Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1021 | 1022 | (Page 1023) | 1024 | 1025 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Mmoja ya washindi wa kitita cha shilingi Milioni 100 kupitia promosheni ya Jaymillions iliyokuwa inaendeshwa na Vodacom Tanzania iliyomalizika mwezi Aprili mwaka huu Irene Mrema, amesema tangu aibuke na ushindi amepata mafanikio makubwa mojawapo ikiwa ni kuweza kujenga nyumba ya kuishi na familia yake maeneo ya Goba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. 
  “Nashukuru Mwenyezi Mungu kwa kunikwamua kimaisha kupitia Jaymillion ya Vodacom kwa kuwa imeleta mafanikio makubwa katika maisha yangu na familia yangu kwa kuwa imetuwezesha kujenga na kumiliki nyumba nzuri ya kisasa ambayo tayari tumehamia pamoja na familia yangu”alisema. 
  Mbali na ujenzi wa nyumba hiyo Irene Mrema alieleza kuwa hivi anajipanga kufungua biashara ambayo bado anaifikiria kwa fedha alizosalia ili kuwezesha kukuza kipato cha familia 
  “Natarajia kufungua biashara katika siku za hivi karibuni kwa ajili ya kuniwezesha kijitegemea na kuongeza kipato cha familia” 
  Aliishukuru kampuni hiyo kwa kubuni promosheni zenye kuboresha maisha ya wateja wake na kuongeza kuwa fedha hizo alizoshinda zimeweza kusaidia katika mambo mbalimbali ya kijamii na akifungua biashara atatoa ajira kwa wafanyakazi ambao nao watanufaika na ushindi wake. 
  ”Mafanikio haya ambayo yanaonekana kwangu kama ndoto ukimwelezea mtu anaweza akashindwa kuamini hususani wale ambao wanakuwa na dhana kuwa promosheni za makampuni kwa wateja kama ilivyokuwa Jaymillion ni za uongo lakini napenda kuwahakikishia kwamba hakuna uongo,upendeleo wala kujuana bali ni bahati ya mtu na akishinda anapewa fedha zake kama ilivyotokea kwangu”,alisema Irene kwa furaha. 
   Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambaye alifanya ziara ya kufuatilia maendeleo ya washindi wa promosheni hiyo alisema amefurahishwa na hatua aliyofikia mshindi huyo ya kupiga hatua ya kimaendeleo kimaisha. 
  “Kwetu Vodacom mafanikio haya ya mteja ni faraja kubwa kwa kuwa mbali na kutoa huduma bora na kubuni huduma za kurahisisha maisha ya wateja pia ni kufanya maisha ya wateja wetu kuwa murua kupitia promosheni zetu”, alisema Nkurlu. 
   Alisema promosheni za kukwamua maisha ya wateja zikiwa na tija na kuleta mafanikio kwa wateja zinahamasisha kampuni kuendelea kubuni promosheni zingine ili ziweze kubadilisha maisha ya wateja wengi zaidi 
  Alimalizia kwa kuwataka wateja wa mtandao huo kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo na zitakazokuwepo katika siku za usoni.
   Irene Mrema aliyekuwa mmoja wa washindi wa kitita cha shilingi Milioni 100 kupitia promosheni ya Jaymillions iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom Tanzania(kushoto) akimwelezea Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu(kulia)alipomtembelea nyumbani kwake kujua maendeleo ya mafanikio aliyoyapata baada ya ushindi wake likiwemo la kumalizia nyumba ya kisasa anayoishi na familia yake maeneo ya Goba  jijini Dar es Salaam.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akisalimiana na Irene Mrema aliyekuwa mmoja wa washindi wa kitita cha shilingi Milioni 100 kupitia promosheni ya Jaymillions iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni hiyo,Alipomtembelea nyumbani kwake kujua maendeleo ya mafanikio aliyoyapata baada ya ushindi wake likiwemo la kumalizia nyumba ya kisasa anayoishi na familia yake maeneo ya Goba  jijini Dar es Salaam.
  Nyumba ya Irene Mrema anayoishi na familia yake Goba jijini Dar es Salaam aliyomalizia kuijenga baada ya kukabidhiwa kitita chake cha shilingi Milioni 100 alichojishindia mwezi wa Nne kupitia promosheni ya Jaymillions iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom Tanzania.


  0 0
 • 11/08/15--00:16: Article 3


 • 0 0
 • 11/08/15--01:30: SIMU TV: Magazeti NOV 8 2015
 • Fuatilia habari mbalimbali za kusisismua kupitia uchambuzi wa magazeti mbalimbali nchini uhabarike na mengi yaliyopewa uzito wa juu leo NOV.8-2015.https://youtu.be/cqQ6IQxg3kg

  Tazama uchambuzi wa magazeti ya michezo nchini upate kufahamu yaliyojiri ndani na katika anga za kimataifa tazama. https://youtu.be/E0uMGfMkg3w

  Fuatilia habari mbalimbali za kusisismua kupitia uchambuzi wa magazeti mbalimbali nchini uhabarike na mengi yaliyopewa uzito wa juu. https://youtu.be/kTeq8Svq_Zk

  0 0


  Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Dr. Helen K. Bisimba amepata ajali ya gari katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es salaam. Amekimbizwa hospitali tunaendelea kufuatilia maendeleo yake na kuwajulisha . Pichani juu na chini ndilo gari alilokuwa akisafiria.
  0 0


  0 0

  Wakaguzi toka ndani na nje na taasisi za serikali wafurahishwa na mafunzo waliyopatiwa kwani yataongeza tija katika kazi zao za ukaguzi.https://youtu.be/htloKTOxl3M

  Mkuu wa wilaya ya Arusha awataka wakazi wa wilaya hiyo kuzingatia kanuni za afya ili kujikinga na kukomesha ugonjwa wa kipindupindu. https://youtu.be/OKiKkXELLFI
    
  Mkurugenzi wa hidhi za taifa hapa nchini asema TANAPA itaendelea na jitihada za kupambana na ujangili nchini ili kendeleza uhifadhi nchini.https://youtu.be/Q2OlWtUqnlk

  0 0

   Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa ya Afrika Kusini ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 (Amaglug-glug) Jumanne jioni kwenye dimba la Eldorado jijini Johannesburg.
  Kwa mujibu wa taarifa toka TFF, mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya maandalizi ya kuwakabili Algeria Novemba 14 jijini Dar es salaa katika uwanja wa Taifa na marudiano yake kufanyika Novemba 17 jiji Algiers kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
  Taifa Stars iliyokweka kambi nchini Afrika Kusini imekua ikifanya mazoezi kila siku katika uwanja wa Edenvale, baada ya kuwa na mazoezi ya stamina na pumzi kuweka uwiano sawa wa mazoezi (fitness level), Kocha wa Stars Charles Mkwasa sasa anaendelea na mazoezi ya kutengeza mfumo kwa wachezaji wake.
  Awali Stars ilikuwa icheze mechi mazoezi kesho Jumapili na timu ya University of Pretoria inayoshriki ligi kuu ya Afrika Kusni (PSL), lakini baada ya Chama cha Soka Afrika Kusini (SAFA) kuandaa mchezo  dhidi ya U23, sasa mchezo dhidi ya Tucks hautakuwepo.


  0 0

  DSC_0896
  Msanii nyota wa Afrika Kusini, Bo Denim "Bo" akitumbuiza jukwaani wakati wa tamasha la msimu wa pili la Karibu Music Festival..!

  Na Andrew Chale, Modewjiblog
  [BAGAMOYO-TANZANIA] Mwanamuziki nyota kutoka Afrika Kusini Bo Denim maarufu ‘Bo’ amewashukuru waandaji wa tamasha la Music Festival linalofanyika kila mwaka mjini hapa huku likihusisha vikundi na wanamuziki mbalimbali kutoka mataifaa tofauti ya Afrika nan je ya Afrikaa.
  Bo ambaye usiku wa jana Novemba 7, aliweza kupiga shoo hiyo kwa kiwango cha Kimataifa, alipata shangwe kwa mashabiki waliofurika kushuhudia tamasha hilo mjini hapa.
  Baada ya shoo hiyo Modewji ilipata kufanya naye mahojiano ambapo amepongeza muziki wa Tanzania wakiwemo wasanii wanaovuma nje ya mipaka ya Tanzania. “Wasanii wa Tanzania wanauwezo mkubwa. Nimeshuhudia kundi la Weusi wamefanya vizuri sana” ameeleza Bo.
  Tamasha hilo ambalo leo Novemba 8.2015, linatarajiwa kufikia tamati, linaratibiwa na Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO) na Legendary Music Entertainment and Promotions Co. Ltd, T kwa kushirikiana na kampuni ya kinywaji cha Jebel Coconut. Wadhaminiwa wengine ni pamoja na Swiss Embassy, Precision Air, Coca Cola, Mwananchi Communication, Kaya fm, Magic fm, Focus Outdoor, Jovago, Kaymu na Time tickets.
  DSC_0858
  DSC_0848
  Bo akipagawisha mashabiki ...
  DSC_0852
  Mambo yalikuwa hivi ..
  DSC_0910
  Host wa Karibu Music Festival 2015, Jazzphaa Nassor na Lulu wakishoo love wakati wa shoo hiyo ya "Bo"..

  0 0

   Mgeni rasmi katika Tamasha la kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani lililoandaliwa na Taasisi ya Dorice Mollel Foundation (DMF), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwa kwenye meza kuu na Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Anna Mgwhira (kushoto), Mkurugenzi wa Hunduma za Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibamayila (kulia) pamoja na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel, wakati wa muendelezo wa tamasha hilo lenye lengo la kufanya harambee kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa vifaa maalum vya kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), lilifanyika kwenye Viwanja wa Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo. Kilele cha kumbukumbu hiyo ya mtoto njiti Duniani kinatarajiwa kufanyika Novemba 17, 2015.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika Tamasha la kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani lililoandaliwa na Taasisi ya Dorice Mollel Foundation (DMF), lilifanyika kwenye Viwanja wa Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo. Akitoa hotuba yake, Makonda amesema kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali ili kuhakikisha watoto njiti wanapata huduma stahiki katika mazingira rafiki ili waweze kuishi kama watoto wengine.
  Mwenyekiti wa chama cha (ACT) Wazalendo, Anna Mgwhira ambaye alikuwa ni mmoja wa wageni waalikwa, akizungumza katika Tamasha hilo la kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani lilifanyika kwenye Viwanja wa Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo
  Mkurugenzi wa Hunduma za Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibamayila akizungumza katika hilo, lilifanyika kwenye Viwanja wa Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
  Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel akizungumza wakati akitoa shukrani kwa wadau mbali mbali waliolifanyikisha Tamasha hilo kwa namna moja ama nyingine.
  Sehem ya wadau mbali mbali na wananchi waliofika katika tamasha la kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani leo katika viwanja vya Leaders Clubu jijini Dar es Salaam (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii).  0 0


  0 0

  Out-going Presidential Communications Director at the State House Mr. Salvatory Rweyemamu speaks during one of the past many Press Conferences with his Assistant Ms. Premy Kibanga
  --------------------------------------------------------

  One of the most admirable attributes of this digital age sweeping our lives, is the capacity it has created for would be volunteers, who are in no way in shortage, in our society, to create and disseminate discriminatory information regarding other people.
  A good example is the nonsense information that has been doing the rounds in the last few hours about my departure, or imminent departure, from my position as the Presidential Communications Director at the State House.
  The truth of the matter is that during my eight plus years at the State House, I have signed numerous contracts, the last of which expired on September 11, this year, 2015 and it was renewed for a further 62 days.
  The end of this contract, as far as I am concerned, is Tuesday, November 10, this year 2015. I will officially hand over office tomorrow, Monday, Tuesday 9, 2015 to Ms. Premi Kibanga, my very able assistant for all those years. In fact today, Sunday, I was clearing my office and preparing my handover notes.
  I leave the State House a very happy person and I would like to thank President Dr. John Pombe Joseph Magufuli and the 4th President of our country HE Jakaya Mrisho Kikwete for their trust in my capacity to be their assistant and the opportunity they gave me to serve our people and our country at this level.
  I would also like to thank all the State House staff under the leadership of, first Chief Secretary Philomen Luhanjo and now Ambassador Ombeni Yohana Sefue, for their unwavering support over all these years. They have been exceptional.
  Finally, I owe huge gratitude to my friends and colleagues in the media. Their invaluable support over the years has been the pillar and strength of my work at the State House during the Kikwete Administration. I thank you all.

  Salva Rweyemamu
  November 8, 2015

  0 0
 • 11/08/15--11:43: Article 10

 • 0 0


  0 0

                                  Ndugu Dickson anayefahamika kwa wengi kama  Mr "DMK "
  Promoter "DMK" wa Kampuni ya DMK GLOBAL PROMOTIONS ashinda Tuzo ya Best Promoter USA katika zile tuzo za AFRICAN ENTERTAINMENT AWARDS USA 2015 ,Tuzo hizo zilitolewa OCTOBER 31 New York ambapo Makampuni 6 yalikuwa yakichuana kipengele hicho na DMK Global kuibuka kidedea,Pia katika Awards hizo Wasanii kutoka Tanzania Diamond alichukua Tuzo ya Hottest Male Single na Ommy Dimpoz tuzo ya People's Choice .

      Kampuni hii inafanya Shuguli zake Marekani za kuandaa Events mbali mbali za burudani kama CLUB EVENT,CONCERTS, CARNIVALS  ikiwa ni pamoja na kuleta wasanii Marekani kutoka Tanzania na Africa kwa ujumla,pia inafanya matamasha ya Burudani na wasanii wa Marekani pia.Baada ya Tuzo hizi Tulimpigia simu bwana DMK na kumpongeza kwa kuiwakilisha vyema Tanzania na East Africa kwa ujumla ambapo aliwashukuru sana waliompigia kura kote Duniani na kuongezea kuwa Tuzo hii ameipata yeye lakini angependa ijulikanekuwa shughuli hizi huwa anazifanya kwa kusaidiana na Partners wake kampuni za Safari Entertainment na J&P Ent ambazo amesema kuwa bila wao kushurikiana nao asingekuwa hapo alipo.

       Bwana DMK amesema tutegemee Mambo makubwa mengi kutoka kwake na Partners wake hivi Karibuni.

  0 0
  0 0

  Mechi ya Mpira wa miguu kati ya E-fm Vs Kivule Veterani iliyochezwa wikiendi hii huko Ukonga, Dar es salam, ilimalizika huku E-fm ikiruhusu washambuliaji wa Kivule Veterani kuziona nyavu mara mbili wakati  Efm wakiliona lango lao mara moja kupelekea matokeo kuwa 2 – 1, na ushindi kwenda Kivule Veterani  ambao waliutumia vyema  uwanja wao wa nyumbani
  Watangazaji wa vipindi vya Sports Headquarters na E Sports, Soud Mkumba na Oscar Oscar wakizungumza na mashabiki kabla ya kushuka dimbani.
  Picha ya pamoja ya kikosi cha E-fm
  Kikosi cha timu ya Kivule Veterani kwenye picha ya pamoja
  E-fm ilipoziona nyavu za Kivule Veterani kupitia mchezaji wake John Makundi
  Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mtanange huo


  0 0  0 0

  SIMU.TV: Babu Seya na mwanawe watua mahakama ya Afrika, Bi Simba anusurika kifo Dar. Pitia habari za magazetini hapa; https://youtu.be/9EhsMIwDS50 

  SIMU.TV: Watumishi wa serikali wametikiswa.Unataka kujua sababu ya mtikiso huo? Pitia magazeti ya leo Novemba 9.2015; https://youtu.be/2n1ZQqzwVss 

  SIMU.TV: Joto la waziri mkuu. Mawaziri lazidi kupanda. Wazanzibari waguswa na Dk.Magufuli. Ni katika magazeti ya leo; https://youtu.be/BAK7Ek_Rjfc

  SIMU.TV: Samatta atwaa taji Afrika, Pluijm agomea usajili Yanga. Wasauz wamgombania Malimi Busungu; https://youtu.be/7Vb5UwcSnWI 

  SIMU.TV: Mtoto wa mwaka mmoja na miezi nane aandaliwa kuwa rais.Pata undani wa habari hiyo katika magazeti ya leo; https://youtu.be/hNfr0uG4ATI

  0 0

   Washiriki wa shindano la Bongo style kwa upande wa picha wakimsikiliza kwa makini mtaalam wao Sameer Kermalli(wa tatu kulia) akitoa maelekezo wakati wa mafunzhayo.
   Baadhi ya washiriki kwa upande wa picha wakiwa wanasikiliza kwa makini somo
  Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Tedvan Chande akiwa na washiriki wa shindano la Bongo Style ambao hawapo pichani , akiwa na Mratibu wa FASDO Tanzania Joyce Msigwa alipofika kuwatembelea na kuongea nao machache.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imemtangaza bwana Benoit Janin kuwa Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo.

  Bwana Janin anachukua nafasi ya Pratap Ghose ambaye ameiongoza kampuni hiyo kwa muda wa miaka mitatu.
  Uteuzi wa Janin unafatia kampuni ya Millicom kununua hisa za kampuni ya Zantel ambapo sasa itashirikiana na serikali ya Zanzibar kuhakikisha kampuni ya Zantel inakua na inaboresha huduma zake.
  Benoit, ambaye ana uzoefu wa zaidi ya miaka 16 katika sekta ya mawasiliano katika nchi za Afrika na masoko yanayokua, alikuwa Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo nchini Chad kwa muda wa miaka mitatu, ambapo aliiwezesha kuwa kampuni namba moja nchini humo.

  Kabla ya kujiunga na Millicom, Benoit amefanya kazi na kampuni ya mawasiliano ya Vimpelcom kama Mkugenzi wa Biashara nchini Cambodia, huku pia akiwa ameshikilia nafasi mbalimbali za kiuongozi katika kampuni ya Orange.

  Akizungumzia majukumu yake mapya, Benoit alisema anatarajia kushirikiana na wafanyakazi wa Zantel katika kuhakikisha kampuni inakua na kufikia malengo yake.‘Nina furaha kubwa kujiunga na kampuni ya Zantel na ninatarajia kushirikiana na wafanyakazi wenzangu kuongeza idadi ya wateja, pamoja na kusimamia ukuaji wa kampuni kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato’ alisema Benoit.

  Kama sehemu ya majukumu yake mapya, Bwana Janin ataboresha huduma za mtandao za Zantel pamoja na kuzindua huduma za 4G hapo mwakani

older | 1 | .... | 1021 | 1022 | (Page 1023) | 1024 | 1025 | .... | 3348 | newer