Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAIPONGEZA JUHUDI ZINAZOFANYWA NA TAASISI YA DORIS MOLLEL FOUNDATION ZA KUSAIDIA WATOTO NJITI

$
0
0
DSC_1839Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki akizungumza mbele ya wanahabari, madaktari na baadhi ya akina mama waliokuwa na watoto waliozaliwa kabla ya wakati maarufu kama Njiti (Hawapo pichani). Kushoto ni DoriS Mollel ambaye ni Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF) na wengine ni maafisa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

Na Andrew Chale, Modewjiblog
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongeza juhudi binafsi zinazofanywa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF) katika harakati zake za kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) na mambo ya elimu hapa nchini huku ikiahidi kuendelea kushirikiana nayo kufikia malengp yake.

Kauli hiyo imetolewa mapema leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki wakati wa kupokea vifaa maalum vya kusaidia watoto njiti vilivyotolewa na taasisi hiyo ya Doris Mollel Foundation tukio lililofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jengo la Watoto.

“Tunatambua mashine hizi ni bei kubwa na Serikali pekee yake haina pesa hivyo kwa kusaidiana na wadau kama hivi n faraja sana na tunapongeza juhudi hizi za taasisi ya DMF kwa kujitokeza kusaidia mashine kwa watoto njiti” ameeleza Mkuu wa Mkoa huyo.

Mkuu wa Mkoa huyo aliongeza kuwa, Mashirika mengine yaendelee kujitokeza kusaidia huduma za kijamii ikiwemo vifaa kama taasisi ya Doris Mollel kwani asilimia 100 ya wagonjwa na watu wengine wenye mahitaji katika tiba wanakimbilia Dar es Salaam hasa Hospitali ya Muhimbili.

“Tunaomba tena mukipata nyingine musisite kutiletea hapa maana Mkoa huu unapokea wagonjwa wengi kutoka maeneo mengi ya Tanzania na vifaa vya tiba mara nyingi vinakuwa ni vichache, Huko mikoani wanapewa rufaa waanakuja hapa pia hivyo DMF musisite kuja tena” alimalizia Mkuu wa Mkoa huyo.

Hata hivyo kwa upande wake Mwanzilishi na mtendaji Mkuu wa DMF, Doros Mollel amemweleza Mkuu wa Mkoa Meck Sadik kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali bega kwa bega katika juhudi za kusaidia watoto njiti nchini ikiwemo kutoa elimu, vifaa na usaidizi kwa jamii dhidi ya kukabiliana na watoto njiti nchini.

Katika tukio hilo, Mkuu wa Mkoa alishudia vifaa hivyo na kupokea kutoka DMF sambamba na kutembelea wote ya watoto njiti pamoja na ile ya Kangaroo ambayo wamama wenye watoto njiti wanakuwa wanapatiwa uangalizi maalum dhidi ya watoto wao ikiwemo kupata joto la Mama na baadae alipanda mti maalum mbele ya jengo hilo la Watoto kama kumbukumbu na juhudi za wadau katika kusaidia jamii dhidi ya watoto njiti.

DMF imeweza kusaidia vifaa katika wodi hiyo ya watoto Muhimbili vikiwemo (Suction machines, Oxygen Concentrators na Feeding tubes). Aidha Doris Mollel amebainisha kuwa baada ya hapo wanatarajia kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa kutoa vifaa kama hivyo huku lengo ikiwa ni kufika mikoa yote ya Tanzania.
DSC_1855
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili wakishuhudia tukio hilo maalum la taasisi ya DMF ilipotoa vifaa hivyo katika kitengo cha Jengo la Watoto.
DSC_1865
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadik akipata maelezo juu ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Taasisi ya DMF.
DSC_1870
Msimamizi wa wodi ya akina mama wanaopatiwa huduma ya Kangaroo dhidi ya watoto wao ambao walizaliwa njiti, akimpatia maelezo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alipotembelea wodi hiyo leo.

BOFYA HAPA WA PICHA ZAIDI

Kukamilika kwa daraja la Mbweni JKT ni furaha kwa wananchi

$
0
0
Daraja lililokuwa linawasumbua mno wakazi na wananchi wa Mbweni JKT, sasa linaelekea mwishoni, hali iliyoanza kuwafurahisha wananchi hao waliokuwa wakisumbuka kuvuka eneo hilo lililokuwa linajaa maji mara kwa mara yanayotoka baharini.


Katika pita pita ya mitandaoni, tuliona picha hizi ambazo tayari zimeshapokewa kwa shangwe kutokana na wananchi hao kuanza kulitumia. Ikumbukwe kwamba kutokuwapo kwa daraja hili kulileta usumbufu mkubwa kwa wananchi. Kabla ya uwapo wa daraja hili, magari yalilazimika kupita kwenye maji na pengine yanapokuwa mengi kushindwa kuvuka. 


Ni kutokana na daraja hili, shukrani za dhati ziende kwa JKT wanaojenga daraja hili, serikali Kuu kwa kupitia Mkuu wa Wilaya Kinondoni, DC Paulo Makonda na watendaji wote waliohakikisha kwamba utengenezaji wa daraja hili unakamilika ili kuondoa adha kwa wakazi na wananchi wa Mbweni JKT.


Mkazi mmoja wa Mbweni aliyeshindwa kutaja jina lake alitumia muda mwingi kuwasifu wahusika kwa kulisimamia vyema daraja hilo litakalokuwa mkombozi kwa wananchi wa eneo hilo na wote wanaoishi jijini Dar es Salaam.

Picha ya daraja hili la Mbweni JKT ilipigwa kwenye gari.

Kwaya ya Wakorintho wa pili kushiriki tamasha la shukrani

$
0
0
KWAYA  ya  Wakorintho  wa Pili ya Wilayani Mafinga mkoani Njombe, imekuwa ya kwanza  kuthibitisha kushiriki Tamasha la Kushukuru linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema uongozi wa kwaya hiyo umekubali kushiriki katika tamasha hilo baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 nchini kote.

“Kwaya  ya Wakorintho wa pili  wameanza kuthibitisha kushiriki tamasha la Shukrani baada ya kufanyika uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu, tunaendelea na maandalizi ya kufanikisha tamasha hilo ambalo litashirikisha idadi kubwa ya Watanzania,” alisema Msama. 

Aidha Msama alisema katika tamasha hilo, Kwaya hiyo itafanya uzinduzi  wa albamu yake ya Mchepuko sio dili yenye nyimbo nane.Nyimbo zilizoko kwenye albamu ya Mchepuko sio dili ni pamoja na Tanzania, Mchepuko sio dili, Watenda mabaya, Eee bwana, Tuokoe baba, Dunia hii, Yahwe Tunakuinua na Hana.  

“Kwaya  ya Wakorintho itafanya matukio mawili katika tamasha hilo, la kwanza ni kushiriki Tamasha la Kushukuru na la pili ni kuzindua albamu yenye nyimbo nane,” alisema Msama.

Mwisho  

YALE YALEEE.......

$
0
0
 Habari kaka Michuzi,
Naomba unifikishie katika blog yako maana naamini mpaka vyombo husika vitaliona hili.

Tarehe 16/11/2015 nilikua napita njia ya Kilwa,nilipofika mivinjeni nikakutana na hilo Gari la kubeba contena kama linavyoonekana katika picha,nikiwa nyuma yake likaingia Barabara ya vumbi iendayo bandarini kupitia Yara, nilimpigia sana honi na kumuwashia Taa huyo dereva asimame afanye taratibu za maksudi kunusuru uhai Wa RAIA wengine ila alikaidi,alishuka utingo wake akaangalia na kuendelea na safari, kiukweli lile kontena lilikua nje ya lock zake na lilikua likicheza sana kwenye njia ya vumbi na cha kushangaza kabisa lilipofika barabara ya bandari/shimo la udongo kulikua na traffic wanne barabarani lakini hawakuchukua hatua yoyote ile zaidi ya kuliangalia tu.

Tutaendelea kupoteza ndugu jamaa n marafiki zetu mpaka lini kwa uzembe Wa watu wachache wasiojali uhai wa wengine?

Wako Mdau.
 Lori hilo likikata kona kutokea barabara kubwa kuelekea bandarini kupitia Yara.

Maana ya jina la Dudumizi na uhalisia wake kwenye IT

$
0
0
Neno Dudumizi si geni katika masikio ya watu wengi. Hapa kwetu Tanzania, Dudumizi inamaanisha ni ndege, ndege huyu mwenye rangi ya ugoro na nyeusi akiwa na macho mekundu ni adimu sana hasa kwa watu wanaoishi mijini, hii inaweza kutokana na uchache wake au mazoea ya ndege huyu. Pia, kwa upande wa pili, neno Dudumizi ni kampuni bora inayojishughulisha na masuala ya huduma za IT kama kutengeneza websitekutengeneza systems za kompyuta na application za simu.

Watu wengi wanaposikia jina Dudumizi kama kampuni, kitu cha kwanza ni mshituko unaoambatana na swali moja, Kwanini tumeamua kuiita kampuni yetu Dudumizi? Kwa wengi, neno Dudumizi bado si neno rafiki huku likihusishwa na mambo mengi sana ambayo si mazuri, na mengi ni imani na si uhalisia, ila kwa upande wa mazuri, Dudumizi ana mengi sana ya kuyachukua kwenye IT.

Hebu tuangalie sifa za ndege huyu anayeitwa Dudumizi. Ndege jamii ya Dudumizi ana sifa kubwa tatu.
1. Dudumizi huwa na mlio tofauti unaoashiria kuwepo kwa uwezekano wa kunyesha mvua.

2. Kiota cha Dudumizi hakijafungwa, na mara nyingi huwa kwenye pachipachi ya mti, hii humrahisishia Dudumizi kukipanua kadri awezavyo bila kuvunja au kuhama, tofauti sana na ndege wengine ambao viota vyao vimefungwa na kutotoa mwanya wa upanuaji.
3. Kiota cha Dudumizi kimejazwajazwa majani na mara nyingi unaweza kudhani ni mrundikano wa majani na siyo kiota, pia kwakuwa kipo wazi, Dudumizi huweza kumuona mvamizi au adui tangu akiwa mbali,hivyo humsaidia kujikinga na wavamizi.

Hizo ndizo sifa kuu za ndege Dudumizi, je sifa hizi zina uhusiano gani na IT. 

1. Ubunifu na uvumbuzi (Innovation): Kwenye IT kuna kitu tunaita Ubunifu wa utendaji au uvumbuzi (Innovation), uvumbuzi huja baada na kufikiria halafu kutenda, kwenye kitabu chake cha Anza na kwanini (Start with Why), mwandishi Simon Sinek amesema, huduma au bidhaa haiwezi kuwa na ubunifu kama huduma hiyo haijaweza kubadili mfumo wa ufanyaji kazi. Mfano mzuri, ni jinsi gani kampuni ya Apple ilivyoweza kubadili matumizi ya simu kutoka button nyingi hadi moja. Na ubinifu husukumwa na mahitaji ya sasa au ya kesho.
 Kama Dudumizi anavyoweza kubashiri ujio wa mvua na kujiandaa, na sisi kwenye IT tunatakiwa kuwekeza kwenye ubinifu na kuja na huduma zinazokidhi mahitaji ya Mtanzania kwa wakati wote (leo na kesho). Na hii ndiyo sababuDudumizi tumeanza kuja na bidhaa zenye kulenga kubadili mtindo wa ufanyaji kazi, Michongo ni moja ya bidhaa yetu ya kwanza kwenye mlengo huu.
 

2. Ukuaji (Scalability): Dunia ya leo si dunia iliyo simama wala kujitosheleza. IT ikiwa muongozaji mkuu wa ufanyaji kazi, ni lazima iwe na uwezo wa kukua na kupanuka kulingana na uhitaji(scalability). Chukulia mfano leo hii umeamua kutengeneza System inayokuwezesha kurekodi maudhurio ya wafanyakazi, kwa sasa una wafanyakazi mia moja tuu, je hali inakuwaje endapo kampuni imekua na sasa inahitaji kuwa na huduma nyingi zaidi na sasa kuna wafanyakazi laki moja?? Je unatakiwa kuanza upya au kuendeleza ulicho nacho??
Tumekuwa tukiona watu wengi wakuchajiwa pesa zaidi na zaidi sawa na kuanza upya pindi wanapotaka kuongeza kitu fulani kwenye website au system. Na mara nyingi hii hutokea pindi unapotaka kuongeza uwezo wa system (feature), mkataba unasemaje kuhusu ukuaji?? Je ulijiandaa kwa hili?
 Dudumizi hujiandaa kwa kuwa na kiota kilicho tayari kupanuka, na kwa mtindo wa ujengaji wa Dudumizi, hata kama ataamua kuhama basi hasumbuki kuanza upya kutafuta zana, tayari anazo na zinamuwezesha kukua atakavyo. 
3. Usalama (Security): Katika maisha ya binadamu, usalama ni kitu cha lazima, na usalama huu siyo tu wa maisha pekee, bali na kila kitu kinachomzunguka au anavyovihodhi binadamu huyu. IT ni moja ya vitu muhimu kwa binadamu wa dunia ya leo. Usalama wa kiota cha Dudumizi unafanana na umuhimu wa usalama kwenye fani ya IT. Iwe ni kwenye Website, kwenye System au hata kwenye vifaa vya kieletronics. Kote tunakutana na kaulimbiu,"Usalama kwanza".
 

Kutokana na sababu hizo, sisi tukiwa kampuni ya IT, tena ya Kitanzania, ndiyo maana tumeamua kijiita Dudumizi. Na ufanyaji wetu wa kazi unaendana na mfumo kamili ya maisha ya Dudumizi. Hivyo, unapofanya kazi na Dudumizi, unakuwa na uhakika wa Ubunifu, Ukuaji na Usalama kama kauli mbiu yetu inavyosema, Fikiri. Gundua(Think.Innovate).
Katika makala zijazo tutaelezea maana ya Logo ya Dudumizi na ni jinsi gani ilivyoweza kuingiza Ubunifu wa Kitanzania.

MAKALA YA SHERIA: MAMBO YA MSINGI KISHERIA KUHUSU UMILIKI WA ARDHI WA PAMOJA

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.

Ardhi  inaweza  kumilikiwa  na  mtu  zaidi  ya  mmoja. Inaweza  kuwa  nyumba  au  kiwanja.  Vyote  hivi  vinaweza  kumilikiwa  na  mtu  zaidi  ya  mmoja. Kumiliki ardhi  kwa  zaidi  ya  mtu  mmoja  sio  lazima  iwe  kwa  wanandoa. Inaweza  kuwa  ndugu ,  marafiki ,  kikundi  cha  watu kama  wafanyabiashara, wana  saccos, kikundi  cha  michezo  na  aina  yoyote  ya  kikundi  cha  kimaendeleo.  Umiliki  wa  ardhi  kwa  pamoja  unatofauti  na  umiliki  binafsi  yaani umiliki wa  mtu  mmoja  mmoja. Tutaona  tofauti  hizo   na  mambo  mengine  ya  msingi  kuhusu  umiliki  wa  pamoja.

1.AINA  ZA  UMILIKI  ARDHI.
Kwa  kuangalia  ardhi  katika  mrengo  wa  umiliki   tunaweza  kusema   kuwa  ardhi  humilikiwa  kwa  namna   mbili.  Kwanza  umiliki  wa  mtu  mmoja  mmoja   na  pili  umiliki  wa  pamoja.  Huu  ni  ule  niliosema  kuwa  ni  mtu  zaidi  ya  mmoja. 

Umiliki  binafsi  wa  ardhi  yaani  umiliki  wa mtu mmoja  mmoja   unatoa  haki  kwa  mmiliki  huyo   kuitumia  ardhi  bila  kuhitaji  ridhaa  ya  mtu  mwingine  yoyote. Anaweza  kuuza,  kuweka  rehani  kama  dhamana  ya  mkopo, kutoa  zawadi,  kupangisha  na  matumizi  mengine  yoyote  halali.  Atafanya  yote  haya  bila  kuhitaji ridhaa  ya  mtu  mwingine  yoyote.

Hii  ni  tofauti  na  umiliki  wa  ardhi   wa  pamoja.  Katika umiliki  wa  aina  hii   mtu  mmoja  hawezi  kuuza, kutoa  zawadi,  kuweka  rehani  kupangisha  au   kuruhusu  matumizi  ya  ardhi   kwa  namna yoyote ile  bila  ridhaa  ya  wengine.  Kama  ni  wawili  basi  ridhaa  itabidi  itokane  na  wawili  lakini  pia  kama  ni  kumi,  saba  ,  watano  au  zaidi  basi  ridhaa  yao  wote  itatakiwa  kabla  ya  kufanyika  kwa  muamala  wowote ule.

Changamoto za Pamba Kupatiwa Ufumbuzi

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana Zidikheri Mundeme amewataka wadau wa zao la pamba kuwalinda wakulima wadogo wa zao hilo kwa kuwapatia mbegu bora na madawa sahihi ili kuboresha zao hilo.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa zao hilo kutoka Kenya, Brazili na vituo mbalimbali vya utafiti vya hapa nchini uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya White sand hivi karibuni,Bwana Mundeme amesema kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa nguvu za ziada zinahitajika katika kumsaidia mkulima mdogo wa pamba hapa Tanzania.

"Kilimo cha mkataba,ukosefu wa soko na uongezaji wa thamani na kipato kidogo cha wakulima wa zao hilo ni baadhi ya changamoto zinazomkabili mkulima mdogo wa pamba ambapo mkutano huu unatakiwa kuzitafutia utatuzi changamoto hizo" aliongeza Bwana Mundeme.

Aidha amevipongeza vituo vya utafiti vya Kanda ya Ziwa kikiwemo kituo cha utafiti Ukiriguru ambacho kilitafiti mbegu mpya ya pamba aina ya UKM 08 ambayo imekuwa ikifanya vizuri sana kwa wakulima.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana Zidikheri Mundeme akihutubia wadau wa pamba (hawapo pichani) hivi karibuni katika ukumbi wa hoteli ya whatesand ilioko Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana Zidikheri Mundeme akisalimiana na wadu wa pamba baada ya kumaliza hotuba yake ilyohusu mikakati ya kuimarisha kilimo cha pamba hapa nchini.

Airtel yafungua duka jipya mjini Moshi

$
0
0
Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Airtel  leo imefungua duka jipya na la kisasa  mjini Moshi lililopo katika mtaa wa Soko Kuu. Uzinduzi wa duka hili linadhihirisha ahadi yake kwa Airtel kujali wateja wake Tanzania nzima na kuwapa huduma iliyobora na ya kiwango cha juu popote pale walipo.

Hii ni sehemu ya mpango wa kampuni hiyo kuhakikisha wanatoa na kuboresha  mpango wake wa huduma kwa wateja wake  ili kuongeza urahisi wa kuwafikia wateja wake mbalimbali popote pale walipo nchi nzima.

Akizungumza katika sherehe fupi ya ufunguzi wa duka hilo,mkurugenzi  wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel, Bi Adriana Lyamba, alisema kuwa ufunguzi wa duka hili jipya na la kisasa mjini Moshi ni mwendelezo wa malengo ya Airtel kuendeleza  kuboresha maisha morani kwa kila mtanzania kwa kupata huduma zenye zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote walipo.

"Tunafuraha kubwa sana kuona tunafanikiwa kuwafikia wateja wetu na kufungua milango kwa wateja zaidi mjini Moshi na kuwahakikishia kuwa    tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea huduma  karibu na wananchi, na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia , "alisema Lyamba

Duka hili jipya  lenye mazingira mazuri kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Airtel ikiwemo huduma za modem, Airtel Money, simu mpya za kisasa za smartphone, huduma zetu za intanet na huduma ya malipo ya bili za awali na mwezi .

               
Bi, Evelyne Zakaria ambae ni Afisa tarafa wa Moshi Mashariki kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga aliwashukuru Airtel kwa dhamira yake ya  uboreshaji wa huduma kwa wakazi wa mji wa Moshi. Pia alibainisha kuwa mawasiliano ni jukumu kubwa katika kuunganisha watu na biashara ya kuendesha maendeleo katika Kata ya Moshi.

Mkuu wa Wilaya aliyaomba makampuni mengine ya simu yajitokeze zaidi na kuiga mfano wa Airtel  katika kutoa huduma bora kwa wakazi wa mji wa Moshi akisema kuwa ofisi yake iko tayari kwa kutoa ushirikiano kwa lengo la kufanya maisha bora kwa wakazi wake.
Toka kushoto ni Meneja wa mamlaka ya mawasiliano kanda ya kaskazini (TCRA) Eng, Annette Mahimbo Matindi na Afisa tarafa wa Moshi Mashariki bi Evelyne Zakaria (kati) wakiwa na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi, Adriana Lyamba wakishirikiana kukata utepe wakati Airtel ikizindua duka jipya mkoani Kilimanjaro mtaa wa Mandela jana. Kulia wakwanzani akishudia ni Meneja wa Biashara wa Airtel kanda ya kaskazini bw Brighton Majwala.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Bi. Adriana Lyamba akijadiliana jambo na Meneja wa tawi la Biashara la Airtel Mkoa Kilimanjaro, Bw. Paschal Bikomagu (kushoto) na msimamizi wa maduka hayo bw, Thomas Chalamila mara baada ya Airtel kuzindua duka la kisasa moshi mtaa wa mandela jana au soko kuu.
Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa Artel, Bi. Adriana Lyamba akimuhudumia Mteja aliefika kwenye duka hilo, Bw. Ally Janja ambae ni Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Kilimanjaro na pia mmoja kati ya wateja maalum wa Airtel wakiwa katika duka jipya la Airtel Moshi lenye kona maalum kwa wateja hao (Airtel Premium) mara baada ya duka hilo jipya na lakisasa kufunguliwa jana na Airtel mkoani Kilimanjaro.
Picha ya pamoja.

Bilioni Mbili kutengwa kwa ajili ya kusaidia utafiti wa zao la Korosho

$
0
0
 Na Lorietha Laurence-Maelezo

Bodi ya Korosho Tanzania imeadhima kutoa asilimia 7 ya mapato yake sawa na shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kusaidia utafiti wa zao hilo unaofanywa na kituo cha utafiti cha Naliendele.

Akiongea wakati wa kufunga kwa mkutano wa tatu wa kimataifa uliowahusisha wadau kutoka nchi mbalimbli duniani ,Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Bw. Muhidhiri Muhidhiri amesema kuwa changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya kuendeshea utafiti wa zao la korosho unaofanywa na kituo cha Naliendele na hivyo wamejipanga kwa kuchangia kiasi cha mapoto ili kufanikisha tafiti hizo .

Muhidhiri aliongeza kuwa licha ya changamoto za ukosefu wa fedha wamepata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kupitia mkutano huo ikiwemo maadhimio ya uzalishaji bora wa zao hilo, namna ya kutatua matatizo ya magonjwa yanayoikumba korosho,dawa asilia zitakazosaidia katika kulinda mbegu, na njia bora ya uzalishaji.

“Mkutano ulikuwa wa kisayansi kwa kuwa umeangalia mambo ya kiutafiti na teknolojia katika uzalishaji wa zao la korosho hivyo ninaamini baada ya hapa ni kuanza utekelezaji wa yale tuliyoyajadili na kufanya vizuri zaidi ” alisema Muhidhiri.



Kwa upande wa Mtafiti Mkuu wa Masuala ya korosho Prof.Peter Masawe ameeleza kuwa mkutano huo wa wadau umewapa fursa ya kufahamu mambo mazuri katika uboreshaji na uzalishaji wa zao la korosho katika kiwango kizuri na kilicho bora .

Pia alibainisha kuwaTanzania ndiyo nchi yenye mtafiti anayetegemewa katika masuala ya korosho na hivyo kupitia mkutano huo wadau wamepata fursa ya kufahamu mambo ya msingi kama vile mbegu bora zinazozalishwa nchini ,mbegu fupi, mbegu zinazostahimili ukame pamoja na kukopa teknolojia ya uzalishaji.

“Mkutano huu umetoa fursa kwa wadau kujua mambo muhimu kuhusu mbegu ukizingatia Tanzania ndiyo nchi pekee barani Afrika inayozalisha mbegu bora hivyo natumai wajumbe wataenda kutendea kazi yale yote waliyojifunza hapa kwetu na nasisi pia tutayafaniya kazi yale tuliyoyapata kutoka kwao ” alisema Prof Masawe.

Mkutano huo wa kimatifa wa wadau wa Korosho umefanyika kwa mara ya pili nchini ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1997 na hivyo kuipa fursa nchi ya kujitangaza kupitia sekta ya kitalii kwa kuwahamasisha wadau waliohudhuria mkutano huo kutembelea sehemu za vivutio ikiwemo Bagamoyo na Zanzibar.

Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya nje akutana kwa mazungumzo na wageni mbalimbali waliotembelea Wizarani

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Maalum wa Serikali ya China katika masuala ya Afrika, Balozi Zhong Jianhua alipotembelea Wizarani tarehe 17 Novemba, 2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Samuel Shelukindo kwa pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Medard Ngaiza wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Zhong Jianhua (hawapo pichani)
Maafisa waliofuatana na Balozi Zhong Jianhua (hayupo pichani) nao wakifuatilia mazungumzo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TANESCO YAAGIZWA KUIMARISHA KIKOSI CHA UKAGUZI WA WATUMIAJI WA UMEME

$
0
0
Na Jovina Bujulu- Maelezo
DAR ES SALAAM
18/11/2015
Mabadiliko ya Tabia Nchi, uharibifu wa vyanzo vya maji katika mito mbalimbali na uchepushaji wa maji kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji ni chanzo cha kukauka kwa mabwawa ya maji yanayotumika katika kuzalisha umeme.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Bi. Badra Masoud alipokuwa akizungumzia ukaguzi wa wezi wa umeme nchini.

“Umeme unaotumika kwa sasa unazalishwa kwa kiasi kikubwa na gesi asilia pamoja na mafuta mazito na diseli ambapo umeme unaotokana na nguvu ya maji unazalishwa kwa kiasi kidogo” alisema Bi Badra.

Akizungumzia hali ya umeme nchini, Badra alisema kwamba kwa sasa hakuna mgawo wowote unaoendelea kwani uzalishaji ni mzuri, kiasi cha umeme kinachopatikana sasa ni megawati 1500 wakati matumizi kwa siku ni megawati kati ya 800 na 900.

Aidha Bi. Badra alisema kwamba Wizara ya Nishati na Madini inatarajia kuunda kikosi maalumu kitakachojumuisha wataalamu kutoka katika taasisi mbalimbali kukabiliana na wizi wa umeme nchini.

“Wizi wa umeme nchini ni jambo linalolikosesha mapato shirika la Tanesco, hivyo kikosi hicho kitajumuisha wataalamu kutoka TANESCO, Wizara ya Nishati na Madini pamoja na vyombo vya usalama” alifafanua Bi Badra.

Pia Wizara imewataharisha baadhi ya watu wanaohujumu miundombinu ya TANESCO kama kuchoma nguzo za umeme, kuiba mafuta ya transforma pamoja na nyaya za umeme na watakaogundulika watachukuliwa hatua za kisheria,

Hata hivyo Shirika la umeme Tanzania TANESCO limeagizwa kuimarisha kikosi chake cha ukaguzi wa watumiaji wa umeme ili kubaini wateja wasio waaminifu wanaoiba umeme wa majumbani na viwandani na kuwachukulia hatua za kisheria.


Katika kuhimiza matumizi bora ya umeme Wizara ya Nishati na Madini imezitaka taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali kuzingatia matumizi mazuri ya Nishati hiyo ili kudhibiti upotevu wa umeme.

BEI YA MADAFU LEO

Wataalamu wa Gesi wametakiwa kujifunza kwa Mkandarasi

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia) akimsikiliza Meneja wa Kampuni ya GASCO, Mhandisi Mhandisi Kapuulya Musomba (katikati). Wa Kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Paul Masanja.
Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba
Baadhi ya mitambo kwenye Kituo cha kuchakata Gesi Asilia cha Madimba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kushoto) na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja mara baada ya kukagua Kituo cha Kuchakata Gesi asilia cha Madimba.

Wataalamu wa Kitanzania wanaofanya kazi kweye Mradi Mkubwa wa Gesi Asilia nchini wametakiwa kuhakikisha wanajifunza kwa ukamilifu shughuli zote za mradi huo kabla mkandarasi hajaondoka.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Omar Chambo na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja walipofanya ziara kwenye mradi huo kwa lengo la kukagua maendeleo ya mradi pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa mradi huo.

Kujengwa kwenye hifadhi ya Bahari Golden Tulip kwazua maswali ya sheria ya mita 60

$
0
0
Kumekuwa na sheria na kanuni mbalimbali zinazoundwa, ingawa wakati mwingine hushindwa kutekelezeka kwa wakati. Ukifika katika hoteli ya Golden Tulip utakuta jinsi eneo hilo linavyozidi kujengwa na kuendelezwa kama lilivyokutwa na mpiga picha wetu. Kujengwa kwa eneo hili lililokuwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi ni kinyume cha sheria ya Hifadhi ya Bahari. Tumeshuhudia maeneo mengi yakivunjwa kwa nyumba zao baada ya kubainika yamejengwa katika hifadhi ya bahari. Haijafahamikaa mara moja kama eneo hili limeruhusiwa kuendelezwa, ikiwa ni tofauti na jengo la Hoteli ya Golden Tulip
Sheria za Hifadhi ya bahari inasema ni marufuku kujenga nyumba mita 60 ilipokuwa bahari. Hali hii imeonekana kuwa tofauti baada ya kukuta hifadhi hii ikionekana kuanza kujengwa na kuanza kuzua maswali mengi kwa wadau wa maendeleo na Waanzania kwa ujumla wanaofuatilia mambo ya maliasili na utalii. Kibao hiki kinaonyesha jinsi eneo hilo lilivyotengwa kwa ajili ya kujenga jambo ambalo ni kinyume cha sheria za mita 60 za bahari.
Gari likipita katika barabara inayoelekea katika barabara ya Golden Tulip Hoteli, ambayo pia inaonekana eneo hilo lililowekwa mabati kwa ajili ya kuanza kulijenga kama lilivyokutwa na mpiga picha wetu. na chini mkazi wa jiji la Dar es Salaam akipita katika eneo hilo, huku ikionekana ramani mbalimbali za ujenzi huo.

BOMOA BOMOA YATIKISA MANISPAA YA KINONDONI JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Baadhi ya Nyumba zikibomolewa mapema leo mchana mtaa Bwawani Manispaa ya Kinondoni,ambapo zoezi hilo linafanyika maeneo mbalimbali katika Manispaa hiyo. Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, imekusudia kuanza kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi. 
 Askari wa jeshi la Polisi wakisimamaia suala la usalama mtaa wa Bwawani wakati wa bomoa bomoa ikiendelea katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar mapema leo.
Baadhi ya wakaazi wa mtaa Bwawani Manispaa ya Kinondoni wakishuhudia bomoa bomoa inayofanyika leo katika manispaa hiyo maeneo mbali mbali ambapo Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.
 Askari wa jeshi la Polisi wakisimamaia suala la usalama mtaa wa Bwawani wakati wa bomoa bomoa ikiendelea katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar mapema leo.
 Moja ya Nyumba iliyojengwa eneo la wazi katika mtaa wa Bwawani ikibomolewa 
 Askari jeshi la polisi wakihakikisha suala la usalama katika tukio hilo
 Ubomoaji wa nyumba ukiendelea eneo la Manispaa ya Kinondoni

TAARIFA ILIYOTOLEWA JANA KUHUSIANA NA UBOMOAJI WA NYUMBA MANISPAA YA KINONDONI

Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.

 Maeneo yaliyotengwa mijini kwa matumizi ya umma ikiwa ni pamoja na maeneo ya wazi, njia za miundombinu na huduma nyinginezo za umma, mara kwa mara hutumiwa vibaya au kuvamiwa na waendelezaji binafsi hivyo kuukosesha umma manufaa yaliyokusudiwa.

Tamko Na. 6.6.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
i. Serikali itahakikisha kwamba maeneo yote mijini yaliyotengwa kwa shughuli za umma yanatumika kwa shughuli zilizokusudiwa na yanalindwa ili yasivamiwe.
Tamko Na. 8.2.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:

ii. Serikali za mitaa zitawajibika kushirikiana na Wizara ya Ardhi kuhakikisha usimamizi mzuri wa ardhi katika maeneo yao.

Sera ya Taifa ya Ardhi imebainisha sababu inayopelekea Wizara kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kuendesha zoezi hili la ubomoaji.

Ubomoaji huu utahusisha nyumba zote zilizojengwa
  a)     Bila kibali cha ujenzi
  b)     Bila kufuata michoro ya mipango miji
  c)      Bila kufuata matumizi ya ardhi (maeneo ya wazi)
Zoezi hili la ubomoaji litaendeshwa na Manispaa ya kinondoni na Wizara ya Ardhi itasimamia sera za ardhi na taratibu za uendelezaji kuhakikisha zinafuatwa na kila mmiliki wa ardhi.

Maeneo ambayo ujenzi wake umekiuka matumizi kusudiwa na yatahusika na ubomoaji huu ni  Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni – Biafra. Kazi hii inatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia jumatano tarehe 18/11/2015 hadi ijumaa tarehe 20/11/2015.

UTURUKI KUIPIGA TAFU MAKUMBUSHO YA TAIFA

$
0
0
Na Sixmund J. Begashe.

Nchi ya Uturuki ipo tayari kuisaidia Makumbusho ya Taifa katika nyanja za Utafiti, Uhifadhi, Maonesho ya vioneshwa vya kimakumbusho na hata katika Maonesho mbali mbali ya muziki na sanaa ili kuboresha na kuendeleza shughuli mbali mbali zinazo fanywa na Makumbusho ya Taifa hapa nchini.

Ahadi hii imetolewa na Balozi wa Uturuki hapa Nchini Mh Yasemin ERALP alipo kutana na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa kwa lengo la kubadilishana mawazo ili kuona ni kwa namna gani Ubalozi wake unaweza kushirikiana na Makumbusho ya Taifa.

Akiongea na Uwongozi huo wa juu wa Makumbusho nchini, Balozi ERALP alisema kuwa, Makumbusho ya Taifa ni sehemu muhimu sana kwa utafiti, uhifadhi, uelimishaji na ustawi wa historia ya nchi yeyote ile husika, hivyo kwa Makumbusho ya Taifa la Tanzania haina budu kusaidiwa ili iweze kutimiza malengo hayo makuu kwa maslai ya watanzania na Dunia kwa ujuma.

Balozi ERALP aliongeza kuwa Ofisi yake, itaiunganisha makumbusho ya Taifa na Makumbusho mbali mbali za nchini Uturuki ili kutoa nafasi za wataalam wa Makumbusho zote kukutana na kubadilishana uzoefu wa kitaalam, na kuahidi kuleta wasanii kutoka Uturuki ili kufanya maonesho katika ukimbi wa kisasa wa maonesho uliopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

Balozi huyo alipata nafasi ya kutembelea jengo la Makumbusho ya kwanzaTanzania la King George V lililopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam na kujionea namna jengo hilo linavyo hitaji ukarabati wa haraka, aliahidi kuwasiliana na Makampuni ya ujenzi ya Uturuki yaliyopo hapa nchini ili kusaidia ukarabati wa jengo hilo.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho nchini, Prof Audax Mabula amemshukuru balozi huyo kwa kuitembelea Makumbusho ya Taifa na kuonesha nia ya dhati ya kushirikiana na Makumbusho hiyo, pia ametoa wito kwa wadau mbali mbali wa ndani na nje ya nchi kushirikiana na Makumbusho ya Taifa ili kuboresha uhifadhi wa vyote vinavyo dhaminiwa na jamii ya hapa nchini.
Balozi wa Uturuki nchini Mh Yasemin ERALP akiwa kwenye ukumbi wa Mila na Destuuri, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam. Nyuma kusho ni Mkurugenzi wa Makumbusho hiyo Bw Achiles Bufure.
Balozi wa Uturuki nchini Mh Yasemin ERALP akiwa kwenye ukumbi wa Mila na Destuuri, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Pichani kushoto ni Balozi ERALP akisikiliza ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula, katikati ni Mkuu wa Idara ya Program Bw;Chance Ezekiel.
Pichani katikati ni Balozi wa Uturuki nchini Mh Yasemin ERALP akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Makumbusho ya Taifa.

BENKI YA NBC YATOA SOMO KUHUSU HUDUMA ZA ISLAMIC BANKING KWA WATEJA MKOANI MWANZA

$
0
0
Meneja Uendelezaji Biashara wa Benki ya NBC, Eddie Mhina (kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika semina waliyowaandalia kuhusu bidhaa mbalimbali zinazopatikana kupitia huduma hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Mwanza hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu (Islamic Banking) za Benki ya NBC, Yassir Masoud (kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika semina waliyowaandalia kuhusu bidhaa mbalimbali zinazopatikana kupitia huduma hiyo.
Meneja Uendeleza Biashara wa Benki ya NBC, Eddie Mhina (kushoto), akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika semina waliyowaandalia kuhusu bidhaa mbalimbali zinazopatikana kupitia huduma hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina kuhusu huduma za kibenki zinazofuata misingi ya kiislamu za benki ya NBC iliyofanyika mjini Mwanza hivi karibuni.

Stanslaus Mabula alitaka Tamasha la Kushukuru

$
0
0
MBUNGE  wa Nyamagana Stanslaus Mabula ameiomba Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Kushukuru linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, lihamie jijini Mwanza kwa lengo la kufikisha shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25. 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex Msama wanayafanyia kazi mapendekezo ya Mabula ili kufanikisha tamasha hilo adhimu lenye nia ya kushukuru Mungu baada ya uchaguzi Mkuu.Msama alisema tamasha hilo litashirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa Injili ambao watawasilisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani na utulivu. 

Msama alisema Kamati yake inajipanga kufikisha ujumbe wa Shukrani kwa Mungu kupitia viongozi wa dini wakiwemo maaskofu na wachungaji wa makanisa mbalimbali hapa nchini.

“Tamasha la Kushukuru Mungu lina mtazamo wa kufikisha asante kwa Mungu baada ya kuendelea kudumisha tunu ya amani ambayo ndio sifa ya Tanzania nje ya mipaka,” alisema Msama.


Aidha Msama alitoa wito kwa Wadhamini na wafadhili kujitokeza kwa lengo la kusaidia tamasha hilo.

LIVE KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO: WABUNGE WALIPIGIA KURA JINA LA WAZIRI MKUU MKUU MTEULE

$
0
0
Baadhi ya Maafisa wa Bunge wakiwa tayari kwa Zoezi la kupiga kura, wabunge kumthibitisha Waziri Mkuu aliyependekezwa na Rais Dk. John Magufuli, Mhe. Kassim Majaliwa, linaloendelea hivi sasa Bungeni Mjini Dodoma.
Zoezi la kupiga kura likiendelea kwa Wabunge Mjini Dodoma.

Vodacom Foundation yatoa msaada wa vifaa vya elimu Kisarawe

$
0
0
Wanafunzi wa shule ya msingi Chazinge A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani wamenufaika kwa kupatiwa msaada wa vifaa vya elimu kutoka taasisi ya kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom Foundation.Vifaa hivyo ambavyo vimetolewa jana ni madaftari ya kuandikia na mikebe yenye vifaa vya kusomea somo la hisabati (Mathematics set)pamoja na kalamu.

Akiongea wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa hivyo kwa wanafunzi jana,Kaimu Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia alisema elimu ni moja ya kipaumbele ambacho taasisi hiyo inatoa na vipaumbele vingine vikiwa ni kusaidia kuboresha sekta ya afya.

“Vodacom Foundation tunaelewa kuwa elimu ni ufunguo wa maisha na hakuna jamii ambayo inaweza kuendelea bila kutoa elimu kwa watu wake ndio maana tumekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha sekta ya elimu nchini”.Alisema Mworia.

Alisema kuwa taasisi ya Vodacom Foundation pia inaendelea kutekeleza mkakati wake wa kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hususani zile zinazomilikiwa na serikali wanapatiwa kompyuta za kuwawezesha kusoma somo hili kwa vitendo ili wasiachwe nyuma katika karne hii ya sayansi na teknolojia.

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake baada ya kupokea msaada huo mwanafunzi Aisha Salum anayesoma darasa la nne shuleni hapo alitoa shukrani kwa msaada huo “Tunashukuru Vodacom Foundation kwa kutupatia vifaa na tuna imani vitatusaidia katika masomo yetu.
Mwanafunzi wa darasa la sita Jonson Khamsini (wa pili toka kushoto) wa shule ya Msingi Chazige A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani akipokea vifaa vya elimu-madaftari,Mikebe yenye vifaa vya kusomea somo la hisabati (Mathematics set) pamoja na kalamu toka kwa Kaimu Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia(kulia) ikiwa ni msaada ulitolewa na kampuni hiyo kupitia taasisi ya kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom Foundation hivi karibuni.
Meneja Biashara wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha Vodacom Tanzania, Grace Lyon (kulia) akiwagawia vifaa vya elimu wanafunzi wa shule ya Msingi Chazige A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani, vifaa walivyokabidhiwa ni,madaftari,kalamu,Mikebe yenye vifaa vya kusomea somo la hisabati (Mathematics set) ikiwa ni msaada uliotolewa na kampuni hiyo kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom Foundation hivi karibuni.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Chazige A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani,wakifurahia na kuviinua juu vifaa vyao vya elimu, Vikiwemo,madaftari,kalamu,Mikebe yenye vifaa vya kusomea somo la hisabati (Mathematics set) ikiwa ni msaada uliotolewa na Vodacom Tanzania kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom Foundation hivi karibuni.

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live


Latest Images