Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1026 | 1027 | (Page 1028) | 1029 | 1030 | .... | 3348 | newer

  0 0

   Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

  Nuru inapoiangazia dunia, huwaangazia viumbe vyote vilivyo hai na visivyo na uhai, viumbe vyenye uhai, hao hufurahia nuru hiyo kwa kuruka ruka na kucheza kufurahia nuru hiyo.

  Kila ifikapo asubuhi na mapema, utasikia sauti na mili­o ya ndege wa angani, wanyama wa kufuga na waishio mwituni, milio na sauti za viumbe hao wakati mwingine kuashiria kuwa kumekucha ili waendelee kufurahia nuru inayowanaagazia kwa manufaa ya maisha yao. 

  Wanadamu nao wakiwa kama viumbe hai wengine, huanza kujiandaa asubuhi na mapema kuelekea huku na kule kutafuta riziki ya kila siku ili maisha yao yaendelee kusonga mbele baada ya nuru kuwangazia.

  Mwandishi wa makala haya anaifananisha nuru hiyo inayoiangazia dunia na Amani. Amani ni tunu adhimu, ni tunu yenye Baraka na fanaka, amani inapotamalaki duniani, binadamu na kila kiumbe chenye uhai huonesha furaha yake kwa namna kiumbe hicho kinavyoguswa na amani hiyo.

  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sheria Na.15 ibara 3 ya 1984 nayo inajali na kuzingatia amani hiyo ndiyo maana inatamka kuwa “Sisi Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani”.


  0 0


  0 0


  Ukosefu wa ajira ni changamoto kubwa duniani kote. Hili linasikitisha kwa kuwa kazi ni chanzo cha heshima binafsi, amani na utulivu. Tanzania, miongoni mwa nchi za dunia ya tatu, imechukua hatua muhimu katika kuendeleza sekta yake ya ajira, japo bado inakabiliwa na changamoto kubwa katika hilo. Asilimia kubwa ya watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi, aidha hawana ajira au ajira walizonazo haziendani na uwezo wao.

  Kutokana na ushindani mkubwa katika soko la ajira na ongezeko kubwa la vijana wanaoingia kwenye soko la ajira (800,000 hadi 1,000,000 kwa mwaka), sekta rasmi imekosa mafanikio katika kuzalisha fursa za ajira, hasa mijini.  Matokeo yake ni; kiwango cha umasikini kimeongezeka.

  Sababu kuu zinazochangia fursa duni za ajira ni pamoja na:
  ·         Kutokuwa na usawa kati ya supply ya wafanyakazi na mahitaji. Ukweli ni kwamba, supply ya wafanyakazi ni kubwa kuliko demand ya wafanyakazi katika soko la ajira. Kila mwaka tunashuhudia ongezeko la vijana wanaomaliza masomo yao ambao wanaingia mtaani kuongeza idadi ya watafutao kazi.
  ·         Vijana kukimbilia kutafuta kazi mijini. Asilimia kubwa ya vijana wakimaliza elimu yao, hufikiria kwenda mijini kutafuta ajira, na wengi wao huwa na mawazo ya kufanya kazi ‘za ofisini’. Hili linasababisha shinikizo na ushindani mkubwa wa fursa za ajira. Laiti kama vijana wengi wangeamua kujikita katika sekta ya kilimo cha kisasa au sekta nyingine tofauti tofauti kwa kutumia elimu yao, ongezeko la watafutao kazi mjini lingepungua kwa kiasi kikubwa.
  ·         Elimu duni. Hili linajumuisha kutokujua kusoma na kuandika na ukosefu wa mafunzo sahihi yanayomuandaa mtu kuingia katika soko la ajira. Hakuna mwajiri anayeweza kuajiri mtu asiye na stadi muhimu za kitaaluma zinazohitajika katika kazi. Inaaminika kuwa, zaidi ya 61% ya wahitimu wanakuwa hawako tayari kiushindani katika soko la ajira.
  Kutokana na mwangaza huo wa hali halisi ya ajira nchini Tanzania mradi wa #RecruitMeumejipanga kusaidia kila mwenye uwezo wa kufanya kazi, vijana na wazee ili waweze kupata ajira wanazotaka. Tunafahamu kwamba ukosefu wa kazi ni jambo linalotatiza wengi na wengi kuhisi kuwa wamenyimwa haki yao kama binadamu ndani ya jamii wanayoishi.

  Kwa hiyo, #RecruitMe kwa makusudi mazima imeamua kujitolea kuweka jukwaa ambalo kila mtu anaweza kulitumia anapotafuta ajira sahihi na kupitia jukwaa hilo, mtu anaweza kugundua fursa mpya zilizopo katika soko la ajira. Zaidi ya hayo, waajiri wanaweza kunufaika sana kutokana na jukwaa hili, kwa kuwa linatoa fursa kwao pia kutafuta wafanyakazi wanaowahitaji.
  Lengo kuu la mradi huu si kuwapa watu ajira yeyote tu, la hasha, bali ni kuwapatia watu ajira zenye hadhi, heshima na kufanya ndoto za mtu kuwa kweli. #RecruitMe itakupatia ajira inayokubalika kisheria, yenye mapato yanayoendana na kiwango cha kazi na ujuzi wako. Tunakuthibitishia ajira itakayojali haki zako kama mwanadamu na mfanyakazi, ikiwa ni pamoja na kujali maslahi yako.
   Ili kupata huduma zetu, tafadhali tembelea tovuti yetu http://goo.gl/zPLquy ambapo utakuwa na uwezo wa kuona fursa za ajira mbalimbali, pamoja na kujenga profile yako mwenyewe. Huna haja tena ya kutokwa na jasho kutembea kutoka ofisi moja hadi nyingine tu na kuishia kunyimwa nafasi. Pumzika, na tembelea tovuti yetu. Tunaweza kukusaidia kupata kazi uitakayo.

  0 0


  0 0

   Ankal alipohudhuria mahafali ya mjomba wake katika Chuo cha Ukutubi cha Bagamoyo kilichopo eneo la Ukuni  mkoa wa Pwani alibahatika kukutana na wadau wake wakubwa akiwem0 mwalimu wa sanaa katika Taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TASUBA) na kupata nao selfie kwa kila staili. Amewaahidi kuwatembelea chuoni na kubadilishana nao uzoefu  katika fani ya upigaji picha na mbinu zingine za kupata picha nzuri
   Ankal na wadau wa TASUBA wakila Selfie
  Selfie ya chini
   Air Force One ikiwa imetia nanga katika ufukwe wa Bagamoyo. Ankal akaomba na kukubaliwa kupata nayo taswira. Hakika huu mji mkongwe na wa kihistoria ukifanyiwa kazi utakuwa kivutio kikubwa mno cha watalii. Hebu wahusika kazeni buti Bagamoyo ifufuke upya....


  0 0

  Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimewasili salama nchini Algeria jana jioni majira ya saa 10, kabla ya kuanza safari ya kuelekea katika mji wa Bilda.

  Msafara wa Taifa Stars unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Athumani Kambi, ambapo jumla ya watu 40 wapo katika mji wa Bilda wakiwemo wachezaji 21 wanaojiandaa kwa mchezo wa marudiano.

  Mara baada ya kufika katika uwanja wa ndege Algiers, Stars ilipokelewa na watanzania na wanafunzi wanaoshi nchini Algeria, na kuongozana na timu mpaka katika mji wa Bilda ilipofikia timu.

  Stars imeanza kufanya mazoezi leo saa 1 jioni katika uwanja wa Mustapha Tchaker utakaotumika kwa mchezo wa marudiano siku ya Jumanne.

  Katika mchezo wa awali uliochezwa jana jioni jijini Dar es salaam, Tanzania ilitoka sare ya mabao 2 – 2 dhidi ya Algeria, hivyo kuifanya Stars kusaka ushindi katika mchezo wa marudiano ili kuweza kusonga mbele.

  Kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema vjana wake wote wapo katik ahali, hakuna majeruhi na wapo tayari kwa ajili ya kusaka ushindi siku ya Jumanne, na kusema makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa jana wanayafanyia kazi yasijitokeze tena katika mchezo unaofuata.

  Taifa Stars imefikia katika hoteli ya Ville Des Roses imetumia takriabn muda wa saa 1 kutoka katika uwanja wa Ndege wa Algiers mpaka katika hoteli hiyo iliyopo eneo la Bilda.

  Namba ya simu ya Afisa Habari wa TFF aliyeambatana na timu nchini Algeria +213 558 465069

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja pamoja na Kamishna wa Nishati, Mhandisi Hosea Mbise hapo jana walifanya ziara kwenye maeneo mbalimbali yanayopitiwa na mradi mkubwa wa Gesi Asilia.

  Lengo kuu la ziara hiyo ni kujionea shughuli zinazoendelea kwenye mradi wa gesi asilia pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa maeneo hayo kuhusu masuala mbalimbali ya shughuli zao za kila siku.

  Maeneo ambayo yalitembelewa na viongozi hao ni pamoja na Kituo cha Kupokea Gesi Asilia ya Mtwara na Lindi cha Somangafungu (Somangafungu Gas Receiving Station) kilichopo wilayani Kilwa, mkoa wa Lindi; Visima vya gesi asilia vya Mnazi Bay na Msimbati; Sehemu iliyoathiriwa na Mmomonyoko wa ardhi ya Msimbati na Kituo cha Kuchakata gesi asilia cha Madimba cha mkoani Mtwara.

  Wengine katika ziara hiyo ni Kamishna Msaidizi wa Nishati sehemu ya Gesi Asilia, Mhandisi Norbert Kahyoza, Meneja wa Kampuni ya Gesi Asilia (GASCO), Mhandisi Kapuulya Musomba na Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

  Ziara hiyo ni miongoni mwa mikakati iliyowekwa na viongozi hao kukagua shughuli mbalimbali za masuala ya Nishati na Madini kote nchini.
  Baadhi ya mitambo katika Kituo cha Kupokelea Gesi Asilia kutoka Songosongo na Mtwara kilichopo Somangafungu wilayani Kilwa Mkoani Lindi
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia) na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja (kushoto) wakimsikiliza Meneja wa Kampuni ya GASCO, Mhandisi Kapuulya Musomba (hayupo pichani) akiwaeleza kuhusu Kituo cha Kupokelea Gesi cha Somangafungu. Katikati ni Msimamizi wa Kituo hicho, Mhandisi Msafiri Peter.
  Baadhi ya mitambo ya kupokelea gesi asilia iliyopo kwenye maeneo kilipo kisima cha gesi asilia cha Mnazi Bay Namba 3.


  0 0

  Habari kaka,

  Napenda kutumia fursa hii kukushirikisha habari ya kusikitisha kuhusu dada Joyce Mwambepo mkazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa 27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na mwanaye mwenye umri wa miaka 4.

  Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo hata hivyo haikusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya raufaa mkoani Mbeya ambako alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu.

  Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwan Joyce amevunjika miguu yote miwili hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya baada ya kudaiwa kukoswa shilingi 550,000/- za matibabu.

  Hadi nakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake ambaye mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wote wawili kufariki.

  Hivyo nimejitahidi kufuatialia ili kujua mahitaji halisi lakini sikufanikiwa kumpata dakttari bingwa wa mifupa .Ili kumsaidia Joyce inatakiwa aanze process upya za matibabu kuanzia hapa Mbeya referral Hosp hadi Muhimbili.

  Gharama za matibabu ni kama ifuatavyo
  1. shilingi 300,000/- za kupima CT-SCAN
  2. Shilingi 250,000/- za MRI
  3. Usafri wa kutoka Mbeya-Dar kwa kukodi gari maalum 700,000/-
  4. Gharama za msaidizi ambaye ni rafiki yake 200,000/-
  5. Chakula (Mchele, Unga, Sukari, Maharage, Mafuta)
  6. Gharama za matibabu (CT-SCAN&MRI) ni vipimo tu
  7. Na mahitaji mengineyo wakiendelea kupata tiba

  Asante sana kwa moyo wako wa kujitoa na Mungu atakubariki

  Deo Kakuru Msimu
  Msamaria mwema
  0769 512 420

  0 0
 • 11/15/15--23:29: Gapco advantage


 • 0 0

  Meneja Mkuu wa mgodi wa STAMIGOLD Mhandisi Dennis Subugwao (kushoto) akikabidhi moja ya vifaa vya kujifunzia wanafunzi kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo, Ndugu Nassib Mmbaga muda mfupi baada ya kuzindua jengo la choo cha wanafunzi Shule ya msingi Mavota, Mkoani Geita.
  Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mavota akizungumza mara baada ya kukabidhiwa jengo la choo cha wanafunzi kilichojengwa kwa ushirikiano kati ya mgodi wa STAMIGOLD na wananchi wa kijiji cha Mavota.

  Moja kati ya darasa lililokamilishwa kwa msaada wa mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo. Pichani ni watendaji kutoka mgodini na halmashauri ya wilaya ya Biharamulo.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio akuzungumza na waandishi wa habari (hapo pichani) kuhusu ujio wa ndege ya utafiti wa awali wa mafuta na gesi asilia kwa kutumia ndege katika Kitalu cha Ziwa Tanganyika Kaskazini, Mkurugenzi wa undelezaji wa mafuta na gesi asilia Dkt. Wellngton Hudson (kulia) mkutano huo ulifanyika makao makuu ya TPDC mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio, katika mkutano wake na waandishi hao mwishoni mwa wiki.
  Ndege ya utafiti wa awali wa mafuta na gesi asilia inayotarajia kuanza utafiti katika Kitalu cha Ziwa Tanganyika Kaskazini ikiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  0 0


  0 0
 • 11/16/15--00:31: KUMBUKUMBU
 • BIBIANA (NKAMALI) PETER BASI KWEKA
  KIFO 16/11/2001

  Bibi yangu mpendwa na somo wangu pia.Leo umetimiza miaka 13 tangu ulipoitwa mbinguni kwa BABA. Hatuna cha kusema,tumebaki kushukuru tuu kwani hata miaka ulioishi ilizidi ile ya Upendeleo.

  Tunakumbuka uzuri wako,Ucheshi,Usafi na Ufanyakazi wako bila kusahau jina lako (BIBI SHAMBA). Kweli ulikuwa mfano wa kuigwa  unakumbukwa sana na mimi somo wako JANE,WAJUKUU WOTE WA KWA BASI,MTOTO WAKO WA PEKEE ALIYEBAKI DUNIANI SR.DEVOTA KWEKA CDNK, WA KWEKA WOTE WA NARUMU,WA –ULOMI WOTE WA USWAA,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI ,MISA YA KUMUOMBEA ITAKUWA NYUMBANI KWAKE NARUMU TAREHE 01/01/2016.
  , WOTE MNAKARIBISHWA
  RAHA YA MILELE UMPE Ee BWANA


  0 0

  SIMU.TV:  Ndungai,Dk.Tulia, Mwinyi wapenya kuwania uspika, rais Magufuli amtumia rais wa Ufaransa salamu za rambirambi; https://youtu.be/gDawuK9CXxI

  SIMU.TV:  Wanafunzi walimishwa mashamba ya walimu kwa sh.200/-, matrafiki 57 Pwani waondolewa; https://youtu.be/1hm7HXxQbBc 

  SIMU.TV:  Stars matumaini kibao Algeria, Samatta, Ulimwengu walala sakafuni taifa, kocha mpya Simba apewa masharti mawili magumu; https://youtu.be/t0AxmnMMoVU

  SIMU.TV:  Siri ya uchaguzi Zanzibar yafichuka, ada elekezi shule binafsi kuanza January.Wanne mbaroni mauwaji ya kigogo CHADEMA; https://youtu.be/raAqpRccYfA

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akizungumza na mkazi wa Kitongoji cha Madukani Wilayani Simanjiro, Loshilaa Moiyo, ambaye alipatiwa sh110,000 za mfuko wa Maendeleo ya jamii nchini (Tasaf) kwa lengo la kusaidia kaya masikini.
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akizungumza na mtoto wa mkazi wa Kitongoji cha Madukani Wilayani Simanjiro Helena Saitabau, ambaye alipatiwa sh 120,000 za mfuko wa Maendeleo ya jamii nchini (Tasaf) kwa lengo la kusaidia kaya masikini.

  0 0

  Wafanyabishara wadogo na wa kati zaidi ya 300 waliopo katika wilaya mbali mbali mkoani Tanga wameongezewa ujuzi wa elimu ya biashara ili waweze kufanya shughuli zao kwa ufanisi na kuweza kuongezaza kipato chao na kuchangia pato la taifa.

  Kampuni ya Airtel Tanzania, kupitia mpango wake wa “Airtel Fursa Tunakuwezesha” imewapatia mafunzo ya ujasiriamali vijana wa manispaa ya Tanga kwa lengo la kuwawezesha kuboresha uendeshaji biashara na kukuza mitaji yao katika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa YDCP uliopo mkoani hapo.

  Akifungua warsha hiyo, meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Tanga Aluta Kweka katika alisema, “lengo letu hasa ni kuwapatia ujuzi vijana wajasiriamali wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 24 ili waweze kufanya biashara kwa tija badala ya kufanya kwa mazoea. Mafunzo haya tunataraji yataongeza tija ya kibiasha ku kuwawezesha Vijana hawa kujenga ajira kwa vijana wengine huku wakichochea upatikanaji wa bidhaa na huduma katika jamii inayowazunguka.

  Kufuatia hatua hiyo baadhi ya wajasiriamali waliohudhuria warsha hiyo wameishukuru Airtel kwa mchakato huo na wameiomba Airtel kuendelea na zoezi hilo kwa wafanyabishara nchi nzima ili waweze kufahamu umuhimu wa kufanya biashara kwa malengo zaidi.

  Aisha Mtangi ni mfanyabiashara mdogo anayejihusisha na biashara ya kuuza matunda aliyenufaika na mafunzo hayo ambaye alisema, “kuwa kwa sasa amepata muongozo mzuri utakaokuza biashara zake na kuzifanya kwa weledi mkubwa zaidi”

  “Hii ni fursa ya kipekee kwangu kama kijana na ninaishukuru sana Airtel kwa mafunzo yenye manufaa kwangu na vijana wenzangu wa hapa Tanga” Alisema Aisha.

  Airtel imejipanga kufikia mikoa 10 kote Tanzania hadi kufikia December mwaka huu. Vijana wa mikoa hii watanufaika na mafunzo ya Ujasiriamali na vitendeakazi kwaajili ya kukuza biashara zao.
  Mkufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tanga,Hassani Juma Hassani akitoa mada wakati wa semina ya Airtel Fursa ilivyofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa YDCP mkoani Tanga.
  Meneja mauzo wa Airtel Mkoa wa Tanga, Aluta Kweka akizungumza na wauzaji wa bidhaa za kampuni hiyo wakati wa semina ya Airtel Fursa ilivyofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa YDCP mkoani Tanga.
  Meneja mauzo wa Airtel Mkoa wa Tanga,Aluta Kweka akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu semina ya Airtel Fursa iliyofanyika kwenye ukumbi wa YDCP mkoani Tanga.

  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla amekabibidhi vifaa vya michezo ikiwemo jezi, mipira,nyavu za magoli na vikombe kwa ajili ya timu ya wafungwa na askari gereza la Karanga Moshi ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa hivi karibuni baada ya kufanya ziara gerezani hapo na kupokea maombi.

  Katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni tatu na nusu aliwakumbusha wafungwa na mahabusu kuwa michezo hujenga umoja, michezo ni burudani, michezo ni kwa afya na zaidi kwa wenye vipaji michezo itumike kulinda vipaji vyao na siku wakitoka waviendeleze vipaji.

  Vifaa alivyokabidhi ni pamoja na nyavu za magoli, vikombe 2 vya kushindaniwa,jezi kwa timu 5 za wafungwa na mahabusu, mipira 10 kwa ajili ya wafungwa na mahabusu, jezi moja na mpira mmoja kwa ajili ya timu ya netball ya wafungwa wanawake na jezi moja , mipira 3 na nyavu za magoili kwa ajili ya timu ya askari magereza.

  Uongozi wa gereza, wafungwa na mahabusu wamemshukuru sana mkuu wa mkoa kwa msaada huo na wamemuhaidi kumuuenzi na kila mwaka watakuwa na ligi itakayoitwa Makalla Cup na wamewataka viongozi na wadau wengine kite nchini kuiga mfano. alioonyesha mkuu wa mkoa wa kilimanjaro
  Sehemu ya vifaa vya michezo vilivyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mh. Amos Makalla kwa Gereza la Karanga Mkoani humo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mh. Amos Makalla akipiga mpira kuashiria kuendeleza michezo Gerezani hapo.


  0 0
 • 11/16/15--01:07: BEI YA MADAFU LEO


 • 0 0

  Dkt. Tulia Ackson Mwansasu.

  0 0

  Mwenyekiti wa chama cha riadha mkoa wa Mwanza Silas Lucas akiwapa maelekezo wakimbiaji wa km 21 wakati wa mbio za Rock City Marathon kabla ya mbio kuanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana.
   Wanariadha katika kundi la km 21 wakikatiza katika mitaa ya jiji la Mwanza kuelekea katika viwanja vya CCM Kirumba kumaliza mbio  hizo.
   Festus Taram kutoka Kenya akimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza jana baada ya kutumia muda wa saa 01:04:40, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini humo Evancy Kiplagan aliyetumia muda wa saa 01:04:55
   Afisa michezo mkoa wa Mwanza, James William, akimkabidhi zawadi ya kitita cha shilingi milioni moja na nusu mshindi wa kwanza wa mbio za km 21 upande wa wanawake Alice Mogire kutoka Kenya baada ya kutumia muda wa saa 01:14:42 kumaliza mbio hizo. Wanaoshuhudia ni Meneja Mkuu kampuni ya Capital Plus International Limited ambao ni waandaaji wa mashindano hayo, Erasto Kilawe (kushoto), Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Mwanza, Hamis Faki (wa pili kushoto), mjumbe wa shirikisho la riadha Tanzania (RT), Peter Mwita (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa chama cha riadha mkoa wa Mwanza, Silas Lucas.

  Washindi wa nafasi tatu za juu katika mbio za km 21 upande wa wanaume wakionyesha medali na pesa taslimu walizopokea kama zawadi baada ya kuibuka washindi katika mbio hizo.

  Mwandishi wetu, Mwanza

  Festus Taram kutoka Kenya aliibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza jana baada ya kumaliza kwa muda wa saa 01:04:40, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini humo Evancy Kiplagan aliyetumia muda wa saa 01:04:55

  Mbio hizo za kilomita 21 zilianzia Uwanja wa CCM Kirumba kupitia Barabara ya ikulu ndogo hadi mzunguko wa samaki na kuelekea Buzuruga kisha kutokea barabara ya pasiansi na kumalizikia uwanjani Kirumba.

  Nafasi ya tatu upande wa wanaume ilichukuliwa na Mtanzania Fabian Joseph aliyetumia muda wa saa 01:05:00, ikiwa dakika chache nyuma ya mpinzani wake.

  Akizungumzia siri ya ushindi wake, Talam alisema hii ni mara ya pili kushiriki mashindano hayo ambapo mwaka jana alishika nafasi ya tatu jambo lililompa chachu ya kujituma kufanya mazoezi zaidi na kukaa kambini muda mrefu jambo lililopelekea kufanya vizuri katika michuano ya mwaka huu.

  “Maandalizi ya mwaka huu ni mazuri na washiriki wameendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka jambo linalotufanya wanariadha kujiwekea mikakati mizuri ili kuweza kukabiliana na ushindani mkali uliopo katika mbio hizi,” alisema.

  Upande wa wanawake mshindi wa kwanza ni Mkenya Alice Mogire aliyetumia muda wa saa 01:14:42 akifuatiwa na Mtanzania Natalia Elisante  aliyetumia saa 01:15:16 huku Raia mwingine wa Tanzania Angelina Isere akishika nafasi ya tatu baada ya kutumia saa 01:15:35

  Washindi wa kwanza katika mbio hizo zilizofanyika kwa mara ya saba jijini Mwanza  waliibuka na kitita cha Sh1.5 milioni kila mmoja, washindi wa pili Sh900,000 na washindi wa tatu Sh700,000 kila mmoja.

  Mashindano hayo ya kila mwaka yaliyo katika kalenda ya RT yaliandaliwa na Kampuni ya Capital Plus kwa udhamini wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bank M, Precision Air, New Mwanza Hotel, Bodi ya Utalii Tanzania na PPF.

  Wakati huohuo, Katibu tawala mkoa wa Mwanza alipongeza waandaaji wa mbio hizo na kutoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana kwa pamoja ili kurejesha hadhi ya mchezo wa riadha nchini.

  Akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio hizo kwenye uwanja wa CCM Kirumba kwa niaba ya Katibu tawala jana, Afisa michezo mkoa wa Mwanza, James William, alisema mbio hizo ni nyenzo muhimu ya kuwaandaa wanariadha wetu nchini kuwa katika nafasi ya kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa na kuirudishia nchi yetu heshima ya kipekee katika mchezo huo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
older | 1 | .... | 1026 | 1027 | (Page 1028) | 1029 | 1030 | .... | 3348 | newer