Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Ngoma azipendazo ankal: CCM MBELE KWA MBELE


SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0


Mkoa wa Kilimanjaro waelezwa kuchomoza kwa mara nyingine kama ngome imara ya upinzani baada ya UKAWA kushinda majimbo 7 kati ya 9.https://youtu.be/x_xWwEKDHWI

Wakazi katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Mara wakabiliwa na tatizo kubwa la njaa kutokana kuoza kwa zao la mihogo. https://youtu.be/EWTxc-rpzN8

Wazazi na walezi nchini washauriwa kuto wabagua na watelekeza watoto wenye ulemavu na badala yake kuwalea kwa upendo mkubwa. https://youtu.be/J3ikLbUSJvE

Wavuvi 2 wafariki dunia baada ya boti zao kuzama bahari ya hindi huku chanzo kikielezwa kuwa ni upepo mkali. https://youtu.be/zsxXkd8HQQM

Mzee Pius Msekwa azungumzia sifa stahiki anazotakiwa kuwa nazo Spika wa bunge ajaye katika bunge la 11. https://youtu.be/Z3x5ueyXEHE

Mwandishi wa AZAM TV asimulia jinsi alivyokutana na Dr.Magufuli katika ziara yake ya kushitukiza wizara ya fedha. https://youtu.be/YRCZzairYLI

Raisi Dk.Magufuli avamia wizara ya fedha na kukuta baadhi ya wafanyakazi hawapo kazini; https://youtu.be/8Fkep8cY1fg

Tume ya uchaguzi Tanzania nec imetangaza nafasi za wabunge wa viti maalumu.https://youtu.be/FhbcWfjkGnM

Watu wanne wamefariki kutokana na mafuriko jijini mwanza; http://simu.tv/ukHJ3An

Watu wanne wamefikishwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya mitandao;https://youtu.be/WUnM8iZHMmE

Serikali mkoani Kagera imeakanusha uvumi wa kuibuka kwa ugonjwa wa kipindupindu;https://youtu.be/DR-_8hHHUCA

Mamlaka ya mbunga za wanyama Tanzania TANAPA imehimarisha ulinzi kwa wanyama aina ya tembo kwa kuwafunga kifaa cha kisasa; https://youtu.be/Y7R52IVA3oU

Serikali mkoani Mbeya imeanza kuwasaidia wakulima za wazo la mpunga ili kuhimarisha uzalishaji wa zao hilo; https://youtu.be/flALkeBjIOk

Viongozi mbalimbali wa dini za kiislamu na kikristo wanatarajia kufanya kongamano la maombi ya shukrani kwa kufanikisha uchaguzi wa amani na utulivu.https://youtu.be/CVmrCxVvuF8

Raisi wa awamu ya tano amuapisha mwanasheria mkuu wa serikali baada ya kumteua hapo jana huku naye akizungumza machache. https://youtu.be/g3m7Nd-q7_k

Tume ya taifa ya uchaguzi imetangaza mgawanyo wa viti maalum vya wanawake kwa vyama ambavyo vilikidhi vigezo vilivyowekwa. https://youtu.be/AQKnDKfic0I

Jeshi la polisi Dar es salaam limeendelea kuwahoji watuhumiwa 38 wa kituo cha LHRC kwa tuhuma za kukiuka mashariti waliyopewa na tume ya uchaguzi.https://youtu.be/lAmq1IZroEA

Polisi nchini yapiga marufuku mikutano na maandamano yote ya kisiasa nchini kwa kile ilichodai ni viashiria vya uvunjifu wa amani. https://youtu.be/9iXynTcIEXQ

SIMU TV: DONDOO ZA MAGAZETI LEO

$
0
0
Simu.tv: Magufuli aduwaza hazina. NEC yatangaza wabunge viti maalum. Pata dondoo za magazeti ya siku ya leo; https://youtu.be/qvg-GM-LaMU
 Simu.tv: Simba yampa Mavugo Shillingi mil 100, Mkwasa asema wachezaji wengi Taifa Stars hawapo fiti. Ni katika magazeti ya michezo ya leo; https://youtu.be/h1CW0OGebso
 Simu.tv: Raisi Magufuli Atisha afanya ziara ya kushtukiza Wizara ya Fedha, Ifahamu orodha ya Wabunge wa Bunge Lijalo.Pata dondoo za Magazeti.https://youtu.be/cBTB45MM1c0
 Simu.tv: NEC Yatangaza wabunge 110 wa Viti maalumu, Regina Lowassa aikatalia CHADEMA nafasi ya ubunge Viti Maalumu. Pata Dondoo hizi.https://youtu.be/jAOnxdavtHs

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 06/11/2015

Mwanamuziki Papa Wemba Awasili Dar, Aelekea Bagamoyo Kunogesha Tamasha la Karibu Music Festival 2015

$
0
0
MWANAMUZIKI nguli wa ndansi kutoka nchini Congo (DRC) Papa Wemba amewasili usiku huu jijini Dar es Salaam tayari kwa kutumbuiza katika tamasha la Karibu Music Festival 2015. 

Papa Wemba ametua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA) majira ya saa nane kasoro na ndege ya shirika la Kenya (Kenya Airways-KQ). 

 Mara baada ya kuwasili msanii huyo pamoja na wanamuziki wake walipokewa na Meneja wake anayeratibu safari hiyo, Chebli Msaidie pamoja na waandaaji wa Tamasha la Karibu Music Festival 2015 linalofanyika mjini Bagamoyo. 

Papa Wemba na msafara wake umeelekea Bagamoyo tayari kwa kukonga mioyo ya washabiki wa Tamasha hilo. Wasanii wengine ambao wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo ni Jhikolaman, Isha Mashauzi, Damian Soul, Juma Nature, Barnaba, Shilole, mshindi wa pili wa BSS, Nassib Fonabo na bendi yake ya Spirit na wengine wengi. Tamasha hilo lililoanza Novemba 6 hadi 8 katika viwanja vya Mwanakalenge, Bagamoyo mkoani Pwani linalengo la kukuza muziki asili ya Afrika.

 Tamasha limeandaliwa na Kampuni ya watayarishaji wa muziki ya Legendary kwa kushirikiana na kampuni ya kinywaji cha Jebel Coconut. Wadhaminiwa wengine ni pamoja na Swiss Embassy, Precion Air, Coca Cola, Mwananchi Communication, Kaya fm, Magic fm, Focus Outdoor, Jovago, Kaymu na Time tickets. huku mgeni mwalikwa akiwa ni mwanamuziki kutoka Congo, Papa Wemba. *Imeandaliwa na www.thehabari.com
Mwanamuziki Papa Wemba (kulia) akisalimiana na mwenyeji wake waandaaji wa Tamasha la Karibu Music Festival 2015 mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wake anayeratibu safari hiyo, Chebli Msaidie akimtambulisha kwa wenyeji wao.
Mwanamuziki Papa Wemba akiwa katika picha ya pamoja na wasanii alioambatana nao waliomo katika bandi yake mara baada ya kutua Tanzania tayari kufanya mashambulizi katika Tamasha la Karibu Music Festival 2015 linalofanyika Bagamoyo.

WASANII WATAKIWA KUCHAGAMKIA MAAZIMISHO YA SIKU YAO

$
0
0
Wasanii nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuhamasika na kushiriki kikamilifu kwenye maazimisho ya Siku ya Msanii maarufu kama Msanii Day ambayo yanatazamiwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu wa 2015 jijini Dar es Salaam na maeneo mbalimbali nchini. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye programu maalum ya kujadili ushiriki wa wasanii kwenye siku hii muhimu kwao marais wa mashirikisho ya wasanii nchini walisema kwamba wakati umefika kwa wasanii wote nchini kuamka na kuwa mstari wa mbele kutambua maazimisho haya ya siku yao kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakitumiwa katika kuazimisha vilele vya tasnia zingine.

“Tumekuwa tukitumika sana sisi Wasanii kung’alisha na kuzifanya kazi za wengine kuwa na mafanikio, tumekuwa tukihamasisha kazi za wengine. Hii siku ya Msanii ni yetu, tuamke, tuibebe zaidi ya tunavyofanya kwenye kazi za wengine. Tuungane tuifanye siku hii yenye tija” alisisitiza Symon Mwakifamba ambaye ni Rais wa shirikisho la Sanaa za Filamu nchini.

Aliongeza kusema kwamba, Wasanii wana nguvu na mchango mkubwa katika jamii na kwamba kwa idadi yao wanatosha kabisa kuwa na uwakilishi katika maeneo mbalimbali ya maamuzi ili kuhakikisha hawaachwi nyuma.
“Naomba wasanii wote tuitumie siku ya Msanii kuonesha nguvu yetu, tuwaoneshe na tutume ujumbe kwa viongozi kwamba kundi hili ni kubwa na muhimu katika kujenga Taifa lenye ustawi” Aliongeza Mwakifamba.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Adrian Nyangamale alisema kwamba siku ya msanii ni mahsusi kwa ajili ya wasanii wote nchini na kwamba kama ilivyo kwa maadhimisho ya siku zingine kama za walemavu, wanawake, wanasheria na nyinginezo wasanii nao hawana budi kuhakikisha wanaifanya siku hii kuwa yenye kufana na mafanikio makubwa.
“Hauwezi kuizungumzia siku ya Msanii bila kuwataja na kuwahusisha wasanii moja kwa moja. Wasanii lazima tujiunge pamoja na tushirikiane kwa dhati ili kuifanikisha siku hii” Alisisitiza Nyangamale. 

Awali viongozi wa mashirikisho ya Wasanii nchini Msule Jumanne (Sanaa za Ufundi), Samwel Mbwana (Sanaa za Muziki), Dennis Mango (Sanaa za Maonesho) na Biko wa Sanaa za Filamu walieleza namna wasanii walivyojipanga kushiriki siku hiyo na kusisitiza kwamba kila msanii nchini ajisikie furaha na heshima kushiriki siku hii muhimu kwao.

Siku ya msanii Tanzania inatarajiwa kuanza kuazimishwa kwa shamrashamra mbalimbali yakiwemo maonesho ya kazi za wasanii, semina na makongamano ya kujadili mustakabali wa sekta hiyo nchini kuanzia tarehe 7-11 Desemba mwaka 2015  na baadaye kilele chake tarehe 12 Desemba mwaka 2015 kwenye Ukumbi wa Blue Pearl uliko jengo la Ubungo Plaza Ubungo jijini Dar es Salaam.

IMETOLEWA NA KITENDO CHA HABARI NA MAWASILIANO, BASATA

Rais Magufuli alipofanya ziara ya ghafla Wizara ya Fedha

BARAZA KUU CUF LAKUTANA ZANZIBAR

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara) bibi Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar) Mhe. Nassor Ahmed Mazurui, pamoja na baadhi ya wajumbe wa baraza kuu la Uongozi CUF, mara baada ya kuwasili katika hoteli ya Mazsons Mjini Zanzibar kwa ajili ya kuanza kikao hicho.

Majina na Jumla ya Wabunge wote wa Bunge la 11 na Majimbo watokayo

$
0
0
1 Dk Charles Tizeba- Buchosa CCM

2 Nimrod Mkono- Butiama CCM

3 Omar Badwel- Chilonwa CCM

4 Kanyasu John- Geita Mjini CCM

5 Pudensiana Kikwembe- Kavuu CCM

6 Sixtus Mapunda- Mbinga Mjini CCM

7 Hassan Masala- Nachingwea CCM

8 Abdallah Chikota- Nanyamba CCM

9 Richard Mbogo- Nsimbo CCM

10 Ester Matiko- Tarime Mjini CHADEMA

11 Mwakajoka Frank- Tunduma CHADEMA

12 Joshua Nassari- Arumeru Magharibi CHADEMA

13 Dk Shukuru Kawambwa- Bagamoyo CCM

14 Andrew Chenge- Bariadi Magharibi CCM

15 Oscar Mukasa- Biharamulo Magharibi CCM

16 Wilfred Lwakatare- Bukoba Mjini CHADEMA

17 Jasson Rwikiza- Bukoba Vijijini CCM

18 Dotto Biteko- Bukombe CCM

19 Eshter Bulaya- Bunda Mjini CHADEMA

Boko Beach Veterans wamkabidhi zawadi Mchezaji bora wa Mwezi Oktoba 2015

$
0
0
Mwenyekiti wa Timu ya Boko Beach Veterans (BBV), Danny Ole a.k.a Aguero (wa nne toka kushoto) akimkabidhi zawadi ya mpira Mchezaji bora wa Mwezi Oktoba, Henry Horombe (wa nne toka kulia), baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwa kipindi chote cha mwezi mwezi huo 2015. Zawadi hizo hutolewa na mdau mkubwa wa soka nchini na mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashion, Othman Tippo Shaaban ambaye nae ni mwanachama wa timu hiyo.
Sehemu ya wachezaji wa Timu ya Boko Beach Veterans (BBV) wakimpongeza mchezaji mwanzao aliebuka kidedea na kutwaa taji la Mchezaji bora wa Mwezi Oktoba, Henry Horombe (katikati) mara baada ya mtanange uliopigwa mapema leo asubuhu katika uwanja wa Boko.
 Timu ya Boko Beach Veterans (BBV) ikiwa imegawanyika katika mchezo wa mazoezi mapema leo asubuhi.

Ratiba Ya Mkutano Wa Kwanza Wa Bunge 2015

Minnesota Muslim Woman BRUTALLY SMASHED IN FACE With BEER MUG For Speaking SWAHILI At APPLEBEE'S!!

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA WANNE WA NCHINI CHINA WAKIWA NA PEMBE 11 ZINAZODHANIWA ZA FARU.

$
0
0




JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE RAIA WA CHINA WAKIWA NA PEMBE 11 ZINAZODHANIWA ZA FARU. RAIA HAO WALIFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. XIAO SHAODAN (29) AKIWA NA PASSPORT NAMBA G.29624553 ILIYOTOLEWA NCHINI CHINA 2. CHEN JIANLIN (33) AKIWA NA PASSPORT NAMBA E.09800855 ILIYOTOLEWA NCHINI CHINA 3. SONG LEI (30) AKIWA NA PASSPORT NAMBA G.52064944 ILIYOTOLEWA NCHINI CHINA NA 4. HU LIANG (30) WOTE WAKAZI WA BLANTYRE NCHINI MALAWI.


WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 06.11.2015MAJIRA YA SAA 08:30 ASUBUHI HUKO MPAKANI KASUMULU KATIKA WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA BAADA YA ASKARI POLISI NA WADAU WENGINE WA USALAMA WALIOKUWEPO MPAKANI HAPO KULITILIA MASHAKA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.103 DERAINA YA TOYOTA HILUX RANGI YA DHAHABU LILILOKUWA LIKITOKEA NCHI MALAWI KUINGIA TANZANIA LIKIWA NA RAIA HAO.


KUTOKANA NA MASHAKA HAYO, MAAFISA HAO WALIFANYA UPEKUZI NDANI YA GARI HILO NA CHINI YA CHASES YA GARI HILO NA NDIPO WALIGUNDUA KUWA GARI HILO LILIKUWA LIMEJENGEWA BOKSI NA BAADA YA KUFUNGUA BOKSI HILO LA BATI KULIPATIKANA PEMBE 11 ZA MNYAMA PORI FARU. 
AIDHA ASKARI POLISI WALIENDELEA NA UPEKUZI KATIKA GARI HILO NA KUKUTA MALI MBALIMBALI ZIKIWEMO:- SIMU MOJA AINA YA SAMSUNG, IPAD MOJA, PESA YA MALAWI KWACHA 1,600/=, TSHS.234,000/=, USD DOLLAR 1,700/=, NOTI 22 @ TSHS 100 = 2,200, NOTI 51 @ TSHS 51 = 2,550, USD 33 @ TSHS. 50 = 1,650, USD NOTI 9 @ TSHS 100 = USD 900, MALAWI KWACHA 18,760 NA CERTIFICATE OF HEALTH EXAMINATION MOJA, SIMU MBILI ZA KICHINA AMBAZO MAJINA YAKE NA AINA HAIKUFAHAMIKA MAPEMA NA SIMU MOJA AINA YA HUAWEI, SIMU MOJA AINA YA SAMSUNG, IPHONE APPLE TANO, SIMU MOJA TARDROVER, NOKIA MOJA NA SMT MOJA.


UPELELEZI KUHUSIANA NA TUKIO HILI UNAENDELEA NA PINDI UTAKAPOKAMILIKA WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA PEMBE ZA FARU/PEMBE ZA NDOVU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA PEMBE ZA FARU/NDOVU KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

  
Imesainiwa na:

[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.




TAARIFA TOKA TFF LEO

$
0
0
 Michuano ya Kombe la Shirikisho ya (Azam Sports Federation Cup) itafunguliwa rasmi kesho Jumapili (Novemba 8, 2015) kwa mechi tatu zitakazochezwa kwenye viwanja vitatu tofauti, ambao jumla ya timu 64 zitashirki kuwania nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.
Mechi rasmi ya ufunguzi itakuwa kati ya wenyeji JKT Rwamkoma ya Mara na Villa Squad ya Dar es Salaam itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
 Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Azam Sports HD ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.


SDL KUTIMUA VUMBI NOVEMBA 15
Ligi Daraja la Pili nchini (SDL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi wikiendi ijayo Novemba 15 katika viwanja mbalimbali nchini, huku timu 24 zinazoshiriki ligi hiyo zikisaka nafasi nne za kupanda ligi Daraja la Kwanza (FDL) msim ujao.  Fuata link chini kwa taarifa zaidi

STARS KUJIPIMA NA U23 YA AFRIKA KUSINI
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa ya Afrika Kusini ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 (Amaglug-glug) Jumanne jioni kwenye dimba la Eldorado jijini Johannesburg. Fuata link chini kwa taarifa zaidi

SAUTI YA MKURUGENZI WA NEC JUU YA WABUNGE VITI MAALUM


SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

$
0
0
SIMU.TV: Mkurugenzi wa NEC akanusha orodha ya wabunge wa viti maalum inayosambaa katika mitandao kuwa sio sahihi na hivyo ipuuzwe;https://youtu.be/_D6sNX2tEwM 
SIMU.TV: Watu 8 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na kuta ya nyumba katika vijiji vitatu tofauti mkoani Iringa kufuatia mvua kubwa kunyesha; https://youtu.be/m80CCtu_rM 
SIMU.TV: Rai wa China wakamatwa na jeshi la polisi wakijaribu kuvuka na pembe za faru katika mipaka ya Tanzania na Malawi;  https://youtu.be/SNwxwzeIw28
 SIMU.TV: Baada Ya Dkt. Magufuli kuapisha kuwa raisi wa Tanzania, baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dodoma wataja vipaumbele kwa hatua za awali.https://youtu.be/PKvBBPEHU2E
 SIMU.TV: Dr.Magufuli apewa shauri kuangalia kwa karibu sheria za uhifadhi wa misitu, mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi; https://youtu.be/0fAPSOYgsQA 
 SIMU.TV: Ria wanne wa China wamekamatwa na jeshi la polisi wilaya Kyela wakiwa na pembe za faru wakitokea Malawi; https://youtu.be/k0CB0awpMHg  
 SIMU.TV: Wahitimu wa vyuo vikuu wameshauriwa kuacha kulalamika na kuchangamkia fursa katika soko la ajira la Afrika Mashariki;https://youtu.be/EI8MUlaAm-Y 
 SIMU.TV: Serikali Yaombwa kuwekeza zaidi kukuza utaalamu wa madaktari na matibabu nchini ili kudhibiti ongezeko la wagonjwa wanaotibiwa nje;https://youtu.be/xHgiy_O-H24
 SIMU.TV: Utafiti Wizara ya afya kuhusu ugonjwa wa kipindupindu wathibitisha,wagonjwa waliofariki wametokana na kutofikishwa hospitalini.  https://youtu.be/cfvMjWnFZWM
 SIMU.TV: Chuo kikuu Huria Tanga Chawalaumu waajiri wenye tabia ya kukwamisha wanafunzi wanaotaka kujiunga na masomo chuoni hapo.https://youtu.be/5HKGNPF6XQg
 SIMU.TV: Taasisi ya utetezi ya watu wenye albinism nchini Tanzania imesema matendo ya ukatili dhidi ya albino yamepungua katika kipindi cha uchaguzi huu:https://youtu.be/czt-ZYTqo08

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MAKATIBU WAKUU, MANAIBU MAKATIBU WAKUU NA WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI LEO IKULU

$
0
0
  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  katika picha ya pamoja Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
PICHA NA IKULU
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


     Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo asubuhi katika Ikulu ya Dar es Salaam  amefanya kikao na Makatibu wakuu, Manaibu Makatibu wakuu, Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  ili kutoa uelekeo wa Serikali anayoitaka  mara baada ya  kuapishwa.

     “Nataka Serikali iendelee kwa nguvu zote na katika kutekeleza dhana ya ‘HAPA KAZI TU’ na viongozi kuzingatia na kukumbuka ahadi nilizotoa ili zianze kuonekana na kufanyiwa kazi mara moja” Rais Magufuli amesema.

     Katika Kikao chake, Rais ametoa mwongozo na kusisitizia kuwa ni lazima kila mtendaji Serikalini kuuzingatia, kufuata sheria na taratibu ili taifa lisonge mbele kwa ufanisi zaidi.

     Katika kikao hicho Rais ameelekeza mambo kadhaa ambayo watendaji hao wanapaswa kuyasimamia, kuyawekea mikakati na kuyapanga vizuri ili atakapo teua Baraza lake la Mawaziri mambo hayo yawe tayari ili Mawaziri watakaoteuliwa waweze kuyasimamia bila kukosa.

     Mambo hayo muhimu ni kama ifuatavyo:

1.      Kuanzia mwezi  Januari mwaka 2016, wanafunzi wote wanaoanza shule watasoma bure bila kulipa ada, Katika jambo hili, Rais amewataka watendaji kuanza kuliwekea mikakati tayari kwa utekelezaji

2.      Suala la mikopo ya wanafunzi nalo lifanyiwe kazi na mipango yake ikamilike kwa ajili ya utekelezaji mzuri zaidi

3.      Amefuta safari zote za nje ya nchi kuanzia leo hadi hapo atakapolitolea suala hilo maamuzi mengine na kueleza kuwa shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchi zifanywe na kusimamiwa  na mabalozi wa Tanzania  wanaowakilisha nchi  huko nje.


Pengine patokee jambo la dharura sana na hata hilo lazima kibali kitolewe na Rais au Katibu Mkuu Kiongozi. Badala yake Rais amewataka watendaji hao kufanya zaidi ziara za kwenda vijijini ili kuzijua na kutatua kero za wananchi wa Tanzania.

     Katika Kikao hicho, Rais amemtaka Kamishna wa TRA, Ndugu Rished Bade kusimamia kwa makini zoezi la ukusanyaji wa mapato nchini na kuhakikisha kero ndogo ndogo kwa wananchi lianze kutekelezwa kama alivyo ahidi kwa  kufanyiwa  kazi mapema  zaidi.

     Rais ameitaka TRA kukusanya mapato hayo kutoka kwa wafanya biashara wakubwa zaidi na wale wanaokwepa kodi bila kuogopa mtu wala taasisi yoyote hapa Tanzania na kusisitiza kuwa katika Serikali hii wa kutoa maamuzi vinginevyo zaidi ya haya ni yeye Rais  ama Makamu wake.

     Rais Magufuli pia ameagiza usimamizi katika suala la manunuzi ambalo limekuwa likitumika vibaya na kuwa mwanya wa kuibia Serikali  kwa watu kuongeza bei ya vitu hata kama ni vya bei ndogo kabisa katika jamii.

     “Ikitokea suala hilo likagundulika kwa watu kuongeza bei ya vitu, watendaji watawajibishwa mara moja”. Rais amesema, na kuwataka watendaji hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo na kuzingatia maadili mema ya kazi.

Imetolewa na Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi

Ikulu,

DAR ES SALAAM.


7 Novemba, 2015

 .





VIDEO: Rais Magufuli alipokutana na Makatibu wakuu wa wizara na manaibu katibu wakuu Ikulu Jijini Dar es salaa

SBL yafadhili wanafunzi UDSM

$
0
0
Katika kuunga mkono juhudi za serikali za kupanua wigo wa elimu Tanzania, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imetoa ufadhili kwa wanafunzi wahitaji katika masomo ya chuo kikuu. 
 Wanafunzi hao waliofaulu daraja la kwanza wanaanza masomo yao mwaka huu wa masomo katika chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Wanafunzi waliopata ufadhili huo ni Michael Daniel na Consolatha Mushi wanaokwenda kusomea uhandisi wa ujenzi na Lisa Kalokola anayekwenda kusomea uhandisi wa madini katika chuo hicho. 
 Ufadhili huo utahusisha gharama za karo, malazi na fedha ya kujikimu kwa mwezi kwa asilimia 100. Meneja Miradi Endelevu wa SBL, Bi. Hawa Ladha amesema mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kuwa ufadhili huo unafanyika kupitia mfuko wa East African Breweries Limited (EABL) Foundation. 
 “Hii ni moja ya mikakati ya kampuni hii kusaidia jamii,” alisema. 
 Alisema mfuko huo hutenga fedha kila mwaka kusaidia miradi mbalimbali ya kijamii ikiwemo ya elimu. Alifafanua kuwa wanafunzi waliopata ufadhili huo ni wale walioomba na kutimiza vigezo vilivyowekwa na kampuni. 
 Aliwataka vijana hao kutumia vizuri ufadhili huo kwa kusoma kwa bidii ili baada ya kuhitimu waweze kutoa mchango kwa familia zao na taifa kwa ujumla. Mmoja wa wanafunzi hao, Bw. Laurent alisema ufadhili huo utamsaidia sana katika masomo yake. 
 “Nimefaulu vizuri kidato cha sita lakini sikuwa na uwezo, ufadhili huu wa asilimia 100 ni ukombozi,” alisema. Alisema atatumia fursa hiyo kusoma kwa bidii na kufaulu vizuri ili ndoto zake katika maisha zitimie. Naye Bi. Kalokola alikipongeza kiwanda hicho kwa kutenga fedha kwa ajili ya kusaidia jamii na hasa katika sekta ya elimu. 
 “Wanafunzi wasio na uwezo wachangamkie fursa kama hizi zinapotangazwa,” alisema. EABL Foundation imeanza kutoa ufadhili huo wa elimu vyuo vikuu tangu mwaka 2005 na kufaidisha zaidi ya vijana 200 katika nchi za Afrika ya Mashariki. Kwa Tanzania, programu hiyo imeshafadhili vijana zaidi ya 25 wanaofanya kazi katika kampuni mbalimbali.
 Meneja Miradi Endelevu wa kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Bi. Hawa Ladha akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kuhusiana na ufadhili uliotolewa na kampuni hiyo kwa vijana watatu katika masomo yao Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.  Ufadhili huo wa asilimia 100 unafanyika kupitia mfuko wa East African Breweries Limited (EABL) Foundation.
Meneja Miradi Endelevu wa kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Bi. Hawa Ladha (wa pili kulia) akimpongeza mmoja wa wanafunzi waliofanikiwa kupata ufadhili wa kampuni hiyo kusoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka huu wa masomo, Michael Patrick mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Wengine ni wanafunzi waliofaidika pia na ufadhili huo, Consolatha Mushi (kushoto) na Lissa Kalokola (wa pili kushoto).  Ufadhili huo wa asilimia 100 unafanyika kupitia mfuko wa East African Breweries Limited (EABL) Foundation.

CHECK OUT RISING RAPPER AND SINGER ALLAN KINGDOM

$
0
0
This past spring, The FADER flew to St. Paul, Minnesota to spend time with rising rapper and singer Allan Kingdom and visit his childhood home for the second in our FADER Documentary series. 
A couple of months earlier, Kingdom had caught the world's ear after being featured on Kanye West's "All Day" and joining him on stage for an unforgettable performance at the BRIT Awards. As Kingdom tells it, an email from Kanye confidante Plain Pat changed his life, but his story began way before that. 
Born in Winnipeg, Manitoba, to a pair of immigrants from Tanzania and South Africa, he was raised in the Twin Cities, where he eventually battled against the odds of being from a flyover State.

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images