Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live

BANKI YA BARCLAYS WAZINDUA OFISI MPYA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0

Mwenyekiti wa bodi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Ramadhani Dau akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ofisi mpya kwenye ghorofa ya pili ya jengo la benki hiyo lililopo jengo la Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akiwa na baadhi ya wadau wa benki hiyo wakati wa kuzindua ofisi ya benki hiyo ghorofa ya pili ya benki hiyo.

Mwenyekiti wa bodi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Ramadhani Dau  akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi wa ofisi ya benki hiyo  katika jengo la benki ya Barclays ghorofa ya pili leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akishuhudia wakati akifungua kitambaa hicho.
Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akizungumza na wafanyakazi wa benki ya Barclays hapa nchini (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.

AMUUA MKE WAKE KISHA YEYE KUJINYONGA MBOZI MBEYA

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.

Na Mwandishi wetu,Mbeya,Jamiimojablog

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanaume mmoja Mkazi wa kijiji cha Malolo Ndugu Chipunguli Mkisi (30) amemuua mke wake kwa kumkata panga kichwani kisha yeye mwenyewe kujiua kwa kujinyonga.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Ahmed Msangi amesema tukio hilo la aina yake limetokea Desemba 15 mwaka huu majira ya saa 7 mchana huko katika kijiji cha Malolo, Kata ya Msia, wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya.

Msangi amemtaja mwanamke huyo kuwa ni Neva Mwaweza (24) Mkazi wa Malolo ambaye ameuwawa na mumewe kwa kukatwa panga kichwani .

Kamanda Msangi amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi baada ya mwanaume kumtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

inadaiwa kuwa baada ya tukio, mtuhumiwa alijinyonga kwa kutumia kamba kwenye mti umbali wa mita 100 kutoka nyumbani kwake.

Aidha mwili wa marehemu [mwanaume] ulikutwa ukiwa na majeraha kwenye vidole na kando kukiwa na panga na alikutwa na ujumbe uliokuwa na maneno “kuwa ameamua kumuua mke wake na yeye kujinyonga kutokana na mke wake kuwa na mahusiana ya kimapenzi na mwanaume mwingine aitwae kilasi nzowa”

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya vwawa. ambapo kwa mujibu Kamanda Msangi uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

MAPAMBANO YA FISTULA YANAENDELEA KWA USHIRIKIANO WA HOSPITALI YA CCBRT NA VODACOM FOUNDATION

$
0
0
Mkurugenzi wa walemavu katika Hospitali ya CCBRT,Brenda Msangi(kulia)akielezea ubora wa simu aina ya ZTE kwa waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa simu 150 zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 6/=zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation kwa ajili ya kurahisisha huduma za mawasiliano kwa mabalozi wa kampeni ya kutokomeza Fistula nchini.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza,Grace Lyon na Chandra Almony.
Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza(kushoto)akimkabidhi moja ya boksi lenye simu 150 aina ya ZTE zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 6/=Mkurugenzi wa walemavu katika Hospitali ya CCBRT,Brenda Msangi(kulia)ikiwa ni msaada uliotolewa na mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation” kwa ajili ya kurahisisha huduma za mawasiliano kwa mabalozi wa kampeni ya kutokomeza Fistula nchini.Wengine katika picha ni wafanyakazi wa Hospitali ya CCBRT na Vodacom Tanzania.

Wizara ya Afya yatangaza Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Donan Mmbando akieleza kuhusu Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya Waandishi wa Habari leo 17 Desemba, 2015.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Donan Mmbando akionyesha aina ya dawa zinazotakiwa kugawiwa kwa umma wakati alipotangaza Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya Waandishi wa Habari leo 17 Desemba, 2015.

Na Shamimu Nyaki.

Serikali kupitia Mpango wa wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yasiyopewa kipaumbele leo imetangaza tarehe 19 hadi 23 mwezi huu kuwa itaanza zoezi la kugawa dawa kwa makundi yanayopaswa kupata dawa za magojwa hayo.

Tamko hilo limetolewa na Katibu mkuu wa Wizara Ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wazee,na Watoto Bw. Donald Mmbando alipokuwa anazungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kusema kuwa Magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele ni Usubi,Vikope (Trakoma), Matende, Mabusha,Ngiri maji, na Minyoo ya tumbo hivyo dawa hizo zitasaidia kupunguza tatizo.

Ameongeza kuwa zoezi hilo la ugawaji wa dawa litatekelezwa katika vituo vyote vya Afya, Zahanati,Hospitali, shule za msingi na sekondari,sokoni,vituo vya usafiri,pamoja na Ofisi za Serikali na Mashirika ya Umma na hivyo wananchi wanaombwa kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo ambayo haina malipo yoyote.

Katibu Mkuu huyo amesema kuwa wahusika wakuu katika kupatiwa dawa hizo ni Watu wote kuanzia miaka mitano na kuendelea,isipokuwa watoto chini ya miaka mitano,wajawazito, mama anaenyonyesha mtoto chini ya siku saba na Wagonjwa Mahututi.

“Tunataka kulinda afya zao na Uhai wao hivyo tunaomba wafuate maelekezo vizuri”.Alisema Bw Mmbando.

Aidha zoezi hilo litatekelezwa katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Singida, Dodoma,Mtwara, Lindi na Pwani kwa ajili ya kujikinga na kutibu magonjwa hayo na Mikoa mingine iliyobaki itafanya zoezi hilo katika ngazi ya jamii na shuleni mwishoni mwa mwezi Januari kuendelea hadi Februari 2016.

Naye Mratibu wa Mpango huo Dkt Edward kirumbi ameeleza kuwa takwimu zainaonyesha kuwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele hapa nchini ni kubwa ambapo ugonjwa wa Usubi umeenea zaidi katika mikoa sita ikiongozwa na Dodoma, Ugonjwa wa Minyoo ya tumbo wagonjwa million 13, kichocho ,Matende na Mabusha tathmini za awali zinaonyesha mikoa 18 imeathirika kwa kuwa na wagonjwa million 12.

Vile vile Dkt Kirumbi ameeleza kuwa Magonjwa haya yamekuwa na athari kubwa hasa kwa kuathiri nguvu kazi ya Taifa hivyo wananchi wanapaswa kupata dawa hizo ambazo zitakuwa zinatelewa kwa mwaka mara moja ili kukinga upungufu wa Damu, kuuwa vimelea vya ugonjwa huo, kupungua kwa magonjwa ya ngozi, na kuongeza virutubisho bora mwilini.

Hata hivyo jamii inapaswa kupewa elimu zaidi kuhusu Magonjwa haya kwa vile bado haijaelewa athari za magonjwa haya kwa kiasi kikubwa hasa kwa maeneo ya vijijini ambayo ndio waathirika wakubwa.

WACHEZAJI WAPYA WENYE ITC RUKSA KUTUMIKA

$
0
0
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya marekebisho ya kanuni za usajili ambapo sasa mchezaji ambaye usajili wake utakuwa umepita kwenye mfumo wa mtandao wa Transfer Matching System (TMS) atapewa leseni na kuitumikia moja kwa moja timu yake mpya.

TFF itatoa leseni ya usajili wa mchezaji ambaye amethibitishwa kupitia mtandao wa TMS baada ya kuwepo nyaraka zote; mkataba uliomalizika, barua ya kuvunja mkataba, barua ya kuachwa (release letter), mkataba mpya na uthibitisho wa makubaliano kati ya klabu zinazohusika.

Licha ya mchezaji kupata leseni, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji bado itakuwa na mamlaka ya kushughulia upungufu, malalamiko ya kiusajili, pingamizi na uhalali wa kimkataba kati ya pande mbili (mchezaji na klabu).

Wachezaji wote wa kigeni waliosajiliwa kwa ajili ya kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) wanapaswa kulipiwa dola za kimarekani U$ 2,000 kwa kila mmoja kabla ya kupatiwa leseni na kuanza kuzitumikia klabu zao katika michuano ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho.

Pia TFF kupitia kamati ya sheria na hadhi za wachezaji inaweza kumruhusu kwa kipindi maalum mchezaji mwenye dosari acheze kwa leseni ya muda (provisional license) hadi dosari hizo kati ya klabu na klabu zitakapomalizwa. Iwapo dosari hizo hazitakuwa zimemalizwa, mchezaji anaweza kuzuiwa kucheza na klabu husika kuadhibiwa.

Timu zote za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili zinatakiwa kufuatilia TFF kujua wachezaji ambao hawana pingamizi na leseni za wachezaji waliopitishwa wanaweza kuanza kutumika kuanzia kesho tarehe 18/12/2015 na kwenye michezo ya kombe la Shirikisho (FA Cup) kama hawakuwa wamecheza raundi ya kwanza kwenye vilabu vya zamani.

MREFA YAANDAA KOZI YA LESENI C

$
0
0
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa kushirikiana na Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya (MREFA) wameandaa kozi ya makocha wa mpira wa miguu Leseni C, itakayofanyika jijini Mbeya kuanzia Disemba 21- 04 Januari, 2016.


Jumla ya makocha 46 kutoka katika kanda ya Nyanda za Juu Kusini wanatazamiwa kushiriki kozi hiyo ya wiki mbili, ambayo itaendeshwa na wakufunzi Kidao Wilfred na Salum Madadi.

Washiriki wa kozi hiyo ni Mussa Kasalika, Steven Viera, Golya, Mlekwa, Matokeo Sigalla, Ernest Nkandi, Felix A. Sosteness, Michael Mwamaja, Daniel Mwaisabila, Deus Nsheka, Albert Gama, Joseph Abiero, Simon Mwapili, Bahati Mwaipopo, Willy Ngailo, Charles Makwaza, Paul Msyahila, Osward Morris, Jacob Ndago, Castor Mahona, Ambilikile Albion, Jumanne Nsunye, Gowdin Mulenga.

Wengine ni Abel Shizya, Matatizo Abdallah, Michael Kasekenya, Thomas Kasombwe, James Wanyato, Rose Njobelo, Amos Chiwaya, Baraka Kibanga, Mohamed Dondo, Josephat Digna, Shabani Mwaibara, Lucas Kibaja, Yusuph Mlekwa, Joel Makitta, Josiah Steven, Rashid Kasiga, Charles Njango, Alex Lusekelo, Shabani Kazumba, Ismail Suleiman, Ibrahim Kasegese, Simon Bernard, Anthony Mwamlima, Christian Simkoko.

WATANZANIA WANNE WAPATA TUZO ZA UANDISHI WA FASIHI YA KISWAHILI AFRIKA

$
0
0

Afisa Masoko wa Alaf, Theresia Mmasy akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani)jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwandishi wa kitabu cha Kolonia Santita, Enock Maregesi na Mwandishi wa Ushairi la Kifaurongo, Christopher Budebah.
Mkuu wa Idara ya Fasihi ya Mawasiliano na Uchapishaji (TATAKI) WA wa chuo kikuu cha Dar es Salaam akiwa na baadhi ya viongozi ya ALAF Limited. 
Mshiriki wa Taaluma ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Adrian Mtembei  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

KWA mara ya kwanza Lugha ya Kiswahili imeingia katika rekodi ya dunia kwa watanzania wanne kuchomoza katika tuzo ya waandishi ya Fasihi Afrika. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mshiriki wa Taaluma ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Adrian Mtembei amesema lugha ya Kiswahili ya kujivunia kutokana na watanzania wenye lugha yao kuwa washindi.

Washindi wa tuzo hizo ni Enock Maregesi ambaye aliandika Kolonia Santita,Chiristophee Bubebah, Anna Manyaza aliandika Penzi la Damu, Mohamed Ghassani aliandika N’na Kwetu.

Walioshiriki katika tuzo hiyo walikuwa 65 na kuweza kuibuka watu wanne ambao ni washindi wakitokea nchini na sherehe hizo zilifanyika Nchini Kenya.

Amesema kwa lugha ya kifaransa na Kiingereza zimekuwa zikijitokeza kila mwaka kwa watu kuandika riwaya na mashairi lakini Kiswahili imekuwa ikisahaulika hivyo na kufanya Chuo Cornell Nchini Marekani iliamua kufanya hivyo kuwa watu kuandika Riwaya na Mashairi.

Katika tuzo hizo Kampuni ya watengenezaji wa Mabati ya Alaf ilizamini tuzo hizo na kutaka watu wajitokeze katika kuinua lugha ya Kiswahili duniani.

Afisa Masoko wa Alaf, Theresia Mmasy amesema kazi wataendelea kushirikiana na watanzania katika kukuza Kiswahili katika kudhamini tuzo hizo.

JAJI MARK BOMANI AMSHAURI MAALIM SEIF AKUBALI UCHAGUZI URUDIWE

$
0
0
Jaji  Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Boman akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

JAJI Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Boman amesema kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja Zanzibar, Maalim Seif Hamad akubali uchaguzi urudiwe Zanzibar kwani kama alishinda atashinda tena kutokana na waliompigia katika uchaguzi ulifutwa watampIgia kura tena.

Boman ameyasema hayo leo jijini Dar eS Salaam , wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa Maalim kujitangazia kuwa ameshinda ni suala ambalo halikufuata utaratibu hivyo kutokana na mazingira hayo uchaguzi ufanyike ili kupata Rais wa Serikali ya Zanzibar.



“Kurudia uchaguzi Zanzibar ni jambo lisilo epukika lakini wakae na kuangalia dosari zilizojitokeza na kufuta uchaguzi lazima lishughukiwe kisheria bila kufanya hivyo kunaweza kuleta matatizo”amesema Jaji Mstaafu, Boman.


Amesema kuwa uchaguzi uliofanyika Zanzibar walitakiwa kukaa na kuona wapi walikosea katika kuondoa changamoto hizo ambapo ilikuwa ngumu kutokana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha na wajumbe walishindwa kuafikiana.


Hata hivyo Boman ametaka suala la katiba lazima lishughulikiwe kuacha kwake ni aibu ya nchi kutokana na mabilioni ya fedha yametumika katika mchakato huo.


Amesema kuwa migogoro inayotokea ya ardhi na wafugaji pamoja wakulima inatokana na kutokuwa na katiba ambayo ndio ingekuwa suluhu ya utatuzi wa migogoro hiyo.

KAMATI YA URATIBU YA SHIRIKISHO LA VYUO ELIMU YA JUU YAANZA VIKAO VYA SIKU MBILI

$
0
0

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Zainab Abdallah (MNEC) akiongoza kikao cha Kamati ya Uratibu Taifa ya la Vyuo vya Elimu ya juu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Zainab Abdallah (MNEC) akiongoza kikao cha Kamati ya Uratibu Taifa ya la Vyuo vya Elimu ya juu, kulia ni Katibu Mtendaji Ally S. Hapi

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Zainab Abdallah (MNEC) akijadiliana jambo pamoja na Daniel Zenda (katikati) na Ally S. Hapi wakati wa kikao cha Kamati ya Uratibu Taifa ya la Vyuo vya Elimu ya juu.
Wajumbe wa kikao wakichambua mambo mbali mbali.

Kamati ya Uratibu taifa ya Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu leo imeanza kikao cha siku mbili kinachofanyika makao makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es salaamchini ya Mwenyekiti wake bi Zainab Abdallah(Mnec). Viongozi wengine wanaohudhuria kikao hicho ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho Ndg. Hamid Mhina (Mnec), Katibu Mtendaji Ally S. Hapi, Katibu mtendaji Daniel Zenda, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa kutoka Shirikisho Joseph Chitinka,Katibu uchumi na Fedha Richard Luhende, katibu wa siasa na uenezi Fikiri Mzome na katibu wa uhamasishaji Mganwa Nzota.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

WAZIRI MHONGO ATOA MWEZI MMOJA KWA TANESCO.

BOMOA BOMOA YAWAFIKIA WANANCHI WANAOISHI PEMBEZONI MWA BONDE LA MTO MSIMBAZI JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Manispaa za jiji la Dar es salaam zitafanya zoezi la kuondoa wavamizi maeneo yote ya Mabondeni, kingo za mito  na za Bahari, maeneo ya wazi, maeneo ya miundombinu na maeneo yote hatarishi zaidi ya 150 katika  jiji la Dar es salaam. Bomoa bomoa ya leo inaendelea katika Bonde la mto msimbazi.Mkuu wa Kitengo cha Sheria Balaza la Taifa la usimamizi wa mazingira Tanzania (NEMC), Manchale Heche akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juu ya zoezi la Bomoabomoa maeneo ya miundombinu na maeneo yote hatarishi nakuwataka wananchi waliojenga katika fukwe za bahari Kingo za mito na mikondo ya bahari kuhamisha mali zao mapema.
Ubomoaji ukiendelea maeneo ya Mto msimbazi jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.

DIRA YA DUNIA ALHAMIS 17.12.2015

Raia wanne wa China wahukumiwa kutumikia miaka 20 jela kila mmoja kwa Uhujumu uchumi mkoani Mbeya

$
0
0

 Washatkiwa  wanne wa China wakipanda karandinga baada ya kuhukumiwa kutumikia jela miaka 20 kila mmoja na kutakiwa kulipa faini ya Zaidi ya shilingi bilioni 10 baada ya kukutwa na makosa matatu ya kuhujumu uchumi.
 Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Msangi akiwa na maafisa wake pamoj na Pembe za Faru walizokamatwa nazo  rai wanne wa China katika mpaka wa Kasumulu wilayani  Kyela mkoani Mbeya.
Raia wanne wa China ambao wamehukumiwa kutumikia jela miaka 20 kila mmoja na kutakiwa kulipa faini ya Zaidi ya shilingi bilioni 10 baada ya kukutwa na makosa matatu ya kuhujumu uchumi mkoani Mbeya.


Na Deo Kakuru wa Globu ya Jamii, Mbeya
Raia wanne wa China wamehukumiwa kutumikia jela miaka 20 kila mmoja na kutakiwa kulipa faini ya Zaidi ya shilingi bilioni 10 baada ya kukutwa na makosa matatu ya kuhujumu uchumi wakati walipokuwa wakisafirisha pembe 11 za Faru katika mpaka wa Kasumulo mkoani Mbeya. Washtakiwa hao ni SONG LEO (33), XIAO SHAODAN (29), CHEN JIANLIN (34) NA HU LIAN (30) ambao walikamatwa Novemba sita huko Kasumulo mpakani mwa Malawi na Tanzania wakijaribu kuingiza pembe hizo kutokea Malawi bila kibali. 
 Washtakiwa hao wanakabiliwa na makossa matatu ambayo ni kuongoza na kushiriki makosa ya uhujumu uchumi kinyume na sheria ya wanyamapori ya mwaka 2002.
 Kosa la pili ni kupatikana na nyara za serikali kinyume cha sheria ya uhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 na kosa la tatu ni kumiliki nyara za serikali kinyume cha seheria hiyo Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Mbeya Michael Mteite ambaye ameeleza kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa jamhuri hivyo na kuona washtakiwa wanayo kesi ya kujibu. 
 Hata hivyo Hakimu Mteite ametupilia mbali ombi la upande wa utetezi uliotaka washtakiwa kupunguziwa adhabu na kwamba hukumu hiyo itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo. 
 Hii ni kesi ya kwanza kwa hakimu Mteite ambayo amejivunia kuiendesha ndani ya kipindi kifupi cha siku 23 tangu washtakiwa hao walipofikishwa mahakamani hapo Novemba 24 mwaka huu. 
 Kesi hiyo ambayo imesikilizw kwa Zaidi ya masaa matano imevuta hisia za wakazi wa mkoa wa Mbeya ambao walikuwa wakiifuatilia kwa karibu na kutaka kujua nini hatima yake. 
 Washtakiwa hao kwa pamoja wamepandishwa kwenye karandinga la polisi tayari kuanza kutumikia adhabu yao gerezani licha ya Hakimu Mteite kueleza kuwa milango ya kukata rufaa iko wazi endapo wataona hawakuridhishwa na hukumu hiyo.

25 kuibuka washindi katika droo ya tatu ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" ya GAPCO

$
0
0
Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa kampuni ya GAPCO Tanzania, Jane Mwita (kati) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" inayoendeshwa na Kampuni hiyo kwa Wateja wake wa jijini Dar es Salaam,ambapo zaidi ya wateja 20 huibuka kidedea kila wiki. Kulia anaeshuhudia ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha nchini, Chiku Saleh na Kushoto ni Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi.

BOMOA BOMOA ENEO LA BONDE LA MKWAJUNI JIJINI DAR ES SALAAM


HOUSTON TEXAS KUWAKA MOTO WA SIFA WAKATI WA SHEREHE ZA KRISMASI.

$
0
0
Kanisa la Agape (Agape Family Church) Houston Texas likiongozwa na Mtumishi Elisha limeandaa maadhimisho ya kipekee ya Krismasi yatakayofanyika Houston Texas kwa siku mbili yaani 24 na 25 Desemba 2015. Habari zaidi soma kipeperushi hapa chini. Inline image 1

Huduma ya kugawa Dawa za Matende na Mabusha kuanza Disemba 19 Dar

$
0
0
Na Shamimu Nyaki - Maelezo

Serikali  kupitia Mpango wa  wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yasiyopewa kipaumbele leo   imetangaza tarehe 19 hadi 23 mwezi huu kuwa itaanza zoezi la kugawa dawa kwa makundi yanayopaswa kupata dawa za magojwa hayo. 

 Tamko  hilo  limetolewa  na Katibu mkuu wa Wizara Ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wazee,na Watoto  Bw. Donald  Mmbando   alipokuwa anazungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kusema kuwa Magonjwa  ambayo hayapewi kipaumbele  ni Usubi,Vikope (Trakoma), Matende, Mabusha,Ngiri maji, na Minyoo ya tumbo  hivyo dawa hizo zitasaidia kupunguza tatizo.

Ameongeza kuwa zoezi hilo la ugawaji wa dawa litatekelezwa katika vituo vyote vya Afya, Zahanati,Hospitali, shule za msingi na sekondari,sokoni,vituo vya usafiri,pamoja na Ofisi za Serikali na Mashirika ya Umma na hivyo wananchi wanaombwa kujitokeza kwa wingi  kupata huduma hiyo ambayo haina malipo yoyote.

Katibu Mkuu huyo  amesema  kuwa wahusika wakuu katika kupatiwa dawa hizo ni Watu wote kuanzia miaka mitano na kuendelea,isipokuwa watoto chini ya miaka mitano,wajawazito, mama    anaenyonyesha mtoto chini ya siku saba na Wagonjwa Mahututi.

“Tunataka kulinda afya zao na Uhai wao hivyo tunaomba wafuate maelekezo vizuri”.Alisema Bw Mmbando.

Aidha zoezi hilo litatekelezwa  katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Singida, Dodoma,Mtwara, Lindi na Pwani kwa ajili ya kujikinga  na kutibu  magonjwa hayo na Mikoa mingine iliyobaki  itafanya zoezi hilo  katika  ngazi ya  jamii na shuleni mwishoni mwa mwezi Januari kuendelea hadi Februari 2016.

Naye Mratibu wa Mpango  huo Dkt  Edward kirumbi ameeleza kuwa takwimu zainaonyesha kuwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele hapa nchini ni kubwa ambapo ugonjwa wa Usubi umeenea zaidi katika mikoa sita ikiongozwa na Dodoma, Ugonjwa wa Minyoo ya tumbo wagonjwa million 13, kichocho ,Matende na Mabusha tathmini za awali zinaonyesha mikoa 18  imeathirika kwa kuwa na wagonjwa million 12.

 Vile vile Dkt  Kirumbi ameeleza kuwa Magonjwa haya yamekuwa na athari kubwa hasa kwa kuathiri nguvu kazi ya Taifa hivyo wananchi wanapaswa kupata dawa hizo ambazo zitakuwa zinatelewa kwa mwaka mara moja  ili kukinga upungufu wa Damu, kuuwa vimelea vya ugonjwa huo, kupungua kwa magonjwa ya ngozi, na kuongeza virutubisho bora mwilini.

Hata hivyo jamii inapaswa kupewa elimu zaidi kuhusu Magonjwa haya kwa vile bado haijaelewa athari za magonjwa haya kwa  kiasi kikubwa hasa kwa maeneo ya vijijini ambayo ndio waathirika wakubwa.

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kabla ya kufungua mkutano wa siku moja wa baraza hilo unaofanyika katika Ukumbi wa Jeshi la Magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Mngodo, kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Obeid Mbaga. Wapili kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka, anayefuata ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Jenita Ndone. Katika kikao hicho Abdulwakil aliwataka watumishi wa wizara yake wafanye kazi kwa uadilifu na weledi ili kuleta mafanikio ndani ya wizara hiyo muhimu katika maendeleo ya nchi.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Mngodo (wapili kushoto), Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara hiyo, Obeid Mbaga. Wapili kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka, anayefuata ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Jenita Ndone wakiwaongoza wajumbe wa Baraza hilo kuimba wimbo wa mshikamano daima kabla ya Katibu Mkuu kufungua kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Obeid Mbaga akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kulia) kuja kuzungumza na wajumbe wa kikao hicho (hawapo pichani) kabla ya kufungua rasmi kikao hicho. Kushoto meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Mngodo. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.

MAKALA YA SHERIA: JE KULEWA, KUTOKUWA NA AKILI TIMAMU NI KINGA BAADA YA KUTENDA JINAI

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.

Wote  tunajua  kuwa  kila  atendaye  kosa  sharti  aadhibiwe.  Na  kuadhibiwa huko  lazima  kuwe  kwa  mujibu  wa  sheria.  Pamoja  na  kuwa  mtenda  kosa  hustahili  adhabu  bado  watenda  kosa  hutofautiana hadhi. Hadhi  hapa  sio  kuwa  fulani ni  mkuu  wa  mkoa  au  mkurugenzi  na  fulani  ni  mkulima  wa  kawaida kijijini  Katanakya.  

Hadhi  ndio  kama  hizo  zilizotajwa katika  kichwa  cha  makala.  Wapo  watenda  makosa   lakini  wakiwa na  umri  mdogo,  wapo  watenda  makosa  lakini  wakiwa  hawana  akili  timamu  halikadhalika  wapo  watenda  makosa  lakini  wakiwa  na  akili  isiyo ya  kawaida  kwa  maana  ya  akili  ya ulevi.  
Sheria inasemaje  kuhusu  hawa  wote  kuanzia  utendaji  wao  makosa,  kushitakiwa  na  kuwajibika    kwao.  Makala  yataeleza  ili   tujue   hadhi  ya  kimashitaka  ya makundi  haya.

1.JE  MWENYE  UGONJWA  WA  AKILI  ANAWEZA  KUSHITAKIWA ?.

Jibu  ni  ndiyo  sheria  haikatazi  kumshitaki  mwenye  ugonjwa  wa  akili( chizi).  Kuna  tofauti  kati ya  kushitakiwa  na  kuwajibika. Kushitakiwa ni  kumfungulia  mashtaka  na  kuwajibika  ni  kupata  adhabu baada  ya  kupatikana  na  hatia. Kwa  hiyo  kushitakiwa atashitakiwa  isipokuwa  sheria  inatoa  mwongozo  kuhusu  kuwajibika kwake.

Kifungu  cha  13 ( 1 )  cha Kanuni  za  adhabu sura  ya  16 kinasema  kuwa  mtu  hatawajibika  kwa  kutenda   kosa  la  jinai  iwapo  wakati  wa  kutenda  kitendo  hicho  alikuwa  katika  hali ya ugonjwa  wowote unaoathiri  akili  yake.  Hiyo  ni  kanuni  ya  jumla  iliyowekwa  na  kifungu  hicho.

Hata  hivyo  kifungu  hichohicho   kimeweka  masharti  kuwa  yapo  mazingira  ambayo  mwenye  ugonjwa  wa  akili  atatakiwa  kuwajibika.  Kinasema  kuwa  mwenye  ugonjwa  wa  akili  hatawajibika  kwa  kutenda  kosa  la  jinai   iwapo  tu  wakati  anatenda  kosa   alikuwa  hajui  anachokitenda,  hana  uwezo  wa  kutambua  kuwa  hapaswi  kutenda  kosa,  na   hana  uwezo  wa  kuzuia  kitendo hicho.

Hii  maana  yake  ni  kuwa  ikiwa  mgonjwa  wa  akili  anao  uwezo  wa  kujitambua wakati  akitenda  kosa  basi  atapatikana  na  jinai hata  kama  ameua  kwa  makusudi   atahukumiwa  kunyongwa.  Maswali  ya  kitaalam(examination)  atakayoulizwa  mahakamani  ndiyo  yatakayotoa  majibu  ikiwa  alikuwa  anajitambua  wakati  wa  kutenda  kosa  au  lah.  Hii  ni  kwasababu  akademia  ya  tiba  inaonesha  kuwa   machizi  wengi  si  wakati  wote  huwa  hawajitambui. 

WBEZ 91.5 - Chicago Public Radio on President Dr. John Pombe Joseph Magufuli

Viewing all 110021 articles
Browse latest View live




Latest Images