Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1060 | 1061 | (Page 1062) | 1063 | 1064 | .... | 3348 | newer

  0 0

  IMG_9172
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akipitia mahudhurio ya watumishi wa wizara kwa siku zilizopita.
  IMG_9181
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akipitisha mstari wa kufunga mahudhurio kwa watumishi ambao wameripiti kabla ya saa 1:30 asubuhi ya leo.
  IMG_9198
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akiendelea na zoezi hilo la kupitisha mstari kwa kila idara za wizara hiyo.
  IMG_9231
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu juu ukaguzi huo katika ofisi za wizara yake ya afya ili kuboresha utendaji wa wizara hiyo na vituo vyote vya sekta ya afya nchini kote.

  Na Rabi Hume, Modewjiblog Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika ofisi za wizara hiyo kwa kusimama getini kuzuia wafanya kazi wote wa wizara ambao walikuwa wamefika ofisini baada ya saa 1:30 asubuhi muda ambao ndiyo mwisho wa wafanyakazi kuingia ofisini. 

  Awali Dkt. Kingwangalla alifika ofisini saa 1:05 asubuhi huku akiingia ofisini kwa kutembea mwenyewe bila kutumia usafiri wa gari na kwenda moja kwa moja ofisini kwake ambapo alitoka ilipofika saa 1:32 na kwenda kusimama getini na kisha kuwaamrisha askari wa geti la kuingia katika wizara hiyo kulifunga geti hilo na wasiruhusu mtu yeyote kuingia ndani. “Fungeni geti na kila atakayefika msimruhusu kuingia ndani ninataka kuona wote ambao wanakuja wamechelewa,” alisikika Dkt. Kingwangalla akiwambia askari wa getini. 

   Baada ya kutoa amri hiyo alimtaka Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Michael John kumpa vitabu vya kusaini kwa vitengo vyote ili aweke mstari wa kuonyesha kuwa muda wa kuingia ofisini umekwisha na akafanya hivyo kwa kuweka mstari kwenye vitabu vya mahudhurio kuwa muda wa kusaini kuingia umeisha. 

  Baada ya kukamilisha zoezi hilo Naibu Waziri alizungumza na wanahabari kuwa ameamua kufanya zoezi hilo katika ofisi za wizara kwa kutaka kuona ni jinsi gani watumishi wa ofisi hiyo wamekuwa na mwitikio wa kufanya kazi kwa kasi anayoitaka rais, Dkt. John Pombe Magufuli. Alisema watumishi hao wameajiriwa na serikali ili kufanya kazi lakini wamekuwa wakichelewa kuingia ofisini na yeye kama Naibu Waziri ana wajibu wa kuwasimamia watumishi hao ili wafanye kazi ambayo serikali imewaagiza kufanya. 

  “Nina wiki moja tangu nimeingia hapa ofisini kuna mambo ambayo nimeyaona hayapo vizuri na sasa naanza na hili ili tujue kuwa ni kina nani huwa wanachelewa na zoezi hili litakuwa ni endelevu, kama mimi sitasimamia watumishi wa serikali basi sitakuwa na kazi wizarani tunataka watumishi ambao wanakuwa wanafanya kazi kwa kujitoa kwa ajili ya maslahi ya taifa,” alisema Dkt. Kingwangalla. 

   Aidha Naibu Waziri huyo alimtaka Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kuhakikisha watumishi wote waliochelewa kufika ofisini wanaandika barua ya kutoa maelezo kwanini wanachelewa kufika ofisini na baada ya hapo Mkurugenzi na yeye atoe maelezo kwanini muda wa kutoka watumishi wanakuwa hawasaini kuwa wametoka. 

   Pia alishauri uongozi wa wizara ufanye mabadiliko ya mfumo wa watumishi kuingia ofisini kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kadi au kidole “Biometric” ili kuwa na taarifa katika mifumo ya mawasiliano kujua wanaochelewa ofisini na wanaowahi kutoka na baada ya hapo uongozi utajadili adhabu za kuwapa watumishi wote ambao wamekuwa wakichelewa kufika na kuwahi kutoka ofisini.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam jana Alhamisi Desemba 17, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na kushoto kwake ni Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa. Kikao hicho ni cha kwanza kufanyika tangu Rais Magufuli atangaze Baraza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Tano wiki iliyopita. 
  PICHA NA IKULU

  0 0

  Efficia 1Royal Philips (NYSE: PHG AEX: PHIA) has announced the launch of its Efficia CM Series patient monitors in Tanzania – these cost effective products are designed to provide clinicians with access to high-quality of care, even in resource-limited facilities. These solutions highlight Philips’ commitment to enhance access and enable quality care across the health continuum – from healthy living and prevention, to diagnosis, treatment, recovery and home care, including in remote areas.

  “As we innovate to improve health care, monetary constraints should not be a reason for limiting access to the best care available for improving a patient’s health,” said Roelof Assies, General Manager, Philips East Africa. “The Efficia suite is designed to bring trusted and effective Philips technology and performance at an affordable price to the health care facilities where resource limitations have prevented this access before.”
  Making quality care affordable.
    Effective patient monitoring can help improve diagnosis and provide earlier intervention, which is not only critical for improving patient outcomes, but can also help hospitals improve operational efficiencies.

  The Efficia CM Series patient monitors provide the same core physiological measurements and algorithms that are present in other Philips patient monitors, but are designed to be more cost-effective and scalable to the needs of budget-constrained health care facilities.The series, including Efficia CM100, Efficia CM120 and Efficia CM150, are solidly built and reliable, able to handle heavy workloads and electrostatic interference, and can be customized for a variety of patient types, acuity levels and clinical settings, and include an intuitive user-interface to ease the burden on busy clinician workflow.

  The Efficia CM patient monitors can be connected to Efficia CMS200 central monitoring system, which provides centralized monitoring and real-time access to patient physiological data and displays waveforms, parameters and alarms for up to 32 patients.Efficia DFM100 – Providing therapeutic care where it is needed mostefficia 2
  To deliver quality care, clinicians need to make quick, informed decisions when responding to an emergency and caring for a patient across the entire course of treatment. The Efficia DFM100 defibrillator/monitor is designed to be easy to use for both basic and advanced life support care providers to meet the demands of patient care in pre-hospital and hospital environments effectively and consistently. The Efficia DFM100 provides functionalities needed to enhance patient care, regardless of where they are located. It is also scalable to ensure affordability across all care settings.


  “Clinicians are constantly under pressure to meet clinical demands on a tight budget,” said Dr. Juma A. Mfinanga, Head of Emergency Department at Muhimbili National Hospital. “The Efficia solutions work with the clinicians and the hospital; they are affordable and intuitive, allowing limited staff to focus on care first.”

  0 0

  Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya UTT AMIS, Daud Mbaga (katikati), akitoa mada kuhusu Uwekezaji wa Pamoja wakati wa mkutano wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu Tanzania uliyofanyika mjini Tanga. (Na Mpigapicha Wetu)
  Mwanachama mpya wa UTT AMIS akijaza fomu ya kuwa mwekezaji katika mfuko wa Uwekezaji wa pamoja wa umoja wa UTT AMIS.
  Washiriki wakisikiliza mada kuhusu faida za Uwekezaji wa Pamoja wakati wa mkutano wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu Tanzania ulioandaliwa na UTT-AMIS.
  Ofisa Masoko Mkufunzi wa UTT AMIS, Waziri Ramadhani,  akitoa Elimu ya Uwekezaji wa pamoja wakati wa mkutano wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu Tanzania.

  0 0

  Elias Maguli Mchezaji wa timu ya Stand United, amekabidhiwa hundi yake yenye thamani ya shilingi Milioni 1/= na wadhamni wakuu wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara(Vodacom Tanzania) kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi hiyo.

  Mchezaji huyo alikabidhiwa hundi hiyo wakati wa mazoezi yaliyokuwa yanafanywa na timu yake katika viwanja vya JKM Park ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga hapo kesho.
  Ofisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania,Ibrahim Kaude(kushoto)akimkabidhi Mchezaji wa Stand United, Elias Maguli(Katikati) mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 1/- kwa kuibuka mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara wa mwezi Oktoba,Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya JKM Park kwa kujiandaa na mchezo wao wa kesho na Yanga,Anayeshuhudia kulia ni Kocha msaidizi wa timu hiyo Athumani Bilal.
  Baadhi ya wachezaji wa timu ya Stand United wakiwa katika viwanja vya JKM Park jijini Dar es salaam wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja hivyo kwa kujiandaa na mchezo wao na Yanga wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara hapo kesho.

  0 0


  Ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Parity Twinomujuni (aliyeketi mbele ya logo ya NHC) ukijadiliana masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nyumba nchini na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa la Tanzania, Nehemia Kyando Mchechu. Ujumbe huo umekuwapo katika ziara ya siku mbili ya mafunzo nchini kujifunza namna utendaji wa Shirika la Tanzania unavyofanyika ili waweze kupata njia za kuweza kuboresha Shirika zaidi Shirika la NHCC Uganda.
  Mojawapo ya nyumba za NHC Mwongozo zilizotembelewa na Ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Parity Twinomujuni. Ujumbe huo umekuwapo katika ziara ya siku mbili ya mafunzo nchini kujifunza namna utendaji wa Shirika la Tanzania unavyofanyika ili waweze kupata njia za kuweza kuboresha Shirika zaidi Shirika la NHCC Uganda.
  Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumkba la Taifa la Tanzania (NHC), Issack Peter akitoa mada kuhusu utendaji wa Shirika hilo kwa Ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Parity Twinomujuni Ujumbe huo upo nchini katika ziara ya siku mbili ya mafunzo nchini kujifunza namna utendaji wa Shirika la Tanzania unavyofanyika ili waweze kupata njia za kuweza kuboresha Shirika zaidi Shirika la NHCC Uganda.


  0 0

  Ofisa wa Benki ya NBC kitengo cha ATM, Pendo Clement (kushoto) akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa ​ ​Chuo cha ufundi stadi cha Future World, Gongo la mboto Chuo cha Ufundi Stadi cha Future World, kuhusu masuala mbalimbali ya kimaisha ikiwa ni sehemu ya mradi mradi wa Kuendeleza Vijana Kiuchumi Dar es Salaam wa kuendeleza vijana kiuchumi Dar es Salaam unaodhaminiwa na benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo, Gongo la Mboto nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana.
  M ​eneja wa ATM na Kadi wa Benki ya NBC, Wambura John (kushoto), akiwafundisha wanafunzi waChuo cha ufundi stadi cha Future World, Gongo la mboto Chuo cha Ufundi Stadi cha Future World jinsi wanavyoweza kutumia mitandao katika kujitengenezea kipato ikiwa ni sehemu ya mradi mradi wa Kuendeleza Vijana Kiuchumi Dar es Salaam wa kuendeleza vijana kiuchumi Dar es Salaam unaodhaminiwa na benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo, Gongo la Mboto nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana.
  Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Future World, Robert Mkolla (katikati) akiwaonyesha maofisa wa NBC mandhari ya chuo hicho katika hafla hiyo. Kushoto ni Meneja Huduma za Jamii, Irene Peter na kulia ni Meneja Mahusiano wa benki hiyo, William Kallaghe.
  Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto) akizungumza na baadhi ya wanafunzi waChuo cha ufundi stadi cha Future World, Gongo la mboto Chuo cha Ufundi Stadi cha Future World walipotembelea chuoni hapo jana ikiwa ni sehemu ya mradi mradi wa Kuendeleza Vijana Kiuchumi Dar es Salaam wa kuendeleza vijana kiuchumi Dar es Salaam unaodhaminiwa na NBC.

  0 0


  0 0

  san2
  Sabina Leonce Komba ambaye ni mtumishi wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) akipozi kwa picha mara baada ya kutunukiwa Shahada yake ya pili (Masters) ya Uongozi wa Miradi aliyoipata Katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwenye mahafali ya 27 ya chuo hicho yaliyofanyika Desemba 16 mwaka huu katika viwanja vya Bungo Kibaha mkoani Pwani. san4
  Sabina Leonce Komba ambaye ni mtumishi wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF akipozi kwa picha na wenzake katika mahafali hayo.
  san5
  Sabina Leonce Komba ambaye ni mtumishi wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF pamoja na wenzake wakisubiri kuanza kwa ratiba ya mahafali hayo.

  0 0

   NEWS UPDATES.:Jumla ya watu. 12 wamepoteza Maisha na 22 wamejeruhiwa leo baada ya basi la New Force kupata ajali Eneo la Mahenge Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa barabara kuu ya Iringa- Dar es salaam..
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,Peter Kakamba amethibitisha watu 12 kupoteza maisha katika ajali hiyo. Wanane ni wanae na wanne ni wanawake. Abiria 28 wamejeruhiwa wakiwemo madereva wa basi la lori na hali zao siyo nzuri.

  Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane alasiri ambapo basi la kampuni ya Newforce aina ya Youtong lenye namba za usajili T483CTF likitoka Tunduma kwenda Dar limegongana na lori aina ya Scania lenye namba T616DEF katika kijiji cha Mahenge,wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa katika barabara kuu ya Dar - Mbeya.

  Majeruhi wamelazwa hospitali ya wilaya ya Ilula.kilomita 45 kutoka Iringa mjini.
   
  =======  ========   ========
   
  WATU kadhaa wanadaiwa kupoteza maisha huku wengine wengi wakijeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria mali ya Kampuni ya NEW FORCE ONE lenye namba za usajili T483 CTF kupinduka mapema mchana wa leo katika eneo la Mahenge Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa barabara kuu ya Iringa- Morogoro, jitihada za kusafirisha majeruhi zinaendelea. 

  Chanzo cha ajali hiyo, inaelezwa kuwa ni Lori la mizigo lililokuwa likitokea upande wa Morogoro, kupasuka tairi ya mbele na kupoteza muelekeo uliopelekea kuligonga basi hilo na kupinduka. Globu ya Jamii inafanya jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa kwa taarifa zaidi. tutaendelea kuwaletea taarifa kadri tutakavyozipata. 
  Sehemu ya Basi hiyo baada ya kupata ajali.  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 18, 2015. Kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum.

  0 0


  uj1

  Mkurugenzi wa barabara Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Ven Ndiyakumana kushoto akisaini mkataba wa awali kuhusu mkopo wa fedha wa riba nafuu utakaosaidia ujenzi wa Barabara ya Arusha hadi Holili kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano Afrika kutoka Japan (JICA) Bw. Hideyuki Manioka wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.
  uj2
  Mkurugenzi wa barabara Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Ven Ndiyakumana kushoto akikabidhiana mkataba wa awali kuhusu mkopo wa fedha wa riba nafuu utakaosaidia ujenzi wa Barabara ya Arusha hadi Holili na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano Afrika kutoka Japan (JICA) Bw. Hideyuki Manioka wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.PICHA ZOTE NA ALLY DAUD-MAELEZO
  …………………………………………..
  Na Raymond Mushumbusi Maelezo
  Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano leo imesaini mkataba wa makubaliano ya awali ya ujenzi wa barabara kutoka Arusha mpaka Holili.
   
  Makubaliano hayo yamesainiwa na Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Ven Ndyamukama kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Naibu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano (JICA) Bw Hideyuki Manioka  kwa niaba ya Serikali ya Japan.
   
  Mhandisi Ven Ndyamukama amesema kuwa Tanzania imesaini mkataba huu wa awali ambao baada ya majadiliano ya awali kati ya Tanzania na Japan, serikali ya Japan itatoa mkopo wa riba nafuu kwa serikali ya Tanzania ili kuwezesha kuanza kwa utekelezaji wa mradi huu mapema marchi mwakani.
   
  “Wamekuja kufanya utafiti na kufatilia taarifa tulizo nazo kuhusu mradi huu na kupeleka taarifa serikali ya Japan na tunategemea June mwakani kusaini hati ya kupata mkopo ambao utawezesha ujenzi wa barabara hii ” Alisema Mhandisi Ndyamukama.Pia ameongeza kuwa baada ya mkopo huo kutolewa wao kwa upande wao wamejipanga katika kufanya mradi huo ukamilike kwa wakati ikiwemo upatikanaji wa wakandarasi kwa ajili ya mradi huo.
  Aidha Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano (JICA) Bw Hideyuki Manioka  amesema kuwa wataendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo.
   

  Mradi huu wa barabara toka Arusha mpaka Holili  yenye urefu wa kilometa105 umefadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia Wakala wa mambo ya Ujenzi(JICA) na unatarajiwa kuanza mapema mwakani,hii ikiwa ni juhudi za Serikali katika kuboresha miundombinu hasa ya barabara kwa kuzifanya barabara nyingi nchini kuwa katika kiwango cha lami.

  0 0

  Ni majira ya saa 10 na dakika 10 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo  alipofika katika mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam kinachomilikiwa na Tanesco bila ya kutoa taarifa na kukuta wafanyakazi pamoja na wahandisi wa kituo hicho cha umeme wakiendelea na kazi katika mitambo hiyo. 

  Prof. Muhongo alipokagua mitambo hiyo leo alibaini kuwa umeme uniti moja inatengenezwa kwa gharama ya shilingi 90 na kuuzwa kwa wananchi kwa shilingi 180 ikiwa ni kiwango kikubwa kwa mwananchi wa kawaida.

  Pia Mhongo amesisitiza kuwa umeme unatakiwa kushuka bei ili kila mwananchi anufaike na umeme hapa nchini.

  Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipokea vifaa vya kuzuia kusikia sauti kuingia masikioni mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Mitambo ya Gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akizungumza na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam, Mohamed Kisiwa mara baada waziri wa Nishati na Madini kutembelea mitambo ya umeme wa gesi wa Tegeta jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipewa maelekezo na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta, Mohamed Kisiwa mara baada ya waziri huyo kutembelea mtambo huo bila kutoa taarifa na kuhoji baadhi ya matengenezo katika mtambo huo.
  Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akitembezwa na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta Mohamed Kisiwa mara baada ya kutembelea mitambo ya Tegeta jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya Mitambo ya Gesi iliyotembelewa na Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0


  Lorraine Marriot (pichani) akiwa katika vazi la ubunifu la Taifa .Vazi hili limebuniwa na Adam Hassana Kijangwa kutoka Zanzibar na imeitwa ‘Angel of Ivory’ maana inaonyesha Malaika wa Tanzania anayelinda Tembo wanaouwawa kwa ujangili kwa ajili ya biashara haramu ya pembe za ndovu.

  Huyu malaika wa Tanzania yupo kwa ajili ya kuwalinda Tembo na rasilimali zetu na kuwaadhibisha majangili. Nguo yake imeshonwa kwa ubunifu na umahiri mkubwa na hekaheka limebuniwa na Mwanakombo Salim. Pia kabeba fimbo la kimasai iliyonakshiwa na rangi za taifa.

  Rangi nyekundu ni alama ya damu ya tembo iliyomwagika na kusafishwa na malaika huyu.

  0 0  0 0

   Aliyewahi kuwa nahodha wa Yanga na Timu ya Taifa (Taifa Stars) Ally Mayay Tembele alikuwa ni miongoni mwa wahitimu zaidi ya 800 waliotunukiwa shahada za uzamili katika fani mbalimbali kutoka katika Chuo kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es salaam .
  Katika sherehe hizo za  mahafali ya 14 ya Chuo kikuu cha Mzumbe Kampasi ya  DSM  zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa J.K.Nyerere jijini Dar es salaam, Tembele alitunukiwa Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Masoko(Msc Marketing management).
  Aidha, akiongea na Michuzi blog, Mayay alitoa wito kwa wanamichezo na wasanii kujiendeleza kielimu katika fani mbalimbali ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo zile zilizomo ndani ya fani zao
  Mayay ambeye ni Afisa  Biashara katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji  ni mchambuzi wa soka katika vituo vya redio na televisheni na pia ni kocha mwenye leseni daraja C kutoka Shitikisho la soka baranai Afrika (CAF).
   Ally Mayay akiwa na mwanae Yumnah baada ya kulamba nondozzzz zake
  Ally Mayay na  msanii wa muziki wa kizazi kipya Gwamaka Kaihula (King crazy GK) ambao wote wamelamba nondozzz ya  shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Mzumbe

  0 0


  0 0

  Prof. Idris Ahmada Rai, the Vice Chancellor of the State University of Zanzibar (SUZA) has been awarded the Africa Education Award at the World Sustainability Congress held in Mauritius on 8-9 December, 2015. 

  Endorsed by World Corporate Social Responsibility (CSR) Day and other organizations, a  number  of  awards has been  given to  various leaders in Africa  whose leadership  in various organizations and in varying disciplines  has demonstrated  significant impact to the community.  

  During the awarding ceremony, Prof. Rai joined around 20 other leaders from various sectors in Africa including three Ministers from Malawi, Sierra Leone and Kenya.

  Since he joined the State University of Zanzibar  as the third Vice Chancellor in 2011, Prof. Rai  has  strategically led  university reforms  from a small university  made of only one school with just over 1,000  students and only six programs   to a university that comprises of five  schools with a total of  about 3,500 students pursuing 36 programs from a diverse range of disciplines at all levels, namely  from certificates to PhD thus making  SUZA an important actor in the country’s  human capital development.  

  Additional areas of significant institutional improvement during his leadership include SUZA’s recognition internationally, active staff capacity building, and increased mobilized revenues by more than 5 folds. In short, SUZA has been well positioned regionally and internationally despite the fact that the journey towards achieving its vision and accomplishing its mission is still long. The task ahead is still daunting.


  0 0

   Mganga Mfawidhi Zahanati ya Kimara, Dk. Alphoncina Mbinda (kushoto) akipokea baadhi ya mashine za kupimia mapigo ya moyo kwa mgonjwa kutoka kwa Meneja Uratibu wa NMB Plc, Thomas Kilongo. Miongoni mwa mashine zilizotolewa ni pamoja na mashine ya kupimia joto la mgonjwa, mashine 10 za kupimia 'BP' kwa mgonjwa, mashine 10 za kupimia mapigo ya moyo, mzani wa kupimia uzito na urefu kwa wagonjwa, vifaa vya kukusanyia taka, spika na kipaza sauti chake pamoja na mashine nyingine za kisasa kwa ajili ya vipimo anuai kwa wagonjwa. 
   Mganga Mfawidhi Zahanati ya Kimara, Dk. Alphoncina Mbinda (kushoto) akipokea baadhi ya mashine za kupimia mapigo ya moyo kwa mgonjwa kutoka kwa Meneja Uratibu wa NMB Plc, Thomas Kilongo. Miongoni mwa mashine zilizotolewa ni pamoja na mashine ya kupimia joto la mgonjwa, mashine 10 za kupimia 'BP' kwa mgonjwa, mashine 10 za kupimia mapigo ya moyo, mzani wa kupimia uzito na urefu kwa wagonjwa, vifaa vya kukusanyia taka, spika na kipaza sauti chake pamoja na mashine nyingine za kisasa kwa ajili ya vipimo anuai kwa wagonjwa. 

  Mganga Mfawidhi Zahanati ya Kimara, Dk. Alphoncina Mbinda (kushoto) akitoa neno la shukrani kwa Benki ya NMB Plc mara baada ya kukabidhiwa mashine mbalimbali pamoja na vifaa vya kutibia wagonjwa katika Zahanati hiyo.


  0 0


older | 1 | .... | 1060 | 1061 | (Page 1062) | 1063 | 1064 | .... | 3348 | newer