu ili wajenge mitambo ya kusafisha gesi.


  Aliwataka wananchi wa mkoa huo wawekeze kwenye ujenzi wa hoteli na nyumba za kulala wageni ili ifikapo Agosti mwakani, watu wanaokuja kushiriki maonyesho ya NaneNane kitaifa mkoani humo wasipate taabu ya malazi kama ambavyo imekuwa ikitokea huko nyuma.

  0 0

  IMG-20151220-WA0012
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wakina mama anayemhudumia mwanae katika wodi ya watoto Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga alipofanya ziara ya kushtukiza leo mchana Disemba 20, 2015.
  IMG-20151220-WA0019
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akimsikiliza mmoja wa akina mama aliyelazwa kwenye wodi ya wazazi wakati wa ziara ya kushtikiza aliyoifanya mchana wa leo Desemba 20, 2015 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga.
  IMG-20151220-WA0011
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wahudumu wa afya (jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi) wa dirisha la dawa katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga alipofanya ziara ya kushtukiza mchana wa leo Disemba 20, 2015.
  IMG-20151220-WA0017
  Daktari aliyekuwa kwenye mafunzo, Dkt. Zuberi (Medical Intern) akitoa maelezo ya namna wanavyohudumia wananchi wanaofika hospitalini hapo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (kulia) aliyefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga mchana wa leo Desemba 20, 2015 ambapo Waziri huyo alikutana na changamoto utoro wa madktari wa zamu kutokuwepo kwenye kituo chao cha kazi katika Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga.
  IMG-20151220-WA0020
  Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO), Dkt. Clement Marceli akimwelezea changamoto wanazokabiliana nazo katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (hayupo pichani).
  IMG-20151220-WA0014
  Baadhi ya madaktari waliokuwa mafunzoni wakizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu  aliyefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo, mkoani Tanga mchana wa leo Disemba 20, 2015.
  IMG-20151220-WA0023

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akipitia orodha ya mahudhurio ya zamu za Madaktari na Wauguzi ambao wengi hawakuwepo kazini wakati wa ziara yake ya kushtukiza katika Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga aliyoifanya leo mchana Disemba 20, 2015.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ulinzi ya Security Group Africa (SGA), Eric Sambu (kulia) akimkabidhi mshine ya kupumulia na mashuka, Mratibu wa Tiba katika Hospitali ya Mwananyamala, Dk Daniel Nkungu. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki. Katikati yao ni Meneja Mahusiano kwa wateja wa SGA, Sophia Luhikula.
   Vitu vilivyotolewa msaada Hosipitalini hapo.
  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ulinzi ya Security Group Africa (SGA), Eric Sambu (kulia) akimkabidhi mshine ya kupumulia na mashuka, Mratibu wa Tiba katika Hospitali ya Mwananyamala, Dk Daniel Nkungu. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mahusiano kwa wateja wa SGA, Sophia Luhikula.

  KWA PICHA ZAID BOFYA HAPA


  0 0

  Ndoa ya Bw. Yassin Shabani Kweka wa Maili Sita mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na bi Rehema Kisarika wa Mbauda jijini Arusha. Ndoa ilifungwa nyumbani Kwa mama Rehema tarehe 19/12/2015.
  Bwana harusi akimlisha asali mkewe wakati wa aqdi mwishoni mwa wiki jijini Arusha
  Hati ya ndoa
  Madada wa Bwana Harusi wakiwa na wifi yao...
  Mawifi kutoka kulia ni aumu ,Leila, Minor na Fatuma.
  Maharusi kwenye pozi ya furaha baada ya kumeremeta

  0 0

  Golikipa wa JKT Ruvu, Shaban Dihile akipishana na mpira uliopigwa na mchezaji wa Coastal Union, Nassoro Kapama katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2. (Picha na Francis Dande)
   Issa Ngao (kushoto), akimtoka mchezaji wa Coastal Union ya Tanga.
    Hamis Shango (kushoto) akichuana na Chidiebere Abasalim.
   Mchezaji wa Coastal Union ya Tanga, Chidiebere Abasalim (katikati) akiwania mpira na wachezaji wa JKT Ruvu.
  Wachezaji wa JKT Ruvu wakishangilia baada ya kupata bao la pili.
   Mchezaji wa JKT Ruvu akimiliki mpira.
    Juma Mahadhi (kushoto) akichuana na Hamis Shango.

  0 0

   Mbeya city yatoka sale na Mgambo Jkt kwa mabao ya goli 1-1  ambapo  Goli la Timu ya Mbeya City Fc lilifungwa na Abdalla Juma Dakika ya 30 huku Fully Zullu Maganga akisawazisha na kuipatia Goli Timu ya Mgambo Jkt Dakika ya 71 katika Mtanange uliochezwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya  katika  muendelezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Kikosi cha Timu ya Mgambo Jkt katika Picha ya Pamoja Kabla ya mechi kuanza.
  Kikosi cha Timu ya Mbeya City Wakoma Kumwanya.
  Mashabiki wa Timu ya Mbeya City wakishangilia Timu yao.
  Kocha Mpya wa Timu ya Mbeya City FC  Abdul Mwingange akizungumza jambo na  Waandishi wa Habari baada ya Mtanange huo kumalizika. 
  PICHA NA MR.PENGO MBEYA.

  0 0

  Na Emmanuel Ghula –NBS 
  Serikali imevitaka vyuo na taasisi za elimu nchini kuhakikisha vinatoa mafunzo bora yanayoendana na mahitaji ya soko la ajira. 
  Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mahafali ya kwanza ya Shahada ya Takwimu Rasmi katika Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema ni vyema vyuo na taasisi za elimu kuhakikisha vinafanya tafiti kujua mahitaji ya wataalamu wanaotakiwa na kutoa mafunzo yanayoendana na soko la ajira.
  “Nchi yetu inahitaji kuwa na watalaamu wa fani mbalimbali hivyo ni wajibu wa vyuo vya elimu ambavyo ndio wazalishaji wa wataalamu hao kuhakikisha vinatoa wataalamu wenye ujuzi wa kutosha unaoendana na mahitaji ya soko la ajira ndani na nje ya nchi,” alisema Balozi Sefue. 
  Balozi Sefue alisema kutokana na umuhimu wa takwimu katika maendeleo, Serikali imekuwa mstari wa mbele kupitia Wizara ya Fedha kuhakikisha inakisaidia chuo hicho kukabiliana na changamoto zinazokikabili ikiwemo uhaba wa fedha za kuendeshea chuo hicho. 
  Aidha, alisema chuo hicho kuanza kutoa shahada ni hatua kubwa kwasababu chuo hicho ndio tegemeo la Afrika katika kuzalisha watakwimu wanaosaidia katika ukusanyaji wa takwimu bora zinazotumika katika kupanga na kupima utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo. Aidha, Sefue amekitaka chuo hicho kubuni miradi mbalimbali itakayosaidia kujipatia fedha kwa ajili ya kutatua baadhi ya changamoto zinazojitokeza chuoni hapo. 
  Alisema Chuo Cha Takwimu cha EASTC mwaka huu kimefikisha miaka hamsini ya utoaji wa mafunzo ya Takwimu na wataalamu mbalimbali wa takwimu wanaofanya kazi Serikalini wamepitia hapo na hivyo ni wajibu wa Serikali kuhakikisha inakiendeleza ili kiwe kituo bora zaidi kwa utoaji wa watakwimu waliobobea. 
  Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Professa Innocent Ngalinda amesema chuo hicho kimejipanga vyema kuhakikisha kinaendelea kuzalisha watakwimu bora na wenye weledi katika fani ya takwimu. 
  “Hivi sasa tumefikia hatua kubwa sana ya kuanza kutoa wahitimu wa Shahada ya kwanza ya Takwimu Rasmi, tutaendelea kuwa mhimili wa uzalishaji wa wataalamu hawa muhimu katika maendeleo ya nchi yetu na bara la Afrika kwa ujumla,” alisema Professa Ngalinda. 
  Professa Ngalinda alisema chuo hicho kitaendelea kufanya kazi kwa karibu na nchi wanachama ili kuhakikisha wahitimu wake wanakuwa chachu ya maendeleo kwa kusaidia ukusanyaji wa takwimu bora na kwa wakati ili zitumike katika kupanga na kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Jumla ya wanafunzi 29 wamehitimu na kutunukiwa Shahada ya kwanza ya Takwimu Rasmi katika mahafali hayo ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika.
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akiwa kwenye maandamano na wahitimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo maeneo ya Changanyikeni  jijini Dar es Salaam. Kushoto  kwake ni  Mkuu wa Chuo hicho, Professa Innocent Ngalinda.
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akihutubia kwenye mahafali ya kwanza ya Shahada ya Takwimu Rasmi ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo maeneo ya Changanyikeni  jijini Dar es Salaam
   Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika pamoja na wahitimu wa Shahada ya kwanza ya Takwimu Rasmi katika chuo hicho kilichopo maeneo ya Changanyikeni  jijini Dar es Salaam. 
  HABARI NPICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA wa NBS  0 0
  0 0

  Bw. Noel Kaganda,  Afisa  Mwandamizi, Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  akizungumza  kwa  niaba ya Tanzania wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  lilipokutana  mwishoni mwa wiki  kujadili kuhusu ajenda ya Afya na Sera ya Mambo ya Nje.
  -------------------------------------------------------------------------
  Mwishoni  mwa wiki, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilijadili ajenda ya Afya na Sera ya Mambo ya Nje ambapo pamoja na mambo mengine lilipitisha azimio linalotathmini utayari wa nchi wanachama kukabiliana na magonjwa ya milipuko na dharura nyingine za kiafya.


  Katika mjadala huo, wazungumzaji wengi, walisisitiza   umuhimu wa kuimarishwa kwa mifumo ya afya, hususan katika nchi za kipato cha chini na cha kati zisizo na uwezo wa kutosha wa kukabiliana na magonjwa ya milipuko. Wazungumzaji hao walieleza umuhimu wa kung’amua mafunzo muhimu ya janga la ugonjwa wa Ebola uliosababisha maafa makubwa katika nchi za Guinea, Sierra Leone na Liberia. 
  Akichangia katika mjadala huo kwa niaba ya serikali ya Tanzania, Bw. Noel Kaganda, Afisa Mwandamizi katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa alisema kuwa pamoja na jitihada zilizolenga kuimarisha sekta ya afya katika kipindi kilichomalizika cha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia, sekta hiyo bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile upungufu wa madaktari na wauguzi; vifaa finyu na vichakavu; na mazingira yasiyo salama. 
  Aksisitiza  kuwa, jitihada za kuboresha afya ya binadamu, hususan ya akina mama na watoto, lazima ziendelezwe kwa ufanisi zaidi katika muktadha wa Agenda ya Maendeleo Endelevu  hadi kufikia mwaka 2030. 
  Aliongeza kuwa pamoja na kuzuia vifo vya watoto wachanga, ambavyo idadi yake ulimwenguni kwa mwaka 2015 imefikia milioni 6, sawa na vifo 16,000, jumuiya ya kimataifa haina budi kuzijengea nchi zinazoendelea uwezo wa kukabiliana na magonjwa ya milipuko kama vile Ebola na mengineyo, ambayo yanaweza kuathiri jamii nyingi duniani kufuatia kushamiri kwa utandawazi na uharibifu wa mazingira unaosababishwa na binadamu. 
  Pamoja na kusisitiza kuwa wananchi wote wapatiwe huduma bora za afya, Tanzania iliunga mkono mapendekezo ya ripoti ya wa Shirika la Afya Duniani kuhusu ulinzi na ustawi wa watumishi katika sekta ya afya. 
  Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watumishi wengi wa sekta ya afya wanadhalilishwa na kushambuliwa wakiwa kazini na wanaathirika na majanga mengine kama vile Tsunami na matetemeko ya ardhi. Tanzania ilisema kuwa vitendo hivyo vinachangia katika kuzorota kwa sekta ya afya, hivyo ilitaka vikomeshwe mara moja. Pia ilipendekeza wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria katika ngazi ya kitaifa na kimataifa. 
  Vilevile ilitaka watumishi wa sekta ya afya wapatiwe mafunzo na zana za kujilinda na maambukizi, ili waweze kutimiza wajibu wao ipasavyo. Kadhalika ilisisitiza umuhimu wa mashirikiano baina ya nchi wanachama na wadau wengine wa afya, kama vile Shirika la Afya Duniani, yenye lengo la kuzijengea nchi zinazoendelea uwezo wa kukabiliana na dharura za kiafya. 
  Taarifa ya Shirika la Afya Duniani imekuja siku chache kabla ya jopo la Ngazi ya Juu lililoteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupendekeza namna bora ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko duniani. Jopo hilo linaloongozwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, linatarajia kuwasilisha taarifa yake mwezi Januari 2016. 

  Katika hatua nyingine, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeazimia kufanya mkutano wa ngazi ya juu kuhusu “antimicrobial resistance” kwa lengo la kubaini kiini cha magonjwa sugu kama kama ilivyo kwa baadhi ya jamii za ugonjwa wa Kifua Kikuu.
older | 1 | .... | 1062 | 1063 | (Page 1064) | 1065 | 1066 | .... | 3348 | newer