Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1036 | 1037 | (Page 1038) | 1039 | 1040 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

   Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla ametembelea uwanja wa ndege Kilimanjaro(KIA) kujionea ujenzi wa ya upanuzi wa uwanja na shughuli za uwanja wa ndege Katika kikao cha menejimenti ya kampuni ya uendeshaji uwanja KADCO mkuu wa mkoa amewapongeza uongozi kwa kuongeza ndege zinazotua na kuruka, uwezo wakujiendesha kwa kuwa na mapato mazuri na uwezo wa kudhibiti vitendo haramu vya madawa ya kulevya, usafirishaji nyara za serikali na ugaidi Pamoja na pongezi hizo mkuu wa mkoa ameagiza yafuatayo yatekelezwe.
   Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla (pichani juu)akizungumza na menejimenti ya Kadco katika uwanja wa ndege kuhusiana na Uwanja huo  usiwe njia ya wapitishaji madawa ya kulevya kwani kuruhusu hilo tunapoteza nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana.
   Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla akitembelea Uwanja wa Kia na kuwaambia kuwa uwanja huo usiwe njia ya kutorosha nyara za taifa kwani kufanya hivyo ni kupoteza mapato ya taifa na raslimali za taifa.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  TUNAOMBA RADHI KWA HABARI ILIYOTOKA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KWAMBA  MMEA WA ROZELA HAUFAI KWA MATUMIZI YA BINADAMU ILIKUWA SIO SAHIHI
  Sampuli iliyochunguzwa na Mkemia mkuu wa serikali Lab no. 241|2013 kwa jina la Tanzaone Red Jea Juice ndio iliyochunguzwa na kuonekana kuwa haifai kwa matumizi ya binadamu na haina uhusiano wowote na Rozela na matumizi yake.
  Akizungumza na waandishi wa habari Tabibu Mkuu wa Tanzaone  Dk.Marwa aliwaomba radhi wakala wa mkemia mkuu wa Serikali, watanzania wote na serikari kwa usumbufu walioupata kuhusu nukuu potofu ya habari kuhusu mmea wa Rozela kuwa haufai kwa bianamu.
  Hata hivyo amesema Dawa Tanzaone Life Cell Cream kwa matumizi ya uzazi kwa akina  mama na Tanzaone Antviral kwa wongojwa wa HIV zilizo chunguzwa na mkemia mkuu zilionyesha kuwa zinafaa kwa matumizi ya binadamu.

  Imetolewa na Tabibu Mkuu wa Tanzania Herbal 

  0 0


   LOCAL internet shopping faithfuls will next on Friday 27th November 2015 have an extravaganza as online shopping mall, Jumia partners with Ecobank Tanzania to bring home an American model of Black Friday.

  Speaking in Dar es Salaam yesterday, Jumia Tanzania Country Manager, Jean-Philippe Boul and Ecobank ‘s Head of alternative channels, Eric Luyangi said an assortment of goods will be sold at throw away prices on the day.


  Boul said prospective buyers will have to do so using Jumia website or Jumia App where mega discounts of up to 90 percent will be made in different goods but mainly electronic products. 
  “Be ready for unbelievable discounts! On 27th November a unique online flash sale event, Black Friday, will take place on Jumia Tanzania (www.jumia.co.tz), Black Friday, one of the most popular shopping events in the world, is all about deals and bargain hunting during only one day,” Boul said. 
  He said the maiden online shopping frenzy will run between Friday until Monday 30th November as the online shopping mall seeks to attract more local customers. 
  “Originally from the U.S. where it started more than 50 years ago, Black Friday, which takes place after Thanksgiving day, is now a well-known sales day both in the U.S. and Europe. People go mad for it,” Boul noted. 

  Jumia (www.jumia.co.tz) is the first online mall in Africa and is present in 11 countries including Tanzania and offers a wide range of merchandise from clothes, electronics such as phones and television sets. Jumia introduced Black Friday to the African market in 2013 through Nigeria and has since made it become the first and largest online shopping event of its kind on the continent
  Commenting on reasons which have convinced Ecobank Tanzania partner with Jumia, Luyangi said the bank wants its clients to learn the art of buying cheap online so that they can save more.

    
  “With its wide network and a wide range of advanced electronic offering Ecobank is the right partner and this cooperation will go beyond Black Friday, whereby Ecobank customers will be able to purchase merchandise on Jumia website at a special discount of rate,” Luyangi noted. 
  He said Ecobank’s mission is to bring services closer to all of its customers on the continent where it is present in 36 countries. Ecobank Tanzania is a subsidiary of Transnational Incorporated (ETI), a multinational bank headquartered in Lome, Togo. The banking giant has 1,200 branches on the continent. 
  Last year's Black Friday sales primarily focused on consumer electronics, with particular interest in digital products such as flat screen TVs, smartphone sand tablets. This year, Jumia predicts that it will also sell fashion and cosmetics too, with great deals falling by as low as 50 percent off. 
  Black Friday will also be a great occasion for Jumia Tanzania to launch InnJoo phones and tablet. InnJoo has already experienced massive success in the other Jumia markets and is now entering the local market for the first time.

   
  “By tapping into this global shopping phenomenon, with the support of our partner Ecobank Tanzania, we have created a powerful event that our customers will love.” concluded Jumia Tanzania Country Manager, Boul


  0 0

  As the worlds youngest film maker, Zuriel Oduwole has already etched her place in history in the movie making industry and she is learning a thing or two about documentary film making. 
  Last year at age 12, she wrapped up filming and production of her 5th documentary [but the first made for the big screen], which premiered in Lagos at the Civic Center. It debuted in the Film House Cinema, and the Genesis Deluxe Cinema in Lekki, making her the youngest person to ever show their self produced and edited film in commercial cinemas.
  The documentary film titled "A Promising Africa" went on to screen and show first in London [UK] in December 2014, and then in Accra [Ghana], Pretoria [South Africa] and Tokyo [Japan] in 2015.
  Her goal is to tell Africas successful stories first on the small screen, and now on the big screen, in addition to showing herself as an example of what an educated Girl can do.
  Having directed a TV commercial for GAP in Los Angeles earlier in July and made a Girl Confidence documentary for P&G in August, she is now hoping to tell perhaps one of her biggest stories yet - about the life and times of the worlds biggest music artise and entertainer - Michael Jackson.

  She met one of his famous and probably more successful brothers - Jermaine Jackson in Los Angeles, and that sparked her interest in making this next movie project, telling the incredible story of the man known as the King of Pop or perhaps also, the first person to Moon-walk.

  "I have known about him since I was 3, learned a few of his dance moves since I was 4. But really, who in the world today has no heard about Michael Jackson before or seen his picture, or tried to dance like him", asks Zuriel in her usual voice of inocence. It would be really cool to work on his story, in the future.
  While there are many splinter Jackson family projects out there, there is none as intrigung though, or that would pit the growing movie documentary making skills of a 13 year old, with the larger than life image of perhaps the greatest entertainer this century, the 'Man In The Mirror' himself.

  0 0

  Mwalimu Kulthum R. Mussa (Mwambambale) wa Nyakato National Mwanza anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mumewe Dr. Hassan Marekero Mdee (pichani) kilichotokea katika Hospitali ya Bugando Mwanza tarehe 22.11.2015. 
  Msiba upo nyumbani kwake Nyakato National Mahina karibu na kanisa la Roma.  Heshima za mwisho zimetolewa siku ya Jumanne nyumbani kwa Marehemu Mahina. Marehemu atasafirishwa leo Jumatano alifajiri kuelekea Moshi Uchira kwa mazishi ambayo yatafanyika siku ya Alhamisi. 
  “Innalilahi Wainnailahi Rajiun”


  0 0

  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepatiwa msaada wa vifaa kumi  vya tiba vya kuwahudumia watoto  mara wapougua na kufikishwa kwenye hospitali hiyo.

  Vifaa hivyo vina thamani ya Dola za Kimarekani Laki moja sawa na zaidi Sh milioni 2 vimetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF),kwa lengo la kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

  Baadhi ya vifaa vilivyotolewa  ni Ventilator, medical, adult –child ,w/access pamoja na Warmer system , newborn, radiant, w/access.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo  Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Dk Jama Gulaid amesema mchango wa UNICEF na michango ya wadau wengine itawezesha watumishi wa hospitali ya Muhimbili kuokoa maisha ya  watoto  ambao wanahitaji huduma za afya.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando  amesema  hadi kufikia mwaka 2013  Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vya watoto hao kwa theluthi mbili.

  Kwa mujibu wa Dk Mmbando, mwaka 2013 Tanzania imepunguza vifo hivyo na kufikia 54 kwa vizazi hai 1,000  na kufikia lengo la Milenia  na kwamba  mafanikio hayo yametokana na kiwango kikubwa cha chanjo , matumizi sahihi  ya dawa za Malaria pamoja na vyandarua.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru amewashukuru UNICEF kwa msaada huo ambao utachangia kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha ya watoto na kuboresha huduma za afya.

  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  1.JE  KITU  GANI  KIFANYKE  ASKARI  ANAPOKUNYIMA  DHAMANA.

  Kwanza  ieleweke  kuwa  dhamana  ni  haki  yako. Haki  ni  jambo  la  lazima.  Haki  ya  dhamana  inaruhusiwa  kunyimwa  katika  makosa  machache  sana kwa  mfano  uhaini, wizi  wa  silaha,  mauaji n.k.  Makosa  mengine  madogo madogo hasa  haya  ya kila  siku  ya  kutukana,  kudhalilisha, kupigana,  ajali ndogo, wizi  usio  wa  silaha, na  mengine   dhamana  ni  lazima.  Hata  hivyo  makosa ambayo  hayaruhusiuwi  kwa  dhamana   ni  lazima  askari  anapokunyima  dhamana  aandike  sababu  za  kukunyima  dhamana.  

  Na  hapohapo  yatakiwa  ahakikishe  anakufikisha  mahakamani  haraka  sana  iwezekanavyo  hasa  ndani  ya  saa  24  ili  mahakama  ikatizame  shauri  lako   na  haki  unazostahili.  Ni makosa  makubwa  askari  kumnyima  raia  dhamana   pale  anapostahili  na  ni  makosa  makubwa  askari  kutomfikisha  mtuhumiwa  mahakamani  haraka  bila  sababu  za  msingi.  Unayo  haki  ya  kumtaka  askari   akufikishe  mbele  ya  hakimu/jaji   haraka  ili  ukaombe  dhamana  huko na  haki  zako  nyingine.  Katika  hili hautaomba  ila   utamtaka  askari kufanya  hivyo. 

  2. JE  DHAMANA  NI  LAZIMA  UWEKE(DEPOSIT) YA KIASI  CHA  FEDHA.

  Hapana  dhamana   si  lazima  uache  pesa. Unaweza  ukapewa  dhamana  kwa  ahadi  ya  maandishi  tu.  Ahadi  ya  maandishi   ni  masharti  ambayo  utayasaini   na  kuahidi  kuyatekeleza  utapokuwa  umeachiwa  kwa  dhamana.  Moja  ya  masharti  hayo   ni  kuahidi  kufika  tena  kituo  cha  polisi  au  mahakamani  katika  muda  utakaopangwa.  Dhamana ya  kuweka  kiasi  cha  fedha  huwa inaamriwa   iwapo  kuna  makosa  makubwa  yaliyotendeka.  Hata  hivyo  fedha  hizo  hutakiwa  kurudishwa  ama  baada  ya  upelelezi  kukamilika  na  kuonekana  mtuhumiwa  hana  kosa au  baada  ya  kuwa  huru  kutokana  na  amri  ya  mahakama.   0 0


  0 0
  0 0


  0 0

  Katika kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka huu, GAPCO, kampuni inayoongoza kwa uuzaji wa mafuta, imeamua kuwapa wateja wake zawadi ya kufungia mwaka. Katika kufanikisha hilo, kupitia mpango wake wa ‘GAPCO Safari Loyalty programme ‘, kampuni imelenga kunufaisha na kuimarisha uhusiano wa kudumu na wateja wake kwa kuwapa mafuta ya bure.
  Mpango huu unaoenda sambamba na promosheni ya ‘Jaza Mafuta na Ushinde’, umedhamiria kutoa lita 4,000 za petroli au dizeli za bure kwa wateja 100 watakao bahatika ndani ya wiki nne. Katika droo za kila wiki, kutakuwa na wateja 25 wanaoweza kujishindia lita 40 kila mmoja. Wateja wanaweza kujiongezea nafasi za ushindi kwa kujaza mafuta mara nyingi zaidi.
  Pia, wateja ambao hawajajiunga na mpango wa ‘GAPCO Safari Loyalty programme’ wanaweza kujiunga katika kituo chochote cha GAPCO kilichopo Dar es Salaam ili waweze kushiriki katika promosheni. Motisha zinazotolewa kupitia mpango huu, ni nje ya zawadi atakazoshida mteja katika promosheni, mteja wa GAPCO atajikusanyia pointi zitakazomwezesha kukomboa mafuta ya bure.
  “Kupitia mpango huu wa ‘GAPCO Safari Loyalty programme‘, tunataka wateja wetu wawe na furaha na waendelee kutumia bidhaa na huduma zetu. Mbali na kwamba tunatoa kadi hizi kwa mteja mmoja mmoja, pia tunaanzisha kadi kwa ajili ya makampuni na wasafirishaji. Kupitia kadi hizi, mbali na wateja kuweza kujikusanyia pointi zitakazomwezesha kupata mafuta ya bure, wateja wetu wataweza kudhibiti matumizi ya fedha zao,” alisema Meneja Masoko wa GAPCO, Caroline Kakwezi.

  Mwanzoni mwa mwaka huu, GAPCO ilifanya mabadiliko makubwa na kuamua kujikita katika kujipambanua kwa namna ya kipekee. Katika mabadiliko haya, GAPCO iliboresha muonekano na mazingira katika vituo vyake vya mafuta vilivyopo Dar es Salaam. Ahadi ya kuwa na mafuta yenye ubora na ujazo wakuaminika, mazingira mazuri na rafiki, huduma bora inayojali mteja na ya haraka ni kati ya faida mahsusi anazopata mteja anayefika katika vituo vya mafuta vya GAPCO nchini.

  “Tukiwa na mtazamo na nia ya kuwapa wateja wetu maili nyingi zaidi na tabasamu zaidi, malengo yetu ya muda mrefu ni kuweza kupanua huduma zetu na kuhakikisha tunatoa huduma za ziada ili kuwaachia wateja wetu kumbukumbu sahihi ya huduma bora na za kisasa,” aliongeza Kakwezi.
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (kushoto) akizungumza na wanahabari wakati wa kutangaza mpango wake wa ‘GAPCO Safari Loyalty ‘, unaolenga kuwanufaisha wateja wake kwa kuwapa mafuta ya bure, ulizindulia kwenye makao makuu ya Kampuni hiyo, Kurasini jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja wa Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO, Jane Mwita.
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (kushoto) na Meneja wa Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO, Jane Mwita, wakionyesha vipeperushi vya Promosheni hiyo, mara baada ya kuizindua rasmi.

  0 0

  Na Francis Godwin
  Unajua nini mtu wangu una kila sababu ya kujivunia kuwa Tanzania wakati na muda kama huu kwani kasi ya Rais wetu Dk. John Pombe Joseph Magufuli inaweka headlines kubwa sana kwa nchi za jirani na si kwa Watanzania pekee!
  Nimetembelea mtandao wa kijamii wa Twitter na nimekutana na tweets za Wakenya juu ya Rais Dk. John Pombe Magufuli na kwenye kuzisoma tweets zao nimegundua sifa za Rais Magufuli na maamuzi yake ya kazi tu toka ameshika rungu la Tanzania zimewafikia.
  Wengi wamemsifia na wengine wameandika wakiomba Mungu awape Rais kama Magufuli….. 
  MAGU

  Kwa kipindi kifupi alichoingia madarakani, Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli amefanya mambo kadhaa ambayo yamewaridhisha na kuwapa moyo Watanzania, mambo hayo ni kama…
  1. Ziara yake ya kushtukiza kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili  ilivumbua vitu vingi na kumpelekea Rais Magufuli kufuta bodi ya Wakurugenzi wa hospitali hiyo pamoja na kumuondoa Kaimu Mkurugenzi wake, Dk. Hussein Kidanto.
  2. Kufuta safari za viongozi kwenda nchi za nje ili kupunguza matumizi makubwa ya pesa za Serikali.
  3. Alielekeza shilingi milion 225 zilizochangwa kwa ajili ya kugharamia hafla ya Pongezi za Wabunge Dodoma kutumika kununua vitanda vya hospitali na shilingi milion 15 tu ndio zitumike kwaajili ya sherehe hiyo.
  4. Jumatatu ya tarehe 23 November 2015, Rais Dk. John Magufuli alitangaza kufuta kwa sikukuu ya Uhuru December 9 na kuagiza fedha za maandalizi ya sikukuu hiyo zitumike kutatua matatizo mengine pia ameagiza siku hiyo itumike kusafisha mazingira ili kupunguza matatizo ya kipindupindu nchini.
  Mambo haya machache na makubwa yamewapa faraja kubwa sana Watanzania na kumfanya Rais Magufuli awe topic kubwa kwenye mtandao wa Twitter kwa raia wa Kenya!
  Kama kawaida kazi yangu ni kuzinasa zile zote zinazoweka headlines wakati huu na hizi ni baadhi ya#tweets nilizofanikiwa kuzinasa, karibu uzipitie moja baada ya nyingine uone jinsi gani Wakenyawalivyoguswa…

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Uongozi wa Mtandao wa Wanawake Tanzania (WFT) wakati viongozi hao walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Nov 24, 2015 kwa mazungumzo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea baadhi ya Vipeperushi na Vitabu vya Mtandano wa Wanawake Tanzania (WFT) kutoka kwa mwenyekiti wa mtandao huo, Prof.Ruth Meena, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dares Salaam, leo Nov 24, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mtandao wa Wanawake Tanzania (WFT) baada ya mazungumzo yao yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dares Salaam, leo Nov 24, 2015. 
  Picha na OMR

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  OFISI YA MAKAMU WA RAIS.

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na uongozi wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania (WFT) ambapo amezungumzia dhamira ya serikali katika kuyatafutia ufumbuzi matatizo mbali mbali yanayowakabili wanawake na watoto wa kike nchini.

  Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais aliueleza ujumbe huo kuwa wakati wa kampeni aliahidi pamoja na kazi za kumsaidia Mhe. Rais bado kama mama atafuatilia kwa karibu utekelezaji wa ahadi ya kupatikana kwa maji safi na salama, kuboresha afya ya mama na mtoto, elimu na mazingira.
  “Nilipokuwa kwenye kampeni nimejionea shida ya maji na wanawake ndiyo wanaopata tabu ya kutembea mwendo mrefu kutafuta maji. Kwa hiyo, pamoja na kazi zangu za kumsaidia Mhe. Rais nitasimamia miradi yote ya maji, alau tuhakikishe maji yanapatikana umbali wa mita 400 kutoka eneo wananchi wanakoishi au karibu zaidi”.
  Alisema kinachofurahisha zaidi suala la maji liko kwenye Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na miradi mingi ikiwemo ya kuchimba visima virefu katika mikoa kama vile ya Singida na Dodoma iko kwenye mchakato na cha msingi ni kusimamia fedha zinatumika kuleta maji kama ilivyokusudiwa.
  Kuhusu afya ya mama na mtoto alisema kazi hiyo ataianza hivi karibuni kwa kushirikiana na Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea haki za wanawake ili kupunguza vifo vinavyosababishwa na mimba za utotoni.
  “Hili tutajitahidi kulipunguza kwa kiasi kikubwa na hasa baada ya serikali ya Awamu ya Nne kusema kwamba shule ya msingi ya lazima ni kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne”, alisema na kuongeza.
  “Katika kipindi hicho binti atakuwa amefikisha miaka 17, atakuwa tayari kukabiliana na mambo ya uzazi tofauti na ilivyo sasa ambapo anamaliza darasa la akiwa mdogo na matokeo yake anapata mimba katika umri mdogo. Mtusaidie kupiga debe huko nje utekelezaji uweze kufanikiwa.”
  Hata hivyo, alisisitiza kusimamia suala la kuhakikisha zahanati, vituo vya afya na hospitali nchini zinakuwa na dawa na vifaa tiba vya kutosha katika wodi za wazazi kwa ajili ya kuhudumia akina mama na wananchi kwa ujumla ambao wengi wanaonekana ni watiifu kwa serikali yao.
  Kwa upande wa elimu Mhe. Samia alisema atasimamia ujenzi wa mabweni kwa watoto wa kike na kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwa sababu uharibifu wa mazingira ndiyo umekuwa chanzo cha upungufu wa maji nchini.
  Aidha aliuambia ujumbe huo kuwa hivi sasa tuna mpango wa kuimarisha utendaji serikalini kuanzia serikali kuu hadi serikali za mitaa ili kinachopatikana kidogo kimfikie kila mwananchi.
  “Tutaendelea kuaihirisha sherehe ili fedha hizo ziweze kutumika kwa mambo ya kijamii. Kwa msimamo huu amabao Mhe. Rais ameanza nao labda watu wote tushirikiane kwa kutatua matatizo yetu kwa gharama nafuuna  kwa ufanisi mkubwa.”
  Mapema akizungumza kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa Mtandao huo Prof Ruth Meena alimpongeza Mhe. Samia kwa kushika nafasi ya juu ya uongozi akiwa mwanamke wa kwanza kuweka historia katika Tanzania.
  Alimweleza Mhe. Makamu wa Rais matarajio yao kwa serikali ya Awamu ya Tano kuwa itatetea misingi ya haki na usawa katika Nyanja zote.
  Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
  Dar es salaam

  0 0

  Tasnia ya michezo hususani kandanda  imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na mwanamichezo mkongwe Majid Adam Issa Maki (pichani) aliyefariki alfajiri ya leo. Msiba upo nyumbani kwa marehemu Yombo, Dar es salaam na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo saa kumi katika makaburi ya Kisutu.
  Marehemu, ambaye ni mtoto wa Mwalimu Adam Issa Maki,  atakumbukwa kama mmoja wa wachezaji mahiri wa klabu ya Sunderland (Simba) na pia mmoja wa waanzilishi wa klabu ya Red star ambako alikuwa team manager.

  Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un
  Marehemu Majid (wa pili kushoto waliochuchumaa) akiwa na kikosi cha Simba enzi hizo.

  0 0

  Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) imeingia kambini jana jioni katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam, kujiandaa na ziara ya mafunzo katika ukanda wa Afrika Mashariki itakayoanza Disemba Mosi mwaka huu.

  Kocha wa timu hiyo Sebastian Mkomwa amesema vijana wote wameshawasili jijini Dar es salaam na leo wameanza mazoezi asubuhi katika uwanja wa Karume watakapokua wanajifua kila asubuhi na jioni mpaka siku ya safari.

  Kikosi cha wachezaji 24 kimeingia kambini kujifua na ziara ya Afrika Mashariki, ambapo timu hiyo inaandaliwa kwa ajili ya kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, zitakazofanyika mwaka 2017 nchini Madagascar.

  Timu ya Taifa ya vijana imeakua na program ya kukutana kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya kufanya mazoezi na kucheza michezo ya kirafiki na timu za kombani za U15 katika mikoa mbalimbali nchini, ambapo kwe mwezi Disemba itakua pamoja kwa wiki tatu katika nchi za Afrika Mashariki ikicheza michezo ya kirafiki.

  Disemba Mosi, U-15 itasasiri kuelekea jijini Mwanza ambapo itacheza mchezo mmoja wa kirafiki na kombani ya jijini Mwanza (U17), kasha kusafiri kueleka mkoani Kigoma itakapocheza michezo miwili dhidi ya kombaini ya mkoa wa Kigoma (U17) na timu ya Taifa ya Burundi (U17).

  Ziara hiyo itaendelea katika jiji la Kigali kwa kucheza michezo miwili dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda (U17), Jinja dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda (U17), Nairobi dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya (U17) na kumalizia kwa mchezo dhidi ya kombaini ya mkoa wa Arusha (U17) na kurudi jijini Dar es salaam.

  0 0  0 0

  Na Jovina Bujulu-Maelezo

  Serikali imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amekomba fedha hazina na kuiacha Serikali bila fungu lolote.

  Hayo yamesemwa jijini dare es salaam na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha Bwa. John Cheyo huku akiwataka wananchi kupuuza habari hiyo kwani hazina ukweli wowote.

  “Hazina inazo pesa za kutosha  na tunajivunia kufanya uchaguzi wa mwaka huu,  kununua mashine za BVR  kwa kutumia pesa za watanzania bila kutegemea msaada wowote kutoka nje ya nchi  na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka huu” alisema Bwa. Cheyo.

  Pia aliongeza kuwa serikali imeendelea kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa bomba la gesi ambalo limekamilika hivi karibuni, vinu vya kuchakata gesi na ujenzi wa barabara nchini.

  Aliendelea kusema kwamba mfumo wa serikali wa bajeti unaiwezesha serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa serikali ndizo hutumika.

  Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa kipindi cha 2015-2016 ni shilingi Trilioni 22.5 na bajeti hiyo inatengenezewa mpango wa makusanyo na matumizi kwa kulipia mishahara ya wafanyakazi na miradi mbalimbali iliyoidhinishwa.

  Pia katika matumizi mengine bajeti hiyo inalipia chakula cha wanafunzi, mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, ununuzi wa dawa na vifaa tiba na chakula cha hifadhi ya taifa.

  0 0

  Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila akifunga Mafunzo ya siku mbili ya Waandishi wa Habari za Mahakama yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
  Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila akitoa ufafanuzi kuhusu Kichwa cha Habari ya Mahakamani kilichoandikwa bila kuzingatia Weledi na moja ya Gazeti la Kila siku wakati wa mafunzo ya siku mbili ya Waandishi wa Habari za Mahakama yaliyofanyika jijini Dar es salaam. Picha/Aron Msigwa –MAELEZO.

  Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

  Mahakama ya Tanzania imesema kuwa itendelea kufanya kazi na vyombo vya Habari nchini katika kuuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa jukumu la Kikatiba ililonalo la kutafsiri sheria mbalimbali na kuzitolea maamuzi ili kuwawezesha wananchi kujua na kupata Haki zao kwa wakati.

  Akifunga Mafunzo ya siku 2 ya waandishi wa Habari za Mahakama jana jijini Dar es salaam Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila aliwataka waandishi hao kutimiza wajibu wao wa kuueleza umma taarifa sahihi za mashauri mbalimbali yanayotokea mahakamani kwa kuzingatia sheria.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   
    Jengo la ujenzi wa kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
    Sehemu ya jengo la ujenzi wa kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma
    Sehemu ya jengo la ujenzi wa kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa NHIF, Michael Mhando akizungumza wakati wa makabidhiano ya  kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
   Mkurugenzi mtendaji kampuni ya ujenzi Tanzania Building Works Ltd, Mohamed Iqbal Moray(kushoto), akimkabidhi funguo za  kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa NHIF Michael Mhando.
   Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na uwezeshaji wa mfuko wa NHIF, Deusdedit Rutazaa akizungumza wakati wa makabidhiano ya kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma
  Wafanyakazi wa mfuko wa NHIF na wa Hospitali ya rufaa ya Dodoma wakishiriki makabidhiano ya kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

  MFUKO wa Taifa wa Bima ya afya(NHIF) umekamilisha ujenzi wa kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambacho kitasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali hiyo.

  Akizungumza katika makabidhiano ya jengo hilo, Kaimu Mkurugenzi wa NHIF,  Michael Mhando, alisema kituo hicho kitakuwa cha kisasa na kitatoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za CT-Scan na kitafunguliwa kabla ya mwezi januari mwakani ili

  “NHIF umelipatia ufumbuzi tatizo la msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kukamilisha ujenzi wa jengo hili ambalo limegharimu kiasi cha sh. Bilioni sita ikiwa ni pamoja na vifaa vya matibabu na samani,”alisema Mkurugenzi huyo.

  Alisema ujenzi wa huo umeanza tangu mwaka 2008 na litakuwa na uwezo wa kuchukua vitanda 34 vya
  wagonjwa.

  “Kituo hichi kitakuwa na vyumba vya madaktari, maabara,  upasuaji, chumba cha kutolea dawa, mapokezi,  chumba cha wagonjwa mahututi, chumba cha dharura, mfumo wa miito ya wauguzi, na vifaa tiba vya kisasa,”alisema Mhando


  Alisema kitatoa huduma kwa wanachama wa mfuko huo, wananchi wa Mkoa wa Dodoma na mikoa jirani.older | 1 | .... | 1036 | 1037 | (Page 1038) | 1039 | 1040 | .... | 3272 | newer