Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Watch "NEWDEAL AFRICA'S TRAVEL LOG-ZIM CULTURAL DIPLOMACY"


DIRA YA DUNIA JUMATATU 30.11.2015

Dr Manyaunyau akanusha kufungwa miaka 3 gerezani, alia na waandishi wazushi

HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

$
0
0
SIMU.TV:  Rais Magufuli ametoa agizo kwa wenyeviti na wakurugenzi kusimamia mashirika ya umma na hukakikisha yanazalisha ili kuingizia taifa faida
SIMU.TV: Mwili wa aliyekuwa mfanyakazi wa Azam Media Ismail Hamza unatarajiwa kusafirishwa kesho na kuzikwa mkoani Morogoro.
 SIMU.TV: Jumla ya walemavu 65 nchini wamepatiwa msaada wa miguu mbadala na kampuni ya Kamal Steels kwa lengo la kuwasaidia kutembea.  https://youtu.be/aYgsa2IAGLU 
SIMU.TV: Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amewataka wakazi wa Mkoa huo kujiunga na kituo cha kuwezesha wananchi kujikwamua kiuchumi POSO ili kupata mitaji ya kujiendeleza kiuchumi;https://youtu.be/9eiTOAdDYf8 
SIMU.TV: Wananwake Mkoani Mbeya walalamikia waume zao juu ya matumizi nabovu ya  fedha za TASAF wanazopokea kutoka serikalini; https://youtu.be/wzoJsMdzQSA 
SIMU.TV:  Rais Magufuli ametoa agizo kwa wenyeviti na wakurugenzi kusimamia mashirika ya umma na hukakikisha yanazalisha ili kuingizia taifa faida;https://youtu.be/_elnHPUbHyI 
SIMU.TV: Hali ya taharuki imeibuka katika mtaa wa Nyasaka B Mkoani Mwanza baada ya mkazi mmoja kumfungia mtoto wa miaka 2 ndani ya nyumba;https://youtu.be/OVGF2FVs-Jc 
SIMU.TV: Serikali yawataka wananchi wote kushiriki katika zoezi la usafi siku ya Uhuru kama kutii agizo la Rais Magufulihttps://youtu.be/mf611qpGt40 
SIMU.TV: Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ametoa siku 3 kwa viongozi wa manispaa za mji huo kuhakikisha wanaondoa taka katika maeneo yao ili kuepukana na mlipuko wa kipindupindu https://youtu.be/BgJzjfICyI4
SIMU.TV: Timu ya soka ya Tanzania chini ya miaka 15 inatarajia kuanza ziara yake ya mafunzo kwa nchi za Afrika Mashariki kwajili ya kujiandaa na michuano ya kimataifa; https://youtu.be/rwZQUGdICoo
TBC: Tanzania imeendelea kupata changamoto uanzishwaji wa ligi ya mpira wa miguu kwa wanawake jambo linalopelekea changamoto kwa wadau wa soka nchini; https://youtu.be/29UzpEUNTWQ

BIASHARA ASUBUHI

$
0
0
Mapema leo asubuhi katika Kitua cha Daladala cha Posta Jijini Dar, Kamera ya yetu imeinasa taswira hii ya Mwanadada huyu akipanga biashara yake ya hela za sarafu (Coins) tayari kwa kuwauzia makondakwa wa daladala.

Masumin wadhamini midahalo ya wanafunzi wa sekondari Dar

$
0
0
Sylivanus Ndayisenga wa shule ya sekondari ya Debrabant, akishiriki katika katika mdahalo wa kitaaluma ulioandaliwa na Masumon Printways na Five Star na kufanyika jijini Dar es Salaam jana. Mdahalo huo ambao ni kwa ajili ya shule za sekondari za Dar es Salaam uliihuisha pia St Antony.

TAMASHA LA MADIVA KUFANYIKA DISEMBA 4 MWAKA HUU MKOANI MBEYA

$
0
0
 Msanii wa kizazi kipya Vanessa Mdee (Wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na madansa wake wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Trust “Divas Only” lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma. Tamasha hilo ni mahususi kwa utoaji elimu ya uzazi wa mpango kwa kina dada ambalo liliratibiwa na Shirika la DKT international.
 Msanii Vanessa Mdee (kushoto) akibadilishana mawazo na wafanyakazi mbalimbali wa Shirika la DKT International kabla ya kufungua rasmi Tamasha la Divas Only ambalo lilifanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. (Katikati) ni Meneja Masoko DKT International Sialouise Shayo.
 Kaimu meneja wa DKT International tawi la Dodoma Bi.Zena Mgoi akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa kina dada waliohudhuria uzinduzi wa Tamasha la “Divas Only” ambalo lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.

 Mwishoni mwa wiki TRUST wazindua mfululizo wa matamasha ya kusisimua ya Divas Only ambayo yalimshirikisha mwanadada na msanii wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee. 

Trust ni chapa ya njia za kisasa za uzazi wa mpango zenye kuaminika pamoja na bidhaa na huduma za maisha na urembo zinazotengenezwa na wanawake kwa ajili ya wanawake. 

Trust ipo ili kuhamasisha madiva wajipange kwa ajili ya baadaye,Madiva wa Trust wanataka kufanya maamuzi na kupanga kwa ajili ya mafanikio, Trust iko hapa kukusaidia wakati wa safari hii. 

Tulifurahia muda tuliopata kukaa na Vanesaa na Madiva wa Trust wa Dodoma, Kama wewe ni Diva wa Trust ama unataka kujua Trust inahusu nini, njoo ukutane na Madiva wa Trust wengine pamoja na Vanessa Mdee katika matamasha yetu mengine Mbeya Desemba 04 pale Sunset Hall, Soweto na Mwanza Desemba 13, Malaika Beach Resort. Huwezi kufika? Tafuta eneo lilipo Dodoma, Mbeya na Mwanza katika tovuti yetu (trustlife.co.tz) na ututembelee leo!

MAJALIWA AKUTANA NA MABALOZI WA CHINA, KOREA NA SUDAN

$
0
0
 Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na balozi wa China Nchini Dkt. Lu Youqing kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es slaam  Disemba 1, 2015. 
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Sudan nchini, Dkt.Yassir  Mohamed Ali Ofisini kwake jijini Dar es salaam Disemba 1, 2015.
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na balozi wa Korea nchini Mhe. Chung Il ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Disemba 1, 2015 kuaga.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

JAJI MAKURU AFUNGUA MAFUNZO MAALUM YA HUDUMA KWA WATEJA KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA YA TANZANIA.

$
0
0
 Watumishi wa Kada mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania waliohudhuria mafunzo ya Huduma kwa wateja ili kuweza kuwajengea ujuzi na ufanisi katika kazi mahakamani.
 Mhe. Jaji Crescencia Makuru, Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, akifungua rasmi mafunzo maalumu ya Huduma kwa Wateja kwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania, leo mkoani Dodoma. 
Mhe. Jaji Crescencia Makuru, Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, (aliyeketi wa pili toka kushoto), Nurdin Ndimbe, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mahakama ya Tanzania, (wa pili kulia), Deus Kibamba, Mkurugenzi wa TCIB, (wa kwanza kulia), Simon Berege, Mwenyekiti wa MISA-Tanzania, (wa kwanza kushoto), katika picha ya pamoja na Watumishi wa Kada mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania washiriki wa mafunzo ya Huduma kwa Wateja,                Mkoani Dodoma.  
                                                                                                                                                                   
MAFUNZO maalumu ya siku mbili yahusuyo huduma kwa wateja na haki ya kupata taarifa kwa watumishi wa Mahakama, yamemalizika leo katika hoteli ya St.Gaspar mjini Dodoma.

Akifungua rasmi mafunzo hayo  Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, Mhe. Crescencia Makuru, amesema moja ya malengo makuu ya mafunzo hayo, ni kuwajengea uwezo watumishi wa Mahakama kwa kuwapa mbinu na mikakati mbalimbali itakayowasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

“Mahakama ya Tanzania kwa sasa inaendelea na maboresho ya utendaji kazi wake kama sehemu ya kuhakikisha kuwa inatoa huduma iliyo bora na kwa wakati”, Jaji Makuru amebainisha.

Mwaka 2014 Mahakama ya Tanzania kama moja ya Taasisi ya Serikali ilifanyiwa tathmini kuhusu utoaji wa haduma zake hasa katika nyanja ya upatikani na utoaji wa taarifa kwa Umma iliyoendeshwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, (Media Institute of Southern Africa-MISA). 

Katika tathmini ile, Mahakama ilikuwa ya mwisho na ilizawadiwa kufuli la dhahabu kama alama ya kuonyesha kuwa taasisi hii ni moja kati ya zilizojifunga sana kutoa taarifa kwa wananchi. Moja ya maeneo yaliyoonekana na udhaifu ni namna masijala za Mahakama zinavyopokea na kutunza nyaraka na hata wanavyowahudumia wateja kwa ujumla.

Mafunzo hayo endelevu yamelenga kuwafundisha makarani na watumishi wa kada mbalimbali nini maana ya uhuru wa Habari na habari ni Nini?, Huduma kwa wateja na ujuzi wa mawasiliano kwa watumishi wa Umma , Njia mbalimbali za upatikanaji wa taarifa katika Taasisi za Umma na Sheria ya utoaji wa  habari katika Mahakama.

Mafunzo haya yameandaliwa na kufadhiliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) pamoja na Taasisi ya Friedrick Ebert Stiftung (FES) ofisi ya Tanzania.

WATENDAJI WA MASHIRIKA YA NDEGE WATAKA BARABARA YA KUELEKEA UWANJA WA NDEGE IPANULIWE

$
0
0
Watendaji wa mashirika ya ndege nchini wameiomba Serikali kupanua Barabara ya Nyerere ili kuwawezesha abiria wanaosafiri kwa ndege kuwahi usafiri kufuatia ongezeko lao kubwa na la ndege pia linalotarajiwa  kufuatia kuwepo kwa jengo jipya la abiria (TB III) linalotarajiwa kukamilika mwaka 2016.

Rai hiyo imetolewa jana na watendaji wa mashirika 19 ya ndege yanayoendesha shughuli zake katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) walipozuru ujenzi TB III ikiwa  ni moja ya ziara za wadau zinazoandaliwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).
Baadhi ya CEOs wa mashirika ya ndege wakitoka kutembelea TB III (nyuma yao) jana JNIA.

Akijibu rai hiyo, Mkurugenzi wa Mradi wa TB III, Mhandisi Mohammed Millanga amesema, wameipokea kama changamoto lakini tayari walishawasiliana na mamlaka husika kuomba kuboreshwa kwa usafiri kwenda JNIA lakini jibu walilopata halioneshi suluhisho la haraka.

“Tuliwasiliana na Wakala wa Barabara (TANROADS) na Shirika la ReliTanzania (RAHCO). RAHCO walisema hawana mpango wowote kuhusu eneo hili. Wakala wa Mabasi ya Mwendo Kasi (DARTS) wao wameiweka Barabara ya Nyerere katika awamu ya tatu ya mradi wao. “amesema.
Mmoja wa CEOs akimwonesha Mhandisi Carloline Ntambo wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) inayojenga TB III, eneo ambalo wangependa kufanyia shughuli zao za huduma kwa abiria wa ndege.

Mhandisi Millanga amesema, katika kuhakikisha hakuna tatizo hilo, TAA iliwasiliana na wawekezaji wa treni ya juu kutoka Afrika Kusini lakini mpango huo haujazaa matunda. Hata hivyo, amesema, anaamini Serikali ya awamu ya tano itapata suluhisho la tatizo hilo mapema.

MISS TANZANIA USA 2015-2016 AEESHA KAMARA ASHINDA KUWA COVER GIRL KWENYE CALENDA YA MISS AFRICA USA

$
0
0
 Miss Tanzania USA 2015-2016 Aeesha Kamara (kushoto) aibuka mshindi na kuwa Cover Girl kwenye Kalenda ya Miss Africa USA 2015-2016 shindano lililofanyika New York siku ya Jumamosi Novemba 28, 2015.
 Mamiss wengine walioshiriki shindano hilo wakipita mbele ya majaji.
 Wadau wakipata picha na mamiss wakati mratibu wa mashindano ya miss Africa Lady Kate alipokua akitangaza shindi.
Ma Winny Casey (gauni jeusi) pamoja na Lady Kate (mwenye miwani) wakiwa na mamiss.

MKUTANO WA KUKUZA SEKTA YA UKARIMU NA UTALII HUFANYIKA KWA MARA YA PILI JIJINI DAR DISEMBA 7 NA 8 MWAKA HUU

$
0
0
INTERNATIONAL hospitality consultancy HD Partnership (HDP) kwa  kushirikiana na shirika la wamiliki wa Hoteli Tanzania (HAT), wanafanya mkutano wa awamu ya pili wa mwaka Disemba 7 na 8 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

 Mkutano huu unahusu sekta ya ukarimu na utalii, Katika jukwaa hilo litategemea kuzungumzia ujumbe juu ya ukarimu kwa wadau wa sekta ya utalii wakiwemo wawekezaji, wamiliki wahoteli, kampuni za usimamizi, bidhaa, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali, wasambazaji na watoaji huduma. Pamoja watajadili juu ya malengo yanayohusu ukarimu na utalii katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara.

Mkutano huu ambao unahusisha wadau wa ndani ya nchi na nje ya nchi, una lengo la kuchochea ukuaji endelevu wa sekta hizi kwa kutoa wataalamu husika kuongea na kutoa ushauri  pia kutengeneza mazingira ya maonyesho ambayo yatatoa fursa za kubadilishana ujuzi baina ya kampuni tofauti kwenye sekta ya ukariimu na utalii. Kwa mujibu wa Meelis Kuuskler ambaye ni mshauri wa kimataifa kuhusu ukarimu na Mkurugenzi mkuu wa HDP anasema “ mkutano wa mwaka huu umejikita katika masuala maalumu ya kiutendaji yanayoathiri shughuli za kiutalii.
Kusoma zaidi bofya HAPA.

TAARIFA KUHUSU UTATUZI WA MGOGORO WA WAKULIMA WA MIWA KILOMBERO

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTATUZI WA MGOGORO WA WAKULIMA WA MIWA KILOMBERO 
Bodi ya Sukari Tanzania imefuatilia na kubaini chanzo cha malalamiko ya wakulima wa miwa wanaozunguka Kiwanda cha Sukari cha Kilombelo (ILOVO).  

Akizungumza katika taarifa yake, Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Sukari Tanzania Bwana Henry Semwanza alisema kuwa, chanzo cha malalamiko yanatokana na kiwanda kuharibika bila kutarajia na kusimamisha uzalishaji kuanzia tarehe 14 hadi 18 Novemba 2015.  

Hali hiyo ilisababisha miwa ya wakulima ambayo ilikuwa imekatwa kuharibika na hivyo kukosa sifa ya kuchukuliwa na kiwanda kwa ajili ya usindikaji. 

Bwana Semwanza aliongeza kuwa hali hiyo ilisababisha tani 250 za miwa kutoruhusiwa kuingia kiwandani kwa vile zilishapita zaidi ya siku tano tangu miwa ilipochomwa. 

 “Miwa hiyo ilichomwa tangu tarehe 14 Novemba 2015 siku ambayo kiwanda kiliharibika, na kilipotengamaa zilikuwa zimeshapita siku tisa, hivyo miwa hiyo kukosa sifa na ubora unaokubalika, na hivyo ikazuiliwa kuingia kiwandani”  

Akizungumzia utekelezaji wa mkataba wa ugavi wa miwa baina ya Kampuni na Vyama vya Wakulima, Bwana Semwanza alibainisha kuwa Kifungu cha 5.2.3.3 cha mkataba huo kinasisitiza kutokuikubali miwa ambayo kiwango cha ubora wake uko chini ya asilimia 80 au miwa iliyopitisha siku tano tangu ilipochomwa kwa mujibu wa kifungu cha 5.2.3.4. 

Ili kupunguza hasara inayoweza kutokea kwa wakulima, Bwana Semwanza aliwakumbusha wakulima  na wamiliki wa kiwanda kuzingatia taratibu za uvunaji wa miwa. 

 “ninatoa wito kwa wakulima kupitia vyama vyao kuzingatia taratibu za uvunaji kwakuwa imedhihirika pasipo shaka kuwa baadhi wamekuwa wanavuna miwa mingi zaidi ya mgao wao wa siku, mambo haya yasipozingatiwa yanaweza kuibua migogoro isiyo ya lazima ” Bwana Semwanza alibainisha katika taarifa yake. 

Aidha, alisisitiza kuwa kamati iliyoundwa chini ya mkataba wa ugavi wa miwa inayojumuisha wakulima na uongozi wa Kiwanda na ambayo hukutana kila siku iendelee kuwa msingi wa kuamua kiasi cha miwa inayotakiwa kuvunwa na kupelekwa kiwandani katika siku inayofuata. 
Semwanza aliongeza kuwa Bodi yake inaendelea kufuatilia utekelezaji wa makubaliano kati ya kiwanda na wakulima, na haitasita kuchukua hatua sitahiki kwa upande utakao kiuka ili kutatua migogoro inayoweza kuzuilika kwa haraka.

Semwanza alisisitza kuwa kwa sasa hali ni shwali ambapo uvunaji na upokeaji wa miwa kiwandani unaendelea kama kawaida na wakulima wameongezewa mgawo wa miwa inayotakiwa kuingizwa kiwandani kila siku. 

“hali ya uvunaji inaendelea kama kawaida na mgao wa wakulima kuingiza miwa yao kiwandani umeongezwa kwa zaidi ya asilimia 50; ili kuhakikisha miwa yote ya wakulima wanaozunguka kiwanda cha Kilombero inavuwa” 
Bodi ya Sukari Tanzania inashirikiana kwa karibu na uongozi wa mkoa na Wilaya ili kushughulikia migogoro isiyo ya lazima. Alihitimisha Bwana Semwanza. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika
Kilimo Complex, 
1 Mtaa wa Kilimo 15471
DAR ES SALAAM.

RAIS WA ZANZIBAR ATEMBELEA MRADI WA UIMARISHAJI MRADI WA MAJI SAFI MAKUNDUCHI

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maji safi (ZAWA) Dkt. Mustafa Ali Garu (kulia) wakati alipotembelea Uimarishaji wa mradi wa maji safi na salama wa uchimbaji wa Kisima kipya na ukarabati wa tangi la maji Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Unguja leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maji safi (ZAWA) Dkt.Mustafa Ali Garu (kulia) wakati alipotembelea Uimarishaji wa mradi wa Maji safi na salama wa uchimbaji wa Kisima kipya na ukarabati wa tangi la maji Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Unguja leo.

KIKOSI CHA TIMU YA KILIMANJARO STARS KUREJE KESHO

$
0
0

KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kinatarajiwa kuwasili kesho mchana jijini Dar ess alaam kikitokea nchini Ethiopia kilipokuwa kinashiriki michuano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.


Kilimanjaro Stars imetolewa katika hatua ya robo fainali na wenyeji Ethiopia kwa mikwaju ya penati, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za mchezo huo, na wenyeji kushinda kwa penati 4-3.


Timu ya Kilimanjaro Stars inayonolewa na kocha Abdallah Kibadeni na msaidizi wake Juma Mgunda, iliongoza kundi lake katika hatua ya makundi kabla ya kukutana na wenyeji Ethiopia katika mchezo wa robo fainali.

Katika michezo wa makundi, Kilimanjaro iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Somalia, ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Rwanda, na sare ya bao 1-1 dhidi ya Ethiopia.

Baada ya kurejea nyumbani, TFF kwa kushirikiana na benchi la ufundi wataanza maandalizi ya michezo dhidi ya Chad itakayochezwa Machi 2016 kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2017.

UJENZI WA KISIWA CHA KITALII WAANZA KATIKA ENEO LA MTONI MARINE KASKAZINI MAGHARIBI ZANZIBAR

$
0
0
 Sehemu  inayoendelea kufukiwa hapo Mtoni Marine ambayo itatumika hapo baadae kwa ajili ya eneo maalum litakalotoa fursa kwa Wananchi  kupata mapumziko.{ Public Beach }. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar { ZIPA } Nd. Salum Khamis Nassor  akimueleza Balozi Seif  hatua zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kuona taratibu za uwekezaji zinachukuliwa kwa wanaowekeza vitege uchumi vyao Nchini. 

MRADI mkubwa wa Kimataifa wa ujenzi wa kisiwa cha Kitalii  ambacho kitatengenezwa kwa mfumo wa ufukiaji Bahari umeanza rasmi katika eneo la Hoteli ya Utalii iliyopo Mtoni Marine kaskazini Magharibi ya Mji wa Zanzibar.

Hata hivyo gharama kamili za Mradi huo bado hazijafahamika  wakati utakapokamilika  rasmi ujenzi wake hapo baadaye.

Mradi huo unaoendeshwa na Kampuni ya Kizalendo  ya Baghresa Group utahusisha ujenzi wa Hoteli ya Kimataifa ya Ghorofa  Tano ya Daraja la Tano { Five Star + }, utengenezaji wa eneo la wazi la mapumziko { Public Beach } pamoja na kutengeneza  Kisiwa cha Mji mpya.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI AZINDUA SAFARI ZA NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LA NCHINI ABU DHABI LEO MCHANA KATIKA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA CHA MWL. JULIUS NYERERE (JNIA)

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka, akiteta jambo na Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu(United Arab Emirate) nchini Tanzania, Balozi Abdullah Ibrahim Al Suwaidi, kabla ya Uzinduzi wa Safari za Ndege ya Shirika la Ndege la Etihad la Nchini Abu Dhabi, leo mchana.
 Magari ya Zimamoto yakimwaga maji kuashiria uzinduzi na ukaribisho wa Safari za Ndege ya Shirika la Ndege la Etihad la Nchini Abu Dhabi, leo mchana katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Mwl. Julius Nyerere (JNIA).
Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu (United Arab Emirate) nchini Tanzania, Balozi Abdullah Ibrahim Al Suwaidi (wa pili kutoka kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (wa tatu kutoka kulia), pamoja na Viongozi Wengine wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Safari za ndege za shirika la Shirika la Ndege la Etihad la Nchini Abu Dhabi leo mchana, katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Mwl. Julius Nyerere (JNIA).
(HABARI PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-UCHUKUZI).

WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA AFUNGUA KITUO CHA UTAMADUNI WA CHINA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (kushoto) akifungua kituo cha utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mkurugenzi wa Utamaduni toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko.
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati) akipata maelekezo toka kwa Mshauri wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. GAO Wei (kulia) wakati Waziri Mkuu akifungua kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.
Kundi la Muziki la Zinijncheng kutoka chuo Kikuu cha Sanaa ya Muziki cha China kikitoa burudani kwa mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania.

TIZA YA JOTO LA ASUBUHI YA REDIO 93.7 EFM DECEMBER 2

FEDHA ZA 9 DISEMBA ZAANZA UJENZI WA KUPANUA BARABARA MWENGE-MOROCCO JIJINI DAR

$
0
0

Scaveter ikisafisha sehemu ya barabara kuanzia Mwenge hadi Morocco kwaajili ya upanuzi wa barabara mbili zinazojengwa kwa fedha ambazo zilitakiwa kutumika katika kusherekea sherehe za uhuru ambazo hufanyika kila mwaka Disemba 9 ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Joseph Magufuli, kazi hiyo imeanza kutekelezwa leo jijini Dar es Salaam.
Vijana wakigombania bango ambalo limevunjwa katika upanuzi wa barabara kuanzia Mwenge hadi Morocco leo jijini Dar es Salaam.

(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii).
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images