Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1042 | 1043 | (Page 1044) | 1045 | 1046 | .... | 3285 | newer

  0 0
 • 12/01/15--07:33: IN LOVING MEMORY
 • THE LATE MRS MERCY PATIENCE MAGANGA

  DIED 03RD DECEMBER 1996

  Dear Mum,

  NINETEEN VERY PAINFULLY YEARS have gone today without you our dear Mother.  The pain of losing you will never go away because you were what we treasured most in our lives. A loving, caring, understanding and devoted mother and a friend.  You were our pillar, a source of happiness and strength.

  Mom, we love and miss you so much and each passing day we wish you were here with us.  We are still struggling to accept the reality of your death.  We however, continue drawing our strength from the unique memories of your love, care and wisdom, and from the solid foundations you laid for us.

  Our guardian Angel, we feel your presence each and every day as we meet and overcome challenges in our lives.  We thank God for His love and Grace for seeing us through all these trying years.  He is indeed taking good care of us.  We are looking forward to reuniting with you and Dad in God’s Glory.  MAY YOUR SOUL REST IN ETERNAL PEACE. AMEN


  Fondly remembered by your loving children Nelly, Gerald, Louisa, Alice, Susan and Andrew, son in-laws Pascal, Rikard, Peter and Alvin, grand children Jadden, Nelly, Andrew, Simon and Mercy, relatives and friends.

  Rest in Peace Mama.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka (wa nne kutoka kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito, wakati akimwelezea namna kiwanda cha kutengenezea breakpad za vichwa vya treni kilivyokuwa kinafanya kazi, na sasa hakifanyi kazi, wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea kiwanda hicho leo asubuhi, Katibu Mkuu ameipa wiki mbili kampuni hiyo na Shirika la Reli Tanzani (TRL) kuuanda timu na kufanya tathmini ya mitambo iliyoharibika na kuhakiki kiwanda hicho kinaanza kufanya kazi.
  Jengo ambalo lilikuwa likitumika kama kiwanda cha kutengenezea breakpad za vichwa vya treni, linavyoonekana baada ya kusitisha uzalishaji wa breakpad hizo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akitoa maelekezo kwa uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), mara baada ya kutembelea eneo la Reli sehemu ya Malindi leo asubuhi.
  Reli ambazo hutumika kubadilisha baada ya ziliyopo kuchakaa, zikiwa kwenye eneo la Malindi, kama zilivyokutwa leo asubuhi. (Habari Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi)

  0 0

   Mazungumzo yakiendelea
   Naam hayo ndivyo yalivyo.....
   Mkurugenzi wa New Habari Corporation  Erasto Matasya akizungumza.

  NA BASHIR NKOROMO.
  Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema, kitampa ushirikiano mkubwa, Rais Dk. John Magufuli, ili aweze kwa ufanisi zaidi mapambano yake dhidi ya mafisadi na mikakati mingine ya kuinua uchumi wa Watanzania.

  Kimesema, kitampa ushirikiano huo Rais Dk. Magufuli, kwa sababu, aliyoanza kuyafanya na atakayoyafanya baadaye katika uongozi wake wa Urais anatekeleza yale yaliyomo katika ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020.

  Hayo yalisemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa akijibu maswali kadhaa yaliyoulizwa na baadhi ya wahariri, aliokuwa akizungumza nao, katika ziara aliyofanya leo, katika Kampuni ya New Habari Corporation, Sinza jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya wahariri, waliohoji ni kwa nini CCM haijitokezi kumpongeza Dk. Magufuli katika juhudi ambazo ameanza kuonyesha katika kupambana na ufisadi ikiwemo kubana fedha za walipa kodi ambazo zingepotea bure katika masuala yasiyo ya lazima na wakati huohuo kuanza kuwabana wafanyabiashara wanaodaiwa kukwepa kulipa ushuru.

  "Yapo mengi tuliyoanisha katika ilani yetu ya Uchaguzi, na yote yahahusiana sana na haya mnayoyaona yanafanywa na Rais Dk. John Magufuli, tena Ilani hii tumeitunga hata kabla ya kumteua kugombea Urais, Sasa anachofaya ni kuitekeleza ilani hii, isipokuwa mbinu anazotumia ni ubunifu wake na hili hatuna tatizo nalo kama Chama maana kiongozi wa aina hii ndiye tuliyemtaka", alisema Nape.

  "Najua wapo wanaojaribu kutengeneza magingira ya kumtaka kumtenganisha Dk. Magufuli na CCM, nawambieni Dk. Magufuli ni zao la CCM na mwana CCM Kindakindaki, hivyo ni upotoshaji wa hali ya juu kujaribu kuuaminisha umma kwamba anayofanya Dk. Magufuli hayana uhusiano na maelekezo ya CCM", aliongeza Nape.

  Alisema, baada ya kutengeneza ilani yake, CCM, ilidhamiria kwamba, awamu hii ya tano ni ya kutafsiri uchumi katika nyanja za huduma za Jamii, ikiwemo miundomboni, maji, afya na elimu.

  "Ni kutokana na lengo hili, ndiyo sababu tukakaa kwa makini na kuhakikisha ilani hii ya sasa tunamkabidhi mwana CCM ambaye utekelezaji wake hautakuwa wa mashaka mashaka, Ndiyo huyo Dk. Magufuli, bila shaka sasa na ninyi ni mashahidi mmeanza kuuona utekelezaji wake wa ilani", alisema Nape.

  Akizungumzia kuhusu Rais Dk. Magufuli kuchelewa kutangaza Baraza lake la Mawaziri, Nape alisema, Chama Cha Mapinduzi kimeshaunda serikali kwa kumpata Rais, kilichobaki sasa ni kwa Rais mwenyewe kuteua watendaji wake, lakini katika kufanya hivyo hakuna mda aliopangiwa kuanza kufanya hivyo na hashurutishwi na Chama wala sheria.

  Nape alisema, Dk. Magufuli hachelewi kuteua Baraza la Mawaziri kwa sababu anakosa wakuwateua, isipokuwa, anayo namna na mda ambao mwenyewe Kama Rais amejipangia, na mda huo ukijiri wa kuamua kufanya hvyo atafanya.

  "Tatizo hapa ni kwamba mnayo kiu kubwa ya kutaka kujua nani atawateua, sasa kiu yenu imepita kiasi, ndiyo maana mnaanza kuhoji, lakini mimi naamini Dk. Rais Magufuli ataikata kiu yetu, wala msipate taabu ya kuhoji kila kukicha", alisema Nape.

  Nape alisema, mbali na Chama kutengeneza ilani ambayo italeta mageuzi makubwa ya kiuchumi hapa nchini, pia Watanzania watarajie kuona mageuzi makubwa ndani ya CCM, kwa sababu yapo njiani kuwadia.

  "Kama ilivyo kawaida yetu, kila baada ya uchaguzi mkuu huwa tunafanya tathmini, baada ya tathmini hiyo, huwa lazima tufanye mageuzi kwa yale ambayo tumebaini kuwa ni kikwazo kwa uhai na maendeleo ya Chama katika nyanja mbalimbali, na mageuzi haya tunayafanya kuzingatia mahitaji ya sasa na wakati ujao", alisema Nape.

  Kuhusu Mwenyekiti wa sasa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kumwachia Ueneyekiti Rais Dk. Magufuli, Nape alisema, hayo si mambo mageni kwa CCM, imekuwa ikifanyika katika awamu zote za Urais, hivyo Kikwete anaweza akaamua kumwachia kabla ya uchaguzi mkuu wa CCM utakaofanyika mwaka 2017 au kabla ya hapo akiona inafaa.

  Zanzibar
  Akizungumzia mgogoro wa Zanzibar uliotokana na kufutwa uchaguzi mkuu wa Rais wa Zanzibar, Nape alikiri kamba ni mbaya na unaitia doa Tanzania, akisema, lakini akasisitiza kwamba njia pekee ya kuumaliza ni kwa mazungumza baina ya viongozi wa ndani bila kushirikishwa mataifa ya nje.

  Alisema, msingi wa mgogoro uliojitokeza Zanzibar, si wa kisheria, bali ni wa kisiasa zaidi, hivyo juhudi ziwekwe kwenye mazungumzo kuutatua, na baada ya kuutatua yaendelee kufanyika mazungumzo ambayo yataleta suluhisho la kudumu kwa kuwa imekuwa ni kawaida kwa Zanzibar kuzuka migogoro kila baada ya uchaguzi mkuu jambo linaloonyesha kuwa tatizo ni la asili zaidi kuliko inavyodhaniwa.

  Katika mazungumzo yake na wahariri hao wa New Habari Corporation Ltd, Wachapishaji wa magazeti ya Rais, Mtanzania na Dimba, alivitaka vyombo vya habari nchini, sasa kushirikiana na Serikali kulijenga taifa.

  "Tunajua wakati wa kampeni kulikuwa na mambo mbalimbali ambayo wakati mwingine vyombo vya habari vililazimika kukampenia vinaowaona kuwa wanafaa kutokana na sababu mbalimbali, lakini kama tulivyokuwa tukisema, kwamba baada ya uchaguzi maisha yataendelea, sasa umefika wakati wa kuendelea na maisha tuwe kitu kimoja", alisema Nape.

  Alivitaka vyombo vya habari, kusaidia kuishari Serikali na CCM, katika kutekeleza yaliyo bora kwa taifa na hata pale vyombo hivyo vitakapoona kwamba Chama au serikali vinaenda kinyume, visihofii kukosoa.

  Kwa upande wao, Mtariri Mtendaji wa Habari Corporation, Absalom Kibanda akimpongeza Nape kwa ushirikiano ambao amekuwa akivipa vyombo vya habari, na kumtaka aendelee kuwacha milango wazi kwa waandishi wa habari kama ambavyo amekuwa akifanya.

  Ziara hiyo ya Nape aliyoianza jana, kwenye vyombo vya habari inatarajiwa kuendelea kesho kwa kutembelea vyombo vingine vya habari vyenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, akifuatana na Bw. Paul Mwafongo alihudhuria mkutano na Bw. Louis Rene Peter Larose, Mkurugenzi Mtendaji, Benki ya Dunia, Kundi la Nchi za Afrika. 
  Wengine waliohudhuria ni pamoja na Bw. Andrew Ndaamunhu Bvumbe, Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, na Bw. WilsonToninga Banda, Mshauri, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji. Shabaha ya Mkutano ilikuwa ni kufuatilia mazungumzo yaliyofanyika Lima, Peru kuhusu kuimarisha ushirikiano kwa maslahi ya Afrika. 
  Mhe. Balozi Masilingi alishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano mzuri uliopo na kwa misaada na mikopo wanayotoa kuunga mkono juhudi za kujenga uchumi na kufanikisha mipango ya maendeleo kwa manufaa ya Watanzania wote. 
  Aidha aliwahakikishia ushirikiano muda wote atakapokuwa katika kutekeleza wajibu wake wa kazi kwa maslahi ya Taifa. Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Dunia, Kanda la Afrika, Bw. Louis Larose, alieleza kwa upande wake kuridhirishwa kwake na ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Benki ya Dunia. 
  Aidha Bw. Larose aliipongeza Tanzania kwa kufanikisha Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba , 2015 kwamba ulikuwa huru na wa haki. Pia, alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John P. Magufuli kwa ushindi na kwa juhudi zake katika kuangalia udhibiti wa ukusanyaji wa mapato ya serikali na kuziba mianya ya uvujaji wa mapatao ili zipatikane fedha kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya Watanzania. 
   Mkurugenzi Mtendaji aliahidi kwamba Benki ya Dunia iko tayari kutoa msaada wowote wa haraka utakaohitajika na kuombwa na Serikali ya Tanzania ili kufanikisha mpango wa kukusanya mapato ya ndani kwa ajili ya kutekeleza program za maendeleo na huduma za serikali. 
   Bw. Larose, alimdokeza Mhe. Balozi kwamba Benki ya Dunia itaandaa siku maalumu mjini Washington, D.C. kwa ajili ya kuitangaza Tanzania na vivutio vyake nchini Marekani na kuomba kwamba Benki ya Dunia itamwalika Mhe. Balozi kuzindua siku hiyo. Akijibu hoja hiyo Mhe. Balozi alikubali mwaliko huo.
  Mhe. Balozi Masilingi ametembelea ofisi ya Bi. Cathy Byrne, Mkurugenzi Mwandamizi wa masuala ya Afrika katika Ikulu ya Marekani (White House). Katika maongezI yao, Bi. Cathy Byrne alimueleza Mhe. Balozi Masilingi jinsi Serikali ya Marekani inavyoridhishwa na mahusiano mazuri baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Marekani. Pia alieleza kuhusu serikali ya Marekani kuridhishwa na hatua za serikali ya Tanzania, katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.
  Mhe. Balozi Masilingi amemhakikishia mwenyeji wake kuwa ataendeleza mashirikiano mazuri sana yaliyopo kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Marekani kwa njia ya diplomasia ya uchumi yenye lengo la kuhamasisha biashara na uwekezaji nchini Tanzania.

  0 0


  0 0
  0 0  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam leo kuhusiana na tuhuma zilizoelekezwa benki ya Stanbic Tanzania kuwa imetumika katika kufanya udanganyifu wa riba ya mkopo dola Milioni 600 iliyopewa serikali ya Tanzania na Uingereza kupitia Kampuni ya Egma ya Tanzania.

  Amesema kuwa Benki kuu ilifanya ukaguzi wa benki hiyo na mambo mengine walibaini malipo yasiyokuwa ya kawaida kuhusiana na kampuni ya kitanzania inayoitwa Egma,malipo hayo yalikuwa kinyume na taratibu za kibenki na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo walishindwa kuvumilia kwa hiyo tetesi tukazipata, wakaguzi wa benki kuu walifuatilia malalamiko hayo na kujiridhisha kuwa uongozi wa benki ya Stanbic Tanzania ulifanya mambo ambayo ni kinyume na taratibu zinazokubalika kibenki, ambapo fedha kiasi cha dola milioni 6 ziliingizwa kwenye kampuni ya Kampuni ya Egmwa na siku chache zilitolewa zote kwa fedha taslimu wala benki haikukusanya kodi ya zuio ambayo kwa mujibu wa sheria ya kodi ilipaswa kutozwa. 
  TAARIFA KAMILI SOMA HAPA

  0 0

  SERIKALI kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 5 katika mwaka 2015/16 kwa ajili ya kuhudumia kambi za Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu ya magonjwa hayo kwa Watanzania.

  Lengo la mkakati huo ni kuhakikisha Wagonjwa wengi wanahudumiwa katika kipindi kifupi pamoja na kupunguza gharama za kusafirisha wagonjwa nje ya nchi, ambao wengi wao husafiri kwa ajili ya matibabu ya magonjwa ya moyo, figo na saratani.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donald Mmbando (Pichani)wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Dkt. Mbando alisema katika wiki ya kwanza iliyoanza wiki hii Madaktari hao wanatarajia kutoa huduma kwa wagonjwa 20 na kuifanya Serikali kuokoa kiasi cha Tsh. Milioni 500 ambazo zingetumika kuwasafirisha wagonjwa hao nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

  “Tumeokoa kiasi cha Tsh. Bilioni 1 zilizopaswa kutumika kuwapeleka nje ya nchi wagonjwa hawa, tutahakikisha kuwa Wataalamu hawa wanafanya kazi kwa pamoja na Madaktari wetu ili waweze kuwajengea uwezo katika kutibu magonjwa haya”  alisema Dkt. Mmando.

  Alisema Serikali pia ipo katika mchakato wa kuzijengea uwezo hospitali mbalimbali nchini ikiwemo Taasisi ya Kansa ya Ocean Road na Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kuziwezesha hospitali hizo kuwa na Wataalamu na majengo ya kisasa kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu kwa Watanzania.

  Aidha alisema Serikali imepanga kufanya mazungumzo na taasisi za kiraia na nyingine ikiwemo taasisi ya Rotary Club zilizokuwa zikisafarisha watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, kuwekeza nguvu nchini kwani Tanzania kwa sasa ina wataalamu wa kutosha kwa ajili ya kuwatibu wagonja hao.

  Kwa mujibu wa Mmbando alisema magonjwa ya moyo ni miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza, hivyo aliwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara na kuacha kunywa pombe na uvutaji wa sigara na kutazama desturi za ulaji.

  Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Prof. Mohammed Janabi alisema katika kipindi cha wiki mbili ambazo madaktari hao watakuwepo hapa nchini wanaweza kuhudumia jumla ya wagonjwa 55, na hivyo kuifanya Serikali kuokoa kiasi cha Tsh. Bilioni 1.2

  0 0


  Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Umma Bw.Peter Mushi (wa pili kushoto) akizungumza alipokuwa akiendesha mkutano kwa njia ya video na Sekretarieti ya Mkoa wa Mara jana jijini Dar es Salaam (watatu kulia) ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Umma Bw. Leonard Mchau .
  Baadhi ya watendaji kutoka wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiendelea na Mkutano kwa njia ya Video na Sektertarieti za Mikoa ya Lindi,Mara,Geita,Singida na Shinyanga jana jijini Dar es Salaam.
  Mwandishi wa Habari kutoka kituo cha Televisheni cha ITV Bw. Hendry Mabumo akimuuliza swali Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao Bw.Charles Senkondo ambaye hayupo katika picha jana jijini Dar es 


  Na Anna Nkinda–Maelezo
  WATANZANIA wametakiwa kutumia technolojia ya mawasiliano ikiwemo kufanya mikutano kwa njia ya video ambayo itawaondolea gharama ya kusafiri na hivyo kuokoa fedha  na muda.

  Rai hiyo imetolea   hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Charles Senkondo wakati akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kazi wa video conference kati ya Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Taasisi zake, Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za mitaa.

  Senkondo alisema kufanya mikutano kwa njia ya video kunamfanya mtu asisafiri na hivyo kuepukana na ajali, kutopoteza muda awapo safarini na na kupata wasaa wa  kukaa na familia yake.

  “Kuanzishwa kwa TaGLA kumeongeza uwezo wa kufanya kazi kwa ubunifu zaidi, kwa njia ya kisasa, kwa maamuzi zaidi ya kiuendeshaji kwa kuangalia kila mara mahitaji ya wadau na kutumia mbinu za soko katika utoaji wa huduma bora”.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano na Huduma Kwa Wateja (Call center) ambacho kitahusika na kupokea na kujibu hoja za wadau mbalimbali zitakazowasilishwa katika Mfuko kupitia Namba ya simu 0800 110063, barua pepe info@nhif.or.tz na mawasiliano kwa njia ya mtandao (Mitandao ya kijamii na simu za mkononi), uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es salaam.Picha na Michuzi Blog
  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Rehani Athumani (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano na Huduma Kwa Wateja (Call center) ya NHIF, uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es salaam.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SoftNet Tech, Nuru Yakub Othman wakishirikiana kuzindua rasmi Kituo cha Mawasiliano na Huduma Kwa Wateja (Call center) cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es salaam.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Meneja uendeshaji wa Modewji Foundation ,Francesca Tettamanzi akiwa ameambata na wafanyakazo wa kampuni ya METL walipotembelea kituo cha mafunzo cha Furahini cha wilayani Mwanga. 
  Afisa Udhibiti wa Ubora wa elimu ya msingi wilaya ya Mwanga ,Richard Joachim akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo cha mafunzo cha vijana cha Furahini klichopo Kisangara wilayani Mwanga. 
  Meneja uendeshaji wa Modewji Foundation ,Francesca Tettamanzi akifungua mfano wa hundi kwa ajili ya kukabidhi kwa mkurugenzi wa kituo hicho
  Wakiwa katika picha ya pamoja.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.


  0 0


  Vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wa Vicoba, Saccos na wasindikaji
  ngozi waMji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,
  wakiwa kwenye kongamanola uhamasishaji wa mpango wa bima ya afya kwa 
  wajasiriamali na vikundivilivyosajiliwa (Kikoa) 
  Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) Mkoani Manyara, 
  Isaya Shekifu akizungumza jana katika kongamano la uhamasishaji wa mpango 
  wa bima ya afya wa kikoa kwa wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mji 
  mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro (kulia) ni Mkuu wa wilaya hiyo 
  Mahamoud Kambona na kushoto ni mratibu wa NHIF na mfuko wa afya ya jamii 
  (CHF) mkoani humo Reginald Kileo.
  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambonaakizungumza 
  wakati akifungua kongamano la uhamasishaji wa mpango wa bima yaafya wa 
  kikoa kwa wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mji mdogo 
  wa Mirerani, (kushoto) ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya 
  Nchini (NHIF) wa mkoahuo, Isaya Shekifu na kulia ni Ofisa Tarafa ya 
  Moipo Joseph Mtataiko.

  0 0

   Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu waliofika Bandari Kuu ya Zanzibar kushuhudia kuwasili kwa Meli mpya ya MV. MAPINDUZI II ikitokea Korea kusini.
  Meli mpya ya  MV. MAPINDUZI II ikiwa nje kidogo ya Bandari ya Zanzibar kabla ya kufunga gati Bandarini hapo.
    Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee akitoa maelezo kwa waandishi wa Habari juu ya matumizi ya gharama zilizotumika mara baada  ya kuwasili kwa Meli ya MV. MAPINDUZI II Mjini Zanzibar.

  0 0


  Mwongozaji mahiri wa filamu ya Homecoming inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni, Seko Shamte. Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Alkemist Media ina ujumbe wa kuhusiana na vishawishi vya rushwa pamoja na athari zake kwa wafanyakazi na jamii kwa ujumla.
  Crew nzima pamoja na baadhi ya waigizaji
  Moja kati ya kamera kali zilizotumika.

  0 0  0 0

    Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati wa kikao na wahariri wa magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania.

    Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akizungumza huku Mhariri Mkuu wa Magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania Ndugu Godfrey Dilunga akimsikiliza kwa makini.
  Mhariri Mkuu wa Magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania Ndugu Godfrey Dilunga akiwatambulisha baadhi ya viongozi wa kampuni ya Magazeti ya Raia Mwema.

  KATIBU wa NEC (CCM) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye leo ametembelea ofisi za kampuni ya Raia Mwema inayotengeneza magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania, kwa lengo la kushukuru na kueleza mikakati ya chama chake
  .

  Itakumbukwa miezi kadhaa iliyopita kabla ya uchaguzi mkuu Nape, alitembelea vyumba vya habari akianzia na Raia Mwema kueleza pamoja na mambo mengine namna walivyojipanga na uchaguzi ikiwemo kupata mgombea urais.

  Akizungumza jana katika ofisi hizo alipokutana na wahariri pamoja na viongozi mbalimbali wa kampuni hiyo alisema, wanafurahishwa na kasi ya Rais John Magufuli, kwa sababu kinachotendeka sasa walikipanga hata kabla ya uchaguzi.

  “Tulitaka mtu wa aina hii, haya mabadiliko tuliyarataji hivyo hatushituki kuyaona, tunachotaka kuwaambia wananchi tu ni kuwa baada ya kumaliza serikalini mabadiliko yatahamia kwenye chama,” alisema Nape.    BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mwandishi Wetu

  VINARA wa Ligi Daraja la Kwanza katika kundi (A) klabu ya Friends Rangers, imesajili wachezaji wanne ambao Emanuel Gabriel, Fred Cosmas, Mussa John 'Rooney' na Ramadhan Chombo 'Redondo' kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi hiyo unaotarajia kuanza hivi karibuni.

  Ofisa Habari wa klabu hiyo Asha Kigundula, alisema kuwa katika kuhimalisha kikosi chao, wameamua waongeze wachezaji wanne ambao watasaidia kupandisha timu yao.

  Kigundula alisema kuwa hata hivyo kikosi chao kitaenda kuweka kambi ya wiki moja Lushoto mkoani Tanga, kama sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili.

  Alisema kuwepo kwa wachezaji hao ambao waliwahi kuvituzimikia klabu kubwa hapa nchini kutasaidia kujenga zaidi kikosi chao ambacho kimekuwa moto wa kuotea mbali.

  Alisema katika msafara huo jumla ya watu 40, wataenda katika kambi hiyo maalum, kikiongozwa na Katibu Mkuu wa timu hiyo na Heyry Chibakasa (Herry Mzozo).

  Rangers yenye maskani yake magomeni Kagera Dar es Salaam, ndiyo wanaoshika usukani wa Ligi Daraja la kwanza katika kundi A.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kulia) akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Volountary Service Overseas (VSO) Dkt.Philip Goodwin alipo mtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuishukuru Serikali kwa ushirikiano inaowapa katika kufanikisha majukumu yao.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (katikati) akielezea jambo wakati wa kikao baina yake na ujumbe kutoka Shirika la Voluntary Serverce Overseas (VSO) jana jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la Kiserikali la Volountary Service Overseas (VSO) Dkt.Philip Goodwin na kulia ni Mkurugenzi wa Voluntary Service Overseas nchini Bw. Jean Van Wetter.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (watatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Shirika la Voluntary Serverce Overseas (VSO)Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Bibi. Esther Liwa,Mkurugenzi wa Kanda wa VSO Bibi. Niki Kandirikirika, Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la Kiserikali la Volountary Service Overseas (VSO) Dkt.Philip Goodwin, Mkurugenzi wa Voluntary Service Overseas nchini Bw. Jean Van Wetter na Meneja Mradi wa ICS kutoka VSO Bibi. Imisa Masinjila Picha na Frank Shija, WHVUM

  0 0

  Dear Mum, 
  NINETEEN VERY PAINFUL YEARS have gone today without you our dear Mother.  
  The pain of losing you will never go away because you were what we treasured most in our lives. A loving, caring, understanding and devoted mother and a friend.  You were our pillar, a source of happiness and strength. 
  Mom, we love and miss you so much and each passing day we wish you were here with us.  We are still struggling to accept the reality of your death.  We however, continue drawing our strength from the unique memories of your love, care and wisdom, and from the solid foundations you laid for us.  
  Our guardian Angel, we feel your presence each and every day as we meet and overcome challenges in our lives.  We thank God for His love and Grace for seeing us through all these trying years.  He is indeed taking good care of us.  We are looking forward to reuniting with you and Dad in God’s Glory.  MAY YOUR SOUL REST IN ETERNAL PEACE. AMEN  
  Fondly remembered by your loving children Nelly, Gerald, Louisa, Alice, Susan and Andrew, son in-laws Pascal, Rikard, Peter and Alvin, grand children Jadden, Nelly, Andrew, Simon and Mercy, relatives and friends.  Rest in Peace Mama.


  0 0

  SIMU.TV:  Waandishi wa habari wametakiwa kutoa taarifa sahihi kuhusiana na sekta ya mafuta na gesi na namna ambavyo wananchi wanavyoweza kunufaika kwa kuwekeza katika sekta hiyo; https://youtu.be/-gTe6ft787E

  SIMU.TV:  Katibu wa CCM Mkoani Mara Adam Ngalawa amesema chama hicho hakitasita kuwachukulia hatua madiwani wateule wa chama hicho watakaoshindwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo; https://youtu.be/aWLqGy90_fU

  SIMU.TV:  Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Fatma Ally amewataka wanafunzi kujikita katika masomo maana wao ndio wanaoweza kuleta mabadiliko ya kweli katika elimu; https://youtu.be/0W4AalnDdh4

  SIMU.TV:  Asasi za kiraia zimetakiwa kuwa wabunifu katika kuendeleza miradi ya maendeleo badala ya kutegemea misaada kutoka nje; https://youtu.be/GAhtEmVVf-4

  SIMU.TV:  Wafanyakazi 635 wa mgodi wa Tanzanite One Simanjiro kupunguzwa kazini kutokana na uzalishaji kutoridhisha; https://youtu.be/Uc9gdRNi9SQ

  SIMU.TV:  Mamlaka ya mapato TRA ikishirikiana na Jeshi la polisi imeanza ukaguzi wa Makontena yaliyokamatwa eneo la Tangi Bovu Dar es salaam. https://youtu.be/9v3LpDchQgQ

  SIMU.TV:  Naibu katibu mkuu wa Ardhi amemtaka Afisa ardhi Halmashauri ya Mkoa wa Tanga kuacha kusoma ramani za viwanja.  https://youtu.be/OWtpN-_eA94

  SIMU.TV:  Asasi za kiraia zaidi ya 250 toka Tanzania bara na visiwani zimekutana jijini Dar kujadili utekelezaji wa mpango wa malengo endelevu wa MDGs 17. https://youtu.be/GJ_jDiTDZu4

  SIMU.TV:  Madereva wa boda boda Manispaa ya Musoma wamefanya mgomo kushinikiza uongozi wa Manispaa kufuta tozo ya sh. 100,000 https://youtu.be/sALK42BX7Wg 

  SIMU.TV:  Mamlaka ya udhibiti wa Nishati na maji EWURA imetangaza kupungua kwa bei mpya elekezi ya Mafuta; https://youtu.be/FqVjtjbi7dE

older | 1 | .... | 1042 | 1043 | (Page 1044) | 1045 | 1046 | .... | 3285 | newer