More Channels
Showcase
Articles on this Page
(showing articles 20481 to 20500 of 65691)
- 11/11/15--23:37: _Airtel yazindua ofa...
- 11/11/15--23:41: _UCHAGUZI WA UBUNGE ...
- 11/12/15--01:50: _WAMWANDIKIA BARUA Y...
- 11/12/15--01:50: _NSSF yapiga jeki Ro...
- 11/12/15--01:55: _Katibu Mkuu Wizara ...
- 11/12/15--02:19: _MIRADI YA MKUHUMI I...
- 11/12/15--12:19: _BBC DIRA YA DUNIA A...
- 11/12/15--12:41: _simu tv: HABARI KUT...
- 11/12/15--19:51: _KATIBU MKUU OFISI Y...
- 11/12/15--20:00: _RAIS DKT JOHN POMBE...
- 11/12/15--20:00: _BARAZA KUU LA USAL...
- 11/12/15--22:41: _TAARIFA YA UJIO WA ...
- 11/12/15--22:59: _JUMUIYA YA WATANZAN...
- 11/12/15--22:59: _MAREKEBISHO YA BARA...
- 11/12/15--23:06: _UCHAMBUZI WA HABARI...
- 11/12/15--23:08: _Mshindi wa Airtel T...
- 11/12/15--23:10: _VODACOM YAPELEKA SO...
- 11/12/15--23:20: _UKEKETAJI WAPUNGUA ...
- 11/12/15--23:32: _NAIBU KATIBU MKUU W...
- 11/12/15--23:49: _WATUMISHI WANNE HAL...
(showing articles 20481 to 20500 of 65691)
Channel Description:
Most read Swahili blog on earth
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua ofa kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel Money kutuma pesa kwa marafiki na familia zao ndani ya mtandao wa Airtel Bure
Ofa hii mpya ijulikanayo kama "Okoa Mapene'' ina lengo la kuinua huduma za kifedha na kuwapatia wateja njia rahisi ya kufanya miamala yao ya kila siku
Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja Uhusiano wa Airtel Bwn Jackson Mmbando alisema " kwa mara nyingine tena tunadhirisha kwa vitendo dhamira yetu ya kutoa huduma za kibunifu, rahisi na zenye gharama nafuu kupitia huduma ya Airtel Money.
Leo tunawawezesha wateja wetu wa Airtel money nchi nzima kuokoa pesa wanapotuma pesa kwenda kwa mtumiaji wa Airtel kwani tozo za kutuma pesa ni BURE kwa kiasi chochote kitakachotumwa. Tunaamini ofa hii ya "Okoa Mapene'' itakuwa kichocheo kikubwa kwa wateja kutumia huduma ya Airtel Money kwa muda wa mienzi mitatu na zaidi"
Aliongea kwa kusema "Okoa Mapene'' ni njia mojawapo ya kuwazawadia wateja wetu wanaotuma pesa kwa ndugu , jamaa, marafiki, familia na washirika wao wa biashara kupitia huduma ya Airtel Money. "Okoa Mapene'' pia kuwawezesha mawakala kupata kamisheni zaidi kutokana na kuwa na wateja wengi watakaofanya miamala mingi kuanzia sasa.
Ili kupata kutuma pesa mteja anatakiwa kupiga *150*60# na kuunganishwa kwenye menu ya Airtel Money na kuanza kufanya miamala yake BURE.
Hiv karibuni Airtel imewazawadia wateja wake kwa kuwapatia gawiwo la faida watumiaji wote wa huduma ya Airtel Money na kuwawekea gawiwo hilo moja kwa moja kwenye akaunti zao za simu.
Meneja Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando akionge na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofa kwa wateja wake itakayowawezesha kutuma pesa kiasi chochote cha pesa kupitia huduma ya Airtel Money bure. Pichani ni Stephen Kimea Meneja kitengo cha Airtel Money ( kushoto) na Aliesikia Peter Afisa kitengo cha Airtel Money.
Meneja Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando (katikati) pamoja na Meneja kitengo cha Airtel Money, Stephen Kimea ( kushoto) na Afisa kitengo cha Airtel Money, Aliesikia Peter kwa pamoja wakionyesha kipeperushi cha ofa mpya itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma pesa kiasi chochote cha pesa kupitia huduma ya Airtel Money bure
0 |
|
0 |
|
Kiongozi wa kampeni ya Okoa Tembo wa Tanzania,Shubert Mwarabu akizungumza na Waandishi wa habari ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO,kuhusiana na Barua yao ya Wazi kwa Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli juu ya mauaji ya Tembo ambayo yamekuwa yakifanyika hapa nchini kwa kiwango kikubwa.Katika barua hiyo ya wazi,uongozi wa kampeni hiyo umetoa wito kwa Serikali kutekeleza ama kufanya yafuatayo1.kuwakamata na kuwashitaki wafanyabishara wakubwa wa meno ya Tembo nchini,bila kujali Utaifa,Hadhi au Mamlaka.2.Kutumia urafiki wa kihistoria kati ya Tanzania na China kufunga masoko ya meno ya Tembo huko china.3.Kuteketeza hadharani ghala ya meno ya Tembo Tanzania-inayosadikika kuwa kubwa kuliko yote Ulimwenguni.
Bwa.Shubert ameeleza kuwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika uhifadhi wa Tembo hapo kapla,anasema Mwaka 1989,Tanzania iliongoza jitihada za kupiga marufuku biashara ya mene ya Tembo Ulimwengu, "tulipochukua hatua kukomesha mauaji ya Tembo,Dunia nzima ilituunga mkono,hivyo ni lazima turejeshe upya dhamira yetu kwa ahadi tuliyojiwekea kwa hatua ya Kimataifa zaid ya miaka ishirini iliyopita,na kuleta ukomo wa biashara yote ya meno ya tembo hapa nchini'',alieleza Bwa.Shubert.

Pichani kati ni mmoja wa Wajumbe wa kampeni ya OKOA TEMBO WA TANZANIA,Bwa.Lameck Mkubulo akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari,kwenye mkutano uliofanyika mapema leo subuhi Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar,kuhusiana na Barua yao ya Wazi waliomuandikia Rais ya kumtaka achukue hatua juu ya suala la kupungua kwa kasi idadi ya Tembo nchini,kutokana na ujangili kwa ajili ya biashara haramu ya meno ya Tembo
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Salim Shao (kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 15 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Capital Plus International Limited, ambao ni waandaaji wa mbio za Rock City Marathon, Bw. Erasto Kilawe, jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni udhamini wa mbio hizo zitakazofanyika katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza tarehe 15 Novemba mwaka huu.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Salim Shao (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hafla fupi ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 15 kwa Kampuni ya Capital Plus International Limited, ambao ni waandaaji wa mbio za Rock City Marathon, jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni udhamini wa mbio hizo zitakazofanyika katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza tarehe 15 Novemba. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Capital Plus International Limited, Bw. Erasto Kilawe.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Capital Plus International Limited, ambao ni waandaaji wa mbio za Rock City Marathon, Bw. Erasto Kilawe (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hafla fupi ya kupokea hundi ya shilingi milioni 15 kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ikiwa ni udhamini wa mbio hizo zitakazofanyika katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanzana tarehe 15 Novemba mwaka huu. Kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Salim Shao.
NSSF yapiga jeki Rock City Marathon kwa Sh 15M/-
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limetoa shilingi milioni 15 kudhamini mbio za Rock City Marathon mwaka huu, huku waandaaji wa mbio hizo wakitangaza zawadi za washindi.
Jumla ya shilingi milioni kumi zimetengwa kushindaniwa katika makundi mbalimbali ya mbio za mwaka huu zilizopangwa kufanyika Novemba 15 (jumapili hii) katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 15 kwa waratibu wa mbio hizo, Capital Plus International Limited, Afisa uhusiano mwandamizi wa NSSF, Bw. Salim Shao alisema kuwa NSSF imeendelea kudhamini mbio hizo kwa mwaka wa saba mfululizo baada ya kuona maboresho yanayofanyika kila mwaka katika mbio hizo zinazowakutanisha wanariadha kutoka ndani na nje ya nchi.
“Kwa upande wetu tunaona ushiriki wetu katika mbio hizi kama fursa ya kukutana moja kwa moja na wateja wetu lakini pia tutatumia fursa hii kuwaelezea washiriki juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko wetu ili waweze kunufaika na huduma za kipekee zinazotolewa na NSSF,” Alisema Bw. Shao.
Mbio za Rock City Marathon, zinazoandaliwa na Kampuni ya Capital Plus International (CPI), kwa ushirikiano na Chama cha Riadha Tanzania (RT), pamoja na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA) zinalenga kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini na pia kukuza utalii wa ndani kupitia sekta ya michezo.
Meneja mkuu kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bw. Erasto Kilawe, alisema kuwa udhamini huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha hatua za mwisho za maandalizi ya mbio hizo na baadhi ya fedha hizo zitatumika kama zawadi kwa washindi wa mbio za mwaka huu.
“Baada ya kupata udhamini huu, tunafaraja kubwa kutangaza zawadi watakazopatiwa washindi. Kwa mbio za Kilomita 21, jumla ya shilingi milioni saba na laki moja zimetengwa kwa ajili ya washindi. Washindi wa kwanza watazawadiwa Tsh 1.5m/- huku washindi wa pili wakijipatia laki tisa na washindi wa tatu watapata laki saba kila mmoja.
Kwa mbio za kilomita tano, zaidi ya shilingi laki nne zimetengwa kwa ajili ya washindi. Jumla ya shilingi laki tatu na arobaini zimetengwa kwa ajili ya washindi wa mbio za kilomita 3 na shilingi laki mbili imetengwa kama zawadi kwa ajili ya mbio za watoto za kilomita mbili.”
Alisema kuwa kamati ya maandalizi ya mbio za mwaka huu imefanya kazi kubwa ili kuhakikisha kuwa kiwango cha mbio hizo kinaongezeka ili kuzifanya ziwe na msisimko zaidi.
“Kwa namna ya kipekee sana nipende kuwashukuru wadhamini wa mbio za mwaka huu ambao ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Precision Air, Bodi ya Utalii Tanzania, New Mwanza Hotel na Bank M,” alisema.
Bw. Kilawe alitoa wito kwa wakazi wa jiji la Mwanza na miji jirani kujisajili kwa kuchukua fomu katika uwanja wa Nyamagana.
“Fomu za ushiriki pia zinapatikana katika ofisi za Kampuni ya Capital Plus International zilizopo ghorofa ya tatu jengo la ATC, mtaa wa Ohio jijini Dar es salaam na Uwanja wa Amri Abeid mjini Arusha,” alihitimisha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kushoto) akijadiliana jambo na Kamishna wa Nishati, Mhandisi Hosea Mbise (katikati). Wa kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, James Andilile.
Wajumbe wa kikao wakimsikiliza katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi (kushoto) akizungumza wakati wa kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia). Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi- EWURA, Profesa Jamidu Katima.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia) akipokea nyaraka mbalimbali kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi- EWURA, Profesa Jamidu Katima. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi.
Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zimeagizwa kutochelewesha kushughulikia maombi ya wawekezaji pale wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wanapoonesha dhamira ya kuwekeza. Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo ametoa agizo hilo hivi karibuni wakati wa kikao chake na Watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo.
Mhandisi Chambo aliwaagiza watendaji hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea, na badala yake wazingatie Sheria na maadili ya kazi zao, kutokana na ukweli kwamba sekta ya Nishati ni sekta nyeti inayohitaji watendaji waadilifu na wabunifu.
Sekta ya ardhi nchini ni ya kipekee katika uthibiti wa mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa ndiyo sekta pekee ambapo ndipo uzalishaji na uondoaji wa kaboni hutokea.
Mfumo wa matumizi mapana ya ardhi ambao siyo endelevu unapaswa ubadilishwe ili nafasi yake ichukuliwe na matumizi ambayo ni sahihi na endelevu zaidi tofauti na hali ilivyokuwa mwanzo. Hatua hiyo ni pamoja na kutumia vyema ardhi iliyopo kwa kupunguza uzalishaji wa gesi joto unaotokana na ardhi.
Mnamo mwaka 2009, Ubalozi wa Ufalme wa Norway nchini Tanzania ulianza kuwa chachu ya uhifadhili wa miradi saba ya majaribio ya Mkakati wa Kupunguza Ukataji Hovyo na Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) kwa kutoa dola za Kimarekani zipatazo milioni 100 kufadhili mradi huo.
Fedha hizo zilipelekwa kwenye taasisi za elimu ya juu nchini ambazo zinajukumu la kuandaa wataalamu mbalimbali.
Taasisi zilizopata fedha hizo ni pamoja na Chuo Kukuu Cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwa lengo la kuendesha mafunzo na utafiti.
Fedha nyingine zilipelekwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, kitivo cha Tathmini ya Rasilimali ambako huko pia waliingia mkataba na Asasi zisizo za Kiserikali (NGO’s) za hapa nchini ili kutekeleza mkakati wa MKUHUMI vijijini.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Julius Ningu hivi karibuni alibainisha kuwa MKUHUMI ni moja ya maeneo ya utekelezaji wa mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi ambao unalenga kupunguza uzalishaji wa gesi joto katika sekta ya misitu, mkataba huo uliosainiwa katika mkutano uliofanyika nchini Indonesia mwaka 2008.
“Gesi joto ni mchanganyiko wa gesi mbali mbali zinazozalishwa kutokana na shughuli anazofanya binadamu kama vile viwanda, kilimo, sekta ya usafirishaji, magari, na mitambo inayotoa gesi mbalimbali ambayo hupanda hadi kufikia umbali wa kilometa moja hadi moja na nusu kutoka uso wa dunia na huko hutengeneza utando mzito (tabaka la gesi joto)”, alisema Dkt Ningu.
Wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha urafiki cha Dar es salaam wafanya mgomo wakishinikiza uongozi wa kiwanda hicho kuwaongea mishahara.https://youtu.be/jv0toXMA8Z0
Jumuiya ya umoja wa ulaya yatoa msaada wa shilingi milioni 400 kwa mashirika ya umoja wa mataifa nchini ili kusukuma gurumu la maendeleo.https://youtu.be/Q8fVScX5Llo
Serikali imesema mapato yatokanayo na uchimbaji wa gesi asilia yatawekwa wazi kwa umma na kuchapishwa mara nne kwa mwaka katika gazeti la serikali.https://youtu.be/D96yy05NE2o
Serikali imesema imejidhatiti katika kukabiliana na utandawazi katika biashara jambo ambalo litasaidia kongeza pato la taifa. https://youtu.be/V2YNUjge5F4
Shirika la uwezeshaji wananchi kiuchumi laingia makubaliano na taasisi ya utafiti ya vyuo vikuu vya mashariki na kusini mwa Afrika ya ushirikiano wa kazi katika maeneo ya utafiti. https://youtu.be/xlOkp8ybaGM
Mchakato wa kuwania kiti cha uspika ndani ya bunge lijalo kupitia CCM washika moto baada ya takribani makada 18 kujitosa akiwemo Ndugai. https://youtu.be/-vYbXoh5zD4
Taasisi ya okoa Tembo yatuma barua ya wazi kwa Raisi Magufuli kumuomba achukue hatua madhubuti kupamabana na majangili ili kuokoa maisha ya tembo.https://youtu.be/m_NBHXjwODs
Uzalishaji wa taka jiji Dar es salaam waonekana kuleta tija kwa baadhi ya wakazi baada ya baadhi y ao kuibua biashara kupitia taka hizo. https://youtu.be/WbxIGcm57tg
Mvua kubwa yam awe iliyonyesha mkoani Rukwa yaelezwa kuleta madhara makubwa kwa wazi wa mkoa huo. https://youtu.be/NISiTT-TBQw
Maandalizi ya Ratiba ya bunge la kumi 11 yaanza rasmi huku wabunge wakianza kuwasili mkoani Dodoma kwa kazi ya usajili wa wabunge.https://youtu.be/_SPssVkz8NE
Baada ya kupokea maagizo ya Raisi John Magufuli hatimaye wizara ya afya yaanza rasmi utekelezaji wa maagizo hayo. https://youtu.be/S-ZkL8-5AoU
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imetekeleza maagizo ya Raisi Dk.Magufuli kwa kutengeneza mashine moja ya MRI; https://youtu.be/cd8ud8lq9cU
Walemavu wa macho nchini wameshauriwa kujishighulisha na kazi ndogo ndogo ili kujikwamua na hali ngumu ya maisha; https://youtu.be/hrE4zhfI3cY
Serikali imesema itamchukulia hatua kali mkandarasi CJ anayetengeneza barabara ya RUAHA hadi Sali- Ulanga mkoani Morogoro; https://youtu.be/3ccJNE1n2y4
Tanzania yashauriwa kuwekeza zaidi kwenye mafuta na gesi ili kujenga uchumi endelevu wa taifa; https://youtu.be/ulDXno0TeM0
Raisi Putin wa Urusi ameagiza uchunguzi ufanyike kwa wanariadha wa taifa hilo wanaotuhumiwa kwa matumizi ya dawa ya kuongeza nguvu;https://youtu.be/Ppkez474kms
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh.Gallawa amesema mkoa wake uko tayari kupokea ugeni wa bunge jipya la 11 wiki ijayo; https://youtu.be/QCcNSyf41Q0
Wanachama wa Chama Chama Mapinduzi wameendelea kujitokeza kwa wingi kuwania kiti cha Usipika na unaibuka Sipika; https://youtu.be/Bi8ZFd-ov8I
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Kandoro ameziagiza halimashauri zote za Mbeya kuunda sheria zitakazotumika kulinda mazingira bonde la Rukwa;https://youtu.be/cMjPk43biV
Halimashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imewasimamisha watumishi wanne kwa matumizi mabaya ya fedha; https://youtu.be/JIFGrunWsuo
Taasisi ya kifedha ya Benki M na taasisi ya Hassani Maajr Trust waingia ubia kusaidia elimu nchini; https://youtu.be/E_7Y0jbnBD4
Wajasiriamali vijana nchini wameshauriwa kuwa wabunifu zaidi kwa mafanikio bora ya biashara zao; https://youtu.be/L9cxozsEpGI
Umoja wa benki za AKIBA kwa nchi za Afrika Mashariki zimesema zinashindwa kuendelea kwa kukosa wateja; https://youtu.be/Q2WenWLfxwg
Baraza la Sanaa la Taifa nchini BASATA limeshauriwa kuwatafutia masoko wasanii wa kitanzania kwa kukuza pato la msanii na taifa kwa ujumla;https://youtu.be/za4PAdhYyDE
0 |
|
0 |
|
Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Mbazi Msuya (wa katika) akieleza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka (wa kwanza kulia) wakati wa ziara ya kukagua mtaro uliojengwa eneo la Buguruni kwa Mnyamani.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka (wa kwanza kulia mwenye miwani) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki wakiangalia hali ya daraja la Buguruni Visiwani walipofanya ziara ya maeneo yaliyoathiriwa na ugonjwa wa kipindupindu.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 |
|
0 |
|
Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais leo Novemba 12, 2015
Rais Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono kwa furaha na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Obeni Sefue alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais
Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati akiongea kabla ya kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea kwa furaha hati ya makabadhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2015
![]() |
Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea kwa furaha hati ya makabadhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2015 |
Rais Dkt John Pombe Magufuli akiiangalia kwa furaha hati ya makabadhiano ya Ofisi aliyoipokea kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2015
Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Makiamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi baada ya hafla ya makabidhiano rasmi ya Ofisi Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi leo Novemba 12, 2015
Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Makiamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya hafla ya makabidhiano rasmi ya Ofisi Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi leo Novemba 12, 2015.
TAARIFA YA MAKABIDHIANO RASMI YA OFISI IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, leo katika Ikulu ya Dar es Salaam amepokea taarifa rasmi ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo mchana na kushuhudiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Maafisa wa Ofisi Binafsi ya Rais.
Utaratibu wa kukabidhiana Ofisi katika Ofisi Kuu hapa nchini ni jambo la kawaida na hivyo imebidi makabidhiano hayo kati ya Rais anayeondoka na anaye ingia madarakani kufanyika.
“Umeanza vizuri, baki na msimamo huo huo utasaidia sana wananchi” . Mhe. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne amemueleza Mhe. Rais Magufuli wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.
Mhe. Rais Mstaafu amekabidhi taarifa rasmi yenye kurasa 53, ambayo kwa ujumla inaelezea kazi zilizokwisha kufanyika, ambazo zinasubiri kukamilika na zile ambazo zinasubiri maamuzi ya utekelezaji. Mengine ni hali halisi ya nchi katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Mhe. Rais Dkt. Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kwa muongozo wake siku zote .“Nikushukuru kwa kuiacha nchi salama na itaendelea kuwa salama, nikushukuru kwa muongozo wako, na taarifa ya muelekeo na ninaahidi kuwa Hapa ni Kazi Tu”.
Mhe. Rais amesema na kumueleza Rais Mstaafu kuwa ametengeneza mazingira mazuri ambayo nchi nyingi zimeshindwa kufanya na hivyo basi kuahidi kuendelea kuchota hekima na busara kwa Marais wote wastaafu wakiwemo Mhe. Benjamin William Mkapa wa Awamu ya Tatu na Mzee Ally Hassan Mwinyi wa Awamu ya pili.
Wakati huo huo Mhe. Rais Magufuli ameendelea kupokea salamu za pongezi kutoka Kwa Msimamizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bibi Helen Clark.
“Chini ya uongozi wako, tunatarajia kuzidi kuimarisha ushirikiano baina yetu, demokrasia, kushughulikia masuala ya umaskini na ajira kwa vijana , kukuza uchumi, na kulinda na kuhifadhi mazingira, masuala ambayo Tanzania na UNDP tumekuwa tukishirikiana kuyaendeleza na kuyatimiza” amesema Bi Clark.
Salamu zingine ni kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Uswiss, Mhe. Simonetta Sommaruga, Rais wa Jamhuri ya Italia Mhe. Sergio Mattarella, Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Joachim Gauck na pia kutoka kwa Rais wa Finland Mhe. Sauli Niinisto.
Pongezi zingine zimetoka kwa Rais wa Jamhuri ya Urusi, Mhe. Vladimir Putin, Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Salva Kiir Mayardit, Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Park Geun-hye na kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. XI Jinping.
Salamu pia zimemfikia Mhe. Rais Dkt. Magufuli kutoka kwa Rais wa Taifa la Eritrea Mhe. Isaias Afwerki na kutoka kwa Rais wa Ufaransa Mhe. Francois Hollande.Katika ujumbe wao, viongozi hao mbali na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamesisitiza kuendeleza na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi zao.
Pia wameipongeza Tanzania kwa kudumisha demokrasia imara na Watanzania kwa ujumla kwa kuimarisha amani na utulivu wakati wa Uchaguzi Mkuu.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi.
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
12 Novemba, 2015
Matthew Rycroft, Mwakilishi wa Kudumu wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa na Rais wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa mwezi Novemba, akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani, mara baada ya Baraza Kuu la Usalama kumaliza kikao chake kilichojadili hali ya Burundi, kikao ambacho pia kilipitisha azimio ambalo pamoja na mambo mengine linamuunga mkono Rais wa Uganda Yoweri Museven ambaye aliteuliwa na Viongozi wenzie wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa msimamizi na mwezeshaji wa majadiliano kati ya pande zinazopinga nchini Burundi.
Na Mwandishi Maalum, New York
BARAZA Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali hali ya kuendelea kwa matukio ya mauaji, utesaji na vitendo vingine vya vinavyokiuka haki za binadamu nchini Burundi.
Pamoja na kukemea hali hiyo, Baraza Kuu la Usalama limeeleza kusudio la kuchukua hatua zaidi kwa nchi hiyo ya Burundi. Pamoja na kumwomba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, katika kipindi cha siku kumi na tano awasilishe mbele ya Baraza hilo taarifa kuhusu uwepo wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi katika siku za baadaye.
Jana ( Alhamisi) Baraza hilo lilikutana katika kikao chake cha 7557 ajenda ilikuwa ni Burundi ambapo, Baraza kwa kauli moja lilipitisha Azimio namba 2248 (2015). Kupitia Azimio hilo, Baraza limetoa wito kwa pande zote nchini Burundi kujiepusha na kukataa fujo ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kutishia Amani na utulivu wa taifa hilo.
Vile Vile Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo kwa mwezi huu wa Novemba Rais wake ni Uingereza limekema vikali kauli za uchochezi zinazotolewa na baadhi ya watu ndani na nje ya Burundi, kauli ambazo kwa mujibu wa Baraza hilo zinalenga katika kushawishi chuki baina ya makundi ya watu nchini humo.
Kufuatia kauli hizo za uchochezi, Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, limeitaka Serikali ya Burundi kuheshimu, kulinda na kuhakikisha haki za binadamu na misingi ya uhuru, kuheshimu utawala wa sheria pamoja na uwajibikaji wa uwazi dhidi ya fujo na itoe ushirikiano kwa Ofisi ya Kamisheni ya Haki za Binadamu.
Kupitia Azimio hilo Baraza Kuu pia limeitaka serikali ya Burundi kuwawajibisha wale wote watakaopatikana na hatia ya ukiukwaji ya Sheria ya Kimataifa ya haki za binadamu na unyanyasajji wa haki za binadamu.
Aidha kupitia Azimio hilo, Baraza Kuu la Usalama limetoa wito kwa Serikali ya Burundi kutoa ushirikiano katika majadiliano yanayoongozwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki na ambayo yameridhiwa na Umoja wa Afrika na limetaka kuitishwa haraka majadiliano yatakayokuwa jumuishi yakiwashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Burundi ili kutafuta muafaka utakaokubaliwa na pande zote.
Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa pia kupitia Azimio hilo limesema linamuunga mkono kwa nguvu zote mwezeshaji wa majadiliano hayo ambaye ni Rais Yower Museveni wa Uganda aliyeteuliwa na Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Katika kusaidia mchakato wa majadiliano hayo, Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa limemkaribisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupeleka timu ya wataalam ambao kwa kushirikiana na Serikali, Umoja wa Afrika na wadau wengine watabuni mbinu za kushughulikia matatizo ya kisiasa na kiusalama.
0 |
|
0 |
|
NAPENDA KUWATAARIFU WATANZANIA WANAOISHI GREATER VANCOUVER AREA, KWAMBA TAREHE 27 HADI 28 NOVEMBA 2015, AFISA KUTOKA UBALOZI WA TANZANIA CANADA (OTTAWA), ATAKUWA MJINI VANCOUVER, BC, KWA AJILI YA KUPROCESS APPLICATIONS KWA AJILI YA PASSPORT RENEWAL.
UJIO HUU UTAGHARAMIWA NA WATANZANIA WATAKAOHITAJI KURENEW PASSPORT ZAO, GHARAMA HIZI NI FLIGHT NA HOTELI. KWA MAWASILIANO ZAIDI TAFADHALI WASILIANA NA PHILIP MWIMANZI KUPITIA NAMBA YA SIMU 16046521864. NI VIZURI TUKAWASILIANA ASAP ILI TUJUE IDADI YA FOMU ZITAKAZOHITAJIKA, ASANTENI.
0 |
|
0 |
|
Meza Kuu , Kutoka Kushoto ni Ndugu Maumba Mgaya, Mwenyekiti wa Jumuiya, Bi Magreth Mjindo na Ndugu Andrew Katibu.
Mnano tarehe 7/11/2015, Jumuiya ya watanzania waishio nchini Thailand ilikutana na kujadiliana mambo mbalimbali ya jinsi gani wanaweza kusaidiana katika mambo mbalimbali, TIT ilianzishwa mnano mwezi wa nne mwaka, 2015 na inahusisha watanzania mbalimbali, wanafunzi,wafanyabishara na wafanyakazi waishio na kufanya nchini Thailand. Mkutano mkuu wa Jumuiya ulifanyika katika Hoteli ya Amari Boulevard Mjini Bangkok na kuhudhuriwa na wanajumiya mbalimbali.
Pamoja na kujadiliana mambo mbalimbali kulifanyika uchaguzi wa viongozi ambapo wafuatao walichaguliwa kuwa viongozi wa jumuiya kwa kipindi cha mwaka mmoja:
Mwenyekiti: Bwana Maumba Mgaya
M/Kiti: Bw. Alois Ngonyani
Katibu: Bw.Andrew Wajama
Katibu Msaidizi: Bw. Emmanuel Mushi
Mhazini: Bw. Adolf Kigombola
Mhazini Msaidizi: Bi.Tumaini Kalindile
Afisa Mawasiliano: Bw. Emmanuel Nyamageni
Afisa Mawasiliano Msaidizi: Bw. Jordan Hossea.
M/Kiti: Bw. Alois Ngonyani
Katibu: Bw.Andrew Wajama
Katibu Msaidizi: Bw. Emmanuel Mushi
Mhazini: Bw. Adolf Kigombola
Mhazini Msaidizi: Bi.Tumaini Kalindile
Afisa Mawasiliano: Bw. Emmanuel Nyamageni
Afisa Mawasiliano Msaidizi: Bw. Jordan Hossea.
Pamoja na uchaguzi kulifanyika sherehe fupi ya kumpongeza Bi Magreth Dionis Mjindo ambaye amemaliza Shahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii na anarejea nyumbani kulitumikia Taifa.
Jumuiya inapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadhamini wao Ndugu Florean Rwehumbiza, Dada Lucy Kileo pamoja na Ndugu Kivea Mbwana (Homeboy) kwa kusimamia uchaguzi na kufanikisha kufanyika kwa mkutano huu muhimu. Shukrani za pekee ziende kwa Kampuni ya Broadhurst Pacific, kwa kusimamia, kudhamini na kufanikisha tukio hili muhimu.
Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi akizugumza siku ya Alhamis wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipokuwa likijadili Taarifa ya mwaka ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi Maalum, New York
Tanzania imekaribisha juhudi zinazochuliwa na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa za kuboresha uwazi na utendaji wenye tija wa chombo hicho juhudi ambazo pia zinahusisha mijadala ya wazi.
Hayo yameelezwa na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lilipokuwa likijadili Taarifa ya Mwaka ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Taarifa hiyo iliwasilishwa siku ya alhamisi na Mwakilishi wa Kudumu wa Uingereza, Balozi Matthew Rycroft ambaye nchi yake ndiye Rais wa Baraza Kuu la Usalama kwa mwezi huu wa Novemba.
Taaria hiyo ambayo ni ya kuanzia Agosti Mosi 2014 hadi Julai 31 2015 imeanisha mikutano ya wazi na ya ndani iliyofanywa na Baraza kwa kipindi hicho, maazimio yaliyopitishwa, taarifa za rais wa Baraza kwa mwezi, na ziara za kikazi zilizofanywa na wajumbe wa Baraza. ambaye ni Mwakilishi wa Kudumu wa Uingereza Balozi katika Umoja wa Mataifa.
Balozi Mwinyi, amesema mijadala ya wazi inayoandaliwa na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa inatoa fursa na kufungua milango kwa nchi nyingi zaidi kushiriki nje ya wajumbe 15 wa Baraza na kwamba Tanzania ni kati ya nchi ambazo zimekuwa ikishiriki mijadala hiyo ya wazi.
Pamoja na kupongeza juhudi hizo, Mwakilishi huyo wa Tanzania, amesema, ni matumaini ya Tanzania kuwa katika siku za usoni, Baraza Kuu la litaanda mijadala katika namna ambayo itawezesha wajumbe kuzingatia hoja zilizotolewa na washiriki wengine kabla ya kupitisha matokoe ya mijadala hiyo.
Vilevile Balozi Mwinyi amesema, juhudi zinazochukuliwa na wadau mbalimbali za kudhibiti matumizi ya kura ya turufu hasa katika kuzuia mauaji ya halaiki, ni juhudi sahihi na zinazopashwa kuugwa mkono.
Akizungumzia zaidi matumizi ya kura ya turufu, Balozi Ramadhan Mwinyi ametoa wito kwa mataifa yenye hadhi ya kutumia kura hiyo kuhakikisha kwamba wanaitumia pale tu inapobidi na kwa kuzingatia matakwa na mamlaka zilizoainishwa Katiba ya Umoja wa Mataifa.
“ Tuna toa wito wa Baraza kuu la Usalama la Umoja wa mataifa, kuingiza katika taarifa zake za baadaye kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, tathmini ya matokeo ya maamuzi pale kura ya turufu ilipotumika na matokeo ya pale ambapo kura ya turufu haikutumika katika maamuzi yaliyofikiwa” akasisitiza Balozi Mwinyi.
Kuhusu yaliyomo katika taarifa hiyo, Balozi amesema, Tanzania inaungana na nchi nyingine katika kutaka taarifa hizo ziwe na uchambuzi wa kina na zilizo makini badala ya kuorothesha kazi za Baraza hilo kama ilivyo sasa.
Tanzania pia kupitia Mwakilisihi wake , imekaribisha namna ambavyo Baraza Kuu la Usalama linavyopanua wigo wa majadiliano na Vyombo vingine zikiwamo Asasi za kijamii na wanazuoni katika kujadilia masuala mtambuka.
“ Hata hivyo tumegundua kuwa baadhi ya mada zinazojadiliwa siyo tu zimekuwa zikiwagawa washiriki lakini pia zinakuwa nje ya mamlaka ya Baraza. Tunaomba tukumbushe kwamba Baraza Kuu la Usalama kama Chombo wakilishi cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Baraza linatakiwa kujiepusha mada ambazo hazina tija”.
Baadhi ya wazungumzaji wengine waliochangia taarifa hiyo ya Baraza Kuu la Usalama, wameelezea kwamba licha ya utekelezaji wa mamlaka ya Baraza hilo katika kusimamia Amani na usalama wa kimataifa, Baraza limeshindwa kabisa kumaliza baadhi ya migogoro kama ule wa Syria ambao umedumu kwa muda mrefu.
SIMU.TV: Rais Magufuli akabidhiwa ofisi rasmi, kufutwa uchaguzi Zanzibar kaa la moto. Bunge la 11 kuanza leo kwa usajili wa wabunge;
SIMU.TV: Philip Marmo, Ndungai wazidisha joto uspika, CCM yazoa viti maalum 1,021 vya udiwani, wane waimamishwa kazi halmashauri ya Hai; https://youtu.be/FxYZqMCAsGQ
SIMU.TV: Maduka ya dawa binafsi Muhimbili kufungwa, serikali kuanzisha maduka yake ndani ya hospitali zote za serikali; https://youtu.be/ZlfbjFp8bs8
SIMU.TV: Pata dondoo za habari za kina za kisiasa, michezo na burudani zilizotawala magazeti ya leo;https://youtu.be/YFkLwTtiMh8
Mshindi wa shindano la muziki la Airtel Trace Music Stars Afrika Nalimi Mayunga anatarajiwa kuondoka nchini jumatatu ya tarehe 16 novemba kwenda Marekani kwaajili ya mafunzo na kurekodi single yake na mwanamuziki Nguli Duniani, Msenegal Akon.
Mayunga aliibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Afrika katika mashindano yaliyoshirikisha nchi 13 barani Afrika yaliyofanyika nchini Kenya mwanzoni mwa mwaka huu na kujishindia zawadi nono ikiwemo deal ya kurekodi wimbo na video pamoja na kupata mafunzo ya mzuki kutoka kwa mwana muziki Akon nchini marekani.
Akiongea na waandishi wa habari, Afisa Uhusiano wa Airtel Bwana Jane Matinde alisema" Tunajisikia furaha kuwawezesha vijana wa kitanzania kupata fulsa na kufikia ndoto zao kupitia program zetu mbalimbali ikiwemo hii ya Airtel Trace Music Stars. tunajivumia kumuwezesha Mayunga na kumpatai fulsa ya kujinoa kimuziki lakini pia kutanganza nchi yetu na muziki wetu ulimwenguni.
Ni matumaini yetu kuwa , program hii itamuwezesha mayunga na vijana wengine watakao pata nafasi ya kushiriki kubadilisha maisha yao na kuwa wanamuziki bora ndani na nje ya nchi na kuweza kutumia vipaji vyao kama mtaji katika kuendesha maisha yao na famila zao kwa ujumla Kwa upande wake Nalimi Mayunga aliwashukuru Airtel kwa kumpatia nafasi hii ya pekee na kuhaidi kutumia fulsa hii vyema.
"kwangu huu ni muujiza wa pekee kupata nafasi ya kurekodi wimbo na kupata mafunzo toka kwa Akon, nawashukuru sana Airtel kwani mimi binafsi nisingeweza kuonana na Akon lakini kwa kupitia program hii na ushindi nilioupata sasa naondoka kwenda kunolewa na kupata ujuzi toka kwa Akon. Natoa wito kwa vijana wenzangu kutokata tamaa katika kufikia ndoto zao na kushirikia katika mashindano kama haya pindi yanapotangazwa kwani nao wanaweza kupata nafasi kama mimi leo Nimejiandaa vyema kuwakilisha nchi yangu na kurekodi single yangu na Akon hivyo naomba watanzania waendelee kuniunga mkono ili niweze kuwa mwanamuziki nyota duniani.
Kufatia ushindi huo Airtel na Trace imesamwezesha mayunga kurekodi single yake nchi South Afrika ijulikanayo kama " nice couple" nyimbo hii inapatikana youtube na pia inapigwa katika vyombo mbalimbali vya habari.
![]() |
Wafanyakazi wa Vodacom,Kana ya Kaskazini wakisikiliza kwa makini maelezo ya Lisa Wolker (hayupo pichani). |
![]() |
Baadhi ya Kompyuta zilizotolewa na Kampuni ya Vodacom kama msaada wa shule ya sekondari ya Shimbwe iliyopo wilayani Moshi vijijini. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA. |
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii, Teresia Irafay akifungua warsha ya wiki moja ya mafunzo juu ya elimu ya Afya ya Uzazi na Maadili iliyojumuisha wakunga wa Jadi, Waganga wa tiba asili, viongozi wa dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii iliyowaleta pamoja wadau mbalimbali katika ngazi ya vitongoji, vijiji na wilaya kujifunza namna ya kufanya kazi shirikishi ili kuleta mabadiliko katika jamii inayofanyika katika hoteli ya Domel-Wasso, tarafa ya Lolilondo katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu, Loliondo
IDADI ya wanawake wanaokeketwa Loliondo wilaya ya Ngorongoro imepungua kufikia asilimia 75 kwa mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto, Loliondo, Bi. Nailejileji Joseph katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii kwenye warsha ya wiki moja ya mafunzo juu ya Elimu ya Afya ya Uzazi na Maadili.
Warsha hiyo inajumuisha wakunga wa Jadi, Waganga wa tiba asili, viongozi wa dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii.
Wadau hao wanatoka ngazi mbalimbali ya vitongoji, vijiji na wilaya.
Lengo la warsha hiyo ni kujifunza namna ya kufanya kazi shirikishi ili kuleta mabadiliko sahihi katika jamii inayofanyika katika hoteli ya Domel-Wasso, tarafa ya Lolilondo katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Bi Nailejileji alisema idadi ya ukeketaji Loliondo inaonyesha kupungua hadi kufikia 57% mwaka 2015 ikilinganishwa na 87% mwaka 2014 kwa wanawake waliojifungulia hospitalini.
Alisema kwamba matokeo hayo yamefanikiwa kutokana na mkakati maalum unaofanyika shuleni kwa kuanzisha vituo vya kirafiki kwa vijana vinavyolenga kutoa elimu na hamasa kuhusu masuala ya ukeketaji.
Aidha mafanikio hayo ni miongoni mwa jitihada za Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kueneza hamasa shirikishi katika jamii, kuelezea ukubwa wa tatizo, athari zinazotokana na ukeketaji kwa kuwashirikisha wazee wa kimila wa jamii ya Kimasai (Laigwanan) kuchukua hatua zipasazo kukomesha ukatili huu dhidi ya wasichana.
Wazee wa kimila wa kimasai ni watu wenye kuheshimika na kusikilizwa kwenye jamii pale wanapotoa matamko mbalimbali yanayopelekea kuleta mabadiliko katika jamii ambao wanaonekana kuwa na uwezo mkubwa katika kukomesha ukeketaji na ndoa za utotoni kwa watoto wa kike ambao huozwa baada ya kufanyiwa ukeketaji mwezi Desemba kila mwaka.
SOMA ZAIDI HAPA
SOMA ZAIDI HAPA
0 |
|
0 |
|
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kushoto), akisalimiana na Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel Mgonja , wakati wa ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji,Kurasini jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile (kushoto), akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, baadhi ya Ofisi za Idara ya Uhamiaji, wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara katika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai),akipewa maelezo alipotembelea Dawati la Mapokezi wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji,Kurasini, jijijni Dar es Salaam.
0 |
|
0 |
|
Na Dixon Busagaga
Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
HALMASHAURI ya wilaya ya Hai,mkoani Kilimanjaro, imewasimamisha kazi watumishi wake wanne kwa tuhuma za kughushi hati za mishahara na kughushi nyaraka zilizofanikisha kuchukua jumla ya kiasi cha sh Mil 73.4 zikiwemo fedha za malipo ya muda wa kazi wa ziada kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali teule ya Machame.
Tuhuma hizo pia zina mtaja Mweka hazina wa Hosptali hiyo anayedaiwa kushirikiana na watumishi wa halmashauri hiyo kufanya ubadhirifu wa fedha na kwamba tayari Uongozi wa hosptali hiyo iliyo chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Kaskazini ,umekwisha mfukuza kazi.
Watumishi wawili kati ya wanne wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbili tofauti,moja ni kughushi hati za mishahara,vitambulisho na sahihi za watumishi waliostaafu na wengine kuacha kazi na kuchukua mikopo wa Mil 35 katika benki ya CRDB kwa majina ya watumishi walioacha kazi.

Mkuu wa Wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akisalimiana na wananchi alipofanya ziara katika hosptali teule ya Machame na kuzungumza na wafanyakazi.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza na wafanyakazi wa Hosptali teule ya Machame (hawapo pichani).

Mkurugenzi wa Hosptali hiyo,Dkt Saitore Laizer akizungumza katika kikao hicho.