Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA KUSITISHWA KWA HUDUMA YA MRI KWA MUDA NA MATENGENEZO YA CT-SCAN


BENKI YA BERCLAYS YAWATANGAZA WASHINDI WA AKAUNTI YA MSHAHARA.

$
0
0
BANKI ya Barclays imewazawadia washindi wa droo ya akanti ya mshahara ambayo imechezeshwa mwezi Oktoba mwaka huu ikiwa wamepata washindi watatu ambapo mshindi wa kwanza amepata 100% ya mshahara wake wa kila mwezi, mshindi wa pili amepata 75%  na watatu  50%  ya mshahara wake anaoweka katika akaunti ya benki hiyo.

Washindi hao ni Massoud Ramadhan Lupeja wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, Nuran Hatibu Hemed wa  na  Moses Mofati Chilongo.

Hayo yamesemwa na  Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa  alipokuwa akitangaza washindi wa tatu wa benki hiyo waliojishindia baadhi ya asilimia za akaunti  za mishahara yao.

  Aidha amesema kuwa promosheni ya droo ya mshahara inaendelea kuchezeshwa kwa wenye akaunti za zamani pamoja na watakao fungua akaunti mpya katika benki hiyo.

Kwa upande wake mshindi wa droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam amesema kuwa "Nimefurahi sana kushinda kwa kiwango cha juu pia itasaidia kutatua baadhi ya matatizo yangu."





 Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa akizungumza katika hafla fupi ya kumkabidhi mshindi wa Droo ya akaunti ya kuweka mshahara wa kila mwezi ambayo inaendelea kuchezwa katika benki hiyo hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa  kitengo cha wateja binafsi wa benki ya Baclyas, Kumaran Pather  na kutoka kulia ni Meneja wa Bidhaa wa benki ya Baclyas, Walence Luteganya na Kaimu mkuu wa kitengo cha masoko wa benki ya Baclyas, Joe Bendera.
Mkurugenzi wa  kitengo cha wateja binafsi wa benki ya Baclyas, Kumaran Pather akimkabidhi msindi wa droo ya akaunti ya kuweka Mshahara katika benki ya Baclyas  ambapo mshindi Massoud Lupeja ambaye amejishindia asilimia 100 ya mshahara wake katika benki hiyo. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika hafla hiyo ya kumkabidhi mshindi  hundi aliyojishindia, iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Breaking Nyuzzzzzz: Muhimbili yatangaza kusitishwa kwa huduma za MRI kwa muda

WATANO WAOKOLEWA KATIKA MGODI WA NYANGARATA KAHAMA.

$
0
0
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
WATU watano wamepatikana wakiwa hai tangu Oktoba 5 mwaka huu walipofukiwa na kifusi cha mchanga katika mgodi wa wachimba wadogo wa mgodi wa Nyangarata wilaya ya Kahama  mkoani Shinyanga, watu hao waligundulika kuwepo ndani ya mgodi hou mita 100 kwenda chini ikiwa mtu mmoja amegundurika kuwa amefariki dunia.

Waliookolewa katika  mgodi huo kuwa ni Josef Burule, Chacha Wambura, Msafiri Gerald, Onyiwa Aindo na Amosi Mhangwa pia limtaja aliyefariki dunia ni Mussa Supana.

Hayo yamesemwa na Afisa habari wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Massoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. 

amesema kuwa watu hao wamekaa chini ya ardhi kwa zaidi ya siku 40 ambapo mgodi huo ulianza kudidimia kwenda chini, Oktoba 5 mwaka huu mpaka Novemba  15 ambapo waokoaji kutioka Wizara ya Nishati na Madini walianza kuwatafuta ndipo jana wakafanyikiwa kuwatoa wakiwa na hali mbaya na kukimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Pia amesema kuwa walipokuwa chini huko wakuwa wanakula magome ya miti pamoja na maji walikuwa wanakinga  yaliyokua yakitililika kidogo na kukinga katika helementi zao ambazo walikuwa wamezivaa walipokuwa wanaingia katika mgodi huo.

Pia Badra alitoa wito kwa wachimbaji wadogo wa Madini kuwa wachimbe kwa kutumia vifaa vya kisasa ili kuepukana na madara yoyote yatakayo jitokeza katika uchimbaji wa madini.
 Afisa habari wa Wizara ya nishati na Madini, Badra Massoud akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO kuhusiana na watu waliopatikana wakiwa hai katika mgodi wa wachimbaji wadogo wa Nyangarata mkoanI Kahama.
Afisa habari wa Wizara ya nishati na Madini, Badra Massoud akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO Kulia ni Afisa habari wa Idara ya Habari MAELEZO, Jaiquline  Mrisho.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

MAKONDA AWAFUNDA WAOKAJI KEKI NCHINI

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa tatu kulia) na Mdau wa Keki, Mama Cynthia Henjewele (wa pili kushoto), wakikata keki maalumu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Watengeneza keki Tanzania (TCBA), uliofanyika katika Mgahawa wa City Lounge Posta mpya Dar es Salaam jana. Kulia ni Mshehereshaji, Makena na Mdau wa Keki, Philip Mbonde.

 DC Makonda akitoa hutuba ya uzinduzi.

 Mwanzilishi wa umoja huo, Stellah Rwabutaza (kushoto), akimlisha keki mgeni rasmi DC Makonda. Katikati ni mdau wa Keki Cynthia Henjewele.

Muokaji  keki,  Roselins Sia Adhero (kulia), akimkabidhi keki DC Makonda.

IDADI YA VIFO VYA WATOTO WACHANGA YAENDELEA KUPUNGUA MBEYA

$
0
0
Na Emanuel Madafa,Mbeya.

IDADI ya vifo vya watoto wachanga imeendelea kupungua Mkoani mbeya kutoka vifo 602 kwa mwaka 2012 hadi kufikia 568 kwa mwaka 2014  ambapo ni sawa na asilimia 5.7.


Hali hiyo inatokana timu ya uendeshaji wa huduma za afya mkoa kukaa pamoja na kutafuta ufumbuzi wa pamoja na kuweka maazimio ambayo wamekuwa wakiyatekeleza kwa pamoja.


Akizungumza jijini Mbeya mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mkoani humo Ndugu Prisca  Butuyuyu  amesema kutokana na usimamizi huo wameweza kufuatilia  mambo mbalimbali yakiwemo ya upatikanaji wa dawa.


Amesema hatua nyingine iliyofanikisha zoezi hilo ni pamoja na kushughulikia  mapungufu  na changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza katika vituo vya huduma.


Amesema  sanjali na mafanikio hayo pia wanatoa pongezi za dhati kwa shirika la UNICEF  kwa kuendelea kusaidia kutoa fedha za usimamizi  shirikishi katika eneo la huduma za afya na uzazi na mtoto.


Butuyuyu amesema kuwa baadhi ya halimashauri  zimeweza kuendesha semina  mbalimbali kuhusu uzazi salama ambazo ni huduma baada ya kujifungua  pamoja na huduma muhimu kwa watoto wachanga.


Hata hivyo  amesema shirika la UNICEF wakishirikiana na KOICA  wamekuja na mpango mwingine wa miaka 4 ya uboreshaji huduma za afya ya uzazi na mtoto.

 JAMIIMOJABLOG

TASO YAPATA VIONGOZI WAPYA WA TAIFA

$
0
0
Moja ya vyama muhimu katika kuleta mapinduzi ya Kilimo Nchini Tanzania ni Tanzania Agricultural Organisation (TASO). Pamoja na majukumu mengine, TASO ndio wamiliki na wasimamiaji wamaonyesho ya nanenane Nchini Tanzania. 

Hadi sasa TASO ina viwanja vitano vya maonyesho ya nanenane kwenye kanda za Kaskazini-Arusha, kandayalati –Dodoma, Mashariki – Morogoro, NyandazaJuu –Mbeya na Kanda ya Kusini – Lindi. Mfumo wa utendaji wa TASO umeanzia kwenye Kata, Wilaya, Mkoa, Kanda naTaifa. 

Juhudi zinafanyika kuanzisha viwanja vya maonyesho kwenye kanda ya Magharibi na kanda ya ziwa katika muda mfupi ujao. Tanzania ikiwa inatumia si zaidi ya asilia 25% ya Aridhi inayofaa kulimwa, Kilimo kinabakia kuwa msingi muhimu wa kukuza uchumi na ajira Nchini Tanzania. 

Pia izingatiwe kuwa Tanzania ina jumla asilimia 46% ya aridhi yote ya Afrika Mashariki hivyo kuwa na fursa kubwa ya kukuza soko na kulisha nchin yingine za Afrika Mashariki na nje.

Jumamosi yaTarehe 14 Novemba 2015 mjini Dodoma, TASO ilifanya uchaguzi wa viongozi wa Taifa ambao wataongoza taasisi hii muhimu katika kukuza kilimo kwa miaka 5. Viongozi waliochaguliwa ni Engelbert Moyo – Mwenyekiti, SharifaAbebe – Makamu Mwenyekiti, Imani Kajula – Katibu Mkuu, Daudi Mwalusyamba – Katibu Mkuu Msaidizi na Michael Lupyana – Mweka Hazina.

Akizungumza baada ya kuchaguliw aMwenyekiti wa TASO Taifa Engelbert Moyo alisema ‘’ Huu ni mwanzo mpya wenye malengo ya kuchochea mchango wa kilimo katika Uchumi, Maisha ya Watanzania, weredi katika kilimo na ajira. Ni fursa adhimu kuwa na viongozi waTaifa wenye ujuzi katika fani mbalimbali; Kilimo, Biashara, Masoko naFedha. Naamini kuwa TASO itapiga hatua kubwa katika kuwa muda muhimu katika kutoa mchango katika sekta hii nyeti’’.

Nae Katibu Mkuu wa TASO Imani Kajula alisema ‘’ Kilimo ni sekta yenye kuajiri watanzania wengi, lakini imekuwa na changamoto nyingi, tunatambua kazi hii tuliyopewa ni adhimu na muhimu katika kuleta mabadiliko ya kukuza soko la mazao, ubunifu watechnojia rahisi za kilimo, upatikanaji wa habariza kilimo, uvuvi, ufugaji na masoko kwa wakulima na pia kuboresha maonyesho ya Nanenane kuwa jukwaa la kuchochea ukuaji wa kilimo na ajira’’.

BONDIA MESHACK MWANKEMWA BINGWA MPYA WA KG 66 TPBC

$
0
0

Refarii wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini Kondo Nassoro kulia akimnyoosha mkono juu bondia Meshack Mwankemwa baada ya kumnyuka bondia Hamisi mwakinyo katikati ni Promota wa ngumi za kulipwa Jay Msangi akimvalisha mkanda bingwa huyo mpya wa Kg 66 anaetamuliwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC kulia ni Shomari Kimbau Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Meshack Mwankemwa kushoto akiwa na bondia Hamisi Mwakinyo na viongozi na kulia ni Shomari Kimbau wa pili kulia ni rais wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa na Jay Msangi.
Bondia Asha Nzowa 'Asha Ngedere' jkulia akipambana na Joyce Awino wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa CCM Mwijuma mwananyamala Dar es salaam mpambano uho ulimalizika kwa sare.

Refarii Kondo Nassoro katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Asha Nzowa kushoto na Joyce Awino baada ya kutoka droo.

KIPINDI CHA DANGA CHEE JUMA HILI: USO KWA USO NA ISHA MASHAUZI

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 16.11.2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

HEPI BETHDEI YA KUZALIWA MTOTO Nasria Salum Mgaya

$
0
0
 Mtoto Nasria Salum Mgaya akiwa kabebwa na baba yake. Katikati ni mama yake na kushoto ni mama yake mdogo Farashuu Tozzo.
 Nasria akiwa katika matukio tofauti pamoja na ma mdogo Farashuu,chini yake ni ma mdogo rehema,na kulia nasria akizima mshumaa.
 Nasria akifanya mpango wa kukata keki yake mwenyewe

Yoga na Mfumo wa “Endocrine Glands”

$
0
0
Na Sensei Rumadha Fundi, 
Yoga & Karate Instructor.



Mazoezi ya Yoga, hayawezi  lingalishwa na aina nyinginezo za mazoezi ya nguvu za misuli. Mbinu za kiundani zenye maigizo ya mikao ya wanyama tofauti, na kupitia mtililiko wa kuvuta pumzi, una imarisha sana nguvu mwilini kuringanisha na mazoezi ya aina yeyote ya nguvu na misuli ambayo mwisho wa zoezi mwili unakuwa umechoka, wakati yale ya Yoga, mwili unakuwa umejenga nguvu zaidi.

Kuna  dalli  nyingi za kupungukiwa na usawa wa kemikali ijulikanayo kama “Hormones” ndani ya damu  mwilini mwa mtu. Baadhi ya mapungufu ambayo hubainika mapema ni pamoja na:

ü  Kuumwa kichwa

ü  Matatizo ya ngozi, kuwashwa au kuwa na mapele madogo.

ü  Maumivu ya viungo

ü  Hali ya kutoweza pata  usingizi.

ü  Uchovu

ü  Kupungua kwa hamu ya unyumba au ngono.

ü  Wepesi wa kuwa na hasira

ü  Ongezeko la uzito mwilini.

ü  Kuzeeka haraka.


Mazoezi ya Yoga ya nauwezo wa kuzisisimua sehemu hizo za “Glands” na kuziamsha kwa kuweza kufanya kazi yake ya kusawazisha na kumiliki usawa wa“Hormones” mwilini.

Mfumo mzima wa “ Endocrine” ni kama ufuatavyo:

The Glands ni  sehemu ya mwili kama kifuko mnamo fanyizwa maji  yenye dawa  yaingiayo damu  au damuni na kufanya  kazi nyinginezo mwilini kwa mizani na makadilio sahihi. Endapo kazi yake itakuwa imevuka au kushuka, pia huleta madhara mwilini na matokea yake ni kuwa na baadhi ya hizo tabia zilizoelezwa hapo juu awali. Kemikali inayo chakachuliwa na hizo Glands,  inajulikana kama “Hormones”. Hizi “Hormones” zina ushawishi mkubwa katika maisha ya mwanaadam, ikiwemo; makuzi ya mwili, kusaga na kuyeyusha chakula, nguvu za mwili, isitoshe na  joto la mwili, ngono, kuhifadhi au kuweka maji  mwilini. Hivyo, zifuatazo hapa ni kazi na majukumu ya kila moja ya “Gland” na madhara yake isipofanya kazi inavyostahili.

1.      Pineal Gland

Hii imekaa ipo katikati ya ubongo wa mwanaadam.  Inakiwango kikubwa cha kupokea damu Zaidi ya viungo vingine vyote vya “Glandular”  mwilini. Kazi kubwa ya Pinea Gland ni kuchakachua hormone itwayo “Melatonin” ambayo  inawajibika kuhakikisha maendeleo ya hali ya kuwa “kiume” au “kike” mwilini mwa binaadam; “Seratonin”, ambayo ni “Hormone” muhimu kwa maendeleo ya akili pia.

Pia, hii “Gland”, inakazi nyingine ambayo ni  kuangalia madadiliko ya tabia ya mwili  za kila siku kama vile  mabadiliko ya jinsi unavyo lala usiku au pengine mchana.


2.     Pituitary Gland: Hii imepewa jina na tasisi za sayansi  ya madawa kama” Master Gland”, katika ukweli wa kazi yake hii nikama mnara wa usambazao mawasiliano kwenye ubongo, sehemu ijulikanayo kama” Hypothalamus” ni kiungo ndani ya ubongo kinacho miliki  mawasiliano ya mishipa ya fahamu kati ya mfumo wa “Glandular “na jinsi mwili unavyo kuwa katika hali ya huzuni, sikitiko au furaha. Hii “Gland” pia humiliki hali ya makuzi na kurekebisha joto mwili. Pungufu la au ongezeko la kazi yake, husababisha makuzi yasio kawaida na kuwa kibonge au mbilikimo. 
3.      Thyroid & Parathyroid Gland:  imekaa shingoni, na inamiliki mabadiliko ya chakula  kilicho liwa mwilini “Metabolism”,  na kumiliki  kima cha joto mwilini”Body heat”. Hali kadhalika makuzi na uchafu ndani ya mwili. Panapokuwa na kasoro ya udogo au ukubwa wa miliki hii, matokeo yake ni kukasirisha mishipa ya fahamu mwilini na kuwa hoi au kuchoka kila mara. Calcium na phosphorus zinamilikiwa na hii Gland. 
4.     Thymus Gland: Ipo katika ya kifua, na huwa kubwa mno utotoni na mtoto afikiapo barehe inapungua kuwa robo ya umbo lake. Hii ni silaha ya kinga za mwili kwa mashambulizi ya magonjwa ya nje  ndani ya mwili. Ina miliki udumishaji ulinzi wa kupambana na magonjwa nayayo shambulia mwili. 
5.     Adrenal Glands:  Hii ipo juu kidogo ya mafigo, kazi yake hasa ni kutoa nguvu na moto la hali ya juu na kuamua penye jambo la hatari au tukio,  hisia ya mwanaadam aidha uamua kukimbia au kupigana kijasili kwa kupambana na tukio lolote. 
6.      Pancreas:ipo chini kidogo ya tumbo na kazi yake ni kuyeyusha kemikali ijulikanoyo kama “Enzyme”. Katika utumbo mdogo, inachanganya “Insulin” hormone inayo punguza nguvu  za sukari katika damu.  Endapo  Pancreas  inashindwa kumiliki vyema utengenezaji wa Insulin mwilini, basi sukari ya damu huimalika Zaidi katika mwili na matokeo yake ni  Diabetes mellitus au ugonjwa wa kisukari. Pia papo hapo, Insulin nyingi nayo sio nzuri, husababisha kutetemeka na udhaifu mwilini. 
7.      Gonards:Uume au uuke, na kazi yake ni kumiliki kazi ya ngono. Zina changanya  Endrogen  ambayo ni hormone ya jinsia ya kiume, pia Estrogen  kwa wanawake. Hizi zote zinafanya kazi ya tabia ya mwili wa kike na kiume kwa jinsia zilivyo tofautiana. 
Maumbile ya mwili mzima wa mwanaadam , inamilikiwa na hizo Hormones.  Hapo ndipo utakuta, kupitia mazoezi ya aina ya “ Yoga Asanas”, mwili unaweza kumiliki na kusawazisha mzani wenye kima cha wastani   katika uchanganyaji wa hizo hormones mwilini.

 Mafunzo ya mazoezi ya Yoga, yanadhihirisha wazi kutokana na masomo mbalimbali ya uchunguzi toka vyuo vikuu vingi maarufu  nchini Marekani na kuandikwa kwa majarida mbali mbali yenye malengo ya kuielimisha jamii kuhusu afya na maumbile kupitia mazoezi ya Yogasanas. 
Imeandikwa na mwalimu wa Yoga, Rumadha Fundi kupitia majarida ya  chuo alicho somea filosofia ya Yoga cha  “College of Neo Humanist Studies”, Gullringen, Sweden na pia Tiljala, Culcutta, West Bengal, India ’87.






Karibuni Ibada ya Sikukuu ya Mavuno | Jumamosi 28 Novemba 2015 Saa Kumi kamili jioni!

$
0
0

IYK-Columbus, Ohio | Karibuni Ibada ya Sikukuu ya Mavuno | Jumamosi 28 Novemba 2015 Saa Kumi kamili jioni!                          

Uhuru-Jamhuri Independence African Dinner Dance


CHAMA CHA AFYA YA JAMII(TPHA) CHAWAOMBA WADAU KUTOA USHIRIKIANO ILI KUPAMBANA NA MATUMIZI TUMBAKU KWA VIJANA

$
0
0
Dk. Adeline l. Kimambo(kulia) kutoka Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) akitoa muhutasari wa Madhara ya Tumbaku mbele ya waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa waliofika kujadili changamoto wanazokabiliwa nazo hasa wanapokuwa wanatoa huduma kwa jamii kuhusu matumizi ya Tumbaku na kuwaomba wadau hao kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufikia malengo waliyojiwekea.Katikati ni Dk Faustine Njau kutoka Chama cha Afya ya Jamii (TPHA).
 (Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)
Mratibu wa Mradi wa Madhara ya Tumbaku (TPHA) Dk. Bertha T.A. Maegga(kushoto) akizungumza jambo kwenye kikao kilichowashirikisha wadau mbalimbali kutoka katika manispaa za jijii la Dar es Salaam kuhusu kushirikiana na wadau mbalimbali hasa kutoka katika manispaa za jiji hilo ili kudhibiti matumizi na madhara ya Tumbaku hapa nchini na kusisitiza kushirikiana ili kupambana na janga hili hapa nchini linalopelekea kupoteza nguvu kazi kubwa.

GLOBAL TV ONLINE:TEGO SEHEMU YA MWISHO JAY AUAWA

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

NSSF YADHAMINI BONANZA LA MICHEZO LA CHUO CHA IFM

$
0
0
Mchezaji wa timu ya mpira wa Kikapu ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Ephraim Mlawa (kushoto) akichuana na Juvenary Shichose wakati Bonanza la michezo la wanafunzi wa Chuo hicho lililofanyika, mwishoni mwa wiki katika Kituo cha Michezo cha JMK Youth Park na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kutoa vifaa vya michezo kwa timu zilizoshiriki mchezo wa soka. (Picha na Francis Dande)
Timu za mpira wa kikapu kutoka Chuo cha IFM zikichuana katika Bonanza la michezo la wanafunzi wa chuo hicho.
Kikosi cha timu ya Soka ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), BBF kikiwa katika picha ya pamoja.

Kikosi cha timu ya Soka ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), DIT kikiwa katika picha ya pamoja.


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TANZANIA YATAKA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA KUTEKELEZA KWA VITENDO DHANA YA UWAZI NA UWAJIBIKAJI

$
0
0
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi ( picha ya Maktaba) ametoa wito kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Ofisi zake kutekeleza kwa vitendo dhana ya uwazi na uwajibikani kama yanavyozishikiza Nchi Wanachama, kwa kile alichosema, utekelezaji wa dhana hiyo haupashwi kuwa jukumu la Serikali peke yake. Ametoa wito huo wakati wa majadiliano ya Ripoti ya Baraza la Haki za Binadamu iliyowasilishwa siku ya jumatatu mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Na Mwandishi Maalum,  New York

Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania,  imetoa wito kwa Mashirika ya   Umoja wa Mataifa, ikiwamo Baraza la  Haki za Binadamu    kuitekeleza kwa vitendo dhana ya uwazi na uwajibikaji.

Tanzania imesisitiza  pia   kwamba,   haitoshi kwa  Mashirika hayo  kuzitaka   nchi wanachama kwa maana ya serikali kuwajibika na kuwa wazi  katika utekelezaji wa majukumu  yake ili hali yenyewe yanafanya kinyume.

Wito huo umetolewa siku ya  Jumatatu na Mwakilishi wa  Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi,  wakati  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,  lilipopokea na kujadili Ripoti   ya Mwaka ya  Baraza la  Haki za  Binadamu ya   Umoja wa Mataifa.

Balozi Manongi ambaye alikuwa  miongoni mwa Mabalozi kati ya wengi waliochangia Ripoti hiyo  iliyowasilishwa na   Rais wa  Baraza la   Haki za Binadamu  Bw.Joachim Rucker .Amesema,  Tanzania  inatoa wito   huo   kutoka kile kinachoonekana  dhahiri   kwamba ama Mashirika hayo  yamekuwa yakionyesha  kuegemea  upande mmoja  dhidi ya mwingine   au  kupendelea  nchi  moja dhidi ya  nyingine  kitendo  ambacho kinakwenda kinyume  na kile  wanachokihubiri.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images