Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

SIMU TV: UCHAMBUZI WA MAGAZETI LEO

0
0


CH10: Magufuli aiteka dunia,madudu mengine yaibuka,hofu bandarini,Magufuli awapa hofu wapinzani, Fuatilia uchambuzi wa magazeti ya leo. https://youtu.be/a9hBxJjFoKI

AZAM TV: Simba yasajili watatu, Manchester city yazama, Arsenal yapeta, Straika mpya Yanga balaa, Manchester United yabwanwa mbavu. Fuatilia uchambuzi wa magazeti ya michezo. https://youtu.be/RGboj9YzVcg



Mzumbe yawataka watanzania kuwekeza elimu kwa vijana

0
0
Watanzania wametakiwa kuwekeza kwa kuwapatia vijana wao elimu ya juu ili kuwawezesha kuwa na maarifa yatakayowasaidia katika maisha yao na kutoa mchango kwa taifa. 
 Akizungumza katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Kaimu Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Josephat Itika alisema elimu bora ndio njia ambayo itaweza kuwezesha vijana kufanikiwa na taifa kupata maendeleo endelevu. 
 “Elimu ndio chachu ya kweli ya maendeleo, ni lazima wazazi na walezi kuzingatia hili,” alisema Prof. Itika mwishoni mwa wiki. 
 Aliongeza kusema kuwa Mzumbe imekuwa kielelezo na kitovu cha elimu bora katika kutoa mchango wake kwa taifa kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Katika Mahafali hayo, Mkuu wa Chuo hicho, Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta aliwatunuku wahitimu mbalimbali katika Kampasi Kuu Mzumbe baada ya kuhitimu masomo yao. 
 Jumla ya wahitimu wote walikuwa 1990; wanawake wakiwa 900 sawa na asilimia 45.2 na wanaume 1090 sawa na asiliamia 54.8. 
 Pamoja na changamoto zilizopo, Profesa Itika alisema chuo kimepata mafanikio mengi na kinazidi kuimarisha miradi ya miundombinu yake, rasirimali watu na vitendea kazi kwa kampsi na vituo vyake vyote. 
 Alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni ufinyu wa bajeti ambao unaathiri uendeshaji wa shughuli za kawaida za chuo na pia shughuli za ukarabati wa miundombinu. Pia kuna uchakavu wa miundombinu ikiwemo mabweni, kumbi za mihadhara, madarasa na nyumba za wafanyakazi na upungufu wa huduma ya maji. 
 Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Profesa Daniel Mkude alisema chuo kitaendelea kutekeleza kwa uadilifu mkubwa sera, mikakati na maelekezo ya serikali ili kiendelee kuwa kitovu cha elimu bora, hasa kuendelea kuweka mkazo katika fani za utawala na menejimenti. Pia aliwapongeza wahitimu kwa kusoma kwa bidii hadi kufikia hatua ya kuhitimu na kuwataka kwenda kuwa mabalozi wazuri wa chuo chao katika kazi. 
 “Mkatumikie vyema stadi mlizopata na epukeni kujitumbukiza katika vitendo vya rushwa, uvivu, uzembe, kufanya kazi kwa mazoea na mkawe mabalozi wetu wazuri,” alisema. 
 Profesa Mkude aliwakumbusha wahitimu hao kufahamu kuwa elimu haina mwisho na kwamba wana wajibu wa kuendelea kusoma machapisho, vitabu na makala mbalimbali ili kuzidi kupata maarifa na kutoa mchango wao kwa jamii.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta (katikati) akimtunukia Shahada ya Udaktari wa Falsafa, Bahati Ilembo katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Mzumbe mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.  Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Profesa Daniel Mkude na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Josephat Itika (kushoto).
 Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mstafu Barnabas Samatta, akimtunukia Shahada ya Udaktari wa Falsafa, Thobias Nsindagi katika mahafali ya 14 ya Chuo hicho mjini Morogoro mwishoni mwa wiki.  Wa pili kushoto ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Josephat Itika na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Profesa George Shumbusho (kushoto).
 Wahitimu wa mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Mzumbe wakifurahia kutunukiwa shahada mbalimbali wakati wa mahafali ya 14 ya Chuo hicho mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
Wahitimu wa mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Mzumbe wakifurahia kutunukiwa shahada mbalimbali wakati wa mahafali ya 14 ya Chuo hicho mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.

WATUMISHI WAANDAMIZI SABA WA TANESCO WAFUKUZWA KAZI KWA TUHUMA MBALIMBALI

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felschimi Mramba akizungumza na waandishi habari juu ya mikakati mbalimbali ya uzalishaji umeme katika mazungumzo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uzalishaji na Huduma kwa Mteja), Mhandisi Sophia Mgonja, Kushoto ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji Umeme, Nazir Kachwamba, kushoto kutoka kulia ni Meneja Uhusiano Adrian Severine.
Waandishi habari wakimisikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felschimi Mramba leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) limewafukuzisha kazi watumishi waandamizi wa Tanesco upande wa maneja na wahasibu kutokana na ubadhirifu wa fedha katika utumishi wao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felschimi Mramba amesema kuwa shirika halitaweza kuwaacha watendaji wakawa wanafanya kazi kwa rushwa wakati wanalipwa mishahara.

Amesema wataendelea kuchukua hatua kwa watendaji wote watakabainika kufanya udanganyifu au kutoa lugha zisifaa kwa wateja na wakati mwingine kuomba fedha kwa huduma ambazo ni haki ya mwananchi kupata.

Mramba amesema Tanesco imeongeza uzalishaji wa umeme unaotumia gesi megawati 300  sawa na asilimia 115  na kufanya kuwa na umeme wa uhakika huku miradi mingi ikiendelea kufanyika.

Amesema  wanatarajia kupata megawati 240 kutoka Kinyerezi namba mbili  wakati wowote  na kufanya shirika kuwa na umeme wa uhakika.

Aidha amesema wakati wa suala miundombinu likifanyiwa kazi wananchi wawe wavumilivu wa kukatika umeme katokana na kuboresha miundombinu hiyo.

Aliongeza kuwa wanaotaka kufanya kazi na Tanesco kwa kupata nguzo lazima wazalishe nguzo zenye ubora wa kuweza kuhimili kwa muda mrefu bila kuanguka kuanguka.

VODACOM YAENDELEA KUNOGESHA SWAHILI FASHION WEEK

0
0
 Mwanamitindo akipita mbele ya watazamaji katika onesho la Swahili Fashion Week lililomalizika jana katika hoteli ya Sea Cliff, akiwa amevalia mavazi ya lebo ya Kibout ya mbunifu wa hapa nchini, onesho hilo limedhaminiwa na Kampuni ya simu ya Vodacom.
 Mbunifu wa mavazi wa lebo la Kibout Evamary Sospeter de Block akipita mbele ya watazamaji jana baada ya kuonesha mavazi yake katiak oneso la Swahili Fashion Week lililomalizika jana katika hoteli ya Sea Cliff chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya Vodacom.
 Wanamitindo wakionesha vazi kutoka lebo ya Jina Langu Ni wakati wa onesho la mavazi la Swahili Fashion Week lililomalizika jana chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya Vodacom.
 Wanamitindo wakionesha vazi la mbunifu wa mavazi Kiarasheba katika siku ya pili ya onesho la siku tatu la Swahili Fashion lililomalizika jana chini ya Udhamini wa kampuni ya simu ya Vodacom.
 Wanamitindo wakionesha mavazi ya lebo ya PSJ Couture katika siku ya pili ya onesho la mavazi la Swahili Fashion Week lililofanyika katika hoteli ya Sea Cliff chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania.
Wabunifu wa mavazi wanaomiliki lebo ya Bobbins & Sief wakipita baada ya kuonesha mavazi yao katika onesho la Swahili Fashion Week lililomalizika jana likiwa limedhaminiwa na kampuni ya simu ya Vodacom.

TAASISI YA SEKTA BINAFSI, BOT, BENKI YA DUNIA WAJADILI MFUMO WA MIRADI YA PPP.

0
0
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk Gideon Kaunda (kulia) akizungumza katika hafla ya ufungaji wa mkutano wa siku mbili kuhusu ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ya umma (PPP), uliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), ikishirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Benki ya Dunia. Kushoto ni Kamisha wa PPP kutoka Wizara ya Fedha, Dk. Francis Mhilu. 
 Kamishna wa Sera ya Ushirikiano wa Sekta Binafsi ya Umma (PPP) kutoka Wizara ya Fedha, Dk. Francis Mhilu (kulia) akiagana na Mtaalamu wa uchumi kutoka Benki ya Dunia, Jeffrey Delmon baada ya kumalizika kwa mkutano wa siku mbili kuhusu ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya ubia sekta binafsi na ya umma (PPP), uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki uliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), ikishirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Benki ya Dunia. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk Gideon Kaunda.

 Washiriki wakipiga picha ya kumbukumbu mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo uliokuwa ukijadili ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ya umma (PPP), uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

WENYEVITI WA CCM MIKOA WAPONGEZA RAIS DK. JOHN MAGUFULI KWA KASI YAKE

0
0
 Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ramadhan Madabida akizungumza na waandishi wa habari (hayupo pichani) juu ya kazi inayofanywa na Rais Dk. John Magufuli leo jijini Dar es Salaam.
 Waandishi wa habari wakimfatilia Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,Ramadhan Madabida leo jijni Dar es Salaam

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WENYEVITI wa Mikoa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamesema kuwa kasi ya Rais Dk. John Joseph Pombe Magufuli kwa kuwachukulia hatua watendaji wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao, wanapongeza kwa kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ,Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wawenyeviti wa Mikoa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida amesema kuwa wenyeviti wanapongeza kwa hatua hizo ambazo amezifanya Rais Dk. John Magufuli.

Amesema watu walikuwa wanatoa huduma isiyo bora kwa wananchi hivyo kila mtu kwa nafasi yake afanye kazi yake kwa mujibu wa sharia

Madabida amesema kwa kasi hiyo wako tayari na maamzi yeyote ambayo anaweza kuyatoa kwa viongozi wa CCM ambao hawakuweza kufuata utaratibu.

Aidha amesema wananchi waunge juhudi ambazo Rais John Joseph Magufuli anafanya katika kuweza kila mtu aweze kuwajibika ipasavyo kuwahudumia wananchi wake.

Ameongeza kuwa Wenyeviti wataendelea kuwa pamoja na Rais katika majumu yake ya kuhakikisha nchi inakuwa na watendaji wanaojituma na kila nyakati ina dhana yake.

SPANISH CULINARY WEEKEND YA SIKU TATU YAZINDULIWA JIJINI DAR.

0
0
Balozi wa Hispania hapa nchini, H.E Felix Costaldes akizungumza wakati wa uzinduzi wa Spanish Culinary week ambayo imezinduliwa Ijumaa usiku  katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Habari Beach jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Balozi wa Hispania hapa nchini, H.E Felix Costaldes akikata keki kuashiria uzinduzi wa Spanish Culinary week iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Watumbuizaji wakitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa  Spanish Culinary week jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wakiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya kuzindua  Spanish Culinary week jijini Dar es Salaam.

YAMOTO BENDI WAINGIA TUZO ZA KORA

0
0
Waimbaji wa yamoto bendi wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Mwandishi Mwetu
WAKATI jana wakiendelea kutoa burudani katika mji wa Washington DC, Bendi ya Yamoto, imeingia katika kuwania tuzo za Kora 2016, ikiingia katika kipengele cha Most Promising Male Artist Of Africa.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Said Fella, alisema kwanza anamshukuru Mungu vijana wake juzi usiku walikuwa na onesho lao la pili lililofanyika Washington DC na kuweza kufanya vizuri, lakini la pili kuingia katik tuzo za Kora. 

Fella ambaye ni diwani wa Kata ya Kilungule alisema ni kitu kikubwa sana kwake kwa bendi yake kuingia katika tuzo za Kimataifa.

Alisema kuingiaa kwa vijana wake katika tuzo hizo ni kitu kikubwa sana na kinazidi kuipandisha bendi yake ambayo sasa ipo nchini Marekani kwa ziara ya maonesho maalum.

"Ni kitu kikubwa sana kinazidi kutupandisha kutoka sehemu moja kwenda kwingine, tunaamini mwenyezi Mungu atatusimamia tuweze kupata kwa mashabiki wetu kuliona hili na kutuunga mkono katika kupiga kura"alisema Fella. 

Kwa upande wa ziara ya bendi yake nchini Marekani alisema vijana hao watafanya onesho la mwisho Desemba 12, katika mji wa Houston na baadae kurejea nchini kwa kazi zao nyingine. 

Alisema katika onesho la juzi walifanya onesho zuri la aina yake na katika mji wa Washington na kuudhuliwa na mashabiki wengi wa muziki. 

"Onesho letu la juzi lilikuwa zuri sana na limezidi kuongeza hamasa kwa vijana wazidi kujituma na kufanya viuri zaidi katika kuhakikisha wanapata mihaliko kama hii ya kuja nchini kama hizi ambazo nazo tumekuwa na mashabiki wetu"alisema Fella.

PPF YAIBUKA KIDEDE KATIKA UTUNZAJI BORA WA HESABU ZAKE, YATWAA TUZO YA WA HESABU UPANDE WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

0
0

Na K-Vis Media/Khalfan Said.
MFUKO wa Pensheni wa PPF, umeibuka kidedea kwa kutwaa tuzo ya uwasilishaji bora wa hesabu zake katika kipindi cha mwaka 2014.

Katika hafla ya kutoa tuzo kwa taasisi za serikali na za watu binafsi, Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu, NBAA, imetoa tuzo hizo kwa makampuni na taasisi mbalimbali nchini, ambapo kwa upande wa kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, PPF ndiyo iliibuka ya kwanza ambapo Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko huo, Bw. Martin Mmari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw. William Erio, alipokea tuzo hiyo kutoka kwa mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Khamis Mwinyimvua. Pichani Bw. Mmari akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Khamisi Mwinyimvua. 
(Picha na K-Vis Media/Khalfan Said)
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Martin Mmari, (katikati), akiwa amekamata tuzo wakati wa kupiga picha na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko huo kwenye hafla ya kutolewa tuzo ya taasisi iliyowasilisha taarifa za mahesabu za mwaka 2014 kwa kuzingatia taratibu na kanuni za mahesabu kwenye kituo cha mikutano cha Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu NBAA, huko Bunju nje kidoto ya jiji la Dar es Salaam, Desemba 5, 2015. PPF ilishika nafasi ya kwanza katika kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Tuzo hizo hutolewa na NBAA.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

HEPI BESDEI YA KUZALIWA MTOTO EUNICE EDSON MAGESA.

0
0
Mtoto Eunice Edson Magesa ametimiza miaka mitano. Sisi wazazi wake,majirani wote tunamtakia maisha marefu ya furaha na fanaka katika kila jambo. Happy Birthday dear Eunice!

' Nyumbani Na Diaspora'- Mtanzania Rama Mkeketu, Kutoka Canada Mpaka Kijijini Lulanzi..

Benki ya NMB yashinda nafasi ya kwanza Tuzo za NBAA kwa mabenki Tanzania

0
0
Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya NMB, Veronica Pascal (wa pili kushoto) akipokea tuzo kwa niaba ya NMB toka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dk. Hamisi Mwinyimvua baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa kuwa na hati safi ya taarifa za fedha kwa upande wa mabenki nchini katika ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2014. Tuzo hizo zilitolewa jana Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu Tanzania. Jumla ya makampuni na taasisi 58 zilishiriki katika kinyang'anyiro hicho cha ukaguzi wa taarifa za fedha kwa hiyari.Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya NMB, Veronica Pascal (wa pili kushoto) akipokea tuzo kwa niaba ya NMB toka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dk. Hamisi Mwinyimvua baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa kuwa na hati safi ya taarifa za fedha kwa upande wa mabenki nchini katika ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2014. Tuzo hizo zilitolewa jana Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu Tanzania. Jumla ya makampuni na taasisi 58 zilishiriki katika kinyang'anyiro hicho cha ukaguzi wa taarifa za fedha kwa hiyari.

Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya NMB, Veronica Pascal (wa pili kushoto) akipokea tuzo kwa niaba ya NMB toka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dk. Hamisi Mwinyimvua baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa kuwa na hati safi ya taarifa za fedha kwa upande wa mabenki nchini katika ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2014. Tuzo hizo zilitolewa jana Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu Tanzania. Jumla ya makampuni na taasisi 58 zilishiriki katika kinyang'anyiro hicho cha ukaguzi wa taarifa za fedha kwa hiyari.
Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya NMB, Veronica Pascal (wa pili kushoto) akipokea tuzo kwa niaba ya NMB toka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dk. Hamisi Mwinyimvua baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa kuwa na hati safi ya taarifa za fedha kwa upande wa mabenki nchini katika ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2014. Tuzo hizo zilitolewa jana Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu Tanzania. Jumla ya makampuni na taasisi 58 zilishiriki katika kinyang'anyiro hicho cha ukaguzi wa taarifa za fedha kwa hiyari.


Wawakilishi wa Benki ya NMB, Veronica Pascal (kushoto) akipiga picha ya ukumbusho mara baada ya kupokea tuzo kwa niaba ya NMB baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa kuwa na hati safi ya taarifa za fedha kwa upande wa mabenki nchini katika ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2014. Tuzo hizo zilitolewa jana na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu Tanzania.Wawakilishi wa Benki ya NMB, Veronica Pascal (kushoto) akipiga picha ya ukumbusho mara baada ya kupokea tuzo kwa niaba ya NMB baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa kuwa na hati safi ya taarifa za fedha kwa upande wa mabenki nchini katika ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2014. Tuzo hizo zilitolewa jana na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu Tanzania.Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya NMB, Veronica Pascal (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya wawakilishi kutoka baadhi ya makampuni na taasisi zilizoshiriki kupokea tuzo za washindi wa hati safi za taarifa za fedha kwa makampuni na idara anuai nchini katika ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2014.Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya NMB, Veronica Pascal (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya wawakilishi kutoka baadhi ya makampuni na taasisi zilizoshiriki kupokea tuzo za washindi wa hati safi za taarifa za fedha kwa makampuni na idara anuai nchini katika ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2014.Mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Hamisi Mwinyimvua (kulia) akizungumza katika hafla ya kutoa tuzo kwa makampuni na taasisi zilizofanya vizuri katika ukaguzi wa taarifa za fedha kwa makampuni na idara anuai nchini katika shindano la ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2014. Jumla ya makampuni na taasisi 58 zilishiriki katika kinyang'anyiro hicho cha ukaguzi wa taarifa za fedha kwa hiyari. Mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Hamisi Mwinyimvua (kulia) akizungumza katika hafla ya kutoa tuzo kwa makampuni na taasisi zilizofanya vizuri katika ukaguzi wa taarifa za fedha kwa makampuni na idara anuai nchini katika shindano la ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2014. Jumla ya makampuni na taasisi 58 zilishiriki katika kinyang'anyiro hicho cha ukaguzi wa taarifa za fedha kwa hiyari.

KATIBU MKUU, WIZARA YA ARDHI AFANYA JITIHADA KUBORESHA MABARAZA YA ARDHI NA NYUMBA YA WILAYA

0
0
Katibu Mkuu wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Alphayo J.Kidata, amefanya ziara katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na kufanya maboresho, pamoja na kuahidi maboresho zaidi. 
Mhe. Kidata amefanya ziara hiyo ya ghafla katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya za Kinondoni na Ilala ili kubaini uendeshaji wa kazi katika Mabaraza hayo. Akisomewa ripoti fupi na mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kinondoni, Bw. Yose Mlyambina pamoja na mambo mengine alisema; “Kumekuwa na tatizo la kuhofia usalama wa majalada, kutokana na kuwa na vitasa vibovu katika baadhi ya milango”. 
Aliendelea kueleza baadhi ya matatizo mengine katika baraza hilo ni ukosefu wa umeme, ambao ulihitaji kulipiwa, mafunzo kwa watumishi, kompyuta, gari la kutembelea katika maeneo ya migogoro, uhaba wa watumishi, stationaries na mazingira bora ya kazi. 
 Kwa upande wake msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, Bi.Bahati Mlole alikiri kuwepo kwa matatizo hayo na kumtaka mwenyekiti wa Baraza la Kinondoni kujitahidi kutoa mafunzo muhimu ya awali kwa watumishi wa Baraza hilo, ikiwa ni moja ya njia ya kuboresha utendaji wa kazi katika baraza hilo. Hata hivyo Mhe. Kidata aliahidi kumaliza tatizo la vitasa vibovu kwa kuvinunua yeye mwenyewe kwa mshahara wake, alitoa pia kiasi cha Tsh.100,000 kwa ajili ya malipo ya umeme, alitoa kompyuta mbili ambazo zilikuwa ofisini hapo baada ya kuazikimwa tu kutoka Wizarani. 
Vile vile Kidata aliahidi kuwapatia gari, pamoja na kuwaongezea watumishi, na kuahidi kuboresha mazingira ya eneo la Baraza hilo ambayo yalikuwa hayaridhishi kiafya. 
Akiwa katika baraza la ardhi na nyumba la wilaya ya Ilala lililopo katika jengo la Mwalimu House – Ilala; Bw. Kidata akiongea na mwenyekiti wa baraza (Bi. Mwendwa Mgulambwa) na Watumishi wa baraza hilo, alisifia mazingira bora ya Baraza hilo na kuahidi kutatua tatizo la upungufu wa samani lililokuwa tatizo zaidi katika Baraza hilo. 
 Aidha Bw.Kidata aliahidi kusimamia kidete suala la malimbukizo ya madeni ya posho za wazee wa mabaraza hayo na kuahidi ifikapo Ijumaa tatizo hilo litakuwa limekwisha.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Alphayo J. Kidata, akipekua baadhi ya majalada katika chumba cha majalada ya Baraza la Ardhi na Nyumba la Kinondoni alipofanya ziara katika baraza hilo.

 Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.  Alphayo J. Kidata, akionyeshwa na Mwenyekiti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya - Kinondoni, Bw.Yose Mlyambina kompyuta zilizoazimwa kutoka Wizarani, kutokana na ufinyu wa vitendea kazi hivyo. Hata hivyo Kidata alitoa ruhusa kwa Mwenyekiti kuchukua Kompyuta hizo moja kwa moja kwa ajili ya matumizi ya Baraza hilo alipofanya ziara katika baraza hilo.

 Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Alphayo J. Kidata, akitoa Tsh. 100,000 kwa Karani kwa ajili ya matumizi ya malipo ya umeme kwa baraza la ardhi na nyumba ya wilaya la Kinondoni alipofanya ziara katika baraza hilo na kubaini baraza hilo kukosa umeme kutokana na kutopata pesa za malipo hayo

Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Alphayo J. Kidata, akieleza kwa Mwenyekiti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya - Kinondoni, Bw. Yose Mlyambina na ujumbe alioambatana nao kutoka Wizarani, kuhusu kuboresha mazingira ya eneo la baraza la ardhi na nyumba la wilaya ya Kinondoni, alipofanya ziara katika baraza hilo.

BUDGET COMMITTEE OF THE Commonwealth Parliamentary Association (CPA) meets in Dar es salaam

0
0
The Treasurer of the Commonwealth Parliamentary Association (CPA) - Africa Region Hon. Request Muntanga (Zambia) chairing the Budget Committee on the Association which met in Dar es Salaam on Sunday. On his right is the Clerk of the National Assembly of Tanzania Dr. Thomas Kashililah who is also the Regional Secretary of the Association.

The Treasurer of the Commonwealth Parliamentary Association (CPA) - Africa Region Hon. Request Muntanga (Zambia) going through the CPA Africa Regional Magazine during the Budget Committee on the Association which met in Dar es Salaam on Sunday.

 The Regional Secretary of the CPA Africa Region Dr. Thomas Kashililah being discusses with his Assistant Regional Secretary  Mr. Demitrius Mgalai during the CPA Budget Committee which met in Dar es Salaam on Sunday
The Chairperson of the Executive Committee of the Commonwealth Parliamentary Association (CPA) - Africa Region Hon. Lindiwe Maseko (South Africa) making his point during the CPA Budget Committee which met in Dar es Salaam on Sunday.


MAHAFALI YA TISA YA TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM (DIT)

0
0
Mahafali ya tisa ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), yanatarajiwa kufanyika Jumamosi 30 Januari mwaka 2016 na yatatanguliwa na utoaji tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mwaka wa masomo 2014/2015.

Sherehe hizo za utoaji wa tuzo kwa wahitimu waliofanya vizuri, zitafanyika mapema 22 Januari mwaka 2016 katka viwanja vya chuo hicho kikongwe cha masuala ya teknolojia nchini.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na taasisi hiyo, inawafahamisha wahitimu wote wa mwaka wa masomo 2014/2015, kusoma utaratibu wa kuthibitisha kushiriki mahafali hayo katika tovuti ya Taasisi www.dit.ac.tz.

Wahitimu hao ni wale wa Shahada ya Uzamili (M.Eng), Shahada ya  kwanza ya Uhandisi (B.Eng.) na  wahitimu wa Stashahada ya Uhandisi (OD) na “Rehearsal” kabla ya mahafali itafanyika Ijumaa tarehe 29/01/2016.

Taarifa hiyo imewataka wahitimu watakaoshiriki kulipia joho la mahafali Tshs 50,000/= (kwa wahitimu wa Shahada ya Uzamili - M.Eng) na  Tshs 30,000/= (kwa wahitimu wa Shahada ya kwanza (B.Eng) na Stashahada (OD).

Wahitimu wametakiwa kulipa fedha hizo  katika tawi lolote la NBC  kwenye akaunti namba 018101003145 na kujisajili kupitia tovuti ya Taasisi www.ac.dit.tz

Taarifa hiyo imebainisha kuwa wahitimu wanatakiwa kuwa makini na kuhakikisha malipo yamefanyika kwa kutumia jina kamili kama linavyoonekana kwenye orodha ya wahitimu wa mwaka 2014/15 iliyopo kwenye tovuti ya Taasisi.


Pia yaonyesha namba ya usajili na madhumuni ya malipo (yaani mahafali) na mwisho wa kujisajili ni 31 Desemba, 2015 na wahitimu wanahimizwa kupeana taarifa kuhusiana na mahafai hayo ya tisa ambayo mgeni rasmi atatangazwa baadae.

Serikali yaahidi kuwapatia vipimo zaidi wahanga wa mgodi wa Nyangalata

0
0
Remija Salvatory na Nuru Mwasampeta

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Omar Chambo amewaagiza    Madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama kuandaa utaratibu wa kuwawezesha  wahanga wa  Mgodi wa Nyangalata  kwenda Hospitali za rufaa   kwa ajili ya uchunguzi  zaidi wa afya zao.

Mhandisi Chambo aliyasema hayo alipowatembelea wahanga hao waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama  kutokana na ajali ya kufukiwa na kifusi na kufanikiwa kuokolewa baada ya kuishi chini ya ardhi kwa siku 41 katika Mgodi wa Nyangalata mkoani Shinyanga.

Katibu Mkuu alitoa maagizo hayo baada ya mmoja wa wahanga hao, Joseph Buruge kueleza kuwa ingawa ngozi za wachimbaji hao zinaonekana kuimarika   lakini bado kuna tatizo la  vijipele vidogo vidogo mwilini ambavyo baada ya muda hutoa usaa hivyo aliomba uchunguzi wa kina ufanyike ili kutibu tatizo hilo.

“Kwa kweli Mheshimiwa tunaendelea vizuri  na matibabu na tunawashukuru madaktari na wauguzi wote wanaotuhudumia na tunaishukuru Wizara na Serikali kwa ujumla  kwa misaada na huduma walizotoa, lakini kwa sababu umekuja Mheshimiwa  tuna maombi yetu ambayo tunaomba Serikari iweze kutusaidia sisi wahanga wote” , alisema Buruge.

KARIBU KUSHEREHEKEA KENYA JAMHURI NA UHURU WA TANZANIA BARA SAFARI SPORTS LOUNGE, HUNTSVILLE, ALABAMA

INTRODUCING OLD SCHOOL BY JOS MTAMBO

TEASER YA JOTO LA ASUBUHI LA 93.7 EF JUMATATU DESEMBA 7, 2015 KUANZIA SAA 12 ASUBUHI

Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images