Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

STANDARD CHARTERED TANZANIA WINS BANK OF THE YEAR AWARD

$
0
0

Tanzania, 07 December, 2015– Standard Chartered Bank Tanzania Limited has been awarded the prestigious ‘Bank of the Year’ award at The Banker Awards 2015. This is the eighth time that the Bank is winning this award which was announced at a grand gala dinner programme held at an award ceremony in London last Wednesday evening.

With more than fifty lenders operating within its borders, Tanzania has a healthy and competitive Banking sector. Standard Chartered Bank Tanzania Limited has stayed ahead of the game by maximising its digital services to make banking a less time consuming activity for Tanzanians. 

TheChief Executive Officer for the Bank in Tanzania, Sanjay Rughanisaid, “We are delighted to have won this prestigious award. It is a testimony of our commitment to serve our clients in this market consistently over so many years. With a reputation for high quality service, innovation and connecting Tanzania to neighbours and the world, we have a special offer to our clients. We are, therefore, proud to be able to make positive contributions in Tanzania.”

Initiatives which motivated the accolade from The Banker were Standard Chartered Bank’s Straight2Bank online service, a fully integrated banking platform that offers a full range of transactions for clients that continues to be a market’s leading service. Additionally, in March this year, the Bank launched the “Straight2Bank Wallet”, a mobile payment service for corporate clients in Tanzania. The service enables the Bank’s corporate clients to make almost instantaneous bulk payments directly from their Standard Chartered Bank accounts into their beneficiaries’ M-PESA and TigoPesa accounts. The Bank’s corporate and institutional services and support continues to enable companies operating in Tanzania to fund their businesses and hedge themselves against currency volatility.

For the award period under review, Q1 2014 to Q2 2105, Standard Chartered Bank in Tanzania ran a pan-Bank staff campaign called ‘MySelf MyBrand’ geared towards personalizing service thereby enhancing customer service.

The Bank also organized a number of client workshops aimed at creating more awareness on its various products and services as well as enhancing financial literacy and skills on running profitable businesses and understanding banking and regulatory requirements.

During the period, the Bank’s net profits grew by 12% and return on equity increased to 23%, reflecting a commitment to shareholder returns. 
Now in its 16th year, The Banker Awards is one of the most prestigious events within the industry. The Banker is the world’s premier banking and finance magazine, read in over 180 countries around the world. The Banker is the key source of data and analysis for the industry. Its unique database of more than 4,000 banks, maps their financial strength and soundness via Tier I capital, profitability, and their performance versus their peers.

This is the eighth time Standard Chartered Bank Tanzania has won the `Bank of the Year’ award. The bank had earlier won this award consecutively from 2002 – 2005, and thereafter in 2007, 2010 and 2011.




BREAKING NYUZZZZ......: RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA KATIBU MKUU WIZARA YA UCHUKUZI, AVUNJA BODI YA MAMLAKA YA BANDARI (TPA) LEO

$
0
0
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amevunja bodi ya Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) pamoja na kutengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari Profesa Joseph Msambichaka pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Awadh Massawe.

Kuvunjwa kwa bodi hiyo kunatokana na utendaji mbovu wa Mamlaka hiyo kwa muda mrefu na kitendo cha kutokuchukua hatua katika vyanzo husika.

Akizungumza  na waandishi wa Habari  Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam leo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kutenguliwa kwa uteuzi huo kunatokana na ziara alizofanya katika Bandari ya Dar es Salaam na kubaini uwepo wa mianya ya ukwepaji kodi ikiwemo ya Makontena 2,387 yaliyopitishwa kati ya Machi na Septemba mwaka jana.

Amesema upotevu huo unatokana na mfumo usiokidhi wa kupokelea malipo ambao unatoa mwanya wa kupoteza mapato ya serikali na kutaka mfumo huo ubadilishe kufikia Desemba 11.

Waziri Mkuu, Majaliwa amesema kuwa kutokana na utendaji wa bandari huo mbovu, ripoti iliwataja waliohusika na upitishaji wa makontena hayo na bila ya kuwepo kwa taarifa yeyote, hivyo amewasimamisha kazi wasimamizi 8 wa Bandari Kavu (ICD) ambao ni Happygod Naftari, Juma Zaar, Steven Naftari Mtui, Titi Ligalwike, Lydia Prosper Kimaro, Mkango Alli, John Elisante pamoja na James Kamwomwa.

Wengine ambao hakuwemo kwenye ripoti hiyo ambao ni viongozi wa sekta zilizotoa ruhusa makontena kutoka ndani ya bandari lakini ni wahusika wakuu ambao ni Shaban Mngazija Aliyekuwa  Meneja Mapato, Rajab Mdoe Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu wa Bandari Kavu, Ibin Masoud Kaimu Mkurugenzi wa Fedha ,Apolonia Mosha Meneja wa Bandari Msaidizi (Fedha).

Waziri Mkuu, amesema kuwa katika ziara yake  kwa Shirika la Reli Nchini (TRL) alibaini matumizi mabaya ya fedha ya Sh.Bilioni 13 nje ya utaratibu ambao uchunguzi unakamilishwa kwa waliohusika. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha kwa waandishi wa habari, ripoti Bandari ya Dar es salaam iliyobaini mianya ya ukwepaji kodi ikiwemo ya Makontena 2,387 yaliyopitishwa kati ya Machi na Septemba mwaka jana. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, Ofisini kwake jijini Dar es salaam leo.

J&M VIRGO WASHUSHA MALI MPYA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MSIMU WA SIKUKUU

$
0
0
 DUKA LA J&M VIRGO LIMEKUTELEA MALI MPYA NA ZA UHAKIKA KABISA KWAKO WEWE MTANZANIA MWENYE KUPENDA KUTOKA KIJANJA KATIKA MSIMU HUU WA SIKUKUU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA, MZIGO UMESHUKA JUZI TU TOKA MAJUU ILI UWEZE KUNG'AA KATIKA KIPINDI HIKI, WATEMBELEE  J&M VIRGO WENYE UHODARI WA KUUZA VIWALO VYA NGUVU NA VYA KISASA KATIKA DUKA LAO LILILOPO PALE MIKOCHENI KWA WARIOBA, JENGO LA C&G PLAZA GHOROFA YA KWANZA,  JIJI LA DAR ES SALAAM.

FIKA ILI UWEZE KUJIPATIA VIWALO VYA KIJANJA,POCHI BABKUBWA,MOKA MATATA NA MICHUCHUMIO YA HAJA KWA KINA DADA.

KWA TAARIFA ZAIDI TEMBELEA LIBENEKE LAO

NYOTA WAZIRI NDANI YA DANGA CHEE

DIRA YA DUNIA JUMATATU 07.12.2017

Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa aitikisa Mamlaka ya Bandari

MFUMUKO WA BEI WA NOVEMBA UMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 6.6

$
0
0
 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari juu ya mfumuko wa bei kwa mwezi Novemba ambao umefikia asilimia 6.6 leo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Meneja wa  Mfumuko wa Bei wa NBS , Ruth Minja.
 02.Waandishi wa habari wakifatilia taarifa kutoka Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,Epharaim Kwesigabo  hayupo picha leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Chalila Kibuda wa Globu ya Jamii)
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa  Novemba 2015 umeongezeka hadi asilimia 6.6 kutoka asilimia 6.3  ya Oktoba mwaka huu.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo amesema kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Novemba.
 
Kwesigabo amesema mfumuko wa bei wa bidhaa ya za vyakula na vinywaji  Baridi  Novemba mwaka imeongezeka  kwa asilimia 11.2 kutoka asilimia 10.2 tofauti na mwezi uliopita.
 
Amesema kuongezeka kwa Mfumuko wa bei wa Novemba 2015  kumechangiwa na kuongezeka kwa baadhi ya bidhaa za vyakula kwa  kipindi cha mwezi uliopita zikilinganishwa na bei za Novemba mwaka jana.
 
Aliongeza kuwa mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kuongezeka Novemba 2015 ukilinganishwa na bei za Novemba 214  ni pamoja na mchele kwa asilimia 25.8, Mahindi asilimia 16.4, unga wa mahindi asilimia 12.0  nyama asilimia 8.7, Samaki asilimia 21.4, Mharagwe asilimia 14.5  Choroko asilimia 15.3 Mihogo asilimia 10.7  pamoja na viazi vitamu 23.4.
 
Kwesigabo amesema kuwa uwezo wa sh.100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia sh.62.31 mwezi Novemba, 2015 kutoka Septemba 2010  ikilinganishwa na Sh. tofauti na Novemba mwaka jana sh.100 uwezo wake ulikuwa ni sh.62.82  ilivyokuwa Oktoba 2015.

Mfumuko wa bei  Afrika Mashariki,nchi ya Kenya  kwa Novemba imeongezeka kwa asilimia 7.32, kutoka asilimia 6.72 ya  Oktoba mwaka huu, Uganga imeongezeka hadi asilimia 9.1kutoka asimia 8.8 ya mwezi uliopita  hali hiyo inafanya nchi ya Uganda kuwa ya kwanza kwa kuongeza mfumuko wa bei.

Polisi waja na mpango wa kuboresha usalama kwenye jamii

$
0
0
Na. Tamimu Adam – Jeshi la Polisi.

Jeshi la polisi nchini, limeanzisha mpango wa   kuboresha usalama wa jamii  nchi nzima ambao unalenga  kuboresha  utoaji wa huduma bora kwa wananchi, kuboresha mawasiliano  ya ndani na nje ya Jeshi la polisi kwa kuwashirikisha wadau  mbalimbali wa usalama ambapo mpango huo utaanza kutekelezwa katika mkoa wa kipolisi kinondoni  ambapo lengo lake ni  kupunguza uhalifu kwa asilimia kumi ifikapo mwaka 2019.

Akihitimisha  maabara ya mpango huo iliyofanya kazi kwa wiki sita, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi  Abdulrahmani  Kaniki  aliwahakikishia  washiriki wa maabara ya kuboresha usalama wa jamii, kuwa Jeshi la polisi litatekeleza  kwa vitendo mapendekezo yote yaliyotokana na maabara hiyo, kwani baadhi ya mapendekezo   hayahitaji bajeti  hivyo utekelezaji wake utaanza mara moja.

 “Kazi iliyofanywa  na maabara hiyo ni kubwa  na umuhimu katika kuboresha usalama wa jamii katika nchi yetu hivyo mapendekezo yote ni lazima yafanyiwe kazi ili kuleta mafanikio chanya”. Alisema Kaniki.

Aliongeza  kuwa mpango huo umeanzia  katika mkoa wa kipolisi kinondoni na baadaye utaenea nchi nzima, ambapo alizitaja sababu zilizopelekea kuanza na kinondoni kuwa ni pamoja na  kuongezeka kwa makosa,  kupanuka mji, idadi kubwa ya watu na uwepo na shughuli nyingi za kiuchumi ukilinganisha na maeneo mengine.

Naye, Mtendaji mkuu wa  ofisi ya Rais ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi (PDB), Omari Issa alisema mpango huo wa uboreshaji wa usalama wa jamii ambao unaanza na mkoa wa Kinondoni uliandaliwa kwa kuwashirikisha wadau kutoka taasisi mbalimbali za serikali na kijamii ambao kwa pamoja walishirikiana kwa pamoja katika kuangalia namna ya kuboresha usalama wa jamii  ili kuwezesha jamii  kuwa salama.

Aliongeza kuwa mpango wa matokeo makubwa sasa unahitaji kuzingatia vitu vikuu vitatu katika utekelezaji wake ambavyo ni kujiwekea vipaumbele, nidhamu ya utekelezaji na uwajibikaji hivyo alisema hana wasiwasi na Jeshi la Polisi katika utekelezaji wa mpango huo hapa nchini.

Mpango wa uboreshaji wa usalama  wa jamii unalenga  kuboresha  na kurahisisha huduma mbalimbali zinazotolewa na Jeshi la polisi ikiwemo kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa askari, usimamizi wa rasirimali watu na vifaa na kuweka mikakati ya kuwashirikisha wadau wa kada mbalimbali ndani  ya jamii katika kuboresha usalama wa jamii.
 Maabara hiyo ya  kuboresha usalama wa jamii ripoti yake inatarajiwa kukabidhiwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi hivi karibuni ili kuanza utekelezaji wake kwa kuanza na mkoa wa kipolisi wa Kinondoni.

Mahojiano na DC Paul Makonda katika kipindi cha JUKWAA LANGU Dec 7 2015

$
0
0
Kipindi cha JUKWAA LANGU hukujia kila Jumatatu kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki kuijadili Tanzania ya sasa na ile tuitakayo
Katika kipindi hiki, tumeungana na Mhe Paul Makonda. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jiji Dar Es Salaam ambaye mbali na mambo mengine, ameeleza "ya moyoni" kuhusu tofauti iliyopo kati ya utendaji wa Rais wa awamu ya nne Mhe Jakaya Kikwete (aliyemteua katika wadhifa huo) na Rais wa sasa Dk John Magufuli. Kabla ya hapo aligusia namna alivyoteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya, na kwanini anaamini inastahili kuwepo namna nzuri zaidi ya kuteua watu katika nafasi kama yake.

Na kabla ya hayo yote, alizungumzia migogoro mbalimbali inayoendelea wilayani mwake kama wa kiwanda cha Urafiki, kubomolewa kwa nyumba za thamani, mgogoro wa Coco Beach nk.

Na kama ilivyo desturi, akapokea maswali na ushauri toka kwa wasikilizaji wetu
KARIBU


NAPE AWAPA MAKATIBU KATA WA JIMBO LAKE PIKIPIKI

$
0
0

 Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akimkabidhi Katibu wa kata ya Mtua Kilimahewa funguo ya pikipiki kwa niaba ya makatibu kata 20 wa jimbo hilo ambao wote wamewezeshwa usafiri wa pikipiki ili kurahisisha ufanisi wa kazi zao.
 Mbunge wa Jimbo la Mtama (CCM) Nape Nnauye akijaribu moja ya pikipiki kati ya 20 alizowapa makatibu kata ili ziweze kuwasaidia kufanya kazi kwa ufanisi kwenye shughuli zao za kujenga na kuimarisha Chama Cha Mapinduzi.
 Sehemu ya pikipiki zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye kwa makatibu kata 20 wa jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akizungumza mbele ya viongozi wa CCM wilaya ya Lindi vijijini ambapo aliwaambia viongozi hao kuwa amejipanga kufanya kazi katika jimbo hilo zenye kuleta tija na kuhakikisha anatekeleza ahadi zote alizozitoa wakati wa kampeni na kuwata makatibu kata waliokabidhiwa pikipiki 20 kuzitumia katika kazi za kujenga na kuimarisha chama.

VIINGILIO VYA KRISMASI VYATAJWA

$
0
0
 KAMPUNI ya Msama Promotions ambayo ni waandaaji wa Matamasha ya Pasaka na Krismasi, imetangaza viingilio vya juu kwenye Tamasha la Krismasi kuwa ni Shilingi 50,000 kwa viti maalum, Tamasha ambalo litafanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo linalokwenda na shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 ambako kabla, Msama waliandaa tamasha la Kuombea Amani uchaguzi Mkuu lililofanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama VIP watachangia shilingi 10,000 na viti vya kawaida watachangia shilingi 5000.Msama alisema watoto watakaohudhuria tamasha hilo watachangia shilingi 2000, alitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ambalo lina lengo la kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kupita kwenye uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.

"Watanzania tujitokeze kwa wingi ili turudishe shukrani kwa Mungu baada ya kutupitisha katika uchaguzi Mkuu ambao ulikuwa tofauti na chaguzi zilizopita, hivyo ni nafasi yetu kumwambia Mungu asante baada ya kutupitisha katika tukio hilo muhimu," alisema Msama.

Aidha Msama michango inayopatikana kupitia viingilio hivyo hurudisha kwa Jamii yenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu, wajane na wengineo wenye uhitaji kama huo.Msama alisema maandalizi ya kuelekea tamasha hilo yanakwenda vizuri, huku waimbaji kama Rose Muhando, Upendo Nkone, Ephraim Sekeleti, Rebecca Malope, Kwaya ya Wakorintho Wapili, Joshua Mlelwa na Christina Shusho wamethibitisha kushiriki tamasha hilo.

WATEJA WA AIRTEL KUONA VIDEO ZA YOUTUBE BURE WAKIJIUNGA NA YATOSHA INTANETI

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kifurushi nafuu cha ‘Yatosha Intaneti’ na ubia kati ya kampuni hiyo na Google ambapo mteja wa Airtel ataweza kupata huduma ya kutazama video zilizopo You Tube Bure. Kulia ni Meneja wa Huduma za Intaneti wa Airtel, Erick Mshana. 
 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) na Meneja wa Huduma za Intaneti wa Airtel, Erick Mshana wakizindua kifurushi nafuu cha ‘Yatosha Intaneti’ na ubia kati ya kampuni hiyo na Google ambapo mteja wa Airtel ataweza kupata huduma ya kutazama video zilizopo You Tube Bure katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

· Airtel waingia ubia na Google kuwezesha wateja kucheki video BURE 
· Bure kupitia vifurushi vya Yatosha intaneti 

KAMPUNI inayoongoza katika mtandao wa intaneti Tanzania, Airtel leo imeungana na Google katika kuwapatia wateja huduma yakutazama video mbalimbali zikiwemo zile za kiswahili BURE kupitia You Tube mara tu wanapojiunga na vifurushi vya Yatosha intaneti. 

Airtel imetangaza kuwapatia wateja wake ofa hiyo ya kuona video za You Tube BURE mara baada kuzindua kifurushi nafuu cha YATOSHA INTANET, Airtel imeeleza kuwa huduma hiyo ya BURE ni muendelezo wa dhamira yao ya kutoa huduma bora za intaneti kwa wateja wake zaidi ya milioni 10 nchini Tanzania ambapo wateja wa Airtel watakaojiunga na YATOSHA INTANET sasa wataweza kujipatia maudhui ya video nzuri wapendazo bila kufikiria tena gharama. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa huduma za inteneti wa Airtel Tanzania Gaurav Dhingra, alisema, "dhamira yetu siku zote ni kuendelea kuwa karibu na wateja wetu, kuelewa mahitaji yao na kuweza kuwapatia huduma bora yenye viwango vinavyohitajika.”

“Tunafahamu vizuri kwamba wimbi la uhitaji wa huduma hii ni kubwa kwa sasa, ongezeko la wanaokupakua au kuona video za aina mbali mbali zikiwemo michezo, muziki, habari za aina mbalimbali kupitia You Tube imeongezeka kwa kasi sana kutokana na wateja wetu wanavyoridhishwa na huduma zetu bora za intaneti.” Alieleza Dhingra 

Bw Dhingra akiendelea kufafanua alisema “Hata hivyo, watumiaji wa huduma hiyo ya kutazama au kupakua video hizo bado wamekuwa na kikwazo cha kufikiria swala la gharama na kutofurahia ubora wa video hizo, hivyo basi Airtel tumeamua kuwapatia wateja wetu MB’s za BURE kupitia You Tube ili waweze kufurahia kuangalia Video kupitia intaneti ya Airtel ".

Charles Murito, Meneja mwakilishi wa google nchini Tanzania, alisema ; "Tunataka kuhakikisha kwamba watumiaji wa simu za mkononi wanaongezeili na kufurahia huduma za You Tube nchini. Kwa kushirikiana na Airtel tutahakikisha kwamba wateja wote wa simu za mkononi wanaweza kutumia simu zao kwa kuangalia video kwa urahisi zaidi na kwa gharama nafuu wakiwa mahali popote. Vile vile watafurahia kutumia You Tube ikiwa na maudhui ya lugha ya Kiswahili na kuweza kufurahia mambo mbalimbali kwenye muziki, habari za biashara, burudani na elimu " .

Akielezea jinsi ya mteja kuweza kujiunga na vifurushi hivyo, Afisa huduma za intaneti wa Airtel Tanzania Erick Daniel Mshana, alisema “mteja wa Airtel wa malipo ya awali anaweza kupata huduma hii kwa kupiga *149*99# kisha kujiunga na kifurushi cha Yatosha intaneti na atafurahia huduma yetu ya Intaneti aliyojiunganayo ikiwa ni ya SIKU, WIKI, au MWEZI na zaidi ataona video za You Tube BURE. 


Airtel pia tuwakaribisha wadau mbalimbali wanaotengeneza na kusambaza video kwa njia ya mtandao kushirikiana nasi kufikisha video zako kwa jamii kupitia OFA hii. Kama wewe ni mtoa huduma wa video, unaweza kuwasiliana nasi kupitia Airtel huduma kwa wateja".

CCM YANYAKUA UENYEKITI WA HALMASHAURI LINDI VIJIJINI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndugu Yahaya Nawanda akihutubia wakati wa ufunguzi wa kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Lindi Vijijini ambapo aliwataka madiwani wao kuhakikisha suala la usafi linatiliwa mkazo kwenye maeneo yao.
 Baadhi ya madiwani wakisikiliza kwa makini.

 Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akipiga kura kumchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lindi Vijijini.

Muhimbili Yaendelea Kupokea Misaada

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vifaa mbalimbali vitakavyotumika kuwahudumia wagonjwa katika hospitali hiyo.

Msaada wa vitanda kumi utatumika katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) pamoja na wodi nyingine. Msaada huo umetolewa na Jumuiya ya Australia na Tanzania.

Vifaa vingine vilivyotolewa ni pamoja na  Stretcher’  nne zitakazotumika kusafirishia wagonjwa ambao hawawezi kukaa, kifaa cha kufanyia  mazoezi  kwa wagonjwa  na baiskeli ya magurudumu matatu.

 Akipokea msaada huo  Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika hiyo Agness Mtawa ameishukuru Jumuiya hiyo na kutoa rai kwa wadau wengine kuendelea kutoa msaada katika hospitali hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mseru akizungumza leo katika mkutano uliowajumuisha viongozi wa Jumuiya ya Australia na Tanzania kabla ya hospitali hiyo kukabidhiwa vifaa vya wagonjwa vikiwamo vitanda na baiskeli za magurudumu matatu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Australia na Tanzania, Didier Murcia akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Mseru leo wakati wa mkutano na viongozi wa jumuiya hiyo na wataalamu wa hospitali hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario wa MNH.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Bi. Agness Mtawa akipokea msaada wa vitanda na vifaa vingine leo kwenye hospitali hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Australia na Tanzania, Didier Murcia akimkabidhi Sister Mtawa vifaa hivyo na kulia ni Mkurugenzi wa jumuiya hiyo, Thierry Murcia.

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI AONGOZA KIKAO MAALUM CHA KUPITIA RASIMU YA MPANGO WA WA JESHI LA MAGEREZA KUJITOSHELEZA CHAKULA, JIJINI DAR

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akifungua Kikao Maalum cha Wadau kutoka nje ya Magereza(hawapo pichani) cha kujadili rasimu ya Mpango wa Jeshi la Magereza wa kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa waliopo Magerezani. Kikao hicho kimefanyika leo Desemba 8, 2015 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
 Mshauri Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Beatus Kundy(aliyesimama) akiwasilisha rasimu ya Mpango wa Jeshi la Magereza wa kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa waliopo Magerezani. Jeshi la Magereza limeandaa rasimu hiyo ili kuipunguzia Serikali gharama za kuwalisha wafungwa waliopo magerezani.
 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa Andiko hilo(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Eng. Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.

Katibu mtendaji BAKITA amkabidhi kamusi kuu mpya ya kiswahili katibu mkuu wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel(kulia) akikabidhiwa kamusi kuu mpya ya Kiswahili kutoka kwa Katibu Mtendaji kutoka baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt Selemani Sewangi.Kamusi hiyo mpya ina jumla ya maneno makuu Zaidi ya elfu thelathini na sita(36000) na kurasa 1264.
Katibu Mtendaji kutoka baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt Selemani Sewangi(kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel kwa baadhi ya maneno ambayo yapo katika kamusi mpya iliyotolewa na Baraza hilo leo jijini Dar es Salaam.

Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa EU watoa wito kwa ukamilishwaji haraka wa mchakato wa uchaguzi Zanzibar kulingana na kanuni za chaguzi shirikishi, za uwazi, zinazotekelezwa kwa wakati na za kuaminika

$
0
0
Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU EOM) kwa Tanzania unatoa tena wito kwa ukamilishwaji haraka wa mchakato wa uchaguzi Zanzibar kulingana na kanuni za chaguzi shirikishi, za uwazi, zinazotekelezwa kwa wakati na za kuaminika. 

Kufuatia Siku ya Uchaguzi tarehe 25 Oktoba, Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya umebaki nchini kufuatilia chaguzi zilizoahirishwa Tanzania Bara na mchakato uliyositishwa Visiwani Zanzibar, baada ya tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) la tarehe 28 Oktoba, lililofuta matokeo ya uchaguzi mkuu Zanzibar.

 EU EOM ilikutana na wadau wakuu Visiwani, vikiwemo vyama vya siasa, Mwana Sheria Mkuu wa Serikali wa zamani na wa sasa, wadau wa sharia na mahakama, asasi za kiraia na maafisa uchaguzi. Bahati mbaya EU EOM haikuweza kukutana na Mwenyekiti wa ZEC.

EU EOM inafahamu kuhusu mazungumzo yanayoendelea kati ya CCM na CUF, yanayowashirikisha Marais Wastaafu wa Zanzibar. EU EOM inarudia tena wito uliyotolewa kwa pamoja na jumbe zingine za uangalizi za kimataifa tarehe 29 Oktoba, unaoishauri ZEC kuonyesha uwazi kamili kufuatia uamuzi wake wa kufuta uchaguzi na uongozi wa kisiasa Zanzibar kuweka maslahi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar kwanza, kwa lengo la ukamilishwaji haraka wa mchakato wa uchaguzi, kulingana na kanuni za kidemokrasia za chaguzi pamoja na sheria za Zanzibar.

SOMA ZAIDI HAPA

TASWIRA MBALIMBALI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Uhaba wa usafiri wahatarisha usalama wa Abiria, kama walivyonaswa na kamera ya mtaa kwa mtaa leo   jijini Dar es Salaam. 
(Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii).

MASHINDANO BAISKELI KILOMITA 115 YA RIFT VALLEY ODYSSEY YAKUZA VIPAJI VYA VIJANA

$
0
0
Washindi wa kwanza wa mashindano.ya baiskeli, ya  Rift Valley Odyssey  ya liyofanyika  jijini arusha  DEC 6 Mwaka huu Sophia Husseni wa kwanza (kulia) na Sophia Adson wa (pili) kutoka kulia wakiwa na Mkurugenzi wa 6degrees Simone Paine wa pili kutoka kulia yaliyo fanyika Arusha ambapo wachezaji toka ndani nan je ya nchi wameshirikai kwa takriban siku mbili kuendesha kwa umbali wa kilomita 115. Masindano ambayo yanawapa ushindi timu ya Warriors ambao wametumia masaa matano na dakika 28
 Mshindi wakwanza wa mashindano ya kuendesha baiskeli  ya   Rift Valley Odyssey  Sophia Husseni ya liyofanyika  jijini arusha  DEC  Jijini Arusha
Washiriki wa mashindano ya baiskeliya  Rift Valley Odyssey  yaliyofanyika  jijini arusha ambapo wachezaji toka ndani nan je ya nchi wameshirikai kwa takriban siku mbili kuendesha kwa umbali wa kilomita 115
 Mkurugenzi wa 6degrees Simone Paine akizungumza na washiriki wa shindano hilo.
Mshindi wa kwanza wa mashindano ya kuendesha baiskeli  ya   Rift Valley Odyssey  Sophia Husseni

AWARD WINNING INTERNATIONAL TANZANIAN FILM, "GOING BONGO" IN DAR ES SALAAM THEATERS FROM DECEMBER 11TH, 2015

$
0
0

Tarehe 11 Desemba, 2015, filamu iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa, “Going Bongo” itaanza kuonyeshwa katika jumba la sinema la Cinemax Century lililopo Mlimani City katika jiji la Dar-es-sallam. 
Filamu hiyo ambayo imetengenezwa Tanzania and katika jiji la Los Angeles kule Marekani inamhusu daktari wa kimarekani anayekuja kimakosa kufanya kazi Tanzania kwa muda wa mwezi mmoja. 
Filamu hii imekwishajishindia tuzo mbali mbali za kimataifa ikiwemo, filamu bora ya Afrika Mashariki (ZIFF) na filamu bora ya kimataifa (BEFFTA). 
Mwandishi/Mtayarishaji/Muigizaji wa filamu hiyo Ernest Rwandalla (Ernest Napoleon) amesema kuwa tiketi za maonyesho ya saa 12 jioni, saa 2 na saa 4 usiku za Ijumaa tarehe 11 Desemba, zimeshaanza kuuzwa pale Mlimani City. Going Bongo ni filamu inayotararijiwa kufanya vizuri katika majumba ya sinema ambayo yamekuwa yakionyesha zaidi filamu za nje.


For  more  inquiries  please  contact:


Mr. Ernest-TEL +46704070827(Whats app)

Da June-TEL 0756735461


GASTON TEL 0715241177

Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images