Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1038 | 1039 | (Page 1040) | 1041 | 1042 | .... | 3272 | newer

  0 0
 • 11/27/15--21:05: Article 16


 • 0 0

  Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

  KATIKA hali inayoonyesha ni joto kali la kuwatumikia Watanzania, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla, amepiga marufuku likizo za Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara kwenye mkoa wake ili kutekeleza kwa vitendo hotuba na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli.

  RC Makalla aliyasema hayo jana katika kikao cha kazi na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa idara wa halmashauri na Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa huo kwa ajili ya kupeana mikakati ya majukumu ya kuwatumikia Wana Kilimanjaro na Watanzania kwa ujumla, ikiwa ni hatua nzuri ya kwenda na kasi ya Dr Magufuli.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla, akizungumza na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara katika Mkoa huo ili kujipanga katika majukumu mbalimbali ya kuwatumikia wana Kilimanjaro na Watanzania kwa ujumla. Picha na Mpiga Picha Wetu.

  Baadhi ya watendaji wa Mkoa Kilimanjaro wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa huo, Aamos Makalla alipozungumza nao jana. Katika kikao hicho, RC Makalla alipiga marufuku likizo kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara ili kujipanga na maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli.


  0 0

  Rais Magufuli amsimamisha kamishna mkuu wa mapato nchini TRA, Papa Fransis Amfufua Mwl. Nyerere. Pata Dondoo za Magazeti ya leo. https://youtu.be/db6i8O15OLQ

  Star TV

  Kasi Ya Magufuli Yamsomba Bosi TRA, Wamachinga walalamikia Ziara Ya Papa Nchini Uganada,. Pata Dondoo za Magazeti hapa. https://youtu.be/_sBpbbkShXo

  CH 10

  Biashara ya Dawa Maduka Ya Muhimbili Yavurugwa, Magufuli afunga kufuli TRA, UKAWA kumuaga Mawazo kwa saa 5. https://youtu.be/y-_V5gOzsIE

  Azam TV

  5 wampasua Kichwa Pluijm, Simba Yapangua hujuma Nzito, Van Gaal amgwaya Vardy wa Leicester, habarika Na Michezo hapa. https://youtu.be/JLRl4gavgO0

  0 0

  Na. Richard Bagolele- Chato

  Baadhi ya wananchi wilayani Chato wameipongeza serikali kupitia mpango wa TASAF Awamu ya tatu wa kunusuru kaya masikini. Wakiongea kwa nyakati Tofauti wananchi hao kutoka kata ya Bwongera ambao ni wanufaika wa Mpango huo wamesema Mpango wa TASAF Awamu ya tatu ni mkombozi kwa wananchi masikini na wameahidi kutumia pesa hizo kwa manufaa ya familia na mahitaji muhimu ya huduma za afya na elimu kwa watoto wao.

  “Tunaishukukuru serikali yetu kwa huu mpango mzuri ambao matunda yake tunayaona hapa hapa, nimepokea hela mwezi uliopita nimenunua mbuzi watatu, malipo ya awamu hii nitaboresha nyumba yangu” alisema Bibi Tabu Paulo mkazi wa kijiji cha Mkolani kata ya Bwongera.

  Kwa upande mwingine baadhi ya wanufaika wa mpango huo wamelaumu baadhi ya akina baba ambao wamekuwa wakiwalazimisha wenzi wao kutokwenda kuchukua fedha hizo na badala yake wakina baba ndiyo wamekuwa wakitaka kukabidhiwa fedha hizo ambapo ni kinyume na mwongonzo wa mpango wa TASAF awamu ya tatu ambao unawataka wakina mama kama wawakilishi wa kaya wapokee fedha hizo kwa niaba ya familia.

  Mratibu wa TASAF wilayani Chato Bw. Alex Manga’ra amesema tangu kuanza kwa zoezi la ulipaji fedha kupitia mpango huo wamekutana na changamoto hiyo ambapo amesema utaratibu wa nani anapaswa kupokea fedha hizo tayari ulikwishaelezwa kwenye mikutano ya serikali za vijiji na mikutano mikuu ya vijiji vyote vinavyonufaika na mpango huo lakini akina baba wamekuwa wakitaka kulipwa wao badala ya akina mama. Hata hivyo Bw. Manga’ra ameahidi kuendelea kutoa elimu kwa wanufaika wa mpango ili tatizo hilo lisiendelee kujirudia.

  Naye Msimamizi Mshauri wa Mpango kutoka TASAF Bw. Richard Komba ameziomba kaya zinazonufaika na mpango kutokufumbia macho pindi waume zao wanapowakataza kwenda kupokea fedha hizo na kuwataka wawasiliane na wawakilishi wa serikali ya kijiji ambao wamo kwenye mpango ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.

  Mpango wa TASAF Awamu ya tatu ulizinduliwa mwezi January 2014 na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Rodrick Mpongolo na mchakato wa kubaini kaya masikini ulianza mapema mwaka huu ambapo kaya Zaidi ya 8000 kutoka vijiji 71 wilayani hapa ziliibuliwa na kuthibitishwa kupitia mikutano mikuu ya vijiji na Hatimaye kukidhi vigezo vya kaya masikini.
  Bibi Tabu Paulo mkazi wa kijiji cha Mkolani kata ya Bwongera ambaye baada ya kupokea fedha za awamu ya kwanza kupitia mpango wa TASAF III alinunua mbuzi 3 kama njia ya kujikwamua na umasikini.
  Bibi Sesilia Bernado (kulia) mkazi wa kijiji cha Mkolani kata ya Bwongera ambaye baada ya kupokea fedha za awamu ya kwanza kupitia mpango wa TASAF III alinunua mabati 6 ili aboreshe makazi yake.


  0 0

  Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' (kushoto) akimpa mazoezi ya nguvu ya kujenga misul, Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mpambano wake dhidi ya Bondia Twaha Kassimu, utakaofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro Desemba 25, mwaka huu.
  Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akifundishwa jinsi ya kupiga ngumi za mkunjo wa juu 'UpperCut' wakati wa mazoezi ya bondia huyo kujiandaa na mpambano wake dhidi ya Bondia Twaha Kassimu, utakaofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro Desemba 25, mwaka huu.

  0 0
 • 11/28/15--04:26: KUMBUKUMBU

 • 0 0

   Waandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo, wakifurahia kupata fagio walizokabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Zahanati ya Mji Mwema Kigamboni, Dar es Salaam, Omary Kombe (kulia), katika hafla iliyofanyika katika chumba cha habari cha gazeti hilo, Dar es Salaam. Kombe ametoa msaada huo kuunga mkono maelekezo ya Rais Dk. John Magufuli ya kufuta sherehe za Sikukuu ya Uhuru ili wananchi washiriki siku hiyo kufanya usafi wa mazingira kwa lengo la kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu nchini. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA).


  0 0
 • 11/28/15--04:49: Lady Jay Dee In London


 • 0 0

  Meneja Mradi Ruvu chini Mhandisi Emmanuel Makasa (aliyevaa tai) akiongea na waandishi wa habari walipotembelea ujenzi wa bomba la maji kutoka Ruvu Chini kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es salaam.
  Fundi akiendelea na kazi ya kuunganisha na kuchomelea bomba la maji ambalo litasafirisha maji kutoka Ruvu Chini kwenda jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya mitambo ya kusafisha maji ambayo yamesafishwa tayari kwa matumizi ya wananchi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani.


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Kiwanda cha Sukari cha  Mahonda  kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akionesha kitu wakati alipotembelea kiwanda cha Sukari cha Mahonda Wilaya ya Kaskazini B. Unguja leo ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,akiwa katika ziara aliyofuatana na Viongozi mbali mbali wa Serikali
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo wakati alipofuatana Meneja wa  Kiwanda cha Sukari cha  Mahonda Bw.Rajesh Kumar (wa pili kulia) kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati naKampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,(kulia ni ) Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiangalia hatua ya ujenzi na kupata maelezo katika  Kiwanda cha Sukari cha  Mahonda  kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo wakati alipofuatana Meneja wa  Kiwanda cha Sukari cha  Mahonda Bw.Rajesh Kumar (katikati) alipotembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja,(kulia) Meneja mradi Tushar Mehta.
  Picha na IKULU, Zanzibar

  0 0

   Waandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo, wakifurahia kupata fagio walizokabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Zahanati ya Mji Mwema Kigamboni, Dar es Salaam, Omary Kombe (kulia), katika hafla iliyofanyika katika chumba cha habari cha gazeti hilo, Dar es Salaam. 
  Kombe ametoa msaada huo kuunga mkono maelekezo ya Rais Dk. John Magufuli ya kufuta sherehe za Sikukuu ya Uhuru ili wananchi washiriki siku hiyo kufanya usafi wa mazingira kwa lengo la kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu nchini. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)


  0 0


  SIMU.TV:  Elimu imeanza kutolewa kwa shule za msingi Ruvuma ili kuelimisha wanafunzi kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia na watoto;https://youtu.be/GFt6GqN4F0s  
  SIMU.TV:  Wananchi wa Zanzibar wameitupia lawama manispaa kwa kushindwa kurekebisha mfumo wa  maji taka katika maeneo yao; https://youtu.be/NOTW6L1y18k 
  SIMU.TV:  Wanachama wa waongoza watalii Mlima Kilimanjaro wamekataa wito kusitisha mgomo wao wa utoaji huduma za upagazi; https://youtu.be/0_ISuS1WcSY 
  SIMU.TV:  Fuatilia muendelezo wa habari ya kuporomoka kwa kifusi katika mgodi wa dhahabu Mkoani Shinyanga; https://youtu.be/NfpQT-mzCXc
  SIMU.TV:  Serikali imetoa ufafanuzi wa bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2014/2015 pamoja na makusanyo ya fedha kwa robo ya mwaka huu; https://youtu.be/LYIDt-MSITQ
   SIMU.TV:  Mashabiki wa timu ya Kagera Sugar wameeleza matarajio yao juu ya maendeleo ya timu hiyo kufuatia matengenezo ya uwanja wa Kaitaba;https://youtu.be/rqIeGph3fhc

  0 0

  Wapili kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa kijamii wa PSPF Adam Mayingu ,kulia ni Afisa mahusiano wa mfuko huo Bw.Abdul Njaidi akifatiwa na meneja Masoko na Mahusiano wa Radio 5 Bi.Sarah Keiya pamoja na Meneja Biashara wa kituo hicho Bi.Angela Maina
  Kampuni ya Tana Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5  pamoja na mfuko wa kijamii wa PSPF imewafikia wadau wa mfuko huo kwa kuwapa elimu kupitia kipindi cha “Good-Morning Tanzania
  Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo Bw.Adam Mayingu akiongozana na Afisa mahusiano wa mfuko huo Bw.Abdul Njaidi walipokelewa na meneja Masoko na Mahusiano wa Radio 5 Bi.Sarah Keiya pamoja na Meneja Biashara wa kituo hicho Bi.Angela Maina
  Akizungumza katika kipindi hicho kinachorushwa na kituo hicho Bw.Adam alisema kuwa ni wajibu wao kutoa elimu kwa jamii ili iweze kupata fursa ya kufahamu vema mfuko huo pamoja na kufaidika na huduma za afya za PSPF kupitia NHIF
  Kwa upande wake Meneja masoko na mahusiano wa Radio 5 Bi.Sarah alisema uwepo wa mifuko ya kijamii inawezesha wananchi kupanga maisha yao ya sasa na baadae  na ndio maana Radio 5 imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mipango ya mifuko hii inawafikia walengwa
  Bi,Sarah alisema kuwa Mkurugenzi wao Bw.Robert Francis amekuwa akiwezesha idara yao ya masoko na biashara kwa kutoa bei nafuu ya matangazo kwa mifuko hii ya kijamii ili kuwezesha kuwafikia wananchi kwa wingi na urahisi

  0 0

  SERIKALI imewasimamisha kazi watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao jana iliamriwa kwamba watahamishiwa mikoani. 

  Watumishi hao ni Bw. Anangisye Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert Nyoni.

  Uamuzi huo umetolewa leo (Jumamosi, Novemba 28, 2015), na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ili kupisha uchunguzi zaidi wa tuhuma zinazowakabili. Kama ilivyo kwa wenzao sita waliosimamishwa kazi jana (akiwemo aliyekuwa Kamishna Mkuu), nao pia hawaruhusiwi kusafiri kwenda nje ya nchi hadi uchunguzi utakapokamilika.
   “Kazi ya kuwachunguza ilianza jana ileile na sasa, tumeona hawa watu wanapaswa kuwa nje ya utumishi ili kupisha uchunguzi ufanyike kwa uhuru zaidi,” alisema Waziri Mkuu.
  Pia Waziri Mkuu amemuagiza Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dkt. Philip Mpango atekeleze maagizo hayo kwa kuwaandikia barua watumishi hao.

  Jana mchana, Waziri Mkuu alifanya ziara ya kushtukiza kwenye bandari ya Dar es Salaam akiwa na nia ya  kukagua namna shughuli zinavyoendelea kwenye bandari hiyo hasa kwenye maeneo ya kupokelea mizigo kutoka nje ya nchi.
  Katika kikao kilichofanyika bandarini hapo na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Serikali, Waziri Mkuu aliamua kuwasimamisha kazi maafisa watano na TRA kutokana na ‘upotevu’ wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-.
  Waziri Mkuu alisema upotevu huo unasababishwa na mchezo unaofanyika baina ya wafanyabiashara na watumishi wa TRA ambao wanaruhusu makontena kupita bila kulipiwa ushuru na hivyo kuikosesha Serikali mapato.

  0 0

  Na Deo Kakuru, Mbeya

  Ndugu Wasamaria wema na wadau,
  Napenda kutumia fursa hii kukufahamisheni  kuwa hatimaye dada yetu Joyce Mwambepo ametoka nyumbani yupo hospitali ya rufaa Mbeya chini ya uangalizi wa Dr. Mboma akifanyiwa mazoezi ya viungo kabla ya kuelekea hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa vipimo na matibabu. 
   Baada ya michango mbalimbali ambayo wasamaria wema wamekuwa wakichangia toka ndani na nje ya nchi, hatimaye Dada Joyce  na mimi tutasafiri pamoja Alhamisi ijayo kwa ndege ya Fast Jet ili kwenda Muhimbili ambapo tayari mawasiliano kati ya madaktari yamekwishafanyika na atafanyiwa vipimo na upasuaji. 
  Hivyo tunaomba wasamaria wema na wote walioguswa kuendelea kutuunga mkono katika kipindi hiki kwa michango yao ya hali na mali ili kuhakikisha dada yetu anapona maana hana msaada wowote zaidi yetu sisi tunaojitoa kwa kile tulichojaaliwa. 
   Hakika michango yenu haijapotea bure.
  Dada Joyce, ambaye hajainuka kitandani toka alipopata ajali mwezi Aprili mwaka jana, anawashukuru sana sana wasamaria wote waliochanga kwa ajili ya matibabu yake. 
  Anarishukuru pia Group la Whatsapp la WANAHABARI ambao memba wake kadhaa wamechangia na wengine kubeba dhamana ya kuratibu michango na hatimaye matibabu.
  Anasema hana cha kuwalipa ila kusema ASANTE SANA SANA NA anamwombea kwa Mola awazidishie pale walipopungukiwa.
  Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo haikusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya raufaa mkoani Mbeya ambako alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu.
  Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwan Joyce amevunjika miguu yote miwili hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya baada ya kukosa pesa ya kufanyia uchunguzi kwa mashine ya CT Scan na MRI kabla ya kupatiwa matibabu.
  Tutaendelea kuwapa updates za kila hatua kabla na baada ya kuondoka kwenda Muhimbili kwa vipimo na matibabu.

  Dada Joyce Mwambepo  (27) mkazi wa Sinde jijini Mbeya akisubiri chakula kinachoandaliwa na na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 
  Mratibu wa misaada ya Dada Joyce Mwambepo, Deo Kakuru, akiwa nyumbani kwa mgonjwa Sinde jijini Mbeya na mtoto wa dada Joyce mwenye umri  wa miaka 4. 
  Dada Joyce Mwambepo  akiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya alikohamishiwa kwa mazoezi na maandalizi ya safari ya Dar es salaam. Chini ni miguu yake ambayo imevunjika na kupooza kiasi kwamba hawezi kukaa wala kusimama na shida zake zote anamalizia hapo kitandani kwa msaada wa bibi yake na mwanae

  0 0

  Wadau wakubwa wa Globu ya Jamii wanaohudumu katika mgahawa maridadi wa Blue Rock Spur ndani ya Spur Steak Ranches iliyoko IT Plaza katikati ya jiji la Dar es salaam wnawatakia wadau wenzao wote wikiendi njema huku wakikubaribisha kupata steki za uhakika hasa katika msimu huu wa mahafali. Leo walikuwa na sherehe ya mahafali ya mtoto Sellah aliyehitimu Kindergarten School pale Shule ya St. Joseph ambapo walimwandalia keki na kumuimbia nyimbo za pongezi.  Cheki video...

  0 0

   Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa uzinduzi rasmi wa kujiunga kwa Benki ya Walimu katika Soko la Mitaji Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
  Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa amekipongeza chama cha Walimu Tanzania kwa kujiorodhesha katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kupitia benki ya chama hicho kwa ajili ya kuendeleza mtaji wake na kukuza kipato cha wanachama wake.
  Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo alipokuwa akizindua rasmi hatua ya benki hiyo, Mwalimu Commercial Bank (MCB) kujiorodhesha DSE mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam tayari kwa kuanza kuuza hisa zake. 
  “Soko la hisa ni njia mpya ya kuwakwamua walimu kiuchumi na kuzidi kujiendeleza kimaisha,” alisema.
  Alisema serikali ya awamu ya tano imeweka kipaumbele katika kuendeleza elimu, ikiwamo kuboresha maslahi ya watendaji wake na kwamba hatua iliyofikiwa na Chama hicho ni chachu ya kufikia malengo hayo ya maendeleo.
  “Chama kimepiga hatua kubwa ya kuanzisha benki kwa kushirikiana na watalaamu mbalimbali, wanachama kuhamasika kuchagia fedha kwa kununua hisa za benki na hatimae leo kujiunga na soko hili,”alisema Waziri Mkuu.
  Pia aliipongeza Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Masoko na Mitaji kwa kutoa mwongozo hadi benki ya chama hicho kufikia hatua ya kuuza hisa kwa waalimu mwezi March 2015.
  “Mimi ni mwalimu na kwa kweli walimu tupo wengi nchini, majengo ya chama cha walimu yaliyopo mikoani pia yatumike katika kufungua matawi ya benki ili kuwafikia walimu wote na wadau mbalimbali,” alisema Bw. Majaliwa.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Benki ya Walimu, Bw. Herman Kessy alisema mafanikio ya benki yaliyopatikana yanatokana na wanahisa wakiwemo walimu wote wa Tanzania, Mfuko wa Watumishi wa Serikali (PSPF), Mfuko wa Afya ya Jamii (NHIF) pamoja na wanahisa wengine wote wa benki.
  “Tumekusanya mtaji wa Tshs Bilioni 31 na matarajio yalikuwa kupata bilioni 25,” alisema na kufafanua kuwa walikusanya zaidi ya matarajio yaliyokuwepo kupitia wanahisa 235,494.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bw. Yahaya Msulwa alisema maandalizi ya awali ya kuanzisha benki hiyo yamefikia hatua nzuri kwani wamepata leseni kutoka benki kuu ya Tanzania na wanatarajia itafunguliwa rasmi Mwezi Mei 2016.
  “Maandalizi meninge ni pamoja na utengenezaji wa majengo, ununuzi wa mtambo wa kompyuta wa kuendeshea benki (Core Banking System) pamoja na ajira kwa wafanyakazi,” alisema.
  Benki hiyo inatarajiwa kuwa mstari wa mbele katika kutatua matatizo ya walimu na watumishi wa serikali na umma kwa ujumla.

  0 0

  Serikali imeamua kutoa elimu pasipo malipo kwa elimu ya msingi kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne, kuanzia mwaka wa masomo wa 2016 kama ilivyoahidi. 
   Azma hii ya serikali ni katika kutekeleza sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ambayo ina lengo la kuhakikisha kwamba watoto wote wa Tanzania wanapata Elimu bila kikwazo ikiwemo ada au malipo. 
   Katika kutekeleza maamuzi hayo, ada zote zilizokuwa zikilipwa kwa ajili ya elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne zimefutwa.
  Pia, waraka wa Elimu namba 8 wa mwaka 2011 kuhusu michango shuleni nao pia umefutwa.
   Aidha, mwongozo wa elimu ya msingi bila malipo unaandaliwa na utatumwa kwa wamiliki wa shule ifikapo au kabla ya tarehe 15 Disemba 2015. Waraka huu umeanza kutumika tarehe 21 Novemba 2015


  0 0
  0 0

  Mwanamitindo atakaye shiriki kwenye maonesho ya Swahili Fashion Week, Nancy Bondo (kulia) akimvisha shanga ya shingoni mteja wake Francisca Mawala,mara baada ya kuinunua wakati wa maonesho ya ” Pop Up Shop”yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika makazi ya Balozi wa Itali nchini ikiwa ni maandalizi kwa wanamitindo nchini kuelekea Onesho la Swahili Fashion week litakalofanyika Disemba 4-6 2015 na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
  Mwanamitindo atakaye shiriki kwenye maonesho ya Swahili Fashion Week, Anthonia Kilame (kulia) akimuonyesha mmoja wa wateja wake waliofika kwenye maonesho ya ” Pop Up Shop”yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika makazi ya Balozi wa Itali nchini ikiwa ni maandalizi kwa wanamitindo nchini kuelekea Onesho la Swahili Fashion week litakalofanyika Disemba 4-6 2015 chini ya Udhamini wa Vodacom Tanzania.
  Mmoja wa wanamitindo nchini alitakayeshiriki kwenye maonesho ya Swahili Fashion Week, akimuonyesha mmoja wa wateja mwamvuli alioutengenza kwa kitenge aliyefika kwenye maonesho ya ” Pop Up Shop”yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika makazi ya Balozi wa Itali nchini ikiwa ni maandalizi kwa wanamitindo nchini kuelekea Onesho la Swahili Fashion week litakalofanyika Disemba 4-6 na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.


older | 1 | .... | 1038 | 1039 | (Page 1040) | 1041 | 1042 | .... | 3272 | newer