Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1051 | 1052 | (Page 1053) | 1054 | 1055 | .... | 3270 | newer

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuzoa taka na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la Oysterbay- Karume Raod, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili eneo la Kituo cha Daladala cha Morocco, kwa ajili ya kuendelea kushiriki na wananchi wa eneo hilo kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiingia kukagua eneo la kuhifadhia Taka lililopo eneo la Kituo cha Daladala cha Morocco, wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuendelea kushiriki na wananchi kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuzoa taka na baadhi ya wananchi wa eneo Morocco, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.
  ***********
  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  OFISI YA MAKAMU WA RAIS
  Anwani ya simu: “MAKAMU”, Barabara ya Luthuli,
  Simu Na. +255 2116919 P.O Box 5380
  Fax Na. +255 2116990 Dar es Salaam. 
  Barua Pepe: km@vpo.go.tz TANZANIA.


  09/12/2015
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABAR
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo ameshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya Mtaa wa Oysterbay na Morocco stand katika wilaya ya Kinondoni katika kuadhmisha miaka 54 ya uhuru wa Tanzania Bara.

  Akizungumza na wananchi waliojumika katika maeneo ya Morroco stand Makamu wa Rais amewaagiza viongozi wa wilaya za mkoa wa Dar es salaam kutoa taarifa za wazabuni wa kufanya usafi ili ziweze kufuatiliwa.

  “Haya makampuni yanapewa fedha kwa ajili ya kazi ya kufanya usafi; lakini inaonyesha hayafanyi kazi ipasavyo kwa sababu mji bado ni mchafu,” Alisema Mhe. Samia.  Alielezea kufurahishwa kwake kwa jinsi wananchi walivyojitokeza katika zoezi hilo ambalo alisema ni endelevu na kuwataka Wakuu wa wilaya na wenyeviti wa serikali za mitaa kupanga siku maalum kwa ajili ya kufanya usafi katika maeneo yao.


  Makamu wa Rais alisema Watanzania hawawezi kujivunia miaka 54 ya uhuru ikiwa miji ni michafu na kuwataka wananchi kushirikiana kutekeleza kauli mbiu ya uhuru na kazi kwa kila mmoja kufanya kazi bidii mahali alipo aweze kuongeza tija ambayo italiwezesha Taifa kupata madawa na elimu bora. 

  Pamoja na wananchi waliojumuika na Makamu wa Rais kufanya usafi katika Mtaa wa Oysterbay, kwa upande wa Morocco stand walikuwepo pia wafanyakazi wa benki ya DTB, Radio ya EFM na wasanii mbalimbali 
  Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais 
  Dar es salaam. 


  0 0

   HAPA KAZI TU ya  Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe  Joseph Magufuli  ikiendelea kufanyiwa kazi kama Rais  huyo akionekana katika picha akiwa sambamba na mkewe Mama Janeth Magufuli,wakishiriki kufanya usafi leo ndani na nje viunga vya Ikulu ikiwemo pia soko la Samaki Feri,ambako alipata wasaa kuwasikiliza wachuuzi wa samaki na wavuvi.
  guf1 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mama Janeth Magufuli wakielekea eneo la ufukwe wa Ferry kufanya usafi katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru tarehe 9 Desemba.
  guf2 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizoa taka katika eneo la ferry jijini Dar es Salaam.
  guf3 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizoa taka katika eneo la ferry jijini Dar es Salaam.
  guf7 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka taka ndani ya ndoo ya Taka katika eneo la Magogoni jijini Dar es Salaam.
  guf8 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiwa pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakifanya usafi katika eneo la ufukwe wa ferry jijini Dar es Salaam.
  guf9guf10 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka taka taka kwenye dastibin wakati akifanya zoezi la kufanya usafi katika eneo la ufukwe wa Ferry jijini Dar es Salaam.
  guf11 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiokota takataka katika eneo la Ferry katika zoezi la kufanya usafi nchi nzima.
  guf12 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiokota takataka katika eneo la Ferry katika zoezi la kufanya usafi nchi nzima.
  guf13 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wavuvi wa ferry huku akiwa ndani ya Mtumbwi. Rais Magufuli alizisikiliza kero zao na kuahidi kuzitatua ndani ya muda mfupi.guf14 
  Rais Magufuli akifanya usafi pamoja na wavuvi wa eneo la ferry waliojitokeza kuungamkono zoezi hilo. Rais Magufuli amewataka Watanzania kuwa na Utamaduni wa kufanya Usafi kila wakati ili kuweka mazingira katika hali nzuri. PICHA ZOTE NA IKULU

  0 0


  0 0

   Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Saruji Tanga, Diana Malambugi (kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakifanya usafi katika Soko Kuu la Mji wa Tanga la Ngamiani mjini humo leo, kuadhimisha Siku ya Uhuru iliyodhimishwa kwa watanzania wote kujishughulisha na shuhuli za usafi wa mazingira. 
   Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Saruji Tanga, wakifanya usafi katika Soko Kuu la Mji wa Tanga la Ngamiani mjini humo jana kuadhimisha Siku ya Uhuru ambayo watanzania nchini kote walijishughulisha na kazi za usafi wa mazingira.
  Wafanyakazi wa Kampuni ya Saruji Tanga wakipiga picha na baadhi ya watendaji wa Soko Kuu la Ngamiani mjini Tanga wakati wafanyakazi hao walipokwenda kufanya shughuli za usafi kutekeleza maagizo ya Rais Magufuli kwa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru yatumike kwa shughuli za usafi wa mazingira.

  0 0

  Mvuvi Waziri Mfaume ambaye ni mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam alikutwa na mpiga picha leo akishimba shimo kwa ajili ya kuhifadhia uchafu kandokando ya barabara ya Barrack Obama ambayo zamani ilifahamika kwa jina la barabara ya bahari (Ocean Road). Anayeonekana akifagia eneo hilo ni Mama Chiku Hamadi Mkazi wa Mwananyamala.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakifanya usafi wa mazingira leo katika soko la samaki la Feri ikiwa ni kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kufanyika kwa usafi wa mazingira nchi nzima ikiwa ni maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
  Picha na Anna Nkinda - Maelezo.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiongoza kwa vitendo zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC na maeneo yanayozunguka barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore UPANGA jijini Dar es Salaam leo. Menejimenti ya NHC imeamua kuwa kufanya usafi kwenye majengo ya Shirika ili kuonyesha kwa vitendo utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli wa kuitumia Sikukuu ya Uhuru na Jamhuri ambayo hufanyika kila ifikapo Desemba 9 ya kila mwaka kwa gwaride na shamrashamra za halaiki kufanya. Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Issack Peter na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi TAMICO, NHC, Lilian Reuben wakishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC yaliyopo barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiongoza kwa vitendo zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC yaliyopo barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Baadhi ya watumishi wakikata matawi ya miti kwa makini bila kuharibu nya za simu yaliyokuwa kizuizi katika barabara eneo la ofisi za wizara ya fedha kwa lengo la kufanya usafi leo jijini Dar es salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akiongea na watumishi wa wizara hiyo leo jijini Dar es salaam mara baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi ikiwa ni mwitikio na utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kufanya usafi katika eneo ya kazi wakati wa maadhimisho ya sherehe za Uhuru mwaka huu.

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
  KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile leo ameiongoza wizara hiyo katika kuitikia na kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kufanya usafi katika eneo lao la kazi katika maadhimisho ya sherehe za Uhuru ya mwaka huu.

  Akiongea na watumishi wa Wizara hiyo, Dkt. Likwelile alisema kuwa maadhimisho ya siku ya uhuru yaendelee kutumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi ikizingatiwa dhana iliyokuwepo tangu uhuru ilikuwa “Uhuru na Kazi” ambapo kwa sasa kaulimbiu ya Rais Dkt. Magufuli inasema “Hapa Kazi Tu”

  “Ni uamuzi mzuri wa Rais, ni wa busara na unaendana na tulipotoka ambapo Tanzania inaamini katika “Uhuru na Kazi”, huu ni mwanzo wa kusimama kwa miguu yetu wenyewe ili kujiletea maendeleo kwa kuendelea kuwapiga vita maadui watatu wa taifa” alisema Dkt. Likwelile.

  Dkt. Likwelile aliwataja maadui hao kuwa ni ujinga, maradhi na umasikini ambao ndiyo wamekuwa chanzo cha kurudisha nyuma juhudi za maendeleo, kwa kuimarisha suala la usafi katika mazingira yote nchini, itakuwa mwanzo wa kupambana na suala magonjwa milipuko ikiwemo kipindupindu ambao asili yake ni uchafu.

  Aidha, Dkt. Likwelile aliwaasa watumishi wa wizara hiyo na Watanzanaia kwa ujumla kuenzi kazi iliyonzishwa na Mhe. Rais Dkt. Magufuli ya kufanya usafi na zoezi hilo liwe endelevu na la kudumu ambapo ameahidi kuwa wizara yake itapanga siku ya kufanya usafi mara kwa mara katika maeneo ya kazi ili kudumisha usafi ambao ni suala muhimu katika kuimarisha afya zao na ikizingatiwa watumishi hutumia muda mwingi wakiwa katika maeneo ya kazini.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu (DHRM) Wizara ya Fedha Deodata Makani alisema kuwa mwitikio wa watumishi katika zoezi la usafi umekuwa mkubwa na wanapendekeza zoezi hilo liwe endelevu maana watumishi hutumia muda mwingi katika maeneo ya kazini hivyo ni vema kuyaweka mazingira hayo katika hali ya usafi ili yawe rafiki wakati wote wa kutekeleza majukumu yao. 

  Naye mmoja wa watumishi wa Wizara hiyo William Muhoja alisema kuwa zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya kazi linatakiwa kufanywa kila wakati ambapo itakuwa ni sehemu ya watumishi kuwajibika kwa jamii katika maeneo yao wanapoishi na wanapofanya kazi.

  Sherehe za uhuru mwaka huu nchini zimeadhimishwa kwa namna tofauti na ilivyozoeleka miaka iliyopita ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mamlaka aliyonayo kikatiba alitangaza maadhimisho ya Sherehe za Uhuru na Jamhuri ya 9 Disemba mwaka huu, Watanzania wote waitumie kwa kufanya kazi mbalimbali kama vile, mashambani, maofisini, sokoni, viwandani na usafi wa miji yao katika kutimiza dhana ya Uhuru na Kazi kwa vitendo.


  Maadhimisho hayo yanaendelea nchi nzima ambapo kila halmashauri inatekeleza agizo la Mhe. Rais kwa vitendo kwa kufanya usafi katika maeneo yao, zoezi linashirikisha Wizara, idara, taasisi za Kiserikali na zisizo za kiserikali, maeneo ya viwanda, shule, vyuo, maeneo ya biashara, masoko na kuzunguka maeneo yote ya makazi ya watu.

  0 0


  Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Welle Ndikilo wakielekea soko kuu la Chalinze kushirikiana na wananchi kufanya usafi wa mazingira leo Desemba 9, 2015 ikiwa ni kuadhimisha miaka 54 ya UHURU kama ilivyoagizwa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli

  Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakifanya usafi katika soko kuu la Chalinze leo Desemba 9, 2015 ikiwa ni kuadhimisha miaka 54 ya UHURU kama ilivyoagizwa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli
  Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakifanya usafi katika soko kuu la Chalinze leo Desemba 9, 2015 ikiwa ni kuadhimisha miaka 54 ya UHURU kama ilivyoagizwa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli.

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Mugendi Zoka akifanya usafi nje ya ofisi yake mjini Ottawa, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli la kufanya usafi siku ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania.
  Balozi wa Tanzania nchini Canada, Balozi Jack Mugendi Zoka, akiwa pamoja na maafisa wa Ubalozi wakitekeleza kwa vitendo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli la kusherehekea Sikukuu ya Uhuru na Kazi yaani siku ya tarehe 9 Desemba kwa kufanya kazi na kusafisha mazingira ya Ubalozi.


  0 0
 • 12/11/15--03:08: ARUSHA WAPATA MEYA MPYA
 • Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fadhil Nkurlu akifungua rasmi Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha. 
  Mwenyekiti wa muda wa Mkutano wa Baraza la Madiwani Jijini Arusha, Ndg. Daniel Machunda ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha akikabidhi madaraka hayo kwa Mstahiki Meya mara baada ya kuchaguliwa kwa kura 33 kati ya kura 34 zilizopigwa. 
  Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Juma Iddi ambaye pia ni Katibu wa Mkutano wa Baraza akitoa muongozo wa namna Mkutano huu wa kwanza unavyoendeshwa kwa mujibu wa kanuni,kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Addoh Mapunda.

  Diwani wa Kata ya Sokoni, Mheshimiwa Calist Lazaro Bukhai(Chadema) akikishukuru baada ya kuchaguliwa kuwa Meya wa Jiji la Arusha. 


  0 0

  Katika kupambana na wimbi la kupunguza umaskini hapa nchini, kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa “Airtel FURSA Tunakuwezesha” unaendelea kutoa mafunzo ya biashara ya ujasiriamali kwa vijana wenye lengo la kuwawezesha na kuwainua vijana hapa nchini .

  Mafunzo hayo ya biashara ambayo yamekuwa yakiendeshwa hapa nchini katika mikoa mbali mbali , wiki ijayo yatafanyika Dar Live  Mbagala Kuu karibu na Big Bon  siku ya Jumanne tarehe 15 ili kuwawezesha vijana kuweza kukabiliana na wimbi hili gumu la kuendesha biashara na kuweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku na kuweza kuinua uchumi wa nchi hii.

  Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo ambayo yamekuwa yakiendelea hapa nchini, Meneja huduma kwa jamii  wa Airtel , bi Hwa Bayumi, alisema “mafunzo haya yanalengo la kuwasaidia vijana wenye umri kati ya miaka 18- 24 ambao wanakiu ya kujikwamua na umasikini. Vile vile “Airtel FURSA Tunakuwezesha” Airtel inawawezesha vijana kwa kuwapatia elimu ya biashara na nyenzo za kuimarisha biashara zao.

  Hivyo basi tunapenda kuwakaribisha vijana wote waishio jijini Dar Es Salaam kuweza kuhudhuria mafunzo haya ambayo yatatolewa bure kabisa bila gharama yoyote. Ili kijana aweze kushiriki  anatakiwa kufika pale Dar Live siku ya jumanne tarehe 15 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni.

  Vile vile ili kijana kushiriki au kufaidika na mpango wa Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. 

  Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara. Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com> aliongeza, Bayumi.

  0 0


  0 0

  Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), limetangaza tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu chini pamoja na baadhi ya maeneo ya Mji wa Bagamoyo mkoani Pwani kutokana  na mtambo huo kuzimwa kwa wastani saa 24 siku ya Jumapili tarehe 13/12/2015.

  Sababu ya kuzimwa kwa mtambo huo ni  kuruhusu kufanya matengenezo na maboresho ya njia kubwa ya Maji inayohudumia eneo la Salasala na viunga vyake vyote.

  Akiongea na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kaimu Meneja uhusiano wa Dawasco, Bi. Everlasting Lyaro, ametoa wito kwa wateja na wananchi  wote kuhifadhi Maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumiz ya muhimu ili kuweza kukidhi mahitaji husika kwa kipindi hicho.
  “Tupo katika maboresho ya huduma ya Maji, mtambo wetu wa Ruvu chini utazimwa kwa takribani saa 24, tunawaomba wateja wetu muhifadhi Maji ya kutosha na kuyatumia vizuri mpaka maketengezo yatakapokamilika, nasi tutajitahidi kadri tuwezavyo kuhakikisha tunarejesha huduma ya Maji kwa wakati uliopangwa” alisema Bi. Lyaro

  Amebainisha kuwa matengenezo hayo  yatasababisha maeneo mengi  ya Jiji la Dar es Salaam kukosa huduma ya Maji ikiwemo Mji wote wa  Bagamoyo, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na Kawe, Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Muhimbili pamoja na eneo la Buguruni.

  Everlasting Lyaro
  Kaimu Meneja Uhusiano
  022 2194800 / 0800110064

  0 0

  Meya Mteule wa jiji la Mbeya Diwani wa Kata ya Nzovwe(CHADEMA) Ndugu David Mwasilindi ambaye aliibuka kidedea kwa kupata kura 34 dhidi ya Mpinzani wake wa CCM aliyepata kura 14 katika uchaguzi uliofanyika Desemba 10 katika ukumbi wa Mkapa jijini humo. 
  Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Ndugu Quip Mbeyela ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti katika Kikao cha Baraza la Madiwani ambacho kiliketi kufanya uchaguzi wa kumpata Meya wa jiji hilo pamoja na Naibu Meya katika Halmashauri ya jiji la Mbeya . 

  Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya jiji la Mbeya Dkt Samuel Lazaro akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani ambalo liliketi kwa ajili ya kumchagua Meya pamoja na Naibu Meya katika Ukumbi wa Mkapa jijini humo. 


  0 0


  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi(watatu toka kushoto) na mkewe Marystella Masilingi (wanne toka kushoto) wakiwakaribisha Waheshimiwa Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao nchini Marekani kwenye mchapalo ulioandaliwa na yeye mwenyewe kwa ajili ya kujitambulisha kwao wakiwemo viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania nchini Marekani, viongozi wa Dini, DICOTA na vyama vya siasa siku ya Alhamisi Desemba 10, 2015 kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo mtaa wa 22 jijini Washington, DC. Kulia ni Afisa Ubalozi Bi. Swahiba Mdeme. Picha na Vijimambo Blog/Kwanza Production
  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akisalimiana na Ben Kazora mmoja ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Dallas, Texas mara tu alipowasili kwenye jengo la Ubalozi kuhudhuria mchapalo wa kujitambulisha kwa Mhe. Balozi Wilson Masilingi, watatu toka kushoto ni mkewe Marystella Masilingi na kulia ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme.
  Afisa Suleiman Saleh akiwa kama mshereheshaji wa mchapalo huo akiwawakaribisha wageni na baadae kumkaribisha Afisa Swahiba Mdeme kwa ajili ya kumkaribisha Balozi Wilson Masilingi.
  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akijitambulisha kwa Waheshimiwa Mabalozi na viongozi wa Jumuiya za Watanzania nchini Marekani kwenye mchapalo ulioandaliwa na yeye mwenyewe kwa ajili ya kujitambulisha kwao uliofanyika siku ya Alhamisi Desemba 10, 2015 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 40 ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama na kuikosesha serikali mapato. Uchunguzi unafanywa kwa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2489 yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu.

  Kati ya hao, watuhumiwa 26 ni watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)na watumishi 03 kutoka Bandari kavu (ICD) YA AZAM wanatuhumiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329. Aidha, watuhumiwa 11 ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)  kwa kuhusika na upotevu wa makontena 2489.

  Uchunguzi unaoendelea pia unahusisha kupitia kumbukumbu mbalimbali na kadhia za forodha ili kubaini mtindo uliotumika na kuwabaini wote waliohusika katika mchakato huo. Makontena 329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya AZAM kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2015, wakati  makontena  2489 yaligundulika kutolewa Bandarini kuanzia Mwezi Machi mpaka Septemba, Mwaka 2014   kinyume cha taratibu kwa lengo la kukwepa kodi na ushuru. 


  Uchunguzi bado unaendelea ili kuwabaini wote wanaohusika na hatimaye majalada ya kesi yatapelekwa kwa mwanasheria wa serikali ili watuhumiwa watakaobainika kuhusika na makosa mbalimbali wafikishwe mahakamani.
  Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na watuhumiwa 40 washikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa tuhuma za ukwepaji kulipa kodi pamoja na mtu mmoja ambaye anatafutwa na Jeshi la Polisi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini.
  Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Suleiman Kova akionyesha picha ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini ambaye anatuhumiwa kwa kutoa makontena 329 kwenye bandari kavu ya AZAM (AZAM ICD) bila kulipia kodi anayetafutwa na jeshi hilo pia ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za “JAS EXPRESS FREIGHT LTD” na “XL CLEARING AND FOWARDING Co. LTD” ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo. Ameonyesha picha ya mtuhumiwa huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
  Meneja wa Huduma na elimu kwa mlipa kodi kutoka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Diana Masalla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kukusanya jumla ya shilingi 10,075,979,462.08 kutoka kwa makampuni 22 ambayo yalihusika na uondoshwaji wa makontena bandarini kinyume cha sheria na taratibu za forodha hadi kufikia tarehe 10 Desemba 2015. 

  Pia kati ya hao makampuni 06 amesema kuwa yamelipa kodi yote iliyokadiriwa pamoja na adhabu, ambapo makampuni 16 yamelipa sehemu ya kodi iliyokadiriwa pamoja na adhabu. 

  Aidha, makampuni 26 hayajalipa kodi kiasi cha shilingi 4,789,924,609.69 pamoja na kwamba zoezi la ukadiriaji limefanyika. 

  hata hivyo amesema kuwa leo ni siku ya mwisho iliyotolewa na Mheshimiwa Rais kwa wafanyabiashara waliokwepakulipa kodi ya makontena,

  Amewasisitiza wananchi wote watoe taarifa kuhusu vitendo vya ukwepaji kodi kutumia namba 0784210209. Pia taarifa za mwenendo wa wafanyakazi wa TRA Wasio waadilifu zitolewe kupitia simu namba 0689 122515 na ujumbe mfupi 0689 122516.
  Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Suleiman Kova wakimsikiliza leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0
 • 12/11/15--05:17: TFF YAMPONGEZA NAPE NNAUYE
 • Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za pongezi mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye kufutia kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika serikali ya awamu ya tano.

  Katika salamu zake, Malinzi amempongeza Nape na kusema TFF ina imani nae katika nafasi hiyo, na kuahidi kushirikiana katika michezo na haswa katika kusukuma gurudumu la maendeleoya mpira wa miguu nchini.

  Aidha pia Malinzi amewapongeza Paschal Kihanga, Mwenyekiti wa chama cha soka moa Morogoro kwa kuchaguliwa kuwa Meya wa manispaa hiyo, na James Bwire mmiliki wa shule ya Alliance kwa kuchaguliwa meya wa manispaa ya Nyamgana.

  Malinzi amewatakia kila la kheri katika nafasi hizo walizozipata za kuwatumikia watanzania, na kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini anawatakia kila la kheri na kuahidi kushirikiana nao.


  0 0


  Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leah Kihimbi akitoa hotuba katika Warsha ya siku mbili kuhusu wasanii wanawake kupinga ukatili wa kijinsia, mafunzo hayo yamefanyika ili kuhitimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na kusheherekea siku ya msanii Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

  Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho Tanzania Agnes Lukanga akitoa mada katika warsha ya siku mbili kuhusu wasanii wanawake kupinga ukatili wa kijinsia, mafunzo hayo yamefanyika ili kuhitimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na kusheherekea siku ya msanii Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana amekutana na Balozi wa Malawi nchini Tanzania na kufanya naye mazungumzo yaliyolenga kukuza uhusiano wa nchi hizi mbili, sambamba na kuongeza tija ya maendeleo huku wakifahamishana nia ya kuwa na miradi ya pamoja itakayolenga kuongeza uhusiano wa pamoja na kupunguza changamoto zinazozikabili nchi hizi.

  Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Makamu wa Rais leo Desemba 11, 2015 amekutana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Hanne-Marie Kaarstad ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo walizungumzia kuhusu uongezaji wa mahusiani na ushirikiano hasa katika suala la mazingira. Balozi Kaarstad ni mpya nchini Tanzania na ujio wake ameelezea kuwa unalenga katika kuongeza tija kwa nchi hizi mbili na kwamba Norway itabakia kuwa rafiki wa karibu wa Tanzania.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Dec 11, 2015 kwa mazungumzo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mhe. Hawa Ndilowe, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Dec 10, 2015 kwa mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad (kulia kwake) na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani, Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine (kulia) na Msaidizi wa Balozi (kushoto) mara baada ya mazungumzo ao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo Desemba 11, 2015.
  Picha na OMR

  0 0

  Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango ikitembelea uwanja wa ndege wa Songwe kujionea maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.
  Mmoja wa waongoza ndege katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, Bw. Emmanuel Mgaza akitoa maelezo ya jinsi ndege inavyoongozwa mpaka kutua kwa timu ya ukaguzi iliyotembelea uwanjani hapo
  Mtaalumu wa kuongoza ndege katika uwanja wa Songwe Bw. Baraka Mwakipesile akitoa maelezo kwa baadhi ya wajumbe wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo waliotembelea uwanjani hapo.
  Jengo la Uwanja wa Ndege wa Songwe.

older | 1 | .... | 1051 | 1052 | (Page 1053) | 1054 | 1055 | .... | 3270 | newer