Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1010 | 1011 | (Page 1012) | 1013 | 1014 | .... | 3272 | newer

  0 0  0 0


   

  STATE HOUSE ZANZIBAR

  OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

  PRESS RELEASE

  Zanzibar                                                              24.10.2015
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza kuwa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika kesho utakuwa huru, haki na wenye utulivu na kuwahakikishia washirika wa maendeleo likiwemo Shirika la Misaada la Uingereza (DFID) kuwa Zanzibar itaendea kuwa na amani kwani ndio msingi wa maendeleo.


  Dk. Shein aliyasema hayo katika mazungumzo kati yake na Kiongozi wa Shirika la Misaada la Uingereza anayefanya kazi zake nchini Tanzania Mhe. Vel Gnanendran, huko Ikulu mjini Zanzibar.


  Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo wa Shirika la DFID ambaye alifuatana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Dianna Melrose kuwa Zanzibar itaendelea kuwa visiwa vya amani na utulivu katika kipindi chote cha uchaguzi mkuu na hata baada ya uchaguzi.


  Dk.Shein alisema kuwa hatua za maendeleo zilizofikiwa na Zanzibar sambamba na amani na  utulivu uliopo ndivyo viliyoyapelekea mashirika mbali mbali ya Kimataifa ulimwenguni kuendelea kuiunga mkono Zanzibar likiwemo Shirika la DFID kwa kuthamini na kutambua juhudi zake hizo.


  Dk. Shein alimuhakikishia kiongozi huyo wa Shirika hilo kuwa Zanzibar itaendelea kushirikiana na Shirika hilo kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu nchini.


  Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alisema kuwa juhudi kubwa zimechukuliwa na vyombo vya ulinzi kwa kuendelea kusimamia amani na utulivu pamoja na vyama vya siasa wakati wote wa kampeni hivyo ni matarajio yake kuwa hatua hiyo itaendelezwa hata kwa siku za usoni ikiwemo siku ya kupiga kura hapo kesho.


  Aidha, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuwahimiza wawekezaji kutoka nchini Uingereza kuja kuekeza Zanzibar katika sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo sekta ya kilimo pamoja na  utafiti wake.


  Sambamba na hayo, Dk. Shein alisisitiza haja ya kuweko mpango maalum wa nafasi za masomo nchini Uingereza kwa vijana wa Zanzibar ikiwa ni pamoja na kupitia Shirika hilo la DFID.


  Dk. Shein aliwaeleza viongozi hao kuwa Zanzibar itaendeleza uhusiano na ushirikiano kati yake na Shirika hilo la DFID.


  Nae  Kiongozi huyo wa Shirika la DFID Mhe.  Vel Gnanendran alimueleza Dk. Shein kuwa Shirika hilo limeazimia kuiunga mkono Zanzibar kwa kutambua juhudi zake katika sekta za maendeleo.


  Alisema kuwa juhudi zilizochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta zake za maendeleo zinahitaji kupongezwa na kuungwa mkono ili zizidi kuimarika.


  Aidha, kiongozi huyo alimpongeza Dk. Shein kwa kuendelea kusimamia amani, utulivu na mshikamano hapa Zanzibar na kueleza kuwa hiyo ndio nguzo pekee itakayoendelea kuikuza Zanzibar kiuchumi na kimaendeleo.


  Balozi wa Uingereza Mhe. Dianna Melrose kwa upande wake alimuhakikishia Dk. Shein kuwa nchi yake inatambua na inathamini uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Zanzibar na Tanzania nzima pamoja na Uingereza uliopo ambao aliahidi kuuendeleza.


  Balozi Melrose alimueleza Dk. Shein kuwa wawekezaji wengi wa nchi hiyo wanavutiwa kuja kuekeza Zanzibar kutokana na kuwepo kwa amani na utulivu sambamba na vivutio kadhaa vya utalii.


  Kwa upande wa mashirikiano katika sekta ya elimu alisema kuwa juhudi za makusudi zinaendelea kuchukuliwa na zitachukuliwa katika kuhakikisha nafasi za masomo kwa Zanzibar  nchini humo zinaongezeka.

  Sambamba na hayo, Balozi huyo alimpongeza Dk. Shein kwa kuisimamia vyema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa ambayo imepata mafanikio makubwa na kuwa kigezo ndani na nje ya bara la Afrika.


  Pia, Balozi huyo aliisifu na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Dk. Shein kwa kutoa fursa sawa ya kufanya Kampeni zilizokuwa huru na amani kwa vyama vyote hapa nchini.


  Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar


  Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822

  E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk


  0 0

  Baadhi ya waandishi wa habari  wakimsikiliza   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Mstaafu Damian  Lubuva kuhusu  alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali ya Uchaguzi Mkuu, ikiwemo kusisitiza mwisho wa kampeni za uchaguzi huo kuwa ni leo saa 12: 00 jioni. 
   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Mstaafu Damian  Lubuva  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dares Salaam kuhusu masuala mbalimbali  ya Uchaguzi Mkuu, ikiwemo kusisitiza mwisho wa kampeni  za uchaguzi huo kuwa ni leo saa 12: 00 jioni.  
  Kulia  ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Emmanuel   Kavishe.

  0 0

  Rais wa Chama cha Waendesha Baiskeli Tanzania, Godfrey Jacks Muhagama, ambaye pia ni miongoni mwa waendesha baiskeli kwenye msafara huo ulioanzia Mbeya akitoa maelezo ya namna shughuli hiyo ilivyofanikiwa.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr. Rashid Rutengwe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waendesha baiskeli na viongozi wa msafara huo.
  Msafara wa waendesha baiskeli ukiingia kwenye mji wa Ilula Mkoani Iringa
  Esther Joshua ambaye ni mwanamke pekee kwenye msafara wa kuendesha baiskeli kutoka Mbeya mpaka Arusha, hapa akiwa nje kidogo ya mji wa Mafinga kuelekea Iringa Mjini.

  Na Dotto Kahindi
  Msafara wa Kampeni ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya tabianchi kupitia uendeshaji wa baiskeli ambao ulianza Octoba 17 mwaka huu kwenye mpaka wa Tanzani na Malawi umefika jinini Dar es Salaam ambako utasimama kupisha zoezi zima la uchaguzi mkuu kabla ya kuelekea Namanga Arusha.

  Msafara huo ambao umekuwa ukipata mapokezi makubwa kutoka kwa viongozi mbalimbali wa serikali, dini na wananchi kwa ujumla, ukiwa Mkoani Morogoro ulipata mapokezi makubwa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo Dr. Rajab Rutengwe.

  Mkuu huyo wa mkoa amewapongeza waendesha baiskeli na kuwaita ni mashujaa na mabalozi wazuri wa kuhamasisha jamii kutunza  mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

  Msafara huo ambao umeanzia Msumbiji kupitia Afrika Kusini Botswana, Zimbabwe, Zambia, Malawi na sasa Tanzania, utafikia kilele chake mjini Nairobi Kenya mwezi novemba mwaka huu.

  Dr. Rutengwe amesema kuwa jambo la kutunza mazingira ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi ni muhimu na ni jambo la kila mmoja wetu.
  Amewakemea viongozi wa serikali wanaoshirikiana na wananchi kuharibu mazingira kwa kukata miti na kuuza mikaa na kuahidi kuwashughulikia baada ya uchaguzi mkuu kumalizika.

  Akizungumzia umuhimu wa milima ya Uluguru, Nguu na Ukaguru anasema ni muhimu kwa kuwa ni moja ya vyanzo vya maji ambayo huwanufaisha watu wa mikoa ya Morogoro, Dodoma, Pwani na Dar es Salaam. 

  “Sisi watu wa Morogoro tukiwa wabinafsi kwa kuharibu vyanzo vya maji kwa kufanya uharibifu kwenye milima ya Uluguru, Nguu na Ukaguru tutakuwa tunawaua wenzetu wanaotegemea milima hiyo” anasema Dr. Rutengwe

  Akitoa taarifa ya msafara huo, Ofisa Miradi wa Norwegian Church Aid, Nizar Suleiman anasema kuwa lengo la msafara huo ni kujenga uelewa kwa jamii juu ya mabadiliko ya tabianchi kwa kupitia uendeshaji wa baiskeli na kutumia vijana kutoka kwenye taasisi za kidini nchini kufikisha elimu hiyo.

  Anasema msafara huo utahusisha pia uchukuaji wa saini za wananchi ili kuweka imani zao kwa viongozi wa kiserikali ambao watakwenda kwenye mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP21 utakaofanyika desemba mwaka huu huko Paris, Ufaransa.

  Msafara huo unatarajiwa kuendelea tena novemba 3 mwaka huu, ukitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Namanga Mkoani Arusha ambapo utakabidhiwa kwa waendesha baiskeli wa Kenya.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. Magufuli ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati wa hitimisho la kampeni.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. Magufuli ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati wa hitimisho la kampeni. 
   Umati wa maelfu ya wananchi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kushudua kilelel cha hitimisho la kampeni za chama cha Mapinduzi CCM katika uwanja wa CCM kirumba.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea machache mtambulisha ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati wa hitimisho la kampeni.
   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akimnadi Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wa pili kutoka kulia, Mgombea Mwenza Mama Samia Hassan Suluhu na wagombea ubunge wa majimbo ya Ilemela Anjela Mabula wa kwanza kushoto  na Stanslaus Mabula Nyamagana wa tatu kutoka kushoto
   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akimnadi Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wa pili kutoka kulia,na wagombea ubunge wa majimbo ya Ilemela Anjela Mabula wa kwanza kushoto  na Stanslaus Mabula Nyamagana wa tatu kutoka kushoto.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwanadi wagombea ubunge wa Mwanza.Kulia ni mgombea wa Ubunge wa jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula na mgombea wa Ubunge wa jimbo la Ilemela Anjela Mabula.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiburudika na Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. Magufuli pamoja na wanakibajaji ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati wa hitimisho la kampeni.
   
  Umati wa maelfu ya wananchi wa jiji la Mwanza wakifuatilia kufungwa kampeni za chama cha Mapinduzi CCM katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

  PICHA NA MICHUZI JR-MWANZA

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  WATANZANIA wametakiwa  kuendelea kudumisha amani hasa kipindi  cha uchaguzi kwani bado nchi yetu inasifika kwa amani dunia kote
  kauli hiyo imetolewa na  mwanaharakati wa amani Mhonda Joseph wakati akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam.


  Mhonda amesema wananchi wahakikishe  amani inakuwepo  na hata  wageni wanaoishi hapa  kutokana na historia ya miaka ya nyuma  ya hapa nchini kuwa ya amani.

  Aidha  amewataka watanzania wasikubali  baadhi ya watu  wachache kuja kuchochea utovu wa amani na wakumbuke amani ikipotea ni vigumu kuirudisha pindi itakapotoweka.


  lakini pia Mhonda ameeleza kuwa  hatua tuliyofikia ya kuwa na vyama vingi  ni moja ya maendeleo  ni mhimu kuhakikisha  tunachagua kiongozi bora  atakao watumikia watanzania wote kutokana na hali ya ugumu wa maisha kwa  sasa.  hata hivyo amewataka mawakala kuhakikisha wanafanya kazi zao bila kukubali kufanya vurugu pindi wanaposimamia wakati wa kuhesabu


  0 0


  0 0

   Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa,Dominician Mkama(wa kwanza kushoto) akishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wenzake kukata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la kampuni hiyo mkoani mwanza baada ya kukarabatiwa upya katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
   Baadhi ya wateja wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakigonganisha glasi kufurahia uzinduzi wa duka la kampuni hiyo upya baada ya kukarabatiwa kwa muda wa miezi miwili jijini Mwanza.
   Mteja wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa,Farida Omar (kushoto)akilishwa keki na Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kanda ya ziwa wa kampuni hiyo,Dominician Mkama(kulia)wakati wa uzinduzi wa duka la kampuni hiyo upya baada ya kukarabatiwa kwa muda ya miezi miwili jijini Mwanza.
  Mteja wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa,John Mwaseka (kushoto)akilishwa keki na Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kanda ya ziwa wa kampuni hiyo,Dominician Mkama(kulia)wakati wa uzinduzi wa duka la kampuni hiyo upya baada ya kukarabatiwa kwa muda ya miezi miwili jijini Mwanza.
   Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wakipatiwa huduma mbalimbali za mawasiliano kwenye duka la Vodacom Tanzania mkoani humo mwishoni mwa wiki baada ya duka hilo kuzinduliwa upya baada ya kukarabatiwa kwa muda wa miezi miwili.
  Hili ndilo duka jipya la Vodacom Tanzania mkoani mwanza mara baada ya kukarabatiwa upya,hafla ya uzinduzi wake ilifanyika hivi karibuni.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihakikiwa kabla ya kutimiza wajibu wake wa kupiga kura kwa ajili ya kuchagua Rais, Mbunge, Mwakilishi, na Diwani  kwenye kituo cha kupigia kura  namba 7 katika Shule ya Sekondari ya Kiembesamaki Zanzibar, kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaofanyika leo Octoba 25, 2015 Nchini kote. (Picha na OMR)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitimiza wajibu wake wa kupiga kura kwa ajili ya kuchagua Rais, Mbunge, Mwakilishi, na Diwani  kwenye kituo cha kupigia kura  namba 7 katika Shule ya Sekondari ya Kiembesamaki Zanzibar, kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaofanyika leo Octoba 25, 2015 Nchini kote. (Picha na OMR)


  0 0

   Wapiga kura kituo cha Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam wakiwajibika kwa utulivu na amani asubuhi hii.
   Utulivu na amani watawala kituo cha Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam
   Nidhamu, utulivu, uvumilivu na amani vyatawala kila sehemu. Hapa ni Kibaha Machinjioni, mkoa wa Pwani
  Hapa ni Kibaha Machinjioni, mkoa wa Pwani
   Kituo cha Afisa Mtendaji wa Kata ya Olorieni jijini Arusha 
  Kituo cha Dispensary ya Kata ya Olorieni, Arusha. 
  Picha kwa hisani ya blogger Seria

  0 0

   Mgombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa Tiketi ya CCM Jimbo la Mahonda ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika foleni ya kusubiri kupiga kura kwenye Kituo chake kiliopo Skuli ya sekondari ya Kitope.
   Balozi Seif akipiga kura ya Kumchagua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Bunge ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Kituo chake hapo Skuli ya Sekondari ya Kitope
   Karani wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar akimuweka alama Balozi Seif kuashiria kwamba ameshakamilisha zoezi la Kupiga kura ya kumchagua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Mbunge, Mwakilishi na Diwani
  Balozi Seif akizungumza na vyombo vya Habari mara tuu bada ya kumaliza kutumia haki yake ya kupiga kura hapo Skuli ya Sekondari ya Kitope ambapo ndio kwenye kituo chake cha uchaguzi. Picha na OMPR,  ZNZ.

  0 0

   Baadhi ya Wananchi wakihakiki majina yao tayari kwa kupiga kura ya kuwachangua Marais, Wabunge, wawakilishi na Madiwani hapo katika kituo cha kupiga kura skuli ya Sekondari Kitope Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unguja.
    Wananchi wakihakiki majina yao tayari kwa kupiga kura ya kuwachangua Marais, Wabunge, wawakilishi na Madiwani hapo katika kituo cha kupiga kura skuli ya Sekondari Kitope Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Baadhi ya Wananchi wakiwa katika foleni kwa ajili ya kupiga kura ya kuwachangua Marais, Wabunge, wawakilishi na Madiwani hapo katika kituo cha kupiga kura skuli ya Sekondari Kitope Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unguja.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija (kushoto) wakati alipowasili katika kituo cha kupiga kura Skuli ya Bungi msingi wilaya ya Kati Unguja leo

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein  akipokea karatasi ya kupigia kura kutoka kwa Afisa  Sibira Ramadhan Iddi katika kituo cha kupiga kura Skuli ya Bungi wilaya ya Kati Unguja zoezi ambalo limefanyika leo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akitumbukiza kura yake sandukuni katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Bungi msingi wilaya ya kati  Mkoa wa Kusini Unguja

   Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein akitumbukiza kura katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Bungi msingi wilaya ya kati  Mkoa wa Kusini Unguja
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akifanya mahojiano na waandishi wa habari baada ya kipiga kura leo katika kituo cha Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija(kushoto)baada ya kupiga kura katika kituo cha kupiga kura Skuli ya Bungi wilaya ya Kati Unguja zoezi ambalo limefanyika leo,(kulia)Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhan Abdalla Ali. Picha na Ikulu, ZNZ. 

  0 0

   Rukia Omari (kushoto), akimsaidia kupiga kura jamaa yake Mwanaharusi Mohamed ambaye ni mlemavu wa macho wakati wa kupiga kura katika kituo cha Mbagala Misheni Dar es Salaam leo asubuhi.
    Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupiga kura katika Kituo cha Mtoni Kijichi Stendi Dar es Salaam leo asubuhi.
   Wananchi wakisubiri kupiga kura katika kituo cha Shimbwe Mbagala Kuu.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Wananchi wa kijiji cha Naiyobi wilaya ya Ngorongoro wakichota maji ambayo hutumia na mifugo kijiji hicho kinakabiliwa na uhaba wa maji

  Na Woinde Shizza,Arusha
  WANANCHI wa Kijiji cha Nayobi  kilichopo tarafa ya Ngorongoro wilayani
  Ngorongoro mkoani Arusha wamelalamikia kero ya uhaba wa maji
  inayowasababishia kukesha kwenye bomba la kijiji kwa takribani siku tatu
  wakisubiri maji jambo linalopelekea shughuli za kijamii na kiuchumi
  kusimama kwa muda mrefu na kinamama kutembea umbali mrefu wakitafuta huduma hiyo.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuwa kwa muda mrefu wamekua wakiteseka kupata huduma za maji huku kinamama wajawazito wakijifungulia bombani apo baada ya kukaa kwa muda wakitafuta maji huku wengine wakilazimika kukesha na watoto wadogo.

  Wanakijiji Daniel Sereki  na  Rehema Laizer  na wamesema kuwa kwa sasa
  wanakabiliwa na tatizo kubwa la uhaba wa maji pamoja na chakula na hata
  pale wanapopata chakula hukosa maji ya kupikia chakula hicho na kuziacha
  familia zao zikitaabika kwa njaa.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji Naiyobi  Meleji  Sikoni amesema kuwa kwa muda wa miaka 20 wamekua wakikabiliwa na tatizo la uhaba wa maji hivyo ameiomba serikali na mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro  iwasaidie kutatua tatizo hilo sugu linalowaathiri  wananchi wengi.

  Mgombea Ubunge Jimbo la Ngorongoro Wiliam Olenasha  ameeeleza kisikitishwa na wananchi wanaoteseka kwa kero ya maji ambayo hushirikiana na mifugo katika matumizi yake hivyo ameaidi kutatua kero hiyo pindi atakapopata ridhaa ya kuongoza wilaya hiyo.

  Wilaya ya Ngorongoro inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa maji pamoja na chakula hasa katika kipindi hiki cha kiangazi ,juhudi zinahitajika kwa upande wa serikali na Mamlaka ya Ngorongoro ili kuweza kuwanusuru wananchi na baa la njaa pamoja na uhaba wa maji.


  0 0

   
  Wasimamizi wa uchaguzi wakiendelea kuwahudumia wananchi waliofika katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama leo jijini Dar kwa ajili ya kupiga kura.
  Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog
  Mmoja wa wazee akisaidiwa na mtu wake wa karibu ili kupiga kura katika kituo cha Chuo cha Ustawi wa Jamii  jijini Dar leo.
  Mlemavu akisaidiwa na mtu wa karibu alipofika katika kituo cha Kenton kwa ajili ya kupiga kura
   
     Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupiga kura katika kituo cha Shule ya Sinza  Mapambano jijini Dar leo.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

   Mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akijiandaa kupiga kura huko kijijini kwake Chato mkoani Geita leo
    Mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipiga kura yake
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM  Dk. John Pombe Joseph Magufuli akikunja vizuri karatasi baada ya kupiga kura yake jimboni kwake Chato mapema leo asubuhi Oktoba 25, 2015.
  Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiweka karatasi kwenye sanduku

  0 0

  Wakazi wa Jiji la Mbeya Mjini wajitokeza kwa wingi kupiga kura katika Vituo mbalimbali walivyo jiandikishia kuajili ya kupiga Kura kama waonekanavyo hapo katika Picha ni baadhi ya watu wakiwa katika kituo kilichopo Mtaa wa Mkombozi Jijini Mbeya wakiwa wamepanga Foleni kuajili ya kupiga Kura.
  Baadhi ya Wapiga kura wakiwa katika Foleni..

  Hapa ni eneo la Mwanjelwa maharufu kwa Jina la Mtaa wa kongo likiwa Pweke kuajili ya uchaguzi hakuna alie leta Biashara yake hapa siku hii ya leo.

  Baadhii ya Maduka ya Vitu vya Jumla na Lejaleja yakiwa yamefungwa Eneo la Kabwa Stendi.

  Jeshi la Polisi linaendelea kuzungukia Mitaa mbalimbali kuhakikisha hali ya Usalama  jijini Mbeya inakuwa shwari katika kipindi hiki cha uchaguzi.
                             PICHA ZOTE NA FADHIRI ATICK-MR.PENGO MBEYA
                                                     PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Wanannchi wakihakiki majina yao katika kituo chao cha kupigia kura.
  Jaji Mutungi akiwa kwenye chumba cha kupiga kura.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika foleni akisuburi zamu yake ya kupiga kura leo katika kituo cha hospitali ya kijiji cha Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo leo.
   Ofisa katika kitu cha kupiga kura akimkabidhi Rais Kikwete karatasi za kupiga kura.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiandika kura yake ya siri.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipiga kura ya Rais Mbunge na Diwani katika kituo cha kupiga kura cha hospitali ya kijiji cha Msoga,Kata ya Msoga wilayani Bagamoyo leo.

  MKE WA RAIS MAMA SALMA APIGA KURA KATIKA KITUO CHA MTANDA HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

older | 1 | .... | 1010 | 1011 | (Page 1012) | 1013 | 1014 | .... | 3272 | newer