Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO AFANYA ZIARA OFISI YA BODI YA MFUKO WA BARABARA

0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani ameitaka Bodi ya Mfuko wa Barabara kutotuma fedha za ujenzi wa barabara kwa halmashauri yoyote nchini ambayo imetumia fedha walizopelekewa kinyume na malengo yaliyokusudiwa. 
Na amemwagiza Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara kuzichukulia hatua halmashauri zote ambazo zimetumia fedha hizo tofauti na malengo yake ikiwa ni pamoja na kutopelekewa fedha mpaka hapo watakapozijeresha fedha walizozitumia. 
“Ongezeni nguvu zaidi katika kusimamia matumizi ya fedha za mfuko wa barabara kwa baadhi ya halmashauri ambazo fedha hizo zinatumika kwa shughuli zisizo za barabara”, alisisitiza Mhe. Ngonyani 
Ameyasema hayo wakati alipotembelea ofisi za Bodi ya Mfuko wa Barabara jijini Dar es salaam na kuelekeza Halmashauri zote nchini kutotumia Wahandisi ambao hawajasajiliwa na Bodi ya Wahandisi (ERB), kusimamia miradi katika halmashauri hizo. 
Naye Meneja wa Mfuko wa Barabara Joseph Haule ameelezea mafanikio ya bodi hiyo toka kuanzishwa miaka 15 iliyopita kuwa mapato yameongezeka kutoka sh bilioni 73 mwaka 2005 hadi sh. Bilioni 752. 
“Kutokana na mapato kupanda mtandao wa barabara umeboreshwa kwa kiwango kikubwa kwa kuwa barabara nyingi zimetengenezwa kutokana na fedha hizo”, alisema Meneja Haule. 
Hata hivyo, Bodi imeendelea kuhakikisha kwamba tozo za barabara zinakusanywa kikamilifu na kuwekwa kwenye mfuko. 
Pia imetoa maelekezo kwa taasisi ambazo zinakusanya mapato ya Mfuko kutumia mfumo wa kielektroniki badala ya kupokea fedha taslimu. Meneja Haule amemhakikishia Mhe. Ngonyani kuendelea kuwa na mahusiano mazuri na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakala wa Barabara (TANROADS) na Mamlaka za Udhibiti za EWURA na SUMATRA katika upatikanaji wa taarifa juu ya makusanyo ya fedha za Mfuko wa Barabara na kuhakikisha vyanzo vipya vya mapato vinapatikana.
 Aidha Meneja Wa Mfuko wa Bodi hiyo aliiongeza kuwa Bodi itaongeza mkazo katika ufatiliaji wa matumizi ya fedha za mfuko wa barabara ili kodi za wananchi ziweze kutumika kama ilivyo kusudiwa na tayari mfuko huo umeanzisha kitengo cha Tathimini na Ufuatiliaji wa fedha hizo. 
Katika kuhakikisha ufatiliaji na usimamizi wa fedha hizo unatekelezwa Bodi tayari imeshachukua hatua kwa Halmashauri tatu zikiwemo Halmashauri ya Kinondoni, Songea Vijijini na Bukoba vijijini ambazo zimetumia fedha za mfuko wa barabara kinyume na malengo yaliyokusudiwa. 
Bodi ya Mfuko wa Barabara imeanzishwa rasmi kwa lengo la kukusanya mapato, kufuatilia matumizi ya fedha hizo na kugawa fedha kwenye taasisi ambapo asilimia 63 zinapelekwa TANROADS kwa ajili ya matengenezo ya barabara kuu na za mikoa, asilimia 30 katika Halmashauri 166 kwa ajili barabara Halmashauri, na asilimia 7 zinapelekwa Wizara ya Ujenzi.
Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), Joseph Haule akitoa taarifa ya utendaji kazi wa bodi hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani mara baada ya kutembelea ofisi hizo na kuangalia jinsi inavyofanya kazi, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akisisitiza umuhimu wa kufatilia fedha za mfuko wa barabara kutumika katika shughuli za barabara kama ilivyopangwa kwa mujibu wa sheria kwa watendaji wa bodi hiyo.
Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), Joseph Haule (wa kwanza kulia) pamoja na maafisa wa mfuko huo wakisikiliza kwa makini maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani.

WAZIRI KITWANGA ALA KIAPO CHA KUWA MWENYEKITI WA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA

0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akila kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga mara baada ya kumuapisha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Picha na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.

WAZIRI MAHIGA MKOANI KUFANYA ZIARA MKOANI ARUSHA

0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga atafanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Arusha kuanzia leo Jumamosi tarehe 19 Desemba 2015.
Atakapokuwa mkoani Arusha, Balozi Mahiga atafanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dkt. Richard Sezibera. Mazungumzo yao yatahusu namna ya kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.
Aidha, Mhe. Waziri atatembelea eneo la Lakilaki ambalo limetengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za taasisi za kimataifa. Ujenzi unaoendelea hivi sasa kwenye eneo hilo ni jengo la ofisi la taasisi ya Mechanism for Crime Tribunals (MICT) inayorithi shughuli za Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) ambayo itakamilisha shughuli zake tarehe 31 Desemba 2015.
Mhe. Waziri pia atatembelea Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kuonana na uongozi wa Kituo hicho kwa madhumuni ya kufahamiana. AICC ni moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Mhe. Waziri atarejea jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili tarehe 20 Desemba 2015.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
18 Desemba, 2015

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI LEO

INTRODUCING Buku Jero official HD Video BY Witnesz kibonge mwepec

SIMU TV: DONDOO ZA MAGAZETI LEO

0
0

SIMU.TV:   Waziri awafungia geti wafanyakazi wa wizara.  12 wafariki ajali ya basi la New Force. CHADEMA yazungumzia kasi ya rais Magufuli;https://youtu.be/oZYeH59y4SI
 SIMU.TV:   Watumishi waliotumia vyeti feki  serikalini kukiona cha moto.  TMA  yasema Elninyo kuendelea mpaka Aprili mwakani; https://youtu.be/wmJb-ZHmd4A 
  SIMU.TV:   Kocha Kerr aficha mbinu.  CCM Kirumba kuchimbika leo. Majabvi  ashtukiwa, akatwa mshahara Simba, https://youtu.be/wqcG-CPluiU
 SIMU.TV:   Pata habari za kina zilizopewa kipaumbele katika magazeti ya leo Jumamosi Desemba 19.2015; https://youtu.be/yPokI-5bXwo

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji atembelea Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

0
0

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji
Naibu Waziri wa Fedha akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na menejimenti ya TRA. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bw. Benard Mchomvu na Kushoto kwake ni Naibu Kamishna Mkuu Bw. Lusekelo Mwaseba.
---
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji ametembelea Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufahamiana na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Uongozi wa TRA na kusisitiza msimamo wa serikali ya awamu ya tano katika suala zima la ukusanyaji wa mapato.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya TRA, Dr. Kijaji pamoja na kutoa pongezi kwa TRA kwa jukumu kubwa la kukusanya mapato, ameomba ushirikiano kutoka kwa Bodi na Uongozi wa TRA ili kuweza kuivusha Tanzania salama.Ameongeza kuwa kuwepo ushirikiano kutasaidia TRA kuweza kufikia malengo ya serikali ya kukusanya kodi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
“Bila mapato hakuna taifa linalosonga mbele”, alisema Naibu Waziri ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Servacius Likwelile.Amesema nchi inategemea mapato kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kwa wananchi na hivyo kuwaongezea wananchi matumaini kwa kuwafikishia huduma muhimu.

Ameutaka uongozi wa TRA kushikamana na kuunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya “Hapa Kazi Tu” kwa kusimama imara na kuwabaini wale wanaoichafua TRA na kuwachukulia hatua za kisheria. “Tusikubali wachache wanaotuchafua waendelee kutuchafua”, amesisitiza Naibu Waziri.
Dr. Kijaji amesema kwamba ili wafanyabaishara waifurahie TRA ni lazima kuimarisha ushirikiano kati yake na wafanyabiashara.
Ili kuzidi kuongeza makusanyo, Naibu Waziri ameshauri kuwa misamaha itolewe kwa vigezo, kuimarisha makusanyo yatokanayo na madini. “Tukusanye kodi maeneo yote yanayostahili ili kupunguza utegemezi. Hakuna haja ya kupiga magoti kwa wahisani”, alisema Naibu Waziri na kuongeza kuwa serikali itaendelea kusimamia mazingira ya uchumi na kuhakikisha hakuna kodi ambazo zinakatisha tamaa wawekezaji.
Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA Bw. Benard Mchomvu amempongeza Naibu Waziri kwa niaba ya wafanyakazi wa TRA kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge na hatimaye kuteuliwa na Rais kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango.
Naye Kaimu Kamishna Mkuu Dr. Philip Mpango amemweleza Naibu Waziri kwamba TRA ina wataalamu wazuri wa kodi na inakitumia vizuri Chuo cha Kodi kufundisha wafanyakazi ambao wengi wanakuwa wataalamu wa kodi. Amesema wafanyakazi wanaogundulika kukiuka taratibu za kazi wanachukuliwa hatua lakini wengine wanachapa kazi kwa kufanya jitihada za kukusanya mapato yanayoendana na uchumi wa nchi yetu. “Wafanyakazi wa TRA wanaipenda nchi yao”, amesema Kaimu Kamishna Mkuu.
Kuhusu kufikia lengo la makusanyo hadi Desemba mwaka huu, Dr. Mpango amesema anaimani idara zote za TRA zitafikia malengo. “Matarajio ni kujitahidi kukusanya na kufikia trilioni 1. 3 mwishoni mwa mwezi Desemba” alisema Naibu Kamishna Mkuu.
 Ziara ya Naibu Waziri Dr. Kijaji ni ya kwanza tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 11 Desemba 2015 kushika wadhifa huo.

MAPITIO YA MAGAZETI LEO


KIGOMA UJIJI YAPATA MEYA TOKA ACT Wazalendo.

0
0
Madiwani wa Manispaa ya Kigoma ujiji wakiwa katika picha ya pamoja .
Mwenyekiti wa uchaguzi wa Meya na Naibu meya mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe akitoa maelezo ya awali kabla ya uchaguzi.
 Meya wa Manispaa ya kigoma Ujiji Hussein Ruhavi akimweleza jambo makamu meya  Athuman Mussa wa manispaa hiyo kushoto ni mbunge wa Kigoma mjini ndiye alikuwa mwenyeti wa uchaguzi
 Mmoja wa Madiwani akipiga kura ya kumchagua meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji

Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii,Kigoma

BARAZA la madiwani la Halmashauri ya Kigoma Ujiji  limemchagua Diwani wa kata ya Bangwe Hussein Ruhavi kuwa meya wa Manispaa hiyo.

Mbunge Zitto Zuberi Kabwe alikuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo alimtangaza diwani Ruhavi kutoka chama cha ACT wazalendo kuwa mshindi wa kiti cha umeya kwa kupata kura 19 kati ya kura 21 zilizopigwa na akamshinda mpinzani wake Masudi Kassim kutoka chama cha mapinduzi(CCM).

Pia Zitto alimtangaza diwani wa kata ya Buzebazeba Athumani Mussa kupitia chama cha ACT wazalendo kuwa naibu meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji alimshinda Mussa Maulid wa CCM aliyepata kura moja.

Baada ya kutangaza matokeo Zitto ambaye ni mbunge wa jimbo la kigoma mjini alisema kuwa watasimamia mipango ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa usawa.

"Diwani yeyote ambaye kwa makusudi ataamua kukwamisha michakato mbalimbalu ya maendeleo tutamshughulikia lwa namna tutakayojua sisi"alisema Zitto

Naye meya Hussein Ruhavi akizungumza baada ya kuchaguliwa aliwashukuru madiwani kwa imani yao waliyoionyesha kwake kwa kumchagua kuwa Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Alisema atafanya kazi kwa kushirikuana na madiwani wote ili kuwaletea wananchi maendeleo,pia aliwataka madiwani kufanya kazi pamoja bila ya kujali itikadi zao

Rais Magufuli amtumia salamu za Rambirambi Rais Kikwete kwa kufiwa na Dada yake

0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye amepatwa na msiba mzito wa kufiwa na Dada yake Mpendwa Bi. Tausi Khalfan Kikwete kilichotokea jana tarehe 17 Desemba, 2015 huko nchini India.

Katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema anaungana na familia ya Rais Mstaafu Kikwete katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na mtu muhimu kwa familia."Kwa masikitiko makubwa nakupa pole nyingi Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwa kufiwa na dada yako ambaye alikua nguzo muhimu katika familia" Amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amemuomba Rais Mstaafu Kikwete kumfikishia salamu nyingi za pole kwa familia nzima na amewaomba wawe na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.Rais Magufuli amemuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema aipumzishe roho ya marehemu Tausi Khalfan Kikwete mahali pema peponi, Amina.

Imetolewa na;
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU


18 Desemba, 2015

CHINA YASAIDIA VITANDA 60 VYA KUJIFUNGULIA WAKINA MAMA KWA MKOA WA LINDI

0
0
  Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing akiangalia baadhi ya vitanda ambavyo vimekabidhiwa kwa mkoa wa Lindi kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye hospitali ya mkoa wa Lindi Sokoine.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiangalia vitanda hivyo vya kujifungulia wakina mama akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Taasisi ya kukuza Urafiki wa Tanzania na China  Ndugu Joseph Kulwa Kahama.
 Bi. Ziada Maulid akitoa shukrani zake mbele ya Balozi wa China nchini  Dk. Lu Youqing mara baada ya ya Balozi huyo kukabidhi vitanda 60 vya kujifungulia wakina mama.
 Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama wakiwasili katika kata ya Kiwalala, jimbo la Mtama tayari kwa kukabidhi vifaa vya matibabu katika Zahanati ya Mauhumbika.
 Wakazi wa kijiji cha Mahumbika wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia makabidhiano ya vifaa vya matibabu katika Zahanati yao.
  Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing akihutubia wakazi wa Mahumbika ambapo pamoja na kuahidi misaada zaidi ikiwemo kwenye matatizo ya maji, Balozi pia aliahidi kusaidia vijana wanaomaliza Chuo Kikuu kwenda kujiendeleza nchini China.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa salaam za shukrani kwa Serikali ya China kwa msaada wa vifaa vya tiba vilivyogharimu zaidi ya milioni 20.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi Ajali ya Basi la New Force Iringa

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza kufuatia ajali ya basi la kampuni ya New Force kugongana na lori, na kusababisha vifo vya watu 12, na wengine 15 kulazwa Hospitali.

Ajali hiyo imetokea tarehe 18 Desemba, 2015 Majira ya saa nane mchana katika Kijiji cha Mahenge, Wilaya ya Kilolo Mkoani IRINGA ambapo Basi la kampuni ya New Force lenye namba T 483 CTF lililokuwa limebeba abiria 49 limegongana na Lori la Kampuni ya Reign-ford Limited lenye namba T 616 BEF na Tela lake lenye namba T 320 DEF lililokuwa na shehena ya mbao .

Rais Magufuli amemuomba Mkuu huyo wa mkoa kufikisha salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote ambao wamepoteza ndugu zao katika ajali hiyo mbaya"Nimesikitishwa sana na kutokea kwa ajali hii, ninawapa pole nyingi wote waliopoteza ndugu zao na ninawaombea Majeruhi wote wapone haraka ili waungane na familia zao na kuendelea na shughuli zao za maendeleo" amesema Rais Magufuli.

Amewaombea marehemu wote kwa Mwenyezi Mungu ili azipumzishe roho zao mahali pema peponi, Amina.Aidha Dkt. Magufuli ametoa wito kwa watuaji wote wa barabara hususani madereva kuwa waangalifu waendeshapo vyombo vya usafiri na amewakumbusha wananchi wanaotumia barabara kwa kusafiri ama kusafirisha mizigo kutoa ushirikiano kwa vyombo husika pale wanapobaini kuwepo vitendo ambavyo ni chanzo cha ajali.

Imetolewa na;  Gerson Msigwa,
                        Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU



                        18 Desemba, 2015

TAARIFA YA MSIBA

0
0
Familia ya Bw. Mgalula Fundikira inasikitika kuwataarifu ndugu, jamaa na marafiki kuwa mwanawe Mlawila (Lawi) Fundikira (18) (pichani) amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kulazwa kutokana na ajali ya gari aliyopata alfajiri ya jumapili ya tarehe 12/11/2015.

Msiba upo Kinondoni block 42 (Bwawani) mtaa ilipo Facebook take away. Mazishi yatafanyika kesho saa 10 jioni katikai makaburi ya Kisutu.

NEC yatangaza Majimbo ya Masasi Mjini na Ludewa kufanya uchaguzi tarehe 20 Desemba, 2015

0
0
Na Joseph Ishengoma, MAELEZO

Majimbo ya Masasi Mjini mkoani Mtwara na Ludewa mkoani Njombe yanatarajia kufanya uchaguzi wa wabunge kesho (20.12.2015) ili kuwapata viongozi watakaoongoza majimbo hayo kwa kipindi cha miaka mitano.

Majimbo hayo hayakufanya uchaguzi tarehe 25.10.2015 kutokana na baadhi ya wagombea katika majimbo hayo kufariki dunia.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damiani Lubuva amewasihi wananchi kujitokeza na kupiga kura kwa amani na utulivu. Jaji Lubuva amesema hayo leo jijini Dar Es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari.

“Tume inawasihi na kuwashauri wananchi kujitokeza kupiga kura kwa amani. Hakuna sababu Masasi na Ludewa kuwa tofauti na majimbo mengine yaliyofanya uchaguzi kwa amani na utulivu,” alisema Lubuva.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo amewaonya      Viongozi wa vyama vya siasa kutoingilia kazi ya tume katika uchaguzi huo. 

“Viongozi wa vyama vya siasa wasiingilie kazi ya Tume ya Uchaguzi. Ulimwengu unatusifia kuwa uchaguzi uliopita ulifanyika kwa amani. Kila mwananchi, viongozi wa dini na vyama vya siasa tushirikiane wote kuhakikisha kuwa viashiria vya uvunjifu wa mani na utulivu vinaepukwa ili uchaguzi uwe huru, wazi na wa haki,” aliongeza Lubuva.

Jaji Lubuva alisisitiza kuwa watu wakisha piga kura waondoke vituoni ili kutowazuia wananchi wanaokuja kupiga kura isipokuwa Mawakala na wasimamizi wa uchaguzi wanaoruhusiwa kwa mujibu wa sheria.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Daftari la Wapiga Kura litakalotumika ndio lile lililotumika wakati wa uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25.10.2015.


Baada ya uchaguzi wa majimbo ya Ludewa na Masasi Mjini, litasalia jimbo la Kijitopele Zanzibar ambalo uchaguzi wake utategemea lini uchaguzi wa Zanzibar utakapofanyika.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva akitangaza taarifa ya Upigaji kura kwa Majimbo ya Masasi Mjini na Jimbo la Ludewa siku ya tarehe 20 Desemba, 2015 mara alipokutana na Waandishi wa Habari leo 19 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Tume uliopo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akifafanua kuhusu taarifa aliyoitoa iliyohusu Upigaji kura kwa Majimbo ya Masasi Mjini na Jimbo la Ludewa siku ya tarehe 20 Desemba, 2015 mara alipokutana na Waandishi wa Habari leo 19 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Tume uliopo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhcgauzi wa Tume hiyo BwanaKailima Ramadhani.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano huo wakifuatiliana taarifa ikiyotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva kuhusu Upigaji kura kwa Majimbo ya Masasi Mjini na Jimbo la Ludewa siku ya tarehe 20 Desemba, 2015 mara alipokutana na Waandishi wa Habari leo 19 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Tume uliopo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bwana Kailima Ramadhani wakijadili jambo mara baada ya kutolewa kwa tarifa ya Upigaji kura kwa Majimbo ya Masasi Mjini na Jimbo la Ludewa siku ya tarehe 20 Desemba, 2015 mara alipikutana na Waandishi wa Habari leo 19 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Tume uliopo Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo)

JESHI LAWASAKA WALIOENEZA TAARIFA ZA UZUSHI MITANDAONI

0
0
Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka tabia ya baadhi ya watu kutoa taarifa za uzushi na uongo kutumia majina ya taasisi, mashirika ya umma na ofisi za Serikali na kueneza taarifa hizo  katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kupotosha wananchi. 

Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na taarifa kuhusu Jeshi la Polisi iliyosambazwa jana katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari  ‘chujio Jesho la polisi, vyeti feki vyawaonndoa askari kazini’  Taarifa hiyo ni uzushi na hajatolewa na Jeshi la Polisi.

Kufutia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapenda kukanusha taarifa hiyo  ya uzushi ambayo haina ukweli wowote  na inalengo la kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi kwa jamii.  

Jeshi la Polisi nchini limeanza upelelezi wa kuwatafuta watu wote waliohusika kueneza taarifa hiyo na kujifanya wao ni Jeshi la Polisi. Aidha, Tunatoa onyo kali kwa watu  wote kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya  kwa kufanya uposhaji na badala yake watumia mitandao hiyo kwa ajili ya ustawi wa jamii.

Imetolewa na:
Advera John  Bulimba – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.

Ligi Kuu ya Muungano ya Netiboli yaendelea Uwanja wa Gymkhana, Zanzibar

0
0
Wachezaji wa Timu ya TTPL na Polisi Moro wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Muungano zinazofanyika katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar timu ya Polisi Moro imeshinda 36--33.
Mchezaji wa timu ya TTPL Mwanaasha Ali ( GS) akiwa na mpira huku mchezaji wa timu ya Polisi Moro Jawa Iddi (GD) akijiandaa kumzuiya katika mchezo wao wa kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu ya Muungano ya Mchezo wa Netiboli yanayofanyika katika viwanja vya Gmykhana Zanzibar Timu ya Polisi Moro imeshinda 36--33.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MRADI WA MABASI YAENDAYO HARAKA (DART) KUANZA JANUARI 10, 2016.

0
0
MRADI wa Mabasi yaendayo haraka (BRT) kuanza Januari 10, 2016 hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa wakati akikagua ujenzi wa miundo mbinu ya Mradi wa Mabasi yaendayo haraka leo jijini Dar es Salaam.

Pia Majaliwa amewaagiza watendaji wizara ya Tamisemi ambao ni wamiliki wa mradi huo kusimamia vyema ili uanze kufanya kazi kama ilivyo pangwa kwa kuwa mabasi 120 yalishawasili jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ameanza kwa kukagua vituo vya mradi huo kuanzia cha Feri, Jangwani, Kimara na kumalizia na Morocco na kuwapongeza kwa kumaliza kujenga vituo 15 kati ya 27 na amewaagiza kumalizia vituo vilivyo baki ili kufikia januari 10 mwakani mabasi yaanze kufanya kazi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na watendaqji mbalimbali wa mradi wa mabasi yaendayo haraka waliofika katika kituo cha Feri cha Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (BRT) leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akitembelea maeneo mbalimbali ya kituo cha Feri jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akipanda basi la mwendo wa haraka mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali katika kituo cha feri leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa katika kituo cha Mradi wa mabasi cha Jangwani kukagua maendeleo ya ujenzi ya kituo hicho ikiwa ujenzi wa kituo hicho upo hatua za mwisho kukamilika.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

WATAOPEWA FEDHA ZA ELIMU BURE WATAKIWA KUWA NA UADILIFU NA UAMINIFU –SHIRIKISHO

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

SHIRIKISHO la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), limesema  kuwa waliopewa wajibu wa kusimamia fedha za elimu  bure wanatakiwa uaminifu na uadilifu kutimiza suala hilo.

Akizungumza na waandishi habari  Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Zainabu Abdallah amesema kuwa kwa wale ambao watakiuka matumizi ya fedha za elimu bure, wamemtaka Rais John Pembe Magufuli  kutokuwa na huruma kwa yeyote atakayefanya urasimu usio na tija kukwamisha utekelezaji wa  ahadi ya wananchi ya kupata elimu bure.

Amesema maazimio hayo yametokana na kikao kilichofanyika hivi karibuni kilichojadili masuala mbalimbali ya serikali ya awamu ya tano na kulitathmini shirikisho na  hatimae kubaini kuwa wako nyuma ya kutokwenda na wakati.

Zainabu amesema katika kwenda na kasi wameunda kamati mbalimbali za shirikisho,amesema mosi wameanzisha dawati la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu  katika kuondoa vikwazo vya kutopata mikopo kwa wakati.

Pili amesema kuwa wameunda kamati ya uwezeshaji ambayo itafanya kazi ya kuibua fursa za ajira katika midahalo na semina hali ambayo  itasaidia kuwafundisha wasomi juu ya kuanzisha biashara na kusimamia.

Zainabu amesema kuwa iwapo wao ni wasomi,inawapasa lazima waendane na kasi ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa ajili ya fedha milioni 50 kwa vijana kuwa wabunifu wa miradi.



Aidha wakati huo huo Shirikisho hilo limeitaka serikali kufanya uhakiki wa watumishi feki kutokana na kazi wanazozifanya sio zao na kusababisha watu wenye sifa kushindwa kupata kazi ili kuweza kuwatumikia wananchi.

NAIBU WAZIRI DKT. KIGWANGALLA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA LEO KATIKA HOSPITALI ZA RUFAA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

0
0
IMG_9550
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na duka la dawa kwa wagonjwa wanaotumia huduma ya bima ya afya katika Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara. Kulia ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa.
IMG_9567
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisikiliza maelezo kutoka kwa Daktari wa zamu kitengo cha dharura hospitalini hapo,Dkt. Ester Tumwanga (kulia) wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa.
IMG_9602
Muuguzi Kiongozi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Getrude Mangosongo (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kushoto) alipotembelea wodi ya akinamama wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo. Kushoto ni Daktari wa zamu kitengo cha dharura hospitalini hapo,Dkt. Ester Tumwanga na wa pili kulia ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa.
IMG_9619
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akiwasili katika jengo jipya la Hospitali ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara ambalo linaendelea kujengwa na litahudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na nchi za jirani ikiwemo Msumbuji.

LONGHORN PUBLISHERS WAKIZINDUA KAMUSI KUU YA KISWAHILI KUTOKA BAKITA

0
0
 Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Magesa Mulongo akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kamusi ya kiswahili huku akishuhudiwa na mwenyekiti wa TAHOSSA Taifa Bonus Ndimbo katika ghafla iliyofanyika kwemye mkutano mkuu wa TAHOSSA jijini Mwanza.
 Mgeni rasmi akiwaonyesha wakuu wa shule nchini (hawapo pichani) kamusi kuu ya kiswahili aliyoizindua, kushoto ni muhariri mkuu wa kamusi hiyo James Mwilaria
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Masesa Mulongo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Longhorn Publishers Ltd.
 Meneja mauzo na msimamizi wa matangazo wa Longhorn Publishers Ltd Deisy Rono akimuonesha mgeni rasmi baadhi ya machaisho yao.

Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images