Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1035 | 1036 | (Page 1037) | 1038 | 1039 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Mheshimiwa Spika;

  Niko hapa leo kutimiza matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 91 Ibara ndogo ya kwanza inayonitaka kulihutubia na kulifungua rasmi Bunge hili. 
  Naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima na afya njema, na kutuwezesha kuwepo hapa siku ya leo. 
  Aidha nitumie fursa hii kuwakumbuka wenzetu ambao, kwa namna na nafasi mbalimbali, walishiriki katika mchakato wa uchaguzi huu na kwa bahati mbaya walipoteza maisha yao kabla ya mchakato haujakamilika. 
  Kwa hao wote waliotangulia mbele za haki ninamuomba Mwenyezi Mungu azirehemu roho zao na awape pumziko la amani.
   Nitumie nafasi hii kuwapa pole ndugu na jamaa ambao ndugu zao walifariki na wengine kupata ulemavu wakati wa mchakato wa uchaguzi huu. Kusoma hotuba kamili BOFYA HAPA


  0 0

  Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Prof. Adolf Mkenda akihutubia wadau mbalimbali wa takwimu katika maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya "Takwimu Bora kwa Maisha Bora".
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya utangulizi katika katika maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya "Takwimu Bora kwa Maisha Bora".
  Baadhi ya wadau mbalimbali wa takwimu wakifuatilia kwa makini matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya "Takwimu Bora kwa Maisha Bora".


  0 0

  Na Mwandishi Maalum, Washington 

  Wakati vikao vya siri vya kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa visiwani Zanzibar vikiwa vimeripotiwa, juhudi za kuupatia ufumbuzi mzozo huo zimehamia kutoka Ikulu ya Zanzibar na kufika Ikulu ya Marekani (White House).
  Wanachama wa ZADIA kutoka majimbo tafauti Nchini Marekani wakionyesha mabango yao.

  Mnamo tarehe 21 mwezi huu, Wazanzibari waishio nchini Marekani waliandamana hadi kwenye Ikulu ya nchi hiyo katika juhudi za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa ili kuupatia suluhisho mzozo huo.

  Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya Ikulu hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) iliyoandaa maandamano hayo Bwana Omar Haji Ali, alisema kuwa maandamano hayo yanakuja katika juhudi za Jumuiya hiyo za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa katika kuukwamua mgando wa kisisas visiwani Zanzibar. 

  Aliendelea kusema kwamba maandamno hayo pia yana lengo la kumkumbusha rais Barack Obama wa Marekani kutekeleza ahadi yake ya kuilinda demokrasia Barani Afrika.

  "Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mapema mwaka huu, rais Obama alisema '.. pale ambapo raia hawawezi kutekeleza haki zao, basi ulimwengu una jukumu la kukemea. Na Marekani itafanya hivyo, hata kama wakati mwengine itakuwa inauma'..", alikumbusha Bwana Ali.

  Aliongeza kuwa "Wananchi wa Zanzibar wameshindwa kutekeleza haki yao kwa zaidi ya nusu karne sasa. Wakati umefika sasa kwa ulimwengu kuchukua jukumu lake. Wakati umefika sasa kwa Marekani siyo tu kukemea, lakini pia kuchukua hatua za kivitendo ili kuhakikisha kuwa sauti za Wazanzibari zinasikilizwa na kuheshimiwa"

  Alipoulizwa ni hatua gani watakazochukuwa iwapo Serikali ya Marekani haikuchukua hatua yoyote kusaidia kumaliza mgando wa kisiasa Zanzibar, Bwana Ali alisema "Tuna imani na rais Obama, na tumemfikishia barua ya malalamiko yetu, na tunasubiri jibu lake, na imani yetu ni kuwa atachukua hatua madhubuti khususan ikizingatiwa kuwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulikuwa wa mwanzo kutoa taarifa kuelezea kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa wa haki na huru" Alidokeza kuwa, iwapo hali itaendelea kubakia kama ilivyo, basi ZADIA itaelekea kwnye Umoja wa Mataifa.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) Bwana Omar Haji, akiongea na moja waandishi wa habari. 

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0


  Baada ya uteuzi wa waziri Mkuu Kassim Majaliwa,fumbo la baraza la mawaziri laendelea kutesa vichwa vya watu wengi huku Wananchi katika maeneo mbalimbali nchini wakitoa maoni yao. https://youtu.be/lu0uKdIO00s

  Wachambuzi mbalimbali nchini waendelea kutoa mitazamo na maoni yao juu ya baraza jipya la mawaziri la serikali ya awamu ya tano. https://youtu.be/BlpbU4iOQTc

  Serikali ya Ujerumani yaipatia Tanzania msaada wa ndege mbili maalum kwa ajili ya kufanya doria katika mbuga mbalimbali ili kusaidia juhudi za kudhibiti ujangili. https://youtu.be/zZ_3w3Gn7lA

  Wananchi mkoani Kagera wajitokeza kusindikiza mwili wa aliyekuwa mtangazaji na mwandaaji wa vipindi Prince Baina Kamukulu. https://youtu.be/WC3TUyzNuPE

  BOFYA HAPA KUONA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Hatimaye albam ya “Sura Surambi” iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa taarab, inazinduliwa Alhamisi hii Novemba 26.

  Albam hiyo kutoka kwao Mashauzi Classic, itazinduliwa ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni huku kundi kongwe la taarab East African Melody, likizindikiza tukio hilo kubwa.

  Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Mashauzi ameuambia mtandao huu kuwa albam ya “Sura Surambi” inaundwa na nyimbo sita kali.

  Ni Alhamisi ya kihistoria ambayo Isha anaitaja kuwa itapambwa na ratiba iliyokwenda shule itakayomwacha mshabiki apate uhondo mwanzo mwisho.

  Isha amezitaja nyimbo hizo kuwa ni pamoja na “Sura Surambi” aliouimba yeye, “Kupendwa Bahati Yangu” uimbaji wake Abdumalick Shaaban, na “Mjinga Mpe Cheo” wa Zubeida Malick.

  Nyimbo nyingine alizozitaja Isha ni “Pendo la Ukakasi” wa Saida Ramadhan, “Ubaya Haulipizwi” ulioimbwa na Asia Mzinga na “Mapenzi Yamenivuruga” mwimbaji akiwa ni Naima Mohamed.

  Nyimbo zote hizo sita zimetungwa na Isha Mashauzi.

  Mbali na Melody, mkali wa tungo za mapenzi wa muziki wa kizazi kipya Cassim Mganga naye pia atasindikiza uzinduzi huo wa “Sura Surambi” ndani ya Mango Garden Alhamisi hii.

  0 0

   Ofisa Mwandamizi Idara ya Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Mshangama akiwaonyesha fomu ya kujiunga na uanchama wa hiari na fao la matibabu baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na NSSF wakati wa tamasha la wa kusoma vitabu wanafunzi wa shule za msingi, lililofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na NSSF. 
  Ofisa Mwandamizi Idara ya Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Mshangama (kushoto) akifafanua jambo kwa wanachama wapya waliojiunga uanchama wa hiari na fao la matibabu wakati wa tamasha la kusoma vitabu wanafunzi wa Shule za Msingi lililofanyika jijini Dar es Salaam kudhaminiwa na NSSF.
   Watoto Brianna Michalis Kelly Godfrey wakisoma vitabu wakati wa tamasha la  kusoma vitabu wanafunzi wa Shule za Msingi lililofanyika jijini Dar es Salaam kudhaminiwa na NSSF.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  IMG_9773
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo akikata utepe kuzindua Kisima cha maji safi na salama katika kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma mwishoni mwa juma lililopita.

  Na Modewjiblog team, Chamwino.
  KIJIJI cha Manchali kilichopo wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, kimekabidhiwa mradi wa dola za Marekani 150,000 wenye lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

  Mradi huo ulikabidhiwa kijiji hicho na Mratibu wa mashirika ya Umoja wa mataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodriguez.

  Mradi huo umelenga kusaidia jamii inayoishi katika kijiji hicho kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

  Mradi huo wa nishati ya jua umelenga kutatrua tatizo la nishati na kufanya matumizi bora ya ardhi na teknolojia ya maji.Mradi huo unasaidia familia 600.

  Kwa uzoefu wa Tanzania na maeneo mengine duniani, familia maskini ndizo zinazopigika vibaya na mabadiliko hayo na ndio haizna uwezo wa kukabiliana nayo.

  Kwa mradi huo wananchi wa Manchali wanatarajia kukabiliana vilivyo na mabadiliko ya Tabia nchi.

  Akizungumza katika kijiji hicho cha Manchali, Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Bi. Awa Dabo alisema kwamba ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi uwezeshaji wananchi kiuchumi ni muhimu sana ili kufanya familia kustawi.
  IMG_9772
  Kisima kilichozinduliwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo.

  0 0

  index
  MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili Afrika Mashariki na Kati, Ephraim Sekeleti amethibitisha kuwa mmoja wa waimbaji watakaopanda jukwaa la Tamasha la Krismasi na kushukuru linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Sekeleti amekubali kuwa mmoja wa waimbaji wa Kimataifa watakaopanda jukwaa la Shukrani ambalo litakuwa katika Sikukuu ya kumbukumbu ya kuzaliwa Masia, Yesu Kristo.

  Msama alisema tamasha hilo ni la Shukrani baada ya kuombea amani uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, Tamasha la Maombi lilifanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

  “Tunarudisha heshima na Shukrani kwa Mungu baada ya kuiepusha Tanzania na majaribu yaliyokuwa na mlengo wa kutaka kuvuruga amani ambayo iliasisiwa na baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere,” alisema Msama.

  Aidha Msama alisema kuandaa tamasha hilo inaonesha namna gani Watanzania tulivyo na shukrani ambako Watanzania tukumbuke kwamba Tukipewa, Tusisahau kushukuru.

  Ujumbe mzito ambao ni kumbukizi kwa Wanadamu ni kwamba binaadam tunapobarikiwa na Mungu hatuna budi kushukuru, hivyo tamasha hilo ni shukrani baada ya Mungu kusikia vilio vya Watanzania baada ya kuisaidia Tanzania katika uchaguzi Mkuu.   

  0 0


  0 0

  MWIMBAJI maarufu wa muziki wa Injili Tanzania, Upendo Nkone naye amejitokeza kuwa mmoja wa waimbaji watakaofikisha ujumbe wa Shukrani kwa Mungu katika Sikukuu ya Krismasi kupitia tamasha linalotarajia kufanyika Desemba 25 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Kamati imefanikisha makubaliano na mwimbaji huyo.Msama alisema Nkone anaungana na wenzake Rose Muhando, Ephraim Sekeleti sambamba na Kwaya ya Wakorintho wa pili.

  "Kabla ya kukubaliana na Nkone, tulikuwa tumeshamalizana na wenzake Rose Muhando, Ephraim Sekeleti ambaye ni raia wa Zambia sambamba na Kwaya ya Wakorintho wa Pili yenye maskani yake Mafinga mkoani Iringa, bado tunaendelea na mawasiliano na waimbaji wengine ili kunogesha tamasha hilo lenye malengo mawili ambayo ni Shukrani kwa Mungu sambamba na Sherehe za kuzaliwa Masiha, Yesu Kristo," alisema Msama.

  Aidha Msama alisema Kamati yake imepanga kufikisha shukrani kwa Mungu kupitia waimbaji na viongozi wa dini na wa kada mbalimbali kama ilivyokuwa kwenye Tamasha la Kuombea Amani lililofanyika Oktoba 4 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambako mgeni rasmi alikuwa ni mke wa rais wa awamu ya nne, Salma Kikwete.

  "Oktoba 4, tuliandaa Tamasha la kumbea amani uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 uwanja wa Taifa, hivyo ni nafasi yetu kumshukuru Mungu baaada ya kupitisha Tanzania kwenye uchaguzi ambao ulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani," alisema Msama.

  0 0
 • 11/24/15--02:45: Article 23
 • Acting Permanent Secretary at the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Amb. Celestine Mushy who was the Guest of Honor at the Algeria's National Day Reception delivers a speech on behalf of the Government of the United Republic of Tanzania. The reception held at the New Africa Hotel on Friday 20th 2015.
  Ambassador of Algeria to Tanzania, H.E Saad Belabed delivers a speech at that Algeria's National Day Reception.
  Invited guests who were dipolamitic community in the country and officials from various public and private institutions listen the speeches.

  MORE PHOTOS CLICK HERE

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA), Bw. Dickson Mveyange (kulia) akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu tathmini ya ushiriki wa Viziwi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Taifa Tanzania Bara uliofanyika 25 Oktoba, 2015. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam 24 Novemba, 2015. 
  Mshauri Mwelekezi Elimu ya Uraia kwa Watu wenye Viziwi, Bw. Novath Rukwago (Kushoto) akijibu baadhi ya maswali toka kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu ushiriki wa Viziwi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Taifa Tanzania Bara uliofanyika 25 Oktoba, 2015. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam 24 Novemba, 2015.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari toka Vyombo mbalimbali wakifuatilia taarifa toka kwa Viongozi wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kuhusu tathmini ya ushiriki wa Viziwi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Taifa Tanzania Bara uliofanyika 25 Oktoba, 2015. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam 24 Novemba, 2015.
  (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO).

  Na Zawadi Msalla
  CHAMA Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kimeeleza masikitiko yao juu ya ushiriki mbovu wa Viziwi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba kote nchini.

  Akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Habari-MAELEZO leo mshauri mwelekezi wa elimu ya uraia kwa watu wenye ulemavu Novat Rukwago amesema licha ya jitihada mbalimbali ambazo walijaribu kuzifanya ili kuhakikisha viziwi kote nchini wanapata haki yao ya msingi na ya kikatiba ya kupiga kura bado ushiriki wao haukuridhisha.

  Rukwago alizitaja changamoto mbalimbali zilizo jitokeza katika uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wataalamu wa lugha za alama zinazotumiwa na viziwi katika kampeni mbalimbali za Vyama vya Siasa, hivyo sera na Ilani za vyama hivyo hazikuweza kujulikana kwa viziwi.

  “Vyama vingi vilisema ni suala la rasilimali na ukosefu wa fedha za kuweka wataalamu hao, ingawa tuonavyo sisi ni kwamba walishindwa kutoa kipaumbele na si suala la fedha,” alisema Rukwago.

  Aidha, Rukwago alisema CHAVITA kwa juhudi binafsi waliweza kutembea jumla ya mikoa 17 kote nchini na kufanikiwa kutoa elimu kwa baadhi ya viziwi ambapo jumla ya viziwi 2516 walijiandikisha, idadi hiyo ikiwa na wanaume 1256 na wanawake 1260. Waliopiga kura walikuwa ni 1807.

  Aliongeza kwa kusema kuwa licha ya changamoto hizo pia mazingira ya kupigia kura hayakuwa rafiki kwa watu wenye uhitaji maalumu kwani hakukuwa na wataalamu wa lugha za alama katika vituo vya kupigia kura.

  Waliiomba Serikali kuzingatia umuhimu wa kuyapa kipaumbele makundi mbalimbali yenye uhitaji kwa chaguzi zijazo na kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya mawasiliano na vyama vya watu wenye uhitaji maalum mapema ili kuweza kushirikiana katika kuondoa changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwaka huu.

  0 0

   Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) , Jumanne Sajini baada ya kuwasili kwenye Ofisi ndogo ya TAMISEMI jijini Dar es salaam kuzungumza na watumishi Novemba 24, 2015.
   Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akizungumza na baadhi ya watumishi wa Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es salaam Novemba 24, 2015. 
   Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es slaam baada ya kuzungumza nao Novemba 24, 2015. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  MAFUNDI kutoka kampuni ya Philips wanaendelea na matengenezo ya mashine za MRI na CT-SCAN katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zilizopata hitilafu za kiufundi hivi karibuni.

  Akizungumza ofisini kwake leo hii Mkuu wa Idara ya Uhusiano Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Aminiel Buberwa Aligaesha amesema mafundi wapo katika eneo la kazi wakitengeneza hizo mashine ili ziweze kurudi katika hali yake ya kawaida.

  “Tumepewa siku tatu kukamilisha ukarabati wa hizi mashine hivyo wananchi wawe na subira kwani mashine zikiwa tayari kwa matumizi tutatoa  taarifa” alisema Aligaesha.

  Ameongeza kuwa wananchi wawape muda waweze kuzitengeneza mashine hizo ili ziweze kutengemaa kwa ajili ya kutoa huduma za MRI na CT-SCAN hospitalini hapo.

  Mashine za MRI na CT-SCAN zilianza kufanya kazi  mara baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kutembelea hospitali hiyo hivi karibuni na kuagiza kutengenezwa kwa mashine hizo na baadae kufanya kazi kwa muda wa siku kadhaa na kuharibika tena kutoka na hitilafu za kiufundi.

  Wakati alipotembelea Hospital ya Taifa ya Muhimbili jana Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue aliagiza mashine hizo kutengenezwa,  ndani ya siku tatu  ziwe zimekamilika kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.

  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imekuwa ni kimbilio la wananchi wengi kupata huduma za afya hivyo serikali inapamabana kwa kila hali kuhakikisha huduma za MRI na CT-SCAN zinarudi katika hali yake ya kawaida hospitalini hapo.

  0 0

       
  • Ni kupitia huduma yake ya M-Pesa
  • Sasa wateja wa Qatar kununua tiketi za kusafiri kupitia huduma hiyo

  SHIRIKA la Ndege la Qatar– Qatar Airways limeingia ubia na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya M-pesa kwa ajili ya kuwawezesha wateja wake kulipia tiketi zao ikiwa ni njia pekee ya kuwarahisishia wateja wao kutumia huduma hiyo kwa njia ya haraka na rahisi kwa kuwawezesha wateja wake kufanya malipo kwa njia ya simu za mkononi.

  Huduma hii inarahisisha maisha kwa wateja wanaotaka kusafiri na shirika la Qatar na wateja wa Vodacom ambapo kwa sasa hivi wanaweza kununua tiketi kupitia njia ya mtandao kupitia tovuti ya www.qatarairways.com/tz au kutembelea ofisi za shirika hilo na kulipia tiketi zao za usafiri kwa M-Pesa.

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania, Nina Pendaeli Eshum (Pichani) amesema “Tunayo furaha kubwa kuona familia ya watumiaji wa M-Pesa inazidi kuongezeka ambapo Shirika kubwa la Qatar limejiunga nasi katika huduma hii.Lengo letu siku zote ni kutoa huduma zinazoenda sambamba na mahitaji ya wateja wetu na ndio maana kupitia huduma hii tumewarahisishia maisha wateja wetu ambao wanataka kusafiri kwa kutumia ndege za shirika la Qatar kununua tiketi kwa rahisi kupitia simu zao za mkononi”.

  Eshun aliongeza kuwa huduma hii ambayo inaongoza kuwa na watumiaji wengi nchini katika kufanya mihamala ya kifedha na malipo itazidi kuboreshwa siku hadi siku ili iendane na mahitaji yao wateja na mitindo yao ya maisha katika kuwarahisishia shughuli zao kupita simu za mkononi.

  Kwa upande wake Meneja wa Shirika la ndege la Qatar nchini Tanzania,Basel Haydar alisema “ Kujiunga kwetu na huduma hii ni kwa ajili ya kuwawezesha wateja wetu kuwa na njia mbalimbali za kufanya malipo kwa ajili ya kupata huduma zetu ambapo hivi sasa wanaweza kutumia huduma hii ya M-Pesa ambayo ni moja ya njia ya kufanya mihamala ya malipo kwa urahisi bila usumbufu wowote”.

  Alisema hivi sasa shirika hilo linatoa ofa mbalimbali kwa wateja wake na limejipanga kwa kuendelea kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wateja katika soko la ushindani.

  Huduma ya M-Pesa ambayo inatumiwa na watu wengi duniani imeweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya fedha na kurahisisha maisha ya watu wengi.Ili kulipia huduma ya tiketi za usafiri kutoka Shirika la Qatar kinachotakiwa kufanyika ni kujiunga na menu ya M-Pesa kwenye simu ya mteja katika sehemu ya kufanya mihamala ya malipo ambapo atatakiwa kuandika namba 331199 ambayo ni namba ya kufanyia malipo ya shirika hilo, baada ya kuingiza namba hizo atatakiwa kuingiza namba za kumbukumbu ya booking yake na kiasi cha fedha alichotakiwa alipe wakati anashika nafasi ya tiketi (booking).Baada ya kutuma fedha mara moja atapata ujumbe mfupi wa maneno wa kumfahamisha kuwa fedha zake zimepokelewa na atapata tiketi yake kwa njia ya mtandao ambapo pia anaweza kuikuta uwanja wa ndege siku yake ya safari yake.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Uongozi wa Mtandao wa Wanawake Tanzania (WFT) wakati viongozi hao walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Nov 24, 2015 kwa mazungumzo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea baadhi ya Vipeperushi na Vitabu vya Mtandano wa Wanawake Tanzania (WFT) kutoka kwa mwenyekiti wa mtandao huo, Prof.Ruth Meena, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dares Salaam, leo Nov 24, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mtandao wa Wanawake Tanzania (WFT) baada ya mazungumzo yao yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dares Salaam, leo Nov 24, 2015. 
  Picha na OMR

  0 0

  Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imeahidi kuipa shule ya Sekondari ya Montofort iliyo Yombo Vituka, Dar es Salaam, Tsh. Milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa maabara huku ikiwataka wanafunzi wasomee  pia usafiri wa anga kwani sekta hiyo inahitaji wataalam marubani, wahandisi, watoa huduma kwenye ndege n.k.

  Ahadi hiyo ilitolewa na Mwanasheria Mkuu wa TAA, Wakili Ramadhan A. Maleta katika mahafali ya kidato cha nne cha shule hiyo iliyo jirani na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Shule hiyo inamilikiwa na Kanisa Katoliki na ni moja ya shule bora kielimu katika mkoa wa Dar es Salaam.

  Wakili Maleta aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi Suleiman S. Suleiman alisema TAA inatoa fedha hizo ikiwa ni mwendelezo wa jitihada zake katika kushirikiana na majirani zake  kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuwataka wanafunzi kushirikiana na TAA kupiga vita ugaidi.

  Alisema hivi sasa dunia inakabiliwa na changamoto kubwa ya ugaidi tukio kubwa likiwa la hivi karibuni nchini Ufaransa ambapo yanatishia usalama wa viwanja vya ndege na abiria wanaosafiri. Hivyo, alisema, wanafunzi hao na wengine, wanao wajibu wa kushirikiana na jamii kutoa taarifa zinazosaidia kudhibiti vitendo vya ugaidi.

  “Tumekubali kuja kushirikiana nanyi kwa sababu tunafahamu kuwa, ninyi ni washirika wazuri katika vita dhidi ya ugaidi, madawa ya kulevya na kama majirani, ni walinzi wakubwa na muhimu katika viwanja vyetu vya ndege. Mkiona kitu au matukio yasiyo ya kawaida yanayotishia usalama wa ndege, tujulisheni mapema iwezekanvyo,” Wakili Maleta aliwaambia.

  Aidha aliwapongeza wahitimu na kuwataka kujiendeleza zaidi kwani kwa dunia ya leo, elimu ya kidato cha nne ni mwanzo tu wa safari ndefu ya kupata maarifa. “Kidato cha nne kiwe mwanzo wa kwenda kidato cha tano na sita na hatimaye chuo kikuu, “ alisema na kuwataka wazazi wajijengee utaratibu wa kuwarithisha watoto wao elimu badala ya mali pekee.

  Mwalimu wa Taaluma, Ndugu  Chiku Sekilasi alisema tangu shule hiyo ianzishwe, imekuwa ikifanya vizuri katika taaluma ambapo mwaka 2013, katika mtihani wa kidato cha nne kitaifa, wanafunzi 11 walipata daraja la kwanza, 23 la pili, 17 la tatu na hakukuwa na daraja la nne wala 0 kati ya wanafunzi wote 51.

  Alisema mwaka 2014, kati ya wanafunzi 39 waliofanya mtihani wa kitaifa kwa muundo mpya, 5 walipata daraja la juu (distinction), 13 merit, 17 credit na 2 pass na hakuna aliyefeli na kwamba wanatarajia mwaka huu matokeo yatakuwa bora zaidi kutokana na juhudi za pamoja zilizoonyeshwa na walimu na wanafunzi husika.

  Mkuu wa shule hiyo, Bruda Dkt. Jim Madavana aliishukuru TAA kwa kuwasaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa maabara na kuomba wasamaria zaidi wawasaidie. Wanafunzi walikabidhiwa vyeti huku wale bora wakipewa zawadi ambapo kinara alikuwa Ndugu Emmy Bosco aliyewazidi wenzake katika masomo yote.


  IMETOLEWA NA KITENGO CHA SHERIA NA UHUSIANO TAA
  DAR ES SALAAM
   24.11.2015

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bibi Sophia Kaduma ameiagiza Bodi ya Sukari Tanzania, kushughulikia mara moja madai ya wakulima wadogo wa  miwa (outgrowers) katika Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kilichopo Mkoani Morogoro  yaliotokana na miwa yao kutonunuliwa na kiwanda. 

  Katika agizo hilo, Katibu Mkuu Bibi Sophia Kaduma ameiagiza Bodi ya Sukari Tanzania kukuta  na Uongozi wa Kiwanda  cha Sukari cha Kilombero na  ule wa wakulima wadogo wa miwa  ili kupata ufumbuzi wa kudumu kuhusu soko la miwa wanayozalisha.

  Aidha, Katibu Mkuu ametoa muda wa siku saba kwa Bodi ya Sukari Tanzania iwe imetekeleza na kutoa taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo. 

  Agizo hilo limekuja kufuatia Serikali kupata taarifa kuwa Uongozi wa Kiwanda hicho umeshindwa kununua miwa ya wakulima hao licha ya makubaliano yao ya awali ya kuzalisha miwa na kukiuzia kiwanda kwa ajili ya kuzalisha sukari.  Wakulima wamedai kuwa miwa hiyo, inakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16.

  Bodi ya Sukari Tanzania imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Sukari Na. 26 ya mwaka 2001 kama ilivyorekebishwa mwaka 2009 na Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Mazao Na. 20 ya mwaka 2009 (Crop Laws (Miscellenous Amendments) Act). 

  Bodi ya Sukari Tanzania inajukumu pamoja na mambo mengine, kusimamia na kuratibu  kilimo cha miwa  na biashara ya sukari nchini,  kusajili wakulima, wazalishaji wa sukari na wafanyabiashara wa sukari. 

  Aidha, Bodi ya Sukari ina dhamana ya kuhakikisha uwepo wa ushindani wa haki kwenye soko la miwa na biashara ya sukari nchini. 

  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
  Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika
  Kilimo Complex, 
  1 Mtaa wa Kilimo 15471
  DAR ES SALAAM.

  0 0

  Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania Dkt. Fatma Mrisho  akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani mwaka huu ambayo inaadhimishwa kwa  kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi  kupima afya zao na kupata elimu ya kujikinga  na maambukizi ya ugonjwa huo. 
   Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa TACAIDS Dkt. Jerome Kamwela akiwaonesha waandishi wa Habari Bango lenye Takwimu za Hali ya Maambukizi ya VVU nchini Tanzania.

  Na Nyakongo Manyama- MAELEZO.
  WITO umetolewa kwa wananchi kote nchini kuyatumia maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Desemba 1 ya kila mwaka kupima afya zao ili kudhibiti maambukizi mapya ya VVU.

  Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania Dkt. Fatma Mrisho amesema  Siku ya Ukimwi Duniani nchini itaadhimishwa kwa  kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kupata elimu ya kujikinga  na maambukizi ya ugonjwa huo.

  Ameeleza kuwa  maadhimisho ya mwaka huu yataambatana na shughuli mbalimbali zikiwemo za Utoaji wa Elimu ya Afya na Upimaji wa hiari wa VVU katika maeneo mbalimbali kote nchini kupitia vituo vitakavyowekwa, Kufungua kituo cha maarifa cha udhibiti UKIMWI eneo la Manyoni mkoani Singida ambayo ni njia kuu kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchi za Jirani za Burundi na Rwanda.


older | 1 | .... | 1035 | 1036 | (Page 1037) | 1038 | 1039 | .... | 3284 | newer