Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Maagizo ya Rais Magufuli kuhusu safari za nje za watendaji wa Serikali yaanza kutekelezwa

$
0
0
Kufuatia maagizo ya Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa hivi karibuni ya kusitisha safari za nje kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeanza kutekeleza maagizo hayo kwa kutoa maelekezo mahsusi kwa Balozi zake nje.

Wizara imezielekeza Balozi zote zilizopo maeneo mbalimbali duniani kujipanga ili kushiriki kikamilifu katika kuiwakilisha Serikali kwenye mikutano yote ya kimataifa na kikanda inayofanyika katika maeneo yao ya uwakilishi. Tanzania inazo Balozi 35; Balozi Ndogo tatu; Vituo viwili vya Biashara; na Konseli za Heshima 17 katika nchi mbalimbali. Hizi zote zitahusika katika kuendeleza utekelezaji wa Diplomasia yetu ya Uchumi na uwakilishi wa maslahi ya nchi yetu.

Aidha, hadi sasa Mikutano ambayo tayari imefanyika na Balozi zetu kuwakilisha ni pamoja na Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoendelea nchini Malta na Mkutano wa Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Habari wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika nchini Lesotho.

Aidha, Wizara inatoa wito kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kuwasilisha mapema taarifa za mikutano inayohusu sekta zao ili kutoa fursa kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuzifanyia kazi kwa wakati ili kuhakikisha ushiriki wa Tanzania unakuwa wenye tija kwa taifa.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inaungana na wadau wengine kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa hatua anazozichukua za kuleta ufanisi mkubwa wa kazi na kubana matumizi ili kuiwezesha Serikali kuwahudumia wananchi kikamilifu.

Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
27 Novemba, 2015

KAMANDA MPINGA AZINDUA OPERESHENI PAZA SAUTI,JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohamed Mpinga, akisalimiana na Mabalozi wa Usalama Barabarani, muda mfupi kabla ya kuzindua Operesheni ijulikanayo kwa jina la “Paza Sauti” yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga, akitoa maelekezo ndani ya moja ya basi linalofanya safari zake mkoani wakati wa kuzindua wa Operesheni Paza Sauti yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Wadau wanaotumia usafiri wa barabara, wakiwemo madereva na abiria wakimsikiliza Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga(hayupo pichani) alipozindua Operesheni Paza Sauti, yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani,Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo na Matukio wa Mabalozi wa Usalama Barabarani,Jackson Kalikumtima(kulia), akitoa elimu kuhusiana na Operesheni ya Paza Sauti kwa mmoja wa wadau wanaotumia usafiri wa barabara, Operesheni hii ilizinduliwa Stendi ya Mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo, jijini Dar es Salaam leo.(Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Mkurugenzi wa Benki ya Amana afunga wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Mwanza

$
0
0


Mkurugenzi wa Amana Bank Dk Muhsin Masoud akimzawadia Bw Juma Kivuruga kwa kuwa mfanyakazi bora kwa tawi la Mwanza, Kivuruga alipigiwa kura na wafanyakazi wenziye wa tawi hilo.
Daud Lweno akizawadiwa na Mkurugenzi wa Amana Bank kama mteja mzuri kulipia miamala ya TRA katika tawi la Mwanza. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

EALA ENACTS FOREST MANAGEMENT BILL

$
0
0
EALA has passed the EAC Forests Management and Protection Bill 2015 in effect putting in place a regional framework to conserve the environment. 
 The Bill whose mover is Hon Christophe Bazivamo sailed through at its 3rd Reading after the Committee stage scrutinized its various clauses, proposing amendments. 
 The Report of the Agriculture, Tourism and Natural Resources was presented by Hon Judith Pareno on behalf of the Chair. 
 The EAC Forestry and Management Protection Bill, 2015 hopes, to promote the development, protection, conservation, sustainable management and use of the forests in the Community especially trans-boundary forests ecosystems, in the interest of present and future generations. It further wants to espouse the scientific, cultural and socio-economic values of forests and harmonise national forest laws. 
 Once amends are integrated, the Bill is expected to undergo assent by the Heads of State in line with Article 63 of the Treaty for the Establishment of EAC.The Bill seeks to operationalize Article 112 (1) d) of the Treaty for the Establishment of the EAC in which Partner States undertook to co-operate in the management of the environment and agreed to take necessary disaster preparedness, management, protection and mitigation measures especially for the control of natural and man-made disasters. 
 The Bill delineates the roles and responsibilities of Partner States and seeks to promote uniformity and integration in the area of Disaster Risk Reduction (DRR) and management.
Finally, the Bill seeks to create a regional mechanism which would enable a timely intervention in disaster situations. The Assembly had at its last sitting in Nairobi in October 2015, adjourned debate on the Bill. 
 The adjournment at Committee stage followed the successful Motion for the same, tabled by the Chair of EAC Council of Ministers, Hon Dr Harrison Mwakyembe, seeking for more time to enable the United Republic of Tanzania to make input. Hon Dr Mwakyembe then informed the House that the United Republic of Tanzania was expected to go to the polls in October and that it was necessary for the debate to be put on hold until such time that a new Government is in place to effectively enable the Partner State to make its input. 
 The Bill has five parts with the Preliminaries and objectives contained in Part 1. Part two covers general measures on forest management and protection while Governance and institutions of forest management and control are entailed in part 3 of the Bill. 
 Part 4 amplifies trade in forest related products while section 5 envisages co-ordination matters under a Board known as the EAC Forests Board to be operationalized by the Council of Ministers. 
 The Plenary sitting resumes on Tuesday next week.
Hon Judith Pareno presented the Report of the Committee on Agriculture, Tourism and Natural Resources
Hon Christophe Bazivamo, mover of the Bill on Forestry Management and Protection Bill, 2015
The Secretary General, Amb Richard Sezibera (left) and the Minister for EAC Affairs, Rwanda, Hon Valentine Rugwabiza in discussions at the Plenary sitting yesterday

The BBC hosts debates throughout Africa as part of the 100 Women season More than 100 conversations across the world will discuss what it means to be a “good girl” or an “ideal woman”

$
0
0
On 1st December, BBC 100 Women – a season dedicated to shining a light on women’s lives around the world –will bring together a series of debates from across the globe, to be broadcast live on television on BBC World News, on Radio on the BBC World Service and online on bbc.com.

The BBC will host debates throughout the day at BBC Broadcasting House in London, while more than 100 conversations will happen across the globe in eight languages. In Africa, many groups across the continent will host discussions to contribute to the BBC’s live feed, including the Rape Crisis Centre in South Africa, Kinshasa Woman in the DRC, Women Journalists of Nigeria and the 50/50 group in Sierra Leone.

Focussing on leadership, image and relationships, the debates will ask women across the world if they feel they have to conform to what is considered the “right way” to behave. They will also be asked what they believe to be a “good girl” and who decides what is “good” – them, their family or society. The debates will also find out how women react to those pressures and expectations, and if they accept or reject them.

Fiona Crack, BBC 100 Women Editor said: “This debate is really special because we are giving women around the world the opportunity to have their voices heard on topics that matter to them. We’ll be tapping in to more than 100 conversations happening in almost 50 countries. The level of response we’ve had of people wanting to take part is testament to how needed these debates are. 
Also taking part in the debates are Solidarité FM Benin, Building Maison De La Bible in Burundi, the Women’s Lobby in Cameroon, Women of Character in Ghana, Marrakesh Inspiration in Morocco, The Senegal Women’s group, The University of West Cape in South Africa, the South Sudan Empowerment Network, the Centre for Domestic Violence Prevention in Uganda, the Zambia National Women’s Lobby and the Women’s Lawyers Association of Zimbabwe, amongst others. 
The BBC’s African languages services will cover these debates throughout the day – including special google hangouts. 
Watch LIVE at bbc.com/100women between 0930 and 1900 GMT
A recording of the event will broadcast on BBC World News at 0930-1000, 1330-1400, 1630-1700 GMT

Listen on the BBC World Service English 
at 1100-1200, 1500-1600, 1800-1900 GMT

 Join the conversation on Twitter #100women

JNIA YAONGEZA UKAGUZI MIZIGO YA POSTA, SASA KUKAGULIWA MARA YA PILI KABLA YA KUPAKIZWA KWENYE NDEGE

$
0
0

  Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, Bw.Injinia Thomas Haule, (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa uwanja huo leo Ijumaa Novemba 27, 2015. 
 
Utawala wa uwanja huo ulio chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, umejipanga upya katika kuimarisha ulinzi ambapo kuanzia sasa, vifurushi na mizigo yote kutoka posta itakaguliwa kwa mara ya pili kabla ya kupakiwa ndani ya ndege, ikiwa ni hatua ya kudhibiti vifurushi na mizigo haramu kupenya kwenye ndege. Kushoto ni Kaimu Meneja Usalama wa Uwanja huo, Bw.David Ngaragi, (kushoto) na Afisa Usalama Mwandamizi wa Uwanja huo, Dorice Uhagile. (Picha na K-Vis Media/Khalfan Said).
 
Na K-Vis Media
UONGOZI wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere unaomilikiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, umetangaza leo Ijumaa Novemba 27, 2015 kuwa kuanzia sasa vifurushi na mizigo mingine yote ya Shirika la Posta Tanzania, itakaguliwa kwa mara ya pili kama mizigo mingine yoyote kabla ya kupakiwa ndani ya ndege.
Uamuzi huo umetangazwa na Mkurugenzi wa Uwanja huo, (JNIA), Injinia Thomas Haule, wakati akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa VIP ulioko uwanjani hapo.Alisema, uamuzi huo ni baada ya Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege, TAA, kutoa maonyo kadhaa, kwa Shirika la Posta, kuimarisha ukaguzi wa vifurushi na mizigo itokayo Posta kwa vile imekuwa ikikamatwa na mizigo ambayo ni tofauti na iliyokusudiwa.
Alitaja mizigo hiyo kuwa ni pamoja nabangi, na kwamba, Uholanzi wamekuwa wakilalamika mara kadhaa kuwa wamekuwa wakikamata vifurushi vya Posta vikiwa na mizigo iliyoharamishwa.
"Sisi Kama Mamlaka, wajibu wetu mkubwa ni kuzuia kitu au vitu vyovyote vinavyoweza kuhatarisha usalama wa abiria wawapo ndani ya ndege au ndege yenyewe haviingii ndani ya ndege." Alianza kwa kusema Injinia Haule na kuongeza kuwa, vitu vingine kama madawa ya kulevya, pembe za ndovu, na vingine vingi, , vinashughulikiwa na mamlaka nyingine ambazo zina maafisa wake hapa JNIA wakishirikiana na maafisa wetu.
Hata hivyo makosa yafanywayo na idara Fulani ya serikali yenye afisa wake hapa JNIA, ni wazi kwamba watakaonyooshewankidole ni TAA, alisema na kubainisha kuwa Mamlaka haitavumilia tena uzembe utakaofanywa na taasisi nyingine ya serikali katika kuhakikisha zinatekeleza wajibu wake ipasavyo.
 Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, Injinia Thomas Haule, akizungumza kwenye mkutano huo
 Meneja wa Usalama wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Bw.David Ngaragi, akifafanua jambo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari
 Waandishiw a habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, JNIA, Injinia Thomas Haule

Airtel Tanzania yaipiga ‘tafu’ Taswa SC

$
0
0
Kampuni ya Airtel Tanzania imeiipiga ‘tafu’ timu ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa SC kwa kuwapatia vifaa vya michezo.

Akizungumza katika makabidhiano hayo jana, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema kuwa kampuni yao inatambua mchango wa waandishi wa habari za michezo nchini katika kuendeleza michezo na kuamua kutoa vifaa vya michezo ambazo ni seti mbili za jezi na mipira.

Mmbando alisema kuwa mbali ya kuwa wadau wakubwa wa michezo, msaada huo ni moja ya muendelezo wao katika shughuli za kijamii.

“Airtel Tanzania ni wadau wakubwa wa michezo na burudani, tumeshiriki katika shughuli mbali mbali ikiwa kuendesha michezo ya Airtel Rising Stars, tumeamua kuunga mkono juhudi za timu ya waandishi wa habari za michezo kuwakutanisha wana-habari na kushiriki katika mazoezi na mechi kwa ajili ya kuhamasisha vipaji na afya zao,” alisema Mmbando.

Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliishukuru Airtel Tanzania kwa msaada huo ambao umetokana na maombi yao kwa kampuni hiyo. Majuto alisema kuwa Taswa SC kwa kujua wadau wake, waliamua kuomba msaada wa vifaa hivyo na Airtel Tanzania kuwajali na kuchukua juhudi za haraka kutoa mchango wao.

“Tumeomba kwa kampuni nyingi, bad hatujapata majibu ya kukubaliwa au la, Airtel Tanzania imeonyesha mfano kwa kutusaidia kwa haraka sana, ni faraja kwetu, tunawaomba wengine waige mfano wao,” alisema Majuto.

Alisema kuwa Taswa SC bado inakabiliwa na changamoto ya vifaa vingine kama viatu kwa timu zake za soka na netiboli na kuwaomba wadau wafikirie kuwasaidia. “ Tupo tayari kupokea vifaa vingine, timu inatakiwa kuwa na vifaa vya kutosha, jezi za aina mbalimbali, mipira ya mazoezi na mechi, hivyo kama kuna wadau wanataka kutusaidia, wasisite kufanya hivyo,” alisisitiza Majuto.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimkabithi vifaa vya michezo moja wa wachezaji wa timu ya Taswa Queens , Imani Makongoro mara baada ya Airtel kuchangia kwa vifaa hivyo kwa timu za mpira wa miguu na netiboli kwa timu za waandishi wa habari nchini. Akishuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimkabithi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary, baada ya Airtel kuchangia kwa vifaa hivyo kwa timu za mpira wa miguu na netiboli kwa timu za waandishi wa habari nchini.

Kleyah aachia video ya Msobe Msobe

$
0
0

Mwanamuziki wa Muziki wa kizazi kipya  Maarufu  kama bongo fleva KLEYAH ambaye anakuja kwa kasi katika Tasnia hiyo  hatimaye amezindua nyimbo yake mpya inayokwenda kwa jina la MZOBE MZOBE wimbo aliomshirikisha msanii maarufu  maarufu kutoka THT Barnaba Boy CLASSIC nyimbo ambayo inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la musiki wa Tanzania.

KLEYAH ambaye ni Mhitimu wa shahada ya mawasiliano kutoka chuo kikuu cha cha Phoenix nchini marekani na baadae kufanya kazi katika shirika la kimataifa la UNDP kabla ya  kuacha na kuamua kurejea nchini kwa ajili ya kuendeleza na kukuza sanaa yake Tayari amefanikiwa kufanya kazi na watayarishaji na wasanii wakubwa ambapo mwaka 2014 alifanikiwa kufanya nyimbo mbili ambazo zilirekodiwa nchini Kenya na mtayarishaji maarufu nchini humo Lucas Bikedo pamoja na kufanyia Video kwa watayarishaji maarufu nchini Kenya kwa sasa OGOPA DJS.

Katika nyimbo yake mpya ambayo ilizinduliwa Tarehe 6 Mwezi November na kuchezwa katika vituo mbalimbali vya Radio nchini Tanzania na Africa mashariki kwa ujumla na hatimaye leo umefanyika uzinduzi wa Video yake ya wimbo wa MSOBE MSOBE unataraji kutambulishwa katika vituo mbalimbali vya Televission kwa ajili ya kumtambulisha msanii huyo ambaye anaonekana kuja kwa kasi katika sanaa hii ya music wa kizazi kipya.

Akizungumza nara Baada ya uzinduzi wa Video yake msanii KLEYAH amesema kuwa kwa sasa mipango yake ni kuendelea kufanya kazi pamoja na watayarishaji wakubwa nchini Tanzania pamoja na wasanii maarufu ili kukamilisha album yake ambayo amepanga kuizindua mwezi July mwaka 2016 album ambayo ametamba kuwa itasheheni aina mbalimbali za misic ili kuwafurahisha mashabiki wanaofwatilia kazi zake.

Ameongeza aliamua kufanya music kwa kuwa ni kitu ambacho kipo ndani ya moyo wake  huku akieleza kuwa kusoma na baadae kufanya music ni jambo la kuigwa na wasanii wa Tanzania kwani itamsaidia msanii kutoboa tu si ndani ya nchi lakini Barani Africa na duniani kwa ujumla 

Pia waweza kumfuata kwenye:
Instagram@kleyahmusic

facebook@kleyahmusic

vevo na utube ni kleyahvevo




Waziri Mkuu Majaliwa azindua ununuzi wa hisa za Benki ya Walimu (MCB) kwenye soko la hisa la Dar es salaam

$
0
0
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akizungumza wakati alipozindua  uuzaji wa hisa za Benki ya Walimu MCB kwenye soko la hisa la Dar es salaam, uliofanyika jijini Dar es salaam leo Novemba 27, 2015
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa akigonga kengelle kuashiria uzinduzi wa ununuzi wa  hisa za Benki ya Walimu- MCB kwenye soko la hisa la Dar es salaam. Uzinduzi huo ulifanyika   jijini Dar es salaam leo Novemba 27, 2015.
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akiteta na baadhi ya Viongozi wa Benki ya Walimu- MCB baada ya kuzindua uuzaji wa hisa za Benki hiyo katika soko la hisa la Dar es salaam.  Uzinduzi huo   uliyofanyika jijini Dar es salaam leo
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akiteta na baadhi ya Viongozi wa Benki ya Walimu- MCB baada ya kuzindua uuzaji wa hisa za Benki hiyo katika soko la hisa la Dar es salaam.  Uzinduzi huo    uliyofanyika jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu,Majaliwa Kassim Majlaiwa akipeana mikono  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile baada ya kuzindua mpango wa Benki ya Walimu MCB -  MCB kuanza kuuza hisa zake kwenye soko la hisa la Dar es salaam Novemba 27, 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dares salaam leo. Picha na OWM

SIMU TV: Ujio wa Teknolojia Ya Mikutano Kwa Njia Ya Video serikalini

KIKAO CHA PILI CHA BARAZA LA BIASHARA KATI YA OMAN NA TANZANIA

$
0
0
 KIKAO CHA JBC KIKIENDELEA KATI YA WAJUMBE WA TANZANIANA OMAN KATIKA MAKAO MAKUU YA OMAN CHAMBER OF COMMERCE KUTOKA KULIA WAPILI NI MWENYEKITI MWENZA-OMANSK SAUD RAWAHI ,WATATU MWENYEKITI MWENZA TANZANIA ND. MAEMBE AKIFUATIA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI OMAN MHESHIMIWA ALI AHMED SALEH

 KIKAO KIKIENDELEA

 PICHA YA PAMOJA BAADA YA KIKAO

 UJUMBE WA TANZANIA PIA ULIPATA FURSA KUSHIRIKI KATIKA MAONESHO MAALUM YA FURSA ZA BIASHARA NCHINI OMAN.

UJUMBE WA TANZANIA UKITEMBELEA ENEO LA VIWANDA NA BANDARI HURU LA SOHAR KILOMITA 200 KUTOKA MUSCAT

Mwanasheria Mkuu wa Serikali alia na mtuhumiwa wa madawa ya kulevya

$
0
0
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju amewasilisha waraka Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam akitaka kushikiliwa na kuzuiwa kwa mali zote za mtuhumiwa wa madawa ya kulevya, aliyejulikana kwa jina la Muharami Abdallah, maarufu kwa jina la Chonji na mkewe, Mwalibora Nyanguri kuhamisha umiliki, kupangisha au kuombea mikopo.

Maombi hayo dhidi ya Muharami na mkewe yaliwasilishwa kwa hati ya dharura mahakamani hapo Septemba 13, mwaka huu mbele ya Jaji Wilfred Dyansobela.
Mwanasheria Mkuu huyo wa Serikali ameiomba Mahakama hiyo imzuie Muharami, mawakala wake au mtu mwingine yeyote kwa niaba yake, kuhamisha umiliki wa mali, kupangisha nyumba au kuombea mikopo (ili serikali ifuatilie uhalali wa upatikanaji wa mali hizo).
Mahakama hiyo imetakiwa kutoa zuio hilo kwa nyumba sita za mtuhumiwa zilizopo maeneo ya Magomeni, Tandale Ziota na Mbezi Juu jijini Dar es Salaam.
Nyumba hizo ni namba 95280 iliyopo Kiwanja Namba 43 Kitalu O, Namba 90292 iliyopo Kiwanja Namba 66 Kitalu P, nyumba iliyopo Kiwanja Namba 68 Kitalu X, nyumba yenye Mita ya Luku Namba 43001304757 na nyumba nyingine yenye Mita ya Luku Namba 04215118664.
Mali nyingine zilizowekewa zuio na kuwa chini ya serikali ni gari aina ya Mitsubishi Canter yenye namba za usajili T 376 BYY, Toyota Verossa yenye namba za usajili T 326 BXF na mali nyingine zote zenye jina au umiliki wa Kampuni ya Mumask Investment ambayo ipo chini ya mtuhumiwa huyo.

Katika maombi hayo, AG amemwomba Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na Ofisa Mtendaji wa Mtaa (husika) wasipitishe uhamishaji wa umiliki wa nyumba hizo na mahakama imwamuru Msajili wa Ardhi kutambua kwamba nyumba hizo zimewekewa pingamizi.

Maombi hayo kwa mara ya kwanza yalitajwa katika mahakama hiyo Novemba 12, mwaka huu ambapo mahakama iliamuru wadaiwa kuwasilisha hati kinzani Novemba 26 (leo) na AG atajibu Desemba 3, mwaka huu na maombi yatasikilizwa Desemba 4, mwaka huu.
Mtuhumiwa anakabiliwa na kesi ya jinai namba 50 ya mwaka 2014 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar ambapo anatuhumiwa kujihusisha na biashara haramu ya kusafirisha madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi 227, 374,500. Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi, Janet Kaluyenda.
Hata hivyo, katika Mahakama ya Kisutu kesi hiyo ilitajwa jana Novemba 25. Mtuhumiwa huyo anapelekwa mahakamani akitokea katika Gereza la Keko jijini Dar.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa akilifungua bunge mjini Dodoma, hivi karibuni, Rais John Pombe Magufuli, alikaririwa akisema amedhamiria kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya ambapo alisema atashughulika zaidi na wauzaji badala ya watumiaji.

INTRODUCING Wanee - Peke Yangu

Airtel Tanzania yapiga ‘tafu’ Taswa SC

$
0
0
Kampuni ya Airtel Tanzania imeipiga ‘tafu’ timu ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa SC kwa kuwapatia vifaa vya michezo. 
 Akizungumza katika makabidhiano hayo jana, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema kuwa kampuni yao inatambua mchango wa waandishi wa habari za michezo nchini katika kuendeleza michezo na kuamua kutoa vifaa vya michezo ambazo ni seti mbili za jezi na mipira. 
 Mmbando alisema kuwa mbali ya kuwa wadau wakubwa wa michezo, msaada huo ni moja ya muendelezo wao katika shughuli za kijamii. “Airtel Tanzania ni wadau wakubwa wa michezo na burudani, tumeshiriki katika shughuli mbali mbali ikiwa kuendesha michezo ya Airtel Rising Stars, tumeamua kuunga mkono juhudi za timu ya waandishi wa habari za michezo kuwakutanisha wana-habari na kushiriki katika mazoezi na mechi kwa ajili ya kuhamasisha vipaji na afya zao,” alisema Mmbando. 
 Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliishukuru Airtel Tanzania kwa msaada huo ambao umetokana na maombi yao kwa kampuni hiyo. Majuto alisema kuwa Taswa SC kwa kujua wadau wake, waliamua kuomba msaada wa vifaa hivyo na Airtel Tanzania kuwajali na kuchukua juhudi za haraka kutoa mchango wao. 
 “Tumeomba kwa kampuni nyingi, bado hatujapata majibu ya kukubaliwa au la, Airtel Tanzania imeonyesha mfano kwa kutusaidia kwa haraka sana, ni faraja kwetu, tunawaomba wengine waige mfano wao,” alisema Majuto. Alisema kuwa Taswa SC bado inakabiliwa na changamoto ya vifaa vingine kama viatu kwa timu zake za soka na netiboli na kuwaomba wadau wafikirie kuwasaidia. 
“ Tupo tayari kupokea vifaa vingine, timu inatakiwa kuwa na vifaa vya kutosha, jezi za aina mbalimbali, mipira ya mazoezi na mechi, hivyo kama kuna wadau wanataka kutusaidia, wasisite kufanya hivyo,” alisisitiza Majuto.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimkabithi vifaa vya michezo moja wa wachezaji wa timu ya Taswa Queens , Imani Makongoro mara baada ya Airtel kuchangia kwa vifaa hivyo kwa timu za mpira wa miguu na netiboli kwa timu za waandishi wa habari nchini. Akishuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary


Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimkabithi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary, baada ya Airtel kuchangia kwa vifaa hivyo kwa timu za mpira wa miguu na netiboli kwa timu za waandishi wa habari nchini

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0
Waziri mkuu Mh.Kassim Majaliwa afanya ziara ya kushitukiza badarini  na kuamuru kufanya kukamatwa kwa kamishina wa kodi pamoja na viongozi wengine 5 kwa kuhusika na upotevu wa kontena 349 katika bandari ya Dar es salaam.https://youtu.be/BBJHMUSpfrM
Baada ya jeshi la polisi kuondoa vituo vyake vya ukaguzi katika barabara kuu ya Mtwara na Lindi baadhi wakazi wa maeneo hayo wahofia kuongezeka kwa matukio ya uhalifu https://youtu.be/sq7eJ_tAaV4
Wizara ya maliasili na utalii yakamata makontena 31 yakiwa na magogo yakitaka kusafirishwa nje ya nchi kinyume cha sheria. https://youtu.be/KkirUUgXTnM
Wanachama wa Chadema mkoani Mwanza wanatarajia kuuaga mwili wa marehemu Alphonce Mawazo siku ya kesho kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Geita;https://youtu.be/D2pnxqwSAs0
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi vigogo wa TRA na kumuagiza mkuu wa jeshi la polisi nchini kuwakamata; https://youtu.be/BoqMdgCGW40
Wafanyabiashara wa dagaa nchini wameiomba serikali kuweka mipango mathubuti ya kuhimarisha soko la ndani na nje ya Tanzania; https://youtu.be/qbRaqXYy1Nc
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi vigogo wa TRA na kumuagiza mkuu wa jeshi la polisi nchini kuwakamata; https://youtu.be/6T_KqRGSWrU
Fuatilia muendelezo wa kisa cha wachimbaji waliokaa chini ya ardhi kwa muda wa siku 41 wilayani Kahama mkoani Shinyanga; https://youtu.be/n4RfnFvIpvk
Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA imekiri uwepo wa changamoto ya ukaguzi wa chakula na dawa bandia nchini; https://youtu.be/ls-JForBWHE
Baadhi ya vifaa vinavyohitajika katika zoezi la uwekaji nyasi bandia uwanja wa Kaitaba Bukoba vyaelezwa kuzuiliwa tena bandarini; https://youtu.be/nHY6EguwFzs
Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza Daniel Sturridge anajiandaa kufanyiwa vipimo vya mguu kwa mara nyingine tena; https://youtu.be/KRcRSExqQnc
Wizara ya maliasili na utalii nchini imekamata kontena 31 zenye magogo katika bandari ya Dare s salaam; https://youtu.be/FS58dBQnTGE
Waziri mkuu Kassimu Majaliwa amewashauri walimu nchini kuchangamkia unununzi wa hisa za benki ya mwalimu; https://youtu.be/MaHhz_2Oe7A
Timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes imeitandika timu ya taifa ya Kenya kwa jumla ya goli 3 kwa 1 katika michuano ya kombe la Challenge inayoendelea nchini Ethiopia. https://youtu.be/Ord2EoWnq_8
Jaji mkuu wa Zanzibar amewataka wawekezaji kuwatumia wanasheria wa ukanda huu wa Afrika mashariki ili kutanua wigo wa ajira; https://youtu.be/xP0isn70ADc
Mamlaka ya maji safi na maji taka DAWASA imebomoa nyumba iliyokuwa ikizuia miundo mbinu ya maji katika eneo la salasala jijini Dar es Salaam;https://youtu.be/DkGQo81MNnk
Serikali imetoa mda wa siku saba kwa kampuni ya huduma za meli nchini  kuhakikisha meli ya MV Butiama inaanza kazi mara moja; https://youtu.be/mqgIfxKMwVk


News Alert: Serikali yakanusha taarifa za upotoshaji zinazomhusu Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

$
0
0
 Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara Fedha Bw. John Cheyo akitoa ufafanuzi  kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu taarifa za upotoshaji zilizoripotiwa na vyombo vya habari hapa nchini kuwa hazina yakauka, taarifa hizo ni za upotoshaji kwani mfumo wa Serikali wa bajeti unaiwezesha Serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na  bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa Serikali ndizo hutumika. Kushoto ni Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw. Immanuel Tutuba na kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya habari Maelezo Bw. Vicent Tiganya.

Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw.Immanuel Tutuba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu namna Serikali inavyokusanya mapato yake na kuyaingiza katika mfuko mkuu wa Serikali  ili yaweze kutumika katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali. Kulia kwake ni Kamishna wa Bajeti  Bw. John Cheyo na kushoto ni msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma.

BREAKING NEWZZZZZ....WAZIRI MKUU MAJALIWA AVAMIA BANDARI LEO, AAMRISHA KUKAMATWA KWA MAAFISA KIBAO WA TRA

$
0
0
WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi maafisa watano na watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-.

Akizungumza na viongozi wa Mamlaka ya Bandari pamoja na viongozi wa TRA katika ziara ya kushtukiza leo mchana (Ijumaa, Novemba 27, 2015), Waziri Mkuu amewataka Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Rished Bade na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Lusekelo Mwaseba wahahakikishe wanashirikiana na polisi kufuatilia upotevu huo na kwamba fedha hizo zinapatikana na zinarudi Serikalini.

Akitangaza uamuzi huo baada ya kufanya kikao na baadhi ya viongozi wa Serikali bandarini hapo, Waziri Mkuu aliwataja maafisa waliosimamishwa kazi kuwa ni Kamishna wa Forodha, Bw. Tiagi Masamaki na Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Wateja, Bw. Habibu Mponezya.

“Hawa wanasimamishwa kazi. IGP ninaagiza hawa watu wakamatwe na kuisaidia polisi. Hati zao za kusafiria zikamatwe na mali zao zikaguliwe kama zinaendana na utumishi wa umma,” alisema Waziri Mkuu.

Maafisa wengine waliosimamishwa kazi ni Mkuu wa kitengo cha TEHAMA, Bw. Haruni Mpande, Bw. Hamisi Ali Omari (hakutaja ni wa idara gani), na Mkuu wa Kitengo cha Bandari Kavu (ICD In-Charge), Bw. Eliachi Mrema. “Hawa wanasimamishwa kazi hadi uchunguzi utakapokamilika na pia wawe mikononi mwa polisi,” alisema.

Pia aliagiza watumishi watatu wa mamlaka hiyo wahamishwe kutoka Dar es Salaam na kupelekwa mikoani. Watumishi hao ni Bw. Anangisye Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert Nyoni.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwagiza Katibu Mkuu wa Hazina, Dk. Servacius Likwelile ambaye alikuwepo kwenye kikao hicho, kuhakikisha kuwa anapeleka wataalamu kutoka Wakala wa Serikali Mtandao (e-Govt) haraka iwezekanavyo ili wakakague mifumo ya taarifa na kubaini jinsi ambavyo wizi huo unafanyika.

“Ninataka uchunguzi uanze kufanyika mara moja, tafuteni njia ambazo zinatumika kama mianya ya wizi kutokea hapa bandarini hadi kwenye ICDs. Nataka hayo makontena yatafutwe hadi yajulikane yako wapi, na fedha hiyo ihakikishwe inarudi serikalini,” alisema.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Bw. Ernest Mangu, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Suleiman Kova, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Bw. Awadh Massawe na viongozi mbalimbali kutoka TRA na TPA.

Mapema akijibu maswali ya Waziri Mkuu, Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Bade alikiri kwamba kuna upotevu wa makontena ambao huwa unafanyika kati ya bandarini na ICDs na hasa ICD ya Ubungo. Akitoa ufafanuzi, alisema kwamba walifanya ukaguzi kwenye ICD moja na kukuta makontena 54 yamepotea kwa njia za wizi. “Hata hivyo, tulipoendelea na ukaguzi, namba iliongezeka na kufikia 327. Tunaendelea kufuatilia kwa kushirikiana na TAKUKURU. Mmiliki wa ICD ametakiwa kulipa faini sh. bilioni 12.6/- na ameshalipa sh. bilioni 2.4/-,” alifafanua.

Alipoulizwa na Waziri Mkuu kama ana majina ya watumishi wanaohusika na wizi huo, Bw. Bade akakiri kwamba anayo lakini siyo kwa wakati huo labda ayapate kutoka kwa wasaidizi wake. Ndipo Waziri Mkuu akamuonyesha orodha ya makontena 349 yenye taarifa zote hadi namba za magari yaliyobeba mizigo hiyo na Bw. Bade akakiri kwamba orodha hiyo ni ya kweli.

“Kwa utaratibu huo hatuwezi kufika, labda baadhi ya watu waondolewe kazini”. Ndipo akaanza kutaja majina ya maafisa hao waliosimamishwa kazi.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na uongozi wa TRA na TPA alipofanya ziara ya kustukiza Bandarini leo asubuhi.
 Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na viongozi wa TRA na TPA
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akikabidhi orodha ya makontena yaliyopotea na ambayo TRA haina taarifa nazo
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa TRA na TPA.

BREAKING NYUZZZZZZ......: RAIS MAGUFULI AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA MKUU WA TRA

$
0
0
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemsimamisha kazi kuanzia leo tarehe 27 Nov. 2015, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndugu Rished Bade kufuatia ziara ya kushtukiza ya Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa Kasimu Majaliwa mapema leo asubuhi Bandarini jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari (hawapo pichani) kuhusu upotevu wa makontena zaidi ya 349 huku akiwa ameshika nyaraka yenye orodha ya makontena hayo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akionesha nyaraka hiyo mbele ya waandishi wa habari waliofika kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakwanza kushoto akifafanua jambo mbele ya wanahabari.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ALIVYOTEMA CHECHE MAMLAKA YA MAPATO (TRA) LEO

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 27/11/2015

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images