Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1024 | 1025 | (Page 1026) | 1027 | 1028 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Hatimaye Shindano la Bongo Style linalo andaliwa na Faru Arts and Sports Development Organization(FASDO) lililo anzishwa mwaka huu na ambalo litakuwa  likifanyika kila mwaka lililowahusisha vijana wenye umri kati ya Miaka 18-25 wakiwemo wapiga picha na wabunifu wa mavazi 20 waliokuwa wamechaguliwa kuingia Nusu   Fainali baada ya kujiandikisha kushiriki  shindano hili kwa kupitia  tovuti ya FASDO www.fasdo.org na kuchaguliwa toka kwa washiriki 300 waliojiandikisha limefikia hatua ya Fainali.

  Katika hatua hiyo ambayo ilikuwa ngumu kutokana na kuwa kila mshiriki alikuwa na radha yake tofauti ya ubunifu katika kazi yake kwa vipengele vyote viwili picha na ubunifu wa mavazi, ambapo wamepatikana washiriki 10 ambao ndio wanaendelea na Shindano hili mpaka siku ya Fainali tarehe 28.11.2015, zitakazofanyika katika ukumbi wa ndani wa Alliance Francaise Jijini Dar es salaam.

  Vijana hao walioshinda hatua ya Fainali kwa upande wa Picha ni pamoja na Rasheed H Rasheed Hamis (24) Dar es salaam, Daniel Msirikale (24) Dar es salaam, Hassan Mohamed (24) Dar es salaam, Aneth Ngowano (21) Dar es salaam na Trevor Gaudence (23) Dar es salaam. Kwa upande wa ubunifu wa mavazi waliopita ni pamoja na Jocktan Makeke(25) Iringa, Winfrida Touwa (21) Mwanza, Anna Ben Paul (23) Dar es salaam, Lilian Ndashau (24) Dar es salaam na Shahbaaz Yusuph (19) Dar es salaam.

  Akieleza juu ya shindano hili baada ya kupatikana majina ya watakao ingia fainali, Mratibu wa FASDO Tanzania Joyce Msigwa alisema washindi wawili kati ya kipengele cha picha na ubunifu wa mavazi watapata Tsh 1,000,000 kila mmoja na  nafasi ya kwenda Uberigiji kwa wiki mbili. Aliongeza  kuwa washiriki wote wa nusu fainali  watapata nafasi ya kutangaziwa kazi zao bure kwa muda wa mwaka mmoja na kushiriki katika masomo/mafunzo mbalimbali pindi yatakapo tokea, mwisho alisema shindano hili litakuwa linafanyika kila mwaka.
  Majaji kwa upande wa Ubunifu wa Mavazi na Picha wakiwa kazini.  

  Mmoja wa washiriki upande wa Ubunifu wa Mavazi(aliyesimama kulia) akielezea kazi zake kwa majaji 
  Akiwa mwenye nyuso ya Furaha mmoja wa washiriki wa Shindano la Bongo Style kwa upande wa Mavazi akiwa ameshika picha ya mfano wa mshono wake ambao amebuni yeye mwenyewe, ambapo Msaani Maarufu Wema Sepetu amemuomba amshonee Mshono huo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0  0 0

  SIMU.TV: Rais Magufuli akabidhiwa ofisi rasmi, kufutwa uchaguzi Zanzibar kaa la moto. Bunge la 11 kuanza leo kwa usajili wa wabunge; https://youtu.be/EXIHGwof-90 

  SIMU.TV: Philip Marmo, Ndungai wazidisha joto uspika, CCM yazoa viti maalum 1,021 vya udiwani, wane waimamishwa kazi halmashauri ya Hai;  https://youtu.be/FxYZqMCAsGQ

  SIMU.TV: Maduka ya dawa binafsi Muhimbili kufungwa, serikali kuanzisha maduka yake ndani ya hospitali zote za serikali; https://youtu.be/ZlfbjFp8bs8

  SIMU.TV: Pata dondoo za habari za kina za kisiasa, michezo na burudani zilizotawala magazeti ya leo; https://youtu.be/YFkLwTtiMh8

  0 0  0 0
 • 11/13/15--01:34: BEI YA MADAFU LEO


 • 0 0


  Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa ofisi ndogo za Bunge  jijini Dar es Salaam kuhusiana na kuachana na uongozi katika siasa.

  ALIYEKUWA Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda amejing'atua rasmi na kuachana na  uongozi katika siasa kutokana na kufanya kazi za Siasa kwa miaka 40.

  ameyasema hayo alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam leo.

  Anne amesema kuwa "Sitagombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  wala sitachukua fomu ya kugombea nafasi ya uspika wala sifikilii kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika"

  Aidha Anne amesema kuwa katika awamu yake ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kulikuwa na changamoto nyingi kutokana na kuwepo na wabunge vijana.

  Hata hivyo kuwa na changamoto nyingi ila amesema kuwa alilifurahiya sana Bunge hilo kutokana na kuwaelewa wabunge mbalimbali tabia zao hasa wakiwa Bungeni.

  Anne amepsema kuwa Spika wa sasa atakaye shinda nafasi awe si mwepesi wa kukasirika kutokana na changamoto atakazo zipata Bungeni wakati wakijadilia masuala mbalimbali ya Serikali, pia awe mtulivu na kukabiliana na changamoto zitakazo jitokeza.
   Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
  Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza nao leo katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.


  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala akizungumza nawanahabari pamoja na Waganga wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro juu ya tishio la ugonjwa hatari wa Kipindupindu.
  Baadhi ya Waganga wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Amos Makala ,(hayupo pichani).
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Novemba 13, 2015.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa taarifa fupi ya Hali ya Magereza nchini kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo(katikati). Naibu Katibu Mkuu  yupo katika ziara ya kikazi katika Idara mbalimbali zinazounda Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi(wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Stephen Pancras.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Wandamizi wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo leo Novemba 13, 2015( wa tatu kutoka kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga.
  (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Shirika la Hifadhi za Taifa limezindua program maalum ambapo tembo 30 wanaoongoza makundi 30 katika mfumo wa Ikolojia wa Ruaha Rungwa watavalishwa kola malum shingoni zenye vifaa vinavyorekodi mienendo yao kwa kutumia satelaiti. Program hii inafadhiliwa kwa pamoja na taasisi za Global Environment Facility pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP).

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa program hiyo hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi alisema kuwa “ Lengo kuu la program hii ni kupata taarifa za kina juu ya mienendo ya tembo katika mfumo wa ikolojia wa Ruaha Rungwa zitakazosaidia kubainisha maeneo ya shoroba na mitawanyiko kwa ajili ya ulinzi wa tembo”

  UNDP kupitia ushirika wake na TANAPA/SPANEST wametoa kandarasi ya kazi hii kwa taasisi ya World Elephant Centre ya nchini Tanzania inayotarajiwa kuongeza hali ya usalama wa tembo hifadhini.

  Teknolojia hiii inawezesha kujua mwenendo wa tembo ndani na nje ya hifadhi, kujua walipo, wanapopita, kasi yao ya kutembea, sehemu wanazojificha, wanazokunywa maji, wanazopumzika, maeneo wanayokaa kwa muda mrefu, kama wamekufa, wamejeruhiwa,wamehama hifadhi moja hadi nyingie na taarifa nyingine nyingi hivyo itakuwa rahisi kwa askari wa wanyamapori kufuatilia usalama wao.

  Kola hizo zenye uwezo wa kufanya kazi kwa miaka mitatu bila kubadili betri zake zinafungwa kwa Tembo 30 wanaoongoza makundi 30.
  Wataalam wa Uhifadhi wakiongozwa na Dk. Alfred Kikoti (wa kwanza kulia) wakiendelea na zoezi la uwekaji kola maalum kwa tembo zinazosaidia kudhibiti mienendo ya tembo ndani na nje ya hifadhi ya Mfumo wa Ikolojia wa Ruaha Rungwa.
  Zoezi la uvalishaji wa kola maalum kwa tembo katika hifadhi ya Ruaha likiendelea.
  Helikopta maalum inayotumiwa na madaktari kwa ajili ya kutambua na kupiga dawa ya usingizi kwa tembo kabla ya uvalishaji wa kola maalum.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Bondia Hamisi Mwakinyo kushoto akitunishiana misuli na Meshach Mwankemwa baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa taifa unaotambuliwa na  Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBC  katikati ni promomota kutoka katika kampuni ya Golden boy Afrika Shomari Kimbau Picha na SUPER D BOXING NESW.
  Promota Shomari Kimbau akiwainua mikono juu mabondia Asha Nzowa kushoto na Joyce Awino baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.


   Rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa akiwakumbusha baadhi ya sheria zitakazo tumika katika mchezo wa ngumi utakaofanyika kesho katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala Dar es salaam.

  NA Mwandishi Wetu
  MABONDIA Meshack Mwankemwa na Hamisi Mwakinyo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa kg 66 unaotambuliwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchi mkanda uho uliokuwa umeachwa wazi na bondia Selemani Zogo kwa kuto utetea kwa wakati sasa utapiganiwa na mabondia hawo kesho

  akizungumza wakati wa upimaji wa uzito promota wa mpambano uho Shomari Kimbau amesema mkanda uho utapiganiwa na mabondia hawo ili apatikane bingwa mpya wa uzito wa kg 66

  mpambano uho utasimamiwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini chini ya rais wake Chauremba Palasa aliongeza kwa kusema mbali na mpambano uho siku hiyo pia kutakuwa na ngumi za utangulizi za mabondia mbalimbali

  Said Mayanga atamenyana na Gido Selemani wakati Mohamed Amir atapambana na Hemed Hemed

  na mpambano mwingine wa kusisimua utakuwa ni wa akina mama ambapo bondia mnaschachali Asha Nzowa 'Asha Ngedere' atapambana na Joyce Awino ambambao ambao unasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wanawake wa mchezo wa masumbwi  


  Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
  Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

  pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

  0 0

   Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,ambaye pia ni Kamishna wa Operesheni, Rogatius Kipali (kulia), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, taarifa ya ujenzi la Jengo laa  linalotarajiwa kuwa Makao Makuu ya Jeshi hilo, alipotembelea Ofisi za Jeshi hilo zilizoko TAZARA ,jijini Dar es Salaam.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza  na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (hawapo pichani), alipotembelea Ofisi za Jeshi hilo zilizopo TAZARA ,jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (wa tatu kutoka kulia waliokaa),akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji muda mfupi baada ya kumaliza ziara ya kutembelea makao Makuu ya Jeshi hilo na Ofisi zilizopo Tazara,jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
  Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Mohamed Seif Khatib mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi,Ofisi Ndogo Lumumba.
   Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Sekretarieti Ndugu Anamringi Macha mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za CCM Lumumba.
   Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wapenzi na wanachama wa CCM waliojitokeza kumpokea kwenye Makao Makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisani kitabu cha wageni mara baada ya kuingia kwenye ofisi yake,waliosimama ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Mohamed Seif Khatib (kulia) na Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara) Ndugu Rajab Luhwavi.

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  SERIKALI imewaagiza watendaji wa Halmashauri zote za jijini Dar es Salaam kusimamia ipasavyo suala la usafi katika maeneo mbalimbali ili kusadia kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu.

  Katika agizo hilo la Serikali ametoa  wiki mbili kwa watendaji wote kuhakikisha wanaliweka jiji katika hali ya usafi na endapo halitatekelezwa hatua zitachukuliwa dhidi yao.

  Akizungumza na watendaji wa Serikali leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, amesema kuwa utekelezaji wa malengo waliyokuwa wamejiwekea tangu  2013.

  “Mlipuko wa ugonjwa wa kipindipindu umekuwa janga, kutokana na uchafu kukithiri katika jiji na kusababisha watu kupoteza maisha na wengine kuendelea kuugua,”alisema Sagini.
  Pia amewataka watendaji wa halmashauri kuwatengea maeneo maalum ya kufanyia biashara, mama lishe na baba lishe badala ya kuwafukuza.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasco), Mhandisi, Cyprian Luhemeja, alisema kipindupindu hakiwezi kumalizika jijini hapa kama Halmashauri hazitashirikiana na Dawassa na Dawasco.

  Alisema kutoshirikiana kwa halmashauri na mamlaka za maji, kuna sababisha ujenzi holela ambao unapita katika miundombinu ya maji taka.

  Pia alisema changamoto kubwa ambayo watu wengi hawaitambui ni kuhusu wasambazaji wa maji majumbani ambao ndio wamekuwa chanzo kikubwa cha kipindupindu.

  “Wasambazaji hawa wamekuwa wakati mwingine wanasafisha maji taka na kuyasambaza majumbani jambo ambalo linasababisha magonjwa hayo.
  Kutokana na hali hiyo sisi kama DAWASCO hatutamruhusu mtu kusambaza maji kama hana kibali maalumu kilichotoka kwetu,”alisema

  0 0

   Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
  WANANCHI wa Kata ya Saranga Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kujitokeza kupiga kura ya Diwani Novemba 15 mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty amesema kuwa kufanya uchaguzi huo kunatokana na kuharibika kwa uchaguzi wa Oktoba 25 ulisababishwa na vurugu.

  Amesema wananchi wanaotakiwa kupiga kura kwa kata hiyo ni wale waliojiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.
  Natty amesema waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura  ni 58,611 ambao ndio wataoruhusiwa kutimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura kwa diwani wanayemtaka kuongoza kata hiyo.

  Amesema vituo vya kupiga vitafunguliwa majira ya saa moja asubuhi na kufungwa saa 10 jioni na baada ya hapo zoezi likiwa limekamilika la uhesabiaji kura atatangazwa mshindi katika uchaguzi huo.

  Uchaguzi wa diwani katika kata hiyo ilitokana na vurugu kubwa ambazo zilianza majira ya 11:000 asubuhi ilifanywa na baadhi ya wasimamizi wa vituo na watu wasiojulikana katika cha kugawa vifaa eneo TANROAD Temboni.

  0 0

  Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Mbeya Ndugu Stellah Kategile akiwasilisha maada kwa wadau wa Sekta ya Afya Mkoani Mbeya katika kikao cha kujadili juu ya kuelekea katika siku ya maadhimisho ya Ukimwi Duniani Tarehe 1 Desemba mwaka huu.
  Mrakibu wa Polisi Mkuu  dawati la jinsi na watoto Mkoa wa mbeya Ndugu Debora Mrema akielezea masuala mbaliimbali  yanayolikumba Dawati hilo katika kupambana na ukatili wa kijinsi Mkoani humo huku akisisitiza juu ya wadau kujitokeza na kutoa michango yao ya kifedha sanjali na rasilimali nyingine ili kuweza kutoa elimu kwa jamii katika maeneo mbalimbali mkoani humo hususani maeneo ya vijijini.
  Wadau wakiendelea na majadiliano katika mkutano huo.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mjukuu wa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, Maryfaustna Mlyambina, aliyefariki Nov 11, 2015. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu zilifanyika leo Nov 13, 2015 Kimara jijini Dar es Salaam, na baadaye msiba huo kusafirishwa kuelekea Mkoani Mwanza kwa maziko.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
  Wazazi wa marehemu wakiwa na baadhi ya wanafamilia, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu.

  0 0

  Hatua ya serikali kutaka kuyafungia maduka yote ya madawa yaliyoko nje ya hospitali za serikali imepongezwa na baadhi ya wananchi na kutaka serikali kuharakisha mchakato huo. https://youtu.be/PKImj6aPKwM
  Kufuatia hali tete ya kisiasa iliyoko Zanzibar, mfumuko wa bei waelezwa kuongezeka na kuvunja rekodi visiwani humo. https://youtu.be/bbg383LfRv0

  Mtoto mwenye umri wa miaka 8 anayesoma darasa la pili aomba msaada wa wananchi msaada wa shilingi laki sita kwa ajili ya upasuaji.https://youtu.be/yRsJnEZ5aqo
  Wakazi mabalimbali wa jiji la Dar es salaam hasa wale waishio pembezoni mwa fukwe za Cocobeach wajitokeza kushuhudia samaki aina ya nyangumi mwenye tani 25 aliyetupwa na maji fukweni hapo. https://youtu.be/A2vYdiI6St8
  Harakati za kuwania kiti cha uspika wa bunge la 11 zaendelea kupamaba moto baada ya mbunge mteule wa Kasuru kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.https://youtu.be/lp_qzemGDYY
  Mchakato wa utoaji elimu bure waendelea kupamba moto baada ya katibu mkuu wa TAMISEMI kukutana na viongozi kulitilia mkazo. https://youtu.be/5MPKc55I8t0
  Wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro wamuomba raisi John Magufuli kutekeleza kwa vitendo aahadi ya kufufua viwanda nchini. https://youtu.be/cLjLCh-SwsU
  Wakulima wadogo nchini waiomba serikali nchini kuangalia namna ya kuboresha sera ya kilimo biashara ili wanufaike na kilimo hicho. https://youtu.be/k1i6TI6W6eI
  Gharama ya usafirishaji katika bandari ya Mtwara yalalamikiwa kuwa juu ukilinganisha na Bandari ya Dar es salaam. https://youtu.be/NYKl7oje_Yo

  Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu na serikali za mitaa TAMISEMI amesema mtumishi wa umma atakayeshindwa kuwajibika atakuwa kajifukuza kazi;httphttps://youtu.be/5ICIOZybiPE

  Wakala wa umeme vijijini REA imefanikiwa kufunga umeme kwa taasisi 18 wilayani Mbozi mkoani Mbeya; https://youtu.be/RLoy0CvFg70

  Baraza la usimamizi wa mazingira nchini NEMC limekifunga kiwanda cha plasitiki cha JIU RONG LIN kilichopo Dar es Salaam kwa kukiuka kanuni za utunzaji wa mazingira;https://youtu.be/ZXHJ6_l-clo

  Serikali mkoani Mara imetuma timu ya wataalamu wa afya vijijini kutoa elimu ya kupambana dhidi ya kipindupindu; https://youtu.be/qyRuGnunobo

  Baadhi ya wanawake wilayani Kahama waiomba serikali kuwachukulia hatua kali baadhi ya wananume wanaotumia vibaya  pesa za TASAF; https://youtu.be/-FH-AUozdHE

  Benki ya maendeo ya TID pamoja na manispaa ya Kinondoni wameingia makubaliano ujenzi wa  eneo la kupumzikia la Coco Beach; https://youtu.be/JZd4IBDQ-zg

  Serikali ya Tanzania na serikali ya China zimekubaliana kushirikiana katika biashara kwa lengo la kukuza uchumi wa Tanzania https://youtu.be/D_xETW3OO1k

  Mfumuko wa bei ya vyakula visiwani Zanzibar umeongezeka kwa kasi kutokana na wafanyabiashara kushindwa kuagiza bidhaa nje ya Zanzibar;https://youtu.be/GK6mw0qJdDY

  Kocha mkuu wa Taifa Stars, Boniphace Mkwasa amesema kuwa kikosi chake kitafanya vizuri dhidi ya timu ya taifa ya Algeria katika mchezo utakaochezwa jumamosi hii katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam https://youtu.be/1fs4TGNGXBs

  Baadhi ya wananchi mkoani Geita wamelalamikia uvamizi uliofanywa na wakala wa misitu na kupelekea kupoteza kwa mali zao; https://youtu.be/FRX1FMp9xKE

  Mkoa wa Manyara umejipanga  vilivyo kwa kuandaa mazingira safi ili kupambana na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu; https://youtu.be/BC_4WVAjE7Y

  Aliyekuwa Spika wa bunge serikali ya awamu ya nne,Mh.Anne Makinda amesema hatongombea na yake kuwatak wabunge wafanye kazi kwa manufaa ya taifa;https://youtu.be/FzQH8aQHmBA

  Uongozi wa shirika la simu la TTCL nchini limekanusha madai yaliyotolewa na chama cha wafanya kazi wa huduma za mawasiliano TEWUTA; https://youtu.be/p-4s-xwLLY8

  Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA imeendelea kuwatahadharisha wakazi wa mabondeni kuhusu mvua za vuli zinazoendelea kunyesha; https://youtu.be/aV4-vrnXwiU

  Tanzania kwa kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa la maendeleo ya viwanda UNIDO kwa pamoja wamezindua elimu kwa njia ya mtandao kwa lengo la kutoa elimu ya kusindika ngozi. https://youtu.be/gRCeqhgjA3U

  Watanzania wameshauriwa kutumia vyama vya ushirika kwa lengo la kujenga uchumi imara na endelevu; https://youtu.be/aNc-tPTrUuA

  Kocha mkuu wa Taifa Stars Boniphace Mkwasa amesema anaamini watafanikiwa kubuka na ushindi dhidi ya timu ya taifa ya Algeria; https://youtu.be/L_xS3R4dUG0

  Mrembo wa Tanzania mwaka 2014-15, Lilian Kamazma amesema atafanya vizuri katika  kuwania taji la mrembo wa dunia; https://youtu.be/ueH0J2rYfbw


  0 0


  0 0

  PHOTO: French fire brigade members aid an injured man near the Bataclan concert hall following fatal shootings in Paris.

  At least 153  people have been killed in multiple attacks in Paris, including one near a stadium where a soccer match was underway and another at a concert hall where a hostage situation is ongoing, French police said.

  Fifteen of the victims have been killed at the Bataclan concert hall in eastern Paris, where at least 100 hostages are believed to have been taken.

  Meanwhile, two explosions close to a stadium have reportedly killed three others and a gunman has attacked a restaurant in Paris with what is said to be a semi-automatic weapon.
  France's president Hollande has declared a state of emergency for all of France and has closed the borders.

  Mr Hollande was at the Stade de France Stadium, where France and Germany were playing a football match, near where two explosions were heard.older | 1 | .... | 1024 | 1025 | (Page 1026) | 1027 | 1028 | .... | 3348 | newer