Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1028 | 1029 | (Page 1030) | 1031 | 1032 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Na Jovina Bujulu- MAELEZO    
                                
  Wakulima wametakiwa kutumia vizuri dhamana waliyopewa ya ya mfumo wa vocha ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.

  Wito huo umetolewa jijini Dar-Es-Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Kilimo, Chakula na Viwanda Richard Kasuga alipokuwa akitoa taarifa ya ruzuku ya pembejeo  za kilimo kwa njia ya vocha nchini.

  Kasuga aliendelea kusema kuwa matumizi sahihi ya mbegu bora na mbolea kwa mfumo wa vocha kunaongeza uwezo wa Taifa kujitosheleza kwa chakula ili kuondokana na umaskini na kufanikisha mapinduzi ya kijani.

  “Vocha ni haki ya mkulima na siyo upendeleo kwa mkulima anayepatiwa pembejeo hizo, hivyo itumike ipasavyo ili kuongeza uzalishaji wa mazao husika na kuleta tija katika mazao ya mahindi na mpunga” alisema ndugu Kasuga.

  Katika utaratibu huo wa vocha, wakulima wa mahindi na mpunga hunufaika kwa kupatiwa pembejeo, ambazo ni mbegu bora na mbolea zinazotosheleza ekari moja ambapo Serikali inachangia asilimia 50 ya bei ya soko kwa kila aina ya pembejeo wanayopewa wakulima hao.

  Vigezo vinavyotumika kutoa ruzuku kwa wakulima nchini ni pamoja na mnufaika kuwa na makazi ya kudumu katika kijiji na awea analima mpunga au mahindi na kaya iwe tayari kusaini hati ya pembejeo ili itumie kanuni ya kilimo bora.

  Kigezo kingine ni kaya kuwa na eneo lisilopungua ekari moja pamoja na kaya zinazoongozwa na makundi maalum hususani wajane na walemavu ndiyo hupewa kipaumbele.


  Akizungumzia faida za mfumo huo wa vocha, ndugu Kasuga alisema kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa chakula, ambapo ongezeko hilo limewezesha wakulima kuuza chakula ndani na nje ya nchi hivyo kuinua hali zao kiuchumi.


  Aidha, Taifa limeondokana na tatizo la kuagiza chakula nje ya nchi jambo ambalo limesaidia kuokoa fadha za kigeni hali inayotokana na elimu bora iliyotolewa kwa wakulima ambao wamehamasika kutumia mbegu bora na mbolea kwa maendeleo endelevu ya kilimo.

  Utaratibu wa kutoa ruzuku ya pembejeo kutoka Serikalini kwa mfumo wa vocha ulianzishwa na mwaka 2008/2009 ili kuboreka mfumo wa namna ya kuwafikishia wakulima ruzuku ya mbegu bora na mbolea ambazo hazikuwa zikiwafikia wakulima walengwa watarajiwa kwa namna iliyotarajiwa.

  Ili kuendeleza kilimo chenye tija, makampuni 23 ya mbolea na 27 ya mbegu bora ya mahindi na mpunga yanaendelea kutoa huduma ya kusambaza pembejeo hizo katika mikoa inayolima mazao hayo.

  Katika msimu wa kilimo wa 2015/16 mbolea tani 99,993, mbegu bora za mahindi tani 10,271 na tani 815 za mpunga zitatolewa kuwanufaisha wakulima wapatao 999,926 nchini.

  0 0

  SIMU.TV:  Spika bunge la 11 ni Ndugai CCM, Medeye UKAWA. Dr.Tulia  alonga, Mashine Muhimbili yaharibika tena; https://youtu.be/fs6B0RAK6dc 

  SIMU.TV:  Mauwaji kigogo CHADEMA, BAVICHA watoa siku 3, wataka polisi iwakamate. Wafukiwa na kifusi siku 41 na kutoka hai; https://youtu.be/JU8pAIl2L8o 

  SIMU.TV:  Malkia amtumia salamu Dr.Magufuli, Kinana awataka wabunge CCM kuchapa kazi. Baba auwa mke na watoto Kilimanjaro; https://youtu.be/-Xa3wRf-31A

  SIMU.TV:  Taifa Stars kufa na kupona leo, Mkwasa atamba kurudi na ushindi. Bosi mpya YANGA ajaza mambo ya kizungu; https://youtu.be/D2-pVkcrFGU

  SIMU.TV:  Pata habari za kina zilizotawala katika magazeti ya leo Novemba 17.2015 hapa Simu.tv; https://youtu.be/_drzaWqLQw0

  0 0


  Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Motisun Group Subhash Patel (wapili kushoto) akiwasha mshumaa pamoja na wawakilishi wa makampuni tanzu za Motisun Group kuashiria uzinduzi wa mabati ya Kiboko Imara. Hafla ya uzinduzi ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar-es-salaam.
   Balozi wa mabati ya Kiboko Jacob Steven ‘JB’ akicheza ngoma ya asili na kikundi cha KP traditional dance katika uzinduzi wa mabati ya Kiboko Imara yanayotengenezwa na kampuni ya MMI STEEL. Hafla ya uzinduzi ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar-es-salaam.
   Mwenyekiti na mkurugenzi mtendaji wa Motisun Group Subhash Patel akimvalisha taji balozi wa mabati ya Kiboko Imara Jacob Steven ‘JB’ katika uzinduzi wa mabati ya Kiboko yanayotengenezwa na kampuni ya MMI STEEL. Hafla ya uzinduzi ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar-es-salaam.
  Kampuni inayozalisha vifaa vya ujenzi, iitwayo Motisun imezindua teknolojia itakayoongeza ubora na kuimarisha vifaa kama mabati kwa ajili ya kuezekea paa za nyumba na majengo.

  Teknolijia hiyo ilizinduliwa jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Sea Cliff na kutangazwa kuanza kwa shughuli ya uuzaji wa mabati hayo katika maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi.

  Mwenyekiti na Muasisi wa kampuni ya Motisun, Subhash Patel alisema, teknolojia hii inahusu utumiaji wa madini ya aluminiamu na zinki ambayo huongeza ubora na kuyafanya mabati kudumu zaidi.Alisema bidhaa hii mpya itakuwa ikipatikana chini ya kampuni tanzu ya Motisun iitwayo MMI. Bidhaa zitakuwa zikiuzwa katika maduka ya rejareja hususani katika maeneo ambapo wateja hupendelea bidhaa za ubora wa hali ya juu.

  “Bidhaa hii itakuwa inajulikana sokoni kwa jina la Kiboko Imara. Ili kuiunganisha na walaji, Kiboko Imara itakuwa ikitangazwa na Msanii maarufu Jakobo Stephen ambaye anafanya zivuri katika fani yake na kuwa na mvuto kwa wengi,” alisema. 

  Bwana Patel anasema kuzinduliwa kwa bidhaa mpya kunaashiria juhudi za kampuni ya MMI kuongeza wigo wa bidhaa kwa kuzingatia mahitaji ya teknolojia ambayo ina manufaa mengi katika sekta ya ujenzi.
  Kampuni ya MMI ni maarufu kwa uzalishaji wa bidhaa za ujenzi kama nondo ambazo zimekuwa zikiuzwa ndani na hata nchi jirani za Msumbiji, Zambia na Uganda zikiambatana na ubora.

  “Tumejiandaa kikamilifu kuifanyia mauzo bidhaa hii mpya katika masoko hapa nchini na nchi   jirani ambapo pia kuna fursa ya masoko,” alisema bwana Patel.Bidhaa za mabati zilizopakwa madini ya aluminiam na zinki zimekuwa zikikubalika sana katika masoko mengi duniani kwa ajili ya makazi ya kuishi na majumba makubwa ya biashara ambayo huweka msisitizo katika viwango vya ujenzi.

  Alisema tayari kuna wimbi kubwa la asili la watu kuhamia katika matumizi ya mabati yaliyopakwa madini ya aluminiamu na zinki kutokana na kuwa na uwezo wa kudumu kwa muda mrefu.
  “Ni kwa sababu hii MMI imechagua kuzalisha bidhaa hii muhimu nchini Tanzania kwa matumizi ya makazi ama miradi ya biashara,” alisema bwana Patel.

  Bidhaa hii ya Kiboko Imara inatoa wigo mpana kwa matumizi mbalimbali mfano urefu, rangi na hata unene wa mabati. “Hii inamaanisha mapaa mbalimbali huhitaji unene na urefu tofauti wa mabati, mfano nyumba ya kuishi inahitaji mabati yenye unene wa kawaida wakati paa za majengo ya viwanda na biadhara kubwa kubwa huhitaji mabati manene zaidi,” alisema.Kwa mujibu wa bwana Patel, utengenezaji wa bidhaa hii mpya umezingatia viwango vya kitaifa na kimataifa kwani zimejaribiwa ili kukidhi viwango vya ubora.

  0 0

  Dk. Bhuvaneshwari Shankar, Mkuu wa idara ya lishe kutoka hospitali za Apollo.

  Na Mwandishi Wetu,

  Novemba 14 kila mwaka tunaadhimisha siku ya kisukari duniani ili kuongeza uelewa kuhusu madhara ya kisukari, matatizo yanayoletwa na huu ugonjwa na taarifa muhimu kuhusu kisukari.

  Siku hii inabeba ujumbe mahususi kwa watu wote ulimwenguni. Kauli mbiu katika siku hii tokea 2014 hadi 2016 ni maisha bora na kisukari(healthy living and diabetes) na mwaka huu kuna mtazamo zaidi katika kuzingatia mlo kamili na kuanza kila siku na kifungua kinywa bora.

  Kutoka katika shirika la kisukari Africa, Tanzania ni kati ya nchi 32 katika shirikisho hilo kwa viwango vya nchi zenye viwango vya kisukari duniani. Kulikuwepo na zaidi ya kesi milioni 1.7 za kisukari hapa Tanzania kwa mwaka 2014. Shirika la afya duniani (WHO) linakadiria zaidi ya watu milioni 180 ulimwenguni wana kisukari, na hiyo takwimu inatarajiwa kuongezeka ifikapo mwaka 2030 kama hamna hatua yoyote itakayochukuliwa.

  SOMA ZAIDI HAPA

  0 0
 • 11/17/15--00:45: BEI YA MADAFU LEO


 • 0 0


  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Polisi, wakati wa mkutano wa Kujitambulisha na kufahamiana na Watendaji wakuu na Maafisa wa Jeshi la Polisi uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mngodo alilipongeza jeshi hilo kwa kusimamia Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu. Kulia kwa Katibu Mkuu ni Inspekta Jenerali wa Jeshi hilo (IGP), Ernest Mangu.
  Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (kushoto) akiwaongoza watendaji wakuu na maafisa wa jeshi hilo kuimba wimbo wa maadili wa jeshi hilo wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (wapili kushoto). Ziara hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo, ilikuwa na lengo la kujitambulisha na kufahamiana na watendaji hao. Watatu kushoto meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki, wapili kulia ni Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa Jeshi la Polisi Clodwig Mtweve, na kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.
  Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (kushoto) akitoa taarifa ya Jeshi hilo wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujitambulisha na kufahamiana na watendaji wa jeshi hilo.


  0 0

  Mkurugenzi wa The African Enterprise Challenge Fund (AECF), Hugh Scott akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na uzinduzi wa awamu ya nne ya dirisha la ufadhili wa kilimo cha biashara maalum kwaajili ya watanzania hapa nchini.
  Afisa mkuu wa usimamizi, Sam Ng'ang'a akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkurugenzi wa The African Enterprise Challenge Fund (AECF), Hugh Scott.
  Mkurugenzi wa kampuni ya Internation Tan Feed LTD, Faustine Lekule akizungumza na waandishi wa habari leo kwa jinsi kampuni yake ilivyoweza kunufaika na ruzuku inayotolewa na AECF kwa kuweza kugundua aina mbalimbalimbali za vyakula vya mifugo hapa nchini.

  Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
  MFUKO wa The African Enterprise Challenge Fund (AECF) umezindua awamu ya nne ya dirisha  la ufadhili wa kilimo cha Biashara na huduma za kifedha vijijini hapa nchini.

  Ameyasema hayo Mkurugenzi wa mfuko wa The African Enterprise Challenge Fund (AECF), Hugh Scott wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  Scott amesema kuwa sambambamba na kuzindua awamu ya nne kutakuwa na shindano lenye lengo la kuhamasisha watu wenye mawazo ya kilimobiashara kwaajili ya kupewa ufadhili wa waombaji watakaoshinda katika shindano hilo.

  "Waombaji watakaoshinda watapewa ruzuku na mikopo isiyo na riba kati la dola za kimarekani laki moja na dola za kimarekani milioni moja", alisema Scott

  Pia Scott ametoa wito kwa makampuni mbalimbali, sekta mbalimbali au vikundi yenye mawazo ya kilimobiashara kutuma maombi kwenye mtandao wa intaneti wa www.aecfafrica.org ili kuweza kuomba  na kushindania shindano.

  Aidha  Scott amesema kuwa shindano hilo lipo wazi kwa makampuni yanayotengeneza faida na linahamasisha makampuni ya ndani na kampuni ya kigeni kuomba nafasi hiyo lakini mawazo yake yawe ya kilimobiashara yatakayopendekezwa katika uombaji lazima yawe yanafanyika hapa nchini.

  Pia amesema kuwa shindano hili limeshaanza kuanzia leo na mwisho wa kutuma maombi ni Disemba 15 mwaka huu.

  Scott alitoa wito kwa sekta binafsi kuchangamkia frusa iliyotolewa na mfuko wa AECF  hapa nchini kutokana na kuzinduliwa kwa mara ya nne na kwa ufadhili wa kilimo biashara ili waweze kuitikia na kuwa na mawazo ya biashara yenye ubunifu ambayo yataleta manufaa kwa maisha ya watanzania waishio vijijini.

  0 0

  Hatimaye Job Yustino Ndugai CCM amechaguliwa kuwa Spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kwa kura 254 sawa na asilimia 70% ya kura zilizopigwa akifuatiwa na mgombea wa CHADEMA Goodluck Ole Medeye ambaye amepata kura 109.

  Hata hivyo wagombea hao ambao walikuwa 7 kati ya 8 wameweza kutoa shukrani na pongezi kwa Ndugai wakisema anastahili na ndio maana akachaguliwa na kumtaka aongoze vyema bunge hilo.

   Job Ndugai ameibuka mshindi wa kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupata kura 254 sawa na asilimia 70 ya kura zote ambapo jumla ya kura zilizopigwa ni 365

  Matokeo ya kura za Spika.

  A: Job Ndugai (CCM)- 254
  B: Goodluck Ole Medeye (CHADEMA) - 109
  C: Hashimu Rungwe (CHAUMA)- 0
  D: Peter Sarungi (AFP) -0
  E: Dkt Godfrey Malisa (CCK)- 0
  F: Richard Lymo (T.L.P) -0
  G: Robert Kisinini (DP) -0

  Kura zilizoharibika ni 2

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari alipokuwa akitangaza mikakati ya kampuni hiyo kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa teknolojia na itakavyotumia kubadilisha maisha ya watanzania na kuwa bora zaidi.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, wakiwa katika mkutano wa waandishi wa habari na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ian Ferrao (hayupo pichani)alipokuwa akitangaza mikakati ya kampuni hiyo kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa teknolojia na itakavyotumia kubadilisha maisha ya watanzania na kuwa bora zaidi.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
  (Picha na Mpigapicha Wetu).


  • Yawekeza zaidi ya Dola bilioni 1 nchini
  •  Mtandao wake wa 2G na 3G umewafikia wananchi kwa 87%
  • Inao mtandao wa mawakala zaidi ya 85,000 wa M-Pesa nchini kote.
  • Biashara zaidi ya 10,000 nchini kote wanatumia huduma ya Lipa kwa M-Pesa
  • Ni kinara wa kulipa  na kukusanya kodi za serikali katika sekta ya mawasiliano


  KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambayo inaongoza kwa kuwa na mtandao mkubwa nchini na mtandao wenye kasi zaidi wa 3G leo imetangaza mikakati yake ya kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa teknolojia na itakavyotumia teknolojia kubadilisha maisha ya watanzania kuzidi  kuwa bora.

  Akitangaza mkakati huo kwa waandishi wa habari leo katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, alieleza mikakati hiyo mbalimbali “Tunafurahi kuona mchango wa Vodacom katika kuleta maendeleo nchini na kubalisha maisha ya watanzania kuwa bora, Hivi sasa tumejizatiti kuboresha huduma za mawasiliano nchini na pia tutaendelea kubuni huduma mbalimbali za kutumia teknolojia ya simu kurahisisha maisha ya wananchi.

  Tutaendelea kuboresha na kusambaza huduma zetu za internet nchi nzima na kutoa huduma za kifedha na malipo kwa kutumia teknolojia,kuuganisha biashara mbalimbali kwa kutumia teknolojia tukiwa tunaenda sambamba na mkakati wa  serikali wa kuleta mapinduzi ya matumizi ya teknolojia katika kupata huduma mbalimbai nchini”

  Mpaka sasa Vodacom imewekeza kiasi cha  zaidi ya Dola bilioni 1 za kimarekani nchini Tanzania,imejenga mtandao wa kutoa huduma za internet ya 2G na 3G na mtandao wake unawafikia asilimia 87 ya watanzania nchini kote.Ikiwa inajivunia kufanya kazi na mtandao mkubwa wa mawakala wake zaidi ya 85,000 wa kutoa huduma ya kifedha ya M-Pesa. Vodacom inayo wateja zaidi ya milioni 12 na pia ni kinara wa kukusanya na kulipa kodi za serikali katika sekta ya mawasiliano nchini.

  Ferrao alisema licha ya changamoto mbalimbali zilizopo katika uwekezaji  kwenye sekta ya mawasiliano nchini kama vile kodi kubwa na ushindani katika bei za kutoa huduma, Vodacom itaendelea kuwekeza na kubuni huduma za kuleta ushindani kwenye mapinduzi ya matumizi ya teknolojia nchini.

  Kuhusiana na ushindani wa bei za kutoa huduma Ferrao alisema  “Ushindani huu wa makampuni katika bei za kutoa huduma unawanufaisha wateja kwa muda mfupi,kinachotakiwa ni kuendelea kufanya uwekezaji endelevu kama vile kusambaza zaidi huduma ili ziweze kuwafikia wananchi wengi hususani wa maeneo ya vijijini.

  Tukiwa ni moja ya nchi inayotoza viwango vya juu vya kodi katika seka ya mawasiliano duniani tunachopaswa kufanya ni kutumia huduma hizi kuleta mapinduzi yatakayoleta mabadiliko kwa wananchi kuwa bora na kujenga uchumi imara na wenye ushindani”Alisema

   Katika kufanikisha  mchango wa sekta ya mawasiliano kuleta mapinduzi nchini alisema kuna mambo yanapaswa kuangaliwa “Tumekuwa tukishuhudia  ongezeko la kodi hususani kodi ya zuio, katika sekta ya mawasiliano ambapo kodi zinazotozwa hapa nchini ni kubwa katika nchi zote za Afrika Mashariki na nchi za SADC.

  Utafiti wa Taasisi ya Deloitte Consulting  katika mkutano wa makampuni ya mawasiliano uliofanyika jijini Dar salaam mapema mwaka huu inaonyesha kuwa sekta ya mawasiliano inachangia asilimia 3.8%  ya pato la Taifa na asilimia 11 ya mapato ya serikali kupitia kodi na  kodi hizo zinaongeza gharama za uendeshaji  kwa kampuni ambapo mzigo wote humwangukia mtumiaji kutokana na gharama za huduma kupanda.

  Kwa mfano serikali ikipunguza kodi ya zuio katika huduma ya muda wa maongezi kutoka asilimia 17 mpaka asilimia 10 itawezesha wateja wapya 1.7 millioni kujiunga na huduma za simu na kwa kufanya hivyo zitawanufaisha katika shughuli zao mbalimbali za uzalishaji na kutakuwepo ongezeko la mapato linalofikia Dola 0.5 bilioni katika pato la taifa hadi kufikia mwaka 2020”.

  Kuhusiana na suala la masafa yaliopo kwa makampuni ya simu  nchini alisema leseni zake zimetolewa kwa makampuni zaidi ya 14  ambayo mengi yao yanashikilia masafa  bila kuyatumia lakini leo hii wateja zaidi ya asilimia 99 wanahudumiwa na makampuni yenye masafa ya mawimbi ya mtandao  ya asilimia 53 ambapo makampuni yanayotoa huduma za mawasiliano hivi sasa hayapati masafa ya kutosheleza mahitaji ya kusambaza huduma zake kwa ufasaha.

   Ferrao alisema wakati umefika kwa masafa ya makampuni kuongezwa hadi kufikia 700Mhz kuwezesha makampuni kuwekeza kwa kutumia teknolojia za kisasa zaidi na zenye gharama nafuu ambazo zinaweza kuwezesha kuzinduliwa interneti mpaka ya 4G nchini.

  Alisema pamoja na changamoto mbalimbali zilizopo Vodacom imewekeza zaidi shilingi Bilioni 180 kwa muda wa miezi sita iliyopita  katika kuboresha mtandao wake wa internet na imejipanga kuboresha huduma zake mbalimbali.

  Ferrao aliongeza “Wakati Vodacom inajizatiti kuboresha huduma zake taasisi yake ya kuboresha huduma za jamii ya Vodacom Foundation imejikita kuendelea kutoa misaada mbalimbali kwa jamii hususani kwa ajili ya kuendeleza akina mama na makundi mbalimbali yenye mahitaji.

  Mwaka huu imewezesha operesheni kwa ajili ya wanawake 2,274 walioathirika na fistula , na kuwezesha wasichana 7,077 kubaki shuleni kupitia mradi wa Hakuna Wasichoweza na imewezesha zaidi ya wanafunzi 6,000 kusoma elimu ya kompyuta kwa vitendo mashuleni.Vodacom Foundation imekwishatumia shilingi bilioni 12 kusaidia jamii tangu ianzishwe mwaka 2006 na itaongeza zaidi kiasi hicho cha fedha kusaidia miradi mbalimbali katika mwaka wake wa fedha ujao”

  Alimalizia kwa kusema “Hatutaacha kubuni na kutoa huduma bora lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha watanzania wote wameunganishwa na huduma ya mtandao wa intaneti”

  0 0

  Senior officials of the Arusha-based United Nations International Criminal Tribunal for Rwanda (UN-ICTR) last week visited Kigali, Rwanda to bid farewell to the people and Government of Rwanda, the diplomatic community and other stakeholders who have supported the work of the Tribunal in its 21 years of operation. The Tribunal will be closing its doors on 31 December 2015. 

  During its duration the ICTR indicted a t total of 93 individuals for the crimes of genocide, crimes against humanity and war crimes committed in the territory of Rwanda in 1994.It arrested 83 of them whose cases have now been completed. One individual died before arrest and 9 others are yet to be arrested. The UN Security Council has established the Mechanism for International Criminal Tribunals (MICT) which will pursue the fugitives.

  In the picture are the ICTR Principals, from right, Mr. Bongani Majola, the Registrar; Justice Hassan Bubacar Jallow, the Prosecutor; and Judge Vagn Joensen, the President laying a wreath at the Gisozi Genocide Memorial Centre in Kigali. Others in the picture are the Centre's Director Mr. Honore Gitare (second left) and the ICTR Public Information Officer, Mr. Danford Mpumilwa (left). 

  0 0

   Vijana wa YAM ( Youth Action Movement) ambao ni waandaaji wa tamasha hili linalofanyika kila mwezi wakionesha igizo lao lililobeba ujumbe unaosema ni jukumu la wazazi kuwaelimisha vijana juu ya afya ya uzazi na ujinsia ili kuwakinga na maambukizi ya VVU mimba katika umri mdogo na ngono katika umri mdogo.
  Mwenyekiti wa UMATI dar es salaam Mr.Harith Shomvi ambae alikuwa mgeni rasmi  katika tamasha hilo akihutubia wananchi na kuwasisitiza wapate huduma za uzazi wa mpango na upimaji ambazo zilikuwa zikitolewa bure katika tamasha hilo. Tamasha hilo lilikuwa na kauli mbiu isemayo "JE kutoa  elimu  juu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana ni jukumu la nani?
  Picha na Maelezo.

  0 0


   Mkutano wa kila mwaka wa Kuwezeka umeme Afrika: Kongamano la Uwekezaji la Tanzania litafanyika Hyatt Regency Dar es Saalam, Hoteli ya Kilimanjaro kuanzia 3-4 Desemba 2015 

  Mkutano ule utalenga siku za usoni za sekta ya kawi ya Tanzania kufuatia uchaguzi wa hivi majuzi, kutambua nafasi za uwekezaji na kubuni maushurikiano  muhimu kati ya wahusika kutoka sekta ya kibinafsi na ya umma. 

  Dhibitisho za hivi karibuni za January Makamba, Mbunge wa Bumbuli, Tanzania, waakilishi kutoka Kitengo cha Rais cha Utekelezaji (PDB), Wizara ya Kawi, Madini na Kampuni ya Usambazaji wa Gesi (GASCO) zinaashiria juhudi zinazoendelea katika sekta ya umma  kuharakisha ufikiaji wa kawi nchini Tanzania kama  hatua muhimu katika ukuzaji wa uchumi. 

  Hadi sasa, kampuni 37 za kipekee kutoka sekta ya kibinafsi zimedhibitishwa kuhudhuria ikiwa ni pamoja na Benki ya Uwekezaji ya Tanzania, Standard Chartered Bank, Mitsubishi Corporation, CitiBank Tanzania, BVI Consulting, Liquefied NG Tanzania, Statoil na Sunfunder. 

  Yale mazugumzo yatalenga mijadala kama vile kujitolea kwa Tanzania kwa mageuzi ya sekta ya kawi, ukuaji wa kitengo hicho pamoja na ukuzaji gesi, mbinu za Tanzania za ununuzi katika sekta za kampuni za umma na umuhimu wa umeme kwa kilimo katika viwanda husika vya kuzalisha kawi. 

  Kufuata ufadhili wa hivi karibuni wa dola za Marekani milioni $5 kutoka IFC kuwezesha Tanzania kuchunguza uwezo wa mitambo ya kawi iliyo ya nguvu za chini, mpangilio ule utachunguza pia njia mbalimbali za kupeana kupasisha kawi hadi nchini Tanzania na nafasi za kawi ya zitokanazo na jua, upepo, joto na maji, kama maendeleo ya ukuzaji wa kawi.
                                   


  0 0


  0 0
  0 0
 • 11/17/15--19:35: Article 21

 • 0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya Watu zaidi ya 120 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi jijini Paris majuzi.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mama Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 120 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi  majuzi.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph  Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Mama Malika Berak mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo na kutoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mhe.  Francois Hollande kufuatia vifo vifo vya Watu zaidi 120 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.

  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili mkoani Dodoma na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Galawa. Rais Magufuli amesafiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa kutumia usafiri wa Gari.


  0 0


  Mheshimiwa Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania nchini Marekani, anasikitika kutangaza kifo cha Bi. Nyamiti Ivan Lusinde, aliyekuwa mfanyakazi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Washington DC.


  Bi. Nyamiti Ivan Lusinde  alifariki dunia Jumanne tarehe 17 Novemba, 2015 Dar Es Salaam, Tanzania ambapo alikuwa likizo yake ya mwaka.


  Kitabu cha rambirambi kipo nyumbani kwa marehemu

  20408 Honey Crisp Lane, Apartment E

  Germantown, MD 20876  Maelezo zaidi kuhusu taratibu za mazishi 
  yatatolewa mara baada kupokea taarifa zaidi  kutoka nyumbani Tanzania. 


  0 0


  0 0

  DSC_1602
  Rais wa klabu ya Rotary Dar es Salaam Oyster Bay kwa mwaka huu wa 2015-2016, Mohamed Versi akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) katika mji wa Kerege jana Novemba 15. wakati wa zoezi hilo la kambi ya bure ya upimaji wa afya. (Picha zote na Andrew Chale ).
  Na Andrew Chale, Modewjiblog

  [BAGAMOYO] Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oyster Bay, kwa mara nyingine tena imeendesha matibabu katika kambi maalum ya matibabu ya bure katika mji wa Kerege uliopo Bagamoyo, Mkoani Pwani.

  Kambi hiyo iliyofanyika siku ya Jumapil Novemba 15.2015 ambapo zaidi ya wahudumu 50 wa Afya walipima na kutibu magonjwa kwa wakazi hao wa Kerege waliojitokeza kwa wingi wanaokadiriwa kufikia zaidi ya 700.

  Kambi hiyo ya matibabu bure imedhaminiwa na benki ya Diamond Trust Bank (DTB) imeweza kuwa faraja kubwa kwa wananchi na wakazi wa Kerege kupata Huduma hiyo kwani imeweza kuwafikia muda muafaka kwao kupata fursa za matibabu na vipimo bure.

  Akizungumza na wanahabari Rais wa klabu hiyo ya Rotary Dar es Salaam Oyster Bay kwa mwaka huu wa 2015-2016, Mohamed Versi amebainisha kuwa wito mkubwa kwa wananchi wa Kerege kujitokeza kunawapa faraja kuendelea kutembelea na kuweka kambi kwa mwaka mara moja katika mji huo.

  “Mwaka huu ni wa tano tokea kuanza kutoa matibabu bure kwa kuweka kambi hizi za matibabu. Kwa hapa Kerege huu ni mwaka wa nne tunafika hapa na kuhudumia wananchi huku zaidi ya wananchi, 600 hadi 700 wanahudumiwa ikiwemo vipimo na matibabu” alisema Versi.

  Aidha, Rais huyo alibainisha kuwa, mbali na kutoa matibabu bure pia wameweza kutoa dawa pamoja na neti za kuzuia mbu kwa kila mwananchi aalijitokeza kwenye kambi hiyo.
  Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko kutoka benki hiyo ya DTB, Bw. Sylvester Bahati amebainisha kuwa kujitokeza kudhamini kambi hiyo ni miongoni mwa taratibu za benki hiyo kuweza kusaidia jamii.
  “Tunawapongeza Rotary Klabu kwa kuona umuhimu wa kusaidia kambi hii ya Kerege matibabu bure na ufadhili wetu hapa unaendana na sawa na taratibu tulizojiwekea za kutoa gawio kwa jamii kama zilivyotaratibu nyingine tulizonazo” alibainisha Bw. Bahati.

  Aidha, ameeleza kuwa Benki hiyo ya DTB ina matawi zaidi ya 20 nchini huku ikitarajia kufungua matawi zaidi kwa nchi nzima ikiwemo Zanzibar.

  Kwa upande wake daktari na mratibu wa magonjwa ya Kisukari, Dk. Bashiru Rajab ameeleza kuwa, wengi wa wa wagonjwa walipatikana katika kambi hiyo ni wale wa matatizo ya mapigo ya moyo (Blood pressure ).

  “Katika kambi hii wengi wa wananchi wanaofika hapa wanakabiriwa na matatizo ya Presha na ugonjwa wa Maralia huku wa kisukari wakiwa wachache. Inatia faraja sana kwani wamepata kujua hali ya afya zao za mwili na tunawashahuri wawe na taratibu ya kupima afya mara kwa mara” alibainisha Dk. Bashiru.

  Kwa upande wao baadhi ya wananchi walipongeza waandaaji wa kambi hiyo ambapo imewasaidia kujua afya zao hivyo kuchukua hatua ikiwemo suala la kuzingatia kanuni za kufuata pamoja na ushahuri wa kitabibu.

  Matibabu, sehemu mojawapo ya Miradi ya Afya ya Jamii, ambayo hufanyika kila mwaka toka ilipozinduliwa mwaka 2011 katika kitongoji cha Chanika jijini Dar es Salaam ambapo takribani wananchi 600 walijitokeza kupima malaria, VVU, Kisukari, magonjwa ya mfumo wa upumuaji, macho na viashiria vya magonjwa sugu na baadae kuamia katika mji huo wa Kerege kwa mwaka wa nne sasa huku wakitoa dawa na miwani bure.

  Kwa mwaka huu imedhaminiwa na benki ya Diamond Trust Bank, Rotary Club of Seattle4 huku ikiandaliwa kwa kushirikiana na Shree Hindu Mandal Hospital, Vital Supplies, Kids Care Tanzania, Elite Dantal Clinic, Whitedent, Sayona, Ultimate Security na wengine wengi.
  DSC_1655
  Mkuu wa kitengo cha Masoko kutoka benki ya Diamond Trust Bank [DTB] akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa zoezi hilo la kambi ya matibabu bure. DTB ndio wadhamini wakuu katika kambi hiyo.
  DSC_1630
  Daktari na mratibu wa magonjwa ya Kisukari, Dk. Bashiru Rajab akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo la kambi ya bure ya Matibabu katika mji wa Kerege,Bagamoyo Pwani.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 1028 | 1029 | (Page 1030) | 1031 | 1032 | .... | 3285 | newer