Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110176 articles
Browse latest View live

DIRA YA DUNIA IJUMAA 04.12.2015


Ngoma azipendazo Ankal: Nyimbo kibao za Moro Jazz na Mbaraka Mwinshehe Mwaruka

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abaas Mwinyi Atimiza Ahadi Zake kwa Kituo cha Afya Fuoni kwa Kukabidhi Dawa na Masinki ya Vyoo kwa Kituo Hicho.

$
0
0
Daktari Dhamana wa Kituo cha Afya Fuoni Said Fadhili Abass akizungumza wakati wa mkutano huo na Mbunge wa Jimbo la fuoni na kumshukuru kwa msaada wake huo kwa Kituo chao. na kusema dawa hizo zitatumika kwa wananchi wa Jimbo hilo wanaofika kituoni hapa kupata huduma mbalimbali za Afya.  
Wauguzi wa Kituo cha Afya Fuoni wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Fuoni Mhe Abass Mwinyi wakati akizungumza na Wafanyakazi hao katika ziara yake kutembelea Kituo hicho na kukabidhi madawa kwa ajili ya Wananchi wanaofika kupata huduma kituoni hapo.
Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassaan Mwinyi akimkabidhi fedha shilingi milioni moja Dakt. Dhamani wa Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar Said Fadhil Abass, kwa ajili ya kutatua makero zinazokikabili kituo hicho cha Afya Fuoni ili kufanya kazi zao kwa kuwahudumia Wananchi kwa ufanisi zaidi.
Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassaan Mwinyi akimkabidhi madawa Dakt. Dhamani wa Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar Said Fadhil Abass, kwa ajili ya matumizi ya kituo hicho kinachotowa huduma mbalimbali kwa Wananchi wa Fuoni zikiwemo za kuzalisha kinamama na upigaji wa vipimo vya utra sound katika kituo hicho na kulaza wagonjwa. 
Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassaan Mwinyi akimkabidhi vifaa kwa akili ya vyoo vya kituo hicho Dakt. Dhamani wa Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar Said Fadhil Abass na kulia Muuguzi wa Afya ya Jamii Kituoni hapo Mwaka Pandu Makame.

5th December #swahilifashionweek

$
0
0
     
SWAHILI FASHION WEEK
P.O.Box 10684,
Dar es Salaam,
United Republic of Tanzania
LIKETWEETFORWARD
You received this email as you are a supporter of Art, Culture , Fashion & Lifestyle.

SIMU TV: DONDOO ZA MAGAZETI YA LEO

Balozi Seif Ali Iddi aifariji familia ya marehemu Koplo Yesaya Mwakambi

$
0
0
Jeshi la Polisi Nchini limeelezea faraja yake kutokana na mfumo wa Viongozi wa Kitaifa kuonyesha muelekeo wa kuwajali watumishi wao kutoka Taasisi tofauti za Umma na hata binafsi lakini zaidi wake watumishi wa ngazi ya chini. 
Afisa wa Polisi S.P Zakaria Benard alitoa faraja hizo kwa niaba ya Jeshi la Polisi wakati akitoa shukrani za Jeshi hilo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika katika Kata ya Goba Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam kutoa mkono wa pole pamoja na kuifariji Familia ya Koplo Yesaya Mwakambi aliyefariki Dunia kwa ajali ya Piki pili Ubungo Jijini Dar es salaam. 
Koplo Yesaya ni miongoni mwa Askari wa Usalama Bara barani wa Jeshi la Polisi Nchini wanaowajibika kuiongoza Misafara ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa akiwemo wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipata ajali akiwa kazini mwezi Mmoja na nusu uliopita . 
S.P Zakaria Benard alisema kitendo cha Viongozi hao wa Kitaifa kuungana na Watumishi wao wa ngazi ya chini kimeonyesha upendo, huruma na moja ya njia itakayotowa mapenzi ya dhati kati ya pande hizo mbili kuendelea kushirikiana katika ujenzi wa Taifa. 
Kamanda Zakaria alimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwa uamuzi wake wa kutenga muda kwa lengo la kuifariji Familia ya Koplo Yesaya. 
Akitoa shukrani kwa niaba ya wanafamilia wa Koplo huyo Mchungaji Isaya Isaleka aliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuisadia Familia ya Marehemu Koplo Yesaya Mwakambi ili iweze kuwa na nguvu za kukabiliana na maisha yao ya baadaye. 
Mchungaji Isaleka alisema katika uhai wake tayari alikuwa aameshaanza kujenga hatma ya familia yake ya watoto wawili wadogo kwa kuwawekea vitega uchumi alivyovianzisha kwa nia ya kuwasaidia hapo baadaye lakini kukatika kwa uhai wa Kijana huyo pia umeenda sambamba na kusita kuendelea kwa vitega uchumi hivyo. 
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiifariji Familia hiyo inayoongozwa na Mke wa Marehemu Bibi Wema Sanga alisema familia ilikuwa ikimpenda sana Marehemu, lakini Mwenyezi Muungu alimpenda zaidi na ndio maana akaamua kumrejesha katika himaya yake ya milele. 
Balozi Seif aliitaka familia ya marehemu Yesaya hasa Mkewe Mama wa watoto wawili Bibi Wema Sanga kwa kuwa na moyo wa subira katika kipindi hichi kifupi walichoondokewa na Mpendwa wao.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seigf Ali Iddi akikabidhi Ubani na Kutoa Pole kwa Mke wa Koplo Yesaya Mwakambi Bibi Wema  Sanga ambaye Mumewe alipata ajali mwezi Mmoja uliopita akiwa kazini kuiongoza misafara ya Viongozi wa Kitaifa Ubungo Mjini Dar es salaam. Balozi Seif ni miongoni mwa Viongozi waliokuwa wakioongozwa na Askari huyo  wa Jeshi la Polisi Marehemu Yesaya wakati wa safari zake awapo Mjini Dar es salaam.
 Mke wa Marehemu Koplo Yesaya Bibi Wema Sanya wa kwanza kutoka kulia akiwa na Dada yake pamoja na watoto wake wawili wakati wakipewa mkono wa pole na  Balozi Seif aliyefika kwenye Kata yao ya  Goba Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam kuwafariji baada ya kufiwa na mpendwa wao.
 Kiongozi wa Familia ya Marehemu Koplo Yesaya  Mwakambi  Mchungaji Isaya Isaleka akitoa ushauri  kwa Serikali Kuu kuisaidia Familia ya Marehemu Koplo Yesaya ambae ameacha familia ya Watoto wadogo.

Afisa wa Polisi S.P Zakaria Benard akitoa shukrani kwa niaba ya Jeshi la Polisi kwa uamuzi wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  wa kuifariji familia ya askari wa ngazi ya chini ya Jeshi la Polisi Nchini Marehemu Yesaya aliyefariki kwa ajali ya Piki piki akiwa kazini. Picha na – OMPR – ZNZ.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akutana na Rais wa China, atunukiwa Heshima ya Companion Award na Commonwealth Partnership for Technological Management (CPTM), aongoza ujumbe wa AU Comoro

$
0
0
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na Rais wa China, Mheshimiwa Xi Jinping pembezoni mwa Mkutano wa Africa na China unaofanyika Johannesburg , Afrika Kusini. Waliosimama pembeni ni Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Tanzania, Rais Thomas Boni Yayi wa Benin, Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.

----------------------------------
Taasisi ya Commonwealth Partnership for Technological Management (CPTM) inayojishughulisha na kukuza ushirikiano katika nyanja ya sayansi na teknolojia kwa nchi za Jumuiya ya Madola, imemtunuku Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, heshima ya Juu ya CPTM (Companion Award) kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha ukuaji wa matumizi ya sayansi na teknolojia ikiwemo matumizi ya huduma za fedha kwa njia ya simu. Rais Mstaafu Kikwete, alikabidhiwa Tuzo hiyo tarehe 1 Desemba, 2015. 
Taasisi hiyo yenye makao makuu yake London ndio inayoendesha Midahalo ya Kimataifa maarufu kama Smart Partnership Dialogue. Mkutano wa mwisho wa aina hiyo ulifanyika Dar es Salaam mwaka 2013 ukiwa Na kali mbiu ya "Kutumia Teknolojia Kuchochea Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Barani Afrika". 
Rais  Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Cheti cha Kumtunuku Yeshima ya Juu ya CPTM (Companion Award). Aliyesimama kushoto kwa Rais Mstaafu ni Dkt. Tan Sri Omar, Mwenyekiti wa Bose ya Wakurugenzi wa CPTM na pembeni yake ni Dkt. Mihaela Smith, CEO wa CPTM. 

Tuzo hiyo imetolewa wakati wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPTM ambao uliambatana na maadhimisho ya Miaka 20 ya Taasisi hiyo jijini London
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa neno la shukurani baada ya kutunukiwa tuzo ya  heshima ya Juu ya CPTM (Companion Award) wakati wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPTM ambao uliambatana na maadhimisho ya Miaka 20 ya Taasisi hiyo jijini London.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliteuliwa na Mama Nkosamana Dlamini Zuma kuwa Mjumbe Maalum wa AU Comoro.  Mhe. Kikwete alikwenda Moroni, Comoro tarehe 30 Novemba, 2015 kufanya mikutano na wadau wa siasa kuhusu mgogoro wa kisiasa unaonukia nchini humo kuhusu mchakato wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utakaofanyika April, 2016


UN-ICTR Yamaliza Kazi yake Arusha, mpiganaji Danford Mpumilwa ashukuru kuhitimisha ngwe yake salama na kwa ufanisi

$
0
0
Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughullikia Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (UN-ICTR) hivi majuzi imefanya sherehe za kumaliza kazi zake baada ya miaka 21 toka ilipoanzishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. 
Sherehe hizo zilikuwa ni pamoja na mkutano mkubwa uliowaleta watu mashuhuri kutoka pande zote duniani na viongozi wa UN kutoka New York, na uzinduzi wa Bustani ya Amani -Peace Park - mjini Arusha.
Mahakama hiyo iliwakamata na kuwahukumu watu wazito wa Rwanda 83 wakiwemo Mawaziri zaidi ya kumi wakiongozwa na Waziri Mkuu; Makamanda wa Polisi na Jeshi; Wakuu wa Mikoa; Waandishi wa Habari Waandamizi; Viongozi wa Kidini; na Wafanya Biashara Maarufu. Milango ya mahakama hiyo sasa itafungwa tarehe 31 Desemba 2015. 
Kwenye picha hapo mpiganaji Danford Mpumilwa, ambaye kwa miaka yote hiyo amekuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari cha mahakama hiyo, ameshukuru kwa kumaliza ngwe yake salama salimi na kwa ufanisi mkubwa wa kiweledi, na hapa anajumuika na wageni mbalimbali kwenye sherehe hizo.
 Mpiganaji Danford Mpumilwa, ambaye kwa miaka yote hiyo amekuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari cha  UN-ICTR , akipozi katika mnara was Bustani ya Amani (Peace Park) mjini Arusha.
Mpiganaji Danford Mpumilwa akiwa na Jaji Mkuu Othman Chande na Balozi Baraka Luvanda (kushoto) 
Mpiganaji Danford Mpumilwa akiwa na Rais wa Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika Jaji Augustino Ramadhani (kushoto) na Jaji wa UN-ICTR William Sekule (katikati).

Balozi Seif Ali Iddi akizawdia vifaa vya michezo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki

$
0
0
Mwenyekiti wa Mtandao wa Afya na Elimu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Bibi Kokushubila Kairuk alisema kitendo cha baadhi ya Viongozi na washirika wa maendeleo kuendelea kuunga mkono Taasisi za Umma za zile binafsi huleta faraja katika Jamii.
Bibi Kokushubila alieleza hayo wakati akipokea msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Mtaa wa Mikocheni Mjini Dar es salaam. 
Vifaa hivyo vikiwa ni pamoja na Seti ya Jezi, Mipira ya kandanda na Vikapu, soksi, Bukta pamoja na sare za mlinda Mlango kwa ajili ya Timu ya Chuo Kikuu hicho viliwasilishwa Chuoni hapo na Daktari wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr.Juma Mbwana Mambi kwa niaba yake vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Milioni Moja. 
Bibi Kokushubila alisema michezo ni moja ya eneo linalounganisha jamii hasa Vijana ambayo linahitaji kupewa msukumo kwa vile huchangamsha Vinjana hao Kiakili na kimawazo. Mwenyekiti huyo wa Mtandao wa Afya na Elimu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki alimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa msaada wake huo ambao umeleta faraja kwa Wanafunzi sambamba na Uongozi wa Chuo hicho.
Bibi Kokushubila alisisitiza umuhimu wa kuendelezwa kwa ushirikiano baina ya Taasisi husika na washirika wa sekta ya Michezo ili kuona fani hiyo inapata nguvu zaidi kwa vile tayari imeshaonyesha muelekeo wa kutoa ajira kwa kundi kubwa la Vijana. 
Mapema akiwasilisha msaada huo wa Vifaa vya Michezo Dr. Juma Mbwana Mambi kwa Niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Mh. Balozi Seif aliahidi kuendelea kusaidia sekta ya michezo kutokana na umuhimu wake kwa hivi sasa. Dr. Mambi alisema juhudi zitaendelea kuchukuliwa na Mh. Balozi ili kuona michezo Nchini inadumishwa na kuendelezwa zaidi kwa faida na ustawi wa Jamii yote. 
Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki kiliopo Mikocheni Mjini Dar es salaam mbali ya kutoa Taaluma ya Elimu ya Afya pia kinadumisha michezo kwa nia ya kuwajenga afya wanafunzi na walimu wake.
 Daktari wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Juma Mbwana Mambi akikabidhi Vifaa vya Michezo kwa Uongozi wa Chuo Kikuu cha Mtandao wa Elimu na Afya cha Kumbu kumbu ya Hubert Kairuki vilivyotolewa msaada na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Makao Makuu ya Chuo hicho Mikocheni Mjini Dar es salaam. Wa kwanza kutoka Kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Afya na Elimu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Bibi Kokushubila Kairuk na kati kati ni Mkuu wa Kitengo cha Michezo wa Chuo hicho Mwalimu Alphage Liwa.
Dr. Mambi akikabidhi pia Kikombe ambacho kinaweza kusaidia mashindano ya Timu za Wanafunzi wa mikupuo tofauti wa chuo hicho cha Kumbu kumbu ya Hubert Kairuki.
Bibi Kokushubila Kairuk wa kwanza kutoka kushoto ambae ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Afya na Elimu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki akitoa shukrani kwa Balozi Seif kutokana na mchango wake chuoni hapo katika sekta ya Michezo. Picha na –OMPR – ZNZ.

SIMU TV: Wachina Wawili Wafikishwa Mahakamani Dar es salaam

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA MFUKO WA PPF

USIKOSE KUCHEKI MECHI ZA LIGI KUU YA HISPANIA KUPITIA DSTV LEO

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA TANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA NA CHINA, JIJINI JOHANNESBURG

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan, akisalimiana Mwambata wa Kijeshi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Brig. Gen Ibrahim A. Kimario, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver Tambo jijini Johanesburg kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan, akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo jijini Johannesburg  kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa China, Xi Jinping, wakati wa Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika  jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika  jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
 Baadhi ya washiriki katika Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo  jijini Johannesburg. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi, walipokutana kwenye ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika  jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika baada ya ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyikajijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

TGDC NA KAMPUNI YA TOSHIBA WATILIANA SAINI MKATABA WA MAELEWANO (MOU) WA UTAFUTAJI WA NISHATI YA JOTOARDHI

$
0
0
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
 Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) pamoja na Kampuni ya TOSHIBA ya nchini Japan zimetiliana saini Mkataba wa Maelewano wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi.
 Utiaji saini wa mkataba huo umefanyika Desemba 4, 2015 Jijini Dar es Salaam katika Ofisi za TGDC ambapo hatua hiyo itaiwezesha TGDC kuweza kupata msaada wa kitaalam ambao utaliwezesha shirika hilo kuweza kuchimba ardhini kwa lengo la kupata mvuke utakaoweza kuzalisha umeme.
 Akiongea ofisini kwake, Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe amesema kuwa kupitia Serikali ya Japan hususani Shirika la Maendeleo Japan (JICA), Kampuni ya TOSHIBA watasaidia kuomba ufadhili wa Serikali yao ili kuweza kuendeleza ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme pamoja na matumizi mengine yanayoendana na nishati hiyo.
 “Katika utafiti wa nishati ya jotoardhi tunahitaji watu wenye elimu na uzoefu na ujuzi wa kutosha, miongoni mwa makubaliano ndani ya mkataba huu tuliosaini leo ni wafanyakazi wetu kadhaa kuwapeleka nchini Japan kwenye vyuo vyao ili kuweza kupata mafunzo ya darasani na kutembelea maeneo ambayo Japan wana vituo vya jotoardhi ili wapate ujuzi wa kufanya kazi na Wajapan na kutuletea ujuzi huo hapa nchini”, alisema Njombe.
 Aidha, ameeleza kuwa kupitia ushirkiano huo na Serikali ya Awamu ya Tano Japan itaendelea kuisadia Tanzania katika kuendeleza nishati ya jotoardhi kwakuwa ni nishati yenye tija katika kutimiza ndoto za Tanzania kwa kuifanya kuwa nchi yenye kipato cha kati kufikia mwaka 2020.
Meneja Mkuu Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe (kushoto) pamoja na Mtaalamu Mkuu toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara wakiweka saini Mkataba wa wa Maelewano (MOU) wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za TGDC zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Meneja Mkuu Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe (kushoto) pamoja na Mtaalamu Mkuu toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara wakikabidhiana Mkataba wa Maelewano (MOU) wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za TGDC zilizopo Jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China

$
0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, na Rais Mstaafu wa awamu ya Tano, Dkt. Jakaya Kikwete, wakiangalia moja ya Ndege ya Kivita ya mfano, wakati walipotembelea Mabanda ya maonesho ya Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, uliofanyika Jijini Johannesburg Afrika ya Kusini jana.  Dkt. Jakaya Kikwete alihudhuria mkutano huo kama Rais Mstaafu mwalikwa. Mkutano huo unamalizika leo Dec 5, 2015.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika ukumbi wa mkutano wakati akijiandaa kuhutubia kwenye Mkutano mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, unaomalizika leo jijini Johannesburg Afrika ya Kusini

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Rutageruka Mulamula, kabla ya kuhutubia katika Mkutano mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, unaomalizika leo jijini Johannesburg Afrika ya Kusini. Picha na OMR

RED AVENUE PARTY RELOADED DESEMBA 26, 2015

Habari njema: Michango ya wasamaria wema yafanikisha Dada Joyce wa Mbeya kuwasili Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu

$
0
0
Ndugu Wasamaria wema,

Tunapenda  kutumia fursa hii kuwapa updates kuhusu dada Joyce Mwambepo, mkaazi wa Sinde jijini Mbeya mwenye umri wa miaka 27 ambaye anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na mwanaye mwenye umri wa miaka 4.


Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambalo dereva wake hakusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya ambako inasemekana alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu kwa kukosa fedha. Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili,  hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya baada ya kukosa pesa za matibabu.

Baada ya mwanahabari Deo Kakuru wa Mbeya kumgundua na kufanya juhudi za kutoa taarifa za dada Joyce katika mitandao mbalimbali, wasamaria wema wengi  wa ndani na nje ya nchi  wakaguswa na kuchangia. 

Mungu mkubwa, kiasi kilichopatikana (kiasi cha 3.2m/-) kimewezesha dada Joyce kupelekwa Dar es salaam toka Mbeya kwa ndege ya Fast Jet Alhamisi iliyopita na moja kwa moja kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alipokelewa katika kitengo cha mifupa cha MOI na kupatiwa kitanda katika wodi mpya ijulikanayo kama Wodi ya Magufuli, ghorofa ya tatu chumba cha kwanza kulia. 
Cha kufurahisha ni kwamba Joyce aliweza kukaa kwenye kiti cha kusukumwa na hata kwenye ndege aliketi kama kawaida, zoezi ambalo hata yeye anasema limemsaidia kwani kwa mara ya kwanza hivi sasa ganzi miguuni inapotea taratibu na ukimgusa anahisi mguso tofauti na ilivyokuwa awali.

Daktari bingwa ameshaonana naye na kumpa matumaini ya kupona, hasa sehemu ya chini ya uti wa mgongo wake ambao inasemekana una matatizo yaliyopelekea kubana  mishipa ya fahamu na kufanya miguu ipooze. Zoezi linalosubiriwa kwa sasa ni kupatiwa vipimo vya MRI ili kubaini kiufasaha tatizo lake na hatimaye kupatiwa matibabu. Zoezi hili linatarajiwa kufanyika wakati wowote kuanzia sasa.


Mpiganaji Deo Kakuru amesharejea Mbeya na kijiti cha kumwangalia dada Joyce amekabidhiwa Ankal ambaye anaomba Wasamaria wema waendelee kumuombea na kumsaidia kwa hali na mali dada huyu ambaye ni yatima.



Kwa bahati njema Ankal alikutana na kuongea na Msamaria mwingine aitwaye Mama Rozi ambaye  anamuuguza mama yake mzazi aliyelazwa  wodi moja na dada Joyce. Msamaria huyu amekubali kumsaidia dada Joyce kwa chakula na pia kumsaidia usafi maana hapo kitandani hawezi kuondoka.
Mungu kweli ni mkubwa. Dada Joyce anatabasamu na kuongea vizuri tu. Anatoa shukurani sana kwa wote waliomsaidia na wanaoendelea kumsaidia. Anasema hana cha kuwalipa ila kusema ASANTE SANA na anamwomba Mola Muumba awazidishie pale patapopungua. Ameomba anayeweza kumtembelea atafurahi sana maana hana ndugu hapa Dar es salaam.

Pia anawashukuru sana madaktari waliomhudumia vyema katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ambao amesema hatowasahau kwa msaada wao.



 Ankal amejitolea kuendelea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba+255 754 271266 kwa jina la Ankal.
AU mratibu-mwenza  Deo Kakuru Msimu

Pia unaweza kuwasiliana moja 
kwa moja na dada Joyce kwa namba hiyo na atafurahi


ukimsalimia ama hata kumtupia kitu kwenye Mpesa yake.
MPIGIE +255 768 084897

 Mpiganaji Deo Kakuru akiwa na dada Joyce ndani ya FastJet wakitoka Mbeya keuelekea Dar es salaam 
 Dada Joyce akiwa ameketi kwa utulivu kwenye siti yake ndani ya ndege
 Mpiganaji Deo Kkuru akiwa na dada Joyce mara baada ya kuwasili  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam
 Msamaria mwema Mama Rozi akimhudumia dada Joyce akiwa kitandani kwake Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa cha MOI katika wodi ijulikanayo kama Wodi ya Magufuli ghorofa ya tatu

Dada Joyce akiwa wodini Moi


Historia Ya Dkt. Magufuli Kazini

SPANISH CULINARY WEEKEND

Viewing all 110176 articles
Browse latest View live




Latest Images