Mrs Bernadette Mathias akiimba Wimbo wa Tanzania Nakupenda kwa Kiswahili
ngoma azipendazo ankal: Tanzania, Tanzania nakupenda.....
↧
↧
JE MNAHITAJI SACCOS, IJUE NAMNA YA KUANZISHA.
NA BASHIR YAKUB.
NILIWAHI kueleza namna ya kuanzisha kampuni pamoja na usajili wa jina la biashara. Katika makala hayo pia nilieleza tofauti kati ya kusajili kampuni na kusajili jina la biashara.
Hii ilikwenda sambamba na maelezo ya tofauti za kiuchumi ya vyote viwili. Ifahamike kuwa hizi zote ni njia za kisasa za kujitafutia kipato. Makala ya leo yanaeleza namna ya kisheria ya kuanzisha SACCOS.
Tutaona utaratibu mzima ambao unaweza kupitia katika kulifanikisha hili. Muhimu ni kujua kuwa SACCOS nayo ni njia kati ya njia za kisasa za kujipatia na kujiongezea kipato. Aidha utaratibu mzima wa kuanzisha na kuendesha SACCOS unaongozwa na Sheria namba 6 ya 2013 ya vyama vya ushirika ambayo ndiyo msingi wa makala haya.
1.SACCOS NI NINI ?
SACCOS ni kifupi cha neno la kiingereza lijukanalo kama Saving And Credit CO-operative Society. Kwa Kiswahili kizuri ni chama cha ushirika cha akiba na mikopo.
Kwa faida tu ni kuwa, kwa mara ya kwanza SACCOS zilianzishwa Ujerumani na mtu aitwaye Fredrick Taylor. Sura ya SACCOS aliyoanzisha Taylor imekuwa ikibadilika kadri shughuli za kijamii na kiuchumi zinavyokua mpaka kufikia aina ya SACCOS zilizopo sasa.
2. SACCOS KIUCHUMI.
Saccos ni asasi ya kifedha. Ni muungano wa watu ambao lengo lao ni kukusanya fedha na kukopeshana au kufanya biashara moja kwa moja na kugawana faida. Taratibu za kukopeshana na kufanya biashara katika Saccos hufanywa na watu wenye msimamo au fungamano linalofanana.
↧
HAFLA YA MCHAPALO (COCKTAIL PARTY) WA KUSHEREHEHEA KUAPISHWA KWA RAIS DKT MAGUFULI
Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete akifuatiwa na mkewe Mama Janet Magufuli
Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kifuatiwa na mkewe Mama Janet Magufuli
Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Hadija Mwinyi akifuatiwa na mkewe Mama Janet Magufuli
Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni wake
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Mtera Mteule Mhe Livingstone Lusinde "Kibajaji". Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
↧
MAGUFULI AAPISHWA KUWA RAIS WA AWAMU YA TANO WA TANZANIA
JK akiaga wananchi kwa furaha wakati akiingia uwanja wa Uhuru katika sherehe rasmi za kumuapisha mristhi wake Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa awamu ya Tano wa Janhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Kikwete akipokea saluti kwa mara ya mwisho kama Rais huku wimbo wa Taifa ukipigwa sambamba na mizinga 21.
Rais Kikwete akikagua gwaride la heshima lililojipanga katika muundo wa Omega - yaani mwisho.
Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akila kiapo.
"....Hapa ndipo panapokustahili Mheshimiwa...." Rais Mstaafu wa awamu ya nne anamwambia Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akila kiapo.
Rais mstaafu na Makamu wake Mstaafu wakiaga rasmi.
Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua gwaride rasmi likiwa katika muundo wa Alpha kuashiria kushika madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu
Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua gwaride rasmi likiwa katika muundo wa Alpha kuashiria kushika madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu
Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitembea kikakamavu bada ya kukagua gwaride rasmi likiwa katika muundo wa Alpha kuashiria kushika madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
↧
BALOZI MULAMULA AWASINDIKIZA MARAIS WA DRC NA MSUMBJI
Rais Kabila (katikati) akielekea kwenye ndege, kulia ni Balozi Mulamula na kushoto ni Balozi wa Kongo nchini Mhe. Khalifani Mpango |
Mhe. Rais Kabila akipita kwenye gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la wananchi Tanzania. |
Katibu Mkuu Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiagana na Rais Joseph Kabila tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini kwake. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA. |
↧
↧
ENEO LA LEBANON KATIKA SOKO LA KIMATAIFA LA SAMAKI LA FERI JIJINI DAR NI HATARI KWA UCHUMI.
Mwenyekiti wa Kamati ya Soko la Samaki la Kimataifa la Feri, Ali Kibwana, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wanaotembelea masoko mbalimbali ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi gani vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia umepungua katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoa mafunzo ya kupinga ukatili katika masoko hayo. Kushoto ni Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Bakari Said.
Mama Lishe wa soko hilo, Taus Barnabas, akichangia neno katika mkutano huo.
Mama Lishe wa soko hilo, Taus Barnabas, akichangia neno katika mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
ENEO la Lebanon katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri ambalo lipo jirani na Ikulu jijini Dar es Salaam limedaiwa kuwa ni hatari kwa wafanyabiashara wa soko hilo na kuwa linadhohofisha uchumi kutokana na kukithiri kwa watu wasio rasmi.
Hayo yamebainishwa na Mwezeshaji wa Sheria wa soko hilo, Asha Malenda wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wanaotembelea masoko mbalimbali ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi gani vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia umepungua katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoa mafunzo ya kupinga ukatili katika masoko hayo.
"Tunachangamoto kubwa sana katika soko letu la Feri tunayoipata kutoka eneo la Lebanon lenye mwingiliano wa watu wasio rasmi kutoka nje ya soko ambao ni kama wamejianzishia soko lao na wamekuwa na maamuzi yao lakini viongozi wa soko la Feri wanashindwa kuwachukulia hatua hali ambayo inatudhalilisha sisi wafanyabiashara hasa mama lishe na kuharibu uchumi wa soko letu" alisema Malenda.
Alisema wengi wa watu waliopo katika eneo hilo lisilo rasmi wamekuwa wakifanya biashara kiholela huku wakipika vyakula katika maeneo yanayoweza kuhatarisha afya ya mlaji wakati katika soko hilo kuna eneo maalumu la mama lishe na wengi wa watu hao wakienda kula eneo hilo rasmi wamekuwa hawalipi fedha na wakibanwa kulipa wanadiliki kutoa visu na silaha za jadi kuwatishia wanaodai.
"Eneo hilo la Lebanon ni hatari na kinachoshangaza linatizamana na Ikulu lakini hakuna hatua yoyote ya makusudi inayochukuliwa na viongozi wetu na linapopelekwa kwa viongozi wa kisiasa wanadai waachwe kwani ndio wapiga kura wao" alisema Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Bakari Said.
Said alisema katika soko hilo kuna changoto nyingi za udhalilishaji wanawake kwa kushikwa katika maungo yao lakini kupitia EfG wamejitahidi kupunguza changamoto hizo kwani wasaidizi wa sheria waliopatiwa mafunzo na shirika hilo wanajitahidi kuupenyeza ujuzi waliopata kuifikishia jamii ambayo imeanza kuelewa kuhusu vitendo hivyo.
Aliongeza kuwa uvaaji wa nguo za kubana na kuacha vifua wazi kwa upande wa wanawake pia ulikuwa ukichochea kukithiri kwa vitendo vya udhalilishaji uliokuwa ukifanywa na vijana wasio rasmi katika eneo hilo la Feri ambao hawana makazi na maisha yao yapo Feri lakini baada ya kufikiwa na mafunzo ya EfG hali hiyo imepungua kwa asilimia 80.
Mwezeshaji Fatuma Saijali alisema changamoto kubwa iliyopo hivi sasa katika soko hilo ni kuzuiliwa kupika chakula katika eneo hilo la Feri lakini wakati huo huo kuna kundi la wanawake wamekuwa wakiingiza chakula kutoka majumbano kwao na kukiuza hivyo kuharibu soko lao la chakula.
Mwenyekiti wa Kamati ya Soko hilo, Ali Kibwana alisema mafunzo waliyopata kupitia EfG yamesaidia sana kupunguza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika soko hilo na kila mtu anayebainika kujihusisha na vitendo hivyo amekuwa akiitwa na kukanywa na kama akiendelea kuwa mkaidi anachukuliwa hatua nyingine kwa kufuata kanuni na sheria.
Kamanda wa Ulinzi na Mazingira wa Soko hilo, Nurdin Hassan amesema hali katika soko hilo ni nzuri kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na EfG ya kufanya semina na matamasha ya uhamasishaji hivyo kuifanyajamii kuelewa kuhusu vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia.
Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa EfG, Shaban Rulimbiye alisema Shirika hilo linaendesha mradi wa miaka mitatu wa Mpe Riziki si Matusi wenye lengo la kutoa elimu ya kupinga ukatili wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na udhalilishaji na nia zaidi mradi huo ni kuusambaza hadi katika maeneo mengine ya nchi.
↧
MTO MSIMBAZI UNAOKATIZA ENEO LA JAGWANI WAANZA KUPIGWA SOP SOP
Mhandisi wa Kampuni ya Chico, David Waruma akizungumza leo jijini Dar es Salaam juu ya kazi ya kusafisha na kuzibua uchafu katika daraja la Mto Msimbazi eneo la Jangwani, Jijini Dar es salaam kuzuia na kukomesha mafuriko yanayotokea kipindi cha mvua ambayo huleta athari kwa jamii inayozunguka eneo hilo pamoja na kulinda Kituo cha Mabasi yaendayo Haraka (BRT) cha Jangwani (Jangwani Depot), kisiathirike na Mafuriko endapo yatatokea.
Kazi ikiendelea ya kusafisha eneo la Mto Msimbazi leo jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakitazama daraja la Mto Msimbazi jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii
↧
Rais Magufuli akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ramtane Lamamra
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Mhe. Ramantane Lamamra Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
(Picha na Freddy Maro)
↧
NEC YATANGAZA MGAWANYO WA VITI MAALUM BUNGENI
↧
↧
MR TZ - LOADING........
↧
Rais Magufuli akutana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala Cha China Mhe.Zhang Ping
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala Cha China Mhe. Zhang Ping ikulu jijini Dar es Salaam leo.Bwana Zhang alimwakilisha Rais wa China katika sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano. Kulia ni Balozi wa China nchini Dr. LU Youqing
Rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala Cha China Mhe.Zhang Ping ikulu jijini Dar es Salaam leo.Bwana Zhang alimwakilisha Rais wa China katika sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano. Kulia ni Balozi wa China nchini Dr. LU Youqing na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini China Lt General (rtd) Abdulrahman Shimbo.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli katika mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala Cha China Mhe.Zhang Ping ikulu jijini Dar es Salaam leo.Bwana Zhang alimwakilisha Rais wa China katika sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano. Picha na Freddy Maro
↧
NEWS ALERT: Serikali yasitisha matumizi ya Picha Rasmi ya Rais Magufuli
Serikali inapenda kuzitaarifu ofisi za umma na wananchi kwa ujumla kwamba imesitisha matumizi ya picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Serikali ya Awamu ya Tano, Mhe.Dkt. John Pombe Josep Magufuli mpaka hapo itakapotangazwa tena.
Awali majira ya saa 6: 00 mchana leo Novemba 6, mwaka huu Serikali ilitangaza kuhusu kuanza rasmi kwa matumizi ya picha ya Rais.
Aidha, Serikali imesema kwamba itazitangazia ofisi hizo na umma wa Watanzania kuhusu kuanza tena kwa matumizi ya picha hiyo hapo baadae.
Imetolewa na
IDARA YA HABARI.
Novemba 6,mwaka 2015
↧
NEWS ALERT: RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AONDOKA RASMI IKULU NA KUELEKEA KIJIJINI MSOGA LEO
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati wakiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita na kurudi kijijini Msoga. kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati akiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu alimoishi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita.
Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu walimoishi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita.
Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Katibu Mkuu Ikulu Mhe Peter Ilomo na watumishi wa Ofisi ya Rais wakiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho kikwete.
↧
↧
Tamko la Waziri wa Mambo ya Nje John Kerry kuhusu Uchaguzi wa Tanzania
Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam TANZANIA | |
5 Novemba, 2015 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI |
Kwa niaba ya Rais Obama na watu wa Marekani, nawapongeza watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uchaguzi wa rais na wabunge ulioendelea kuthibitisha rekodi nzuri ya Tanzania katika kujenga demokrasia imara.
Wakati Rais John Pombe Joseph Magufuli na serikali yake wakichukua majukumu yao, tunatarajia kuendelea na ubia wetu wa karibu na kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya nchi zetu mbili tunapofanya kazi pamoja ya kusaidia ujenzi wa demokrasia, kukuza usalama wa kikanda na kuendelea kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Aidha, napenda kumshukuru Rais aliyemaliza muda wake Jakaya Kikwete kwa jitihada zake za kujenga uhusiano imara na wa kudumu kati ya Marekani na Tanzania.
Hata hivyo, Marekani inaendelea kustushwa sana na tamko la mamlaka visiwani Zanzibar la kusudio la kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais wa Zanzibar wa Oktoba 25.
Kwa dhati kabisa, tunatoa wito kwa serikali mpya kuhakikisha kuwa maamuzi ya watu wa Zanzibar yanajidhihirisha katika ukamilishwaji wa haraka, wa haki na wa amani wa mchakato wa uchaguzi visiwani Zanzibar.
↧
Rais Magufuli akiwa Ofisini Kwake Siku ya Kwanza
↧
Rais Magufuli afanya Ziara ya Kushtukiza Hazina
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili katika makao makuu ya Wizara ya Fedha(HAZINA) kwa ziara ya kushtukiza leo mchana.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Servacius Likwelile.Rais Magufuli alitembelea na kukagua ofisi zote wizarani hapo na kisha kuongea na viongozi waandamizi.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na wafanyakazi wawili wa Wizara ya Fedha ambao ni walemavu Bwana Fundi Maruma na Frank Mkyama wakati Rais alipofanya ziara ya kushtukiza wizarani hapo leo.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha wakati alipofanya ziara ya kushtukiza Wizarani hapo ambapo alitoa maagizo ya kuziba mianya ya wakwepa kodi.(picha na Freddy Maro)
↧
KIONGOZI MKUU WA CHINA ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA JIJINI DAR
Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala cha Nchini China Mh ZHANG PING akiwa kwenye ukumbi wa Historia wa Makumbusho na Nyumba ya Utamani Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala cha Nchini China Mh ZHANG PING katikati akiwa kwenye ukumbi wa Sanaa wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala cha Nchini China Mh ZHANG PING watatu kushoto akiwa kwenye chumba mahususi akipewa maelezo na Dr Amandus Kweka ya fuvu la Zinjanthropus lililopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
↧
↧
UZINDUZI WA KANISA HOUSTON
↧
JUMAMOSI 7 NOV 2015 ! NGOMA AFRICA BAND JUKWAANI MJINI BREMEN.UJERUMANI
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni yenye makao nchini Ujerumani ,itatumbuiza mjini Bremen,Ujerumani
Leo jumamosi 7 November 2015,katika ukumbi wa Weserterrasse, uliopo
mtaa wa Osterdeich 70b, D- 28205 Bremen kuanzia saa usiku, onyesho hilo limeandaliwa na Pan-African Org tawi la Bremen ambalo linasherekea miaka 10 ya kuanziswa kwake. bendi ya Ngoma Africa band kwa sasa wanatamba na CD yao mpya La Mgambo na pia song lao jipya waliloliachia juzi tu "Mapenzi ya Pesa" nyimbo zote hizo zinapasua anga ya kimataifa
unaweza pia kusikiliza at www.ngoma-africa.com
↧
Rais Magufuli alipofanya ziara ya ghafla Wizara ya Fedha
↧
More Pages to Explore .....