Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo afanya ziara TBC na BASATA.

$
0
0
nap1
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia moja ya kazi za wasanii katika kiwanda cha kutengenezea batiki alipotembelea ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) leo hii jijini Dar es Salaam.
nap2
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi Lilian Beleko (kulia) akimkaribisha kwa furaha waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye wizarani hapo leo hii jijini Dar es Salaam.
nap4

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye(kushoto) akiongea na menejimenti ya shirika la Utangazaji Tanzania-TBC(hawapo pichani) wakati alipotembelea makao makuu ya shirika hilo ili kujua changamoto walizonazo na jinsi gani atawasaidia kama waziri mwenye dhamana.

NHIF yapeleka Madaktari Bingwa Kagera, Yaonya wadanganyifu

$
0
0
Na Grace Michael, Kagera

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya umesema hautawavumilia watumishi katika hospitali ya Mkoa wa Kagera wanaojihusisha na vitendo vya kughushi nyaraka za kuchukulia dawa katika maduka ya dawa na kuusababishia Mfuko kulipa fedha ambazo hazijatumika kihalali.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bw. Michael Mhando ameyasema hayo mjini hapa wakati akizungumza na uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Kagera kabla ya uzinduzi wa mpango wa Madaktari Bingwa ambao wamepelekwa na Mfuko huo kutoa huduma kwa wanachama na wananchi kwa ujumla.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bw. Michael Mhando akiongozana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Nasoro Mlambila kukagua maeneo wanayofanyia kazi madaktari bingwa ambao NHIF imewapeleka katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera. 

“Niseme tu kwamba tumekuwa tukichukua hatua mbalimbali zikiwemo za kuwaonya kwa barua na wengine kuwafutia usajili na wengine kuwafikisha mahakamani watoa huduma ambao wanajihusisha na vitendo vya udanganyifu lakini niseme kwamba kwa hospitali hii natangaza rasmi kuwa kuanzia sasa naanza kuchukua hatua kali kwa watumishi ambao watabainika kujihusisha na udanganyifu wowote,” alisema Bw. Mhando.

Alisema kuwa Mfuko unalo jukumu la kulinda fedha za wanachama wake na kuhakikisha zinatumika katika matumizi sahihi hivyo hauko tayari kuendelea kuvumilia watoa huduma ambao sio waaminifu.

“Nawaomba sana toeni huduma kwa wanachama wetu na sio kutumia vitambulisho vyao kughushi nyaraka mbalimbali zikiwemo za kuchukulia dawa katika maduka ya dawa…sisi tuko tayari kusaidia kituo chochote katika uboreshaji wa huduma zake ili wananchi wanufaike kwa ujumla na sio kikundi cha watu wachache,” alisema Bw. Mhando.
Daktari Bingwa wa Masuala ya Usingizi na Wagonjwa Mahututi Vence Sakwari akijadili jambo na mwenyeji wake katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera kabla ya kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wake. 

Katika hatua nyingine aliitaka Hospitali hiyo kuangalia namna ya uboreshaji wa huduma zake hususan upatikanaji wa dawa ambao umeonekana kuwa tatizo kubwa linaloikosesha mapato hospitali hiyo.

Alisema kuwa mpaka sasa Hospitali ya Mkoa wa Kagera imekuwa ikipoteza mapato mengi kutokana na ukosefu wa dawa na vipimo ambavyo ndivyo vinaingiza fedha nyingi katika vituo vya kutolea huduma hali ambayo inakwamisha uboreshaji wa huduma.
Sehemu ya wagonjwa wakisubiri kuelezwa utaratibu wa kuwaona madaktari bingwa waliofika hospitalini hapo. 

WANANCHI WATAKIWA KUWA MAKINI KUELEKEA MSIMU WA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA

$
0
0
Na. Tamimu Adam- Jeshi la Polisi

Jeshi la polisi nchini  limewataka wananchi kuimarisha na kutekeleza kwa vitendo dhana ya ulinzi jirani katika kipindi hiki cha kuelekea kuadhimisha sikukuu za  mwisho wa mwaka na kusherekea mwaka mpya kwani  ulinzi jirani ni mkakati madhubuti katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao hapa nchini.

Hayo yalisemwa  na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mrakibu mwandamizi wa Polisi Advera Bulimba wakati akitoa tahadhari ya usalama katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka,  ofisini kwake  makao makuu ya Jeshi la Polisi,  jijini Dar es salaam.

“Uzoefu unaonyesha kuwa  kipindi cha kuelekea mwisho  wa mwaka na hususani sikukuu za mwisho wa mwaka  baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo  kujipatia kipato kwa njia isiyo halali kwa kufanya udanganyifu, wizi na utapeli katika maeneo mbalimbali hivyo wananchi wanatakiwa kuwa macho katika shughuli zao” Bulimba alisema. 

Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi nchini limejipanga kikamilifu kwa kufanya doria  katika maeneo yote kuhakikisha wananchi wanasheherekea na kumaliza mwaka kwa amani na usalama pasipo hofu yoyote yakufanyiwa vitendo vya uhalifu.

Aidha, aliwataka wafanyabiashara na wamiliki wa hoteli hapa nchini kuweka kamera na vifaa maalumu vyenye uwezo wa kufuatilia mienendo ya watu wanaoingia na kutoka katika maeneo yao ya biashara ili kuweza kuwabaini wahalifu na uhalifu kwa haraka. 

Pia alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi wanapowatiria shaka watu wasiowafahamu katika maeneo yao kwa  kutoa taarifa kwa namba za bure ambazo ni  111 na 112, namba hizi ni za dhalura na ukipiga katika mkoa wowote ulipo  zitapokelewa na hatua za haraka zitachukuliwa.

KAPUMZIKE KWA AMANI MPAMBANAJI MWENZETU DOTTO MZAVA.

$
0
0


BLOGGER chipukizi nchini Dotto Mzava, amefariki Dunia katika ajali ya barabarani Desemba 14, 2015 hapa jijini Dar es Salaam. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Nchini, (TBN), ambao marehemu alikuwa ni mwanachama wake, Bw. Joackim Mushi amesema Dotto ambaye alikuwa akifanyia kazi Jamii Media (Wamiliki wa mtandao wa Jamii Forum, amefariki kwa ajali ya pikipiki ingawa haikuelezwa ajali hiyo imetokea maeneo gani hasa ya jiji la Dar es Salaam. 

Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina lake Lihimidiwe Amin.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGIWA KWA TSN SUPERMARKET

WAZIRI MKUU MHE KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA KADHI MKUU WA TANZANIA

$
0
0
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majliwa akizungumza na Kadhi Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abdallah Mnyasi  ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 14, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kesi ya kupinga matokeo ya ubunge iliyowailishwa na aliyekuwa Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu yaanza

$
0
0
 Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (wa pili kulia) akitoka nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kusikiliza kesi yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyomtangaza Abdallah Mtolea (CUF) kuwa  Mbunge wa jimbo hilo Dar es Salaam. Kulia ni msemaji wa wa Timu ya Simba Haji Manara
  Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Mhe. Abbas Mtemvu (kulia) na mkewe wakitoka nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

Mgombea urais kupitia Chama cha  Chauma na  amekuwa Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Hashim Rungwe Spunda (wa pili kulia) akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (wa tatu kulia) baada ya kutoka nje  ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kusikiliza kesi yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyomtangaza Abdallah Mtolea (CUF) kuwa  Mbunge wa jimbo hilo.

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imetoa wiki moja kwa upande wa Jamhuri katika  kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), kuwasilisha majibu yao.

Jaji Ama Isario Munisi, alisema hayo leo mahakamani hapo, wakati shauri hilo lililofunguliwa na Mtemvu dhidi ya wadaiwa watatu akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), lilipokuja kwa kutajwa.
Wadaiwa wengine katika kesi hiyo ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke na Mbunge wa Jimbo hilo, Abdallah Mtolea (CUF).
Jaji alisema  upande wa Jamhuri unatakiwa kuwasilisha majibu yao Desemba 21, mwaka huu na  upande wa wadai uwasilishe majibu yake Desemba 24, mwaka huu.
Alisema shauri hilo litatajwa Desemba 29, mwaka huu, kuangalia iwapo pande zote husika zimewasilisha majibu yake ili kupanga tarehe ya usikilizwaji.
Awali, Wakili wa Mtemvu, Egidi Mkoba, alidai Mtolea hayupo lakini mara ya mwisho alikuwepo na alikuwa anajua kama kesi inakuja jana.
Jaji  alisema shauri lilikuja kwa kutwaja, ambapo alihoji utaratibu unaotumiwa na upande wa Jamhuri kwa sababu bado haujawasilisha majibu yake.
Wakili wa Serikali Mkuu, Ponsiano Lukosi kwa niaba ya wadaiwa, alidai anaendelea kujibu na pia wanaendelea kupata maelekezo kutoka kwa mdaiwa wa kwanza  na wa pili kwa kuwa wanavielelezo vingi ambavyo lazima avisome na kujibu.
Jaji Munisi aliutaka upande wa wadaiwa kufuatilia kwa kuwa hawezi kwenda likizo kabla ya usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo.
Wakili Lukosi alidai atalifanyia kazi hilo, kwa sababu maelezo anaandika mwenyewe na wiki hii watakuwa wameshawasilisha, hivyo aliomba apewe wiki mbili awe amewasilisha majibu yao.
Jaji alihoji hayo maelezo ya awali yatasilikilizwa lini, wakati wiki ya kwanza ya Desemba wadaiwa walikuwa wameshapatiwa hati ya madai na  alitegemea wanamalizia kuwasilisha.
Wakili Lukosi alidai wanakuja kuna haja ya kuwasilisha mapema, lakini kuna mkono wa tatu wa kupata maelezo ambayo ni ya mdaiwa wa kwanza, vielelezo vya mdaiwa wa pili tayari, lakini  Mwanasheria Mkuu wa Serikali vielelezo vyake ni vingi ambavyo huwezi kusoma kwa mara moja.
Jaji alisema lazima wamalize kusikiliza maelezo ya awali, ili kesi iweze kupangiwa Jaji mwingine wa kuisikiliza.
Mtemvu amefungua kesi hiyo akiiomba mahakama hiyo itengue ushindi wa  Mtolea kwa madai ya kwamba hakupata nafasi ya kurudia kuhesabu kura na hapakuwepo na majumuisho.

WAZIRI KITWANGA, NAIBU WAZIRI WA USALAMA WA RAIA WA CHINA WASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

$
0
0
mbo1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) na Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang wakisaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama wa Raia kati ya Wizara hizo mbili, katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
mbo2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), wakibadilishana Hati za Makubaliano ya Ushirikiano waliosaini na Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang, katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
mbo3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), akimpa zawadi ya kinyago Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang, mara baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya wizara hizo mbili. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
mbo4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang, mara baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya Wizara hizo mbili. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
mbo5
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wa pili kushoto), akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang (kulia), kabla ya kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya Wizara hizo mbili. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu, Mbarak Abdulwakil. Picha na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
mbo6
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (watano kulia-mstari wa mbele),  Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang (watano kushoto-mstari wa mbele), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (watatu kulia-mstari wa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Mawaziri hao kumaliza kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya wizara hizo mbili. Tukio hilo lilifanya katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMPOKEA WAZIRI JENISTA MHAGAMA NA NAIBU MAWAZIRI MAVUNDE NA POSSI

$
0
0
si11
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama wakati aliporipoti Ofisini kwake jijini Dar es salaam kuanza kazi Desemba 14, 2015. 
si12
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde  wakati aliporipoti Ofisini kwake jijini Dar es salaam kuanza kazi Desemba 14, 2015. Katikati ni Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenisa Mhagama 
si13
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Abdallah Possi   wakati aliporipoti Ofisini kwake jijini Dar es salaam kuanza kazi Desemba 14, 2015. Wapili kushoto  ni Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenisa Mhagama  na kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde
si14
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama  (wapili kushoto), na Naibu Mawaziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Abdallah Possi  (wapili kulia)  na Anthony Mavunde (kulia) baada ya kuwakabidhi taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakati waliporipoti Ofisini kwa Waziri Mkuu kuanza kazi Desemba 14, 2015.
si15
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama (katikati), Naibu Mawaziri Dkt. Abdallah Possi (kulia) na Anthony Mavunde (wapili kulia)) baada ya mawaziri hao kuripoti  Ofisini kwake kuanza kazi Desemba 14, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt, Florence Turuka, Wanne kushoto ni katibu Mkuu Kazi na Ajira, Eric Shitindi na watatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Regina Kikula.
si16
Waziri Mkuu, Kassim majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama  (kushoto) na Naibu Mawaziri, Dkt. Abdallah Possi (Wapili kulia) na Anthony Mavunde (kulia) baada ya Waziri huyo na Manaibu wake  kuripoti Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kuanza kazi Desemba  14, 2015. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN, AMKARIBISHA WAZIRI WAKE MAKAMBA OFISINI, AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MABALOZI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Januari Makamba, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika mazungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Januari Makamba, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na  Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Yasemin Eralp, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mhe Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2015 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na  Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Mhe. Jorge Luis Lopez, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mhe Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2015 kwa mazungumzo.



Filamu Nne Kutoka Proin Promotions zaingia kwenye kinyanganyiro cha Africa Magic Viewers Choice Awards 2016, wadau tunaomba tuzipigie kura zilete ushindi nyumbani

$
0
0
Proin Promotions Ltd imefanikiwa kuingiza filamu zake nne katika Shindano la Africa Magic Viewers Choice Awards 2016 (AMVCA 2016) katika vipengele viwili huku Filamu zote nne zikiingia katika Kipengele Kimoja cha BEST MOVIE - EAST AFRICA filamu zilizoingia katika kipengele hiko ni  MAPENZI YA MUNGU, KITENDAWALI, MPANGO MBAYA, DADDY’S WEDDING huku filamu ya KITENDAWILI ikiingia katika Kipengele kingine cha BEST INDIGENOUS LANGUAGE MOVIE/TV SERIES – SWAHILI.
Filamu zote nne zimeingia katika kipengele kimoja zikichuana zenyewe huku mbili zikitokea nchini nyingine.
 Tunawaomba watanzania kuweza kuzipigia kura filamu hizi ili kuweza kuibuka mshindi. Jinsi ya Kupiga kura fuata tovuti hii www.africamagic.tv
Washindi wa shindano hii wanatarajiwa kutangazwa Mwakani 2016 mwezi wa 3.

Ziara ya Dkt.Kalemani katika kituo cha uzalishaji umeme kwa kutumia Gesi Kinyerezi.

$
0
0
Na Anitha Jonas –MAELEZO 
Wizara ya Nishati na Madini imewaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha uzalishaji wa umeme katika Mradi wa Kinyerezi I na Kinyerezi II unakamilika ifikapo mwezi Februari 2016 na kuanza kufanya uzalishaji ilikuongeza kiasi cha nishati ya umeme kufikia zaidi ya Megawati 100. 
 Agizo hilo lilitolewa leo na Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani alipofanya ziara yake katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya Gesi cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam,hii ni baada ya kuelezwa kuwa kituo hicho kwa sasa kinazalisha 70 Megawati za umeme ambaohautoshelezi kwa matumizi ya watanzania. 
 “Watanzania wamechoshwa na mgao wa umeme na wanaimani kubwa na uzalishaji wa kituo hiki cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi hivyo wanatarajia umeme wa uhakika katika kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji na kujipatia kipato”,alisema Dkt.Kalemani. 
 Hata hivyo Dkt. Kalemani aliwapongeza watendaji wa TANESCO na wakandarasi wanaosimamia uendeshaji wa mitambo hiyo ya uzalishaji huku akiwasihii waongeze jitihada za dhati kwani watanzania bado hawaridhishwi na kiasi cha umeme kinachozalishwa kwa sasa. 
 Kwa upande wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Omari Chambo alisema kuna mradi mpya uitwao Kinyerezi Extension unakaribia kuanzishwa hivi karibuni ambao utazalisha Megawati 345 za umeme na kupitia mradi huu uzalishaji wa umeme utaongezeka kwa kiasi kubwa. “Tutajitahidi kwa sasa umeme usikatike mara kwa mara na jitihada za kusafisha mitambo miwili ya phase I na Phase II inafanyika na itakapokamilika tunatarajia kuzalisha zaidi ya Megawati 140 za umeme na usafishaji wake unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu”,alisema Mhandisi Chambo. 
 Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Bw.Decklan Mhaiki alisema mradi wa Kinyerezi Extension ambao utagharimu jumla ya kiasi cha Dola Milioni 340 unatarajia kuanza hivi karibuni mara baada ya kukamilika kwa Mkataba na malipo ya 15% kwa mkandarasi. 
 Pamoja na hayo wizara ya Nishati na Madini imetoa angalizo kwa watendaji wote wanaozalisha umeme kwa kutumia maji walinde vyanzo vya maji na kuacha kutumia maji hayo kwa matumizi mengine kama ya kilimo. 
 Uzalishaji wa umeme kwa kutumia Nishati ya Gesi utasaidia kupunguza gharama za watumiaji wa umeme pamoja na kushusha gharama za uzalishaji.
 Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (kushoto) akimsikiliza Naibu Mkurugenzi Mtendaji Tanesco Bw.Decklan Mhaiki alipokuwa akimwonyesha mradi wa Kinyerezi I mara baada ya kuwasili katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam.

 Meneja Mradi TANESCO Mhandisi Simon Jalima (wa pili kushoto) akimwonyesha  Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa pili kulia) moja ya mtambo unaopokea gesi kutoka mtwara na kuisambaza mpaka kituo cha Ubungo alipofanya ziara ya kuona maendeleo ya mradi huo leo katika eneo la mradi Kinyerezi jijini Dar es Salaam, wa kwanza kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Tanesco Bw. Decklan Mhaiki.

 Meneja Mradi TANESCO Mhandisi Simon Jalima (wa pili kushoto) akimtembeza Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa pili kulia) kumwonyesha mitambo mbalimbali ya uzalishaji wa umeme uliyopo katika kituo hicho cha Kinyerezi I, jijini Dar es Salaam.

 : Mmoja wa wataalamu wa kuendesha mitambo inayosambaza nishati ya umeme uliyozalishwa kwa kutumia gesi (Shift Supervisor) Bw. Mohamed Lanzi akimwonyesha Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza kulia) mtambo wa usambazaji wa umeme wa Morogoro unaotokea  Kinyerezi I namna wanavyouendesha.

Meneja Mradi  wa Kinyerezi Extension kutoka Kampuni ya Sumitomo Japan Bw. Shoji Watanabe akimweleza  Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani ni kwa muda gani mradi huo utakamilika mara baada ya kupewa mkataba wa kuanza kazi hiyo, leo Kinyerezi jijini Dar es Salaam.

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

$
0
0

SIMU.TV:   Mbunge wa Lindi mjini Hassan Kaunje  ameanza mikakati ya kuondoa kero ya maji ikiwa ni utekelezaji wa ahadi alizotoa wakati wa kampeni;https://youtu.be/LrgiliHiBkM
 SIMU.TV:   Migogoro ya familia na ukosefu wa haki vimetajwa kuwa chanzo kikuu cha ongezeko la ukatili kwa watoto; https://youtu.be/QUBxgDtc_vs
 SIMU.TV:   Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bunda ameazimia kuwafichua wabadhirifu wa fedha za miradi; https://youtu.be/z5gSqLInXbo
 SIMU.TV:   Wakazi wa Kongwa wamepunguza magonjwa ya milupuko zaidi ya asilimia 90 kutokana na elimu waliyoipata ya usafi wa mazingira;https://youtu.be/_Ue031daNYA
SIMU.TV:   Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Singida wameuomba mfuko wa Bima ya afya wa NHIF kupunguza kiwango cha kuchangia malipo ya huduma za afya. https://youtu.be/Wtaz5Byy-AA
 IMU.TV:   Wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu wametakiwa kutowaficha watoto wao majumbani na badala yake wawapeleke katika shule maalumu. https://youtu.be/R1Gppw4kvB4
 SIMU.TV:   Mtifunao wa ligi kuu soka Tanzania bara umeendelea kwa timu za Coastal Union na African Sports kutoka sare ya bao 1 kwa 1.https://youtu.be/o01HpE7hFUE
 SIMU.TV:   Watoto 42 kati ya 100 nchini wana udumavu kutana na kukosa lishe bora ikiwemo wazazi kutokuwanyonyesha watoto wao.https://youtu.be/wPFzso8GbRE
 SIMU.TV:   Madiwani wa Halmashauri ya Ileje mkoani Mbeya wametakiwa kubuni vyanzo vya mapato na kusimamia vyema matumizi ya wilaya hiyo. https://youtu.be/an0ni-aNlKc

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO ATEMBELEA OFISI ZA ILIYOKUWA WIZARA YA UCHUKUZI NA KUONGEA NA MENEJIMENTI NA WAKUU WA TAASISI LEO ASUBUHI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani (Kushoto), akisalimia na Kaimu Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi, mara baada ya kuwasili ofisini hapo leo asubuhi.  
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi ya Naibu Waziri iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi mara baada ya kuwasili ofisini hapo leo asubuhi.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Kapteni Kenan Mhaiki, akijitambulisha wakati wa mkutano wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani (hayupo pichani) na Menejimenti ya iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi na Wakuu wa Taasisi zilizo chini yake, leo asubuhi. Naibu Waziri Huyo amewasisitiza watendaji wote kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani (Kulia), akiongea na Menenjimenti ya Iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi pamoja na wakuu wa taasisi zilizo chini yake, hapo leo asubuhi.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani (Kushoto), akimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Elias Mshana wakati wa mkutano wake na Menejimenti ya iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi na Wakuu wa taasisi zilizo chini yake , leo asubuhi.

Achia Body by Ommy Dimpoz ComingSoon


TANZIA

$
0
0
Maria Mtura wa Kitanda
1933 - 14 Desemba, 2015 

Familia ya Jaji Mstaafu Steven James Bwana wa Plot. No. 903 Chakechake Rd. Masaki jijini Dar es salaam  inasikitika kutangaza kifo cha Mama yao mpendwa Maria Mtura wa Kitanda kilichotokea jana tarehe 13 Desemba, 2015. 
Mwili wa marehemu utasafirishwa kesho tarehe 15 Desemba, 2015 saa Kumi Alasiri kuelekea kijijini Etaro, Musoma kwa mazishi. Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote. 

Bwana alitoa, 
Bwana ametwaa.
na jina lake lihimidiwe.

Hoja ya haja: Kasi ya “HAPA NI KAZI TU” ni nzuri, ila itekelezwe kwa tahadhari kubwa

$
0
0
Na Mathew Mndeme
Tunamshukuru Mungu kwamba Rais kateua mawaziri na serikali imeanza kazi rasmi. Kila waziri kwa sehemu yake ameonesha kwamba ana hamasa na motisha ya kufanya kazi na kwa mara ya kwanza (huenda tangu nipate akili) tumeshuhudia mawaziri wakianza kazi lisaa limoja baada yakuapishwa huku kukiwa na habari kwamba h
Hii ni njema sana na ni dalili nzuri katika kujenga Tanzania mpya inayothamiawa kunywa hata juice walizoandaliwa kwenye ukumbi wa kuapishwa. 
Ni kazi na utumishi kwa wananchi badala ya wanaopewa uongozi kujiona ni miungu-watu, kuona nafasi zao ni za kula bata, na kujinufainya wenyewe na wanaowazunguka. Ninashawishika kwamba, kwa kiwango cha uwajibikaji walichokiweka Rais na Waziri Mkuu (high standard), hakuna waziri atakayelala wala kushindwa kazi kwa visingizio. Hata wale wanaodhaniwa kwamba “sio wazuri sana” katika nafasi walizopewa, nashawishika kwamba watafanya kazi tu hata kama ni kwa kujifunza upya.

Pamoja na kukiri huku, ninaona hatari mbele iwapo mawaziri hawa, ambao wengi katika nafasi walizopewa ni wanasiasa na sio wataalamu, watafanya maamuzi au kutoa maelekezo kwa haraka, bila kuwa na taarifa sahihi kuhusu jambo husika. 

Ninasema hivi kwa sababu baadhi ya mambo ni ya kitaalamu na yanahitaji taaluma husika katika utekelezaji wake hivyo maelekezo yanapotolewa kwamba yafanyike kwa siku/wiki/miezi kadhaa, ni kinyume kabisa na uhalisia.   
Uwezekano wa kufanyika makosa unatokana na ukweli kwamba wakuu wa idara/taasisi/mamlaka wanaoelekezwa kutekeleza haya maagizo, wengi wao wanaonekana kuna na hofu na kutetemeka na kila maagizo wanayapokea tu na kuitikia bila kuwaonesha viongozi wao kwamba mengine hayatekelezeki kwa muda au mtindo wanaotaka wao. 
Mtaalamu yeyote yule katika nafasi yake, lazima awe na uwezo wa kujiamini na kutetea utalaamu wake ikiwa ni pamoja na kusema ukweli kwa kinachoagizwa mbele ya yeyote. 
Sidhani kama kumweleza Rais, Waziri Mkuu, Waziri, au Naibu waziri, kwamba jambo hili uliloagiza linahitaji kuangaliuwa kitaalamu kabla ya kuchukua maamuzi ni kukosa nidhamu au kutokutii. 
Ni bora ujibu kilicho sahihi uadhibiwe (sina hakika kama watafanya hivi) kuliko kuitikia tu halafu ukashindwa au ukaenda kufanya maamuzi ya ajabu ya kitaalamu. Ngoja nitoe mifano miwili:



Kuendelea kusoma Makala hii BOFYA HAPA

EAC PAINTS CYANIKA TOWN WITH CROSS BORDER FESTIVAL

$
0
0
In a bid to promote stronger cross border interactions and community engagements, the EAC Secretariat, in collaboration with East Africa Local Governments Association (EALGA), the International Republican Institute (IRI) and the German International Development Agency (GIZ), organized a fun-filled sports and cultural festival at Cyanika town on the border of the Republics of Rwanda and Uganda over the weekend. 

Following up on the recommendations of the 21st Sectoral Council of Ministers Responsible for EAC Affairs and Planning meeting in October 2014, which recommended that the activities in the concept note to declare 2015 as the year of the “East African Citizen” be implemented as sensitization programmes; the Festival aimed at engaging ordinary citizens of the EAC Partner States about the privileges available to them, as well as providing a platform on which they can meet, share, have fun and interact as one community under the EAC. 
Local dancers from Rwanda entertaining the festival- goers.

Bringing together over 1,300 festival-goers, the town of Cyanika was painted in an array of sports, including football, volleyball and cycling, cultural expressions and artistry from Uganda and Rwanda. The Festival was graced by Mr. Sam Byibeshyo, the Lord Mayor of Kisoro town, Uganda and Mr. Samuel Sembagare, the Lord Mayor of Burera district-Northern Provence, Rwanda. Other attendees included government officials from the district regional offices in Kisoro, Uganda and Burera, Rwanda, police and immigration officers from the local border authorities, women and young traders. 

“This is an exciting step forward for the Community in getting East Africans more engaged in the integration process,” said Mr. Owora Richard Othieno, EAC’s Principal Information and Public Relations Officer. “We hope that after today, other border communities will initiative similar activities at their border points,” he said. 
Children showing-off their dance moves during the Festival.

The year of the East African Citizen is in line with the EAC Consultative Dialogue Framework which ensures continuous dialogue between the EAC Secretariat, Organs and Institutions, Local governments Civil Society Organizations (CSOs), Private Sector Organizations (PSOs) and other Interest Groups both at the national and regional level.  

BBC SWAHILI DIRA YA DUNIA JUMATATU 14.12.2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images