Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1054 | 1055 | (Page 1056) | 1057 | 1058 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Kampuni ya TCCIA Investment Limited imeongeza mtaji wake kutoka Tshs Bilioni 21 mwaka 2013/2014 hadi kufikia Tshs Bilioni 33 mwaka 2014/2015 kutoka kwa wanahisa wake. 
   Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa kumi wa wanahisa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Donald Kamori alisema ongezeko hilo linatokana na usimamizi mzuri wa Bodi ya wakurugenzi wa TCCIA Investment Company Limited, kufanya kazi kwa ufasini na waledi.
   “Miaka kumi iliyopita mtaji wetu ulikua ni kiasi cha Tshs bilioni 2 lakini kwa sasa tunaongelea bilioni 33 kuishia Desemba mwaka 2014,” alisema Kamori. 
   “Sisi ni wadogo, lakini tunakwenda vizuri, hii inatokana na usimamizi mzuri wa watu wetu wa mahesabu kwa kushirikiana na Bodi,” aliongeza. 
   Alisema mwaka 2014 kampuni ilipata faida ya jumla ya Tshs Milioni 784 Kabla ya kulipa kodi ambayo aliielezea kuwa ongezeko kubwa kulinganisha na mwaka 2013 ambapo faida ilikua ni Tshs milioni 588. 
   Kutokana na kupata faida kubwa, kampuni imeridhia kutoa gawio kwa wanahisa wake ambapo itatumika jumla ya Tshs milioni 274. 
   “Kutokana na hilo Bodi imeridhia kulipa gawio la Tshs 48 na senti 26 kwa kila hisa moja kwa mahesabu yaliyokaguliwa ya mwaka 2014 kulinganisha na gawio la Tshs 36 na senti 96 kwa mwaka 2013 kwa hisa moja,” aliongeza. 
   Akizungumzia mwenendo wa kampuni na ukuaji wake, Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Mhandisi Aloyce Mwamanga, alisema kwa sasa kampuni ipo katika mchakato wa kubadilisha jina kutoka TCCIA Investment Company Limited na kuwa TCCIA Investment Public Limited Company. “Kutokana na sheria ya makampuni ya mwaka 2002 kampuni ikishazidi wanachama zaidi ya hamsini ni lazima ijulikane kama ni public na sio binafsi,” alisema Mwamanga. 
   Aidha aliwataka wanachama kuzidi kuwekeza katika kampuni hiyo kutokana na kukua kwa kampuni yao kila mwaka.
   “Kampuni yetu inakua kila mwaka, hivyo ni fursa ya wanahisa hasa wale wadogo kuwekeza,” alisema. Aliongeza kuwa ifike mahali wanachama wenyewe wawe ndio wamiliki wa kampuni kwa asilimia kubwa na kusema kuwa uwekezaji ni jambo zuri.
   Wajumbe wa mkutano Mkuu wa kumi wa wanahisa wa Kampuni ya TCCIA Investment Limited wakisikiliza moja ya mada zilizokuwa zinatolewa wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wanahisa hao kabla ya kuanza mkutano huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
   Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa kumi wa Kampuni ya TCCIA Investment Limited, wakimsikiliza mtoa mada, Bw. Arphaxad Masambu, kwenye smina ya kuwajengea uwezo kabla ya kuanza kwa mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa muda wa Mkutano Mkuu wa wanahisa wa TCCIA Investment Company Limited, Mhandisi Peter Chisawilo (kushoto) akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa kampuni hiyo (hawapo pichani) mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Donald Kamori.

  0 0

  STAR TV: Jihabarishe na habari zilizopewa kipaumbele kupitia Magazeti ya leo Dec 13. Fuatilia kwa bofya hapa. https://youtu.be/vE3w_CmnwH4   

  CH10: Je ni habari gani zimepewa uzito wa juu katika magazeti ya leo nchini? Fuatilia habari kemkem kupitia uchambuzi wa magazeti ya leo. https://youtu.be/iPeuGHs59I8

  AZAM TV: Tazama uchambuzi wa magazeti ya michezo ya leo Dec 13 upate kuyajua mengi yaliyopewa uzito wa juu. https://youtu.be/2nShr52l1zA

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela (kulia) akipokea moja kati ya msaada wa mashuka 100 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kutumiwa na wagonjwa wa hospitali ya mji wa Babati (Mrara) anayemkabidhi ni meneja wa NHIF Mkoani humo, Isaya Shekifu.
   Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela (kulia) akipokea msaada wa mashuka 100 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kutumiwa na wagonjwa wa hospitali ya mji wa Babati (Mrara) anayemkabidhi ni meneja wa NHIF Mkoani Manyara, Isaya Shekifu.
   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Manyara, Isaya Shekifu akizungumza mara baada ya kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Babati Crispin Meela mashuka 100 waliyotoa msaada kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara), ambayo inakabiliwa na upungufu wa mashuka kwa wagonjwa.
   Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa mashuka 100 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kutumiwa na wagonjwa wa hospitali ya mji wa Babati (Mrara), kushoto ni meneja wa NHIF mkoani humo, Isaya Shekifu na kulia ni Ofisa ushirika wa halmashauri ya mji huo Keneth Shemdoe.
  Baadhi ya wakazi wa mji wa Babati Mkoa wa Manyara, wakishuhudia Mkuu wa Wilaya ya Babati Crispin Meela akikabidhiwa msaada wa mashuka 100 yaliyotolewa na Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoani humo, Isaya Shekifu kwa ajili ya hospitali ya mji huo (Mrara) ambayo inakabiliwa na upungufu wa mashuka ya kujifunikia wagonjwa wanaolazwa.

  0 0

  Mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Zitto Kabwe amekabidhi bweni la wanafunzi Shule ya watoto wenye ulemavu wa ngozi Buhangija iliyoko mkoani Shinyanga baada ya kutoa msaada wa kujenga bweni hilo. 
   Katika makabidhiano hayo Mhe.  Zitto alisema Tarehe 18 April mwaka huu alitembelea Shule hiyo akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Mama Anna E Mghwira kwa lengo la kusalimia watoto na walimu wao na kutazama mazingira ya watoto. 
   "Nilifika hapa kwa lengo la kuona mazingira ya shule na watoto niliona namna Shule ambavyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo haswa nafasi za kulala, Nilishuhudia watoto wakilala karibu watano katika kitanda kimoja. Niliumizwa sana," alisema Zitto kwa masikitiko. Anasema alionyeshwa ujenzi wa Bweni jipya la watoto na kuelezwa kuwa linajengwa na aliyekuwa mrembo wa Tanzania Mwaka 2012, Brigitte Alfred kupitia Taasisi yake ya Brigitte Alfred Foundation. 
   Aidha aliambiwa kuwa ujenzi umesimama kutokana na changamoto mbali mbali ikiwemo ufinyu wa bajeti, "Wakati huo nilikuwa nimeng'atuka Ubunge na nilikuwa nasubiri malipo ya kiinua mgongo Kwa mujibu wa Sheria, niliamua hapo hapo kwamba sehemu ya gratuity yangu nitaitoa kama mchango wangu katika juhudi za Briggitte kuboresha mazingira ya malezi ya watoto wetu katika shule hii." 
   Zitto alisema aliamua pia kusaidia matibabu ya saratani watu wenye ulemavu wa ngozi katika hospitali ya Ocean Road, Dar Es Salaam kupitia fedha hiyo. NaAlisema anamshukuru Mungu kwamba alimuwezesha kutimiza dhamira yake hiyo na hivyo kuchangia juhudi hizi za Briggitte Alfred Foundation kwa Gratuity yake yote ambao sasa umekamilika. 
   "Leo tupo hapa Buhangija kushuhudia ukamilifu wa kazi hii adhimu, nampongeza sana Miss Tanzania 2012 kwa mradi huu unaotoa changamoto kwa watanzania wengine kutumia nafasi zao katika jamii kusaidia jamii yetu," alisema Zitto. 
   Zitto aliitaka Serikali kuhakikisha kuwa Shule muhimu kama Buhangija zinapata uangalizi maalumu kwani mahitaji yake ni maalumu. Alisema nchi yetu haiwezi kuwa na sifa yeyote nzuri duniani kama bado kuna baadhi ya raia wake wanaishi kwa mashaka na hofu ya maisha yao hivyo ni wajibu wa viongozi kuhakikisha kila mtanzania anajivunia badala ya kuvumilia Utanzania wake.
  Sehemu ya wanafunzi Shule ya watoto wenye ulemavu wa ngozi Buhangija iliyoko mkoani Shinyanga
  Mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Zitto Kabwe akiwa meza kuu na mrembo wa Tanzania Mwaka 2012, Brigitte Alfred 
  Baadhi ya anafunzi Shule ya watoto wenye ulemavu wa ngozi Buhangija iliyoko mkoani Shinyanga wakiwaimbia wageni wakati wa hafla hiyo
  Wageni na sehemu ya wanafunzi Shule ya watoto wenye ulemavu wa ngozi Buhangija iliyoko mkoani Shinyanga

  0 0

   Mkurungezi Mkuu wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay akizugumza na wananchi  (hawapo pichani)  kwenye bonanza la uzazi wa Mpango kwa vijana ambalo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwembeyanga,Temeke jijini Dar. 

   Mgeni rasmi Zukrah Mkwizu akizungumuza na wananchi (hawapo pichani) kuhusiana na suala zima la Uzazi wa Mpango,na kusisitiza kuwa uzazi wa mpangp ni silaha imara ambayo vijana wanaweza kuitumia kupangilia maisha yao na kujikinga dhidi ya utoaji mimba usio salama na kulinda ndoto zao dhidi ya mimba zisizotarajiwa.
   Balozi wa vijana wa Marie Stopes , Doreen Benne akifafanua jambo mbele ya wakazi wa mji wa Temeke na viunga vyake waliofika kwenye kwenye Bonanza la Uzazi wa Mpango kwa Vijana lililofanyika mwishoni mwa wiki ndani ya viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam.
   Mwanamuziki Barnabas Elias 'Barnaba akionesha umahili wake wa kulitawala jukwaa katika Bonanza la Uzazi wa Mpango kwa Vijana Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam
  Sehemu Ya Wananchi Waliofika Katika Bonanza La Uzazi Wa Mpango Kwa Vijana wakifuatilia yaliyokuwa yakijili kwenye bonanza hilo ndani viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Jijini Dar Es Salaam.

   (Picha na Emmanuel Massaka , Globu ya jamii).


  0 0

  Finland and TradeMark East Africa (TMEA) signed an agreement for additional funding on Friday December 11th to further support TMEA's work in enhancing trade across the East African Community to increase prosperity in the region. 
   The agreement was signed by the Finnish Ambassador to Tanzania, H.E. Pekka Hukka and Mr. Ali Murufuki, TMEA Board Chair. Finland has supported TMEA since 2013. 
  The grant agreement will make available an additional Euro 2 million (approximately TZS 4.7 billion) to TMEA activities in Tanzania. The additional funding is intended to fill some funding gaps in the implementation of TMEA's Strategy 1. 
  They will help TMEA to achieve its goals of enhancing trade and removing trade barriers more efficiently than with their original budget. The funds will be directed at enhancing one-stop border posts at Holili, Mutukula and Kabanga and improving cross-border trade. The logistics industry will also be supported to be organized more efficiently. 
   At the moment, East Africa’s trade corridors are characterized by long transit times and high costs. Freight costs per kilometre are more than 50% higher than costs in the United States and Europe. "Tanzania needs a business friendly environment that attracts investment, both domestic and from abroad. A key part of this equation is making logistics cheaper and more effective," emphasized the Finnish Ambassador, H.E. Mr. Pekka Hukka. 
   TradeMark East Africa Board Chair Ali Mufuruki noted that the high transit times and costs in the region are impacting the region negatively. For Tanzania and the region to attract investments, these impediments to growth must be addressed. 
   “I want to thank the Finnish government for their support under TMEA Strategy 1 whose focus has been to invest in projects which have resulted in decreasing transit costs for business and an improved business environment. 
  We applaud the new Government of Tanzania administration’s zeal to modernise Dar Port and the Central Corridor, driving economic growth and job creation.” Said Mr. Mufuruki. 
  His view was reiterated by TradeMark Tanzania Country Director Dr. Josephat Kweka, who noted this support is expected to improve Tanzania’s trade competitiveness and increase its profile as an investment destination within the East African Community. 
   “Facilitating regional trade is an effective means to alleviate poverty," said Dr. Kweka. He added "The Finnish government is an important partner in promoting regional and economic integration in East Africa. This investment in supporting these projects is the catalyst needed to bring prosperity to the region,” 
   TMEA and its partners work to reduce the costs of transport to and within East Africa which in turn is expected to reduce the costs of imports and grow private sector commerce and government revenues. 
   Finland and Tanzania are long-term partners in development cooperation. In addition to supporting sustainable economic growth, Finland works with Tanzania in sectors of good governance and natural resources, with special attention to forestry.
  The  Finnish Ambassador to Tanzania, H.E. Pekka Hukka and Mr. Ali Murufuki, TMEA Board Chair sign the agreement at the New Africa Hotel in Dar es salaam over the weekend.
  Finnish Ambassador to Tanzania, H.E. Pekka Hukka and Mr. Ali Murufuki, TMEA Board Chair sign the agreement.
  The  Finnish Ambassador to Tanzania, H.E. Pekka Hukka and Mr. Ali Murufuki, TMEA Board Chair exchange documents after the signing.
  The  Finnish Ambassador to Tanzania, H.E. Pekka Hukka speaks during the signing ceremony.


  0 0

  Serikali imesema kuwa ina taarifa ya wahitimu wa Taasisi ya Maendeleo ya Maji (WDMI),kukosa nafasi za ajira hivyo suala hilo limefanyiwakazi na serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa maji hivyo wawe na uhakika wa kuajiriwa na wasibweteke wakipata hizo fursa kwani hakutakuwa na nafasi kwa wazembe au wasiowajibika. 
  Akizungumza wakati wa mahafali ya saba ya taasisi hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mbogo Mfutakamba alisema ukosefu wa ajira kwa wahitimu hao ni kilio cha muda mrefu na yeye na serikali wanakitambua. 
  “Tunakitambua kilio hicho, tunafahamu umuhimu wa maji kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Taifa hasa kipindi hiki ambapo Taifa limejielekeza katika miradi mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji” alisema na kuongeza kuwa licha ya wahitimu kutegemea serikali lakini pia wadau wengine sasa wamehusishwa. 
  ”Serikali yetu hivi sasa haina mambo ya mchakato au sijui vitu gani isipokuwa jambo ambalo ninawahakikishia ni kuwa changamoto hiyo imefanyiwakazi kwa kuwashirikisha wadau wengine na kwa wale ambao mtapata nafasi muende mkafanyekazi kwani kwa sasa hakuna lugha nyingine isipokuwa kazi tu” alisema. 
  Alibainisha kuwa chuo hicho kina umuhimu wa pekee katika maendeleo ya nchi hususan kipindi hiki ambacho kumekua na mahitaji makubwa ya maji kwa ajilio ya shghuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kilimo cha umwagiliaji. 
  Alisema hatua ya chuo hicho kudahili wanafunzi wa program ya maji shahada ya kwanza fani ya Uhandisi wa Maji na Umwagiliaji inapaswa kuungwa mkono na serikali kwa kukiwezesha chuo kutimiza malengo yake na pia kuwahakikishia wahitimu ajira. 
  “Tuna upungufu mkubwa wa watalaam wa maji hivyo serikali imehakikisha mnapata ajita” alisema na kuongeza kuwa mpango wa ujenzi wa jengo la ghorofa sita kwa ajili ya chuo hicho upo hatua za mwisho na wakati wowote utekelezaji wa mradi utaanza. 
  Katika risala yao kwa mgebni rasmi wahitimu hao pamoja na mamo mengine walilalamika uchakavu wa majengo, uhaba wa vifaa vya kujifunzi na ukosefu wa maabara za kutosha na maktaba ikiwa ni pamoja na chumba cha kompyuta.
   Wahitimu katika Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI), wakiwa katika maandamano kuelekea katika mahafali ya saba ya taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam juzi. Jumla ya wahitimu 288 walitunukiwa Astashahada na Stashahada  katikia sekta ya maji.

   Wahitimu katika Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI), wakiwa katika maandamano kuelekea katika mahafali ya saba ya taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam juzi. Jumla ya wahitimu 288 walitunukiwa Astashahada na Stashahada  katikia sekta ya maji.

   Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mbogo Mfutakamba akizungumza wakati wa mahafali ya saba ya Taasisi ya Maendeleo ya Usimamizi wa Maji (WDIM), jijini  Dar es Salaam juzi. Jumla ya wahitimu 288 walitunukiwa Astashahada na Stashahada  katikia sekta ya maji.

   Sehemu ya wahitimu katika Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI), wakiwa katika maandamano kuelekea katika mahafali ya saba ya taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam

   Burudani ya ngoma ya asili ya Zanzibar


  0 0

  Magogo ambayo yanasagwa na kuwa vipande vidogo vidogo ambavyo vinasagwa na kuwa karatasi.
  Vipande vidogo vidogo vya miti vikiwa katika mkanda (conveyer belt) wa kupeleka kwenye mashine ya kutengeneza karatasi.
  Matius Makupa, Meneja wa Kiwanda cha Karatasi cha Mufundi akitoa maelezo juu ya utengenezaji wa karatasi kwa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo waliotembelea kiwandani hapo.


  0 0

  Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakiwa wamebeba mfano wa majeruhi wa ajali, mara baada ya kumuokoa kutoka eneo la tukio wakati wa maonyesho ya kufunga mafunzo ya kozi ya awali ya Sajini na Askari wa Jeshi hilo,yaliyofanyika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
  Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakionyesha jinsi ya kuzima moto wakati wa maonyesho ya kufunga mafunzo ya kozi ya awali ya Sajini na Askari wa Jeshi hilo,yaliyofanyika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki.
  Wahitimu wakionyesha mafunzo ya karate waliyopata mara baada ya kuhitimu kozi ya awali ya Sajini na Askari wakati wa kufunga mafunzo hayo katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.


  0 0


  0 0

  Na Rahma Khamis -Maelezo, Zanzibar 
  Waalimu Nchini wametakiwa kuwapa fursa na kuwahamasisha wanafunzi wa Skuli mbalimbali kushiriki katika michezo ili kuwezesha kupata timu nzuri na kushiriki katika mashindano ya Kimataifa. 
  Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari Utamaduni Wasanii na Michezo Tanzania Leonaed Thadeo katika Uwanja wa Amani nje wakati alipokua akifunga Shamrashamra za Tamasha siku ya Walimu Duniani. 
  Amesema nchini  Tanzania wananchi wengi hulalamika kwa kutofanya vizuri katika michezo kutokana na Waalimu kusahau wajibu wao wa kuwajenga wanafunzi wao kimichezo tangu wadogo wakati wapo Maskulini jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya michezo hiyo. 
  Aidha amefahamisha kuwa iwapo jamii itashiriki katika michezo mbalimbali itaweza kujiepusha na mararadhi sambamba na kujenga afya hivyo zoezi hilo liwe endelevu kwani kufanya hivyo kutasaidia walimu kuwa imara kimichezo. 
  Hata hivyo Mkurugenzi huyo amewataka waalimu kutoa fursa kwa kushirikiana na Wizara huusika kwenda kusoma katika Chuo cha Maendeleo ya michezo Tanzania Bara ilikuongeza uwezo na idadi ya waalimu wa michezo. 
  Kwa upande wake mwalimu Mussa Abdulrabi kutoka Wizara ya Elimu amesema lengo la kufanya tamasha hilo ni kuwafanya walimu kushiriki michezo mbalimbali na kuonesha vipaji vyao katika michezo hiyo. 
  Amesema katika mwaka huu hakuna changamoto zilizojitokeza hivyo wanajiandaa mwakani ili wawe na uwezo wa kufanya vizuri zaidi katika tamasha lijalo . 
  Sambamba na hayo mwalimu huyo ameaahidi kuwa watawashajiisha walimu wenzao kwenda kujiunga na Chuo cha Maendeleo ya Michezo ili kupata walimu wengi kwa ajili ya michezo kwani Serekali ina nia ya kuendeleza Michezo . 
  Wakielezea furaha zao washindi katika Tamasha hilo wameiomba Wizara kuangalia suala la michezo zaidi kwa kuandaliwa mafunzo maalum ili kuweza kushiriki katika mashindano mbalimbali. 
  Katika shamrashamra hizo kumefanyika michezo ya ikiwemo kuvuta kamba, Mpira wa Mkono, mbio za Gunia pamoja na Mpira wa miguu kutoka katika Mikoa mitatu ya Zanzibar ikiwemo Mkoa Kusini Unguja , Kaskazini Unguja na Mkoa wa mjini Magharib ambapo Mkoa wa Kaskazini na Mjini ndio walioibuka washindi ikifuatiwa na Mkoa wa Kusini Unguja.
   Walimu walioshiriki mashindano ya michezo mbalimbali wakionyesha vipaji vyao katika mashindano yaliyofanyika viwanja vya nje Amani Mjini Zanzibar 
    Walimu walioshiriki mashindano ya michezo mbalimbali wakishindana kuvuta kamba
    Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Tanzania Leonard  Thadeo akitoa maneno ya shukurani wakati wa  kuwakabidhi  zawadi  washindi  wa  mashindano mbali mbali  ya Walimu kutoka Wilaya 3 Kaskazini, Mjini na Kusini huko katika viwanja vya nje Amani Mjini Zanzibar.
   Washindi walishiriki  katika mashindano mbali mbali wakipewa zawadi na Mgeni Rasmi Leonard  Thadeo  mara baada ya kumaliza mashindano hayo
   Washindi walishiriki  katika mashindano mbali mbali wakipewa zawadi na Mgeni Rasmi Leonard  Thadeo  mara baada ya kumaliza mashindano hayo
  Picha zote na Miza Othman - Maelezo, Zanzibar

  0 0


  0 0

  Picha ya Lorraine Marriot -Miss Universe Tanzania 2015 akiwa Las Vegas - Official Photo Head shot

  0 0

  Inline image 1

  LISTI  YA WANAMUZIKI WA SIKINDE WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI…

  1.       Abdallah Dogodogo
  2.       Abel Baltazar
  3.       Adam Bakari
  4.       Ally Makunguru
  5.       Charles John “Ngosha” (2011)
  6.       Chipembele Said “Bob Chipe”
  7.       Fadhili Uvuruge  “Santimaa”
  8.       Gaspar Kanuti
  9.       George Kessy
  10.   Gervas Herman
  11.   Hamisi Juma “Maalim Kinyasi”
  12.   Haruna Lwali
  13.   John Malyanga
  14.   Joseph Mulenga “King Spoiler”
  15.   Juma Banduki
  16.   Juma Hassan Town (1997)
  17.   Kassim Mponda “De La Chance”
  18.   Kassim Rashid ‘Kizunga’
  19.   Kitwana Amasi
  20.   Machaku Salum
  21.   Michael Enock ‘Teacher’ (31-May-2006)
  22.   Mohamed Banduki
  23.   Mohamed Mwinyikondo (1996)
  24.   Michael Bilali (1996)
  25.   Mohammed Idd “Control” (2012)
  26.   Muharam Saidi (1988)
  27.   Muhidin Kisukari
  28.   Nassir (Francis) Lubua
  29.   Shaaban Mabuyu
  30.   Suleiman Mwanyiro “Computer” (2002)
  31.   Thomas Mamwinyi
  32.   Tino Masinge ‘Arawa’

  WALIOPITA KWA MUDA
  1.       Omari Zumo
  2.       Mohamed Shaweji
  3.       Banza Tax

  IMETAYARISHWA NA WILLIAM KAIJAGE

  0 0

  Na  Bashir  Yakub

  Makubaliano  ni  sehemu  ya  maisha  yetu  ya  kila  siku.  Shughuli  zetu  za  kila siku  hutegemea  makubaliano.   Ukimkuta  mtu  anabeba  zege  kwa  ajili  ya  ujenzi  yupo  katika  makubaliano. Ukimkuta  mtu  anaendesha  daladala, bodaboda   yupo  katika  makubaliano. 

  Ukimkuta  mtu  katika  ofisi  yoyote  ya  umma  yupo katika  makubaliano,walio kwenye  ndoa  na  uchumba nao  ni  makubaliano,  mfanyakazi  wa  ndani  yupo katika  makubaliano.  Aliyechukua  mkopo,  aliyeuza, kununua  nyumba au  kifaa  kingine  chochote  nao  wote  wapo  katika  makubaliano. Haraka  utaona kuwa  makubaliano  hubeba  sehemu  kubwa  ya  maisha yetu  ya  kila  siku.

  Yatutosha  kusema  kuwa  makubaliano  ndio  maisha  yenyewe haswaa.Hata  biashara  yoyote  unayoshirikiana  na  mwenzako  nayo  bila  shaka ni  zao  la  makubaliano. Tutaona hapa makubaliano  yenye  hadhi  ya  kuitwa  mkataba na  ikiwa  mkataba  wa  maneno  unakubalika.

  0 0
  0 0

  Na Sixmund J. Begashe 
  Watanzania wamehusiwa kuwapenda watu wenye ulemavu wa ngozi kama albino, na kuachana kabisa na imani putofu kuwa viongo vya watu hao vinaweza kuwapatia bahati katika maisha yao, kama wanavyo fanya sasa baadi ya watu waovu hapa nchini. 
   Wito huu umetolewa na Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Mh Bella Bird alipotembelea Makumbusho ya Taifa kujionea onesho maalum la picha zinazoelezea namna watu wenye ulemavu wangozi wanavyo nyanyasika kwa kuishi maisha ya wasiwasi kuofia waovu wenye nia mbaya na miili yao. 
   “Onesho hili linaumiza sana rohoo, linaumiza tena sana, maana linanifanya na mimi nihisi kama ndio mmoja wa hawa watoto wanaoishi katika kambi hii ya Kabanga, hawawezi kutoka nje na kufurahi na watoto wenzao, hawawezi kuishi na wazazi wao, hii inaumiza sana” alisema Mh Bird huku akitokwa na Machozi. 
   Mh Bird ameendelea kwa kutoa wito kwa vyombo vya habari kusaidiana na Makumbusho ya Taifa katika kuielimisha jamii kwa kupitia njia hii adhimu na yakisayansi ili jamii ielimike na kuondokana na fikra potofu za kuwauwa na kuwakata viungo watu wenye ulemavu wa ngozi. 
  Akimshukuru Mkurugenzi huyo Mkazi wa Benki ya Dunia hapa Nchini kwa ofisi yake kudhamini onesho hilo, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula ameahidi kuwa Makumbusho ya Taifa itaendeleza kampeni za utokomezaji wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa kutoa elimu kwa jamii ili waachane kabisa na tabia hiyo ya ukatili. 
  Prof Mabula pia alitumia nafasi hiyo kumwomba Mh Bird ofisi yake ifikirie namna ya kuiwezesha Makumbusho ya Taifa kulitembeza onisho hilo hasa sehemu kuu zilizo adhirika na Mauaji ya watu wenye ulemavu wangozi kama Mikoa ya Mwanza na Shinyanga ambapo Mkurugenzi huyo alikubaliana na ombi hilo na kuwa atalifanyia kazi. 
   Prof Mbula aliendelea kwa kuziomba taaisisi mbali mbali, za serikali na zile za binafsi kuisaida Makumbusho ya Taifa kuendeleza vita hii ya mauaji ya kinyama hapa nchini ili kuwafanya watanzania wote waishi kwa amani kwani sisi sote kama watanzania ni sawa na kila mmoja atambue kuwa kila mtu anahaki ya kuishi. 
   Onesho hilo la picha lenye kuonesha namna gani watu wenye ulemavu wa ngozi albino wanavyoishi kwa shida, mashaka, uzuni, hofu, hawako huru kama watu wengine, limefanyiliwa na Benki ya Dunia na litaendelea kuoneshwa hadi mwishoni mwa mwezi wa Kwanza hapo mwakani.
   Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini Mh Bella Bird kwa uzuni akitafakari baada ya kuitazama picha ya watoto wenye ulemavu wanguzi.

   Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini Mh Bella Bird akipokea maelezo kutoka kwa mtaalam wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Bi Flora juu Picha ya mtoto wenye ulemavu wa ngozi.

   Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini Mh Bella Bird akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula mwenye shati jeupe kushoto.

  Mkurugenzi wa Makumbusho nchini, Prof Audax Mabula akimshukuru Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia kwa kutembelea Makumbusho kujionea onesho la mateso yanayowapata watu wenye ulemavu wa ngozi.


  0 0

   Magogo ambayo yanasagwa na kuwa vipande vidogo vidogo ambavyo vinasagwa na kuwa karatasi.
   Vipande vidogo vidogo vya miti vikiwa katika mkanda (conveyer belt) wa kupeleka kwenye mashine ya kutengeneza karatasi. 
   
  Matius Makupa, Meneja wa Kiwanda cha Karatasi cha Mufundi akitoa maelezo juu ya utengenezaji wa karatasi kwa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo waliotembelea kiwandani hapo.    Mhandisi wa madawa (chemical engineer) Beatrice Kigodi (mwenye shati jeupe) akitoa maelezo juu ya upimaji wa karatasi zinazozalishwa na kiwanda hicho. Kulia kwake ni Mhandisi Happiness Mgalula (Naibu Katibu Mtendaji- Miundombinu na Huduma, Mkurugenzi Mkuu Bw Y. Y. Choudary na Paul Sangawe, Naibu Katibu Mtendaji (Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya Kiuchumi) 

   Baadhi ya wajumbe wa timu ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo wakiangalia gurudumu za karatasi zikiwa  tayari kwa kusafirishwa.  0 0


  0 0

  MAASKOFU wa madhehebu  mbalimbali wa Makanisa hapa Tanzania wamempongeza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kukubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Tamasha hilo linalokwenda sambamba na Shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 kwa amani na utulivu, uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Askofu wa Kanisa la KKKT, Dk Alex Malasusa anasema ni jambo jema kumshukuru Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani na utulivu kiasi cha kumpata rais mchapakazi.

  Amefurahishwa na kukubali kuwa mgeni rasmi kwa kuitikia wito wa ombi la madhehebu mengine ingawa yeye ni Muislamu kwani kufanya hivyo ni kuzidi kuvunja makundi ya udini ndani ya nchi yetu.Anasema ni  wakati wa kumshukuru Mungu baada ya  tukio kubwa la uchaguzi Mkuu ambako kabla yalifanyika maombi ya kumuomba Mungu kuwapitisha katika uchaguzi Mkuu ambao ulifanyika kwa amani na utulivu.     
    
  Askofu Dk. Valentino Mokiwa wa Kanisa Anglican,  jimbo Kuu la Dar es Salaam, amempongeza Msama Promotions kwa kuandaa matamasha ya kumuimbia na kumtukuza  Mungu kupitia matamasha yake.Askofu Mokiwa anasema ni suala la kujivunia ikiwa ni mara ya kwanza kuwa na mgeni rasmi ambaye ni mwanamke wa kwanza nchini kuwa Makamu wa Rais na kitendo chake kinaonekana kuwa ni cha kizalendo.

   Anasema ni jambo la kumshukuru Mungu baada ya kufanikisha kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu hivyo amemtaka Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama kuendelea kujitolea kuandaa matamasha  kama hayo yenye tija kwa taifa.Naye  Askofu Mkuu wa jimbo la Mashariki la Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk Lawrence Kametaanasema amefurahishwa  na  Makamu  wa  Rais, kuonesha uzalendo na kukubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo lenye lengo la kushukuru baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

  Anasema kuwa kitendo hicho cha Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  kuwa Mgeni rasmi kimezidi kuiaminisha Dunia kuwa Tanzania ni ya amani na haina matabaka ya kidini na ukabila.Katibu Mkuu wa Makanisa ya Kipentekoste nchini, Askofu David Mwasota amesema kwamba Tanzania  imezaliwa upya kwa kutinga katika neema ambayo ilikuwa inatarajiwa na wengi.

  Askofu Mwasota anasema  kuwa Rais Magufuli  hakukosea kumteua mama Samia kuwa makamu wa Rais  wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Askofu wa Kanisa la Wasabato, Warwa Marekana anasema wamefurahishwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani kukubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Krismasi ambalo linakwenda sambamba na kushukuru Tanzania kupita kwenye uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25.

  Marekana anasema kukubali kuwa mgeni rasmi inathibitisha kwamba tamasha hilo halina ubaguzi wa dini kwani Waislamu na Wakristo   Askofu  wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Telesphor Mkude amesema kuwa kama amani itakuwepo nchini ana amini serikali ya Awamu ya Tano chini ya John Pombe Magufuli kutakuwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.

  Amesema kuwa wao kama viongozi wa dini wanafurahishwa na jinsi kiongozi mwanamama shupavu tena muislamu kuamua kuabudu pamoja na wakristo katika  tamasha hilo la shukrani.

  Hiyo ni nzuri na sisi kama viongozi wa dini tunaiunga mkono kampuni ya Msama Promotions kwa kutoa mwaliko kwa Makamu wa Rais hivyo tunaamini atakuwa chachu ya kuwahimiza wananchi wengine ambao sio wakristo kujumuika katika kutoa shukrani kwa mungu mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

  Alisema, hata kama Magufuli atakuwa ni kiongozi bora kiasi gani lakini kama amani haitapatikana itakuwa ni kazi bure hivyo amewataka wananchi kuienzi amani iliyopo.Alisema amekuwa akifuatilia matamasha yanayoandaliwa na kampuni ya Msama Promotions, yamekuwa yakilenga katika jamii hivyo ni kitu  cha kushukuru kwa kampuni hiyo kuandaa matamsha kwa lengo la kuenzi amani.

  Amesema angeomba hali hiyo iendelee hata mikoani  ili kuwafanya wananchi wa mikoani kuona umuhimu wa amani haiitajiki Dar es Salaam pekee.Amesema kuwa anashukuru kumaliza kwa uchaguzi mkuu kumalizika salama  na nchi imepoa baada ya kupatikana Rais ambaye anaonekaa kuwa na dhamira ya kweli katika kuhakikisha anaipelekea Tanzania katika uchumi wa kati.

  Askofu Mkude amesema suala la amani ni muhimu na amewataka Maaskofu na Mapadri kuhakikisha wanahubiri amani wanapokuwa katika ibada zao.Askofu wa Kanisa la Menonite, Amos Mhagache amesema ni nafasi yetu kumshukuru Mungu kwa kutubariki kupita katika kipindi kigumu cha uchaguzi Mkuu.

  Askofu Mhagache anasema kwamba Yesu Kristo ni mwokozi hasa sasa hivi ndio nchi Mungu aliyotupa katika kipindi hiki baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25.

older | 1 | .... | 1054 | 1055 | (Page 1056) | 1057 | 1058 | .... | 3286 | newer