Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1040 | 1041 | (Page 1042) | 1043 | 1044 | .... | 3270 | newer

  0 0

  SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeandikisha wakulima wa Korosho zaidi ya 300 mkoani mtwara kwenye kampeni ijulikanayo kama NSSF Kwanza ambayo ilifanyika mahususi ili kuwafikia watu ambao wako kwenye sekta isiyo rasmi.

  Kampeni hiyo yenye malengo ya kufikia umma wa Watanzania ambao haujafikiwa na elimu ya Hifadhi ya jamii, Kuwaandikisha kujiunga na NSSF ili kuongeza wigo wa wanachama na pia Kupata mrejesho wa huduma zetu kutoka kwa wanachama wa mfuko.

  Imemaliza mkoani Mtwara na itaendelea kwenye mikoa mingine.
  NSSF inaendelea kuwasihi Watanzania waendelee kujiunga na NSSF.
  Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (wa pili kulia), akiwapa maelezo kuhusu huduma zitolewazo na NSSF wakulima wa Kijiji cha Msijute, Kata ya Mayanga, mkoani Mtwara, kwenye kampeni maalumu ijulikanayo kama ‘NSSF Kwanza’, ambayo inaendelea kwa kuwafikia watu walio kwenye sekta binafsi.
  Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akiwapa maelezo wakazi wa kijiji cha Msijute jinsi ya kujiunga na Huduma ya mafao ya Matibabu bure kwenye kampeni maalumu ya kuwaelimisha wakazi wa Mkoa wa Mtwara juu ya faida za Hifadhi ya Jamii kupitia NSSF.
  Wakazi wa Kijiji cha Msijute kata ya Mayanga Mkoani Mtwara wakijiandikisha NSSF ili kuweza kujipatia mafao bora kutoka NSSF yakiwemo mafao ya matibabu bure kwa wanachama na familia zao.

  0 0

  Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Samson Majwala (katikati) na akionyesha Mkuu wa Bidhaa za Rejareja, Sylvester Manyara wakionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) simu zilizoingia kwenye kampeni maalum ya Msimu wa Sikukuu ijulikanayo kama “Jiekotishe na Huawei”, wakati wa uzinduzi wake uliofanyika leo Jijini Dar es salaam. Kulia Meneja Masoko wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Lyidia Wangari.
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Lyidia Wangari, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni maalum ya Msimu wa Sikukuu ijulikanayo kama “Jiekotishe na Huawei”, wakati wa uzinduzi wake uliofanyika leo Jijini Dar es salaam. Wengine pichani toka kulia ni Msemaji Mkuu wa Kampuni ya Huawei, Jimmy Jin, Mkuu wa Bidhaa za Rejareja, Sylvester Manyara pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Samson Majwala.
  Mabalozi wa kampeni ya “Jiekotishe na Huawei” wakilifanyikisha tukio ya Selfie kwa kutumia simu mpya aina ya Huawei P8 lite.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  Chama cha Mapinduzi CCM kimekanusha Taarifa iliyozagaa katika Mitandao ya Kijamii kwamba Chama hicho kimeridhia aliyekuwa Mgombea wa Urais wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akabidhie nchi kuiongoza kwa miaka mitano. 

  Akikanusha Taarifa hiyo mbele ya Waandishi wa Habari Afisini kwake Kisiwandui Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai amesema taarifa hiyo ni uzushi uliotungwa ili kuwatia taharuki WanaCCM na Wananchi kwa Ujumla. 

  Amesema toka kusambaa kwa Taarifa hiyo Jana amekuwa akipigiwa simu na Watu mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kujua ukweli wa Taarifa hiyo hasa ikizingatiwa kuwa ilidaiwa kusainiwa na Naibu huyo. “Huu ni Uzushi Mkubwa na kwamba unafaa kupuuzwa maana hauna lengo jingine zaidi ya kuwagawa WanaCCM” Alismema Vuai. 

  Amesema kilichopo nikwamba CCM inajiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa Marejeo kama ambavyo Tume ya Uchaguzi ilitangaza kuufuta Uchaguzi na hivyo kurudiwa upya. Aidha Vuai amesema kuwa tayari wamewasiliana na Wanasheria wao pamoja na wataalamu mbalimbali ili kuwabaini waliohusika kusambaza Taarifa hizo na kuwapeleka katika Vyombo vya Sheria. 

  “Tumeshafanya mawasiliano na Wataalam wetu na tukiwabaini Sheria ya Makosa ya mtandao itachukua nafasi yake” Alisema Vuai. 

  Katika taarifa hiyo iliyosambaa na kudai kusainiwa na Vuai Ali Vuai ilisema kuwa Chama cha mapinduzi kimeridhia na kukubali kumpa nchi Maalim Seif Sharif kupitia chama chake cha Cuf kuwa ndio rais wa uchaguzi ulopita,na yeye ndio atakayeongoza serikali ya umoja wa kitaifa. 

  Taarifa hiyo ilieleza kuwa CCM imekubali kushirikiana na maalim Seif katika kuongoza nchi chini ya serikali ya umoja wa kitaifa na kukubali kutoa makamo wa kwanza wa rais na nusu ya mawaziri. 
  Vuai amerejea kauli yake kuwa mazungumzo yanayofanywa na Viongozi wa Kitaifa kwa kushirikiana na Viongozi Rais Wastaafu wa Zanzibar hayawezi kubatilisha maamuzi ya Tume ya kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita. 


  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR


  0 0

  Na Mark B. Childress, Balozi wa Marekani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

  Mwaka mmoja uliopita wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, niliandika makala kuhusu jitihada za kuwa na kizazi kisicho na UKIMWI nchini Tanzania.  Toka wakati huo, kwa pamoja tumepiga hatua muhimu kuelekea katika kufikia azma hiyo, tukielekeza rasilimali na shughuli zetu kwenye maeneo yenye mahitaji zaidi nchini kote. Hata hivyo, bado tunahitajika kuongeza nguvu na kufanya zaidi. Bila ya kuongeza kasi yetu katika mwelekeo huu, maambukizi mapya yataongezeka, jambo litakaloongeza idadi ya Watanzania watakaokuwa wakiishi na VVU hivyo kuathiri maendeleo na ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

  Kipindi cha miaka mitano ijayo ni kipindi muhimu sana katika kufikia lengo la kutokomeza kabisa UKIMWI duniani ifikapo mwaka 2030. Rais Obama ameweka malengo makubwa kwa Mpango wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti UKIMWI (PEPFAR), akitangaza kuwa hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017, PEPFAR itakuwa inawasaidia watu milioni 12.9 kupata matibabu yanayookoa maisha ya  kufubaza VVU na kuwawezesha wanaume milioni 13 duniani kote kupata tohara.  Aidha, kwa kushirikiana na wadau wa kiserikali, asasi za kiraia na sekta binafsi, PEPFAR itajielekeza katika kupunguza maambukizi ya VVU kwa asilimia 40 miongoni mwa wanawake vijana na wasichana katika nchi zilizoathiriwa zaidi  zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

  SOMA ZAIDI HAPA

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika tarehe 09 Desemba 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami.

  Tayari fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara hapa nchini TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo, linalopaswa kuanza mara moja.

  Akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi PATRICK MFUGALE Ikulu Jijini Dar es Salaam, Dkt. Magufuli ametaka ujenzi wa barabara hiyo uanze haraka ili kukabiliana na adha ya msongamano wa magari katika  barabara hiyo
  Kujengwa kwa njia hizo kutaifanya barabara ya Morroco hadi Mwenge kuwa na njia tano.

  Wakati huo huo, Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba Ikulu Jijini Dar es salaam.

  Katika Mazungumzo hayo Prof. Lipumba amempongeza Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kwa kutoa hotuba nzuri ya uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokonga nyoyo za Watanzania.

  Kwa Upande wake Rais Magufuli amempongeza Prof. Lipumba kwa msimamo wake thabiti wa kupinga ufisadi na amemtakia heri katika shughuli zake.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
  Dar es Salaam.
  30 Novemba,2015
  Sehemu ambako utaanzia upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami kufuatia agizo la Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli la kutumia fedha shilingi bilioni nne zilizopaswa kutumika kugharamia Shamrashamra za siku ya Uhuru Desemba 9, 2015 kutumika kufanya upanuzi wa barabara hiyo. PICHA NA IKULU

  0 0

   Mbunge wa jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi akizungumza na wananchi wa jimbo la mlalo wakati Mkuu wa mkoa wa Tanga alipotembelea mradi wa maji wa  jimbo hili na wakatiwa sherehe ya kumpongeza, katika hafla fupi ilifanyika maeneo ya Mlalo Mkongoloni mwishoni mwa wiki.
   Mkuu wa mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza atembelea wilaya ya Lushoto na kuangalia miradi ya maendeleo ya Serikali ikiwepo maabara na mradi wa maji wilayani Lushoto Mkoani Tanga  baada ya kabla ya hafla fupi ya Mbunge wa jimbo la Mlalo iliyofanyika maeneo ya Mlalo mwishoni mwa wiki.
  Baadhi ya wananchi na madiwani wa jimbo la Mlalo waliokusanyika kwaajili ya kukubali wito wa Mbunge wa Mlalo,Rashid Shangazi mara baada ya Mkuu wa mkoa wa Tanga kukagua mradi wa maji katika jimbo la Mlalo, na Mbunge wa jimbo hilo kufanyiwa sherehe ya kumpongeza hafla hiyo iliyofanyika katika jimbo hilo wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

  0 0


  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Moshi.

  MKUU wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, amefanya ziara ya kushtukiza katika masoko manne ya Manispaa ya Moshi pamoja na dampo za kukusanyia uchafu, ili kujionea hali ya usafi na utendaji kazi katika mkoa huo. Katika ziara hiyo, RC Makalla alitumia muda huo kuwaagiza watendaji wake, hususan katika mchakato mzima wa kuifanya Moshi iwe kwenye usafi.
  Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla mwenye miwani, akikagua soko lililopo kwenye Manispaa ya Moshi, mkoani humo, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kujionea hali ya usafi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

  Akizungumzia ziara yake hiyo, Makalla alitoa siku tatu kwa watendaji wa Manispaa ya Moshi kuhakikisha kwamba lundo la takataka katika soko la Kwasadala linaondoshwa haraka iwezekanavyo. Alisema hawezi kukubali kuona Manispaa hiyo inashuka kiwango chake cha kuifanya Moshi inaendelea kuheshimika katika suala zima la usafi.
  Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla aliyesimama mlangoni, akiendelea na ziara yake ya kushtukiza kwenye Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro kujionea hali ya usafi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto) akizungumza na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati Rais na Waziri Mkuu walipomtembelea Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015 kwa mazungumzo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiagana na  Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015. Wa pili (kulia) ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais, Mohamed Khamis. 
  Picha na OMR.

  0 0

   Kamera ya Mtaa kwa Mtaa yanasa muendesha Bajaji akivunja sheria kwa kupita pasipo ruhusiwa kupita, hii ni pamoja na kuharibu miondo mbinu ya Barabara ya  mabasi yaendayo haraka ya Morogoro (Strabag) jijini Dar es Salaam.
  Madereva wa magari haya mambayo yameshindwa kupishana kwa usahihi  wakielewana mara baada ya kugongana leo katika Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, kama walivyonaswa na kamera ya Mtaa kwa Mtaa.
  Mchana huo marekebisho ya hali ya tumbo yakiendelea katika sehemu ya chakula kama ilivyonaswa na kamera ya Mtaa kwa Mtaa.

  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii).

  0 0


  0 0

  Na Shamimu Nyaki-Maelezo 

  Serikali imewaagiza watumishi wa umma kushiriki zoezi la usafi wa  nchi  litakalofanyika tarehe 9 disemba mwaka huu katika maeneo yao wanaoishi.

  Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw Assah Mwambene alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijin Dar es salaam na kusema kwamba Watumishi wa Umma  wanatakiwa wabaki nyumbani na kufanya usafi katika maeneo yao na  yale watakayo pangiwa na viongozi wa mitaa wanayoishi.

  “Kila mwananchi ahakikishe eneo lake ni safi”Alisema Mwambene.

  Mkurugenzi ameongeza kuwa Watumishi wa Umma hawataenda kazini badala yake  watabaki  nyumbani na kufanya usafi kwa kushirikiana na wananchi kusafisha maeneo yanayozunguka mitaa wanayoishi ikiwemo hospitali,kuzibua mitaro iliyoziba pamoja na kuzoa taka zilizolundikana sehemu ambazo sio rasmi.

  Ameongeza kuwa muongozo kuhusu namna zoezi la usafi litakavyotekelezwa umeshatolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI  kwa Uongozi wa Mikoa hadi Mitaa na kilichobaki ni utekelezaji tuu wa agizo hilo kwa kila mwananchi sehemu anayoishi,anayofanyia shughuli nyingine za kila siku kuhakikisha anafanya usafi.

  Aidha Mkurugenzi amewataka viongozi wa kila eneo kutengeneza utaratibu mzuri ambao utafanikisha zoezi la usafi  kufanikiwa kwa kuhakikisha wanasimamia kwa ukamilifu na kuwahimiza wananchi kuwa na tabia ya kusafisha maeneo wanaoishi kwa kuwa ni wajibu wao kufanya hivyo.

  Hata hivyo tarehe tisa disemba kila mwaka huwa ni siku ya kusherehekea Uhuru wa Tanganyika uliopatikana miaka hamsini na nne iliyopita lakini kwa mwaka huu itaadhimishwa kwa kufanya usafi nchi nzima.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Michael Mhando akikagua Kituo cha Kisasa cha Matibabu kilichopo katika Hospitali ya Mkoa Dodoma. Kituo hicho kinatarajiwa kuanza kutumika mwishoni mwa mwaka huu.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF akionesha ufunguo wa kituo hicho baada ya kukabidhiwa na baadae alikikabidhi rasmi katika uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
  Na Mwandishi Wetu

  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekabidhiwa kituo chake cha matibabu cha mfano mara baada ya ujenzi wa kituo hicho kukamilika.

  Makadhiano hayo yalifanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Uongozi wa NHIF, hospitali ya mkoa na timu ya wakandarasi akiwemo mshauri mkuu wa mradi huo wa kampuni ya Nosuto Associates.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando amesema kukamilika kwa jengo hilo ni hatua kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na kazi iliyoko sasa ni ya ununuzi wa vifaa na samani za jengo ili lianze kutoa huduma kabla ya sikukuu ya Krismasi.

  Amesema timu ya wataalamu kutoka Sekteratarieti ya mkoa tayari iko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchagua vifaa tiba mbalimbali vitakavyotumika. Ameongeza kuwa vifaa vyote hivyo pamoja na samani za jengo hili vitalipiwa na Mfuko wa NHIF.

  Kituo hicho cha matibabu cha kisasa kinayo mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika utoaji wake wa huduma ikiwemo miito kwa wauguzi, utayarishaji wa madai na utambuzi wa wagonjwa.

  Amesema malengo makuu ya ujenzi wa kituo hicho ni kuwa na kituo cha kisasa kitakachowezesha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na umma wa watanzania kwa ujumla kupata huduma bora za matibabu wanapokuwa Dodoma katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.

  Naye Mkurugenzi wa fedha, Mipango na Uwekezaji wa NHIF Bw. Desudedit Rutazaa amesema Kituo hicho vilevile kitasaidia kuwepo na watalamu wenye uzoefu nchini kwani itakuwa ni sehemu ya kujifunzia kwa wataalamu wa kada mbalimbali za udaktari na utabibu wawapo masomoni katika mkoa wa Dodoma na mikoa mingine ya Tanzania. Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma_sehemu ya mapokezi.

  0 0


  0 0
 • 11/30/15--07:17: BIASHARA POPOTE


 • 0 0

  Unasumbuliwa  na  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  ?
  Unahitaji  kupata  tiba  sahihi  na  ya  uhakika  ya  tatizo  lako ?  Kama  jibu  ni  NDIO  basi  hii  ni  HABARI  NJEMA  SANA   kwako.

  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL FOODS  CLINIC    ni  duka  linalo  uza  dawa  mbalimbali  za  asili.  Tunayo  dawa  asilia iitwayo  JIKO  ambayo  inatibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.  Dawa  hii  ni  ya  asili  kabisa, isiyo  na  kemikali  za  viwandani  na IMETHIBITISHWA  NA  MKEMIA  MKUU  WA SERIKALI.

  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU. Tunapatikana  UBUNGO  DAR  ES  SALAAM   karibu  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

  Kwa   wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu, watapelekewa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  Dar  Es  Salaam. Kwa  wateja  waliopo  mikoani, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  mabasi. Kwa  wateja  waliopo  Zanzibar  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  Boti  na  kwa  wateja  waliopo  ughaibuni  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

  Kufahamu  zaidi  kuhusu  tatizo  la  ukosefu & upungufu  wa  nguvu  za  kiume  na  jinsi  dawa  ya  JIKO  inavyo  fanya  kazi, tafadhali  tembelea :


  Na  kwa  mahitaji  yako  ya  awa  ya  JIKO
   wasiliana  nasi  kwa simu 0766  538 384.

  0 0

   Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai  Bw.Diwani Athumani (CP) akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo katika picha leo jijini Dar es Salaam kuhusu uchunguzi wa sakata la watuhumiwa wa wizi wa makontena 329.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Bw.Diwani Athumani (CP) alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu uchunguzi wa watuhumiwa wa wizi wa makontena kwa Mamlaka ya Bandari na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

  Na Nyakongo Manyama-Maelezo
  KUFUATIA agizo laWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka watuhumiwa wa wizi wa makontena 329 katika bandari ya Dar es salaam kuchukuliwa hatua na Jeshi la Polisi, tayari Jeshi hilo limewashikilia watuhumiwa kumi na mbili wanaohusika na wizi huo. 

  Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CP) Diwani Athumani amesema kuwa, uchunguzi unaofanywa na wataalamu waliobobea katika makosa ya uhalifu wa kifedha umeweza kuwabaini watu kumi na mbili ambao wamehusika na wizi huo.
  “Kati ya watuhumiwa hao kumi na mbili, watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na saba bado wapo katika upepelezi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Athumani.


  Wanaoshikiliwa kutokana na tuhuma mbalimbali ni Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru TRA Bw. Tiagi Masamaki, Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru na  Habibu Mponezia, Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha.
  Watuhumiwa wengine ni pamoja na Bi. Eliaichi Mrema, Msimamizi Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta Bw. Haroun Mpande na Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara Bw. Hamis Omary.


  Aidha Kamanda Athumani amewaomba wananchi wenye taarifa za ubadhilifu wa mali za Umma kuendelea kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yake. 

  0 0

  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa Korea ya Kusini hapa nchini Mhe. Chung IL, wakati akimkaribisha na kufanya nae mazungumzo, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.
  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Korea ya Kusini hapa nchini Mhe. Chung IL, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.
  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.
  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.


  0 0
 • 11/30/15--12:00: Article 5


 • 0 0  Hiki choo cha ajabu kiko Shinyanga maelezo yapo chini.Leo Jumatatu Novemba 30,2015 ambapo mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameanza kufanya ziara kutembelea kata za manispaa hiyo ili kuangalia hali ya usafi wa mazingira kubwa zaidi ni kukagua vyoo vya wananchi ilimkukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.Mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga alikuwa ameambatana na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna,mwanasheria wa manispaa hiyo Simon Jilanga,afisa afya wa manispaa hiyo Heri Nakuzelwa,waandishi wa habari na askari wa jeshi la polisi.Mkuu huyo wa wilaya ametembelea kata ya Chibe na Kambarage na kubaini kuwa kaya nyingi hazina vyoo na kuagiza wajenge vyoo haraka huku akifunga maduka matano kutokana na kukosa vyoo.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo kwenye msafara huo ametusogezea picha 37 kilichojiri....  Ziara ilianzia katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga.Pichani ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(mwenye kofia) akijiandaa kutembea mtaa kwa mtaa kukagua vyoo.Ziara ya mkuu huyo wa wilaya imekuja siku chache tu baada ya kufanya mkutano mkubwa na akina mama wa manispaa ya Shinyanga kujadili namna ya kupambana na ugonjwa wa kipindupindu ambapo mpaka sasa umeua watu watatu kati ya wagonjwa 98 waliripotiwa kukumbwa na ugonjwa huo unaotokana na mtu kula au kunywa kinyesi cha mtu mwingine baada ya kuingia kwenye maji au chakula.  Msafara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ukielekea katika mtaa wa Chibe ambapo katika kata ya Chibe ina jumla ya kaya 1500 lakini kaya 398 hazina vyoo,lakini kati ya hizo kaya 1500 nyingi hazina vyoo bora.
  Kwa picha na habari zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1040 | 1041 | (Page 1042) | 1043 | 1044 | .... | 3270 | newer