Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

Waziri na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wawasili rasmi Wizarani baada ya kuapishwa

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha  Wizarani kwa mara ya kwanza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga mara alipowasili Wizarani baada ya kuapishwa Ikulu tarehe 12 Desemba, 2015. Aliyesimama pembeni ni Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Joyce Mapunjo.
Mhe. Balozi Mahiga akikaribishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Simba Yahya.
Mhe. Balozi Mahiga akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa Watumishi wa Wizara Bi. Nsia Paul wakati wa mapokezi yake Wizarani
Naibu Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Suzan Kolimba akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa Watumishi wa Wizara Bi. Tagie Mwakawago mara baada ya kuwasili rasmi Wizarani
Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakimpokea Mhe. Waziri Wizarani. Pichani Mhe. Waziri akisalimiana na Balozi Anisa Mbega, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora. Kwa picha zidi BOFYA HAPA

UZINDUZI WA MELI MPYA YA MV MAPINDUZI II MJINI ZANZIBAR LEO

$
0
0
 Picha ya Meli MV-Mapinduzi II ilipokuwa katika hatua za matengenezo Nchini Korea Kusini
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto)akikata utepe kama ishara rasmi ya uzinduzi wa Meli ya MV-Mapinduzi II katika bandari ya Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar akiwepo na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi (wa pili kulia) Nahodha wa Meli hiyo Abubakar Mzee (kulia) na Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mabaharia waMeli ya MV-Mapinduzi II baada ya uzinduzi rasmi uliofanyika leo katika bandari ya Malindi Mjini Zanzibar,pamoja na kuitembelea kukagua sehemu mbali mbali za meli hiyo akiwa na Viongozi mbali mbali
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na wafanyakazi wa Kike katika  Meli ya MV-Mapinduzi II wakati alipokuwa akifanya ukaguzi na kutembelea sehemu mbali mbali za Meli hiyo akiwa na Viongozi mbali mbali aliofuatana nao baada ya uzinduzi rasmi  uliofanyika leo katika bandari ya Malindi Mjini Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakipata maelezo kutoka kwa Nahodha wa Meli ya MV-Mapinduzi II Abubakar Mzee (katikati) wakati walipofika katika chumba maalum cha mitambo ya kuendeshea meli inapokuwa safarini,maelezo hayo yalitolewa katika shamra shamra za sherehe za uzinduzi uliofanyika leo katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar.

Article 15

Kenya Embassy Celebrates 52 Independece Anniversary

$
0
0
Permanent Secretary at the Minisry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Amb. Liberata Mulamula who was the Guest of Honor delivers a speech at the reception hosted by the Kenya Embassy to mark 52 years of Independence. 
Kenyan Ambassador to Tanzania, H.E Chirau Ali Mwakwere presents a statement at the 52 Independece anniversary reception held at his residence yesterday. 

Invited guests who were Diplomatic Community in the country, government officials and Private Sector follow attentively the statements delivered by the Guest of Honor and Kenyan Ambassador to Tanzania. 

EALA ARE CHAMPS:, …Four time winners, Parliament of Uganda are dethroned, coveted trophy heads to Arusha

$
0
0
Finally, EALA are champs of the Inter-Parliamentary Football tournament. The Regional Assembly late Thursday put to a halt, Parliament of Uganda’s dominance in soccer, beating them 4-3 on penalties.

The regular time score ended 1-1. EALA took the lead through their striker who picked a loose ball from Wycliff Ketto to latch the ball past Goalie Ssekide Dan, sending the crowd in to a frenzy. The match started on a high note with EALA dominating the play.

Hon Martin Ngoga and Hon Taslima Twaha controlled the midfield in the earlier stages of the match. EALA Speaker, Rt. Hon Daniel Kidega could have put the victors ahead in the 17th minute but he shot wide with the Parliament of Rwanda Goalkeeper, Bosabose Emile beaten.
Speaker of the Chamber of Deputies, Rt. Hon Mukabalisa Donatile (third from left)presents the volleyball trophy to members of the Parliament of Rwanda team.

Parliament of Uganda then settled and began making inroads into the EALA defence line marshalled by Peter Asiimwe and Hon Straton Ndikuryayo. Captain Hon Patrick Nsanja missed a sitter after receiving a pass from striker Hon Nsereko Muhammad mid-way as the match progressed.

In the second half, Parliament of Uganda came back a more rejuvenated side following Coach, Tom Lwanga’s pep talk to his charges. Hon Otto Odonga collected the ball from the midfield and beat two defenders to set a through pass to Hon Nsanja Patrick who slotted home the equalizer.
A section of the Parliament of Uganda Netball team celebrate after receiving the winner's trophy award at the Kigali Regional Stadium, Nyamirambo

The match went into extra-time but ended in a draw resulting in a penalty. EALA Goalkeeper saved a crucial penalty taken by Hon Muhammad Nsereko as the match ended 4-3 in their favour.

Dan Ssekide, Edward Mubiru and Hon Nsanja Patrick scored the spot kicks. Hon Gatabazi JMV won the Most Valuable Player’s award after having tied with EALA striker Wycliff Ketto. The rules governing soccer provide that where a Member of Parliament ties with a staff, then the former shall be accorded the prize.

The golden boot (top scorer) went to Hon Patrick Nsanja of Uganda while Parliament of Kenya won the most disciplined team.
Part of the Parliament of Rwanda players lift up their coach moments after beating Parliament of Kenya 2sets to 0 in the finals at the Petite Stade, Amahoro.

Earlier on Parliament of Rwanda scooped position three after beating Parliament of Kenya 4-2 in penalties after a match that ended in a barren draw. It was yet another day when Parliament of Kenya’s strikers failed to find the back of the net. Scorers for the Parliament of Rwanda were Nshimiyimana Ernest, Habimana Augustin, Ngoboka Eric and Ndagijimana Eric.

Senator Isaac Melly and Jorum Baraza scored for Parliament of Kenya while Hon Peter Kaluma and Jillo Yezeli shot wide.Parliament of Kenya also bagged the volleyball men’s tournament, athletics men and the overall trophy in athletics.

In women’s volleyball, Parliament of Rwanda were declared winners beating Parliament of Kenya by 2 sets to 0 (25-20) and 25-16.Parliament of Uganda were declared the champs of the 2015 netball tournament. Parliament of Uganda beat Parliament of Kenya 45-9.

Leading goal shooter, Hon Susan Netasiire won the golden hand after amassing 79 points while Hon Winifred Kiiza was declared the Most Valuable Player.
EALA football coach, Simba Kitwana gestures as he advises the team at half-time. EALA beat Parliament of Uganda 4-3 on penalties to capture the trophy

WAZIRI WA AFYA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu akimjulia hali mmoja wa watoto waliolazwa kwenye wadi ya Watoto, Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza ili kujionea hali ilivyo Hospitalini hapo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu akimsalimia mmoja wa mama aliyelazwa kwenye wodi ya kina mama wajawazito, Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Donan Mmbando.
Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam akisikiliza malalamiko mbalimbali toka kwa wananchi waliofika Hospitalini hapo kupatiwa matibabu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo (hawapo pichani), ambapo amewasihi kutumia lugha nzuri wakati wanapotoa huduma kwa wananchi.
Baadhi ya watumishi wa hospitali ya mwananyamala wakimsikiliza waziri wakati wa majumuisho ya ziara hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu, akiongea na wananchi wanaosubiri kuingia Hospitali ya Mwananyamala kuangalia ndugu zao.

Mpiganaji Haruni Sanchawa wa Global Publishers aagwa Dar, kuzikwa Serengeti Mkoani Mara

$
0
0
MWANDISHI wa habari wa Global Publishers Ltd, Haruni Sanchawa, aliyefariki dunia Desemba 9 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar, ameagwa leo nyumbani kwa mjomba wake Kitunda jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea Mugumu-Serengeti, mkoani Mara, ambapo atazikwa kijiji cha Lemungololi.

Sanchawa alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo, alifariki saa chache baada kuhamishiwa katika hospitali hiyo baada ya kupewa rufaa kutoka Hospitali ya Amana alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.
Marehemu Haruni Sanchawa enzi za uhai wake.Mke wa Marehemu, Adelina Haruni Sancha akiuagwa mwili pamoja na wanaye wawili.Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (wa kwanza mbele ) akiwa na huzuni msibani hapo.Waombolezaji wakiwa msibani.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA MUHONGO ATEMA CHECHE, Awataka TANESCO kufanya kazi

$
0
0
Serikali imeliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuacha mara moja tabia ya kukata umeme bila sababu ya msingi. Agizo hilo limetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Naibu wake, Dkt Medard Kalemani walipofanya ziara ya kushtukiza kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Wizara hiyo. 
 Mara tu baada ya kuapishwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Naibu wake, Dkt Medard Kalemani walifanya ziara hiyo ya kushtukiza kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuzungumza na Menejimenti ya Shirika hilo. 
 Profesa Muhongo alisema wananchi wamechoshwa na tabia ya shirika hilo ya kukatakata umeme bila kuwepo na sababu ya msingi ya kufanya hivyo. 
 “Haiwezekani kila mwaka matatizo ni yaleyale na nyie bado mpo ofisini, hili halikubaliki na halivumiliki. Ninataka tutengeneze historia ya kutatua matatizo ya umeme nchini. Umeme ukiendelea kukatikakatika lazima muondoke,” alisema Profesa Muhongo. 
 Alisema wananchi wanahitaji umeme wa bei nafuu ili waweze kujikwamua na umasikini huku akieleza kwamba ni wakati mwafaka suala hilo likatazamwa kwani bei ya huduma ya umeme ikishuka bidhaa nyingine pia zitashuka. 
 Mbali na hilo, Profesa Muhongo aliwataka watendaji hao kujieleza ni kwanini umeme umekuwa ukikatika mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuwataka waeleze wao kama Menejimenti ya Shirika hilo ni hatua zipi ambazo tayari wamezichukua kuhakikisha hali hiyo haijirudii. 
 Alisema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuifanya Tanzania inakuwa nchi ya viwanda na hivyo inatakiwa kuwa na umeme wa uhakika. Vilevile aliwataka waeleze ni kwa nini huwa wanachelewa kufika maeneo ambayo kumetokea hitilafu hali yakuwa wananchi wanatoa taarifa mara tu wanavyoona hitilafu husika. 
 “Huduma zenu haziridhishi, unakuta transfoma imeharibika ama nguzo imeanguka na taarifa mnaletewa niambieni ni kwanini huwa hamfiki kwa wakati,” alihoji Profesa Muhongo huku akiwasisitiza wabadilike. Profesa Muhongo alisema tangu ametangazwa amepokea simu nyingi kutoka kwa Watanzania wakisikitishwa na hali ya umeme nchini. 
“Nimepokea simu kwa wananchi wa mikoa mbalimbali nchini hususan Arusha na Mwanza wakinilalamikia kuhusu kukosekana kwa huduma ya umeme kwenye mikoa hiyo. Nataka leo hii mnipe jibu tatizo ni nini,” alihoji Profesa Muhongo. 
 Alisema ni wakati sasa viongozi hao wawe wabunifu vinginevyo Serikali haiwezi kuwaelewa kwani kila kukicha tatizo la umeme linaonekana kuendelea kuwa palepale. “Kwa miaka yote mliyofanya kazi hapa Tanesco naona mmeshindwa kubuni mbinu zitakazolipeleka shirika kule ambapo wananchi wanataka. Ninawaagiza kujitathmini kama kweli mnafaa kuendelea na majukumu yenu,” alisema Muhongo. 
Alisema wananchi wamechoka kusikiliza maneno bila kuona vitendo na hivyo kuwaagiza kuhakikisha wanabadilika haraka iwezekanavyo kabla Serikali haijachukua hatua zingine. Akizungumza wakati wa kikao hicho, Naibu Waziri wa wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani alisema kazi kubwa ya shirika hilo ni kuwapelekea wananchi huduma ya umeme na si vinginevyo. Alisema ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imebainisha lengo la Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapelekewa huduma ya umeme na sio ahadi na maneno yasiyokuwa na tija. Aliwaagiza kuhakikisha katika utendaji wao wanazingatia masuala makuu manne ambayo aliyaelezea kuwa ni maadili, uadilifu, uwajibikaji na kuzingatia taaluma badala ya kufanya kazi kwa mazoea. Akizungumzia suala la wizi wa umeme, Dkt Kalemani alisema watumishi wasio waadilifu wa shirika hilo nao wanahusika kwa namna moja ama nyingine na hivyo kuwaagiza watendaji hao kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa mapema iwezekanavyo. 
 “Tubadilike, tutafsiri mipango yetu kwa vitendo, tupange na tutekeleze. Hakuna muda wa kuendelea kuzungumza mipango bila utekelezaji. Wananchi wanahitaji kuona utekelezaji unafanyika,” alisema. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba aliwapongeza viongozi hao kwa kuteuliwa kwao na kuahidi kuendeleza ushirikiano ili kutatua changamoto mbalimbali. “Tumefurahi na uteuzi huu kwani mnaielewa vizuri sekta hii ya nishati; tupo tayari kufanya kazi na tunawahakikishia kuzingatia maagizo yenu bila kuchelewa,” alisema Mramba. 
 Baada ya kuzungumza na menejimenti ya shirika hilo, Waziri Profesa Muhongo alisema kesho atasafiri kuelekea katika Bwawa la Hale ili kujionea hali ilivyo ikiwa ni pamoja na kuzungumza na Watendaji walioko katika maeneo hayo na huku Naibu wake akikutana na taasisi pamoja na makampuni mbalimbali yanayohusika na sekta ya nishati nchini.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya TANESCO. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao chake cha kushtukiza na Menejimenti ya TANESCO. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo.

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni aanza Kutekeleza Ahadi Zake kwa Wananchi wa Jimbo la Chumbuni kwa Ujenzi wa Ukuta Kituo cha Afya Chumbuni

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar na Kamanda wa Vijana Jimbo la Chumbuni Mhe. Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwahutubia Vijana wa UVCCM Tawi la Chumbuni wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu wa Vijana Mhe Shaka Hamdu Shaka kutembelea Jumuiya za Vijama katika Majimbo ya Zanzibar.
Vijana wa CCM wakimsikiliza Mbunge wao wakati wa mkutano ziara ya Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Mhe Shaka Hamdu Shaka,mkutanom huo wa Vijana umefanyika tawi la CCM Chumbuni Karakana
Mbunge wa Chumbuni Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwa na Katibu Mkuu wa Vijana CCM TanZania Mhe Shaka Hamdu Shaka wakielekea katika ujenzi wa Taifa wa kuchimba msingi wa ukuta wa Kituo cha Afya cha Chumbuni ikiwa ni moja ya ahadi za Mbunge kukiimarisha Kituo hicho kwa kuaza ujenzi wa Ukuta ikiwa nin hatua za mwazo za kukiimarishas kituo hicho kutoa huduma bora kwa wananchi wa jimbo la chumbuni na jirani zao.
Mhe Mbunge AMJAD akichimba msingi wa ujenzi wa ukuta wa kituo hicho cha Afya Chumbuni Zanzibar.

Mhe Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Pondeza AMJAD akishgiriki katika ujenzi wa taifa wa uchimbaji wa msingi wa kituo cha Afya Chumbuni ikiwa ni ahadi yake ya kujenga ukuta huo kukiweka katika mazingira mazuri kituo hicho cha Afya Chumbuni kwa ajili ya kutowa huduma bora. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

WAZIRI KITWANGA AKARIBISHWA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI MARA BAADA YA KUAPISHWA IKULU LEO

$
0
0


 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kulia) akimkaribisha wizarani Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga mara baada ya kuapishwa Ikulu, jijini Dar es Salaam leo.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akimkaribisha Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, ndani ya ofisi ya waziri huyo iliyopo Mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akisaini kitabu cha wageni kilichopo ndani ya ofisi yake, mara baada ya Waziri huyo mpya kuingia ndani ya ofisi hiyo baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kushoto) akimfafanulia Waziri mpya wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kulia), shughuli mbalimbali zinazofanywa na wizara hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo. Tukio hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, mara baada ya Waziri huyo kuapishwa Ikulu leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akijadiliana na watendaji wa wizara hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya wizara hiyo, mara baada ya Waziri huyo kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Wanne kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), John Minja, Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi (D/IGP), Abdurahman Kaniki na Kamishina wa Fedha na Utawala wa Idara ya Uhamiaji, Piniel Mgonja (hayupo pichani). 
Picha zote na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.


Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Nafisa and Gulam Punjani Visited Izaas on 4thdec 2015

Hepi Besdei ya KUZALIWA mtoto NAZIR (a.k.a KALAMAGI) HAMIS KIKWAPPE

$
0
0
Hapa anaonekana Nazir Hamis akimlisha Keki mdogo wake Sameer wakati wa sherehe ya kuzaliwa ambapo Nazir amefikisha miaka minane a.k.a 8 Oclock. Allah ampe maisha marefu na amuwezeshe kufanikisha ndoto zake.

Kenya Embassy Celebrates 52 Independece Anniversary

$
0
0
Permanent Secretary at the Minisry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Amb. Liberata Mulamula who was the Guest of Honor delivers a speech at the reception hosted by the Kenya Embassy to mark 52 years of Independence.
Kenyan Ambassador to Tanzania, H.E Chirau Ali Mwakwere presents a statement at the 52 Independece anniversary reception held at his residence yesterday.
Invited guests who were Diplomatic Community in the country, government officials and Private Sector follow attentively the statements delivered by the Guest of Honor and Kenyan Ambassador to Tanzania.
Permanent Secretary at the Minisry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Amb. Liberata Mulamula (L) and Ambassador of Kenya to Tanzania, H.E Chirau Ali Mwakwere raise their glasses in a toast to the health of the Presidents of Tanzania and Kenya and prosperity of these two nations. For more CLICK HERE

SIMU TV: HABARIK KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

updates za dada Joyce Richard Mwambepo wa mbeya aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuvunjika miguu ajalini

$
0
0
Ankal akiwa wodini kumtembelea dada Joyce 
 Dada Joyce alipowasili Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wiki iliyopita

Dada Joyce akiwa wodini MOI

Ndugu Wasamaria Wema,
Tunapenda kutumia fursa hii kuwashirikisha tena habari ya kusikitisha kuhusu dada Joyce Rishard Mwambepo (pichani akiwa na mwanaye wa miaka 4, na miguu yake iliyopooza) mkaazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa miaka 27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na huyo mwanaye wa miaka 4.
Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana wa 2014 dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo dereva hakusimama kumsaidia. Kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa  Mbeya ambako alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu, kwa kukosekana nyenzo pamoja na pesa  za kumfanyia uchunguzi.
Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili,  hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa tena Mbeya baada ya kukosa pesa  za vipimo na matibabu.
Hadi  Msamaria mwema na Mpiganaji Deo Kakuru anakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake ambaye ni mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wake wote wawili kufariki dunia. 
Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye huyp na bibi yake.  Inasikitisha.
Hivyo Deo Kakuru, kwa msaada mkuwa wa michango ya Wasamaria Wema,  amefanikiwa kumsafirisha dada Joyce kwa Fast Jet kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya  hadi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha MOI jijini Dar es salaam ambako alipokelewa na kulazwa katika jengo jipya liitwalo Wodi ya Magufuli ghorofa ya tatu wodi namba 2.
--------------------------------------
UPDATES:
Baada ya Deo Kakuru kuweka mitandano tatizo la dad Joyce, Wasamaria Wema kadhaa wakajitokeza kumsaidia.  Hatuna uhakika kwamba wote wangependa majina yao yawekwe hadharani, Ila tunapenda hadi sasa kukiri upokeaji wa Tshs:
1. 505,000/-
2. 50,000/-
3.100,270/-
4. 10,000/-
5. 100,000/-
6. 500,000/- (ahadi ya uhakika)
7. 500,000/- 
7. 800,000/-  (Kulipia gharama za vipimo vya CT Scan Regency Hospital mgonjwa atapofikishwa Dar es salaam).

Hivyo ndiyo kusema jumla ya Tshs. 2,565,270/-  tayari zilikusanywa kumsaidia dada yetu huyu anayeteseka. Kwa niaba ya mgonjwa tunashukuru sana kwa msaada huo, hana cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mola mzidishiwe pale mlipopungukiwa. KUTOA NI MOYO.

Aidha, kwa kiasi kilichopatikana tayari dada Joyce ameshafanyiwa vipimo vya MRI  Alhamisi  iliyopita na hivi sasa yanasubiriwa majibu siku ya Jumatatu ambapo baadaye Jopo la Madaktari Bingwa litaka na kuamua nini kifanyike kimatibabu. Tunashukuru madaktari na watumishi wote wa MOI kwa kuhitimisha hilo, nasi tunaendelea kuwaomba waendelee na huduma hiyo hadi dada Joyce atapopata matibabu.
Vile vile tunamshukuru sana Msamaria Mwema Mama Rozi aliyejitolea kumhudumia dada Joyce pale wodini ambako mama yake mzazi amelazwa na ana matatizo karibu sawa na ya dada yetu. Bila kuchoka mama Rozi amekuwa akimletea chakula na vinywaji dada Joyce kila siku na kumfanyia huduma za usafi kila siku. Ubarikiwe sana Mama Rozi.
Shukurani pia ziwaendee wasamaria wema wengine pamoja na wadau ambao baada ya kuguswa na matatizo ya dada Joyce wamekuwa wakimtembelea hapo wodini na kumfariji. Asanteni sana.

Wito wetu tunaomba tuendelee kumsaidia kwa hali na mali dada Joyce kwani mara baada ya majibu ya vipimo yatapotoka Jumatatu, ni dhahiri kutakuwa na mahitaji zaidi katika matibabu yake. 

Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal anaendelea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha MOI. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba+255 754 271266 kwa jina la Ankal.
Mratibu mwenza Deo Kakuru naye anaendelea kusaidia kwa kumtunza bibi yake Joyce na mwanae mwenye umri wa miaka 4 huko Mbeya.
Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema




TASWIRA MBALIMBALI KATIKA USIKU WA TUZO YA MWAJIRI BORA WA MWAKA 2015

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kikombe, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na utawala wa benki ya CRDB, Bi Ngalija wakati wa kutoa zawadi katika hafla hiyo. Kutokea (kulia) ni Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Kaarstad, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Florens Turuka, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki na Makamu Mwenyekiti wa ATE, Zuhura Muro. 
Mwakilishi wa Kampuni ya Maswala ya Kisheria ya Yakubu & Associates Chamber, Dkt. Timoth Kyepa akipokea tuzo kutoka kwa kwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa wakati wa kuhitimisha hafla hiyo. Kulia ni Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Kaarstad, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Florens Turuka, Katibu Mkuu wa TUCTA, Mwkt wa ATE, Mh. Almasi Maige, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, Makamu Mwkt wa ATE, Zuhura Muro, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE na Dkt. Aggrey Mlimuka.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza Bwana, Norman Msigala wa CCBRT baada ya kutoa hotuba nzuri katika hafla hiyo. 
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Florens Turuka, akiongea katika hafla hiyo. 

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI LEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii na Jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri , leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashantu Kijaji katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Lameck Nchemba katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimwapisha waziri wa Sera, Bunge, Kazi ,Vijana,Ajira na Walemavu, Dkt. Abdallah Possi katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, na manaibu Waziri leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

PICHA ZAIDI YA TUKIO HILO BOFYA HAPA

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AAPISHA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRi

Tano Bora ya Hoteli za Kitalii Tanzania

$
0
0
Ukiachana na hifadhi za taifa zitakazokufanya usichoke kutembelea miji na mikoa mbali mbali ndani ya Tanzania, ni uwepo wa hoteli za kifahari zenye utofauti wa kipekee na hoteli za nchi nyingine. 

Jovago Tanzania, wadau wanaohusika na masuala ya Hoteli kimataifa, wanapenda kukuorodheshea tano bora ya hoteli zilizo kwenye chati ya kukupa mandhari zuri ya kiutalii wa kifahari hapa Tanzania. 
Manta Resort-Pemba: Ni hoteli ya kipekee yenye chumba cha kulala chini ya bahari ya Hindi. Hoteli hii inakupa mandhari ya peponi utakapo jaribu kukaa ndani ya chumba hicho, hii ni moja ya utalii ambao hutaweza kuusahau utembeleapo eneo hili kisiwani Pemba.

Essque Zalu Zanzibar: Essque Zalu ipo Zanzibar, ni hoteli bora ya kimataifa yenye viwango vya huduma kwa hali ya juu (five star). Ni sehemu pekee itakayokupa historia nzima ya Zanzibar na fursa ya kutembelea fukwe kubwa nzuri zinazopatikana  maeneo ya Nungwi. Imejengwa kwa nakshi za kishwahili na za kisasa za kuvutia.

1      Singita sasakwa Lodge –Serengeti: 

Eneo lake ni zaidi ya ekari 300,000. Hoteli inavyumba vilivyojengwa kwa mandhari ya kitamaduni za kiafrika,  na uwezo wa  kuona madhari ya hifadhi ya taifa na mbuga ya wanyama Serengeti. 

1     Park Hyatt –Zanzibar: 

 
Ni hoteli inayokupa mandhari kamili na historia ya Zanzibar, hoteli imezungukwa na bahari ya Hindi  katika eneo la kihistoria la Stone town. 

      Hyatt Regency- Dar es Salaam:Hii ni hoteli yenye kiwango cha juu cha ubora wa kimataifa (Five star), ina uwezo wa kubeba watu wengi zaidi ya hoteli yoyote Dar es Salaam. Ina mandhari nzuri ya bahari ya Hindi, na vyumba vilivyojengwa kwa teknolojia ya hali ya juu, inafaa zaidi kwa masuala ya makazi  kwa mikutano ya  kibiashara pia inakupa fursa ya kutembelea  sehemu tofauti tofauti zilizo  katikati ya mji wa Dar es salaam.
 

Dj Bonny Love alivyokonga nyoyo za mashabiki wa burudani katika usiku wa Heart & Soul kiota cha maraha cha Raphsody ndani ya Jengo la Viva Towers jijini Dar

$
0
0
Mkali wa magoma hapa nchini na nje, Dj Bon Love akifanya yake katika Usiku wa Heart & Soul uliofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye kiota kinachobamba zaidi hapa mjini cha Raphsody, ndani ya Jengo la Viva Towers katikati ya Jiji la Dar. Dj Bon Love na maDJ wengine wakali hukutana pamoja kwenye kiota hicho ili kukonga nyoyo za wapenda Burudani kutoka maeneo mbalimbali.Usiku huo uliwezeswa kwa Udhanimi Mkubwa wa Kilaji ya Heineken.
Baadhi ya Wadua wa Burudani wakiwepo DJ. Venture na Mwanalibeneke Haki Ngowi wakiwakilisha katika Usiku wa Heart & Soul.
 
Mmoja wa maDJ wanaopiga katika Usiku wa Heart & Soul akifanya mambo yake.

Dj Bonny Luv na mdau
 Mdau Othman Michuzi (kulia) na marafiki wengine nao hawakutaka kupitwa  Usiku wa Heart & Soul ndani ya kiota pendwa cha Raphsody, Jengo la Viva Towers katikati ya Jiji la Dar.

Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>