Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

TAARIFA KWA UMMA TOKA NMB KATIKA SIKU YA UHURU DAy


TEASER JOTO LA ASUBUHI LA 93.7 EFM JUMATANO DESEMBA 9, 2015 KUANZIA SAA 12 ASUBUHI

UTARATIBU WA KUSHIRIKI ZOEZI LA KUFANYA USAFI SIKU YA TAREHE 9 DISEMBA, 2015 MKOA WA DODOMA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alitoa agizo la kumtaka kila mtu kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya Uhuru tarehe 9 Disemba, 2015 kwa kushiriki zoezi la kufanya usafi wa mazingira. 
Katika Mkoa wa Dodoma, zoezi hilo litahusisha kazi za usafi wa makazi na maeneo ya shughuli mbalimbali, kufagia barabara za lami na vumbi, kufyeka nyasi kandokando mwa barabara na katika maeneo ya wazi na jamii, kuokota  takataka  (mifuko ya Rambo) na kuzibua mitaro ya maji ya mvua kama ipo katika  eneo husika kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana. 
Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kupitia Ofisi zao ndio waratibu wa zoezi la usafi kwenye Wilaya husika. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, ameainisha maeneo ambayo taasisi mbalimbali za Mkoa wa Dodoma zitayashughulikia kufanya usafi Mjini Dodoma (Orodha imeambatishwa). 
Kutokana na uhaba wa vifaa vya kufanyia Usafi. Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma anashauri taasisi mbalimbali zitakazohusika na zoezi la usafi wa mazingira, ziwe na vifaa vyake vya kufanyia usafi. 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma anasisitiza zoezi la usafi kwa taasisi, lizingatie maeneo yaliyotajwa kwenye  jedwali lililoambatishwa na Uongozi wa Serikali Mkoa wa Dodoma unamtaka kila mwananchi na taasisi zilizopo Dodoma kushiriki kikamilifu katika usafi huu.


Imetolewa na:

OFISI YA MKUU WA MKOA

DODOMA


Disemba 8, 2015

Jeshi la Polisi laja na mpango wa kuboresha usalama kwenye jamii.

$
0
0
Na Tamimu Adam, Jeshi la Polisi.

Jeshi la polisi nchini, limeanzisha mpango wa   kuboresha usalama wa jamii  nchi nzima ambao unalenga  kuboresha  utoaji wa huduma bora kwa wananchi, kuboresha mawasiliano  ya ndani na nje ya Jeshi la polisi kwa kuwashirikisha wadau  mbalimbali wa usalama 
ambapo mpango huo utaanza kutekelezwa katika mkoa wa kipolisi kinondoni  ambapo lengo lake ni  kupunguza uhalifu kwa asilimia kumi ifikapo mwaka 2019.


Akihitimisha  maabara ya mpango huo iliyofanya kazi kwa wiki sita, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi  Abdulrahmani  Kaniki  (pichani) aliwahakikishia  washiriki wa maabara ya kuboresha usalama wa jamii, kuwa Jeshi la polisi litatekeleza  kwa vitendo mapendekezo yote yaliyotokana na maabara hiyo, kwani baadhi ya mapendekezo   hayahitaji bajeti  hivyo utekelezaji wake utaanza mara moja.

 “Kazi iliyofanywa  na maabara hiyo ni kubwa  na umuhimu katika kuboresha usalama wa jamii katika nchi yetu hivyo mapendekezo yote ni lazima yafanyiwe kazi ili kuleta mafanikio chanya”. Alisema Kaniki.

Aliongeza  kuwa mpango huo umeanzia  katika mkoa wa kipolisi kinondoni na baadaye utaenea nchi nzima, ambapo alizitaja sababu zilizopelekea kuanza na kinondoni kuwa ni pamoja na  kuongezeka kwa makosa,  kupanuka mji, idadi kubwa ya watu na uwepo na shughuli nyingi za kiuchumi ukilinganisha na maeneo mengine.

Naye, Mtendaji mkuu wa  ofisi ya Rais ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi (PDB), Omari Issa alisema mpango huo wa uboreshaji wa usalama wa jamii ambao unaanza na mkoa wa Kinondoni uliandaliwa kwa kuwashirikisha wadau kutoka taasisi mbalimbali za serikali na kijamii ambao kwa pamoja walishirikiana kwa pamoja katika kuangalia namna ya kuboresha usalama wa jamii  ili kuwezesha jamii  kuwa salama.

Aliongeza kuwa mpango wa matokeo makubwa sasa unahitaji kuzingatia vitu vikuu vitatu katika utekelezaji wake ambavyo ni kujiwekea vipaumbele, nidhamu ya utekelezaji na uwajibikaji hivyo alisema hana wasiwasi na Jeshi la Polisi katika utekelezaji wa mpango huo hapa nchini.

Mpango wa uboreshaji wa usalama  wa jamii unalenga  kuboresha  na kurahisisha huduma mbalimbali zinazotolewa na Jeshi la polisi ikiwemo kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa askari, usimamizi wa rasirimali watu na vifaa na kuweka mikakati ya kuwashirikisha wadau wa kada mbalimbali ndani  ya jamii katika kuboresha usalama wa jamii.


 Maabara hiyo ya  kuboresha usalama wa jamii ripoti yake inatarajiwa kukabidhiwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi hivi karibuni ili kuanza utekelezaji wake kwa kuanza na mkoa wa kipolisi wa Kinondoni.

MISS TANZANIA Lorraine at Miss Universe 2015

$
0
0
 Lorraina C. Marriot, Miss Universe Tanzania 2015 poses for a photo at The Venetian in Las Vegas, Nevada on Monday, December 7th. The 2015 Miss Universe contestants are touring, filming, rehearsing and preparing to compete for the DIC Crown in Las Vegas. Tune in to the FOX telecast at 7:00 PM ET live/PT tape-delayed on Sunday, Dec. 20, from Planet Hollywood Resort & Casino in Las Vegas to see who will become Miss Universe 2015. HO/The Miss Universe Organization
Keywords: Miss Universe 2015, The Venetian, Grand Canal Shoppes, The Palazzo, Canaletto Restaurant
Photographer: Matt Petit

SERIKALI YA JPM NI NOMA! UKIBEEP TU, WANAPIGA! DKT MPANGO ATINGA TRA SAMORA BAADA YA MWANANCHI KUTUPIA UJUMBE MTANDAONI

$
0
0
Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA Dkt. Mpango (kushoto), akizungumza na walipa kodi hao kwenye tawi la TRA, barabara ya Samora jijini Dar es salam leo Desemba 8, 2015.  
KUNA ule msemo wa watu wa mjini, "Uki-beep, napiga" na kweli leo hii Desemba 8, 2015 pale Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA, barabara ya Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, mlipa kodi mmoja alitupia ujumbe kwenye mtandao wa kijamii akiomba wataalamu wa IT wa TRA, wafike haraka kwenye ofisi zao za TRA Barabara ya Samora kwani mitambo ya ku-print Motor Vehicles License ime-collapse", na watu wamekaa tu wasijue la kufanya. 
Ilichukua kama dakika 15 au 20 hivi, watu wawili waliovalia suti maridhawa na dada mmoja "aliyeshiba", walitinga kwenye ofisi hizo, na kukuta walipa kodi wakiwa wamejazana kwenye mabenchi wakijipepea tu, kutokana na joto kali. 
Mmoja wa watu hao waliovaia suti, alianza kuwauliza walipa kodi, "Jamani vipi huduma za hapa mnaridhika nazo."? Aliuliza mmoja wao. 
Walipa kodi hao kwanza walimtazama, na mmoja "akajilipua", hapana haturidhiki nazo, hapa unapotuona tumeshakaa sana, huduma hakuna tunaambiwa mtandao haupo, tumeshindwa kuchapishiwa stika za malipo ya kodi ya barabarani. 
Mwingine akasema, hata hali ya hewa humu ndani kama unavyoiona joto kali, hakuna viyoyozi, na tumekuja kulipa kodi hii ni sawa...?? akahoji mlipa kodi huyo. 
Baada ya majibu hayo, Mlipa kodi mmoja aliibuka na kuwaambia wenzake, jamani semeni huyo ndiye bosi mpya wa TRA, "tiririkeni" yaani semeni, na hapo malalamiko yakawa mengi.
Naye bosi huyo ambaye hakuwa mwingine bali  Dkt. Philip Mpango, ambaye hivi karibuni,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, alimteua kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa TRA, akiziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Kamishna Rished Bade, akawajibu, nimeyapokea malalamiko yenu, na ndiyo maana mmeniona niko hapa.
"Nilipokea ujumbe kutoka kwa mlipa kodi akilalamika kuwa hapa kwenye tawi letu huduma zimesimama. Nikaona nfike kujua nini kimetokea", alisema Dkt. Mpango akiwaambia walipa kodi hao ambao walionekana kufurahishwa na maneno hayo.
Wakati akiwaeleza hayo, mitambo hiyo ghafla ikaanza kufanya kazi na waliokuwa jirani na madirisha walianza kuitwa mmoja mmoja na kupatiwa huduma.
Hiyo ndiyo serikali mpya ya awamu ya tano yenye kauli mbiu "Hapa Kazi Tu". Hakuna kulala kila mtu anapiga kazi tu.
 "Figisu figisu" ya kile wafanyakazi wa hapo waliwaambia wateja wao kuwa "system iko down", yaani kwa maana ambayo wao wamezoea kuwaambia wateja kuwa mtandao wa computer haufanyi kazi kwa hivyo walipa kodi kibao waliokuwepo kwenye ofisi hizo, walilazimika kukaa tu kwenye mabenchi wakimuomba Mungu mtandao huo upone ili waweze kupata "stika" za magari yaani Motor Vehicles License.

Habari njema: Malipo ya vipimo vya MRI yafanyika kutoka Michango ya wasamaria wema yaliyofanikisha Dada Joyce wa Mbeya kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi

$
0
0
Ndugu Wasamaria wema,


UPDTAES ZA LEO
Kwa kutumia michango ya wasamaria wema, leo tayari Ankal ameshalipia malipo kwa ajili ya vipimo vya MRI kwa dada Joyce yanayotarajiwa kufanyika Alhamisi hii ama Ijumaa. Baada ya matokeo ya vipimo vyake jopo la madaktari  bingwa litakaa na kuamua nini cha kufanya kumsaidia dada Joyce. Hivyo tuendelee kumsaidia kwa hali na mali pamoja na dua.

 Kama umeguswa na unataka kutoa msaada  unaweza kuwasiliana na Ankal kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba+255 754 271266 kwa jina la Ankal.
AU mratibu-mwenza  Deo Kakuru Msimu

Pia unaweza kuwasiliana moja 
kwa moja na dada Joyce kwa namba hiyo na atafurahi


ukimsalimia ama hata kumtupia kitu kwenye Mpesa yake.
MPIGIE +255 768 084897
-----------------------------------------
HISTORIA YA MATATIZO YA DADA JOYCE
Ifuatayo ni historia fupi ya matatizo ya dada Joyce Richard Mwambepo, mkaazi wa kitongoji cha Sinde jijini Mbeya mwenye umri wa miaka 27 ambaye anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na mwanaye mwenye umri wa miaka 4.
Ikumbukwe kuwa mwezi wa nne (April) mwaka jana dada huyu aligongwa na gari ambalo dereva wake hakusimama kumsaidia. Wasamaria wema walijitokeza na kumpelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya ambako  alikaa wodini kwa miezi mitatu bila kupata matibabu kwa kukosa fedha. 

Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili,  hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi lakini nako huko pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya kwa  kukosa pesa za matibabu.
Akajitokeza mwanahabari Deo Kakuru wa Mbeya ambaye baada ya kumgundua alitoa taarifa za dada Joyce katika mitandao mbalimbali, ambapo wasamaria wema wengi  wa ndani na nje ya nchi  wakaguswa na kuchangia.
Mungu mkubwa, kiasi kilichopatikana ( 3.2m/-) kimewezesha dada Joyce kupelekwa Dar es salaam toka Mbeya kwa ndege ya Fast Jet Alhamisi iliyopita na moja kwa moja kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alipokelewa katika kitengo cha mifupa cha MOI na kupatiwa kitanda katika wodi mpya ijulikanayo kama Wodi ya Magufuli, ghorofa ya tatu wodi namba 2  chumba cha kwanza kulia. 
Cha kufurahisha ni kwamba Joyce aliweza kukaa kwenye kiti cha kusukumwa na hata kwenye ndege aliketi kama kawaida, zoezi ambalo hata yeye anasema limemsaidia kwani kwa mara ya kwanza hivi sasa ganzi miguuni inapotea taratibu na ukimgusa anahisi mguso tofauti na ilivyokuwa awali.

Daktari bingwa ameshaonana naye na kumpa matumaini ya kupona, hasa sehemu ya chini ya uti wa mgongo wake ambao inasemekana una matatizo yaliyopelekea kubana  mishipa ya fahamu na kufanya miguu ipooze. Zoezi linalosubiriwa kwa sasa ni kupatiwa vipimo vya MRI ili kubaini kiufasaha tatizo lake na hatimaye kupatiwa matibabu. Zoezi hili linatarajiwa kufanyika wakati wowote kuanzia sasa.
Mpiganaji Deo Kakuru amesharejea Mbeya na kijiti cha kumwangalia dada Joyce amekabidhiwa Ankal ambaye anaomba Wasamaria wema waendelee kumuombea na kumsaidia kwa hali na mali dada huyu ambaye ni yatima.



Kwa bahati njema Ankal amekutana na kuongea na Msamaria mwingine aitwaye Mama Rozi ambaye  anamuuguza mama yake mzazi aliyelazwa  wodi moja na dada Joyce. Msamaria huyu amekubali kumsaidia dada Joyce kwa chakula na pia kumsaidia usafi maana hapo kitandani alipo hawezi kuondoka...Hivyo mambo yote anamalizia hapo hapo.
Mungu kweli ni mkubwa. Dada Joyce anatabasamu na kuongea vizuri tu. Anatoa shukurani sana kwa wote waliomsaidia na wanaoendelea kumsaidia. Anasema hana cha kuwalipa ila kusema ASANTE SANA na anamwomba Mola Muumba awazidishie pale patapopungua. Ameomba anayeweza kumtembelea afanye hivyo na atafurahi sana maana hana ndugu hapa Dar es salaam zaidi ya Ankal.
Pia anawashukuru sana madaktari waliomhudumia vyema katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ambao amesema hatowasahau kwa msaada wao mkubwa waliompa wakati wa kupata ajali na huu.


Dada Joyce pia anawashukuru sana Dkt Hellen na Dkt Mtei ambao amesema wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba huduma anazopata hapo MOI ni zitamsaidia kupata matibabu yake. 

Hati ya malipo kwa ajili ya vipimo vya MRI kwa dada Joyce iliyotolewa leo baada ya kulipiwa. Inatarajiwa atapimwa Alhamisi ama Ijumaa kabla jopo la Madaktari kuamua nini cha kumfanyia.
 Mpiganaji Deo Kakuru akiwa na dada Joyce ndani ya FastJet wakitoka Mbeya kuelekea Dar es salaam Alhamisi iliyopita.
 Dada Joyce akiwa ameketi kwa utulivu kwenye siti yake ndani ya ndege wakati wa safari ya kutoka Mbeya kuelekea Dar es salaam.
 Mpiganaji Deo Kkuru akiwa na dada Joyce mara baada ya kuwasili  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam
 Msamaria mwema Mama Rozi akimhudumia dada Joyce akiwa kitandani kwake Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa cha MOI katika wodi ijulikanayo kama Wodi ya Magufuli ghorofa ya tatu

Dada Joyce akiwa wodini Moi


KAMATI KUU YA CCM YAIPONGEZA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KWA UTENDAJI WAKE


SERIKALI YATOA UFAFANUZI KUHUSU NAMNA YA KUADHIMISHA SIKU YA UHURU

DIRA YA DUNIA JUMANNE 08.12.2015

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETINI

$
0
0
Magufuli kila kona duniani. Wengi waguswa na utendaji kazi wake, wataka viongozi wa Afrika kumuiga.
SIMU.TV:  Siku 35 za Magufuli. Vigogo 78 wafyekwa, kasi yake yawatia wengi tumbo joto. CCM yampa baraka kutumbua majipu; https://youtu.be/mZba3DzjuvU
SIMU.TV:  Geti namba 5 kichaka ufisadi bandari. Mgombea CUF Mbagala ashinda pingamizi.  Daktari wa Tanzania apeta kimataifa; https://youtu.be/lSTzVW2uL08  
SIMU.TV:  Yanga kama Magufuli. Azam yaipiga mkwara Simba. SECAFA inahitaji mipango mipya. Stars under 15 yarejea Dar; https://youtu.be/-te0uv3RjP4  
SIMU.TV:  Pata habari motomoto zilizotawala katika magazeti ya leo Disemba 9.2015 hapa Simu.tv;https://youtu.be/EpSCvEEWeDM

SSRA emerged the First winner in the National Board of Accountants and Auditors (NBAA) - Best presented Financial Statements Competitionusing IPSAS

$
0
0

THE Social Security Regulatory Authority (SSRA) has emerged the First winner in the National Board of Accountants and Auditors (NBAA) Best presented financial statements competition. SSRA competed in the International Public Sector Accounting Standards (IPSAS) category with other public entities using IPSAS. 

It’s the fourth year consecutively since SSRA started participating in the competition and throughout the period the Authority became number one for the all four years. It’s the Authority’s pleasure to be associated and acknowledged in this prestigious and highly recognized best financial statements competition.
SSRA Board Chairman( at the center) with SSRA staff in a jovial mood after emerging theFirst winner in the National Board of Accountants and Auditors (NBAA) Best presented Financial Statements Competition from left Ms. Lightness Mauki Director of  Compliance and Registration; Mr. Emil Mkaki – Finance Manager; Mr. Mohamed Nyasama –Director of Finance & Administration & Mr. Peter Mbelwa – Chief Internal Auditor.
SSRA Director of Compliance & Registration Ms. Lightness Mauki receiving award trophy from   Dr. Hamis Mwinyimvua Deputy Permanent Secretary- Ministry of Finance looking from left is Mr. Peter Mbelwa – Chief Internal Auditor.
SSRA Director of Compliance & Registration Ms. Lightness Mauki receiving award trophy from   Dr. Hamis Mwinyimvua Deputy Permanent Secretary- Ministry of Finance.
SSRA Director of Finance & Administration Mr. Mohamed Nyasama in a jovial mood holding a trophy with Ms. Lightness Mauki – Director of Compliance and Registrations.
SSRA Director of Finance & Administration Mr. Mohamed Nyasama in a jovial mood holding a trophy with Ms. Lightness Mauki – Director of Compliance and Registrations.

WANANCHI, WAFANYA BIASHARA, WANASIASA, NA WANAFUNZU WA JIJI LA MBEYA WATIMIZA WAJIBU WA KUFANYA USAFI KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA JIJI LA MBEYA.

$
0
0
Wananchi, Wafanyabiashara, Wanasiasa na Wanafunzi wa Jiji la Mbeya waitikia wito wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kufanya Usafi katika Maeneo Mbalimbali ya Jiji la Mbeya kama waonekanavyo hapo na zifuatazo hapo chini ni Taswira Mbalimbali za Jinsi hali ya Mambo ilivyo kuwa katika baadhi ya Maeneo ya Jiji la Mbeya. 
Mitaa Mbalimbali ya Jiji la Mbeya imepokea vyema wito wa Rais wa Awamu ya Tano juu ya agizo la kufanya Usafi Nchi  nzima kwa siku hii ya leo
PICHA ZOTE NA MR.PENGO GLOBU YA JAMII MBEYA. AU

FILAMU MPYA 'GOING BONGO' KUZINDULIWA RASMI IJUMAA CENTURY CINEMAX MLIMANI CITY JIJINI DAR

$
0
0
FILAMU mpya inayokwenda kwa jina la ‘Going Bongo’ ambayo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa filamu ndani na na nje ya nchi  imekamilika  sasa kuzinduzliwa rasmi kesho  Ijumaa kwenye ukumbi wa sinema wa Century Cinemax uliopo Mlimani City, Jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi huo mtunzi na muandishi ambaye pia ameisimamia  katika kuitengeneza na kuigiza filamu hiyo, Ernest Napoleon alisema, 

“Naamini kuonyeshwa kwa filamu hii kutaandika historia muhimu kwenye tasnia ya filamu  nchini Tanzania”“Tunashukuru kupata  nafasi hii kwani tunategemea tutaweza kubadilisha utamaduni wa kuangalia filamu haswa pale filamu nyingi za hapa nyumbani zikipana nafasi ya kuonyeshwa kwenye majumba ya majumba ya sinema” alisema.

Filamu hiyo ambayo mpaka sasa imetwaa tunzo kadhaa, ina maudhui ambayo yanonyesha maisha ya Daktari aliyejitolea kwenda kufanya huduma  nchini Tanzania kwa muda wa  mwezi mmoja.
Filamu hii imerekodiwa   majiji makubwa mawili ambayo ni Dar es Salaam na California  Marekani, inaelezea sehemu ya maisha ya kweli aliyonayo Daktari  mwenye asili ya nchini Ufaransa  aliyeondoka Ulaya na kwenda kufanya kazi  barani Afrika. 

Kati ya tuzo ambazo filamu hii imeshinda ni pamoja na, Filamu Bora Afrika Mashiriki katika tamasha la Zanzibar International Film Festival (Ziff)  na Filamu Bora ya Kimataifa katika tamasha la ‘Black Entertainment Fashion’,  ‘Film and Television Awards’  (BEFTA).


Amewaomba mashabikmi wa filamu kujitokeza kwa wingi kesho kwenye uzinduzi huo ambapo tiketi zimeshaanza kuuzwa Century Cinemax Theaters Mlimani City.

MBUNGE WA JIMBO LA MTAMA NAPE NNAUYE ASHIRIKI KUFANYA USAFI NA WANANCHI JIMBONI KWAKE

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Yahaya Nawanda (mwenye fulana nyeusi) akishiriki usafi pamoja Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye na wakazi wa jimbo hilo ikiwa sehemu ya kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli inayowataka wananchi kushiriki usafi wa mazingira kwenye siku ya kilele cha kusheherekea uhuru wa Tanzania, Desemba 9.
Usafi ukiendelea Mtama ambapo wananchi wamesafisha mitaro yote pamoja na maeneo ya sokoni.

Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akishiriki kufanya usafi jimboni kwake ikiwa sehemu ya kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli inayowataka wananchi kushiriki usafi wa mazingira kwenye siku ya kilele cha kusheherekea uhuru wa Tanzania, Desemba 9.
Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa jimbo lake waliojitokeza kushiriki usafi.


Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akishiriki kufanya usafi jimboni kwake ikiwa sehemu ya kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli inayowataka wananchi kushiriki usafi wa mazingira kwenye siku ya kilele cha kusheherekea uhuru wa Tanzania, Desemba 9.
Wakazi wa jimbo la Mtama wakijitokeza kufanya usafi.
Wakazi wa jimbo la Mtama wakishiriki usafi.

WAFANYAKAZI HOSPITALI YA MUHIMBILI WAFANYA USAFI

$
0
0

VE1 
Baadhi ya Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakifanya usafi leo nje ya jengo la Kibasila akiwamo Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithnashery Jamaat ya jijini Dar es Salaam, Dewji Azim (katikati).
VE2 
Kushoto ni Mwanasheria wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Veronica Hillary, Mkuu wa Idara ya Upasuaji,  Dk Julieth Magandi, Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario na Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithnashery Jamaat ya jijini Dar es Salaam, Dewji Azim wakifanya usafi leo Desemba 9 ambayo ni siku ya kuadhimisha Uhuru wa Tanzania. Usafi huo umefanyika katika Jengo la Kibasila.
VE3Mkurugenzi wa Upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk John Kimario akisomba takataka ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la Rais John Pombe Magufuli kwamba leo Desemba 9, siku ya Uhuru watu wote wajumuike kufanya usafi.
VE4
VE5 
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha (wa pili kulia) akishiriki kufanya usafi katika hospitali hiyo leo Desemba 9, 2015.
VE6 
Mkuu wa Idara ya Sheria, Veronica Hillary, Ofisa Uhusiano Msaidizi, John Stephen, Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario na Mkuu wa Idara ya Upasuaji, Dk Julieth Magandi wakijumuika pamoja kufanya usafi leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ikiwa ni kuitikia agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufanya usafi leo Desemba 9, siku ya Uhuru.

VE7Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithnashery Jamaat ya jijini Dar es Salaam, Dewji Azim akifanya usafi leo katika hospitali hiyo.

WANAFUNZI WA CHUO CHA KODI JIJINI DAR WATIMIZA WAJIBU KUFANYA USAFI KATIKA CHUO CHAO

$
0
0
CHUO cha Kodi cha Mwenge jijini Dar es Salam wameitikia wito wa kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Joseph Magufuli kufanya usafi katika mazingira ya Chuo hicho.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kodi, Edward Mwakimonga amewasihi wanafunzi pamoja na wananchi kwa ujumla kuwa usafi ni afya na ikiwezekana iwe ni kawaida kufanya usafi kila baada ya wiki mara moja ili kuweka mazingira safi.

Nae Waziri Mkuu wa serikali ya chuo cha Kodi, Jeremia Shushu amewashukuru wanafunzi pamoja na menejimenti ya chuo hicho kwa kukubali na kujitokeza kwa wingi kushirikiana kufanya usafi katika mazingira ya chuo chao.
Wanafunzi wa chuo cha Kodi wakishirikiana bega kwa bega kufanya usafi katika chuo chaoo leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni kusherekea sikukuu ya Uhuru Desemba 9.Wanafunzi wakizoa takataka.
Usafi ukiendelea kila kona.

Wafanyakazi NMB Waifanyia Usafi Hospitali ya Sinza, Parestina jijini Dar.

$
0
0
Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas (tatu kushoto) ambaye ni Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya NMB, akimkabidhi Mganga Msaidizi Hospitali Sinza Parestina, Dk. Faith Mdee (wa tatu kulia) baadhi ya vifaa vya usafi ili vibaki vikitumika kusaidia zoezi la usafi katika hospitali hiyo. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB wakishirikiana na wafanyakazi wa Hospitali ya Sinza Parestina wakifanya usafi maeneo anuai ya hospitali hiyo ikiwa ni kuitikia mwito wa Rais Dk. John Pombe Magufuli wa kutangaza siku ya 9 Desemba itumike kufanya usafi maeneo mbalimbali ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB wakishirikiana na wafanyakazi wa Hospitali ya Sinza Parestina wakifanya usafi maeneo anuai ya hospitali hiyo ikiwa ni kuitikia mwito wa Rais Dk. John Pombe Magufuli wa kutangaza siku ya 9 Desemba itumike kufanya usafi maeneo mbalimbali ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu. 

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO AFANYA USAFI NA WANANCHI WA UPANGA MASHARIKI

$
0
0


Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel aliyeshika koleo akishiriki zoezi la usafi na wananchi wa Kata ya Upanga mashariki ikiwa ni kuitikia wito wa
kutikia agizo la Mh. Rais John Pombe Magufuli la kufanya usafi siku ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanzania .


Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel aliyeshika toroli akishiriki zoezi la usafi na wananchi wa Kata ya Upanga mashariki ikiwa ni kuitikia wito wa kutikia agizo la Mh. Rais John Pombe Magufuli la kufanya usafi siku ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel aliyeshika toroli akishiriki zoezi la usafi na wananchi wa Kata ya Upanga mashariki ikiwa ni kuitikia wito wa
kutikia agizo la Mh. Rais John Pombe Magufuli la kufanya usafi siku ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanzania .

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA USAFI SOKO KUU LA KARIAKOO

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafisha mtaro wa maji machafu kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitoka eneo la shimoni kwenye soko kuu la Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015. Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na umati ulioshiriki katika kufanya usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
(Pichana Ofisi ya Waziri Mkuu)
                                          KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images